Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

SWEDEN YATOA BILIONI 66 KUKARABATI KITUO CHA KUZALISHIA UMEME HALE HYDRO SYSTEMS WILAYANI KOROGWE

$
0
0

SERIKALI ya Sweden imetoa kiasi cha fedha Bilioni 66 za kitanzania sawa na dola za Marekani milioni 30 ambazo zitatumika katika kukarabati mitambo katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Hale Hydro System wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wakati alipotembelea mgodi huo ambapo upo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga. Amesema kuwa Tanzania na Sweden zina historia za muda mrefu katika uhusiano wa kidplomasia na nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.

Amesema kuwa nishati ni jambo muhimu kwa maendeleo ya viwanda hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo kwa nia moja serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha katika kukarabati mgodi huo." Nishati ni jambo muhimu katika maendeleo ya viwanda na Tanzania tayari imeweka mikakati mizuri katika maendeleo ya viwanda hivyo,serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha kwa kukarabati mgodi huo "alisema.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia wakati alipomtembelea ofisini kwake kufanya mazungumzo naye pia alitembelea Kituo cha kufufua umeme kwa njia ya Maji kilichopo Hale wilayani Korogwe

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili kutoka kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia kitu wakati walipotembelea kituo hicho
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU

$
0
0
SERIKALI  ya Mkoani Tabora imesema kuanzia msimu ujao mazao yote ni lazima yalimwe kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora kinachosisitiza matumizi ya mbolea na ujazaji wa mazao kitaaalamu ili kuhakikisha kunakuwa na mavuno mengi ambayo yatawawezesha wakulima kuzalisha ziada ambayo itawasaidia kuwaletea maendeleo yao binafsi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiendelea na  kampeni zake za kuelimisha wakulima wa pamba juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu waharibifu katika pamba.

Alisema ulimaji wa hivi sasa kwa  wakulima walio wengi hauzingatii ujazaji wa miche(plant population) kitaalamu katika mashamba yao na matumizi ya mbolea jambo linalopelekea kuwepo na mavuno machache katika eneo kubwa shamba hatua ambayo inamfanya mkulima kuwa na mavuno machache.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kilimo kijacho ni lazima wakulima wote waliopo  Mkoani Tabora walime kilimo kinachowasaidia kuzalisha ziada na kupata fedha kwa ajili ya kupanua kilimo chake na kuboresha maisha yao.

"Kuanzia sasa ni marufuku kwa wakulima kwa Mkoa huu kulima zao lolote iwe mchicha, viazi , mahindi na mazao ya biashara bila kufuata mistari na kujaza mazao katika shamba...siwezi kuendelea kuvumilia wakulima wanaendelea kulima kilimo ambacho hakiwasaidia kupiga hatua na kuondokana na umaskini kwa kuzalisha mazao mengi katika eneo dogo" alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga( wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Mratibu wa Pamba wa Wilaya ya Kaliua Samwel Mushi(kushoto) na Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage(kulia).
 Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage(kulia)  akitoa maelezo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga(kushoto) na Afisa Tarafa ya Kaliua Bethod Mahenge (wa pili kulia)
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kushoto) akizungumza jambo jana kwa Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga( kushoto) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Afisa Tarafa ya Kaliua Bethod Mahenge(wa pili kulia) na Mshauri wa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage(kushoto). Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UNESCO wafunda ujasirimali Walimu kufundisha wanafunzi kujitambua

$
0
0
Walimu wanaopatiwa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO) chini ya ufadhili wa program ya Malala wametakiwa kuhakikisha wanatumia elimu waliyopata kuwafanya wanafunzi hasa wa kike kujitambua na kukamilisha malengo yao.

 Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu wakati akifungua semina hiyo inayoshirikisha wajumbe 64 wakiwemo walimu 40 na wakuu wa Shule 20 na maofisa elimu wanne kutoka wilaya nne za mkoa wa Tanga. Wilaya zinazohusika ni za Pangani, Muheza, Korogwe na Lushoto. Semina hiyo ni sehemu ya mradi wa kuwafanya watoto hasa wa kike kujitambua, kupunguza utoro na mimba za utotoni ili kufikia malengo yao ulioanza mwaka 2015.

 Mayasa alisema kwamba ili wawasaidie watoto hao wamalize masomo yao ni vyema walimu hao wakatambua umuhimu wa mafunzo hayo na kuwa karibu na watoto na kuishi nao kutambua shida zao na kuwasaidia kukabiliana nazo ili waweze kusonga mbele. Alisema kama walimu wakiamua kufanyakazi ya kufundisha tu bila kuwa karibu na watoto dhima ya kuwasaidia kufikia malengo hata ya kujiajiri wenyewe wakimaliza masomo haitafikiwa.

 Aliwataka walimu hao kusogeza elimu yao kwa wenzao na katika hilo kuweza kusaidia kufanya vyema kwa watoto katika masomo na pia utayari wa maisha. Aliwakumbusha walimu kusikiliza watoto kutambua shida zao na kujua namna ya kuwasaidia badala ya kubaki kulalamika kwamba watoto hao ni wakorofi au wanakiuka kanuni za shule. Alisema alishawahi kutembelea shule moja na kukuta mtoto ambaye anachelewa kufika shule lakini alipohoji aligundua kwamba kijana huyo wa kidato cha nne ana mama mgonjwa mahututi na lazima amhudumie kwa kuwa baba yake alikwishafariki.

Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Jennifer Kotta akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.

Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga. Kushoto ni Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Jennifer Kotta na kulia ni Simon Mombeyi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, wa Idara ya Elimu.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala wakisikiliza kwa umakini nasaha za mgeni rasmi (hayupo pichani) yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.

Simon Mombeyi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, wa Idara ya Elimu akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.

Mkufunzi wa mafunzo ya ujasiriamali kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Jacqueline Stenga akiendesha mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala kwa wajumbe 64 wakiwemo walimu 40 na wakuu wa Shule 20 na maofisa elimu wanne kutoka wilaya nne za mkoa wa Tanga yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani humo.

Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wan ne kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala kwa wajumbe 64 wakiwemo walimu 40 na wakuu wa Shule 20 na maofisa elimu wanne kutoka wilaya nne za mkoa wa Tanga yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA MHE. ASSUMPTER MSHAMA ALONGA NA KINAMAMA

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI AUFUNGUA KIWANDA CHA MOUNT MERU OIL MILLERS,SINGIDA.MACHI 11,2018.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

BINA:TBS ICHUNGUZE KEMIKALI BANDIA WANAZOUZIWA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
Na Joel Maduka,Geita

Serikali kupitia Shirika la Viwango nchini, TBS limetakiwa kuchunguza kemikali bandia zinazouzwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa wachimbaji wadogo wa madini hali inayosababisha hasara kwa wachimbaji hao.

Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw John Bina amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha wachimbaji wadogo Mkoani Geita kwa lengo la kujadili namna Serikali inavyoweza kufanikisha ujenzi wa soko la madini kwa kanda ya ziwa.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza kemikali bandia kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuwasababishia hasara.“Tunaomba serikali na TBS kuangalia sanaa haya madawa ambayo yanaingia nchini kuhakikisha wanachunguza kemikali hizi kwani kwa sasa uzalishaji unashuka kwa kiasi kikubwa wa madini ,na nyie wachimbaji niwaombe muwe mnachunguza kabla ya kununua kwani kweli mnaingia hasara kubwa sanaa”Alisisitiza Bina.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Bw Nuru Shabani alisema kwa kuuziwa Kemikali hizo bandia amekuwa akiathirika katika shughuli zake.“Kiukweli tunaathirika sanaa na hili halina ubisha sasa hivi unaweza kununua tani moja ya kaboni unakuta inapitisha bila ya kushika mali inamaana hadi iwe na pipim kuanzia mia saba hadi mia nane ,Ila kwa sasa nashukuru walau serikali imetambua mchango wetu na imetuthamini mimi nilikuwa naomba kupitia Kitengo chetu tuwe na wasimamizi ambao watatusaidia kubaini kemikali hizi”Alisema Nuru.

Bw John Bina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo alisema pamoja na matatizo hayo lakini wachimbaji hao wamekubaliana kuanzishwa kwa soko la madini Mkoani Mwanza ili kudhibiti vitendo vya utoroshwaji wa madini.
Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw John Bina ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo akizungumza na wachimbaji wadogo wakati wa kikao cha kujadili soko la madini ya dhahabu kilichofanyika Mkoani Geita .
Katibu msaidizi wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo,Bw Gregory Kibusi akijitambulisha na kuelezea lengo ambalo limewapeleka Mkoani Geita mbele ya Afisa madini wa Mkoa huo. 
Afisa madini Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akizungumza na Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo ambao walikuwa wamewasili kwenye ofisi za madini Mkoani Humo. 
Bw,Nuru Shabani ambaye ni mchimbaji mdogo akionesha kemikali ambayo amekuwa akiitumia kukamatia madini kwenye eneo la mgodi wake. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambaye pia ni mchimbaji ,Bw Leornad Kiganga Bugomola akiwakaribisha wajumbe kwenye mkutano wa wadau wa madini. 
Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale ambaye pia ni mchimbaji na Mjumbe kwenye kamati hiyo,Hussen Nassoro Kasu akiwataka wachimbaji kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kwenye shughuli zao. 
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa kwenye kikao hicho.

REPOA YATOA UTAFITI WAKE,YAKIRI WANANCHI WENGI WAMERIDHISHWA NA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti ya REPOA, Dr. Donald Mmari akizungumza kuhusu matokeo ya utafiti wa Afro Barometer kuwa hali ya uchumi nchini ambapo matokeo yake yameonesha kuwa Wananchi wengi wameridhishwa na hali ya kukua kwa uchumi nchini huku wakipongeza upatikanaji wa elimu bure.
 Mtafiti kutoka Repoa, Thadeus Mboghoma akieleza baadhi ya matokeo ya utafiti huo katika nyanja ya ukuaji wa uchumi na matarajio ya watanzania kwa serikali ya sasa.
 Dr Lucas Katera kutoka Repoa ambaye alikuwa akiongeza mjadala kuhusu matokeo ya utafiti huo wa hali ya uchumi nchini akichangia jambo wakati wa mjadala .
 Mtafiti kutoka Repoa, Stephene Mombela akifanya mawasilisho ya Tafiti ya Afro Barometer  iliyohusu hali ya Uchumi nchini ambayo imeonesha kuwa Wananchi wamekiri kuwa Uchumi katika serikali hii unapanda
 Msomi na Mtafiti , Profesa Mwesigwa Baregu (Katikati) akichangia mada wakati wa mjadala wa matokeo ya utafiti wa Afro Barometer.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti ya REPOA, Dr. Donald Mmari  akichangia katika mjadala wa matokeo ya utafiti wa Afro Barometer ambao umeonesha kuwa idadi kubw aya Watanzania wameridhishwa na ukuaji wa uchumi hapa nchini
Sehemu ya Washiriki katika Matokeo yaya utafiti wa Afro Barometer ambao umeonesha kuwa idadi kubw aya Watanzania wameridhishwa na ukuaji wa uchumi hapa nchini
--

Serikali yajipanga kupokea mradi wa Global Learning XPRIZE

$
0
0
Serikali imesema inajiandaa kuupokea mradi wa ‘Global Learning XPRIZE’ unaowawezesha watoto walio nje ya mfumo rasmi kujifunza stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kupitia Michezo iliyowekwa kwenye tableti, kutoka kwa wadau wanaoufadhili baada ya kumalizika muda wa majaribio. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi wakati akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali. 
Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi akizungumza kuhusu maandalizi ya serikali kuupokea mradi wa Global Learning XPRIZE.

“Kama serikali mradi unapomalizika tunaangalia namna ya kuuendeleza. Tutaendelea kushirikiana na halmashauri zetu zilizoko kwenye mradi wauone kama ni wa kwao na kwamba badala ya watoto kuzurura mitaani wanaendelea kujifunza,” amesema Mushi na kuongeza. “Tunaagiza wale wahusika, wadau wa elimu katika ngazi zote za kijiji hadi mkoa wa Tanga waone kama hiki kilicholetwa kwetu ni zawadi,na ni lazima kuuendeleza ili kupunguza watoto walioko nje ya mfumo rasmi; kwa maana hiyo inatakiwa tuwe na ushirikiano kuona changamoto baada ya huu mradi kumalizika ili kuzifanyia kazi.” 
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

Akielezea utekelezaji wa mradi huo tangu ulipoanza na ulipofikia, Afisa Msaidizi wa Mradi kutoka UNESCO, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 2000 kutoka vitongoji 141 katika wilaya 6 za mkoa wa Tanga wamenufaika na mradi huo. “Baada ya miezi 15 ya mradi kukamilika, mradi utakabidhiwa kwa serikali ili kuendelea kuusimamia, ambapo tumekutana leo Tarehe 13/3/2018 na wawakilishi kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (BMT) , Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na TAMISEMI ili kuweza kuangalia ni jinsi gani watoto walio katika mradi wataingia katika mfumo rasmi katika ngazi husika,” amesema. 
Wadau mbalimbali wakichangia katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

KAULI YA RAIS MAGUFULI ALIPOWEKA JIWE LA MSINGI KIPANDE CHA PILI RELI YA KISASA

NURU YA AFYA

$
0
0
Ungana pamoja nasi katika usiku wa kipekee tukila, kunywa na kuburudika katika 2018 Nuru Ya Afya Fundraising Masquerade Ball inayoletwa kwenu na TAHMEF (Tanzania Health and Medical Education Foundation)

Ili kuunga juhudi za kuboresha afya ya uzazi na upatikanaji wa huduma za bima ya afya kwa watanzania.

MGENI RASMI: Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii,Jinsia,wazee na Watoto, Mheshimiwa DK. FAUSTINE NDUGULILE

Usisite kuwasiliana nasi kujipatia tiketi na maelezo zaidi kupitia:

Simu: +255 656 597 434, +255 768 326 387

Tovuti: www.tahmef.or.tz

#NuruYaAfya #600lives 

TAZAMA JINSI SIMU YA MKONONI INAVYOBADILISHA MAISHA YA MAELFU NCHINI TANZANIA.

$
0
0
Je wajua yakuwa unaweza baadilisha maisha na mtandao wa simu? Hebu angalia video hii kujua wengine wamefanyaje?




HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI

$
0
0
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akikabidhi Msaada wa Vitanda 4o na Magodoro 40 kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe kwaajili ya hospitali ya mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusheherekea siku ya Mwanamke duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8. Benki hii imetoa vitanda na magodoro kwaajili ya wodi ya akina mama katika hospitali hiyo.
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya Mwananyamarla jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe na kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akishukuru kwa Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda  kwa kuiona hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa kunahospitali nyingi"Tunashukuru Mchango wenu sana Mungu awabariki ."
kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda na Kulia ni Mkuu wa matawi ya Kanda Elizabeth Mayengo.

BENKI  ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa Mwananyamala, jijini Dar es Salaamkwa kuwa Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika hospitali ya Mwananyamala wakiongozwa na wafanyakazi wanawake wa Benki ya Exim kwenye hospitali hiyo jengo la utawala  katika hospitali hiyo ukipokelewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala Dk. Khadija Shebe.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda amesema “Katika kuadhimisha sherehe za wanawake mwezi huu, Benki ya Exim inatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii na kwenye ukuaji wa uchumi. Msingi wa mpango wetu huu wa mwaka mzima wa kujali jamii ni kuelewa kiasi gani wanawake ni muhimu katika jamii".

Benki imejitolea kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 kwa kusaidia wanawake kwa kuboresha huduma za uzazi katika sekta ya afya. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa ya kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu na sisi tumejizatiti kwenye mpango huu."

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa wanawake nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii .”

Mawakala wa Tigo Pesa Wajinyakulia Mamilioni

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni ya pesa kwa utendaji wao mzuri.

Wakala RBB RBB ya Sinza, Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka Tigo Pesa, huku Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi ya pili ya TZS 5 millioni katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo. ‘Nilishinda zawadi ya kanda katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi kuwa uwekezaji na juhudi nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha kutangazwa kama mojawapo wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.

Pamoja na zawadi hizio kwa washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za TSH 3 millioni na TZS 2 millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda nchini. Pia zawadi za bonasi zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia malengo waliowekewa katika kipindi cha promosheni hiyo.

Mojelwa Mlinga wa Ukonga, Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya Pwani na kujinyakulia kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia hela alizoshinda kuboresha mtaji wake wa biashara. ‘Nilishinda zawadi ya pili kitaifa katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa natarajia kushinda zawadi ya kwanza kitaifa, ila nashukuru kuwa nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema.
Robert Butambele (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Sinza, Dar es salaam akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni kumi kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Butembele aliibuka mshindi wa kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge.
Said Khatib (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Mkunazini, Zanzibar akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni tano kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Khatib aliibuka mshindi wa pili kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge.
Baadhi ya mawakala mbali mbali walioshinda zawadi katika promosheni ya mawakala wa Tigo pesa iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo. Hii ilikuwa baada ya kupokea zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


TRA: MAAFISA MAWASILIANO NINYI NI MABALOZI WA KUELIMISHA WANANCHI KUHUSU KODI

$
0
0
Na: Veronica Kazimoto
Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wameombwa kuwa mabalozi wazuri katika sehemu zao za kazi na katika jamii wanayoishi kwa kuwaelimisha wananchi masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Kodi kwenye Kikao Kazi cha Maafisa hao kinachoendelea  jijini Arusha , Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo, alisema elimu ya kodi itawafikia watu wengi zaidi kwa kuwa maafisa hao wana ushirikiano mkubwa katika kutoa habari sahihi kwa umma.

"Kila mmoja wetu anachokifanya ni sauti kwa mwenzake mahali alipo, ndio maana hata katika mitandao mbalimbali tumekuwa tukisaidiana kwa kuwa, ukiona jambo baya linasemwa juu ya taasisi ya mwenzako au Serikali unamsaidia kutoa ufafanuzi, hivyo, mkielewa mada yangu hapa, najua mtanisaidia kuelimisha masuala ya kodi katika sehemu zenu za kazi na maeneo mengine", alisema Kayombo.

Kayombo alisema kuwa, maafisa hao wana nafasi kubwa katika kuelimisha jamii na kusahihisha baadhi ya wananchi ambao wanakuwa na elimu isiyo sahihi kuhusu masuala yanayohusu kodi na ukusanyaji wa mapato kwa ujumla. 

Aidha, pamoja na mambo mengine, Richard Kayombo aliwakumbusha Maafisa hao suala zima la kudai risiti kila wakati wanaponunua bidhaa ili kuchangia maendeleo ya nchi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo, akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Kodi kwenye Kikao Kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kinachoendelea jijini Arusha.  Kikao hicho kinatarajia kumalizika tarehe 16 Machi, mwaka huu. (Picha na Benedict Liwenga).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

AFANDE SELE AJIUNGA CCM RASMI MBELE YA RAIS DKT JOHN MAGUFULI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MSANII maarufu nchini katika muziki wa kizazi kipya Selemen Msindia a.k.a Afande Sele amesema amefurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli na kwamba amekuwa mbishi wa kukubali lakini kazi ya Rais imemfanya aamue kumfuata Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Afande Sele amesema kuwa anamfananisha Rais Magufuli kama dereva wa gari ambaye analiendesha vema na yeye kama abiria ametulia anakunywa soda yake na hivyo anachoweza kumlipa kwa vitendo ni kujiunga CCM ili ashiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.

Msanii huyo amesema hayo leo mchana huu mbele ya Rais Magufuli aliyeko mkoani Morogoro ambako kuna tukio la kufanyika uzinduzi wa Kiwanda cha Sigara cha Philip Moris kilichopo Kingolwira mkoani hapo.

"Nimekuwa ni mtu wa kufikiria na kubisha hadi pale ninapojiridhisha.Naomba nitumie nafasi hii kumwambia Rais Magufuli tangu umekuwa Rais umefanya kazi kubwa ambayo binafsi na Watanzania wengine imenivutia. Kuanzia muda huu naomba Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro mnipokee rasmi.

"Utendaji kazi wa Rais Magufuli umenifanya nikubali kwa ridhaa yangu niwe upande wake.Nchi inakwenda na mambo mengi yanafanyika kwa ajili yetu na hata mataifa mengine duniani yanajua kazi ambayo inafanywa na Rais wetu,"amesema Afande Sele.

Baada ya kutangaza uamuzi huo, wananchi waliokuwa mbele ya Rais walianza kushangilia kwa shangwe huku wengine wakipiga kelele kuonesha furaha yao kutokana na uamuzi wa msanii huyo kujiunga CCM. Afande Sele amekuwa vyama vya upinzani kwa muda mrefu na historia yake inaonesha amewahi kupita CUF,Chadema na ACT-Wazalendo na leo amejiunga CCM rasmi.

MASAUNI AZINDUA VITUO MWENDO SITA VYA POLISI,AWAASA WANANCHI KUJIKITA KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akisikiliza maelezo ya Kituo Mwendo cha polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro (katikati), baada ya kuzindua moja ya vituo hivyo ambavyo idadi yake ni sita, lengo ikiwa vitumike katika maeneo ya mkoa huo kudhibiti uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu huku akiwaasa wananchi kujikita kwenye shughuli za maendeleo. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi kutoka Mkoa wa Polisi Kinondoni, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
Moja ya Vituo Mwendo vya Polisi vilivyozinduliwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), ambavyo vitatumika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA

$
0
0
*Kufanyika kesho jijini Dar es Salaam, Mhandisi Tumbo aomba wananchi kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo na Watanzania kwa ujumla kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo ambapo kesho Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harembee ya uchagiaji fedha kufanikisha ujenzi huo.

Kwa sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.

Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.

Mhandisi Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.

Amefafanua tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha fedha hizo.

"Kesho tutakuwa na harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni ambapo wananchi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi Dar es Salaam pamoja na watanzania wengine tunaomba wajitokeze kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo(wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Muheza katika ukumbi wa Golden Tulp jijini Dar es Salaam leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAMBURA AWAJIBU TFF,ASUBIRI BARUA YA MAAMUZI KAMATI YA MAADILI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MAKAMU Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Michael Wambura ameeleza suala Kamati ya Maadili ya shirikisho ni la kimkakati zaidi na si la kisheria.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Wambura amesema suala hilo lilianza miaka 14 iliyopita akiwa raia wa kawaida tuu.Wambura anatuhumiwa kufoji barua na kupokea malipo yasiyo halali kutoka Kampuni ya JICK System Ltd,pia kushusha hadhi ya TFF.

Akizungumzia zaidi suala hilo Wambura ameeleza  tatizo lililopo ni uenyekiti wa TFF, fedha na ajira za TFF hasa nafasi ya Katibu Mkuu.Pia Wambura amesema kuwa kama Makamu Mwenyekiti wa TFF ataendelea kufanya kazi kama kawaida na lawama hizo zishindwe kabisa.

Ameongeza, kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya Shirikisho hilo na wananchi watalijua mapema na ameitaka kamati tendaji kufikiri tena kabla ya kufanya maamuzi.Hata hivyo amesema anasubiri barua rasmi ya kamati hiyo na ndipo atakuwa na cha kuzungumza,hivyo anasubiri maana kwa sasa amesikia tu taarifa kuhusu kusimamishwa kujihusisha na soka.

Kwa upande wa Wakili wa Wambura Emmanuel Muga amesema, kikao hakikufuata sheria hali iliyompelekea kushindwa kufanya kazi yake, amesema barua ya mwito ilicheleweshwa na ilipelekwa nyumbani kwake ili hali Wambura yupo TFF. 

Pia ameeleza kanuni ya 48 ya maadili ya TFF inayoeleza kuna siku 3 za kuitikia mwito haikuzingatiwa na pia kamati haikuzingatia kanuni ya 58 inayoeleza kuhusu kesi na kupanga siku ya kuleta vielelezo na mashahidi haikuzingatiwa kwa mteja wake.

Pia Muga ameeleza kuwa kikao hicho hakikutoa majibu ya moja kwa moja na walieleza watatoa uamuzi siku nyingine.

JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ametoa miezi miwili kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuhakikisha linakamilisha uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika kiwanja cha ndege cha Dodoma ili kuwezesha jengo hilo kuhudumia abiria wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Ametoa agizo hilo, mkoani Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa jengo baina na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) na NHC na kusema kuwa kukamilika kwake kutawezesha abiria zaidi ya 100 kuhudumiwa kwa wakati mmoja ambapo kwa sasa jengo linahudumia abiria 35.

“Mkataba tunaoshuhudia ukisainiwa leo unaitaka NHC kukamilisha mradi huu ndani ya miezi mitatu lakini niagize mradi huu ukamilike ndani ya miezi miwili kwa sababu fedha zipo na cheti mlichonacho cha daraja la kwanza kinaonyesha namna mnavyoweza kufanya kazi hii kwa haraka’ alisema Mhandisi Nditiye.

Aidha Naibu Waziri Mhandisi Nditiye ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), pamoja na maboresho hayo kuhakikisha inafanya maboresho kwa kujenga maduka ya kubadilishia fedha na bidhaa ili abiria watakaotumia kiwanja hicho hiyo waweze kupata huduma mbalimbali wakati wanaposubiria kupanda ndege.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dodoma kwa sasa ndio Makao Makuu ya Serikali hivyo miradi yote inayotekelezwa chini ya Wizara lazima izingatie viwango na thamani ya fedha ili kuendana na hadhi ya mji.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia), akioneshwa na Meneja Mradi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Focus Kadege, jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ambalo litafanyiwa uboreshwaji ili kuweza kuchukua abiria 100 kwa mara moja, Mkoani humo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa kuboresha jengo la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde, akitoa hotuba katika hafla ya utiaji saini wa uboreshaji wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege Dodoma, Mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi (kulia waliokaa), wakisaini mkataba wa uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia), Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (kulia), Felix Maagi wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma mara baada ya kusaini, Mkoani humo. 


Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images