Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu

$
0
0

Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akionesha kitabu cha vyeti vya kuzaliwa pamoja na simu ya kisasa alipozindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill. Kulia ni Mwenyekiti was Bodi ya RITA, Prof. Hamisi Dihenga. 

MARA  – Mkoa wa Mara na Simiyu imezindua kuanza kwa mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watoto 700,000 walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo. 

Uzinduzi huo uliofanyika katika mji wa Musoma, ulihudhuriwa na Mheshimiwa Waziwa wa Katiba na Kisheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, UNICEF na Mwakilishi wa Serikali ya Canada na wageni wengine mashuhuri. Mfumo huo wa usajili uliorahisishwa utasaidia usajili wa watoto wote wachanga na kupunguza idadi kubwa ya watoto ambao hawajasajiliwa walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo miwili. 

Mfumo huu ambao unajitegemea usio ratibiwa kutoka serikali kuu unasogeza huduma ya usajili karibu na jamii. Inaanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya, ambavyo vinatoa huduma ya afya ya uzazi na watoto, na kwenye jamii katika ofisi za mtendaji wa kata kuendana na sera ya serikali ya ugawaji wa madaraka kwa serikali mitaa.  

Zoezi hili limeziba pengo la mijini na vijijini, kwa kuzipa jamii za pembezoni nafasi ya kusajili watoto wao. Inatatua suala la msingi la upatikanaji na uwezo wa kumudu jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa katika usajili wa vizazi nchini Tanzania. 


WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMKIA KAZI ZA BARABARA

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema itahakikisha wanawake walio katika Sekta ya Uhandisi na Ukandarasi wanapata fursa za kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na matengenezo ya barabara.Hatua hii inalenga kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika sekta hiyo ili kufikia lengo la kuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza mkoani Morogoro, wakati wa ufungaji wa semina elekezi kwa waratibu wa mikoa wa ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka ofisi za Wakala wa Barabara (TANROADS), mikoa yote Tanzania bara, Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali, amewashauri kuwa mabalozi wazuri wa kuwahamasisha na kuelimisha wanawake katika maeneo yao ya kazi kuchangamkia fursa hizo.

Aidha amewaasa waratibu hao kuhakikisha wale wanawake ambao tayari wamefanikiwa kupata kazi hizo zifanywe kwa kuzingatia ubora, gharama nafuu na kuzingatia muda uliopangwa kwenye mkataba.Bw. Mliyapatali ametumia fursa hiyo kutoa wito na kuwahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao hususan wa kike katika Vyuo vya Ufundi ili kupata ujuzi wa masuala ya Ujenzi utakaosaidia kuondoa dhana kuwa masomo ya ufundi ni kwa ajili ya watoto wa kiume tu.

“Mimi pia ni mwalimu hapa chuoni, kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa ukimfundisha mtoto wa kike anakuwa mahiri na weledi wa hali ya juu, tofauti na mtoto wa kiume”, amesema Bw. Mlyapatali.Kwa upande wake Mratibu wa kitengo cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Rehema Myeya, amewahimiza waratibu walioshiriki semina hiyo kutoka Mikoa mbalimbali kuwa chachu ya maendeleo katika vituo vyao vya kazi na kuhakikisha kuwa wanawake watakaopata kazi za ujenzi au matengenezo ya barabara zinakuwa katika viwango vinavyokubalika.

Naye Mratibu kutoka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Prisilla Mushi, ameahidi kusimamia, kuelimisha, kuhamasisha na kutoa msukumo kwa jamii katika ushiriki wa wanawake kwa kutumia teknolojia katika kazi za barabara.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Rehema Myeya, akimkaribisha Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali, kufunga semina elekezi kwa waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania bara, mkoani Morogoro.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck  Mlyapatali, akifunga semina elekezi kwa waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka mikoa yote ya Tanzania bara (hawapo pichani), iliyokuwa na lengo la kuwajengea ujuzi, uwezo na njia mbadala za kuongeza idadi ya wanawake katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, mkoani Morogoro.

Baadhi ya waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka mikoa yote ya Tanzania bara wakifurahi jambo wakati wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw.  Melkzedeck Mlyapatali, wakati akifunga semina elekezi iliyoandaliwa na Wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), na kufanyika katika ukumbi wa chuo hicho mkoani humo.

Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck  Mlyapatali (kulia aliyekaa kwenye kiti) akiwa na waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka mikoa yote Tanzania bara, mjini Morogoro. Pembeni yake ni Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Rehema Myeya.

WATU 26 wamefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa ajali iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani .

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK inayofanya safari zake Kimanzichana - Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya Mkuranga.Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi 10 ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Inasemekana majeruhi waliopelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wengine wao wamekatika viongo mbalimbali vya mwili.Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya.Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega ,aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini .
Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe.

"Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao." alieleza Ulega.



WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

$
0
0
Na Hamza Temba, Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic Affairs-SECO.


Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza  ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.


"Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la  Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja  iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 26 ajali Mkuranga, Pwani

Kampuni ya Pennyroyal, Internalional Volunteers Oman wakabidhi Viti na Meza Skuli ya Sekondari,Msingi Matemwe Zanzibar

$
0
0


Pennyroyal Limited kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar wakishirikiana na International Volunteers kutoka Oman wametoa msaada wa madawati 200 yenye thamani ya Tsh 18,000,000/- ( Shilingi millioni kumi na nane).

Akiongea katika sherehe za kukabidhiana, Mkurungezi Mkuu Bw. Brian Thomson alikua na haya ya kusema:“Best of Zanzibar imejitolea kuboresha elimu katika shule za Kijini na Mbuyu Tende. Tumejiwekeza katika progamu tofauti za kielimu katika shule hizi mbili zikiwemu Masomo ya ziada (After Hours Tutoring program) kwa wanafunzi 500, na kuwasomesha walimu 30 masomo ya lunga ya Kingereza na mbinu za kufundishia ili kuongeza uwezo na ujuzi wa walimu hao.

Tunawashukuru sana International Volunteers kwa moyo wao wa kujitolea na kushirikiana nasi katika kutoa huduma kwa mashule.”Mkurungenzi huyo alisisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii na ukuwaji wa uchumi wa nchi, ndio maana Best of Zanzibar imejikita katika uboreshaji wa elimu Zanzibar.

“Nia yetu kuu ni kuleta manufaa na kuedeleza msingi mzuri wa kiuchumi Zanzibar. Kwa muda mrefu sana watoto wa shule ya msingi Kijini na Mbuyu Tende wamekaa chini bila madawati kuwaletea ugumu katika kuelewa masomo na kupunguza ufanisi wao wa masomo.

Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti 205,Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal, kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Mwakilishi wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar Mohammed Issa akitowa maelezo kabla ya hafla ya makabidhiano wa vifaa kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.
Mwakilishi wa International Volunteers Oman Danny Kim akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205, kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja Skuli hizo zinapata ufadhili kupitia Mradi wa Bset of Zanzibar, uliooko chini ya Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar, inayojenga kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar. 
Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibar B. Safia Rijal akizungumza wakati wa hafla hiyoya kukabidhiwa Viti na Meza 205 kutoka kwa Mradi wa Best of Zanzibar kwa kushirikiana na Internalional Volunteers Oman, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.na kuhudhuriwa na Wananchi wa kijiji hicho. 

WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WATETEZI wa Rasilimali wasio na Mipaka-WARAMI wameupinga waraka wa Ujumbe wa pasaka kutoka kwa baraza la maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) uliotolewa jana, kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Da res Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI, Philipo Mwakibinga amedai kuwa maskofu kama viongozi wa dini wanatakiwa kujikita katika masuala yanayohusu dini na si siasa.

“WARAMI tunaamini kwamba wajibu wetu ni kuhakikisha jamii inapata haki pasipo upendeleo wowote, kufuatia hili tumeona si sahihi kukaa kimya, tukaona tupaze sauti kuona tunaijenga jamii kulingana na tofauti zao. Kwenye nafsi zao wanavyo vyama vyao mbali na uongozi wa kidini. Hisia za kivyama zisilete mtafaruku kwenye Imani. Wajitafakari kuchagua aina ya maneno wanayotoa kwa jamii ili kulinda na kukuza amani,” amesema na kuongeza.

“Tunashangaa kwa nini waraka huu wa salamu za pasaka haukujikita katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma biblia na maandiko mengine ya dini na badala yake wanajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza.”

Mwakibinga amedai kuwa, Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka huo ni malalamiko kuhusu mchakato wa katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni, ambao ulikwamishwa na wansiasa wa upinzani waliosusia kushiriki mchakato huo.  

“Maaskofu wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini hawajajikita kuelezea kwa kina kisa hasa ni kipi. Sisi tunafahamu kuwa wapo walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa baadhi ya vijana ambayo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo,” amesema.
 Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini katika ukumbi wa Traventine Magomeni.

KUELEKEA UCHUMI WA KATI, BAOBAB WAFUNGUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MITA ZA LUKU

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WAZIRI wa nishati mh. Menard Kalemani leo Machi 24 ametembelea kiwanda kipya cha utengenezaji wa mita za luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) kilichopo Goba jijini Dar es Salaam.

Kalemani ameeleza kuwa lengo la kutembelea kiwanda hicho ni kukagua na kujiridhidha ili kutoa zuio la kuagiza mita nje ya nchi.

Aidha Kalemani amefurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho ambacho huzalisha mita 38 elfu kwa mwezi na mita 56 elfu kwa mwaka ambayo ni zaidi ya mahitaji ya TENESCO na REA ambao huhitaji mita 20 elfu pekee kwa mwezi hivyo wamejiridhisha na uwezo wa kiwanda na kutoa miezi mitatu ya matazamio baada ya hapo hakuna mita zitakazoagizwa nje ya nchi.

Pia Kalemani ameeleza sababu za kuanzishwa viwanda hivi ni kwenda sambamba na uchumi wa viwanda, urahisi katika upatikanaji wake na ubora.Pia ameeleza faida za mita hizi ambazo ni pamoja na kuongeza mapato kwa TANESCO, kudhibiti wizi wa umeme kwa asilimia 90 kwa kuwa mita hizi ni za kisasa, kuokoa umeme wa asilimia 38 unaopotea kila siku na kuondoa kero kwa wateja.

Amewataka wawekezaji wawe na ushindani kwa kufungua viwanda kama hivi maeneo mengine ili kurahisisha usafirishaji kwani hadi sasa ni viwanda viwili tuu ndivyo vinavyozalisha mita hizi na kuwataka waendeleze viwanda hivi. Pia ametoa rai kwa TANESCO na REA kufanya kazi kupitia teknolojia hii ili kuepukana madeni na mizigo na amewataka wananchi kuwekeza kwenye miundombinu ya nishati kama Baobab.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Hashim Ibrahim amemshukuru waziri na kueleza kuwa wanaunga mkono sera ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda, na kufafanua kuwa kiwanda hiki kilianza kufanya kazi Machi 15 mwaka huu na walianza kama wasambazaji wakishirikiana na TANESCO kwa zaidi ya miaka 10 na amehaidi kufanya kazi na TANESCO katika upatikanaji, usambazaji na uhifadhi kama walivyokuwa wanafanya kazi miaka iliyopita.

Mtaalamu wa IT wa Kampuni hiyo Isaya Hezron ameeleza kuwa wameungana na kampuni ya EDMI ya Singapore ili kuweza kurahisisha huduma kwa wateja wake aidha ameeleza kuwa mita hizo hufanyiwa matengenezo pindi zinapoharibika tofauti na mita nyingine pia mita hizi ni zilezile zinazohitajika na TANESCO kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.

 Waziri wa Nishati,Menard Kaleman azungunza na akifafanua jambo mble ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mita za luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) kilichopo Goba jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Mita za Luku, Hashim Ibrahim(kulia) akitoa maelezo mafupi mbele ya Waziri wa Nishati,Menard Kaleman leo alipotembelea kiwanda hicho.
 Waziri wa Nishati,Menard Kaleman (wakwanza kushoto) akiwa ameambatana na viongozi mblimbli wakiwasiri katika kiwanda cha kutengeneza mita za luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) kilichopo Goba jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa IT wa Kiwanda hicho,Isaya Hezron akijibu maswali ya waandishi wa hari leo jijini Dar es Salaam. 
Wafanyazi wakiwanda hicho wakiendelea na kazi.

(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

JOKETI 'ATUMBULIWA' NAFASI YA KATIBU UHAMASISHAJI UVCCM

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

KAMATI ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Chama Cha Mapanduzi(UVCCM) imemtema Jokate Mwegelo kwenye nafasi ya Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa jumuia hiyo uanzia leo.

Uamuzi huo umetolewa leo Mjini Dodoma huku sababu za kuondolewa kwake zikiwa hazijawekwa bayana.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia simu ya mkononi akiwa mkoani Dodoma,Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema Jokate ameondolewa kwenye nafasi hiyo ambayo kimsingi alikuwa anaikamu na ameitumikia kwa mwaka mmoja.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya UVCCM ,Baraza Kuu la jumuiya hiyo ndio lenye jukumu la kuteua jina kwa ajili ya kulipendekeza na kulipitisha kwenye nafasi hiyi lakini Jokate alipata nafasi hiyo kupitia Kamati ya Utekelezaji.

Amesema hawezi kusema ni sababu gani ambayo imesababisha aondolewe lakini moja ni hiyo ya kwamba wenye uwezo wa kupitisha jina kwenye nafasi hiyo ni Baraza Kuu na yeye aliipata kupitia Kamati ya Utekekezaji.

Ameongeza ifahamike Jokate alikuwa anakaimu tu nafasi hiyo na unaweza kuilezea kama alikuwa bado kwenye majaribio ,hivyo nafasi hiyo itajazwa baada ya Baraza Kuu Kukutana kwenye kikao chake kwani leo haikikuwa kikao cha baraza.

"Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM ndio iliyotoa uamuzi huo na si  Baraza Kuu la jumuiya yetu.Kamati hiyo ndio ilimkamisha nafasi hiyo na ndio iliyomuondoa," amesema Shaka.

Alipoulizwa sababu za msingi za kumuondoa kwenye nafasi hiyo ni zipi?Shaka amejibu ni mapema kusema sababu   ila kikubwa alikuwa anakaimu nafasi hiyo na sasa ametenguliwa.

"Ujue unapokuwa umakaimu nafasi inakuwa ni kipindi cha majaribio na lolote linaweza kutokea aidha kuthibitishwa kwenye nafasi unayokaimu au kutothibitishwa," Shaka.

Kuhusu kikao cha leo amefafanua hakikuwa kikao cha Baraza Kuu la UVCCM bali ilikuwa ni semina elekezi kwa vijana wa jumuiya hiyo.

DJ Luke Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV 2018

$
0
0
Matokeo ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Lucas Mukami (DJ Luke) ameibuka mshindi wa Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa kura 315, dhidi ya Liberatus Mwang'ombe, aliepata kura 262. akifuatiwa na Rebeca 24.
VICE PRESIDENT Joha 352 Joyce 248. SECRETARY Cleopatra 311 Omby 214 Dotto 70. ASST SECRETARY Saria 360 DMK 23. ASST. TREASURY Magret 263 Mikidadi 329.... BOARD Mashaka 413 Zena 296 Jabil 330. Pius 454 Asha 386 Hamza 295 Ruth 250.

WANANCHI BUKOBA WADAI VITAMBULISHO VYA TAIFA VITAWASAIDIA KUONDOKANA KERO ZA MIPAKANI

$
0
0

Wananchi mkoani Kagera wameeleza kero kubwa wanayoipata, ukiwemo usumbufu mkubwa wanapokuwa kwenye shughuli zao nje ya mkoa hasa maeneo ya mpakani kwa kukosa Vitambulisho vya Uraia.
Hayo wameeleza wakiwa kwenye vituo vya Usajili unaoendelea mkoani humo;  ukihusisha Wilaya zote za Mkoa Kagera.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamedai kuwa lengo la kujitokeza kwa wingi ni kutokana na umuhimu wa Vitambulisho hivi; kwani wengi wao hupata shida pindi wanapotoka nje ya mkoa wao ikizingatiwa kuwa mkoa huo upo pembezoni kabisa mwa nchi ya Tanzania.
Wakazi wa kata ya Nshambya Wilaya ya Bukoba ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza licha ya changamoto ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Akizungumzia zoezi hilo; Kaimu mtendaji kata ya Nshambya Bi Fatma Christian Majengo, amesema wananchi waliojitokeza ni wengi na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutokubali kuuziwa fomu za Vitambulisho vya Taifa, kwani fomu hizo zinatolewa.
Kwasasa zoezi hilo limekuwa linaendeshwa kwa Kata ili kutoa fursa kwa kila mwananchi kupata fursa ya kusajiliwa; hivyo wananchi wametakiwa kuwa makini kufuatilia ratiba ya lini zoezi litafika kwenye Kata zao.

 Wakaazi wa kata ya Nshambia, Bukoba, mkoa wa Kagera wakiwa katika foleni ya kusubiri kupigwa picha wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa licha ya mvua kubwa zilizokuwa zikiendelea kunyesha.
  Afisa uhamiaji Bw. Issa Juma akifanya mahojiano na Bi. Kemilembe Ishengoma wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulishi vya Taifa kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba Mjini.
  Bi. Hadija Abeid, Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akitoa maelekezo kwa wananchi wa kata ya Nshambya waliojitokeza kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.

 Baadhi ya wakazi wa kata ya Nshambya wakisubiri kukamilisha usajili wa Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hilo likifanyika katika kituo cha Chuo kikuu Huria kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba.
 Bw. Daniel Michael  Afisa Usajil akimsaidia Bi. Monica Kagasheki kukamilisha zoezi la uchukuaji alama za vidole wakati wa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.


HASSAN BICHUKA ATOA BURUDANI, ATHIBITISHA KUWEPO DAR CCM FAMILY DAY APRIL 21, 2018 LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM

KONGAMANO LA BIASHARA LA TCCIA LAFANA

$
0
0
Kongamano la biashara lililoandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) limefanyika jijini Dar es salaam na kuzungumzia mambo kadha wa kadha hususani fursa katika bomba la mafuta la Tanga hadi Hoima, Huduma za fedha kurahisisha biashara za kimataifa na pia makubaliano ya biashara kati ya TCCIA na Chemba ya biashara kutoka China.
Akizungumza wakati wa kufungua rasmi kongamano hilo Charles Itembe ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania alisema “ ikiwa wafanyabiashara watatumia huduma za fedha za kimataifa kama Letter of Credit basi itapunguza utapeli na hivyo kukuza biashara. Pia alielezea jinsi benki ya Azania ilivyo tayari kushirikiana na wafanya biashara katika kukuza biashara na uchumi wa viwanda”Nae Mwenyekiti wa Infotech group Ali Mfuruki aliwaasa wafanya biashara kujenga viwanda vyenye kusaidia lengo la Serikali la kuhakikisha viwanda vinajengwa.
Makamu wa Rais wa TCCIA Octa Mshiu alishukuru wanachama wa TCCIA na waalikwa  kwa kufika na kibadilishana uzoefu na changamo.Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo kwa kushirikiana na TCCIA,Imani  Kajula “ alisema mkutano huu ni mwendelezo wa lengo la TCCIA kuwawezesha wanachama wake kuwa na jukwaa la mashauriano.
Wadhamini wa kongamano hilo ni Azania, ATCL na Zurich Insurance.

WAZIRI UMMY AMTAKA DED TANGA KUTENGA ENEO KWA AJILI YA TAASISI YA GIFT OF HOPE

$
0
0
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutenga eneo la hekari 10 kwa ajili ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Gift of Hope Foundation ambayo inasimamia kituo cha Sober House.

Hayo ameyazungumza alipotembelea kituo hicho kinacho wasaidia waat hirika wa madawa ya kulevya kilichopo eneo la Kange kata ya Maweniambapo alikabidhi pikipiki 1 kwa ajili ya kituo hicho.Waziri Ummy alisema jambo linalofanywa na taasisi hi yo lazima liungwe mkono na Serikali kutokana na jitihada zao za kukabiliana na mapambanoya matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa waathirika.

Alisema nguvu kubwa inatumiwa na waanzishaji wa nyumba hizo kwa lengola kusaidia vijana huku wakikosa msaada wa kudumu wa kuwawezeshawaweze kujitegemea tofauti na ilivyo sasa wanavyoishi kwa kuomba misaada.“Jambo linalofanywa hapa sobber house ni juhudi kubwa na lazima sis ikama serikali tuwaunge mkono hawa watu wakishindwa makundi haya kama yatarudi mitaani hali inaweza kuwa mbaya zaidi”Alisema.

Aidha alisema kufuatia taarifa ya taasisi hiyo ya kuhitaji eneo lakutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,shughuli za mikono ikiwamou fugaji,kilimo cha mbogamboga na hata ufundi ni jambo la msingi naviongozi wote wanatakiwa walione kwa jicho la tatu.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akimkabidhi pikipiki Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House cha Gift of Hope kilichopo Kange Jijini Tanga Saidi Bandawe kwa ajili ya kuitumia kwenye matumizi yao 
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi ambao waliambatana nae ikiwemo vijana matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya. 


WAKAZI WILAYA YA MKINGA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI

$
0
0
Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na kusambaza huduma za maji la Water Missions International Tanzania, mwishoni mwa wiki limezindua mradi mkubwa utakaonufaisha vijiji 7 vya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utaowawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa matumizi yao na matumizi mengineyo na shughuli za kiuchumi. 

Kwa kipindi cha muda mrefu wilaya ya Mkinga imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji salama, kutokana na kutokuwepo na vyanzo vya uhakika vya maji katika eneo hilo.Vijiji 4 vya Mkinga, Mtenguleni, Mwakihonda and Karoyo vimekuwa vikitegemea kupata maji ya bomba kutoka tanki la zamani la kusambaza maji kutoka kijji jirani cha Parangukasere, ambalo limekuwa halitoshelezi mahitaji ya maji kwa wakazi wa vijiji hivyo. 

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Gregory Ndunguru,ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Mkinga,kuzinduliwa kwa maradi huu wilayani hapa kutawezesha wananchi kupata maji safi ya uhakika wakati wote,kwa niaba ya serikali nalishukuru shirika la Water Missions International Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini”. 

Mhandisi Ndunguru, alisema mradi huu utanufaisha maisha ya mamia ya wananchi wakazi wa Mkinga na kupunguza adha kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kifamilia .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Ndunguru (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza wadau mbalimbali kufungua bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mkinga mkoani Tanga. 
Wadau wa mradi wa maji wa Mkinga wakibeba ndoo kwa pamoja wa hafla ya uzinduzi wa mradi. 
Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania, Isack Abdiel, akielezea mradi huo kwa waandishi wa habari. 
Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo. 
Kisima cha maji kilichokuwa kinatumika kabla ya mradi mpya. 
Sehemu ya miuondombinu ya mradi mpya.


MAGAZETI YA LEO JUMATATU MARCH 26,2018

Je! Unajua unaweza kupata bei bora za soko kwa shamba lako la kuzalisha kwa kutumia mtandao wa simu?

$
0
0
Je! Unajua unaweza kupata bei bora za soko kwa shamba lako la kuzalisha kwa kutumia mtandao wa simu? Tazama na ujifunze jinsi wengine wanavyofanya.




MRADI WA SOKO TUNGWI-SONGANI MANISPAA YA KIGAMBONI WAZINDULIWA,WANANCHII WAASWA KUITUNZA MIUNDO MBINU YAKE

$
0
0
Wananchi wa mtaa wa Tungwi-Songani Kata ya Pembamnazi Manispaa ya Kigamboni wametakiwa kutunza miundombinu ya soko ili soko liweze kudumu kwa muda mrefu na kunufaisha wananchi wote kwa ujumla. 

Rai hiyo imetolewa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja alipokuwa akizindua mradi wa soko hilo ijumaa lililojengwa Mtaa wa Tundwi-Songani , alisema kuwa mradi huu umenza ujenzi muda mrefu tangu mwaka 2002, hivyo tunatarajia ukamilikaji wake utaleta maendeleo kwa wananchi wote wa Tundwi Songani na jamii nzima ya Kata ya PembaMnazi hivyo ni muhimu kuhakikisha unatunzwa. 

Alisema kuwa ulinzi uimarishwe wa miundombinu na kuhakikisha lengo lililokusudiwa la kuboresha mazingira na utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na wananchi wa Tundwi na kata ya Pemba Mnazi kwa ujumla linafikiwa. 

Akitoa taarifa ya mradi Mratibu wa TASAF Manispaa ya kigamboni Bi.Janet Kacholi alisema kuwa, mradi wa soko ni miongoni mwa miradi iliyoibuliwa na wananchi kupitia program ya TASAF, ambapo umelenga kutoa ajira kwa vijana kwa kupata fursa ya kuuza mazao mbalimbali na kuiwezesha Serikali kupitia Halmashauri kukusanya mapato kutokana na ushuru mbalimbali utakaotozwa kwa wafanyabiashara. 

Aliongeza kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo jumla ya Tsh.91,858,842.24 zimetumika ambapo wananchi wamechanga kiasi cha Tsh.34.040.427.27 mchango wa TASAF ni Tsh.26,416,827.27 na Halmashauri ya Manispa ya kigamboni imetoa Tsh.31,401,587.7 ambazo zimekamilisha ujenzi wa meza za ndani baada ya Halmshauri ya Temeke kushindwa kutoa fedha za ukamilishaji kama ilivyoahidi wakati wa uibuaji wa mradi kabla ya kugawanywa. 
 ​Mstahiki Meya wa Manispaa ya kigamboni Mh. Maabadi Hoja akifungua kitambaa cha jiwe la msingi kuonesha uzinduzi rasmi wa soko​


 ​Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi. Janet Kacholi akisoma taarifa ya mradi kabla ya uzinduzi.​
 ​Mstahiki Meya akiwa ameongozana na wananchi wakikagua soko mara baada ya uzinduzi. 


 ​muonekano wa soko kwa nje​
 ​Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa soko​.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ESRF wapongezwa kupitia SIDP

$
0
0
TAASISI ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), imepongezwa kwa kazi zake inazofanya za utafiti na kutoa mwelekeo sahihi wa uanazuoni kwenye masuala mazito yanayotakiwa kutekelezwa na wananchi wa Tanzania kuendeleza ustawi na kuinua uchumi.

Aidha imepongezwa kwa kurejea kuipitia sera ya maendeleo endelevu (SIDP) ya mwaka 1996 ambayo kwa sasa inahitaji kufanyiwa marekebisho kuendena na maizngira ya sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Elisante Ole Gabriel, katika hotuba iliyosomwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara hiyo, Obadiah Nyagiro wakati akifungua mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara?

Alisema kwamba majadiliano hayo yanakwenda sawa na juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kujikita katika maendeleo ya viwanda ambapo uwekezaji na biashara ni vitu muhimu.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Obadiah Nyagiro akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof Elisante Ole Gabriel uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk. Tausi Kida wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtafiti mshiriki wa ESRF Prof. Samwel Wangwe, akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya vigezo vya kuipitia upya sera ya maendeleo endelevu wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtafiti wa Huru wa masuala ya Jinsia na Maendeleo Prof. Marjorie Mbilinyi akichangia hoja wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano akichangia mawazo wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Obadiah Nyagiro (katikati) na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia).

17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI AJALI MKURANGA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga 
 WATU 17 kati ya 26 waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani ,wametambuliwa majina yao ambapo hatua inayoendelea ni kuwakabidhi kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi. Aidha watu wengine 10 waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu. 
 Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK (pichani) inayofanya safari zake Kimanzichana - Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori. 
 Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga, Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi hao ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani wakati wakipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
 Mganga mkuu huyo aliwataja waliofariki na kutambuliwa majina yao ni 17 kati ya 26 waliofariki kuwa ni pamoja na Selemani Guli (36) mkazi wa Kongowe,Modesta Sheleli (24 ) mkazi wa Vianzi,Doreen Selemani Seleli (5), sheila Hamad Mkuba ( 8 )mkazi wa Vianzi na Mariam Hussein Sadik (15 )mkazi wa Mwarusembe. 
Wengine aliotaja ni Nassoro Hamis( 48) mkazi wa Jaribu Mpakani, Asha Athumani (24)mkazi wa Songosongo ,Nasma Athuman 22 Songosongo Mwanahawa Athuman (52),Mohammed Saidi (25) mkazi wa Njopeka na Mwajabu Jongo (20)mkazi wa Njopeka"; 

 Dokta Mwandambo aliwataja marehemu wengine kuwa ni Mwarami Mbunju(37) mkazi wa Mkamba na Abisaalom Uloga (25)mkazi wa Kimanzichana ,Kijongo Kibwana Jongo(26 )anakaa Jaribu Mpakani na Recho Japhet (16),Mariam Selemani (36)mkazi wa Mbagala na Melania Kapatwa (38)mkazi wa Jaribu Mpakani.


Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata akithibitisha anesena ajali imetokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya humo. 

 Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya. Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini. 
 Mhe. Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe. "Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao." alieleza Ulega.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images