Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

TAIFA STARS, CONGO KUKIPIGA KESHO UWANJA WA TAIFA

0
0
Na Agness Francis Blogu ya Jamii
BAADA ya Taifa Stars kuchapwa mabao 4-1 dhidi ya Algeri wakiwa ugenini sasa wanawakaribisha nyumbani kikosi cha timu ya Taifa ya Jamuhuri  kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wao wa kirafiki.

Mchezo huo wa aina yake kati ya timu hizo mbili utachezwa kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni na kiingilio kwa VIP ni Sh.5000 na viti vya mzunguko na vyenye rangi ya Chungwa ni Sh.1000.

Akizungumza leo Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa Stars  Hemedi Moroccoleo, amesema mchezo utagumu kwao lakini amewahakikishia Watanzania kupata ushindi katika mchezo huo.

"Tunatarajia kufanya vizuri katika mchezo wa kesho ili kupata ushidi ili kusogea mbele kuwa kwenye nafasi nzuri  tutajitahidu kadri ya uwezo wetu kupambana kwa kuwa wenzetu wacongo wako vizuri na makini katika mchezo wa Soka" amesema kocha Morocco.
 Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemedi Morocco akizungumza na waandishi wa habari Leo katika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuhusu maandalizi ya kumenyana na Timu ya Taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasiya ya Congo katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kesho uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Kocha Mkuu wa Timu ya Congo, IBenge Florent akizungumza na wandishi wa habari leo katika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa miguu  Tanzania (TFF) akizungumzia ujio wao pamoja na maandalizi katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Timu hizo mbili utaokachezwa katika Dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Da ea Salaam.
Mchezaji wa Taifa Stars, Himidi Mau akizungumza na wandishi wa habari kwa ni aba ya wenzake   kuelekea kesho kwenye dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam  katika  mchezo wa kirafiki na Kikosi cha Congo Leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Nahodha wa Kikosi cha Timu ya Congo, Benic Adobe akizungumza na wandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu maandalizi ya mechi hiyo itakayochezwa kesho katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA

0
0
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Albert Ntabaliba akizungumza wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Wizara ya fedha na Mipango walioongozwa na Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019, katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Wizara ya fedha na Mipango (hawapo kwenye picha) wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Maria kangoye akizungumza wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Riziki Lulidi
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Wawekezaji Wazawa Wapewa Rai Kujenga Viwanda vya Dawa

MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Lauraean Bwanakunu pamoja na mafanikio ambayo wameyapata katika kutekeleza majukumu yao ya kununua, kusambaza, kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba, changamoto inayowakabili ni ya ununuzi wa vifaa vya kitaalam toka wazalishaji.

Ametaja baadhi ya vifaa hivyo ni  vya macho, meno, moyo na  figo ambapo vinaagizwa kwa uchache na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na ORIC.

Azungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya Rais John Magufuli  wakati wa uzinduzi wa magari mapya ya msaada ya kusambaza dawa ambayo yametolewa na Global Fund kwa MSD, Bwanakunu amesema wazalishaji wa vifaa hivyo wanaona oda ni ndogo na hivyo wamekuwa na wakati mgumu kupata.

Amemhakikishia Rais Magufuli kuwa, MSD wamejipanga kukabiliana na changamoto hiyo na mwezi ujao watazungumza na Shirika la IDA lililopo Denmark na wengine ili kuwakusanyia vifaa hivyo pamoja na nchi nyingine kwa lengo la kuwapunguzia gharama za manunuzi.

Amesema kampuni hizo hufanya manunuzi ya nchi mbalimbali ikiwemo umoja wa mataifa na hivyo wanataka kufaidika na mfumo huo.

Bwanakunu amemueleza Rais Magufuli , changamoto ya pili wanayokabiliana nayo ni ya maoteo kutokana na kutokuwa sahihi na kufanya suala la ununuzi kuwa la kubahatisha.

Akizungumzia kuongezeka kwa bajeti ya kununua dawa kutoka Sh.bilioni 31 hadi Sh.bilioni 250, Bwanakunu amesema yale yalikuwa maajabu na kama ndoto na kila mtu kwenye mnyororo wa ugavi alichanganyikiwa ghafla.

"Kuna zahanati ilikuwa inapata dawa za Sh.400,000 kwa mwaka na sasa inapata Sh.milioni 10. Furaha hii haikuwa kwa vituo vya kutolea huduma za afya , watumishi wa afya lakini zaidi sisi watumishi wa MSD umetuondolea kero ya Watanzania kudhani mtu akiumwa na mbwa au nyoka basi shida ni MSD wakati hatuna fedha za kununua dawa hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC MATIRO APIGISHA KURA ZA SIRI KUBAINI WAUAJI WA WANAWAKE SHINYANGA VIJIJINI

0
0
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Kufuatia kuibuka kwa taarifa za kuwepo kwa mauaji ya wanawake yanayoambatana na imani za kishirikina katika kata ya Salawe wilaya ya Shinyanga, mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro amefanya mkutano na wananchi wa eneo hilo kwa ajili ya kutafuta chanzo na ufumbuzi kumaliza mauaji hayo.

Wananchi wa kijiji cha Songambele kata ya Salawe wanasema mauaji hayo yameanza kutokea tangu mwezi Desemba mwaka jana wakidai kuwa wanawake hukatwa mapanga ama kunyongwa na watu wasiofahamika ambao hutoweka na viungo vya siri vya wanawake wanaowaua. 

Inaelezwa kuwa katika kipindi cha  Januari Mosi hadi Machi 23 mwaka huu watu waliouawa katika kata hiyo ni wanne huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina.Kutokana na hali hiyo Mkuu wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, alifika katika kata ya Salawe kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mauaji hayo kwa njia ya kuwashirikisha wananchi.

Aidha baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa hadhara,mkuu huyo wa wilaya aliagiza kufanyika/kupigwa kwa kura za maoni kwa ajili ya kuwabaini wahusika wa mauaji hayo na kuondoka na kura hizo kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wananchi kutoa ushirikiano katika vyombo vya sheria ili kukomesha mauaji katika kata ya Salawe
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAHANDISI WA BAM INTERNATIONAL WASHAURI WASICHANA WAPENDE MASOMO YA SAYANSI

Introducing Brand New Linex "I'M Sorry" Audio/Video

Wagombea Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV MArekani Waongea Baada ya Matokeo ya Uchaguzi


MWALIM MKUU KAKONKO AJINYONGA AKIWA OFISINI KWAKE,AANDIKA UJUMBE MZITO

0
0

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi.

Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi.

Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini.

Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii, na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),alifika nyumbani kwake juzi akitokea Dodoma.

Kwa upande wa Mlinzi wa Shule hiyo Kajolo Kajabojabo amesema alikutana na Mkuu wa shule mapema asubuhi akiingia ofisini na kumuomba chaki ambazo alipewa na kuziwasilisha kwa walimu."Nilimuona kabisa tukasalimiana, nikamuuliza kama anaweza kuwa na chaki, akaingia ofisini akanipatia boksi moja la chaki.Nikachukua na kisha nikampelekea mwalim aliyehizihitaji, alikuwa kwenye hali nzuri tu, lakini baada ya muda ndo tukio hilo likatokea,"amesema Kajoro.

Akizungumza baada ya kufika shuleni hapo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua sababu ikiwa marehemu aliacha ujumbe wowote au laa.Hatujajua sababu lakini ni muhimu jamii ikajenga utamaduni wa kueleza matatizo ya ndani yanayoyasibu.Hiyo inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuepusha madhara kama haya,"amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno amesema baada ya kupekuliwa kwa mwili wa marehemu walikuta karatasi imeandikwa ujumbe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi asipodhibitiwa ataua wengi.

"TUNA WAJIBU WA KULINDA UTAMADUNI WA NCHI YETU"-WAZIRI MWAKYEMBE

MAVUNDE AIPONGEZA OSHA KUBORESHA UTENDAJI WAKE

0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mh. Antony Mavunde, ameupongeza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa jitihada unazozichukua katika kuimarisha hali ya usalama na afya katika sehemu za kazi nchini.

Mh. Mavunde alizitoa pongezi hizo alipozungumza na wafanyakazi wa OSHA katika kikao cha pili cha baraza la tatu la watumishi hao kilichofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

“Niwapongezi kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuboresha hali ya usalama na afya katika maeneo ya kazi hapa nchini. Kwakweli kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika utendaji wenu hasa katika kipindi cha hivi karibuni,” alisema Mh. Mavunde.

Aliongeza: “Kipindi cha nyuma mlikuwa mnafanya kazi zenu kama askari polisi jambo ambalo lilikuwa linawapa hofu kubwa wadau wenu ambao badala ya kuuelewa wajibu wao kisheria na kuutekeleza, waliishia kuwakwepa na kuwalalamikia.”

Kiongozi huyo wa serikali alieleza kwamba kwasasa watumishi wa OSHA wamekuwa wakijitahidi kufanya kazi kwa weledi mkubwa ikiwemo kuwaelimisha wadau ili waweze kuutambua wajibu wao kisheria na kuutekeleza bila kushurutishwa.
Wafanyakazi waliokingwa ipasavyo wakifanya kazi za ujenzi katika mradi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu ya kwanza ya mradi huo. OSHA huhakikisha kwamba wafanyakazi wanafanya kazi zao katika mazingira salama.


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

DKT KALEMANI ATOA MAAGIZO WAKANDARASI WA REA NCHINI

0
0
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wakala wa nishati vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki ili kutoa fursa ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo muhimu. 

Dkt Kalemani aliyasema hayo jana wakati akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III) katika kijiji cha Magumbani kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga. 

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uwashwaji wa huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili kuwawezesha kupata huduma hiyo ilikuwa haipo awali katika eneo hilo,Alisema kwani hayo ndio malengo waliowapa ikiwa ni mpango mkakati wa kuha kikisha wanafikia malengo ya kuwapelekea umeme watanzania wote ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze kunufaika kupitia huduma hiyo .

“Leo tutaangalia mlipowasha lakini niwaagize wakandarasi tunataka kuona kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kwani wananchi wanauhitaji mkubwa wa kufikiwa na huduma hiyo hivyo hakikisheni hilo mnalitilia mkazo mkubwa “Alisema. 
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii ch a Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Y ona Mark na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuluni Selemani Omari
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waataalamu mbalimbali wanaotekeleza mradi wa rea awamu ya tatu mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 27,2018

Waziri Mwakyembe atangaza rasmi Maudhui ya Mtandaoni.


FUATILIA HAPA MOJA KWA MOJA: CAG AKIWASILISHA RIPOTI YAKE KWA RAIS DKT. MAGUFULI

0
0
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja muda huu ambapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) anawasilisha ripoti yake kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

TAARIFA YA KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI YA DRFA

0
0
Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) iliketi Machi 25, 2018 katika kikao cha kawaida kinachofanyika kila baada ya miezi mitatu kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni kama yafuatayo:

1. KUZINDULIWA KWA MPANGO MKAKATI (Stategic Plan) WA MIAKA MINNE

Mara baada ya Uongozi huu wa DRFA kuingia madarakani uliazimia kuandaa mpango mkakati wa miaka minne ambao ulibuniwa ili kuepuka kuendesha chama bila mipango iliyoainishwa kabla. Mpango huo utakaozinduliwa siku moja kabla ya mkutano mkuu wa DRFA.

2. MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU

Mkutano mkuu wa DRFA umepangwa kufanyika kabla ya mwezi wa sita huku jukumu la kupanga mahali na tarehe maalum likiachwa kwa Sekretarieti ambayo itatangaza hivi karibuni. Mkutano huu ni wakikatiba na wajumbe wake wametajwa kwenye katiba, kwa maana viongozi wa wilaya na vingozi wa vyama shiriki.

3. MAANDALIZI YA MAFUNZO YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA SOKA

Baada ya kufanikiwa katika kozi ya kwanza ya makocha wa soka la vijana iliyomalizika mwanzoni mwa mwezi huu, DRFA inaandaa kozi nyingine awamu hii ikigeukia upande wa uongozi wa klabu na vyama vya soka. Lengo la kozi hii ni kuwaongezea uwezo na utaalam viongozi wa soka mkoani Dar es Salaam ili kuhakikisha klabu na vyama vya soka vinaongozwa na watu wenye weledi kwa manufaa ya soka la mkoa huu na taifa kwa ujumla. Hii itafanyika Aprili katika tarehe itakayotangazwa na sekretarieti hivi karibuni. Kozi hiyo itafuatiwa na nyingine ya waamuzi ambayo ina lengo la kuongeza idadi ya waamuzi wenye uwezo mkubwa mkoani Dar es Salaam.

4. MWENENDO WA LIGI YA MKOA

Ligi ya mkoa inaendelea vizuri katika hali ya utulivu bila kuwa na malalamiko mengi toka kwa klabu. Hii imetokana na usimamizi kabambe uliowekwa na DRFA katika vituo vyote ili kuhakikisha sheria 17 za soka zinafuatwa wakati wote. Ni imani ya DRFA kwamba usimamizi huo utapelekea kupatikana kwa wawakilishi watatu watakaokwenda kuonyesha ushindani wa kweli kwenye ligi daraja la pili ngazi ya Taifa. Ligi hiyo yenye makundi matatu inatarajiwa kumalizika Machi 30 huku mechi zake zikichezwa kila siku katika viwanja vitano tofauti.

5. UGENI TOKA ZANZIBAR

Kuna uhusiano mkubwa uliodumu kwa miaka mingi kati ya DRFA na chama cha soka mkoa wa Mjini Magharibi ambapo kila mwezi wa nne vyama hivi hutembeleana kwa zamu kwa ajili ya kujadili na kupeana ushauri wa masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya soka. Mwaka huu DRFA itatembelewa na ndugu zetu wa Zanzibar hivyo kamati hiyo imeandaa utaratibu wa mapokezi ya maafisa wa chama hicho watakaokuja ikiwa ni pamoja na mchakato mzima wa uwepo wao hapa jijini Dar es Salaam.

6. MAANDALIZI YA LIGI YA MKOA YA VIJANA (U15) IJULIKANAYO KAMA NDONDO ACADEMY

Baada kuzalisha makocha 25 wa soka la vijana katika kozi iliyomalizika Machi 10, DRFA iliwaagiza kwenda kuitumia elimu waliyoipata kwa kufundisha vijana kwenye vituo mbalimbali kukuza soka la vijana (Academy). Michuano ya Ndondo Academy si tu imeandaliwa kwa ajili ya kuibua vipaji vipya, bali pia ni katika kupata mwendelezo bora wa progaramu ya maendeleo ya soka la vijana iliyoanza kwa mafunzo ya ukocha. Ligi hii itasimamiwa kwa pamoja na Kamati ya Soka la Vijana na Kamati ya Mashindano ya DRFA.

7. MAANDALIZI YA LIGI YA MKOA YA WANAWAKE CHINI YA MIAKA 15 (U15) 

Kamati ya Utendaji ya DRFA imegundua kwamba idadi ya wasichana walio na utayari wa kuchezo soka imepungua na kwamba hakuna chanzo maalum cha kuzalisha wachezaji wapya. Kwa kuliona hilo DRFA imeamua kufungua 'kiwanda' cha nyota wapya wa soka la wanawake kwa kuanzisha ligi ya vijana, ligi itakayosimamiwa na Chama cha Soka la Wanawake, Kamati ya Soka la Vijana na Kamati ya Mashindano ya DRFA.

Ahsante
Karim Boimanda
Afisa Habari na Mawasiliano
DRFA

RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema mtumishi yoyote wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto atakayecheleweshwa dawa na vifaa tiba kutoka bandarini atamchukulia hatua mara moja.

Ametoa kauli hiyo kutokana na taarifa alizonazo kuwa kuna ucheleweshaji wa dawa zinapofika bandarini na hivyo akatoa msimamo wake asisikie dawa zinachelewa kutolewa na iwapo ucheleweshwaji huo unafanywa na waliokuwa wizarani hapo basi ni vilaza.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa akizindua magari mapya 181 yaliyotolewa msaada na Global Fund kwa Bohari ya Dawa(MSD),ili yatumike kusambaza dawa, Rais amesema hataki kusikia tena kuwa dawa zinapofika bandarini zinacheleweshwa.Amesema hatasita kuchukua hatua kwa yoyote ambaye atabainika kuhusika a kukwamisha kwani upo uwezekano wa kukwamishwa kwa dawa za Serikali halafu nyingine za watu binafsi zikatolewa kwa wakati.

Wakati anazungumzia suala hilo la ucheleweshwaji wa dawa bandarini alihoji kama wanaotoa kibali ni Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA) au laa.Hata hivyo akaelezwa jukumu hilo lipo chini ya Wizara ya Afya.Amewaambia viongozi wa Wizara hiyo dawa zinapoingia bandarini zitolewe haraka ili ziende kutumiwa na watanzania kuokoa maisha yao kwani kuna uwezekano wakati dawa zinacheleweshwa bandarini kuna wagonjwa wanapoteza maisha kwa kukosa dawa.

Pia akafafanua au kama wizarani watashindwa kumchukulia hatua anayekwamishwa dawa kutoka kwa wakatai bandarini basi atakachokifanya ni kuwatumbua wote walioshindwa kuchukua hatua na yule ambaye anakwamisha atampa nafasi.

"Kama kuna mtu anakwamisha dawa zisitolewe kwa wakati na wote mliokuwa wizarani mnatii maana yake ni kwamba huyo anayekwamisha ana nguvu kuliko ninyi."Hivyo nitampa nafasi yeye na ninyi nitawaondoa.Wala siwatishii lakini niwaambie ukweli sitaki kusikia habari ya dawa kuchelewa tena bandarini,"amesema Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaingia madarakani moja ya eneo ambalo lilikuwa ni changamoto ni uhaba wa dawa lakini anafurahi kuona hali kwa sasa iko vizuri na ametoa kipaumbele kwa wizara ya afya kwani ni moya wizara ambayo bajeti yake inatengewe fedha nyingi.

MEYA WA JIJI LA DAR ATOA NENO ZITO KUHUSU JPM

TANZIA

0
0
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, ndugu Nyakimura M. Muhoji  anasikitika kutangaza kifo cha Bibi, Hafsa Anzerani Mrisho aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, “DAHRM” Tume ya Utumishi wa Umma kilichotokea usiku wa leo Jumanne tarehe 27 Machi, 2018 Dar es Salaam.
Msiba upo nyumbani kwa baba wa marehemu Mzee Shabani Mrisho, Mwananyamala Koma Koma, Karibu na Kanisa la Anglikana. Mazishi yatafanyika leo siku ya Jumanne tarehe 27 Machi, 2018 saa 10 jioni baada ya Swala, katika makaburi ya Mwananyamala.
Habari ziwafikie:-
1.Dkt. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma akiwa Dodoma.
2.Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, wa Dar es Salaam.
3.Bw. Adam Mayingu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
4.  Watumishi wote wa Umma, Ndugu, Jamaa na Marafiki   popote walipo.


Tumeya Utumishi wa Umma inatoa Pole kwa Familia na Wote walioguswa na Msiba Huu. “Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi – Aamiin”

“Inna Lillah wa Inna Illayhi Rajiuni”

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images