Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

DC MTWARA AKAGUA ENEO LA CHUO CHA KILIMO MATI LILILOVAMIWA NA WANANCHI

$
0
0
 Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda jana machi 21/2018 ametembelea eneo la Chuo cha Kilimo MATI mkoani Mtwara ili kujionea uvamizi uliofanywa na baadhi ya wananchi kwenye eneo la chuo ambapo wavamizi wamefyeka na kupanda mazao ya kudumu kuashiria kujitwalia isivyo halali maeneo hayo.


Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Mtwara wakati walipokagua eneo la chuo cha Mati Mtwara lililovamiwa na wananchi.
Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akimsikiliza Mmoja wa wazee majirani walioshuhudia wakati serikali ikitwaa eneo hilo la hekta 560 na kuwalipa fidia wenyeji mwaka 1974 wakati akiongea na kamati
Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akizungumza baadhi ya wajumbe wakati wa ukaguzi wa eneo hilo la hekta 560 ambalolimevamiwa na wananchi.

Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akizungumza baada ya kukagua eneo hilo la hekta 560 ambalo serikali ililitwaa na kuwalipa fidia wenyeji mwaka 1974.

USHAHIDI WA DAKTARI KUHUSU SABABU ZA KIFO .

$
0
0

Na Bashir Yakub.


Unaweza kuwa wewe, ndugu yako,rafiki au  jamaa yako ameunganishwa katika kesi ya mauaji. Aghalabu, daktari anasubiriwa kutoa ushahidi mahakamani kuhusu sababu za kifo cha marehemu.

 Na ni ushahidi huo wa daktari utakaokuondoa katika kesi  hiyo ya mauaji au utakuingiza katika kesi hiyo na hivyo kutiwa hatiani na kuadhibiwa.


Lakini sio daktari tu bali wenye kesi wote ambao ushahidi wake unahitaji mtaalam(expert) kuthibitisha mfano mkemia, mtaalam wa muandiko na sahihi, mtaalam wa biashara , mtaalam wa DNA  nk.


1.USHAHIDI WA DAKTARI.


Kifungu chac 47 cha Sheria ya Ushahidi kinaruhusu kutumika na kukubalika kwa ushahidi wa mtaalam( expert). Mtaalam ni pamoja na daktari.


2. MAMBO  6  MUHIMU UNAYOTAKIWA KUJUA.

A ).  Kabla daktari au mtaalam mwingine yoyote hajaanza kutoa ushahidi wake ni ni muhimu sana athibitishe kwa ushahidi kuwa yeye ni mtaalam kweli (expert) kwa hicho anachotaka kutolea ushahidi. Usikubali akaanza  kueleza kabla ya kuthibitisha utaalam.Mtake athibitishe hilo kwanza.


Utaalam unathibitishwa kwa taaluma(professional). Kama ni daktari na mtaalam wa eneo fulani la tiba ,mfano mifupa, moyo, nk, aoneshe cheti cha taaluma katika eneo hilo. Halikadhalika kwa wataalam wengine nao wanatakiwa kufanya hivyo. Kama hawezi kuthibitisha hilo basi hiyo ni faida kwako kwakuwa ushahidi wake ni wa kutia shaka.


Na hapo haijalishi mtaalamu(expert) huyo ameletwa na nani. Awe ameletwa na polisi, PCCB, au idara nyingine yoyote. Msimamo huu ulitolewa na mahakama  katika kesi ya MUHAMMED AHMED V 

REPUBLIC(1957)E.A. C.A 523.

B ). Daktari au shahidi yoyote mtaalam, asiwe tu mtaalam wa vyeti, bali awe mwenye ujuzi wa uzoefu wa kazi husika. Kwa mfano, daktari au mtaalam ambaye amemaliza chuo, ana cheti lakini hajaajiriwa wala kuwahi kuifanyia kazi taaluma yake popote hawezi kuitwa mtaalam mwenye uwezo(competence) wa kutoa ushahidi wa kitaalam.

                 
   KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com


WAZIRI MKUCHIKA ATAKA POLISI KUWA MSTARI WA MBELE KUKEMEA RUSHWA

$
0
0
Aipongeza Taasisi ya Uongozi kuwaandaa watumishi wa Serikali kuwa uongozi wazuri

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika amewataka Jeshi la Polisi kuwa mstari wa mbele katika kukomesha vitendo vya rushwa huku akisisitiza kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya utawala bora.

Mkuchika ametoa kauli hiyo jana jioni jijini Dar es Salaam kwa maofisa wa Jeshi la Polisi 32 kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao wamehitimu mafunzo ya Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute).

Mafahali hayo ni ya kwanza kutolewa na taasisi hiyo ambayo wameshirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland na hivyo kufanya mafunzo hayo kutambulika na kukubalika kimataifa kuhusu masuala ya uongozi.Hivyo akizungumza na maofisa hao pamoja na wageni wengine waalikwa ,Mkuchika amewapongeza wahitimu hao lakini awakata kuwa mstari wa mbele wao pamoja na jeshi la polisi kwa ujumla wake kupambana na komesha rushwa.

Amesema katika mataifa mbalimbali maeneo ambayo rushwa inaangaliwa sana ni katika Mahakama na Polisi .Hivyo ni vema polisi nchini wakawa mstari wa mbele kukomesha rushwa.

"Mataifa mengi yanapimwa katika mambo ya kupambana na rushwa pamoja na kuangalia maeneo mengine pia wanaangalia na Jeshi la Polisi.Na kwa bahati mbaya kwenye nchi nyingi baadhi ya polisi wamekuwa wakituhimiwa kujihusisha na rushwa, hivyo ni vema waliopata mafunzo hayo ya uongozi wakawa mabalozi wa kukemea rushwa nchini,"amesema Mkuchika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YATEKELEZA MAOMBI 5 YA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

$
0
0
Serikali kupitia, Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), imetekeleza maombi 5 ambayo yanawasaidia wafugaji hao  kuongeza thamani ya mifugo yao  kupitia Soko la Kimkakati la mifugo Longido lililojengwa na Program hiyo.

Mwishoni mwa mwaka 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama, alikuwa na ziara ya kukagua  ujenzi wa soko hilo wilayani humo, ambapo  baada ya ukaguzi alikutana na wafanyabiashara ya mifugo, ambao  waliwasilisha maombi  5,  ambayo yangeweza kuongeza Thamani Biashara za Mifugo na kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.

“Serikali ya awamu ya tano imeamua kuwasikiliza watu wanyonge na ambao wanajituma kuchapa kazi, lakini pia lengo la Program ya MIVARF ni kuongeza kipato kwa  wananchi hasa waishio vijijini, kwa mantiki hiyo nilimuelekeza Mratibu wa Program Kutekeleza maombi yao haraka sana ili wafugaji hawa wapate tija ya ufugaji kupitia soko hili” alisema Mhagama

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema maombi waliyowasilisha serikalini ili waweze kupata tija ya mifugo kupitia soko la Kimkakati la Mifugo Longido yamefanyiwa kazi na Program ya MIVARF ndani ya miezi mitatu tangu wayasilishe, ikiwa ni; Mizani ya kupima mifugo, Maji ya kunyweshea mifugo, machinjio, Josho, pamoja na  umeme.

“Tulihitaji maji hapa ili mifugo isije ikafa wakati inasubiri kuuzwa kwa kukosa maji, lakini umeme hapa ni muhimu kwani biashara zetu zinafanyika usiku, tayari hadi jenereta imeletwa kwa ajili ya kuhakikisha biashara haikwami kwa dharura yoyote ile, lakini mizani itasaidia kutowauza mifugo kwa kuangalia kwa macho bali kwa uzito wao” alisema Laizer
 Sehemu ya kunyweshea mifugo iliyojengwa katika ​​Soko la Kimkakati la Longido,  Wilayani Longido kwa ufadhili wa  Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Baadhi ya mifugo wakiwa katika eneo la kunywa maji kablaya kuuzwa katika Soko la Kimkakati la Longido,  Wilayani Longido ambalo limejengwa kwa  ufadhili wa  Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BEI ZA BIDHAA MATUNDA NA MBOGABOGA SOKO LA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mboga aina ya Spinach fungu sh. 500, Tembele sh 500
Mkungu wa ndizi katika soko la Kinondoni unauzwa kati ya sh 25,000 hadi sh 30,000.
Bei za mchele katika soko la Kinondoni kama inavyoneshwa katika vibao
Mfanyabiashara akitembeza biashara zake katika maeneo ya kinondoni
Embe katika soko la Kinondoni linauzwa kati ya sh 1000 hadi sh 1500, Papai sh 2000 hadi 400 hutegemeana na ukubwa wa Papai, Nanasi sh 3000 hadi sh 4000, Ndizi Mbivu inauzwa kati ya sh 250 hadi sh 300.(Imeandaliwa na Emmanuel Massaka , Globu ya Jamii).

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MGODI WA BUHEMBA NA CATA MINING

$
0
0
Na Veronica Simba – Mara
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imetembelea na kukagua Mgodi wa Buhemba na ule wa CATA Mining Ltd iliyopo mkoani Mara ikiwa katika ziara ya kazi Machi 15 mwaka huu.
Katika Mgodi wa Buhemba, Kamati ilielezwa kuwa, Serikali iliukabidhi Mgodi huo wa dhahabu kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mwaka 2011 ili iuendeleze, kutoka kwa mmiliki wake wa awali ambaye ni Kampuni ya Meremeta Limited.
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi Sylivester Ghuliku, aliieleza Kamati kuwa Shirika limekamilisha upembuzi yakinifu katika mabaki ya dhahabu yaliyoachwa kipindi cha nyuma ambapo umebaini kuwapo takribani tani 796,400 za mabaki ya mchanga wa dhahabu yenye wastani wa kilo 852 za dhahabu.
“Aidha, upembuzi huo ulibaini kuwa mabaki hayo ya mchanga yatachenjuliwa kwa kutumia teknolojia ya Carbon in Leach (CIL). Mtambo unatarajiwa kuchakata mabaki ya mchanga wa dhahabu kiasi cha tani 246,240 kwa mwaka,” alisema.
Aliongeza kuwa, tathmini ya kiuchumi ya mradi imeonesha gharama za uwekezaji zinakadiriwa kufikia Dola milioni 3.96 na kwamba gharama za uendeshaji kwa mwaka zinakadiriwa kufikia Dola milioni 4.46 na kutarajiwa kuingiza faida inayofikia Dola milioni 3.45 kwa mwaka.
Kuhusu tathmini ya mashapo katika miamba migumu, Kamati ilielezwa kuwa taarifa za kitaalam zinaonesha kwamba wakati Kampuni ya Meremeta inafunga uzalishaji katika mgodi, kiasi cha wakia 600,000 zilisalia kwenye miamba migumu.
Akifafanua zaidi, alisema kuwa STAMICO imeamua kufanya upya tathmini ya mashapo hayo ili kujiridhisha. “Hadi sasa kiasi cha mashapo yenye wakia 441,772 kimethibitika kuwemo kwenye miamba migumu kutoka katika migodi ya wazi. Ukadiriaji wa mashapo unaendelea,” alisema.
Vilevile, ilielezwa kuwa Shirika lilifanikiwa kuchoronga shimo moja katika eneo la Nyasanero ili kutathmini mkanda mpya wa dhahabu. Tathmini kamili ya kiasi cha dhahabu kilichopo kwenye mwamba itakamilika mara baada ya kupokea majibu ya maabara.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kulia) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, mambo kadhaa kuhusu Mgodi wa Dhahabu wa CATA Mining uliopo Mara, walipotembelea Mgodi huo wakiwa katika ziara ya kazi Machi 15 mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila (kushoto) wakishiriki katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, katika Mgodi wa CATA Mining mkoani Mara, Machi 15 mwaka huu.
 Wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Migodi ya Madini ya Buhemba na CATA Mining iliyopo mkoani Mara, Machi 15 mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA LEO AL-HAMIS MARCH 22,2018

KINYWAJI KIPYA CHA MOËT & CHANDON CHA TAMBULISHWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud akionesha kinywaji cha Moet & Chandon ambacho kimetambulishwa jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinywaji cha Moët & Chandon Tanzania.
 Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kinywaji cha Moet &Chandon hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinywaji cha Moët & Chandon Tanzania na kushto ni Meneja Masoko wa Kinywaji cha Moët & Chandon hapa nchini, Alexandre Kelaine.
 Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon, Pierre-Louis Araud  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kinywaji cha Moet &Chandon hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinywaji cha Moët & Chandon Tanzania na Kutoka kushoto ni  Meneja wa Chapa (Band) wa Kinywaji cha Moët & Chandon na Kulia Meneja Masoko Afrika Mashariki wa  Moët Hennessy, Alexandre Helaine.

 KINYWAJI  kipya cha Moët & Chandon kimetambulishwa leo jijini Dar es Salaam ambacho ni Kinywaji kizuri, chenye rangi ya Njano na chenye radha nzuri.

Akizungumza wakati wa kutambulisha kinywaji hicho Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud amesema kuwa ni kinywaji chenye uhai na ukarimu, kikiwa na rangi ya njano iliyong'arishwa na dhahabu na kinajitofautisha na vingine kwa ustadi na utajiri wake  wa ladha.

Amesema kuwa "Urafiki, ushirikiano na ukarimu" ni kati ya maadili ya chapa ya Moët. Moët & Chandon inashiriki katika kuunganisha watu ulimwenguni kote na kujenga urafiki wa kudumu. Tunapofurahia uzinduzi wa Moët Nectar nchini Tanzania, pia tunataka kusheherekea watanzania kama marafiki wapya wa Moët na tunaendelea kuwapa moyo wale wote wanaopenda kufurahia maisha kushukuru kwa kila wakati na kusheherekea mafanikio kila yanapotokea." 

Harufu ya Moët Nectar Impérial ina wingi wa matunda ya kitropiki kama mananasi na maembe, viungo vitamu vya mdalasini na vanila. Kikiwa mdomoni kina mchanganyiko wa ladha nzuri ya krimu na mazabibu.

Mchanganyiko wa kinywaji cha Moët Nectar Impérial unajengwa kwenye muundo wa zabibu ya aina mbali mbali ikiwemo wa aina ya Pinot Noir (asilimia 40 kwa 50), pia aina ya Meunier (30 kwa 40) na pia aina ya Chardonnay kwa asilimia (10 kwa 20). Matumizi ya asilimia 20 hadi 30 ya mvinyo ambayo imehifadhiwa kwa uangalifu yanakamilisha uundaji wa kinywaji hiki na kukiboresha zaidi. 

WACHIMBAJI WASUBIRIA HATMA YA MAOMBI YA LESENI MIAKA MINNE SASA BILA MAJIBU WAKATI SHERIA YA MADINI YA MWAKA 2010 NI NDANI YA SIKU 28

$
0
0
Pichani ni Eneo lililotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kata ya Changaaa ambalo mmiliki wa Kampuni ya Kidee mining alilowapora wachimbaji wadogo baada ya kupewa leseni kinyemela kwa umiliki wa eneo hilo ambalo wachimbaji teyari walitafiti tokea mwaka 2012 na sasa wanatakiwa kuwa chini ya mwekezaji huyo kwa kivuli cha kikundi badala ya kampuni picha zote na mahmoud ahmad Kondoa. 
Semina ikiendelea kwa Wachimbaji wadogo zaidi ya 100 wakipewa elimu ya uchimbaji sanjari na ulipaji kodi za serikali japo walipokuwa wakihoji masuala mbali mbali walikuwa wakikataliwa na maofisa madini wa ofisi ya afisa madini mkazi Dodoma hawapo pichani kama walivyokutwa na kamera yetu kwenye kata ya Changaa wilayani Kondoa.
Mbele kwenye meza ni mwenye kofia ni diwani wa kata ya Changaa Issa Bhou na kutoka kushoto ni Maafisa madini Affa Affa na Joshua Nduche pamoja na katibu tarafa ya Kolo na Mwenyekiti wa kijiji cha Bubu changaa Kenyata Fonda na aliekuwa anaongea amesimama ni Afisa misitu na maliasili wilaya ya Kondoa Kasisi wakitoa semina kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu bila kutaka kuhojiwa maswali. 

Na Mahmoud Ahmad Arusha.
Wachimbaji wadogo wameendelea kusotea eneo lao kwa mikataba migumu inayowagawa na kuwafukuza katika maeneo yao ambapo kumekuwapo na utambulisho wa leseni tofauti tofauti katika eneo moja na kuwaacha na sintofahamu na kuelekeza lawama kwenye ofisi za Kamishna msaidizi kanda ya kati Sosthenes Masola kwa kuendelea kubariki leseni kwa kummilikisha mtu mmoja huku akitambua ana maombi halali ya wachimbaji wadogo kwenye ofisi yake bila majibu hadi sasa wakati sheria ya madini ya mwaka 2010 inasema ni ndani ya siku 28 majiubu yanakuwa teyari huku Coordness zikiksoma maombi ya wachimbaji ndani ya wizara ya madini.

Leseni hizo ambazo zimekuwa zikitolewa baada ya mh. raisi kuzuiya utoaji wa leseni hadi itakapoundwa tume zinaonekana kutaka kuwakimbiza wachimbaji katika eneo hilo kwa kigezo cha umiliki wa leseni jambo ambalo wanaziomba mamlaka kulitupia macho jambo hilo kwa uwepo wa hadaa na ukwepaji wa kodi za serikali kama ilivyobainishwa katika kikao cha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Fallesy Kibassa na wachimbaji terehe 1\12\2017 kata ya Changaa.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji hao Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Juma Ramadhani Chuha amesema kuwa lengo la muongozo wa mkuu wa wilaya ya Kondoa bi Sezaria Makota kumaliza mgogoro linaonekana kugonga mwamba kwa hatua hii ya kuingia mikataba ya maduara badala ya kikundi kwa mkutano halali wa kisheria ambao ulitolewa muongozo.

Amesema badala yake amekuwa akiwaita wachimbaji kinyemela na kuwapa mikataba badala ya kukaa nao na kujadili namna nzuri ya kuainisha haki za wachimbaji na uwepo wao katika eneo lao la mgodi badala yake kumekuwepo na taratibu za kuwaondoa katika maeneo yao kwa mikataba batili ya vichochoroni badala ya kuitisha mkutano huru wa wachimbaji wote.

“kwa mujibu wa muongozo wa kamati ya ulinzi na usalama kuwataka pande zote kushirikiana na mwanasheria wa halmashauri ili kupata ufafanuzi wa kisheria jambo hilo limekiukwa na kuwa kitendawili cha kutoheshimu sheria na maamuzi ya vikao” alisisitiza Chuha

Nae Moja wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye kijiji cha BubuChangaa Mataka Iddy alisema kuwa lengo lao lilikuwa ni kufikia kumiliki eneo hilo kisheria na kulipa mapato ya serikali lakini cha kushangaza mamlaka zinatutaka tuwe chini ya mmiliki wa leseni batili ambazo ni no 005012CZ na 005013CZ ambaye wakati tunaomba eneo hilo hakuwepo wala maombi yake yalitumwa nyuma ya maombi yetu na kupimiwa eneo na kulipia cha kushangaza sisi hatujapewa majibu hadi sasa kama tulikosa au kupata .

Amesema kuwa kimsingi wataendelea kudai haki zao hata kwa kufika kwa mh.Rais kwani wamekuwepo kisheria na wanaendelea kusotea kusimamishwa kazi kwa migogoro ilioanzishwa na wachimbaji wenzao kwa kushirikiana na mporaji wa maeneo kwa leseni mpya no 006092CZ hadi 006099CZ ambazo hapo awali kwenye kikao cha mgogoro hazikutambulishwa kwani wilaya yote imekuwa ni mali yake kwasasa katika migodi na anamiliki leseni zaidi ya 20 zisizo na tija wala ajira kwa vijana wa changaa na wilaya kwa ujumla.

Amesema kuwa pamoja na mamlaka mbali mbali walizoziendea kushindwa kutambua uhalali wa maombi yao kimsingi na majibu ya Afisa madini mkazi Kondoa Silimu Tegalile kusema wazi kuwa anamiliki leseni mbili inaonekana kuwa ni kinyume na alivyoainisha mbele ya mkuuu wa wilaya bi Sezaria Makota, jambi hili inaonekana kukidhana na leseni zinazotambulishwa kwa sasa kwenye mkataba aliotupatia wachimbaji, kwani wali zozitambulisha mbele ya mkuu wa wilaya ni leseni mbili kwenye mkataba zipo saba.

UAMUZI MAOMBI YA DHAMANA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYAKAZI MSTAAFU WA TAZAMA KUJULIKANA APRILI 5 MWAKA HUU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema uamuzi wa maombi ya dhamana katika kesi  ya kuhujumu uchumi inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama),  Samwel Nyakirang'ani(63) na wenzake sita, kujulikana Aprili 5, mwaka huu.

Uamuzi huo ambao ulitakiwa kutolewa leo, umeahirishwa kwa sababu Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema bado hajamaliza kuuandaa kutokana na kuwa na majukumu ya kikazi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wakili wa utetezi, Kusalika Augostine kuwasilisha maombi mahakamani hapo akidai wateja wake wanahitaji kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro( 54) mwalimu wa shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni, mfanyabaishara, Farijia Ahmed (39) mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias b(39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus (25) mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko (40) mkazi wa Tungi Kasirati na Hunry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni nq Audai Ismail

washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta ya  dizeli, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.

Ilidaiwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka (TPA).

Inadaiwa walijiunganishia mafuta hayo kutoka katika bomba la rangi ya silva lenye upana wa inchi 24 ambalo halishiki kutu.

katika shtaka la kuharibu miundo mbinu, ilidaiwa,  kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa walitoboa na kuharibu bomba la mafuta ya dizel lenye upana wa inchi 24, ambalo lilikuwa likitumika kufirisha mafuta,  mali ya (TPA).

Aidha washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la mafuta mazito( Crude oil) lenye upana wa Inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya (TPA)

COCA COLA YAJA NA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA NA COKA'

$
0
0
 Maofisa wa kampuni ya Coca-Cola mkoani Mwanza, kutoka kushoto Meneja Mauzo Mkoa , Mnyamuhanga Gavana,Meneja Mauzo na Masoko Samuel Makenge na Meneja Mauzo Mwandamizi Deus Kadico, wakionyesha mfano wa chupa zenye vizibo vyenye zawadi ya promosheni ya ‘Mzuka wa Soka na CoKa’ iliyozunduliwa jijini humo.
Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya soda ya Cocacola tawi la Mwanza Samuel Makenge, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni. 

 Lengo ni kuwezesha wapenzi wa soka kupata burudani ya Kombe la Dunia 2018 Wakati michuano ya Kombe la Dunia 2018, ambayo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya Coca-Cola inakaribia kuanza,kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Nyanza Bottlers leo imezindua promosheni itakayotoa fursa kwa wateja wake kujishindia luninga za kisasa, zitakazowezesha kufaidi uhondo wa michuano ya kombe la dunia wakiwa majumbani kwao. 

 Promosheni hii ambayo inajulikana kama ‘ Mzuka wa Soka na CoKa’ itawahusu watumiaji wa soda za Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparleta na Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kanda ya ziwa . Mbali na zawadi za televisheni,watumiaji wa vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola, kupitia promoheni hii wataweza kujishindia zawadi nyinginezo mbalimbali ikiwemo ,fedha taslimu kati ya shilingi 5,000 mpaka shilingi 100,000/-kofia, t shirt,soda za bure na zawadi kubwa ya bodaboda. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI RAIS WA SIMBA EVANS AVEVA NA MAKAMU WAKE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 5

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

UPELELEZI katika kesi ya utakatishaji fedha, dola za Marekani 300,000 inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange, maarufu kama Kaburu, umekamilika na itaanza kusikilizwa Aprili 5 mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.  
 Katuga aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa Aveva hayupo mahakamani hapo kwa kuwa ni mgonjwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Baada ya taarifa hiyo, Wakili anayewatetea washtakiwa hao,Steven Mwakibolwa aliiambia Mahakama kuwa wapo tayari kuendelea na kwamba hali ya Aveva inaimarika ila siyo nzuri.

WCF YAWAELIMISHA MAAFISA WAAJIRI MISINGI KULINDA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina juu ya masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahala pa kazi na Fidia kwa wafanyakazi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam Machi 22, 2018. Wengine pichani  I Mkurugenmzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (katikati), na Meneja wa Tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Risk Assesment Manager), Bi. Nanjela Msangi.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NIWAJIBU wa mwajiri kutoa taarifa kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ya kuumia kwa mfanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kifo.

Hayo yamesemwa leo Machi 22, 2018, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, wakati akifungua semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Wafanyakazi, (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Pia ni wajibu wa mwajiri kumpatia vifaa vya kujilinda (protective gears), mfanyakazi wake,  kulingana na kazi anayofanya ili kumlinda na madhara yatokanayo na kazi anayofanya.
“Lengo la Mfuko sio tu kusajili waajiri na kupokea michango lakini pia ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maenmeo ya kazi na ndio msingi mkuu wa seemina yetu ya leo, katika kutekeleza jukumu letu hili ni kujenga uelewa wa kutosha kwa mwajiri ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuzuia ajali sehemu za kazi.” Alisema na kuongeza.
Nia ya Mfuko ni kuona tunakinda nguvu kazi ambapo tunahakikisha kwamba wafanyakazi hawa wawapo kazini hawaugui au kuumia au kufariki kutokana na kazi, alissisitiza Bw. Peter.
Alisema washiriki watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wawapo kazini. “Mtaelimishwa kuhusu masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitria mada mbalimbali zitakaziowasilishwa na wataalamu, kutekeleza vyema jukumu la kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda usalama mahala pa kazi, masuala ya fidia kwa wafanyakazi, wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
Alisema, uwepo wa Mfuko umeleta faraja kubwa kwa waajiri na wafanyakazi ambapo leo hii, endapo Mfanyakazi atapata madhara kutokana na kazi, anao uhakika kuwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, utatoa fidia stahili kulingana na mikataba ya kazi na mwajiri husika.
“Yote haya yanawapa wafanyakazi utulivu wawapo kazini kwani wanajua kuwa lolote likitokea ipo taasisi ambayo itasimamia na kunifidia nah ii inaondoa migogoro sana sehemu za kazi.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Mwajiri anao wajibu wa kumuwekea mazingira bora, salama na yana afya ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. “Sio tu kupewa mazingira mazuri lakini pia apewe vifaa kinga kitaalamu vinaitwa personal protective equipmentskwa kufanya hivyo utakuwa unalinda usalama wake na afya yake.” Alisema Dkt. Omar.
“Mfanyakazi anayo haki ya kumdai mwajiri wake kumpatia vifaa vya kujilinda na mwajiri haruhusiwi kumfukuza kazi au kumwadhibu mfanyakazi anayedai mazingira bora toka kwa mwajiri wake ili aweze kuwa amekingwa.” Alifafanua.
Pia alisema mfanyakazi naye anao wajibu kuvitumia vifaa vya kujikinga katika mazingira yake ya kazi kwa usahihi na wakati wote awapo kazini.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo, BwAlly Kinga Shamte, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Badri East Africa Enterprises, mesema tayari kampuni yake imeanza kufaidika na kujiunga na Mfuko huo ambapo mmoja wa wafanyakazi wake, aliyepata shoti ya umeme ameweza kushughulikiwa na Mfuko na tayari anahudumiwa.
“Hii imekuwa ni kama Bima kwa wafanyakazi wetu, sisi hatushughuliki tena na madhara anayopata mfanyakazi, tulichofanya ni kujaza fomu zao za taarifa ya ajali hiyo na mara moja walianza kumshuhhulikia.” Alisema.

UNZIP TANZANIA: Heavenly Magoroto

MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote katika jiji hilp kuajiri watumishi ambao watakuwa wanazika miili ya watu ambao watabainika kutokuwa na ndugu wa kuwazika.

Ametoa kauli hiyo leo kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaambia madiwani hao kuna taarifa amezipata za halmashauri kutokuajiri watumishi kwa akili ya kuzika watu wasiokuwa na ndugu.

Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini humo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu Dar."Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzika na Jijijiji,na tulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda," amesema.

Amefafanua kuwa watu hao wasiokuwa na ndugu wanapokufa wapo ambao wanakaa hospitalini zaidi ya siku 20,hivyo wapo ambao wanazika kwenye halmashauri mbalimbali.Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu katika kupumzisha mwili wa marehemu,halmashauro jukumu lao ni kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.

Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ua kuzika miili ya watu ambao wamefariko na hawana ndugu.Hivyo amezikumbusha halmashauri zote kuajiri watumishi hao ili kufanikisha kupumzisha miili hiyo.

"Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka," amesema Meya Mwita.

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU MAJALIWA ASAINI MKATABA WA UANZISHWAJI WA SOKO LA PAMOJA KATIKA UMOJA WA AFRIKA

MMILIKI MTANDAO WA FACEBOOK AWAOMBA RADHI WATEJ A WAKE

$
0
0

ZUCKERBERG AFUNGUKA SAKATA  LA FACEBOOK.

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MWANZILISHI  na mmiliki wa mtandao wa Facebook  Mark Zuckerberg ameibuka na kuomba msamaha kwa wateja wake baada ya sakata la kudukuliwa kwa data za watumiaji  zaidi ya milioni 50 wa mtandao huo na kampuni ya taarifa na takwimu ya Cambridge Analytica. 

Kashfa hiyo imeipa hasara ya zaidi ya bilioni 45 kwa siku mbili kutokana na hofu na upotoshaji uliotokea kwa watumiaji wake. Zuckerberg amehaidi uaminifu na umakini zaidi wa kulinda data za watumiaji wake na hazitoingiliwa tena.

Sakata hilo linakuja baada ya utumikaji wa data wa watumiaji wa mtandao wa Facebook kudukuliwa na kutumika vibaya katika uchaguzi wa nchi za Kenya na Marekani (2016) ambapo Donald Trump aliibuka kidedea.

Mamlaka ya Cambridge analytica imemsimamisha kazi mkuu wake Cambridge Nix Alexander kwa kuhusika na sakata hili pia mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Cambridge  anayehusishwa na kampuni hii ya Uingereza ya utafiti data bado anaandamwa na kashfa ha kutengeneza Application iliyotumiwa kudukulia data na udukuzi huu ulimpa ushindi Donald Trump.

Imeelezwa kwamba Facebook ndio mtandao wenye watumiaji wengi zaidi duniani, ulianzishwa February 4 mwaka 2004 na Mark Zuckerberg na hadi kufikia mwaka 2010 ametangazwa kuwa miongoni mwa matajiri 100 duniani na mtu mwenye ushawishi zaidi.

MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI DAR WAHOJI KUHUSU FEDHA ZINAZOTOLEWA NA KARIAKOO

$
0
0

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BARAZA la Madiwani wa Jiji la  Dar es Salaam limeomba kufahamu kiasi cha fedha kinachopatikana katika Soko la Kariakoo maana wamechoshwa na kauli ya kwamba soko hilo linaendeshwa kwa hasara.

Baadhi ya madiwani hao wamekiambia kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo leo jijini Dar es Salaam wamesema Jiji linamiliki soko kwa asilimia 51.Diwani wa Kata ya Mbezi Humphrey Sambo amekiomba kikao hicho kupata taarifa za mapato ya soko hilo kwani kwa mtazamo wa kawaida wamedai fedha inayopatikana ni nyingi lakini wao wanaambiwa linaendeshwa kwa hasara.

"Tufuatilie ili kujua nini ambacho kinaendelea katika Soko la Kariakoo kwani nimechoka kusikia kila siku wanapata hasara lakini watu wanakwenda kazini," amesema.Amefafanua kwa kuwa Jiji linahisa ya asilimia 51 ni vema ikajulikana kinachopatikana na mgao wa Jiji ni kiasi gani.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Tabata Patrick Asenga amesema soko la Kariakoo si kweli linapata hasara kwani hata vizimba vya biashara vilivyopo kodi yake ni Sh.300,000 hadi Sh.400,000.Amesema ni vema Jiji likatoa kauli ya kuwaita wanaosimamia soko hilo ili waeleze kuhusu soko hilo na kwamba hakubaliani na kauli ya soko kuendeshwa kwa hasara.

Kutokana na maelezo hayo ya madiwani,Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amemuomba Mkurugenzi wa Jiji hilo kuyafanyia kazi na kwenye kikao kijacho majibu yatolewe."Mkurugenzi wa Jiji naomba ukae na menejimenti yao  kushughulikia suala hili kwanza na  na menejimenti yake na baada ya hapo taarifa itolewe," amesema.
Mstahki Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiongoza kikao cha robo ya pili ya baraza la madiwani leo, kushoto ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana.

WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

WANAFUNZI wa kike 110  waliotekwa February 19 katika shule ya bweni Dapchi nchini Nigeria  wamerejeshwa nyumbani kutoka kwenye mikono ya waasi.

Waziri wa habari nchini humo Alhaj Lai Mohammed ameeleza kuwa wanafunzi 101 kati ya 110 wamerejeshwa salama na hiyo ni baada ya jeshi kuweka juhudi ili kunusuru maisha ya watoto hao.

Licha ya Wizara kutothibitisha inasemekana wasichana watano wamefariki dunia na hiyo ni kutokana na maeleza ya Aisha Kachalla Bukar (14) mmoja wa manusura hao aliyoyatoa kwa baba yake.

 Pia inasadikika kuwa mmoja wa wanafunzi hao(mkristo) bado anaendelea kushikiliwa na waasi hao baada ya kukataa kuslimu.Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari ameeleza kuwa janga la utekaji ni la kitaifa na ametoa pole kwa waathirika wote.

Ifahamike kuwa mwaka 2014 wanafunzi 300 walitekwa huko Chibok na hadi sasa wanafunzi 100 bado hawajapatikana.

KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI AVEVA,KABURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 5

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

UPELELEZI katika kesi ya utakatishaji fedha, dola za Marekani 300,000 inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange, maarufu kama Kaburu, umekamilika na itaanza kusikilizwa Aprili 5 mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.  

 Katuga aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa Aveva hayupo mahakamani hapo kwa kuwa ni mgonjwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Baada ya taarifa hiyo, Wakili anayewatetea washtakiwa hao,Steven Mwakibolwa aliiambia Mahakama kuwa wapo tayari kuendelea na kwamba hali ya Aveva inaimarika ila siyo nzuri sana.

Hakimu Simba, amesema kama hali ya Aveva itakuwa imetengemaa kesi hiyo wataisikiliza mfululizo na kuongeza, kesi ilifunguliwa Juni 26, mwaka jana  na wajitahidi isikilizwe na kumalizika ndani ya miezi 12.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matano ya kutakatisha fedha na kughushi ambayo wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni 29,mwaka 2016 Dar es Salaam Aveva na Nyange kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata Dola za Marekani 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>