Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

AWESO-SIPO TAYARI KUONA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINATUMIKA VIBAYA

$
0
0

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatakuwa tayari kuona fedha za miradi ya maendeleo zinatumika vibaya huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sabasi Chambasi kuwa makini nayo.

Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa baadhi ya miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali kujengwa chini ya kiwango jambo ambalo linasababishwa na kutokuwa makini kwa viongozi wanaoisimamia. 

Aweso aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo limegharimu kiasi cha milioni 600 linalosimamiwa mkandarasi Kisyeri Chambiri kutoka kampuni ya Wesers Limited.

Alisema mradi huo una umuhimu mkubwa sana kwa wilaya hiyo hivyo lazima watumishi wakiwemo wale ambao wanasimamia suala hilo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wakitekeleza suala hilo.

“Mkandarasi huu mradi ni muhimu sana kwa Halmashauri yetu hivyo sitopenda kuona unajengwa chini ya kiwango lakini pia hakikisheni unakamilika kwa wakati kwa lengo la kufanya kazi “Alisema.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimueleza jambo Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah akizungumza katika ziara hiyo kulia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi 
Sehemu ya jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo ujenzi wake unaendelea
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea


MWENYEKITI APPT-MAENDELEO PETER KUGA MZIRAY AFARIKI DUNIA DAR, KUZIKWA KIJIJINI KWAKE SAME

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Chama cha APPT-Maendeleo Peter Kuga Mziray amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rabincia iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo mkongwe amefariki jana saa nne asubuhi wakati akiendelewa kupatiwa matibabu ambako alilazwa hapo kwa muda wa wiki mbili kabla ya umauti kumfika.

Akizungumza na Michuzi Blog kuhusu kifo cha Mziray,Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda amesema baraza hilo limeshutushwa na kifo cha mwanasiasa huyo aliyekuwa mstari wa mbele kupogania maslahi ya watanzania na Taifa.

Shibuda amesema kwa mujibu wa taarifa za kaka wa marehemu Mziray ni kwamba msiba upo maeneo ya Faya nyuma ya kituo cha Mafuta ambako kuna nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)zilizopo eneo hilo.

Amesema ameelezwa taratibu za kuupumzisha mwili wa marehemu Mziray zitafahamika baada ya mkewe ambaye yupo nchini Japan kuwasili nchini."Taarifa ambazo ninazo Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa kutoka kwa ndugu wa marehemu Mziray zinasema mkewe anaweza kuingia nchini kati ya siku mbili hizi.

" Akifika ndio watajua wanazika lini na huenda mwili ukaaga Jumamosi.Hata hivyo tutajua zaidi baada mkewe kuwasili nchini."Tumejulishwa mazishi ya marehemu Mziray yatafanyika katika kijiji cha Kihurio wilayani Same mkoani Kilimanjaro," amesema.

Akimzungumzia Mziray wakati wa uhai wake,Shibuda amesema baraza hilo na siasa za Tanzania kwa ujumla zimempoteza kiongozi muhimu ambaye mchango ulikuwa bado unahitajika."Ni pigo kubwa kuondokewa na mwanasiasa ambaye alikuwa anaipenda nchi na siku zote alisisimamia masuala yenye tija kwa nchi yetu.

" Alikuwa na masikio sikivu katika kusikiliza ushauri na kubwa zaidi siasa zilijikita katika kuunganisha Taifa.Ni mwanasiasa ambaye hakuwa anaamua mambo kishabiki bali aliamua kwa kuangalia maslahi ya nchi kwanza,"amesema Shibuda.

Amefafanua nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini ambayo anaitumikia hivi sasa aliichukua kutoka kwa Mziray baada ya kumalizima muda wake wa kuliongoza baraza hilo.

Hivyo amesema akiwa Mwenyekiti wa Baraza hilo kuna mambo mengi mazuri aliyayofanya kwa maslahi ya vyama vya siasa,"amesema.

Shibuda amesema kwa niaba ya Baraza la vyama vya siasa anatoa pole kwa familia,ndugu,jamaa,marafiki,wanasiasa wote na watanzania kwa ujumla na Mungu ailaze mahali pema popeni roho ya marehemu Mziray.

Je! Unajua unaweza kupata bei bora za soko kwa shamba lako la kuzalisha kwa kutumia mtandao wa simu?

$
0
0
Je! Unajua unaweza kupata bei bora za soko kwa shamba lako la kuzalisha kwa kutumia mtandao wa simu? Tazama na ujifunze jinsi wengine wanavyofanya.




KAMATI YA LAAC NA PAC ZAPEWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO

$
0
0


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), baada ya wajumbe hao kupatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ukaguzi. Semina hiyo imefanyika katika Ofisi za Ukaguzi Mkoa wa Iringa.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakifuatilia mada katika semina iliyohusu masuala mbalimbali yanayohusu ukaguzi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mddhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza katika Mkutano wa Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati Kamati hiyo ilipokutana na Watendaji wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoani Singida.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI

WANAFUNZI MVOMERO WATAKIWA KUJIKITA ZAIDI KATIKA MASOMO YA SAYANSI ILI WAWE WATAFITI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Mvomero-Morogoro.

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi ya Mvomero mkoani Morogoro wametakiwa kujikita zaidi katika masomo ya Sayansi ili waweze kulisaidia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti.

Mwito huo umetolewa wilayani humo leo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi ya Wema E2109 inayostahimili ukame iliyotolewa na COSTECH kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

"Ninyi wanafunzi nawaomba someni sana masomo ya sayansi ili hapo baadae muweze kuwa watafiti wa masuala mbalimbali jambo litakalosaidia taifa" alisema Hussein.Alisema tafiti zozote zinafanywa na wataalamu waliobobea katika masomo sayansi hivyo aliwataka wanafunzi hao kujifunza kwa bidii masomo hayo ya sayansi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo, Mohamed Utalli aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kupeleka mradi huo katika wilaya yake ambapo amewataka wananchi kuzichangamkia mbegu hizo.
Mtifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu ambao ndio waliofanya utafiti wa mbegu hiyo, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
Uzinduzi wa shamba darasa katika shule ya msingi Mvomero.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli akizindua shamba darasa kwa kupanda mbegu hiyo ya Wema 2109
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utalli, akizungumza na wakulima wanaounda kikundi cha Tupendane kilichopo Kijiji cha Didamba.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Kijiji cha Didamba, Mwanahamisi Omari (kushoto), akikabidhiwa mbegu.

JAJI KIONGOZI AWAFUNDA MAHAKIMU WAPYA

$
0
0

Na Mary Gwera, Mahakama

MAHAKIMU wapya wanaotarajia kuanza kazi rasmi ndani ya Mhimili wa Mahakama wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Mhimili huo.

Akizungumza na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni katika Ukumbi wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam mapema Machi 20, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali amewaasa Waajiriwa hao kufanya kazi kwa maadili na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

“Katika ufanyaji kazi wenu wa Uhakimu, mnatakiwa kuzingatia mambo makuu manne ya msingi ni; Ujuzi wa taratibu na mazoea ya Kimahakama, Uelewa kuhusu Sheria za Msingi ‘Substantive law’ na Sheria za Mwenendo ‘Procedural Law’ kuangalia mazingira ya utoaji haki na kadhalika,” alieleza Mhe. Wambali.

Aidha Jaji Kiongozi pia aliwataka Mahakimu hao pia kufanya kazi kwa kuwaheshimu Wadau wote wanaojumuika nao katika mchakato mzima wa utoaji wa haki, ikiwa ni pamoja na Makarani, Wazee na Baraza na wengineo.“Heshimuni kila mtu mnayeingia naye Mahakamani, kila mtu ana mchango katika upatikanaji wa haki, na moja ya sifa ya Hakimu ni upole lakini upole sio udhaifu,” alisisitiza Mhe. Jaji Wambali.Mbali na kuwaasa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, Mhe. Jaji Kiongozi aliwaasa pia Mahakimu hao kutojihusisha na masuala ya siasa katika kazi zao.

“Ibara ya 113A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema, Hakuna Jaji au Hakimu anayeruhusiwa kuwa Mwanachama wa Chama chochote cha Siasa” alisisitiza Mhe. Jaji Kiongozi.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward Nkembo amesema kuwa jumla ya Mahakimu wapya 78 kati ya 100 wameripoti kazini.

“Jumla ya Mahakama wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo wameripoti, hata hivyo baadhi wametoa taarifa ya kushindwa kuripoti kutokana na dharura mbalimbali,” alisema Mkurugenzi huyo.Bw. Nkembo ameeleza kuwa baadhi ya Mahakimu na Watumishi wa Kada watakaoshindwa kuripoti ndani ya siku 14 tangu Machi 20, nafasi zao zitatafutiwa watu wengine watakaoomba na kukidhi vigezo.

Mahakimu hao na Watumishi wengine wa Kada mbalimbali walioajiriwa na Mahakama hivi karibuni watasambazwa katika Mahakama mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuongeza nguvu kazi katika kuendelea kuboresha huduma ya utoaji haki kwa wananchi.
Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (wa pili kulia) akiongea na jumla ya Mahakimu wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo (hawapo pichani) walioripoti katika Ofisi za Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, wa kwanza kushoto ni Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kulia ni Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha.
Baadhi ya Mahakimu wapya wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi
Wakiendelea kumsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi
Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (Katikati), Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania (aliyeketi kushoto) na Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni.(Picha na Mary Gwera, Mahakama

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA WATAIFA UBORESHAJI HUDUMA YA UPASUAJI

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI ya kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mpango wa taifa wa kuboresha huduma upasuaji ambayo kila mtu anaweza kumudu kufikia 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduaji wa mpango huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa mpango huo umekuja wakati mwafaka kutokana na sera ya afya miaka mitano kuisha hivyo mpango huo kuingia katika sera ya miaka mitano.

Dk.Mpoki amesema kuwa mpango huo uko katika muda mwafaka kutokana na hatua mbalimbali za uboreshaji afya kwa wananchi katika upatikaji wa huduma za upasuaji hali ambayo itaokoa maisha pamoja na kuongeza uzalishaji.

“Upasuaji salama ni ishara ya kila Mtanzania anaweza kupata huduma za afya na kuongeza uzalishaji ,kuboresha huduma za upasuaji bora pamoja na dawa za usingizi ni muendelezo wa kuboresha afya ya uzazi kwa nchi nzima” amesema Dk.Mpoki.

Amesema Tanzania ni nchi ya tatu duniani ambayo imejizatiti katika utoaji wa huduma za upasuaji endelevu na kuingiza katika mpango wa taifa wa upasuaji pamoja watalaam wa dawa za usingizi. Amesema kuwa serikali itasomesha madakitari pamoja na wataalam wa dawa usingizi ili kuweza katoa huduma bora za upasuaji kwa kiwango kikubwa kulingana na wahitaji wa upasuaji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa taifa wa huduma ya upasuaji, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese akizungumza kuhusiana na Tanzania kupokea mpango wa upasuaji na kuingiza katika mpango wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi akizungumza hali ya upasuaji nchini, jijini Dar es Salaam.
Sehemu wataalam wa afya wa nchi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa afya unaofanyika nchini.


WAZIRI KABUDI AWATAKA WASAJILI VYETI VYA KUZALIWA MIKOA YA SIMIYU, MARA KUZINGATIA UMAKINI NA UZALENDO

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wasajili wa vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwenye mikoa ya Simiyu na Mara, kufanya kazi hiyo kwa umakini na uzalendo mkubwa katika kuhakikisha wanawasajili watoto wenye sifa.

Waziri Kabudi ametoa rai hiyo Machi 20 wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, katika mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

“Mikoa ya Mara na Simiyu ina muingiliano mkubwa sana na wananchi wa nchi jirani hivyo wasajili wawe makini na watangulize uzalendo wakati wa kutekeleza mpango huu, tusisajili mtoto ambaye hahusiki na pale ambapo tuna mashaka kuwa mtoto huyo anaweza kuwa wa nchi za jirani, tutoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili hatua za kiusalama zichukuliwe” alisema Profesa Kabudi.

Amesema kuwa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano unafanyika bila malipo hivyo wasajili wasitumie kwa namna yoyote mpango huo kama fursa ya kujipatia fedha kwa udanganyifu.Aidha, Waziri Kabudi ameahidi kutoa tuzo maalum kwa mkoa (kati ya Simiyu na Mara) utakaofikia asilimia 80 ya lengo la usajili kwa kipindi cha miezi miwili tangu usajili ulipoanza na wakati huo huo akawataka Viongozi wa Taasisi zote Umma kuvitambua vyeti vitakavyotolewa chini ya mpango huo kwa kuwa ni vyeti halali

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA) Profe. Hamis Dihenga amesema kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, RITA inakusudia kusajili jumla ya watoto 735, 545 katika mikoa ya Simiyu na Mara kwenye vituo 463 (Mara) na Vituo 324 (Simiyu).

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Adam Malima amesema hadi sasa Mkoa huo umesajili jumla ya watoto 78, 625 na watahakikisha watoto wote wanaopaswa kusajiliwa wanasajiliwa ndani ya miezi miwili na baadaye kuendelea na usajili kwa watoto watakaozaliwa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(wa tatu kushoto) akizindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) akionesha nakala ya cheti cha kuzaliwa kinachotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri huo na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimkabidhi mkazi wa Manispaa ya Musoma cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri wa chini ya miaka mitano, mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA JIJINI DAR

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na balozi wa Italia nchini Tanzania Roberto Mengoni masuala mbalimbali ya uushirikiano baina ya Itali na Wizara ya mambo ya Ndani.Maongezi hayo yamefanyika leo katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam.


Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi ya NHC na kuivunja

$
0
0
Alieyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)



DRAW YA PLAY-OFF YA CAF CONFEDERATION CUP

$
0
0
-Draw ya mechi za Play-Off za Caf Confederation Cup kufanyika leo makao makuu ya CAF, Cairo Misri majira ya Saa 8:30 Mchana

-Draw hiyo inahusisha timu 32 timu 16 ambazo zilitolewa kwenye klabu bingwa Afrika (Caf Champions Leagu) na timu 16 ambazo zilifuzu hatua ya 16 bora kutoka kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup)

-Kutakuwa na Pot 4, ya Kwanza ni Pot A itakuwa na timu 4 ambazo zipo juu kwenye Rank ya klabu  kwa timu zilizotolewa kwenye Caf Champions League timu hizo ni Al hilal Omdurman (Sudan), St George (Ethiopia), As Vita Club (DR Congo) na Zanaco (Zambia).

-Pot ya Pili ni Pot B ambayo itakuwa na timu 4 ambazo zina Rank kubwa kwa vilabu kutoka kwenye timu 16 ambazo zilifuzu 16 bora ya Caf Confederation Cup timu hizo ni USM  Alger (Algeria), Super Sport United (Afrika kusini), Hilal Obayed (Sudan) na Enyimba (Nigeria).

-Pot ya Tatu ni Pot C ambayo itakuwa na vilabu 12 ambavyo vimebaki zilizotolewa kwenye Caf Champions League Timu hizo ni UD Songo (Msumbiji), Yanga Sc (Tanzania), CF Mounana (Gabon), Bidvest Wits (Afrika Kusini), Williamsville AC (Ivory Coast), Génération Foot (Senegal), Mountain On Fire (Nigeria), Plateau United (Nigeria), Gor Mahia (Kenya), Asec Mimosas (Ivory Coast), Rayon Sports (Rwanda) na Aduana Stars (Ghana).

-Na Pot ya 4 itakuwa Pot D ambayo itakuwa timu 12 ambazo zimebaki baada ya kutoa 4 (16-4=12) ambazo zilifuzu kutoka Caf Confederation Cup timu hizo ni La Mancha (Congo Brazzavile), Belouizdad  (Algeria), Djoliba (Mali), RSB Berkane (Morroco), Raja Casablanca (Morocco), Al Masry (Misri), Fosa Juniors (Madagascar), CARA Brazzavile (Congo Brazzaville), Costa do Sol (Msumbiji), Akwa United (Nigeria), Deportivo Niefang (Equatorial Guinea) na Welayta Dicha (Ethiopia)

-Wataanza draw na Pot A  vs Pot C kwa timu 4 kutoka Pot A na Timu 4 kutoka Pot C. wanaenda Pot B vs Pot D kwa timu 4 kutoka Pot B na Timu 4 kutoka Pot D baada ya hapo zitakuwa zimebaki timu 8 kutoka Pot C na Timu 8 kutoka Pot D wanachezesha tena Pot C vs Pot D kwa timu 8 kutoka Pot C na Timu 8 kutoka Pot D hapa maana yake ni kwamba timu ambazo zipo Pot A na Pot B haziwezi kukutana  kutokana na kuwa na ranking kubwa Afrika kwa miaka 5 iliyopita.

Kamati ya kitaifa ya UN na Serikali yakutana kupanga kazi za mradi wa Koica

$
0
0
KAMATI ya kitaifa inayoendesha mradi wa pamoja kati ya mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa (UNESCO, UN Women na UNFPA) na serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wizara nyingine ambazo zinahusika na maswala ya Elimu hususani TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Watu Wazima na Watoto na Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na mfadhili wa mradi KOICA imekutana kwa mara yake ya kwanza kujadili mwelekeo wa mradi unawo husu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu.

Mkutano huo uliokuwa chini ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo uliangalia na kubadilishana mawazo ya hatua zilizofikiwa katika mradi huo ulioanza mwaka 2016 na kutekelezwa katika wilaya nne nchini Tanzania (Kasulu, Ngorongoro, Sengerema na Mkoani, Pemba) kwenye kata 22 na kupitia mpango wa mwaka 2018.

Akizungumza kabla ya kusimamia mazungumzo, Dk Akwilapo aliwashukuru wafadhili na pia wadau wengine waliojipanga kufanikisha mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wanawake nchini Tanzania na uchumi kwa ujumla.

“Mradi huu ni muhimu sana kwetu, kwa kuwa unachangia juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) na wizara nyingine zinazofanyakazi kwa pamoja bila kuchoka kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu zikiwemo Wizara za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu na Wizara ya Katiba na Sheria MoCLA” alisema.
 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkazi wa KOICA nchini, Joonsung Park ambao ndio wafadhili wa mradi huo akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa akizungumza kwa niaba ya Anne Theresa  Ndog-Jatta wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou akitoa salamu za UN WOMEN katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa mwaka 2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kubaisa (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo (katikati) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou (kushoto).
 Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Jennifer Kotta akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Afisa Programu anayeshughulikia masuala ya Afya ya Uzazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Fatina Kiluvia akishiriki katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA ambao umefanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI

$
0
0
MAAFISA Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake watangaze mafanikio hayo kwa umma.

Hayo yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Thadeus alisema Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na hoja mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi hiyo.

“Maafisa Habari, msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti zenu ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.

Aidha, alisema ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza taarifa mpya kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Mwezeshaji na Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah akiwasilisha mada kuhusu mtindo wa uandishi wa habari katika tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Afisa Tehama kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Alfred Chali akichangia hoja wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

BEKI WA AZAM FC KUELEKEA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BEKI wa kati wa Azam FC, Daniel Amoah, anatarajia kwenda jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya goti Jumatatu ijayo.

Amoah ameshindwa kupona majeraha hayo tokea ayapate Desemba 19, mwaka jana, wakati Azam FC ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania na kuichapa mabao 3-1.

Februari 7 alirejea tena uwanjani na kucheza mechi dhidi ya Simba, Azam FC ikipoteza kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo alijikuta akijitonesha tena hali iliyomfanya kukaa nje ya dimba hadi sasa.

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, amesema kuwa beki huyo ataenda kutibiwa katika Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo nchini humo na akiangaliwa kwa undani tatizo lake kwa muda wa siku nne.

“Daniel Amoah analalamika au ana tatizo la maumivu makali katikati ya goti kwa hiyo timu ya Azam inampeleka Afrika Kusini kwa matibabu na uchunguzi zaidi na atakwenda Cape Town Jumatatu ijayo katika Hospitali ya Vincent Pallotti kuonana na Daktari bingwa wa mifupa Dr. Nickolas na atakaa huko kwa muda wa siku nne na itategemeana kama tatizo litakuwa ni kubwa basi ataongezewa muda wa kukaa huko,” alisema.

Beki huyo wa zamani wa Medeama ya Ghana aliyesajiliwa na Azam FC msimu uliopita, anakuwa mchezaji wa nne wa timu hiyo msimu huu kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, awali mwaka jana walipelekwa Josepha Kimwaga, Shaaban Idd kufanyiwa upasuaji kabla ya wiki nne zilizopita nahodha Himid Mao ‘Ninja’ naye kupelekwa kwa uchunguzi wa goti lake na sasa akiwa fiti kabisa.

PUMA ENERGY YAENDELEZA UFADHILI WAKE MPANGO WA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI

$
0
0
 Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa miundombinu ya usalama barabarani katika shule za Msingi Mikumi na Mzimuni ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa uboreshaji wa usalama barababarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam ambao unaratibiwa na shirika la Amend kwa ufadhili wa Mfuko wakampuni ya Puma Energy na Mfuko wa FIA. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti,  walimu na maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani.
 Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikabidhi msaada wa jaketi la usalama barabarani kwa mwanafunzi Nuru ambae ni Muhanga wa ajali za barabarani. Nuru alilazimika kukaa hospitali kwa kipindi cha miaka miwili akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari maeneo jirani na shule hiyo.
 Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akishirikiana na wanafunzi wenye ulemavu kutoka shule ya Gilman Rutihimaba kuimba nyimbo zenye mafunzo ya usalama barabarani.
 Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti,  walimu  na wanafunzi  wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.

WAZIRI MWAKYEMBE ASIKITISHWA NA KAULI ZILIZOTOLEWA NA MSANII DIAMOND

MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama
MAHAKIMU wapya wanaotarajia kuanza kazi rasmi ndani ya Mhimili wa Mahakama wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Mhimili huo.
Akizungumza na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni katika Ukumbi wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam mapema Machi 20, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali amewaasa Waajiriwa hao kufanya kazi kwa maadili na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
“Katika ufanyaji kazi wenu wa Uhakimu, mnatakiwa kuzingatia mambo makuu manne ya msingi ni; Ujuzi wa taratibu na mazoea ya Kimahakama, Uelewa kuhusu Sheria za Msingi ‘Substantive law’ na Sheria za Mwenendo ‘Procedural Law’ kuangalia mazingira ya utoaji haki na kadhalika,” alieleza Mhe. Wambali.
Aidha Jaji Kiongozi pia aliwataka Mahakimu hao pia kufanya kazi kwa kuwaheshimu Wadau wote wanaojumuika nao katika mchakato mzima wa utoaji wa haki, ikiwa ni pamoja na Makarani, Wazee na Baraza na wengineo.
“Heshimuni kila mtu mnayeingia naye Mahakamani, kila mtu ana mchango katika upatikanaji wa haki, na moja ya sifa ya Hakimu ni upole lakini upole sio udhaifu,” alisisitiza Mhe. Jaji Wambali.
Mbali na kuwaasa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, Mhe. Jaji Kiongozi aliwaasa pia Mahakimu hao kutojihusisha na masuala ya siasa katika kazi zao.
 Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (wa pili kulia) akiongea na Mahakimu wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo (hawapo pichani) walioripoti katika Ofisi za Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, wa kwanza kushoto ni Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kulia ni Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha.
 
 Baadhi ya Mahakimu wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo (hawapo pichani) walioripoti katika Ofisi za Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi katika mkutano huo.
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (Katikati), Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania (aliyeketi kushoto) na Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

VIJIJI VITATU VYAWASHIWA UMEME

$
0
0
Na Veronica Simba 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepewa heshima ya kuwasha umeme katika vijiji vitatu ambavyo huduma ya kupeleka umeme imekamilika.
Zoezi hilo lilifanyika kwa nyakati tofauti, Machi 15 hadi 18 Mwaka huu, wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta za nishati na madini katika Mikoa kadhaa nchini.
Vijiji vilivyowashiwa umeme ni Nyabange kilichopo Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Kijiji cha Idala wilayani Nzega pamoja na Kijiji cha Kisaki kilichopo Mkoa wa Singida.
Akitoa ufafanuzi kwa Kamati husika, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisema kwamba, Vijiji hivyo vimepata huduma ya umeme kupitia mpango wa upelekaji umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mradi mkubwa wa umeme wa Backbone.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustun Kitandula (katikati) akiwasha umeme katika Kijiji cha Nyabange wilayani Butiama, Machi 15 mwaka huu, wakati wa ziara ya Kamati hiyo mkoani Mara kukagua miradi ya umeme. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) na Kamishna wa Nishati Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) wakitoka katika nyumba ya mkazi wa kijiji cha Idala wilayani Nzega (inayoonekana pichani), ambayo iliwashiwa umeme wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kijijini hapo, Machi 16 mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Chumboni Zanzibar ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ussi Pondeza akiwasha umeme katika Kijiji cha Kisaki Mkoa wa Singida, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kijijini hapo Machi 18 mwaka huu. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
Kazi ya kufunga umeme ikiendelea kwa hatua za mwisho katika Kijiji cha Kisaki mkoani Singida, kama taswira hii ilivyochukuliwa wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika eneo hilo, Machi 18 mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

58 WAKAMATWA OPERESHENI YA DAWA ZA KULEVYA

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images