Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

ABUDHABI YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUJENGA BARABARA YA UVINZA HADI MALAGARASI KWA KIWANGO CHA LAMI

0
0
Benny Mwaipaja, Abu Dhabi
Tanzania imeendelea kuaminiwa na Jumuiya ya Kimataifa ambapo Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Falme za Kiarabu-Abu Dhabi, umeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 15, sawa na shilingi bilioni 34 za Tanzania, kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami
Hafla fupi ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika katika makao makuu ya Mfuko huo yaliyopo Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, amesaini kwa niaba ya Serikali, na Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kwa niaba ya Mfuko huo.
Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo, Katibu Mkuu-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa ni kiungo kikuu cha usafiri wa abiria na mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigoma na nchi jirani za Burundi na Kongo DRC.
Amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuboresha barabara hiyo kwa kiwango cha lami umelenga kuchochea uchumi wa nchi kwa kuwezesha usafirishaji wa mazao ya wakulima pamoja na kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kufanya biashara na nchi hizo jirani.
"Tutabakiwa na kipande cha barabara yenye urefu wa kilometa 28 kutoka Urambo hadi Kaliua na kilometa 42 kutoka Chagu hadi Kazilambwa, barabara ambazo Serikali inaendelea kuzitafutia fedha ili kukamilisha barabara yote inayoelekea ukanda huo wa kati kutokea Dar es Salaam, Manyoni (Singida), Tabora hadi Kigoma" Alisema Mhandisi Iyombe.
Ameushukuru Mfuko huo kwa kuendelea kuiamini Serikali na kutoa mkopo huo wenye masharti nafuu baada ya kufanya hivyo hivi karibuni kwa kutoa mkopo mwingine wa dola milioni 57, uliofanikisha kuboreshwa kwa barabara ya Kidahwe hadi Uvinza yenye urefu wa kilometa 77 kwa kiwango cha lami.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi, kwa upande wake, amesema kuwa Mfuko huo uko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Amefafanua kuwa mradi huo ambao mkataba umesainiwa mjini Abu Dhabi, utakuwa ni wa nne kufadhiliwa na Mfuko wake Tangu uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Tanzania uanzishwe mwaka 1977, ukiwemo mradi wa kuendeleza kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mradi wa Maji Vijijini huko Viwani Zanzibar na Mradi wa kuboresha barabara ya Kidahwe hadi Uvinza kwa kiwango cha lami.
 Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk amesema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni kiashiria cha kukubalika kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ya haraka na kuungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.
"Hatua hii ni uthibitisho wa mahuasiano mazuri ya kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu uliodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 1977" Alisisitiza Mhe.Mbarouk
Mhe. Mbarouk amebainisha kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ya Uvinza hadi Malagarasi kutachochea maendeleo ya kiuchumi na mapinduzi ya viwanda kwa kuunganisha shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na maliasili pamoja na kukuza utalii.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akisalimiana na mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, alipowasili Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Abu Dhabi, kwa ajili ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (wa tatu kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami. kulia kwake ni Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk na Mkuu wa Dawati la Abu Dhabi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Kuchaka.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto),  na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto),  na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakibadilishana mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto),  na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakionesha mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
-Wizara ya Fedha na Mipango

ALICHOKISEMA RAIS JOHN MAGUFULI KUHUSU MRADI WA USIMIKAJI WA MFUMO WA RADA

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA NDEGE MPYA YA TATU AINA YA BOMBARDIER DASH 8 Q400

0
0
 Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 2, 2018
 Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku ikipewa heshma ya  kumwagiwa maji(water salute) mara baada ya kutua.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa uzinduzi wa ndege Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



 Marubani walioileta ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 kutoka Canada (wawili waliosimama kulia) na marubani na wahudumu wa ATCL mara baada ya kuwasili kwa ndege hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa viongozi wa dini na wa ATCL wakiwa ndani ya ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome na marubani walioileta ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakala wa Safari (TASOTA) Bw. Mustapha Khatawa kwa kuwasili kwa ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

RAIS DKT.JOHN MAGUFULI ASEMA NCHI IKO SALAMA NA ITAENDELEA KUWA SALAMA.APRILI 2,2018

RAIS DKT.JOHN MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA WAUNGANE KATIKA MASWALA YA KITAIFA

PWANI KUJENGA VIWANDA VITATU VYA MADAWA NA BAADHI YA VIFAA TIBA

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

SERIKALI mkoani Pwani, imeitikia wito wa serikali ya awamu ya tano ya kujenga viwanda vya madawa na baadhi ya vifaa tiba ambapo inatarajia kuwa na viwanda hivyo vitatu hali itakayoondoa adha ya kuagiza madawa nje ya nchi .

Aidha imekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wawekezaji ya kutoa ajira kwa watu kutoka nje ya nchi na kuwabania fursa hiyo wanaPwani ama watanzania.

Akielezea masuala ya uwekezaji na ajira ,wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mjini Kibaha ,mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alisema Viwanda vya madawa vitawezesha kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakitumika kununulia madawa nchi jirani na nje.

Alieleza viwanda vitatu vinajengwa Mkoani Pwani ikiwemo Kairuki Pharmaceuticals industry Ltd ,Zinga pharmaceuticals ambacho kitajengwa kwa ubia na waislael na kipo mbioni kuanza kujengwa na Bahari pharmaceuticals .

"Tunaikitia wito wa rais Dk.John Magufuli ,lakini pia tangu kipindi cha nyuma tumejipanga kujenga viwanda hivyo ,kupitia ziara hii tunawathibitishia wananchi tunaunga  mkono kauli ya serikali yetu"alifafanua Ndikilo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU APRILI 2, 2018 NA SALIM KIKEKE

SUKOS YATOA ELIMU KUKABILI MAJANGA KWA WANAFUNZI SHULE ZA SEKONDARI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
IMEELEZWA ipo haja ya kutoa mafunzo ya elimu ya majanga na maafa kwa wanafunzi kwani husaidia kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii kuelezea namna ya kuchukua tahadhari mapema.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu wakati Taasisi ya Sukos kwa kushirikiana na Vodacom Foundation kutoa vifaa mbalimbali vya kujikikinga na majenga.

Ambapo amesema kuwa vifaa vya kutumia wakati majanga yanatokea ni muhumu sana na kuongeza SUKOS na Vodacom Foundation zimeona mbali zaidi katika kutoa vifaa vya kutumia pale majanga yanapotokea hasa katika shule ambapo zimekuwa zikikumbwa na majanga ya moto.

Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau katika kujitoa kwa jamii kwa ajili ya kutoa elimu ya majanga na namna ya kuweza kukabili.
 Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kupambana na majanga mbalimbali katika shule za sekondari za jijini Dar es Salaam.
 Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos, Kamishina Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akizungumza na wanafunzi kuhusiana na majanga mbalimbali yanayotokea na kushindwa kuyakabili kutokana na kukosa elimu ya majanga pamoja na elimu ya kutumia vifaa mbalimbali katika kujiokoa katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald akipokea chati cha kutambua mchango Vodacom Foundation katika kutoa vifaa vya kukabiliana majanga mbalimbali ikiwemo Moto katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari wa Jeshi la Zimamoto, Amani Hassan akiwafundisha wanafunzi jinsi ya kutumia Fire Extyingusher wakati moto ukiwa unatokea katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: BREAKING NYUZZZZ......: MASOGANGE AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA AU KULIPA FAINI YA SH. MILIONI MOJA NA NUSU

0
0


Na Bakari Majeshi, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuhukumu mrembo na video queen,  Agnes Gerald a.k.a Masogange kulipa faini ya Sh.milioni 1.5 au jela miaka tatu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zakulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Hukumu hiyo kwa Masogange imsomwa leo mahakamani hapo Kisutu ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri  amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi watatu waliopelekwa mahakamani hapo,wamethibitisha mashtaka dhidi ya Masogange kuwa alitenda kosa.

Huku utetezi ukiwa na shahidi mmoja. Hakimu Mashauri amesema,

 "Upande wa mashtaka pasipo kuacha wamethibitisha mashtaka,  hasa kutokana na uthibitisho uliotolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali unaonesha mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za kulevya.

"Hivyo kutokana na kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka na kuzingatia utetezi wa upande wamshtakiwa ambaye alijitetea mwenyewe, namtia hatiani mshtakiwa kwa makosa hayo ya kutumia dawa za kulevya," amesema Hakimu Mashauri wakati anasoma hukumu hiyo

Hata hivyo kabla ya kusomwa kwa hukumu iliyomtia Masogange hatian, upande wa mashtaka uliombamshtakiwa apewe adhabu kali huku ule wa  utetezi ukiomba apewe adhabu ndogo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema, katika kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya Heroinmshtakiwa anahuhukumu kulipa faini ya Sh.Mil 1 ama jela miaka 2, ”Na katika shtaka la pili la kutumia dawa zakulevya aina ya Oxazepam, mshtakiwa anahukumiwa kulipa faini ya Sh.500,000  ama jela miezi 12,"amesema.

Nje ya mahakama hukumu hiyo imezua gumzo kubwa hasa kutokana na watanzania wengi hasa wanaofuatilia mambo ya mastaa wa kibongo walikuwa wakiifuatilia kesi hiyo kwa karibu zaidi.

DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na baadhi Viongozi wa Ujumbe wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo chini ya kiongozi wake Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya (katikati).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya (wa pili kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na aliofuatana nao leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo. Picha na Ikulu, Zanzibar.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UHOLANZI WAANDAA WARSHA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI JIJINI THE HAGUE

0
0
Katika kutekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi kwa kushirikiana na Taasisi ya Wafanyabiashara ya Uholanzi (Dutch Council for International Business - DCIB) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zimeandaa Warsha ya Biashara na Uwekezaji iliyofanyika jijini The Hague nchini Uholanzi tarehe 29/03/2018.

Lengo kuu la Warsha hiyo, pamoja na kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uholanzi, ni kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan katika Sekta za Viwanda, Ufugaji, Uvuvi, Utalii, Ujenzi, Kilimo na Miundombinu ya Kilimo. 

Aidha, Warsha hiyo iliyohudhuriwa na Wawakilishi wa Makampuni takriban sitini (60) ni mwendelezo na jitihada mbalimbali ambazo Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa kushirikiana na Balozi za Tanzania zilizopo nje ya nchi kuendeleza diplomasia ya uchumi ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania na kufikia malengo ya Serikali kuwa nchi ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, Irene Kasyanju,  akitoa neno la ukaribisho wakati wa Warsha ya Biashara na Uwekezaji.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Warsha ya Biashara na Uwekezaji Jijini The Hague wakimsikiliza Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geoffrey I. Mwambe akitoa mada kwa wahusika wa Makampuni mbalimbali kutoka Uholanzi waliohudhuria Warsha hiyo.

Michezo Taasisi za Afya kuboreshwa

0
0
Serikali imesema itaendelea kuboresha michezo sehemu za kazi ili kuifanya iwe endelevu na kuwawezesha watumishi wengi kushiriki.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu-Kitengo cha Utafiti Zanzibar, Hamisi Rashid Mohamed wakati alipokua akizungumza katika hafla  ya kufunga tamasha la michezo ya Pasaka 2018, iliyoshirikisha timu za michezo kutoka Wizara ya afya Zanzibar,  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) , Taasisi ya Tiba ya Mifupa  Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Amesema michezo hiyo ni ya muda mrefu ilianzishwa mwaka 1972 na kwamba  hakuna budi kuindeleza na kuiboresha zaidi ili kuleta hamasa kwa wanamichezo wa taasisi hizo kushiriki kwa wingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Bw. Makwaia Makani ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amesema ushiriki wa michezo ni jambo zuri kwani inawaepusha vijana kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa.

Amesisitiza mipango iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kuhakikisha michezo hiyo inaboreshwa na kutoa fursa kwa watumishi wengi kushiriki.

‘’Hospitali ya Taifa Muhimbili inaipa kipaumbele michezo na nina ahidi kwamba mapungufu yote yaliyopo tutayafanyia kazi kikamilifu na michezo hii tutaendelea kuiboresha,’’ amesema Mkurugenzi Makani.

Tamasha la michezo ya Pasaka lilianza Machi 30, 2018  na kumalizika Aprili 2 , 2018 likihusisha mchezo wa mpira wa miguu ,pete pamoja na kuvuta kamba .

Tamasha hilo mwakani litafanyika  Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makwaia Makani akizungumza kwenye tafrija ya kuwaaga wachezaji wa Timu ya Michezo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), timu ya Wizara ya Afya Zanzibar, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) baada ya timu hizo kushiriki tamasha la Michezo ya Pasaka 2018.
Baadhi ya wachezaji na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakimsikiliza Mkurugezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makani wakati akizungumza nao.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti- Zanzibar, Hamisi Rashidi Mohamed akizungumza kwenye tafrija ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara ya Afya Zanzibar na Timu ya Michezo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makwaia Makani na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti- Zanzibar, Hamisi Rashidi Mohamed akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu hizo baada ya kumalizika kwa tafrija hiyo.

TPB YAKAKABDHI HUNDI YA SH. MILIONI MBILI KWA JUKWAA LA WAHARIRI

0
0
Meneja wa mawasiliano wa Benki ya TPB, Chichi Banda (kulia), akimkabidhi Mfano wa hundi ya Sh.milioni 2 Kwa mratibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Anita Kosuri, kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya mkutano mkuu wa wahariri Tanzania utakaofanyika hivikaribuni mkoani Morogoro. (Na Mpigapicha Wetu).

WABUNGE MTULIA WA KINONDONI NA MOLLEL WA SIHA WAAPISHWA

0
0
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akimwapisha, Godwin Aloyce Mollel kuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mheshimiwa Godwin Aloyce Mollel akiapa kuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. 
  Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akimwapisha, Maulid Mtulia kuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. 
 Mheshimiwa Maulid Mtulia akiapa kuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BENCHI LA UFUNDI LAZUNGUMZIA MATIBABU YA JUNIOR, AMOAH NCHINI AFRIKA KUSINI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENCHI la Utabibu la Azam FC, limetoa ripoti ya maendeleo ya wachezaji wawili wa timu hiyo, mshambuliaji Wazir Junior na beki Daniel Amoah, ambao wamepelekwa Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa matibabu.

Wakati Junior akiwa anasumbuliwa kwenye enka na Amoah kwa upande wake alikuwa akisikia maumivu kwenye goti, majeraha aliyopata miezi miwili iliyopita katika mchezo wa kirafiki wa Azam FC dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kudondokea sakafu nje ya uwanja.

Daktari Mkuu wa Azam FC, Dk. Mwanandi Mwankemwa, amesema Amoah amekutwa na tatizo kubwa kwenye goti lake na atafanyiwa upasuaji Alhamisi hii na atalazimika kukaa nje ya dimba kwa miezi tisa.

“Daniel tulimpeleka Afrika Kusini Machi 26 na baada ya uchunguzi ikaonekana kwamba amepata matatizo ya kukatika mtulinga wa kati wa goti na pia ikaonekana vilevile amechanika washa ‘meniscus’ ambayo ipo katikati ya goti na pia vilevile ameonekana ana sehemu ndogo iliyovunjika katika sehemu ya juu ya mfupa wa ugoko ‘tibia’ karibu na maungio ya goti,” amesema.

Amesema amemuacha mchezaji huyo jijini Cape Town, ambapo Jumatano atalazwa katika Hospitali ya Vincent Pallotti kabla ya kesho yake kufanyiwa upasuaji na kukaa hospitali hadi Ijumaa hii.

“Aprili 9 ataonwa na daktari na itakapofika Aprili 10  atarudi hapa Dar es Salaam, suala na Amoah ni la kusikitisha kidogo kwa sababu ule utaratibu wake baada ya operesheni na kurudia tena kwenye ushindani utamchukua muda wa miezi tisa kwa hiyo ataonekana tena uwanjani baada ya miezi tisa kupita toka siku aliyoumia ambayo ni wiki nane zilizopita kwa hiyo bado miezi mingine saba,” amesema.

Akizungumzia matibabu ya Junior nchini humo, Mwankemwa amesema mchezaji huyo hajakutwa na tatizo kubwa na atatakiwa kupumzika kwa muda wa siku tano.

“Wazir Junior yeye aliumia kifundo cha mguu na kule alienda aliangaliwa na akapatiwa matibabu ya sindano na pia vilevile akashauriwa kupumzika kwa siku tano, kwa hiyo ataanza mazoezi ya kwenye sehemu za tifutifu (mchanga) siku ya Aprili 5 (Alhamisi) na 6 (Ijumaa) na atajiunga mazoezini na wenzake ambao watakuwa hawajakwenda safari ya Mbeya,” amesema.


RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA KINYEREZI ll JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibofya kitufe kuashiria kuzindua  rasmi mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Waziri wa Nishati Dkt. Menard kalemani  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa    Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Dkt.Tito Mwinuka  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018  
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018
 Bila kujali mvua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mamia ya wananchi waliojitokeza kushuhudia akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA

BUNGE LA RIDHIA AZIMIO LA MAKUBALIANO YA PARIS CHINI YA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amewasilisha Bungeni azimio la kuridhia Makubaliano ya Paris chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, Bunge limeridhia azimio hilo leo
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mhe. Innocent Lugha Bashungwa mara baada ya Bunge kuridhia Makubaliano ya Paris chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mhe. Suleiman Sadiq mara baada ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge hii leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisisitiza jambo kwa watendaji wa Ofisi yake. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Bi. Butamo Phillip Naibu Katibu Mkuu.

PWANI YAJIPANGA KUKUZA ZAO LA MUHOGO

0
0
Na Munir Shemweta, Pwani

Mkoa wa Pwani umeanza uhamasishaji wa uwekezaji katika zao la muhogo ili kuwawezesha wakulima kujiongezea kipato sambamba na kuendanana soko la China ambapo Tanzania imepata fursa kuuza muhogo nchini humo. Hali hiyo imebainika mwishoni mwa wiki wakati maofisa kutoka Wizara ya Kilimo walipotembelea mkoa huo ikiwa ni mkakati wa wizara kuhamasisha ulimaji zao la muhogo na kuangalia changamoto zake kwal engo la kuongeza tija na uzalishaji waza ohilo.

Akielezea harakati za wilaya ya Kibiti katika kuhamasisha zao la muhogo Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Bwenda Ismail alisema, uhamasishaji huo unaenda sambamba na utoaji mafunzo, utoaji mbegu bora kwa wakulima pamoja na kuhakikisha kila kaya inakuwa na hekari moja ya muhogo jambo litakaloongeza uzalishaji. Kwa mujibu wa Ismail sasa hivi zao la muhogo katika wilaya ya kibiti limekuwa la kibiashara na hali hiyo inatokana na usafirishwaji wa muhogo mbichi kwa wingi kila siku kutoka wilaya hiyo kuenda dar es salaam.
Afisa Kilimo Wilayaya Kibiti Bwenda Ismail (kulia) akiwa na AfisaUgani wa wilaya hiyo Organess Semwenda wakiangalia muhogo unaolimwa katika shamba la Kibiti Farm Estate lilipo kata ya Bungu wilaya ya Kibiti.

Alisema kuwa, hatua nyingine inayofanywa na halmashauri ya wilaya ya Kibiti ni kusaidia wakulima katika uuzaji muhogo hasa baada ya kubainika wakulima katika wilaya hiyo wamekuwa wakipunjwa wakati wakuuza muhogo kwa wafanyabiashara na sasa wilaya imejenga soko la pamoja lililogharimu milioni 65 na mategemeo ya wilaya ni kuwa muhogo utauzwa kwa vipimo stahiki tofauti na sasa ambapo wakulima wanapunjwa kwa mihogo kutenganishwa ile mikubwa na midogo.

Afisa kilimo huyo wa wilaya ya Kibiti alisema, uhamasishaji umewekwa pia katika ujenzi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha muhogo unaonunuliwa kutoka kwa wakulima unasindikwa sambambana kuhakikisha wilaya kibiti m inatenga maeneo kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi, wawekezaji wakubwa, wakati na wadogo pamoja na maeneo kwa ajili ya vijana na msisitizo ukiwa kila kata itenge eneo.
Meneja wakiwanda cha kusindika muhogo cha Ukaya kilichopo Mkuranga Joseph Mtanga (kulia) akimueleza Afisa Mazao wa Wilaya hiyo Derick Samuel namna kiwanda chake kilivyokwama kuendelea nauzalishaji kutokana na kukosekana kwa umeme.

Kwa sasa Wilaya ya Kibiti umekamilisha sheria ndogo ambapo kila kaya itatakiwa kulima zao la muhogo jambo litakalosaidia kusukuma watu kuingia shambani ikiwemo vijana ambapo sasa watalazimika kuingia katika kilimo ili kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda na soko la china la muhogo kwa kuzalisha muhogo wa kutosha.

Kwa upande wa wilaya ya Mkuranga, serikali wilayani humo katika bajeti yake imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kununua na kusambaza mbegu za muhogo kwa wakulima mbalimbali. Afisa Kilimo wilayani humo Bi. Julita Bulali amebainisha kuwa kutokana na jitihada za kusambaza mbegu kwa wakulima kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watu kuwekeza katika zao la muhogo.
Shamba la muhogo lilipo kata ya Bungu wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani.

Hata hivyo, changamoto kubwa katika wilaya hiyo ni kusitishwa kwa huduma katika kiwanda cha Ukaya farm ambacho imekuwa mkombozi mkubwa wa kununua muhogo kutoka kwa wakulima kutokana na kukosekana kwa umeme katika kiwanda hicho.

Kwa mujibu wa meneja wa kiwanda hicho bw. Joseph Mtanga, awali kiwanda hicho kilikuwa kikitumia jenereta lakini mara baada ya kuharibika najitihada za kupataumeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kushindikana shughuli za kiwanda zimesimama na hivyo kuwakosesha wakulima kuuza muhogo katika kiwanda hicho. Meneja huyo wa kiwanda cha Ukaya Farm alisema kiwanda chake hununua wastani wa tani nne mpaka mpaka kumi na mbili kwa siku kutoka kwa wakulima na kusitishwa kwa usindikaji kumesababisha pia ajira za watu thelathini mpaka arobaini kusimama. Baadhi ya wakulima mkoani humo walisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa soko la uhakika jambo linalosababishwa mzunguko wa biashara kutoenda vizuri.
Baadhi ya wakulima wa zao la muhogo wilaya ya Mkuranga wakiwa katika picha ya pamoja.

Walisema biashara ya muhogo wakati mwingine inakwama kutokana na masuala ya kisera ambapo bidhaa zao zinahitaji kuhalalishwana shirika la viwanga Tanzania (TBS) jambo linalofanya kushindwa kuingia katika ushindani kutokana na kutokidhi vigezo. Pia ukosekanaji wa vipimo stahiki katika uuzaji muhogo katika magari unawanyonya wakulima kwa kuwa bei wanayakubaliana mazao yakiwa shambani tofauti nabei wanayouza.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA STARTIMES BUNGENI MJINI DODOMA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Makampuni  ya StarTimes Group, Bw. Pang Xin Xing kabla ya mazungumzo yao, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Makampuni ya Star Times Group, Pang Xin Xing (watatu kushoto) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Star Media Tanzania Limited,Wang Xiao Bo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Makampuni ya Star Times Group,Zhang Ye  na kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Star Media Tanzania Limited, Juma Suluhu Sharobaro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MAKAMU WA RAIS AHAMASISHA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO MKOA WA MJINI MAGHARIBI

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya shamba la mpunga katika bonde la Kizimbani toka kwa Katibu wa Jumuiya ya Wakulima Kizimbani Bw. Shafii Kibwana Said ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuweka kaa kwenye maji kama ishara ya kuhamasisha utunzaji mazingira na uzalishaji wa katika eneo la Fuoni Kibondeni. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanachama wa CCM wa Tawi la Fuoni Kibondeni mara baada ya kuweka jiwe la ujenzi wa Tawi hilo mkoa wa Mjini Magharibi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images