Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAADHIMISHO YA SIKU YA USONJI KUFANYIKA KESHO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Wazazi wanapaswa kuwapa nguvu, moyo na kupata haki ya elimu kwani wao pia wanauwezo wa kufanya kazi mbalimbali katika jamii  hivyo katika matembezi hayo yatasaidia kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji(Autism) kuonekana wanaweza na wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.



Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi  wa shule za Almuntazir Mohammad Ladack amesema lengo  la maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji (autism) na kuondoa dhana ya kuwaona watoto hao kama hawawezi hivyo wametakiwa kuwapa nafasi ya kufanya na kuona umuhimu wao katika jamii.

"Wazazi tunapaswa kuwapa nafasi watoto hawa na kuona kuwa wanaweza kufanya na wanahaki ya kupata elimu hivyo wazazi wawape nafasi ya elimu kwani wanaweza kufanya mambo mbalimbali hivyo tuwalinde na tuwapende pia" Amesema Mkurugenzi Ladack.



wa upande wake mwalimu wa watoto maalumu Eva Wigira amesema matembezi hayo yana lengo la kuelimisha jamii kuweza kufahamu watoto kama hawa wapo katika jamii na hivyo wana haki ya kupata elimu na wanauwezo mzuri wa kuweza kujifunza na kufanya mambo mbalimbali kwa manufaa yao ya badae.

"Watoto wenye usonji wapo katika jamii zetu hivyo matembezi haya yataelimisha jamii kuhusu watoto hawa kupata elimu pamoja na kuona wanaweza kufanya vizuri katika masomo na mambo mbalimbali baada ya kupata mafunzo ya namna ya kufanya kama tunavyofundisha hapa shuleni kwetu" Amesema Eva Wigira.

Vilevile ikiwa ni siku ya maji wanafunzi wa shule ya Almuntazir Islamic school ya wasichana wamefika kuwapatia maji watoto wenye usonji (Autism) ikiwa ni ishara ya kuwatia moyo na kuwafanya wajione ni sawa na wengine hawapaswi kutengwa wala kuonekana hawezi.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Makamu mkuu wa shule ya wasichana  Joan Soka amesema watoto hao wametembea lengo likiwa ni kuelimisha na kuwawezesha kufahamu maana ya usonji  pamoja na kuwatia moyo watoto wenye Autism na kuwafanya kuona wanakubalika katika jamii na ni muhimu kama wengine.

Amesema wazazi wanapaswa kuona umuhimu wa watoto hawa wanapaswa kupewa elimu na kuona ni changamoto ya kila mzazi kuwapenda na kuwalinda watoto wenye usonji (Autism) hivyo amewataka wazazi na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika matembezi hayo.

Matembezi hayo yatafanyika siku ya Jumapili tarehe 25, March mwaka huu ,ambapo yataanza muda wa saa moja na nusu asubuhi katika barabara ya Obama


UBALOZI WA KUWAIT NA TAASISI YA DORIS MOLLEL WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WATOTO NJITI, HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA, DODOMA

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, sehemu ya vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti, vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma. Wengine pichani ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Hospitali hiyo, Neema Tawale (wa pili kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Huduma za Uuguzi, Salome Kasanga.

The Ambassador of Kuwait in Tanzania His Excellency Hon. Jaseem Al Najem (L) Handing Over Equipments to support Premature babies at Benjamin Mkapa Hospital to the Executive Director of the Hospital, Dr. Alphonce Chandika, A support from the Embassy of Kuwait in Collaboration with Doris Mollel Foundation end of this week in Dododma. second from left is Ms. Doris Mollel Founder of Doris Mollel Foundation and Ambassador to Preterm babies in Tanzania , Neema Tawale(second from right) together with Acting Director of Nursing at Benjamin Mkapa Hospital Sr Salome Kasanga.
 Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya vifaa hivyo vilivyogharimu dola za Marekani elfu ishirini (20,000 USD) huku Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (kulia) wakimsikiliza, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem,  Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Januarius Hingi wakati akitoa maelezo ya namna vifaa hivyo vitakavyosaidia wakina mama wanaojifungua watoto wanaozaliwa kawaida na wale wanaozaliwa kabla ya wakati. 
Sehemu ya vifaa hivyo.

WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA

$
0
0
Na Mwandishi Maalum
Jumla wa wagonjwa wa akili 55 waliokuwa  wametenda makosa mbalimbali yakiwamo ya jinai wakiwa na  ugonjwa wa akili, wameachiwa huru baada ya mahakama kutowatia hatiani.
Hayo yameelezwa leo  mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi ( Mb) wakati alipokuwa akiwasilisha  Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara Katiba na Sheria na Taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.  Kamati hiyo ilikuwa nchini ya Uenyekiti wa Mhe. Najma Murtaza Gingo ( Mb). Waziri  Kabudi ameieleza  Kamati hiyo kwamba,   kifungu cha 219 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20, kinampatia Waziri mwenye dhamana ya masuala ya  sheria mamlaka ya kuwaachia huru wagonjwa wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai yakiwamo ya mauaji.
“ Kutokana na mamlaka hayo ya kisheria,  katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, nilisaini hati ya kuachiliwa huru wagonjwa 55 wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai wakiwa na ugonjwa wa akili na hivyo mahakama  kutowatia hatiani” akabainisha Waziri Kabudi.
Na kuongeza kwamba, kwa muda mrefu wagonjwa hao walikuwa wakihifadhiwa kwenye Taasisi ya Isanga kusubiri amri ya Waziri. "Na kutokana  na hali ya afya zao za akili kuimarika, niliamua waachiliwe huru, ili waungane na familia zao na kuendelea na matibabu wakiwa nje ya taasisi hiyo”.
Pamoja na kuelezea kuachiwa huru kwa wagonjwa wa  akili, Waziri Kabudi pia alianisha mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na Wizara pamoja na  Taasisi zake katika suala zima la utoaji na usimamiaji wa haki katika kipindi cha bajeti cha 2017/2018.Baadhi ya  mafanikio hayo ni  kwa Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika uendeshaji wa mashauri ya daawa ili pata ushindi katika mashauri 82 yaliyokuwa na thamani ya shilingi 1,064,581,955,743bn/-. Kwa mujibu wa  Waziri wa Katiba na Sheria  ushindi huo umewezesha pamoja na mambo mengine maamuzi ya serikali pamoja na sheria za nchi kutobadilishwa kwa msingi ya kuikuka Katiba.
Mafanikio  mengine ambayo yametajwa na   Waziri Kabudi ni pamoja na Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea na utoaji wa ushauri wa kisheria kwenye mikataba na makubaliano mbalimbali  yanayofanywa na Wizara Idara na Taasisi za Serikali. Katika eneo hilo , hadi kufikia mwezi  February, 2018 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uhakiki  na kutoa ushauri wa mikataba 691 yenye thamani ya Shilingi 1,720,026,713,823bn/- na Dola za Kimarekani 1,0884,472,366, mikataba hii ilihusu ununuzi , ukarabati wa majengo, utoaji wa huduma za jamii na ujenzi wa barabara.
Katika uendeshaji wa kesi za jinai,  Waziri wa Katiba na Sheria alieleza Kamati ya kudumu ya   Bunge ya Katiba na Sheria kwamba, katika kipindi kinachoishia February 2018. Ofisi ya  Taifa ya Mashtaka iliendelea na kuratibu shughuli za upelelezi wa makosa ya jinai mahakamani.Mashauri ya jinai yaliyoshughulikiwa ni pamoja na yaliyohusu wanyamapori, dawa za kulevya, uhujumu uchumi, rushwa  na mauaji. Ambapo washtakiwa waliotiwa hatiani walipewa adhabu mbalimbali zikiwamo vifungo, faini na mali kutaifishwa ambapo jumla ya shilingi za kitanzania 2,169 ,983,500 zilitozwa kama faini kutoka kwa washtakiwa.
Aidha kwa upande wa mali zilizotaifishwa ni pamoja na  kilogramu 24.5 za dhahabu yenye thamani ya Shilingi 2,012,357,164 na fedha za kigeni kutoka  mataifa 15 zenye thamani ya shilingi 908,019,979. Mali nyingine zilizotaifishwa ni pamoja na  magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya Audi yaliyokamatwa katika banari ya Dare s Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba.
Mali nyingine   zilizotaifishwa katika  kipindi hicho ni pikipiki, mifugo, mafuta na  basi la abiria lililokuwa likitumika kusaifirishia meno ya tembo  yanazokadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya shilingi 3,242,787, 915.
Kwa upande wa  uandishi wa Sheria, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, iliandaa jumla ya miswaada 15 ya sheria ambayo iliwasilishwa Bungeni na kupitishwa na kuwa sheria. Hali kadharika, iliadaa sheria ndogo na matamko mbalimbali ya serikali yapatayo 164 ambayo yalichapishwa kwenye gazeti  la serikali.
Mpango  na Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019,   Wizara inaomba takribani Shilingi 183,223,038,000bn/- zikiwamo fedha za mishahara,  matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo.
Katika kikao cha leo  mafungu yaliyopitishwa  na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria na Katiba   ni yale ya Wizara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka .  
Kikao hicho  cha uwasilishaji wa   mpango na bajeti ya Wizara kilihudhuriwa pia na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi,  Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali   Paul Ngwembe, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Biswalo Mganga, pamoja na wawakilishi kutoka  Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Taasisi ambazo zipo chini ya  Wizara ya Katiba na Sheria ni Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe Profesa Palamagamba Kabudi ( Mb) akiwasilisha  mbele ya  wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara na Taasisi zake leo  Dodoma, pembeni yake ni  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk.Adelardus Kilangi
 Mbunge wa Ubungo Mhe. Saeed Kubena ambayi ni mjumbe  wa  Kamati ya Kudumu ya  Bunge  ya Katiba na Sheria  akinyosha mkono  kuashiria kutaka kuuuliza jambo wakati  mara baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi kuwasilisha  Mpango na Makadirio ya Bajeti.
 Sehemu ya  wajumbe wa  Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria  wakisikiliza uwasilishwaji wa Mpango na   Makadirio ya  Bajeti ya Wizara  ya Katiba na Sheria na Taasisi zake leo mkoani  Dodoma

Naibu  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu  ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Gingo (kushoto) akiteta jambo na Katibu wake  wakati wa uwasilishaji wa Mpango na Makadirio ya  Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake

TCCIA NA AZANIA BANK ZAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, akitoa mada katika mkutano huo.
 Wadau.
 Kaimu Meneja Huduma na Uwezeshaji Brella, Bosco Gadi, akitoa mada katika mkutano huo.
Mwakilishi kutoka UWURA, Mr. Keneth akitoa mada.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group Ltd, Ali Mfuruki akizungumza katika mkutano huo.


 Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja, akizungumza katika mkutano huo. 
Maofisa wa Benki ya Azania wakiwa wamepozi kwa picha kabla ya kuanza kwa mkutano uliondaliwa na TCCIA kwa ajili ya wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizopo katika uwekezaji.  Mkutano huo ulidhaminiwa na benki hiyo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA



WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

$
0
0
*Asisitiza kwamba kazi ndiyo msingi wa maendeleo 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.

Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ili vijana waweze kupata maendeleo lazima wafanye kazi kwa bidii.

Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani washirikiane na Serikali katika kuimarisha ulinzi na usalama. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya kuwahudumia.

Amesema Serikali imetoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.
 “Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.
Pia, Waziri Mkuu amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho. Gari hilo limetolewa na Rais Dkt. John Magufuli ili kuimarisha huduma za afya kituoni hapo. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, MACHI 24, 2018.

TUKUTANE COVENTRY JUMAMOSI TAREHE 05/05/2018, MKUTANO MKUU WA PILI (AGM – 2018) – JUMUIYA YA WATANZANIA UK NA IRELAND KASKAZINI.

$
0
0

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania UK na Northern Ireland inapenda kuwatangazia Wanachama wake na Watanzania wote wanaoishi nchini Uingereza, Wales, Scotland na Ireland ya Kaskazini (Ireland)
kuwa Mkutano Mkuu wa Pili (AGM – 2018) Utafanyika katika Jiji la Coventry hapa nchini Uingereza
Anuani – ST. MARY & ST BENNEDICT
                 52A RAGLAN STREET
                 COVENTRY –  CV1 5QF
Kuanzia saa tano asubuhi hadi saa kumi na moja Jioni, Ajenda kuu kubuni mikakati Zaidi kwa maendeleo ya Jumuiya Yetu
Kuongeza Ushirikiano na Jumuiya mbalimbali hapa UK na Ireland
kutakuwa na chakula cha mchana na vinywaji Baridi
WANACHAMA HAI BUREE NA ASIYE MWANACHAMA NI £15 (£5 ADA YA KUJIUNGA NA £10 CHAKULA)WATAKAOJIUNGA SIKU HIYO KUPEWA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUWA MWANACHAMA HAI NA WATAKAVYOWEZA KUSHIRIKI KATIKA UJENZI WA JUMUIYA (Terms and Condition Apply)
Mara baada ya Mkutano ni burudani ya Muziki katika Club Junction – Coventry mpaka majogoo
DISCOUNTED GROUP HOTEL BOOKING – AVAILABLE

FOR MORE INFO, PLEASE CALL – 07402344004/07941656446/07956485119/07903828119

WOTE MNAKARIBISHWA



Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

“Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie

SBL imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium Lager ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza idadi ya bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania. 
 
Moja kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama YA sbl ni kujenga na kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni chini ya asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuimarisha mahusiano na wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji yao kwa kuwahakikishia bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara yetu,”anasema mkurugenzi huyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, 

WANANCHI DODOMA WAAMKA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0


Wananchi mkoani Dodoma wameendelea kufurika kwenye vituo vya Usajili mkoani humo kushiriki zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa- NIDA.

Zoezi hilo ambalo limelenga kuwasajili wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea limeonekana kuwavuta wananchi kwa wingi tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma wakitokea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na viunga vyake.

Kata ya Chamwino na Chang’ombe zilizopo Wilaya ya Dodoma mjini leo zimetia fora kwa maelfu ya wananchi waliomiminika alfajiri kupata huduma hiyo huku baadhi wakionekana kwenye mitaa ya mji huo wakihaha kutoa nakala (copy) ya viambatisho vyao kwenda kujaza fomu.
Akizungumzia mwenendo wa zeozi hili ambalo lilianza tangu mwezi Februari,2018; Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe Bi. Neema Makinda amesema mwitikio wa watu ni mkubwa na wamejipanga kuwahudumia wananchi wote wa Kata hiyo ambao idadi yao ni Zaidi ya elfu 25.
 Mtendaji  wa Kata ya Chang’ombe Bi. Neema Makinda akimpitishia fomu mmoja wa wananchi wa Kata hiyo aliyefika kwenye kituo cha Usajili kusajiliwa.
 Bw. Jumanne Bakari akikaguliwa fomu yake na Mwenyekiti wa Mtaa wake Bi. Havijawa Ramadhani ( wa kwanza kushoto) na pembeni yake ni Bi. Tatu Kimwaga mjumbe wa Mtaa.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Chamwino wakiwa wamejipanga kwenye foleni  kwenye viwanja vya wazi nje ya Shule ya Msingi Chamwino wakisubiri kusajiliwa  Vitambulisho vya Taifa.
 Bi. Asha Twaha Mruma, mwananchi katika Mtaa wa Chamwino akiwa anajaza fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa huku pembeni mtoto wake mdogo wa kiume akishuhudia mama yake akijaza fomu hiyo kwa umakini mkubwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA KIFUA KIKUU WAZIRI HAMAD ATOA WITO WAMAPAMBANO

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Jamii imetakiwa kulifahamu vyema tatizo la kifua kikuu na kushirikiana na Wizara ya afya kupitia Kitengo shirikishi cha UKIMWI, Homa Ya Inni, Kifua kikuu na Ukoma ili kukabialiana na tatizo hilo.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed alipokuwa akizungumza na Wanahabari ofisini kwake Mnazimmoja mjini Zanzibar kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani.

Amesema Maradhi ya Kifua kikuu, ni moja kati ya maradhi ambayo Shirika la afya Duniani limeyapa kipaumbele ili kuweza kufanikisha mapambano dhidi yake.

Waziri Hamad amesema kila ifikapo Machi 24 ya kila mwaka ndiyo siku ya maadhimisho ya  Kifua Kikuu ulimwenguni ambapo hutumika kuikumbusha  na kuishajihisha jamii kuwa Kifua Kikuu bado ni janga kubwa katika jamii.

Aidha kupitia maadhimisho hayo Wizara ya afya ikishirikiana na Viongozi mbali mbali huitumia fursa hiyo kutathmini juu ya hali ya maradhi nchini na kuandaa mikakati madhubuti ya kupambana nayo.
  Msaidizi Meneja kitengo shirikishi Ukimwi,Kifua kikuu na Ukoma Issa Abeid akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa afya Hamad Rashid Mohamed kuzungumza na waandishi wa habari  kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku hiyo.
 Meneja kitengo shirikishi Ukimwi,Kifua kikuu na Ukoma Farhat Khalid akitoa ufafanuzi namna ya kupunguza maambukizi ya Kifua Kikuu.
 Waziri wa afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali hawapo pichani kuelekea  katika kilele cha maadhimisho  ya  siku ya Kifua Kikuu.
 Mwandishi wa habari wa ITV na Radio ONE, Farouk Karim akiuliza maswali katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Harusi Said Suleiman akitoa shukurani kwa waandishi wa habari na wadau mbalimbali waliojitokeza katika mkutano huo.(Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANAWAKE WA ARUSHA WAPEWA MKOPO WA MILIONI 120

$
0
0
Na Alice Mapunda, Arusha.
Wanawake wa Arusha watakiwa kutumia vizuri mikopo yao kwa kuwekeza kwenye shughuli  mbalimbali za maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi na kuwaletea mapato yakutosha katika familia zao.
Ameyasema hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Jenista Muhagama alipokuwa akikabizi hundi ya milioni 120 ya mkopo wa akinamama wajasiliamali, Jiji la Arusha.

Amewataka wanawake waonyeshe kuwa wanaweza kuinuka kiuchumi na kuacha utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla.

“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata tunda la embe katika mti wa miba,yani haitakaa itokee tena mkapatiwa mikopo hiyo kwa mara nyingine”.alisema

Aidha,amewahasa wakatumie vizuri  mikopo hiyo na waache kwenda kununua vitu ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendelea yao na familia zao.

Serikali ya awamu ya tano imelenga katika kuhakikisha matunda ya nchi yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake kupatiwa mitaji kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakutelekeza ilani ya chama cha mapinduzi.

Amesema wizara yake ipo tayari kuwasaidia wakimama wote watakao fanikiwa kumaliza marejesho yao na atawasaidia kupata mikopo mingine ya riba nafuu huku wakiwa katika vikundi.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Muhagama , Antony Mavunde na Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakikabidhi mfano wa Hundi ya Milioni 120 kwa akinamama 600,Jijini Arusha.
Baadhi ya Wadau na akinamama walioudhuria sherehe za kuwakabidhi mikopo akinamama 600 wa Jiji la Arusha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali kutoa uamuzi kuhusu uingizaji wa mita za umeme nchini baada ya miezi mitatu

$
0
0
Na Teresia Mhagama
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amesema kuwa, baada ya miezi mitatu Serikali itatoa uamuzi kama nchi iendelee kutumia mita za umeme zinazotengenezwa nje ya nchi au kupiga marufuku uingizaji wa mita hizo baada ya kujiridhisha  na uwezo wa viwanda vya ndani katika kuzalisha  mita husika.
Dkt. Kalemani ameyasema hayo  jijini Dar es Salam tarehe 23 Machi, 2018 wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za umeme lengo likiwa ni kujiridhisha na uwezo wa kiwanda hicho katika kukidhi mahitaji ya mita nchini.
"Serikali imeweka miezi mitatu ya matazamio ili kuona kama viwanda  vyetu ambavyo sasa ni viwili, vina uwezo wa kuzalisha mita za umeme  za kutosha na zenye ubora zitakazokidhi soko la ndani kisha tutatoa uamuzi kuhusu uingizaji wa mita hizo nchini," alisema Dkt. Kalemani.
" Miezi kadhaa iliyopita Serikali ilitoa katazo la kuagiza nguzo za umeme na transfoma kutoka nje ya nchi, baada ya kujiridhisha kuwa uwezo wa kuzalisha vifaa hivyo tunao. Sasa katika mita hizi za umeme pia tunafanya ukaguzi ili kujiridhisha na uwezo wetu," aliongeza  Dkt Kalemani.
Alisema kuwa, uzalishaji wa vifaa vya umeme nchini una faida mbalimbali ikiwemo kupungua kwa gharama za usafirishaji, mita kupatikana kwa haraka, kwa gharama nafuu na kwa wingi.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za umeme nchini . Katikati ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hashim Ibrahim.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza mara baada ya kufika katika kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za umeme nchini. Wengine katika picha ni watendaji wa kiwanda hicho, Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
za umeme katika  kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za umeme nchini. Wengine katika picha ni watendaji wa kiwanda hicho, Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hashim Ibrahim na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.

JUMUIYA YA WAZAZI ILALA WAAMUA KUWA WALEZI SHULE YA MSINGI MCHIKICHINI

$
0
0
 JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imechukua jukumu la kuwa mlezi wa Shule ya Msingi Mchikichini ili kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam  na Katibu wa Elimu ,Malezi   na Mazingira (EMA)Wilson Tobola  wakati wa maadhimisho ya wiki ya Wazazi Ilala.

Tobola aliingia jukumu hilo la kuwa mlezi na kuahidi kumaliza changamoto za shule hiyo baada kuona ina  uhaba wa kadhaa vifaa vya Steshenali, na uzio wa shule.

 " EMA leo tunadhimisha wiki ya wazazi kwa kugawa vifaa vya shule vya thamani ya Sh. 700,000  katika shule hii vilivyotolewa Azim Khan ambaye ni  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa Dar es Salaam ili kusaidia wanafunzi wa Mchikichini" amesema Tobola .

Tobola pia ambaye ni mlezi wa shule hiyo alikabidhi Sh.200, 000 kwa ajili ya nauli za walimu wa shule hiyo katika kipindi cha likizo  na Sh .600,000 kwa ajili ya mitihani ya Majaribio.

Wakati Sh.300, 000 zilitolewa na Azim Khan na Sh. 300, 000 zilitolewa na EMA Ilala Tobola.

Aidha vitu vingine ambavyo wameaidi kupeleka mwisho wa mwezi huu EMA Ilala  ameaidi mashine ya photocopy na Azim khan Compyuta.

Kuhusu suala la changamoto ya ukuta wa shule ameahidi kutafuta wadau waweze kutatua tatizo hilo.Pia atazungumza na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema na mkurugenzi wa Ilala.

" Nampongeza Azim Khan kwa msaada huu mkubwa na mimi kama EMA wa Ilala ndio mlezi wenu naomba mnishirikishe vikao na walimu nipate muda wa kuzungumza nao niweze kujua changamoto zao naitaji taaluma iwe juu shuleni hapa,hivyo kama walimu wangu nitakuwa nao pamoja" amesema.

Kwa upande wake Azim Khan amesema anatekeleza Ilani ya chama katika kukuza taaluma shuleni  ili baade wapatikane wanafunzi bora.

Khan amesema jukumu la kusaidia sekta ya elimu ni la kwetu sote sio kuiachia serikali  .

" Tunaungana na serikali yetu pendwa  ya Ilala kumsaidia Rais Magufuli na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema kuakikisha taaluma inapanda katika shule za msingi zilizopo wilayani  Ilala" amesema Khan.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mchikichini Wilson Mahemba amesema shule hiyo ina idadi ya walimu 23 na wanafunzi 503 kati yao wavulana 253 na wasichana 250.
Katibu wa Elimu  Malezi na Mazingira Wilaya ya Ilala  (EMA) Wilison Tobola akiwa na wajumbe wake Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi vifaa vya Shule katika shule ya msingi Mchikichini Dar Es Salaam leo  vyenye thamani ya 700,000 vilivyotolewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu (CCM ) Mkoa Dar es Salaam Azim Khan (Kushoto) Kulia Mwalimu mkuu wa shule hiyo . Wilson Mahemba ( Picha na Heri Shaban)

DC MATIRO AMPONGEZA DKT. MWAKYEMBE KUTATUA CHANGAMOTO ZA WASANII

Introducing "Jeraha" by Abdu Kiba

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MARCH 25,2018


FAHAMU KUHUSU JUMA KUU KUELEKEA SIKU YA PASAKA

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MATAWI KANISA LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipeana amani na Masista wa Kanisa Katoliki walipojumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akishukuru baada ya kupokea Sakramenti takatifu wakati wa Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018. Picha na IKULU

WAZIRI MKUU AKAGAUA MRADI WA UJENZI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA RUANGWA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Ruangwa Mkoa wa Lindi (DED) Bwana Andrea Chezue wakati akiangalia mchoro wa Uwanja wa Michezo wa kisasa Wilaya ya Ruangwa. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

KINANA AZINDUA SEMINA ELEKEZI KWA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa leo katika Ukumbi wa NEC katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi ,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Meza kuu ikifuatilia Semina hiyo.



FEMINA HIP YAKABIDHI TUZO KWA WANAFUNZI KUMI WA WA SHULE ZA SEKONDARI WALIOIBUKA WASHINDI SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA

$
0
0
Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya vijana, Femina Hip limetoa tuzo kwa washindi kumi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi, lililoshirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa kumi na tano nchini.

Akizungumza na wanahabari wakati wa utoaji tuzo kwa washindi, Kiongozi wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip ambayo iliendesha shindano hilo, Lydia Charles amesema shindano hilo lililenga kuleta uelewa pamoja na kubaini changamoto kuhusu masuala ya hedhi wanazokabiliana nazo watoto wa kike katika jamii.
Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Yassin Haji kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.

Amesema wanafunzi karibu 88 walishiriki shindano hilo, ambapo wavulana walikuwa 27 na wasichana 61. Na kwamba walioibuka washindi ni wasichana 5 na wavulana 5, huku shule ya Sekondari Chang’ombe ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya washindi na washiriki.

“Shindano hili lililenga kupaza sauti za changamoto za wasichana wanazokutana nazo wakiwa katika siku zao.Huu mradi ulilenga kumsaidia mtoto wa kike kuwa shuleni siku zote ambazo ana hedhi, kuhakikisha uwepo wa maji shuleni na vyoo visafi,” amesema.
Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi. Kushoto ni
Kiongozi wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip ambayo iliendesha shindano hilo, Lydia Charles.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Femina Hip, Sauda Simba amesema shindano hilo limebainisha changamoto wanazopata watoto wa kike wakiwa kwenye siku zao, ikiwemo ukosefu wa taulo za kujihifadhi-Pad, na kuitaka serikali pamoja na jamii kuhakikisha watoto wa kike wanapata hedhi salama.

Kwa upande wake, Balozi wa masuala ya hedhi salama, Badru Juma ameitaka serikali na jamii kutatua changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike hasa wa kijijini.

Washindi hao ni pamoja na Veronica Felician kutoka Kondoa Girls High School kutok Dodoma, Jemima Carlos, Yasin Said,, Humphrey Otedo wote kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe, na Latifa Salumu kutoka Shule ya Sekondari Zinga. 
Wanafunzi kutpka shule za sekondari walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo.Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akiwa na baadhi ya washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi na wachama wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip.
Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Humphrey Otedo kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images