Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

KAMPUNI ZA BIMA ZATAKIWA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA UWAZI

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kampuni za bima nchini zimeshauriwa kuwahudua wananchi kwa uwazi na kutoa huduma za kiwango cha juu ili kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba wakati mkutano wa wadau bima ulioandaliwa African Insurance Digital Banking uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa bima imeanzishwa kwa ajili ya kulinda biashara na mali hivyo wananchi wanatakiwa kuhudumiwa katika kulinda biashara na mali zao huku wakitoa elimu kwa uwazi.

Aliongeza kuwa mtu mwenye bima katika biashara au mali likitokea janga haiwezi kuwa sifuri kutokana na kukata bima kwa ajili ya biashara na mali hizo.

"Kampuni za Bima ili ziweze kufanya kazi ni lazima zisajiliwe katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi," alisema.

Alisema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda sekta ya bima zina mchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi.

Nae Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano wa Bima uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo. 



KUTOA HABARI NA TAARIFA SERIKALINI NI TAKWA LA KISHERIA - DKT. HASSAN ABBAS

NHIF yapeleka huduma kwa wananchi

0
0
Wananchi wamejitokeza kupata huduma za upimaji wa afya bure na usajili wa watoto kwenye huduma za NHIF.
 Huduma ya upimaji wa afya bure na ushauri wa kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
 Wananchi wakiendelea na huduma zinazotolewa na NHIF Mkoa wa Geita.

Na Grace Michael, Geita
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umeendelea na mkakati wake wa kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwa kuwapelekea huduma zake lakini pia upimaji wa afya bure kwa lengo la kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Katika wiki hii, NHIF iko katika Mkoa wa Geita ukitoa huduma za upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kampeni ya usajili wa watoto chini ya umri wa miaka 18 mpango unaojulikana kwa jina la Toto Afya Kadi.

Huduma hizi mkoani hapa zilianza tarehe Machi 28 na zitamalizika Aprili 2, mwaka huu wakati wa kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru. 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja wa NHIF Mkoa wa Geita, Dk. Mathias Sweya amewaomba wananchi kutumia fursa hii kujua hali ya afya zao na kupata elimu ya kujikinga na magonjwa lakini pia faida za kujiunga na Mfuko.

“Nawahamasisha wananchi wote wafike eneo la Soko Kuu la zamani ambapo tumeweka kituo kwa ajili ya kutoa huduma na viwanja vya Magogo siku ya  Jumatatu wiki ijayo tarehe 2/04/2018,” anasema Dk. Sweya.

Wananchi waliofika bandani hapo wameupongeza Mfuko kwa jitihada zake za kuwafikia na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
“Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mmetusaidia sana kutuletea hii huduma hapa, hii inatusaidia kujua hali ya afya zetu lakini pia kuujua Mfuko na huduma zake ambazo ni mkombozi kwa maisha ya kila mwananchi hivyo huduma kama hizi ziwe endelevu,” alisema Edson Kamzola mkazi wa Geita.

DK ABBAS AZUNGUMZIA UMUHIMU MAOFISA HABARI KUTOA TAARIFA

0
0

Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
MSEMAJI wa Serikali Dkt. Abbas Hassan amesema utoaji taarifa na habari kwa sasa ni takwa la kisheria na si utashi wa ofisa habari na tayari wameelezwa hilo na wanaliambua.

Dk.Abbas ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza kutoa matokeo ya utafiti mpya wa mwaka 2018.Utafiti huo umetolewa leo jijini.

Amesema utafiti huo umeonesha namna ambavyo wananchi wametoa maoni yao katika suala la upatikanaji wa taarifa nchini na kufafanua kwa sasa suala la kutoa taarifa ni takwa la kisheria.

"Tunayo sheria sasa ambayo inatoa ulazima wa taarifa kutolewa pale inapohijika.Kutoa taarifa ni hatua moja lakini pia lazima tuangalie sasa hiyo habari ikoje katika suala la usalama wa nchi.Kwa upande wetu wote ambao wanahusika na utoaji taarifa wanajua ni wajibu wao na lipo kisheria,"amesema Dk.Abbas.

Amesema wananchi wengi wanaamini na kusikiliza au kupata habari kupitia redio na kwamba mchango wao kama Serikali wanao mchango wao na kwamba hadi jana inaonesha magezeti na majarida, machapisho ambayo yamesajiliwa ni 169 ambayo yamesajiliwa na redio 150 ambazo zimepewa leseni.

Amefaanua wanatoa kipaumbele kwenye maendeleo ya redio na kwamba wamejikita katika kutoa mafunzo mbalimbali.Kuhusu maofisa habari amesema  dhana nzima ya utoaji habari na taarifa zi lazima uvae suti na kufafanua kwa sasa kwa ofisa habari kutoa habari si utashi binafsi bali ni takwa la kisheria

Amepongeza utafiti wa Twaweza na kusisitiza uwe endelevu kwa kufanyika hata kila baada ya miezi sita.Pia sheria zifuatwe na kuhusu suala la uhuru wa habari ameeleza kuwa ni muhimu lakini uzingatie haki na wajibu wake.


"Kikubwa tufahamu sisi wote ni wadau na hivyo tushirikiane na kwamba kikubwa ni kupigania haki ya kupata habari.Kuna taratibu za kufauata na hata pale unaposikia kuna haki ya kuishi lazima ufurukute ili uishi.Nashauri mambo mengi kuhusu masuala ya habari na hilo ndio kazi yangu,"amesema Dk.Abbas.

Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT WAZALENDO) amesema kwa mujibu wa utafiti watu wengi wamesema hawajisii kumkosoa Rais, Makamu wa  Rais na Waziri Mkuu.

Pia utafiti unaonesha wananchi wengi hawaamini taarifa mbalimbali ambazo zinatoka kwenye vyanzo mbalimbali na hivyo iko haja ya watoa taarifa hizo zitazamwe na kufafanua huenda jamii inaona habari zinazotoka hata kwenye vyombo vya habari si sahihi.

Amesema utafiti unaonesha kuwa wananchi wengi sasa wanamini zaidi matamko ya Rais na Waziri Mkuu na kuomba Twaweza kuagalia mbunge wa Kigoma mjini amepongeza taasi hii na ameshauri kuwe na ulinganifu kwa kuangalia huko nyuma kulikuaje.

"Tunapaswa kupata ulinganifu wa kimuda ambao haujafanyika kwenye utafiti na kwamba anamini huko mbele wataonesha na ulinganifu kati ya mwaka mmoja na mwingine kwa yale ambayo wanayafanyia utafiti,"amesema.

Akizungumzia utafiti huo Mkurugenzi wa TWAWEZA Aidan Yakuze ameeleza utafiti huo kati ya mambo ya waliyoangalia ni uhuru wa kumkosoa Rais, makamu wa Rais na waziri mkuu ambapo matokeo yameonesha kuwa  wananchi hawajisikii huru kumkosoa Rais kwa asilimia 60, Makamu wa Rais asilimia 54 na Waziri mkuu asilimia 51.

Pia utafiti huo unaonesha wananchi hawapo huru kuwakosoa Mawaziri kwa asilimia 47, wakuu wa mikoa asilimia 46, na Wakuu wa wilaya kwa asilimia 43.

Aidha utafiti huo umeonesha kuwa wananchi wengi wana imani kubwa na taarifa zitolewazo na Rais kwa asilimia 70, na Waziri mkuu asilimia 64.

Pia kwa upande wa wawakilishi wabunge wa Chama tawala kwa asilimia 26, wabunge wa upinzani  asilimia 12, viongozi wa serikali asilimia 22 huku idadi ndogo zaidi wanawaamini Wenyeviti wao wa vijiji kwa asilimia 30.

Pia utafiti huo umeonesha kwamba uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari unaungwa mkono na wananchi walio wengi wao kwa asilimia 62 wameeleza kuwa gazeti lililochapisha taarifa za uongo ama zisizo sahihi liombe radhi na kuendelea kuchapisha.

Aidha utafiti huu umeonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawafahamu sheria mpya zinazosimamia masuala ya taarifa hasa za kimtandao na zile za kitakwimu.
 Mbunge wa kigoma Mjini Zito Kabwe akizungumza na waandishi wa Habari akiwapongeza Taasisi ya Twaweza kwa kazi nzuri walioifanya,akiwataka wasiishie mjini tu waende na vijijini.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa Habari Mara baada ya kupokea ripoti hizo kutoka kwa Twaweza,na akiwataka kufanya tafiti hizo kuwa endelevu kwa kila Baada ya miezi 6 Leo katika makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza Aidan Yakuze akizungumza wakati wa kutoa ripoti ya namna ya uwasilishwaji wa Taarifa na habari kwa Jamii leo makumbusho ya Taifa Jijini Dar ea Salaam.

DC LYANIVA AAHIDI KUTATUA KERO ZA WAFANYABISHARA TANDIKA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Temeke Dar es Salaam  Felix Lyaniva amekutana na wafanyabiashara wa Tandika ambapo amewaahidi kuhakikisha anatatua kero ambazo zinawakabili kwenye biashara zao. 

Ametoa aahadi hiyo leo wilayani Temeke akiwa katika ziara yake ya kutembelea maeneo yanayotoa huduma za jamii katika wilaya ya Temeke ambapo amewaambia wafanyabiashara hao kuwa ataondoa kero zote zinazolikumba soko hilo .

Moja ya kero kubwa inayoikumba soko hilo ni miundombinu inayoizunguka soko hilo, ikiwemo kutuama kwa maji kipindi cha mvua ambapo Lyaniva amewaahidi wafanyabishara kushughulikia kero hizo ili kuhakikisha mahali hapo panakua salama kwaajili ya kutoa huduma za kijamii.

Katika ziara hiyo aliambatana na katibu Tawala wilaya,watumishi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,diwani wa Tandika,wenyeviti wa Mitaa,wakuu wa vyama vya siasa mbalimbali,wajumbe wa Mitaa,ofisa Tarafa Chang'ombe na wadau wa utoaji huduma za jamii mbalimbali ikiwemo TARURA,TAKUKURU,DAWASCO na TRA.

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ameenda katika Ofisi ya kata ya Tandika ambapo alifanya kikao cha wadau wa maendeleo na wananchi. Akiwa hapo amesisitiza kuhakikisha wanafunzi wote waliofauru darasa la saba 2017 kama wameripoti shuleni.

Amewataka wazazi kutoa ushirikiano ili watoto wao wasibaki nyumbani kujiingiza katika makundi hatarishi.

Hata hivyo Lyaniva aliwataka wananchi kutoa kiwango stahiki cha kuzoa takataka ili kusaidia zoezi la ukusanyaji taka kuwa rahisi. 

Pia alisisitiza usafi wa kila jumamosi kwa wananchi wote ni lazima.
Pia aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo ya jamii inayotolewa na serikali kwa riba nafuu kupitia benki ya DCB. 

Wakinamama na vijana wamehamasishwa kwenda kuchangamkia fursa hiyo ili kujikwamua katika hali ya kiuchumi na jamii.

Lyaniva alisisitiza kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo endapo mwananchi atakutana na mazingira yoyote ya rushwa atoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU Wilaya ili hatua kali za kisheria zichukuliwe. 

Amesema huduma za jamii ni bure kwa kila mtu hivyo wananchi wasiruhusu vitendo vya rushwa na kuwataka wananchi kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ili kuiongezea mapato Serikali,na kwa mapato hayo hayo yatasaidia kuboresha huduma za jamii. 

Ziara hiyo ya mkuu wa wilaya yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo katika jamii itaendelea katika kata zote zilizopo wilaya ya Temeke katika vipindi tofauti tofauti.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Tandika ambapo amewaahidi kuhakikisha anatatua kero ambazo zinawakabili kwenye biashara zao
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Tandika

IGP SIRRO AWATUNUKU STASHAHADA NA ASTASHAHADA ASKARI POLISI

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akiwasili katika viwanja vya Mahafali ya kiwatunuku Askari Polisi waliohitimu astashahada na stashahada za Sayansi ya Polisi na Upelelezi kutoka vyuo vya Polisi. Sherehe zilifanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akitoa hotuba katika Mahafali ya kuwatunuku Askari Polisi waliohitimu astashahada na stashahada za Sayansi ya Polisi na Upelelezi kutoka vyuo vya Polisi. Sherehe zilifanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

Baadhi ya wahitimu waliohitimu astashahada na stashahada za Sayansi ya Polisi na Upelelezi kutoka vyuo vya Polisi wakiwa kwenye  Sherehe zilifanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

MKUTANO MKUU WA YANGA SASA RASMI MEI 5

0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ua Jamii

KATIBU Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa ametangaza siku maalumu ambayo klabu itafanya mkutano mkuu wa wanachama wote,kujadili masuala mbalimbali muhimu ya maendeleo ambayo itakuwa Mei 5 mwaka huu.

Mkwasa amesema  kuwa wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada zao mapema kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.

Akizungumza leo ,Mkwasa amesema mkutano huo utafanyika Mei 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam, hivyo wanachama wenye kadi aina zote mbili wataruhusiwa kuingia ukumbuni, kwa maana ya wale wote wenye kadi za zamani na kadi mpya zinazotolewa na benki ya Posta.

Akiendelea zaidi Mkwasa amesema  kupitia kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika Jumapili iliyopita, kamati   imeridhia kufanyika kwa Mkutano huo, na kuomba wanachama kujindaa kwa ajenda ambazo zitatangazwa baaadae.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: HAKUNA TISHIO LA USALAMA NCHINI

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazosambazwa na watu wasioitakia mema nchi, zinazotishia usalama wa raia na mali zao. Taarifa hizo zimewatia hofu baadhi ya raia wa kigeni na wanadiplomasia wanaofanya kazi na kuishi hapa nchini.

Taarifa hizo zimekuwa zikidai kuwa kutakuwa na maandamano yatakayofanyika tarehe 26 Aprili 2018 na zinawaonya raia wa kigeni wasiende Zanzibar katika kipindi cha Sikukuu ya Pasaka na sherehe za Muungano kwa sababu za kiusalama.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahakikishia wanadiplomasia na raia wote wa kigeni wanaofanya kazi na kuishi nchini na wananchi kwa ujumla kuwa, waendelee na shughuli zao ikiwemo kusafari kutoka eneo moja kwenda jingine bila ya hofu yeyote kwa kuwa hakuna dalili zozote za uvunjifu wa amani, usalama na utulivu wa nchi.Vyombo vya usalama vipo makini vinatekeleza majukumu yake ipasavyo kuhakikisha kuwa matukio yote ya uhalifu yanadhibitiwa kabla ya kuleta madhara kwa umma.  
Hivyo, Wizara inawaomba wanadiplomasia, raia wa kigeni wanaoishi nchini na wananchi kwa ujumla kuzipuuza taarifa hizo. Wananchi waendelee kushirikiana kwa karibu na Serikali yao kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo vinavyoaminika badala ya kutegemea propaganda za watu wanaotumia mitandao ya kijamii kwa maslahi binafsi.  
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dar es Salaam, 29 Machi 2018


WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI CHA KUPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA MJINI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma , Machi 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuongoza Kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018.
Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri cha Kupitia Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wapili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpamgo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) baada ya kuongoza Kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANAFUNZI UTUMISHI WATOA MISAADA KWENYE KITUO CHA KULELEA WAZEE WASIOJIWEZA CHA MWANZAN

0
0
CHUO cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga kimetoa msaada kwenye kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Mwanzange Jijini Tanga ikiwa ni mpango wao wa kuona namna ya kusaidia jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali.
Msaada uliokabidhiwa ni mchele kg 500, unga kg 300, sukari mifuko 2 kg100,sabuni ya unga mifuko 3,sabuni ya maji box 10,sabuni ya kuogeakatoni 2,maharagwe kg 100,chumvi katoni 10,mbuzi wawili.
Vitu vyengine ambazo vilikabidhiwa ni majani ua chai katoni 2,dagaa kg10,ngano kg 50,miswaki katoni 5,dawa za meno katoni nne,mafuta yakula ndoo tatu na mafuta ya kupikia katoni 10 vyote vina thamani yash.milioni 2.2
.
Akizung umza wakati wakikabidhi msaada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma JijiniTanga Elibariki Mushi aliwataka wanafunzi wajifunze taaluma hiyokatika mtazamo mpana ambao utawasaidia kuwajenga katika nyanja yakutatua changamoto zinazozikabili jamiihusika.
Mushi alisema mbali na wanafunzi hao ku jifunza mambo mbalimbali yauga vi na utawala pia wanaowajibu wa kuona umuhimu wa kujali jamii hasazile zinazoishi katika mazingira magumu.
“Tunaimani wanafunzi wetu wanajifunza masuala  ya  kuutumikia um ma lakini lazima wajikite kuangalia uhalisia halisi katika jamii zetuzinazotuzunguka na tukifanya hivyo tunaweza kuzifikia malengo yakuzisaidia jamii zilizo katika maisha duni”Alisema.
Aidha alisema swala la maadili lipo katika mitaala ya masomo yao hivyolazima wanafunzi hao wajifunze kivitendo kusaidia jamii h itajikaambapo walijitolea kupitia michango yao kwa kujitolea vyakula.

Awali kziungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzange Jijini Tanga Otilia Chilumba aliwashukuru huku akiwataka kuwa makini kwa kuzingatia masomo ili waweze kupata manufaa kwenye maisha yao  
“Ndugu zangu niwaambieni kuwa ujana ni maji ya moto tuutumie vizuri lakini pia acheni kukataa mimba mnazowapa wasichana mtoto utakayemzaandie anaweza kuja kukuokoa baadae “Alisema.
“Wapo baadhi ya wazee walishawahi kunililia walikwisha kuwate lekeza  watotowao ndio sababu za kuwepo kwenye kambi za kulea wazee hivyo niwasihiacheni kuwakataa kwani mnaweza kukumbana na changamoto mbeleni
  Alieleza pia sababu za baadhi ya wazee wengi kuishi maisha ya t a bu na kulazimika kulelewakwenye vituo maalumu imeelezwa kuchangiwa na baadhi yao kuwakanawatoto wao jambo ambalo linawapelekea kujikuta wakiingia kwenyechangamoto za namna hiyo.
Hatua hiyo inat ajwa kuwapa majukumu mazito wasichana ambao wamekuwaw akikumbana na kadhia hiyo ambao kwa asilimia kubwa wanakuwa wakiishikwa manunguniko (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Tanga Elibariki  Mushi  wa pili kutoka k ulia ni akimkabidhi vyakula na vifaa Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza MwanzangeJijini Tanga Otilia Chilumba kutoka kwa wanafunzi wa chuo cha utumishiwa Umma tawi la Tanga ikiwa ni mkakati wa kusaidia jamii isiyojiweza kulia ni Dastan Kingalu ambaye ni Mratibu wa shughuli hiyo
 Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Tanga Elibariki  Mushi  wa pili kutoka kulia ni akimkabidhi mbuzi mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kwa niaba ya wenzake

EFM YAWEKA MILIONI 300 SHIKA NDINGA KWA MIKOA SITA

MBOWE NA WENZIE WATANO CHADEMA KULA PASAKA MAHABUSU

Habari za UN: Ndio sisi ni Albino, hata mikate tukioka hamnunui?

NSSF YADAI ZAIDI YA BILIONI 58 KWA WAAJIRI

MBULU YAPATIWA FEDHA ZA KUHAMIA HAYDOM

0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, imepokea kutoka serikali kuu kiasi cha sh1 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu mapya yatakayojengwa Mji mdogo wa Haydom. Pia, kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 Halmashauri hiyo imetengewa sh. 2.3 bilioni za ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba za kuishi watumishi. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hudson Kamoga aliyasema hayo jana wakati akizungumza juu ya mikakati ya ujenzi wa makao makuu mapya yatakayojengwa Haydom. Alisema baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo kupitisha uamuzi wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kuwa Haydom, hivi sasa wapo kwenye mchakato wa utekelezaji. 

“Hadi mwakani kipindi kama hiki tutakuwa tumeshahamia kwenye makao makuu mapya ya halmashauri yetu kule Haydom na kuondoka hapa Mbulu mjini,” alisema Kamoga. Alisema awali Mbulu iligawanywa mwaka 2015 na kuwa na halmashauri mbili ya mji na wilaya, hivyo huu ni wakati wa kujenga ofisi zao mpya kwa lengo la kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi. 

“Tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kutupatia fedha hizo za ujenzi wa makao makuu mapya ya halmashauri yetu ya wilaya,” alisema Kamoga. Mkazi wa mji mdogo wa Haydom, Paul John alishukuru uamuzi wa kujengwa makao makuu mapya kwenye eneo hilo tofauti na uamuzi wa awali wa kujenga Dongobesh. 


“Huku kuna huduma mbalimbali za kijamii nyingi ikiwemo kituo kikubwa cha polisi, benki hospitali kubwa, tofauti na Dongobesh ambayo haina hata benki,” alisema John. Mkazi wa Dongobesh Aloyce Martin alisema kuenea kwa unywaji na biashara ya pombe haramu ya gongo kwenye eneo hilo kumewagharimu hadi kusababisha makao makuu mapya ya halmashauri hiyo yakahamishiwa Haydom. 

“Makosa ni ya kwetu sisi wenyewe kwani tulipata nafasi badala ya kuitumia ipasavyo sisi tukaichezea hadi ikawadondokea watu wa Haydom,” alisema Martin.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akimkabidhi zawadi ya daftari mwanafunzi wa darasa la tatu wa shule ya msingi Barazani Kata ya Maghang, Julieth John kutokana na utunzaji bora wa vyanzo vya maji na mazingira, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akizungumza na wananchi wa Kata ya Maghang juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji. 

ROMA MKATOLIKI, PRETTY KIND WARUDISHWA KWA MASHABIKI

0
0
Na Leandra Gabriel, globu ya jamii

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe leo Machi 29 ametoa tamko kuhusu wasanii waliofungiwa kazi zao za sanaa.

Akizungumza jijini Dar es salaam Dk.Mwakyembe ameeleza kuwa Serikali haina ugomvi na msanii yeyote ila ugomvi wao upo katika suala la mmomonyoko wa maadili na suala hilo halitofumbiwa macho, pia ameeleza kuwa kuna mipaka katika kulinda maadili na wasanii ndio mabalozi, kuhusu suala la Abdul Naseeb maarufu kama Diamond la kutoa kauli nzito mtandaoni Mwakyembe amesema kuwa wanampenda sana Diamond na wanataka afike mbali zaidi na amefurahi sana kwani vijana hao wameelewa.

Akieleza maamuzi hayo naibu Waziri wa wizara husika Juliana Shonza amesema hawana ugomvi wala chuki na msanii wa Tanzania na kuhusu suala msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty kind amesema amefurahishwa na hatua alizochukua kama kujisajili katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wanaamini amebadilika hivyo wanamsamehe adhabu yake iliyotakiwa kuisha Julai Mosi mwaka huu.

Pretty kind ameshukuru Wizara pamoja na Baraza la sanaa la taifa (BASATA) kwani kupitia wao amejifunza mengi na atakuwa balozi mzuri wa maadili nchini na amewashauri wasichana hasa wasanii kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na BASATA na wabadilike kupitia yeye.Kuhusu suala la Roma Mkatoliki, Shonza ameeleza kuwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilimpa maelekezo ya mabadiliko ya wimbo wa kibamia na kuhudhuria kikao kilichopangwa na Baraza hilo vitu ambavyo Roma hakuvitekeleza.

Aidha Shonza ameeleza kuwa Roma aliandika barua ya kupunguziwa adhabu ombi ambalo wamelipokea ila lazima akajisajili BASATA pamoja kufanya marekebisho ya wimbo huo.Baada ya msanii Roma kuamua kwa ridhaa yake mwenyewe mbele ya vyombo vya habari kwamba wimbo huo uondolewe kabisa kwenye vyombo vya habari hasa kwa mfumo wa sauti na video Waziri Mwakyembe amesema kuwa pindi atakapokamilisha usajili wake na kuwa na hati kutoka BASATA adhabu yake itakuwa imeishia hapo.

Mwisho waziri Mwakyembe amewaomba wasanii kuwa mabalozi wa maadili ya watanzania kwa kumnukuu baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kusema Taifa lisilo na maadili yake ni taifa mfu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza (katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii hao baada ya kuongea na wanahabari.

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WASANII WA FILAMU MKOANI ARUSHA

0
0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo akitoa maelekezo kwa wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu wa mkoa huo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha Bi. Irene Ngao akizungumza na Wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu yaliyofanyika leo jijini Arusha. Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.
Wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha wakifuatilia mafunzo ya uandaaji wa filamu yaliyofanyika leo jijini Arusha, mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania yamehusisha zaidi ya wasanii mia moja.
Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Arusha Mjini Bw. Antony Mushi akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha yaliyofanyika leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) akicheza ngoma na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Mtikisiko Sanaa Group cha jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu mkoani humo mapema hii leo. Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.PICHA ZOTE NA:OCTAVIAN KIMARIO,WHUSM

KIPINDI CH BBC DIRA YA DUNIA

DC MTWARA AKAGUA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MANGOPACHANNE

0
0
boi1
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mtwara Mh. Evod Mmanda metembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Mangopachanne Mtwara vijijini na kujionea ujenzi wa shule hiyo unavyendelea.Mh. Mmanda amemuaguza mkandarasi wa ujenzi wa shule hiyo kufanya kazi kwa bidii na kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa ili shule hiyo ianze kutumika na kuwasaidia wanfunzi kutotembea umbali mrefu kwenda kupata elimu.
boi2
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mtwara Mh. Evod Mmanda akitoa maagizo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo.
boi3
Diwani na wataalamu wa halmashauri nilioandamana na Mkuu wa wilaya huyo hayupo pichani mara baada ya kukagua ujenzi huo.

NAIBU WAZIRI MGALU AKAGUA KITUO CHA KUZALISHA,KUSAMBAZA UMEME MKOANI MTWARA

0
0


Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akikagua kituo cha uzalishaji umeme na kusambaza umeme mkoani Mtwara . wakati alipotembelea kituo hicho jana akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalaama Bw. Evod Mmanda.
Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akipata maelezo katika kituo cha uzalishaji umeme na kusambaza umeme mkoani Mtwara wakati akipokea ripoti ya kituo hicho alipotembelea akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalaama Bw. Evod Mmanda.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images