Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU ATAKA SULUHISHO LA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa za Afrika kutoa mapendekezo ya namna ya kutokomeza magonjwa yasiyo ambukiza kwa wakuu wa nchi hizo ili yafanyiwe kazi.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Machi 19, 2018) wakati akifungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC)

Alisema magonjwa yasiyo ambukiza ni miongoni mwa magonjwa ambayo yameendelea kuwatesa wananchi kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi za Bara la Afrika, hivyo vema mawaziri hao wakatoa mapendekezo ya namna ya kuyatokomeza.Waziri Mkuu alisema magonjwa hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kuhamasisha wananchi kuboresha lishe na kusisitiza ulaji wa vyakula bora, kufanya mazoezi na kubadili mitindo ya maisha.

“Magonjwa yasiyoambukiza yanaongoza kwa kusababisha vifo katika baadhi ya nchi wanachama wa ECSA. Magonjwa haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfumo wetu wa lishe na maisha, hivyo ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi.”

Waziri Mkuu alisema magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa mengine ya milipuko kama ebola, homa ya bonde la ufa, dengue, homa ya manjano yamekuwa kikwazo cha maendeleo kwa katika baadhi ya nchi.

Pia, Waziri Mkuu aliongeza kuwa sekta ya afya ni muhimu kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya nchi zote zikiwemo zilizoendelea na zinazoendelea, hivyo changamoto zote zinazoikabili zinapaswa zipewe kipaumbele katika utatuzi.Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema malengo ya mkutano huo ni kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazohusu sekta ya Afya na kuyapatia ufumbuzi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ambazo ni Tanzania, Malawi, Lethoto, Uganda, Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Muwakilishi kutoka nchini Mauritious.Pia Katibu wa jumuiya hiyo Profesa Yoswa Dambisya, Muwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Paolo Belli pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka nchi hizo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya wa Uganda .Sarah Opendi ,wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) kushoto ni Wazri wa Afya wa Malawi Atupele Muluzi,Waziri Mkuu amefungua mkutano huo jana March 19, 2018 Jijini Dar es salaam.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro

0
0
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro 12  pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini  hapo.

Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt.  Juliethi Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kufanya  upasuaji wa ubingwa wa juu.

“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania Society kwa msaada huu  walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,”.  amesema Dkt. Magandi.

Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu  ya nusu ya vitanda hivyo.  “Hivyo  msaada huo umekuja wakati muafaka  kwani hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
 Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
 Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
 Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MFANYABIASHARA APANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA KUSAFIRISHA GRAMU 214 DAWA ZA KULEVYA

0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mfanyabiashara, Hariri Mohammed Hariri (45), mkazi wa Kinondoni, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu Tuhuma za kusafirisha zaidi ya gramu 214 za dawa za kulevya.

 Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Clara Chalwe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi imedaiwa Machi 2 mwaka huu huko Kinondoni Matitu ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 214.11.

 Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevy isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na imeahirishwa hadi Aprili 4 mwaka huu

DC KIBAHA AZINDUA CHUO CHA VETA KUWASAIDIA VIJANA WA VIJIJINI

0
0
KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda  hatimaye  kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani limeamua kujenga chuo cha ufundi stadi (VETA) kwa lengo la kuwawezesha  vijana wanaotoka katika maeneo ya vijijini ili waweze kujifunza fani mbali mbali ambazo zitawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha viwanda vidogovidogo na kujiajiri wao wenyewe.

Kauli hiyo ilitolewa na  Askofu mkuu  wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC), Samwel Meena wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa chuo hicho ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini, serikali pamoja na wageni kutoka nchini Ujerumani ambao wanajiusisha na masuala ya kuwasaidia vijana kuwainua  kiuchumi kupitia makanisa.

Askofu huyo alibainisha  kuwa lengo kubwa la kuanzisha chuo hicho ni kutokana na kubaini kuwepo kwa wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana hususan wale wanaoishi vijijini na kujikuta wanashinda kutwa nzima bila ya kujishughulisha na kazi yoyote , hivyo ana imani  kuwepo kwa chuo hicho ni moja na ukombozi mkubwa ambao utaweza  kuwasaidia kuondokana na hali ngumu ya kimaisha na kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) kilichojengwa na kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
 Askofu mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC),  Samwel Meena kulia akimpa maelezo mafupi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama wakati wa halfa ya ufunguzi wa chuo hicho cha VETA.
Askofu mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC), Samwel Meena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa chuo hicho cha ufundi stadi amabcho imejngwa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia vijana wanaotoka katika maeneo ya vijiji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATUHUMIWA WIWILI WA UJAMBAZI WAUAWA WAKIJIBIZANA RISASI NA POLISI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa ni majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi.

Pia limesema limekamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi 17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema wilayani Kasulu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo kuwa Machi 19 mwaka huu, tano usiku kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.
Amesema watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata.
"Baada ya kuhojiwa na polisi waliwataka wenzao na kufanikiwa kuwakamata wanne.Katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio mauaji, na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.

"Hata hivyo baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na baada ya kupekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu,"amesema.Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.

Amesema hali hiyo ilisababisha askari kulala chini na watuhumiwa hao ambapo watu hao watuhumiwa hao wa ujambazi walifariki dunia. Aidha Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote wenye silaha katika kambi za wakimbizi kuzisalimisha polisi kabla ya Machi mwishoni na baada ya hapo watanza msako kupitia kamati ya ulinzi na usalama na mkoa huo.

Wakati huohuo Solomoni Ntihazo kwa kosa la kukutwa na pembe za ndovu vipande tisa ambapo vipande viwili ni vikubwa na vipande saba ni vidogo.

WAUZA DAWA ZA KULEVYA KUNYONGWA MAREKANI

0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii.

RAIS wa Marekani Donald Trump ameeleza mpango wake wa kupambana na wauzaji wa dawa za kulevya chini humo.

Akihutubia huko Manchester, Trump amesema kuwa dawa za kulevya yanagharimu maisha ya watu wengi kutokana na matumizi ya dawa na wanaosababisha vifo hivyo hupewa adhabu ya muda mfupi.

Amefafanua na tayari Bunge limetenga kiasi cha dola za Marekani bilioni sita kwa ajili ya kupambana na tatizo hilo.

Ameeleza lazima kuwe na umakini na kuelekeza adhabu kali sambamba na ile ya kifo kwa wauzaji wa madawa ya kulevya.

Ifahamike katika kampeni zake za urais Trump alitoa ahadi nzito zikiwemo kujenga ukuta ili kudhibiti wahamiaji haramu,  kutengua mpango wa afya wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Obama Barrack na ile ya  Marekani kwanza.

ISACA TANZANIA CHAPTER WORKSHOP: UNDERSTANDING COBIT 5 IMPLEMENTATION ESSENTIALS

HOTUBA YA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA 19 MARCH 2018


MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI WA UJENZI WA NYUMBA 36 ZA JESHI LA POLISI MFIKIWA CHAKE CHAKE PEMBA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. 
kuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akihutubia mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipokea mifuko ya saruji zaidi ya elfu sita kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Tanga Cement Bw.  Lawrence  Masha jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA WATAIFA WA UBORESHAJI WA HUDUMA YA UPASUAJI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI ya kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imezindua mpango wa taifa wa kuboresha huduma upasuaji ambayo kila mtu anaweza kumudu  kufikia 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduaji wa mpango huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa mpango huo umekuja wakati mwafaka kutokana na sera ya afya miaka mitano kuisha hivyo mpango huo kuingia katika sera ya miaka mitano.

Dk. Mpoki amesema kuwa mpango huo uko katika muda mwafaka kutokana na hatua mbalimbali za uboreshaji afya kwa wananchi katika upatikaji wa huduma za upasuaji hali ambayo itaokoa maisha pamoja na kuongeza uzalishaji.

“Upasuaji salama ni ishara ya  kila mtanzania anaweza kupata huduma za afya na kuongeza uzalishaji  ,kuboresha huduma za upasuaji bora pamoja na dawa za usingizi ni muendelezo wa kuboresha afya ya uzazi kwa nchi nzima” amesema Dk.Mpoki.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa taifa wa huduma ya upasuaji, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese akizungumza kuhusiana na Tanzania kupokea mpango wa upasuaji na kuingiza katika mpango wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi akizungumza hali ya upasuaji nchini, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akikata utepe kuashiria uzinduzi mpango wa taifa kuboresha huduma za upasuaji, jijini Dar es Salaam.
Sehemu wataalam wa afya  wa nchi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa afya unaofanyika nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB

0
0
*Ummy Mwalimu azindua dawa ya TB kwa watoto,aagiza wanafunzi nao kupimwa ugonjwa huo 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wapo kwenye mchakato wa kuingia mkataba na waendesha bodaboda ili watumike kusafirisha makozi ya Kifua Kikuu(TB) kutoka vituo vya afya kwenda Hospitali kwa ajili ya vipimo.

Pia amezindua rasmi dawa ya TB kwa ajili ya watoto wenye kubainika kuwa na ugojwa huo ambayo ni tamu na ina ladha ya matunda huku akisisitiza umuhimu wa kila mmoja wetu kupambana kutokomeza TB kwani ni janga la kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa watalaam na wadau wa afya na hasa katika ugonjwa wa TB, Waziri Ummy Mwalimu amesema ugonjwa huo ni tishio nchini na duniani kwa ujumla.

Hivyo amesema kuna jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema licha ya kufanikiwa kuwatambua wagonjwa wa TB lakini changamoto kubwa bado wengi wao wanajificha.Hivyo inakuwa ngumu kutambua na ubaya wake TB inaambukizwa kwa hewa.
Amesema takwimu zinaonesha mgonjwa wa TB anaweza kuambukiza watu wengine 20, hivyo kazi inayofanyika sasa ni kuendelea kuelimisha jamii kupima ili kubaini iwapo wana TB au laa.

Pia amesema kutokana na uhaba wa vifaa vya kupima wenye ugonjwa wa TB inalazimu kwenye vitio vya afya baada ya kuchukua makozi ya mtu anayedhaniwa kuwa na ugonjwa huo husafirishwa kwa gari hadi hospitalini.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungungumza wakati wa mkutano wa wadau wa afya waliokuwa wanajadili namna ya kutokomeza Kifua Kikuu(TB) ambapo ametumia mkutano huo kuzindua dawa ya TB kwa watoto waliobainika na watakaobainika kuwa na ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi kabla ya kumpatia dawa ya TB mtoto Salome Makulusi(3) aliyebainika kuwa na ugonjwa huo.Waziri Mwalim amesema dawa ya TB tayari imeingia nchini na leo ameizundua rasmi wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammed Bakari Kambi.
 Baadhi ya wadau wa afya hasa wanaojihusisha na tiba ya ugonjwa wa TB wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Magufuli kuwaapisha Mabalozi Wateule wawili kesho Ikulu Dar es Salaam

NEWS ALERT

NEWS ALERT:WAWILI WAPOTEZA MAISHA,MKURUGENZI TBC ANUSURIKA KIFO KUFUATIA AJALI YA GARI WILAYANI KASULU,MKOANI KIGOMA

0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kuwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

 Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika ku
 Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

.

DUNIA YAMPOTEZA FARU MWEUPE ALIYESALIA

0
0

Na Leandra Gabriel,Globu ya jamii
FARU dume mweupe maarufu kama Sudan amefariki akiwa na umri wa miaka 45.

Imeelezwa kuwa kifo chake kilisababishwa na matatizo ya kiafya hasa umri wake ambapo ilisababisha kudhoofu.Hadi kifo kinamkuta Sudan alikuwa chini ya ulinzi mkali dhidi wa majangili.

Jumanne wiki iliyopita ilitangazwa kuwa hali ya Sudan sio nzuri na amekuwa chini ya uangalizi  maalumu katika hifadhi ya Ol Pejeta nchini Kenya.

Aidha Mwakilishi wa hifadhi ya Ol Pejeta Sampere Elodie amemuelezea Sudan kama Faru jasiri aliyekuwa mlinzi wa wenzake dhidi ya majangili mbugani hapo na aliogopwa kutokana na umbo na muonekano wake.

Aidha imeelezwa baadhi ya jeni (genetics) zake zimeweza kuhifadhiwa na zawezwa kupandikizwa kwa  mmoja wa faru aliowaacha (Najin) kupitia seli ili kuweza kupata faru wa aina yake tena.

Faru Sudan ameacha faru jike wawili wa aina yake (mtoto na mjukuu) maarufu kama Najin na Fatu ambaye ni tasa.


WAZIRI MKUU AMKABIDHI MSAADA BIBI TACLA HAMIDU (MLEMAVU)

0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes).PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

MIKOA YATEKELEZA ASILIMIA 49.4 YA UJENZI WA VIWANDA.

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema kuwa jumla ya viwanda 1,285 kati ya 2,600 vimejengwa katika mikoa mbalimbali ikiwa ni miezi mitatu tangu atoe agizo la ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

Akizungumza katika kikao kazi cha kupitia bajeti ya TAMISEMI na Mikoa, kilichofanyika leo mjini Dodoma Jafo amesema viwanda hivyo vilivyojengwa ni sawa na asilimia 49.4 na kutoa ajira.Amesema agizo hilo bado linaendelea kutekelezwa ambapo hadi kufikia Desemba 31, mwaka huu kila mkoa unatakiwa kuwa na viwanda 100 ambavyo ni sawa na viwanda 2600.

Amebainisha kuwa kupitia wakuu wa mikoa ajenda ya Rais John Magufuli ya Viwanda inatekelezwa na kuwataka waendelee kuitekeleza.Kwa mujibu wa Waziri Jafo, viwanda vidogo vinavyojengwa  ni vile vinavyoanzia sh.milioni 2.5 hadi sh.milioni 10.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya bajeti kwa mwaka huu Waziri Jafo amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanawapitisha vizuri Wakuu wa Mikoa ili waelewe bajeti za mikoa yao na wahakikishe kuwa randama zinakaa vizuri.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo akifunga kikao kazi kilichohusisha Wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa mikoa na Wakurugenzi wa Idara Tamisemi leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo akifunga kikao kazi kilichohusisha Wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa mikoa na Wakurugenzi wa Idara Tamisemi leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Rais, Tamisemi,Dk.Zainabu Chaula akizungumza wakati wa kikao kazi cha Ofisi hiyo kilichojumuisha Wakuu wa Mikoa,Katibu Tawala wa mikoa,Wakuu wa Idara Ofisi ya Tamisemi kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akitoa taarifa ya Mkoa wake kuhusu utekelezaji wa agizo la ujenzi wa viwanda 100 kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa mikoa, kilichofanyika Wakurugenzi wa Idara Tamisemi leo mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakishiriki kikao kazi.

SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI TANO KWA AJILI YA KUNUNUA MASHINE NYINGINE YA KUPIMA VIPIMO VYA TB.

0
0
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini. 

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini leo jijini Dar es salaam. Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert " alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure. Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa takriban watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016. Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .

Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akionyesha dawa kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo leo jijini Dar es salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimuangalia mtoto Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa Salome Bi. Upendo Jeremiah.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 21, 2018

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images