Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109924 articles
Browse latest View live

INTRODUCING LADY JAYDEE'S NEW HOT DROP "ANAWEZA" (Official Video) Featuring Luciano


TANZIA: MKURUGENZI MWENDESHAJI WA AICC NDUGU E. KAAYA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

$
0
0
Bibi  Eliatirisha Teveli  Sumari
Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC  Ndugu Elishilia    Kaaya anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi Bibi  ELIATIRISHA  TEVELI SUMARI kilichotokea katika Hospitali ya AICC jijini Arusha leo.

Mipango ya Mazishi inaendelea nyumbani kwa marehemu kijijini Nguruma, wilayani  Arumeru.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.

MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI  - AMEN

NACTE YAZUIA VYUO 163 KUFANYA UDAHILI

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) imevizuia vyuo 163 nchini kutofanya udahili kwa wanafunzi mwaka huu baada ya kubainika vyuo hivyo vina kosoro mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi ufatiliaji na Tathimini kutoka (NACTE) Dkt. Annastella Sigwejo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema Nacte ilifanya ufatiliaji wa kuangalia ubora wa vyuo mbali mbali vilivyosajiliwa na Baraza hilo.

Amesema katika kufutia huo walivikagaua vyuo 459 ambapo vikabainika vyuo 290 tu ndio vilivyokidhi vigezo vya kufanya udahili wa wanafunzi kujiunga navyo huko vyuo 163 vikawa vinakosoro mbali mbali ambapo haviwezi kuendelea kufanya udahili.



Dkt Sigwejo ametaja baadhi ya kasoro hizo ni kutokuwa na watalamu wenye sifa za kufundisha ,kutokuwa na miundomibinu lafiki ya kufundishia.

Hata hivyo,Dkt Sigwejo amewataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo ambavyo vina sifa wanakatiwa kuangalia kwenye mtandao wa Baraza hilo (WWW.NACTE.GO.TZ) ambapo amefafanua huko kutakuwa na oradha ya vyuo vyenye sifa pamoja na kitabu ambacho kitatoa mwongozo wa mwanafunzi kuelewa kwa undani chuo na kozi anayotaka kuisomea.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Udahili kutoka (NACTE),Twaha Twaha amesema zoezi la udahili kwa wanafunzi wa Stashahada na Astashahada mbalimbali ambapo zoezi hilo limesha aanza tangu Februari ,2018 hadi Marchi 25 mwaka huu.

Twaha amesema katika udahili huo kozi za Afya udahili waka mwisho utakuwa 10 Aprili mwaka huu.Ambapo udahili hauhusishi kazo za Afya katika vyuo vya serikali ambapo udahili wake unafanywa na wizara ya Afya,Maendeleo Jinsia na Watoto ambapo wanadhamana ya kufanya udahili katika vyuo vya afya vya serikali.
Kaimu Mkurugenzi ufatiliaji na Tathimini wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Dkt. Annastella Sigwejo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua walizozichukua kwa vyuo vya ufundi vinavyoendedha mafunzo bila sifa leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkuu wa kitengo cha Udahili kutoka (NACTE),Twaha Twaha.
Mkuu wa kitengo cha Udahili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) (NACTE),Twaha Twaha akizungumza kuhusiana na udahili wa Stashahada na Astashahada ulionza machi na kuishia Aprili 25 leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi ufatiliaji na Tathimini wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Dkt. Annastella Sigwejo.

BITEKO ATOA WITO KWA WADAU KUZINGATIA SHERIA MPYA YA MADINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa wito kwa wadau wote wa sekta ya madini nchini, kuzingatia sheria mpya ya madini ambayo inaelekeza namna bora ya usimamizi wa sekta hiyo.
Alitoa wito huo jana, Machi 22 mwaka huu kwa nyakati tofauti, alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Dodoma, kukagua shughuli mbalimbali za madini.
 “Moja ya mambo muhimu ambayo sheria mpya ya madini inaelekeza ni kutunza rekodi za uzalishaji wa madini ili Serikali iweze kujua ni kitu gani kinazalishwa na hatimaye tuweze kujua kodi gani zinalipwa na wenye leseni husika,” alifafanua.
Aidha, Naibu Waziri aliwataka wenye leseni kushirikiana na wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kunufaika kupitia kazi wanazofanya. “Kwa maneno mengine, asitokee mtu wa kumnyanyasa mchimbaji mdogo eti kwa sababu tu ana leseni,” alisisitiza.
Akizungumza na wamiliki wa leseni pamoja na wachimbaji wadogo wa madini wa dhahabu katika eneo la Nholi wilayani Bahi, Naibu Waziri alipongeza uamuzi wao wa kuanzisha kampeni ifikapo Aprili mwaka huu, kupanda miti kwenye maeneo yao ili kurejesha hali nzuri ya mazingira.
Vilevile, aliwaagiza kuweka wigo kuzunguka mashimo yaliyo wazi ili kuonyesha hali ya tahadhari kuwa eneo hilo ni hatari na linaweza kusababisha ajali, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuzingatia usalama migodini.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akizungumza na wananchi wa Nholi wilayani Bahi, kulipo na machimbo ya madini ya dhahabu, alipowatembelea Machi 22 mwaka huu, kujionea shughuli wanazofanya.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili kutoka kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Halmashauri, wakati wa ziara yake kukagua shughuli za uchimbaji dhahabu katika eneo la Nholi, Wilaya ya Bahi, Machi 22 mwaka huu. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu.
 Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Dodoma, Silimu Mtigile (kulia) akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Nholi wilayani Bahi, wanaojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu; wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), Machi 22 mwaka huu

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI WAFANYA KIKAO CHA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO,WAJIWEKEA MALENGO

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma akifungua kikao cha  Majaji wa Mahakama ya Rufani, lengo la kikao hicho cha siku moja kimelenga katika kufanya tathmini yaUtendaji kazi wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2017 na kuweka Mkakati na malengo ya mwaka, 2018, kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T),. Benard Luanda. 
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Katarina Revokati akitoa Mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliopo katika kikao cha tathmini na uwekaji wa mpango wa malengo ya utekelezaji kwa mwaka huu.
Msajili-Mahakama ya Rufani (T) akitoa Mada katika Kikao cha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani (T), katika Mada yake Mhe. Msajili amesema kuwa Mahakama ya Rufani imefanikiwa kushusha kiwango cha mlundikano kutoka asilimia 37 mwaka 2016 hadi asilimia 10 mwishoni mwa Desemba, 2017.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya ‘Oceanic’ iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
 Jaji Mkuu,  Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye picha ya pamoja.
(Picha na Mary Gwera)

KUWAIT KUING'ARISHA DODOMA KWA BARABARA

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.

Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem, akizungumzia uhusiano mzuri ambao umeendelea kuwepo kati ya Tanzania na Kuwait alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa mazungumzo Mjini Dodoma.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

MARUFUKU MADAKTARI KUJAZA FOMU ZA UCHUNGUZI AFYA BILA KUPIMA WANAFUNZI TB-UMMY MWALIMU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa madaktari kujaza fomu za uchunguzi wa afya bila kupima wanafunzi husika iwapo ana ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB) au laa kwani kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.

Pia amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB na huku akieleza mpaka sasa takribani watoa huduma 1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu na hivyo wanaweza kuwabaini wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

Waziri Mwalimu ametoa kauli hiyo leo kwenye tamko lake   kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya TB duniani ambayo hufanyika Machi 24 ya kila mwaka ambapo amefafanua TB ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi duniani.

Hivyo amasema ili kukabiliana na ugonjwa huo pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa amewaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya kuanza masomo.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye Picha), wakati wa Maazimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani, tukio limefanyika mapema leo katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma.
Baadhiya  Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa ukaribu tamko la Kifua Kikuu (TB) lililokuwa linatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma mapema leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TPDC yaimarisha Sekta ya Afya Kidundai

$
0
0
Katika jitihada endelevu za utekelezaji wa dhana ya uwajibikaji kwa jamii, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo ni Shirika la Mafuta la Taifa kwa mujibu wa Sheria ya Petroli (2015) limeendelea kuitekeleza dhana hiyo kwa vitendo kwa kutoa vifaa vya ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kidunda Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Katika tukio la makabadhiano la tarehe 22 Machi, 2018, TPDC imeweza kukabidhi hundi ya Shilingi milioni nne ambazo Kijiji kiliomba kusaidiwa ili kuwezesha ujenzi wa zahanati hiyo ambapo kwa mujibu wa serikali ya Kijiji, fedha hizo zitawezesha manunuzi ya mizunguko ya nondo 40 yenye futi 40 kila moja, mifuko ya saruji, matofali na gharama za kumlipa fundi ambapo mpaka kufikia hapo zahanati itakuwa imefanikiwa kuezekwa.  

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai kilichopo Kata ya Vuga, Ndg. Waziri Mdoe alisema “kwa niaba ya halmashauri ya kijiji, tunayo furaha isiyo kifani kwa ndugu zetu kutoka TPDC kwa moyo wa kutoa walioonyesha kwa kusaidia ujenzi wa zahanati yetu ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho ili kuondokana na adh ya kutembea umbali wa kilomita nane ili kupata huduma ya afya”.  

Ndugu Mdoe aliongezea kuwa, ni matumaini ya kijiji kwamba TPDC litaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Kijiji cha Kidundai kwani mahitaji yao ni mengi yakiwemo maji, barabara na shule 

Akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa Kijiji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Ndg. Asiad Mrutu ambaye ni Mjiolojia alisema “kipekee nimshukuru Mwenyekiti na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji kwa ushirikiano waliouonyesha toka tulipofika siku ya kwanza katika Kijiji hiki tukiwa na lengo la kutafuta eneo la uwekezaji, niseme tu kuwa huu ni mwanzo na tutaendelea kushirikiana bega kwa bega kusukuma gurudumu la maendeleo ya Kidundai mbele.” 

Pamoja na kukabidhi hundi hiyo, Ndg. Mrutu aliusisitiza uongozi wa Kijiji kuchanganua gharama za miradi ya maendeleo iliyopo katika mipango ili kurahisisha pale ambapo mdau wa maendeleo anaetaka kuchangia kufahamu ni kiasi gani kitatosha badala ya kueleza mahitaji kwa ujumla, hii itasaidia kupata msaada kirahisi na pia kupata msaada unaokidhi mahitaji ya mradi husika. 

Mchango wa ujenzi wa zahanati hiyo umekuja baada ya TPDC kufanikisha zoezi la kupata ardhi kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya utafiti wa mafuta na gesi hapa nchini kwa lengo la kuongeza kiasi cha gesi asilia nchini ambacho kwa sasa ni futi za ujazo trilioni (TCF 57.538) na upatikanaji wa mafuta ili kuweza kulihakikishia taifa nishati ya kutosha kwa ajili uzalishaji wa umeme, vyombo vya usafiri, matumizi ya nyumba na kuhakikishia nishati ya kutosha kwa maendeleo ya viwanda nchini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai,  Waziri Mdoe (Kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni nne kutoka kwa mwakilishi wa TPDC, Asiad Mrutu (Kulia). Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya jengo la zahanati inayoendelea kujengwa katika Kijiji hicho. 

TAMISEMI KUBAINI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

$
0
0
KAIMU Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Ernest Mkongo amefunga Mafunzo Elekezi ya kubaini watoto wenye mahitaji maalum yaliyowahusisha wataalam watambuzi hao mjini Morogoro.


Akitoa hotuba yake, mbele ya walimu, maafisa ustawi wa Jamii na baadhi ya madaktari, Mkongo amesema ana imani kubwa na wataalamu hao ambao wamepatiwa mafunzo ya kubaini kwa kutumia vifaa maalum kuwa watafikia malengo ya kazi waliyoelekezwa na Serikali ili kuboresha huduma ya elimu bora kwa watoto wenye mahitaji maalum nchini.


“Ni matumaini yangu baada ya mafunzo haya kuwa kila mmoja wenu atakuwa na ujuzi wa

kutosha kutumia vifaa maalum kuwabaini watoto wenye changamoto za uoni hafifu, ujongeaji wa viungo vya mwili, usikivu, changamoto nyingine ambazo hutegemea hali ya afya na mazingira,”Amesema.


Amesema Watoto hao wanatarajiwa kutoka rika la miaka minne hadi sita na kwamba wataalam hao watatoa ushauri wa kitaalam na kitabibu kwa wazazi na walezi wa watoto hao, na walimu wa watoto watakaobainika hivyo ni vema wakaifanya kazi hiyo kwa umakini na weledi mkubwa ili malengo ya Serikali yatimie.

 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Ernest Mkongo akifunga Mafunzo Elekezi ya kubaini watoto wenye mahitaji maalum yaliyowahusisha wataalam watambuzi hao mjini Morogoro.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu (Elimu ya Watu Wazima), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kassim Kaoneka akitoa neno la awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi. 
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Ernest Mkongo (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu (Elimu ya Watu Wazima), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kassim Kaoneka.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo Elekezi ya kubaini watoto wenye mahitaji maalum yaliyowahusisha wataalam watambuzi hao mjini Morogoro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.

“Serikali imejiimarisha katika kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa jengo hili kutachangia ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia sekta ya utalii nayo itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini wataongezeka.”

Amesema mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali inaendelea kuvikarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma, Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.

Akisoma taarifa za ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Christianus Ako amesema mradi huo umeajiri wafanyakazi 1,400 kwa sasa na wanatarajia kuongeza watumishi na kufikia 1,800.

Pia wanatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa vya umeme kuanzia Julai, 2018 kwa kuwa tayari utekelezaji wa kazi kubwa za ujenzi wa mradi huo zimefanyika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 23, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(wa pili kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo March 23, 2018 . Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kudhoto ni Msimamizi wa Mradi, Eng. Julius Ndyamukama .

WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA

$
0
0
Wakati umefika wa kufanywa utafiti wa kina kujua mazingira halisi ya Watu wenye mahitaji Maalum Nchini ili kupata mwanga wa uhakika wa kuelewa pamoja na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu mahitaji wanayopaswa kupatikana kwa kundi hilo katika Jamii.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Omar Seif Abeid alieleza hayo wakati akitoa Taarifa kwenye Kikao cha Majumuisho ya Ziara ya kamati hiyo hapo katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Mh. Omar alisema ushirikishwaji wa Watu wenye Mahitahi maalum yaani Walemavu bado ni mdogo hasa katika maeneo ya Vijiji jambo ambalo husababishwa kukumbwa na changamoto nyingi likiwemo wimbi la udhalilishwaji wa Kijinsia ambalo kwa sasa limeshika kasi na kuendelea kuwaathiri kiakili.

Alisema ipo haja kwa Taasisi za Umma kuendelea kuwatumia Masheha pamoja na Makundi ya Kioraia katika maeneo husika kuliona tatizo hili na kutafuta mbinu ya pamoja na kulitatua.

Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya Mwenyekjiti wake waliokaa kati kati Kulia Mheshimiwa Omar Seif Abeid wakiwa katika Kikao cha majumuisho ya ziara yao ndani ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kilichofanyika Vuga Mjini Zanzibar.
Baadhi ya watendaji Wakuu na Maafisa wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walioshiriki katika Kikao hicho cha Majumuisho ya Kamati hiyo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika Kikao hicho cha Majumuisho ya ziara yao ndani ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PANITA YAISHAURI SERIKALI KUHUSU MUHIMU WA LISHE BORA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JUKWAA la Lishe Tanzania(Panita) limeishauri Serikali kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kuhusu lishe kwenye jamii ya Watazania ili kuwa na taifa lenye uwezo wa kujituma na kuleta maendeleo.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa Program wa Panita, Jane Msagati wakati anazungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhusu lishe bora.

Amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha suala la lishe linapewa kipaumbele nchini kwa jamii kupata elimu itakayosaidia kutambua umuhimu wa lishe bora katika Taifa.

"Ukosefu wa lishe bora mwilini unasababisha udumavu na utapiamlo na matokeo yake husababisha magonjwa ambayo ni gharama kuyatibu na wakati mwingine husababisha ulemavu wa kudumu.

"Tatizo la lishe chini limesababisha kuongozeka kwa watoto wenye udumavu wa mwili na akili.Serikali inatumia fedha nyingi kugharamia matibabu, na hiyo ni hasara kubwa,"amesema Msagati.
Akizungumza kuhusu lishe  amesema ni msingi wa maendeleo kwa wote na jamii ihakikishe watoto wote wanapata lishe sahihi hususani siku 1000 za kwanza.

Pia amesema wababa wahusike kwenye malezi ya watoto na jamii ihakikishe kaya zinauhakika wa chakula kwa kuzalisha vyakula vya kutosha na kutotumia vyakula vyote kutengeneza pombe.

Amezungumzia umuhimu wa jamii kutengeneza bustani ndogondogo kuzunguka nyumba, bustani makasha/viroba kwa ajili ya mboga za majani.Pia kufuga wanyama wadogo kama kuku na  sungura.

Amesema ukosefu wa virutubisho mwilini husababisha njaa iliyojificha ambayo huchangia kwa kiwango kikubwa katika kusababisha magonjwa na vifo hususani kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na akina mama walio katika umri wa kuzaa

Kuhusu mafunzo ya lishe kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini, Msagati amesema wanatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha umma.

Msagati amesema wahariri wa vyombo vya habari ndio wenye jukumu la kupitisha habari kwenye vyombo vyao na hivyo kukutana kati ya Panita na wahariri hao kutatoa fursa ya kuelezea umuhimu wa kuzipa kipaumbele habari za lishe bora.

Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Bakari Kimwanga na Mgariri wa Jarida la Afya na Ajira kutoka Gazeti la Mwananchi, Lilian Timbuka wamezungumzia umuhimu wa mafunzo yaliyotolewa na Panita kuhusu lishe bora na kwamba watatumia vyombo vyao kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuzingatia lishe bora.
Meneja wa Program wa Jukwaa la Lishe Tanzania(Panita), Jane Msagati akitoa mada kwenye semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika leo Dar es Saalam leo Semina hiyo ilikuwa inangumzia umuhimu wa lishe bora kwa jamii.
Mwandishi Mwandamizi wa Mlimani TV, Annuary Mkama akitoa somo kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.
Wahariri na waandishi wa habari wakisikiliza mtoa mada katika semina la lishe bora kutoka kwa Meneja wa Programu wa Panita Jane Msagati(hayupo pichani).
Mtaalam wa masuala ya lishe kutoka Jukwaa la Lishe Tanzania(Panita), Deborah Esam akitoa mada kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Katiba na Sheria yajivunia utekeleziji wa Ilani ya CCM

$
0
0
Na Maura Mwingira, Dodoma 

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Palamagamba Kabudi ( Mb) amesema, Wizara yake pamoja na Taasisi ambazo zipo chini yake, imeendelea kutekeleza ahadi zote za Ilani ya Chama cha Mapinduzi zinazoambatana na na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria. 

Waziri Kabudi ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma. 

"Wizara yangu imekuwa ikiwajibika vilivyo katika kuhakikisha kuwa inatekeleza ahadi zote za Ilani zinazoambatana na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria" ameeleza Mhe. Waziri 

Akazitaja ahadi hizo kati ya nyingi, kuwa ni, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubathirifu wa mali ya umma, kukuza, kulinda haki za binadamu na utawala wa sheria katika ngazi zote za uongozi, kuimarisha mfumo wa utoaji wa haki na kukamilisha mchakato wa Katiba mpya. Akiwasilisha Mpango na Bajeti ya Wizara na Taasisi zake nane, Waziri aliiomba Kamati hiyo kupitisha zaidi ya Sh. 183.223.058,000bn/- zikiwa ni fedha za mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo kwa Wizara na Taasisi zake. 
Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi amesema Wizara yake   pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika sekta ya sheria, ambapo pamoja na mambo mengine, wananchi wanauelewa mkubwa wa namna ya kutafuta na kupata haki yao kisheria. Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.Pamoja naye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi.



MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MARCH 24,2018


VIDEO:FISSOO: WADAU WA FILAMU TUMIENI FURSA ZA MASOKO YA FILAMU KUJINUFAISHA

MADINI YA UJENZI, VIWANDA YANACHANGIA ZAIDI KWENYE UCHUMI KUPITA MENGINE – BITEKO

$
0
0

 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Dodoma, alipowatembelea akiwa katika ziara ya kazi, Machi 22 mwaka huu.

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akisalimiana na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Dodoma, alipowasili katika Ofisi hiyo akiwa katika ziara ya kazi, Machi 22 mwaka huu.

 Shughuli za uchimbaji madini ya nakshi zikiendelea katika Mgodi uliopo Ntyuka Dodoma, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) mgodini hapo Machi 22 mwaka huu.

Sehemu ya shehena ya mawe ya nakshi aina ya Graphite. Taswira hii ilichukuliwa Machi 22 mwaka huu wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) katika Mgodi uliopo Itiso wilayani Chamwino.


ØYachangia bilioni 7.1 mrabaha 2016/17

ØAsema usimamizi mzuri unaweza kukuza mchango huo kufikia bilioni 15 kwa mwaka.


Na Veronica Simba – Dodoma

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, amesema kuwa madini ya ujenzi na viwanda yanaipatia Serikali fedha nyingi kupita aina nyingine zote za madini yanayopatikana nchini.


Akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Dodoma, Machi 22 mwaka huu akiwa kwenye ziara ya kazi, Biteko alisema kuwa takwimu za makusanyo ya Serikali zinabainisha hayo.


“Mfano mwaka 2016/17, takribani tani milioni 15.6 za madini ya ujenzi zilizochimbwa, zilizalisha shilingi bilioni 230.6; ambapo katika hiyo, ulipatikana mrabaha wa shilingi bilioni 7.1,” alisema.


Akifafanua zaidi, Naibu Waziri Biteko alieleza kuwa, idadi ya wachimbaji wa dhahabu na madini mengine nchi nzima ikijumlishwa, haiwezi kufika hata robo ya wale wanaofanya shughuli za madini ya ujenzi nchini.


Alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inaongeza vituo vya madini ya ujenzi na viwanda kutoka 85 vilivyopo sasa nchi nzima hadi kufikia 174. “Nina uhakika tukiviongeza vituo kufikia idadi hiyo, tutakusanya mrabaha wa zaidi ya shilingi bilioni 15 katika madini hayo pekee.”

AMOS CHEREHANI ENDORSES LIBE KUWA RAIS WA JUMUIYA DMV

$
0
0
Bwana Amos Cherehani usiku wa Alhamis March 22 amethibitidha kumu endorses Liberatus Mwang’ombe, ambae anawania kiti cha urais wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washington

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

$
0
0
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa.  Katikati  mwenye tai akikagua maendeleo ya ujenzi  wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa   Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam,leo March 23/2018 .Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kulia ni Msimamizi wa Mradi. Eng. Julius Ndyamukama.
 Mwonekano wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka na kuwa na.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.

“Serikali imejiimarisha katika kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa jengo hili kutachangia ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia sekta ya utalii nayo itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini wataongezeka.”

Amesema mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali inaendelea kuvikarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma, Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.
Akisoma taarifa za ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Christianus Ako amesema mradi huo umeajiri wafanyakazi 1,400 kwa sasa na wanatarajia kuongeza watumishi na kufikia 1,800.

Pia wanatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa vya umeme kuanzia Julai, 2018 kwa kuwa tayari utekelezaji wa kazi kubwa za ujenzi wa mradi huo zimefanyika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 23, 2018.

KAMPUNI YA DATA VISION KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPELEKA NCHI KWENYE UCHUMI WA KATI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
KAMPUNI ya International Data Vision inayohusika na masuala ya Utafiti, imeahidi kushirikiana na Serikali ili kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda.

Ahadi hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Geofrey  Maclean wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Pia amesema licha ya kueleza mafanikio ya shirika hilo ameeleza mbinu mkakati za kiubunifu  za kutofanya biashara kimazoea na hiyo ni kwa kuhusisha matumizi ya teknolojia(ICT) na tafiti mbalimbali na kujua mahitaji ya soko la dunia.

Aidha ameomba ushirikiano wa wafanyakazi na watu wanaowafikia katika maeneo mbalimbali.

Kuhusu kushirikiana na Serikali katika kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati Mwaijonga ameeleza wanaunga mkono dhamira hiyo na wanashiriki kwa namna mbalimbali kama vile kulipa kodi stahiki kwa Serikali, kutengeneza ajira na kuleta ubunifu mpya katika biashara.

Pia Mwaijonga amesemaleza wana mpango mpya wa kusafirisha maarifa (skills)ili  zikatumike katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuiongezea nchi kipato kitakachosaidia kuifikisha kwenye uchumi wa kati.
 Mkurungenzi  Mtendaji wa Kampuni  ya Data Vision International, Geofrey  Maclean Mwaijonga aizungumza na wafanyaazi wa kampuni hoyo  katika maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
 Wafanyaazi wa kampuni  Data Vision International  wakimsikiliza Mkurungenzi  Mtendaji wa Kampuni hiyo, Geofrey  Maclean Mwaijonga wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Viewing all 109924 articles
Browse latest View live




Latest Images