Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SERIKALI YA UINGEREZA YAFUATA NYAYO ZA JPM KATIKA MUSTAKABALI WA PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI

$
0
0
Muonekanao wa E-Passport zilizotolewa mapema mwaka huu.

*Yavuja mkataba na kampuni iliyonyimwa tenda ya kutengeneza passport ya kielekroniki za Tanzania
*Lengo ni kukataa kutengeneza passport kwa gharama kubwa
*ni baada ya kugundua Tanzania imeokoa fedha nyingi kwa kuinyima tenda kampuni hiyo iliyokuwa na mkataba wa miaka kumi na serikali ya uingereza

KAMPUNI ya De La Rue  (BOFYA HAPA KUIJUA KWA UNDANI) ambayo ilishindwa kwenye zabuni ya E-Imigration ambapo ingetengeneza e-passport, e-Visa, e-Imigration nchini Tanzania imepata pigo jingine baada ya mkataba wake kusitishwa na Serikali ya Uingereza ya kuendelea kutengeza hati za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Aliance News imesema kuwa kampuni ya De La Rue ilikuwa na mkataba na Uigereza wa miaka 10 lakini nchi hiyo imeamua kuvunja mkataba kati yake na kampuni hiyo.

Imefahamika lengo la Serikali ya Uingereza kuvunja mkataba huo wa kutengenezwa hati za kusafiria ni kutokana na gharama kuwa kubwa za utengenezaji wa hati hizo na hivyo kuamua kuipa zabuni kampuni ya French firm Gemalto.

"Hati mpya za kusafiria za Uingereza hazitatengenezwa tena na kampuni ya De La Rue ambayo ndio iliyotengeneza hati zitumikazo kwa sasa.

"Hivyo hati hizo mpya za rangi ya blue ambazo zitatumika baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya zitatengenezwa na kampuni ya French firm Gemalto. Kubadilika kwa rangi ya hati hiyo kunatafsiriwa kuwa ni alama ya kurudi kwa nguvu ya Uingereza, umesema mtandao ulitoa taarifa hizi.

Pia taarifa zinaeleza kuwa Kampuni ya De La Rue inafikiria kukata rufaa baada ya kukosa na kushindwa katika zabuni ya kutengeneza hati hizo mpya.

Kampuni hiyo imeripotiwa ikidai haikuridhishwa kwa kupoteza zabuni hivyo hivyo inaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza

Hata hivyo Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya De La Rue Jitesh Sodha amesema kitendo hicho kimesababisha hisa za kampuni yao kutoka asilimia 14 ya Jumanne ya wiki hii hadi kufikia asilimia 0.4 leo Machi 22 ya mwaka huu.

"Tumechukizwa na kitendo cha Serikali ya Uingereza kusitisha mkataba wetu wa kutengeneza hati za kusafiria za nchi hiyo wa miaka 10 kwani ulikuwa mkataba unamalizika Julai mwakani.

Hivi karibuni katika uzinduzi wa E-Passport, Rais Dk. John Magufuli amesema kuwa kuna wajanja awali walipanga kuutekeleza mradi huo kwa gharama kubwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 226 ambazo ukizibadili kwa Dola moja sawa na shilingi 2245 mradi huo ungegharimu shilingi za kitanzania bilioni 507.

Rais Magufuli alisema baada ya kugundua ujanja huo Rais alivituma vyombo vya dola kufuatilia na kubainika mradi huo unaweza kutekelezeka kwa gharama nafuu na za kawaida ambapo baadae mradi umeonyesha kutelekezwa kwa dola milioni 57.8 sawa na bilioni 129 za kitanzania na hivyo kuliokolea taifa upotevu ambao ungeweza kujitokeza wa zaidi ya shilingi bilioni 380.

Moja ya kampuni ambayo ilikosa zabuni ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria nchini Tanzania ni hiyo ya De La Rue na moja ya sababu ilikuwa ni kiasi kikubwa cha fedha ambazo walikihitaji lakini Serikali iliwashutukia na kuamua kutoa zabuni kwa kampuni nyingine iliyotengeza kwa gharama nafuu.

Hata hivyo vyanzo vya kuaminika kutoka Serikali ya Tanzania vilibanini mambo mazito yaliyoibuka baada ya kubainika kampuni hiyo kuhonga mamilioni ya fedha ili kuichafua mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla.

Facts The Economist Got Them Wrong on Magufuli

$
0
0
By Dr. Herman Louise Verhofstadt
 “A BIT like President Donald Trump, Tanzania’s president, John Magufuli, likes to fire employees on television. In November Mr. Magufuli used a live broadcast from a small town in the north of the country summarily to dismiss two officials,” this is an extract from a recent online article I came across from the newspaper that I admired when I was growing up in Europe back in 1990’s; the Economist. 

 Before I venture into other serious issues, the excerpts above contains gross factual errors; my own fact-check indicates that in the named public rally during the opening of Kagera Airport, there was no summary dismissal of the two officials instantly on television, as alleged. Instead, the two, one District Executive Directors for Bukoba Urban and another for Rural were relieved their duties later through a press release from President’s Office. 

 This is my prima impressio reading the Economist this week, a publication known for its top notch ethical and analytical standards, that has now vanished into a hell of sensational journalism, half baked facts, lack of objectivity and a clear sense of bias. 
 Contrary to the fact deprived article, it is my candid observation that to objectively critique Magufuli’s presidency in the circumstances of the transformation he is doing for his people in Tanzania, requires the level of conscious that is unfortunately lacking in the current editorial team at the Economist. 
 Living in Tanzania for close to half a decade now, it makes me a better eye-witness than the Westminster based editorial team. To say the least, this man Magufuli rose into power in a country that was downed by massive corruption scandals, political demonstrations that caused deaths and worse enough he found media fraternity that was being corrupted to work for interest groups. In my stay here before and after his presidency, I have witnessed real transformation, his work is exemplary and fascinating one. 
 Everybody here—may be just like what Theresa May is doing in London and what Trump is focusing in Washington, is aware that Tanzania is on the move towards pro-people development; something the Economist is unhappy for and would frame it with usual western biases; suppression of democracy, violation of press rights etc etc! 
 Under Magufuli’s “rogueness” I have seen leaders going into prison or dismissed for lack of action in protecting public funds, I’m seeing public service regaining its lost fame and massive social projects being implemented across the country-sadly the Economist would reduce all these far-fetching achievements to nothing but “rogueness.”

MKAZI WA MOSHI KUTIMIZA NDOTO ZAKE BAADA YA KUSHINDA BAJAJI

$
0
0
Mkazi wa Moshi Ndugu Erasto Dismas Floridi (22) akabidhiwa bajaji yake mara baada ya kuibuku kuwa mmoja kati ya washindi wa promosheni ijulikanayo kama Jiongeze na Mpesa, Shinda na SportPesa inayoendesha na kampuni ya michezo ya mubashiri SportPesa wakishirikiana na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom PLC.

Najishughulisha na biashara ya duka kama unavyoona na watu wa kwanza juwapa taarifa juu ya ushindi wangu ni marafiki zangu, kusema ukweli hakuna aliyeamini juu ya ushindi wangu mimi mwenyewe sikuamini ila nikasema ngoja nione mwisho wa hichi kitu utakuwaje”

Sikuwahi kufikiria kama siku ntapata bajaji katika maisha yangu, hii ni zawadi kubwa kwangu na naimani itabadili maisha yangu kwa kiasi kikubwa kwa sababu ntaifanyia biashara na pesa ntakayoipata ntawekeza ili kuchukua mkopo na kufungua duka langu mwenyewe huku biashara yangu ikiwa inaendelea”
Mimi ni kaka wa familia na nina mdogo wangu ambaye namsomesha kwa sababu mama yetu ni mjane kupitia bajaji hii itakuwa imetusaidia sana kwenye kulipia vitu mbali mbali vya familia ikiwemo kumalizia nyumba yetu”.

Kwa upande wa SportPesa Meneja Uhusiano Bi. Sabrina Msuya alisema “Mpaka sasa mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kupata washindi watatu huku mikoa mingine kama Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Nj’ombe, Mara, Musoma Songea na Sumbawanga ikiwa na mshindi mmoja mmoja”

“Pointi zetu za kuweka ubashiri wako ni nzuri kulinganisha na kampuni nyingine, endapo mteja wetu atashinda kwenye ubashiri wake pesa itaingizwa muda huo huo mara baada ya mechi kuisha, kitengo chetu cha huduma kwa wateja kinafanya kazi saa ishirini na siku saba za wiki ili kuhakikisha mteja wetu anapata huduma inayostahili sambamba na kuhakikisha inasikiliza na kutatua matatizo ya wateja wetu.”

TAARIFA KWA UMMA

RC RUVUMA AZINDUA MRADI WA PANDA MITI KIBIASHARA

$
0
0
Mkuu wa wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINA MNDEME amezindua siku ya upandaji miti kimkoa katika halimashauri ya MBINGA,ambapo katika zoezi hilo zaidi ya miti laki mbili imepandwa wilayani humo aina ya paini inayokadiriwa kukomaa baada ya miaka saba Serikali kupitia mradi wa panda miti kibiashara imetenga shilingi milioni mia moja kwa wilaya ya Mbinga,Nyasa, Na Halimashauri Ya Madaba ,Huku wastani wa hekali moja mkulima anaweza kujipatia shilingi milioni ishirini, HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

MPANGO WA PAMOJA TANZANIA,CHINA KUONGEZA UZALISHAJI ZAO LA MAHINDI MKOANI MOROGORO WAZINDULIWA

$
0
0
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin, akimuonyesha Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, moja ya picha katika Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini, katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji hicho. Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro na Chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha China. Nyuma yao ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro.
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, akisalimiana na Profesa Wu Jiu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji  cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
 Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. 
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
 Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.

SHIRIKA LA AGPAHI LAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE KWA WILAYANI MUHEZA

$
0
0
SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy machine).

Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.

"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema Mwakyusa.Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze kazi.

Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

TRUMP AMFUTA KAZI MSHAURI WA USALAMA, AMPA KIJITI BOLTON JOHN

$
0
0
Mshauri mteule wa masuala ya usalama Marekani, Bolton John (69).

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
RAIS  wa Marekani, Donald Trump amemteua  Bolton John (69) kuwa Mshauri wa masuala ya usalama baada ya kumwachisha kazi aliyekuwa katika nafasi hiyo H.R  McMaster.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Trump ameandika kumteua Bolton John (69) kuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa na mteule huyo kuanza kazi rasmi ifikapo mwezi Aprili.

Inasemekana kupishana kauli kati ya Trump na McMaster siku za nyuma  ndiko juu ya sera za nchi hiyo ndiko kulikopelekea maamuzi ya Rais Trump kumfukuzisha kazi.

John Bolton anakuwa mshauri wa tatu wa masuala ya usalama huku akiwa amehudumu katika mihula kadhaa na aliwahi kuhudumu kama mwakilishi wa Marekani Umoja wa Mataifa.

McMaster ataungana na aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje, Rex ambaye alifutwa kazi siku chache zilizopita kutokana na maamuzi ya Rais Trump.

AZAM KUJIPIMA NGUVU KWA FRANCE RANGERS KABLA YA KUVAANA NA MTIBWA SUGAR

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wanawakaribisha France Rangers katika dimba lao la nyumbani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.

France Rangers ni timu ambayo imemaliza msimu huu daraja la kwanza Mkoa wa Dar es Salaam yenye kikosi kizuri na wachezaji walio fiti uwanjani.

Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya timu hizo mbili utachezwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi  utakaofanyika kesho Jumamosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari Azam FC Jaffary amesema pamoja na kikosi chao kinaendelea na mazoezi  kukabiliana na Mtibwa sugar katika mchezo wa robo Fainali kombe la  FA  machi 31 mwaka huu, mwalimu na benchi la ufundi kuweza kuwapima wachezaji kwa kuomba mechi ya kirafiki dhidi ya France Rangers ya Dar es Salaam.

"Ni sehemu tu ya benchi  la ufundi na mwalimu kuweza kuangalia baada ya mazoezi ya wiki moja na nusu pengine tu ni kutaka kuona kiwango cha  wachezaji pamoja na uwezo  wa kila mchezaji walichokielewa katika hazoezi hayo" amesema Jaffary.

Amesema katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao mahiri wanne ambao ni Himidi Mau, Yahaya Zayd na Shabani Chilunda ambao wameitwa katika timu ya Taifa (Taifa Satars),mwengine ni Daniel Amor kutoka Ghana ambaye ni majeruhi.

"Mchezaji wetu nyota wa kimataifa kutoka nchini Ghana Daniel Amor anasumbuliwa na tatizo la goti, uongozi utamsafirisha  Amor  Siku ya  Jumatatu kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu" amesema Jaffary.

POLISI YATOA ONYO WANAOIBIA WATALII ZANZIBAR.

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limesema Operesheni ya kukabiliana na mtandao wa dawa za kulevya katika Visiwa vya Zanzibar itaendelea sambamba na kuwadhibiti wahalifu wanaofanya vitendo vya kuwaibia na kuwadhuru watalii jambo ambalo linatia doa usalama uliopo katika visiwa hivyo.
Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa Operesheni maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas ambaye yupo Zanzibar akiongoza timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Kamisheni ya Polisi Zanzibar kwa lengo la kuongeza nguvu katika kuzuia na kupambana na mtandao wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu dhidi ya watalii.
DCP Sabas amesema Operesheni hiyo haitawaacha wahalifu hao salama kwa kuwa inafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa haiachi mhalifu yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo viovu ambavyo vimekuwa vikichafua taswira nzuri ya usalama.
“Operesheni hii ni endelevu na niwape tu salamu wahalifu kuwa jambo la msingi ni wao wenyewe kujisalimisha kwa kuwa awamu hii hata wakikimbia tutawasaka na kuwakamata  kwa kuwa nguvu ipo na tunapata ushirikiano kwa wananchi wema wanaochukia vitendo vya uhalifu” Alisema Sabas.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hasina Tawfiqi amesema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin jumla ya Kete 695 sawa na ujazo wa gramu 31.3 pamoja na Watuhumiwa 21.

Amewasihii wakazi wa Kaskazini Unguja na mikoa jirani kuendelea kutoa taarifa ili kuweza kukomesha mtandao wa biashara hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa watalii wanaotembelea mkoa huo wanafanya kazi zao kwa amani na usalama.
Operesheni hiyo pia imefanyika katika Mkoa wa Mjini magharibi ambapo Jumla ya watuhumiwa 58 walikamatwa pamoja na dawa za kulevya aina heroin Kete 1293 na Vifuko vitatu sawa na Gramu 74.385.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Hasina Tawfiqi wakati wa Operesheni maalum ya kukabililiana na mtandao wa dawa za kulevya na uhalifu dhidi ya watalii inayoendelea katika mikoa ya Zanzibar. (Picha na Jeshi la Polisi)

JAYDEE ATAJA WAKALI WATAKAOSHIRIKI SHOO YAKE YA UNAWEZA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
MALKIA wa muziki wa Bongo fleva nchini, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee ametaja majina ya wasanii wengine watakaomsindikiza katika Tamasha la  Unaweza linalotarajia kufanyika Machi 31 mwaka  katika Hotel ya Golden Tulip Ostetbay.

Akizungumza na Michuzi blog Jaydee amewataja wasanii hao ni Bushoke, Nick Mbishi, Alawi Junior na Wengine wengi.

"Hii ni shoo ambayo nataka kila mtu afurahie muziki akiwa nyumbani na ladha ambazo walikuwa wamezikosa kwa muda mrefu, hivyo kupitia onesho hilo nitaka kiu yao ya kutonusikia kwa muda kidogo," amesema Jaydee

Aidha mwanamuziki huyo amesema siku hiyo kutakuwa na watu maarufu akiwamo MC Pilipili na wengine wengi.

Amesema maandalizi ya shoo hiyo yamekamilika na kwamba amejiandaa vya kutosha.

Amefafanua shoo hiyo itaanza  saa12 jioni ambapo Machozi Band watakuwa jukwaani na kumalizika  saa  sita usiku atamaliza lakini ana uhakika watakaofika watakuwa wameandika historia ya aina yake kutokana na namna alivyojiandaa.

BEST "YOU'LL NEVER WALK ALONE" EVER!

KATIBU MTENDAJI BODI YA FILAMU AFANYA ZIARA YA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (kulia) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msevela (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo. Bi Joyce Fissoo yupo mkoani Shinyanga kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke iliyoandaliwa na kikundi cha sanaa cha Bongo Movie Shinyanga.
 Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga, Mariam Ally akizungumza na umoja wa Chama cha Wasanii wa mkoa wa Shinyanga wakati wa mafunzo ya uandaaji wa filamu yaliyofanyika leo. Mafunzo haya ni sehemu ya utangulizi kabla ya uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke iliyoandaliwa na kikundi cha sanaa cha Bongo Movie Shinyanga utakaofanyika baadae hii leo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kuandaa filamu yaliyofanyika mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Shinyanga, Saidu Miraji na Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga, Mariam Ally. Bi Joyce Fissoo yupo mkoani humo kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke iliyoandaliwa na kikundi cha sanaa cha Bongo Movie Shinyanga utakaofanyika baadae hii leo.

TBA YATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA WAKATI

$
0
0
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wametembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika eneo la Njedengwa mkoani Dodoma.

Mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo wajumbe hao wameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi ya Wakala wa Majengo nchini Tanzania (TBA) wanaojenga jengo hilo na kuwataka waukamilishe mradi huo kwa wakati kama ilivyopangwa.


Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi

$
0
0
Na Greyson Mwase, Pwani
Wilaya za Mkuranga, Kibiti na wilaya ya Rufiji katika kata ya  Ikwiriri zimeanza  kupata nishati ya uhakika ya umeme mara baada ya kuunganishwa katika Gridi ya Taifa na kukamilika kwa kituo cha kupozea umeme cha Mbagala kilichopo jijini Dar es Salaam.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na wananchi wa Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani katika ziara yake ya siku moja jana (tarehe 22 Machi, 2018) ya kukagua miundombinu ya umeme iliyounganishwa na Gridi ya Taifa kutokea katika kituo cha kupoza umeme cha Mbagala hadi Ikwiriri na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Dkt. Kalemani alisema lengo la kuunganisha wilaya hizo na Gridi  ya taifa ni kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya umeme wa uhakika na kuondokana na umeme unaotokana na mitambo ya mafuta ya Somangafungu  ambayo imekuwa ikiharibika mara kwa mara.

Alisema awali kabla ya wilaya hizo kuunganishwa na Gridi ya Taifa, kulikuwepo na changamoto ya kukatika kwa umeme katika wilaya hizo kutokana na mitambo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali iliamua kuunganisha  wilaya hizo kwenye Gridi ya Taifa ili kuwepo na umeme wa uhakika ambao mbali na matumizi ya majumbani unategemewa na viwanda  vilivyopo katika mkoa wa Pwani.

Katika hatua nyingine akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinyanya kilichopo katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani ambapo aliwasha rasmi umeme, Waziri Kalemani aliwataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kupitia REA kuhakikisha vijiji vyote na  vitongoji vyake vinapata umeme wa uhakika.
 Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Alex Adam (wa pili kushoto) akielezea shughuli zinazofanywa na kituo cha kupoza umeme cha Mbagala kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) katika ziara hiyo.
 Mafundi wa kampuni ya Sengerema Engineering wakikamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa ajili ya kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa katika kijiji cha Kinyanya kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akibonyeza kitufe kuashiria uwashaji wa umeme katika kijiji cha Kinyanya kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DAMU SALAMA NA MEWATA WAFUNGUA UKURASA MPYA WA USHIRIKIANO

$
0
0
Chama cha madaktari wanawake Tanzania (MEWATA) kinaendesha kampeni (tarehe 22- 24 machi ) ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi mkoani Lindi  katika hospitali ya mkoa ya sokoine.  Kampeni hiyo ilizinduliwa na mke wa rais mstaafu Mhe. Mama Salma Kikwete Mbunge wa viti maalum, baada ya ufunguzi wa kampeni hiyo, akinamama na wasichana mkoani Lindi, walipata fursa ya kufanya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya matiti na mlango
wa kizazi.
Mpango wa Taifa wa Damu Salama kanda ya kusini Mtwara unashiriki katika kampeni hiyo kwa kuendesha zoezi la kuchangia damu kwa wananchi wenye afya na vigezo vya kuchangia damu mkoani Lindi.
Akizungumza baada ya kuchangia damu Raisi mstaafu wa MEWATA Dkt. Marina Njelekela aliwaasa wananchi wenye uwezo na vigezo vya kuchangia damu wajitokeze kuchangia damu kwani mahitaji ni makubwa kutokana na ajali za barabarani na kina mama wakati wa kujifungua, Dkt. Marina aliendelea kusema “viwango wa kimataifa vinaelekeza mwanaume achangie damu kila baada ya miezi mitatu na mwanamke kila baada ya miezi minne”.

Kwa upande wa Damu Salama  Afisa mawasiliano na uhusiano wa Mpango bwana Rajab Mwenda alitoa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari na pia alikumbusha Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kushirikiana na Timu za damu salama halmashauri zinatarajia kuendesha kampeni ya mwisho ya robo mwaka (Januari- machi) tarehe 26- 30 machi nchi nzima hivyo aliomba wananchi waunge mkono kwa kujitokeza kuchangia damu.
 Dkt. Marina Njelekela akichangia damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi mkoani Lindi  katika hospitali ya mkoa ya sokoine.
Mhe. Mama Salma Kikwete akicheza nyimbo ya nani kama Mama ya Christian Bella baada ya uzinduzi wa Kampeni ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi iliyofanyika mkoani Lindi  katika hospitali ya mkoa ya sokoine.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFANYA UKAGUZI WA VIFAA VYA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MOTO

$
0
0
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Edgar Mwakapala akionesha jinsi ya kuzima moto kwa kutumia blanket maalumu la kuzimia moto kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala iliyopo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wakati wa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto mapema leo asubuhi.
Mmoja kati ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala akifanya mafunzo ya kuzima moto kwa vitendo kwa kutumia kizimia moto  chenye mchanganyiko wa maji na povu (Foam) wakati wa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto mapema leo asubuhi. 
(Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFANYA UKAGUZI WA VIFAA VYA KINGA NA TAHADHARI, DHIDI YA MOTO NA KUTOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO VYA HUDUMA YA KWANZA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

VOA Swahili: Duniani Leo 22 March 2018

MICHUZI TV: UBONGO TIME

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BILL MELINDA GATES FOUNDATION

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates, Rodger Voorhies kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates, Rodger Voorhies kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images