Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema ili kuleta  ufanisi mkubwa katika usimamizi  wa miradi ya maji safi na salama  vijijini, ipo haja ya kuwa na chombo cha kusimamia  huduma za maji vijijini utakaosimamiwa na wizara kwa lengo la kuleta uwajibikaji wa karibu kwa watumishi wanaosimamia sekta ya maji nchini.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jumaa Aweso alisema hayo  kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali kikiwemo cha Dumila juu katika Kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

Kabla ya kuzungumza na wananchi  alipata fursa ya  kukagua ujenzi wa mradi wa maji Dumila  ambao ulianza kujengwa tangu Januari 24, 2014 na kukamilishwa Desemba 15, 2017 kwa gharama ya Sh milioni 800.5.

Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya wiki moja  mkoani Morogoro  iliyomfikisha katika   halmashauri za wilaya sita  kati ya tisa ambazo ni  Malinyi, Ulanga, Kilombero, Mvomero, Manispaa ya Morogoro na Kilosa .

Alisema  kuwa,  miradi mingi ya maji safi na salama inayotekelezwa vijijini imekosa usimamizi wa karibu, ufanisi na mingi imejengwa chini ya viwango na baadhi katika maeneo ambayo vyanzo vyake vya maji si  vya kuaminika.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuwapelekea mafundi wa ujenzi  kwa ajili ya  ukamilishaji  wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 katika mji wa Malinyi, ( kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda akichanganya saruji na mchanga kwa ajili ya ujenzi huo.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuchanganya mchanga na saruji  kwa  ajili ya  ukamilishaji  wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 mjini Malinyi na ( kushoto kwake ) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda ,  na ( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo Majura Kasika.
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji , Jumaa Aweso,  akimsiliza Mzee Said Mazinge  wa  Kata ya Kibati, wilaya ya Mvomero , mkoa wa Morogoro  kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama  alipofanya ziara  wilayani Mvomero. .
 Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa mji wa Mlimba , wilaya ya Kilombero  juu ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya namna ya kutatua changamoto za ukosefu wa maji maeneo ya vijijini na mijini.
 Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso  akipambu maji katika moja ya kisima kirefu  mara baada ya kukizundia katika kijiji cha Chikuti, wilaya ya Ulanga kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa kijiji hicho .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI

$
0
0

WANANCHI wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga wametakiwa kufanya subira wakati mgogoro wao wa fidia na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan Afro Asian Engineering ukitafutiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa wito huo Machi 12, 2018 kwenye mkutano na wananchi hao uliofanyikia kwenye Kitongoji cha Mahiga na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Serikali.

Mkutano huo unafuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alilolitoa Machi 11, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kahama ambapo alielezwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum kuwa wananchi wa Mahiga wana mgogoro wa muda mrefu na mwekezaji hususan kuhusiana na suala la ulipaji fidia ili kupisha mradi.

Kufuatia maelezo hayo ya Mbunge, Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Naibu Waziri Biteko kuhakikisha anafika kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi. 

Rais Magufuli alisisitiza kuwa ni wakati sasa Watanzania waanze kunufaika na rasilimali zao ikiwemo madini. "Tunataka madini yawanufaishe Watanzania," alisema Rais Magufuli.

Alisema wawekezaji wakifika nchini ni lazima wahakikishe Watanzania wananufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo ajira, kodi na tozo.

"Jukumu langu nimeamua kusimamia suala hili; Nawahakikishia Serikali iko imara kwa ajili ya kuwatetea wanyonge," alisema Rais Dkt. Magufuli.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo Wilayani Shinyanga (hawapo pichani) kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) akizungumza kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum akizungumza na wananchi wake wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga kuhusiana na mgogoro wao na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.

FUATILIA LIVE RAIS DKT MAGUFULI AKIWEKA JIWE LA MSINGI WA RELI YA KISASA (Standard Gauge ) LEO MKOANI DODOMA

$
0
0

Pichani chini ni sehemu ya eneo ambalo Rais Dkt John Pome Magufuli leo anatarajia kuweka jiwe la Msingi sehemu ya pili ya Ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge ) kuanzia Morogoro hadi Makutopora mkoani Dodoma.Sherehe hizo zinafanyika eneo le Ihumwa mkoani humo,ambapo tukio hilo linarushwa LIVE kupitia Redio na Televisheni. 

Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umeteketeza kwa moto kilo 48 za Nyama kutoka Afrika Kusini ambazo ziliingizwa nchini kinyume na sheria.

Nyama hizo zilizokuwa mali ya Kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam zilikamatwa Uwanjwa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza katika zoezi hilo Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa hatari zinazotokana na Chakula Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hizo ni katazo lililotolewa na ZFDA yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata Chakula na Dawa zilizokuwa salama.

Amesema maamuzi ya katazo hilo yametokana na uwepo wa maradhi ya mripuko ya Listeria nchini Afrika Kusini hivyo Ofisi yao ikapiga marufuku uingizwaji wa Nyama, Maziwa na Samaki kutoka nchi hiyo.

Amesema katazo hilo si kwa Zanzibar pekee bali pia Tanzania bara na nchi nyingine kutokana na utaratibu wa biashara kimataifa.
 Nyama kutoka Afrika ya kusini zilizoingizwa Zanzibar kinyume na sheria na Kampuni ya Qamar zikiwa zimewekwa katika Maboksi kabla ya kuteketezwa huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
 Mkuu wa Jiko la kuteketezea bidhaa mbovu Khamis wa Khamis Mkanga akiziingiza nyama katika jiko hilo kwa ajili ya kuteketezwa baada ya kuingizwa nchini kinyume na sheria kutoka Afria ya Kusini. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
 Nyama kutoka Afrika ya kusini zilizoingizwa Zanzibar kinyume na sheria na Kampuni ya Qamar zikiwa zimeingizwa katika Jiko tayari kwa kuteketezwa huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
 Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa hatari zinazotokana na Chakula kutoka Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), Aisha Suleiman akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi la kuteketeza  nyama zilizoingizwa nchini kinyume na Sheria na Kampuni ya Qamar ya Jijini Dar es Salaam kutoka Afrika ya Kusini. 
Mkaguzi wa bidhaa za Chakula hususan Nyama, Daktari Othman Juma Othman akielezea ugonjwa wa Listeria na madhara yake mara baada ya zoezi la kuteketeza nyama kufanyika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU GEITA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA baada ya kufika kwenye ofisi yake . 
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda akimashukuru Mkuu wa Mkoa baada ya kutembelea miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwenye Wilaya za Bukombe pamoja na Chato. 
Meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta ,Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya Tatu kwenye baadhi ya maeneo. 
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi.

Na, Joel Maduka,Geita
Mkoa wa Geita unatarajia kunufaika na mradi kabambe wa usambazaji umeme vijijini REA awamu ya Tatu kwa kuongeza shughuli za kiuchumi kwa wananchi kutokana na vitongoji 220, vijiji 372 na Kata 499 ambazo zinatarajia kunuifaika na Nishati ya Umeme.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta amesema Mradi huo kwa mzunguko wa kwanza utaunganisha wateja wapatao 12,944 na hivyo kukamilika kwa Mradi huo utafanya umeme kuongezeka kwa Asilimia 51 kwa wateja waliopo sasa.

“Mategemeo yetu ni kwamba mzunguko wa pili ambao unatarajia kuanza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2020 na 2021 utafanya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita kupata umeme kwa asilimia mia moja” Alisema Ruweta.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kujua kuwa hakuna fidia ambazo watalipwa kutokana na mradi huo.

“Wito kwa wananchi wa Mkoa wetu wa Geita watoe ushirikiano Katika vijiji vyote ambako wataalamu wetu watapitia wajue kuwa hakuna fidia kwasababu mradi huu utakuja kwaajili ya kutupatia maendeleo na unapowasha umeme itasaidia kukua kwa uchumi wa eneo husika na Mkoa wetu” Alisema Luhumbi. 

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda alisema hadi sasa hivi bado hawajaona tatizo lolote ambalo lipo kwenye mradi huo na kwamba wanaamini watafanikisha kwenye maeneo yote ambayo mradio huo umepangwa kufanyika.

Mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza Mkoani Geita unatekelezwa na mkandarasi aitwaye White city Guangdong JV ambaye ni ubia wa Kampuni ya Kitanzania na Kampuni ya nje na unatarajia kugharimu zaidi ya Shilingi za kitanzania Bilioni 61 na fedha za Kimarekani Dola milioni 7.8.

RC MNDEME AMEMWAGIZA MKUU WA WILAYA YA NYASA KUMATAWA WALIOVAMIA MILIMA YA LIVINGSTONE

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME amendesha zoezi la upandaji miti aina ya mitiki katika wilaya ya nyasa na mkumwagiza mkuu wa wilaya ya nyasa ISABELLAH CHILUMBA pamoja nakamati yake ya ulinzi na usalama kuwamata watu waliovamia milima ya livingstoni na kuharibu misitu kwa kuchoma moto.HABARI MAKILI HII HAPA VIDEO YAKE

YARA TANZANIA YAPUNGUZA BEI YA MBOLEA YA YARAMILA OTESHA

$
0
0
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Uzalishaji Mbolea ya  Yara , Linda Byaba akizungumza na waandishi habari kuhusiana na punguzo bei ya mbolea ya YaraMila Otesha leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya uzalishaji Mbolea ya Yara , Linda Byaba akionyesha ubora wa mbolea aina ya YaraMila Otesha leo jijini Dar es Salaam.

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KUELEKEA uchumi wa viwanda kampuni ya usambaaji  mbolea ya Yara Tanzania imepunguza gharama Mbolea YaraMila Otesha kwa asilimia 50 ili kuwezesha wakulima wazalishe mazao  bora yatayongia katika viwanda  vya bidhaa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Linda Byaba amesema kupunguza bei ya mbolea kwa asilimia 50  ni kuwawezesha wakulima waweze kumudu gharama hizo.

Amesema Yara ni kampuni inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa mbolea zenye virutubisho linganifu kama YaraMila. Kila punje moja ya YaraMila ina virutubisho vyote kama Nitrojeni, Fosiforasi, Kalisiam, Boroni, Magniziam kwa ajili ya kuupa mmea lishe linganifu.

Byaba amesema wakulima wanaozalisha mazao ya nafaka, kahawa, chai, sukari, tumbaku, alizeti, viazi na mbogamboga wanafaidika na mbolea zenye virutubisho kupitia matawi yake yaliyopo Tanzania na Rwanda.

Amesema faida za mbolea hii ya Kupandia ya YaraMila Otesha , lishe linganifu ya mmea ,ni mbolea ya NPK yenye kiwango cha juu cha kirutubisho cha Fosforasi na ina jumla ya virutubisho 7 kulinganisha na mbolea zingine za kupandia, haichachushi wala udongo,huchochea uotaji wa mizizi mingi hivyo kuufanya mmea kuwa imara muda wote,huchochea machipukizi mengi  yanayoleta mavuno mengi  katika zao la mpunga.

Aidha amesema faida zingine ni kuyeyuka kwa haraka zaidi kwenye udogo na kufanya mmea upate vizurubisho vyake stahiki kwa muda unaohitajika
Pamoja  asilimia 50% ya ongezeko la uzalishaji kwa wakulima waliotumia.

OIF yaelezea fursa zilizopo kwa Watanzania wanaojua Kifaransa

$
0
0
Shirika la Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muhimu kwa Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa kwa sababu kuna fursa nyingi wanaweza kuzipata kwa kuzungumza lugha hiyo. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa kama Burundi, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na hivyo kwa wananchi wa Tanzania hiyo ni fursa ambayo wanaweza kuitumia katika shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.
Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier akizungumza kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25.

"Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu waitumie.""Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa," alisema Clavier. 

Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française, Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

MENEJA MPYA PARK HYATT ZANZIBAR KUSHIRIKI KUINUA VIPAJI VYA VIJANA

$
0
0
Meneja mpya wa Park Hyatt Zanzibar Nicolas Cedro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa na akielezea mikakati yake ya kuinua vipaji vya vijana katika masuala ya upishi na hoteli Visiwani humo. Kushoto ni Meneja Masoko Milvas Burnice.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Hotel ya Hyatt umemtambulisha meneja mpya wa Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar  Nicolas Cedro ambaye amejizatiti katika kusaidia kuinua vipaji vya vijana hususani katika masuala ya upishi na hoteli.

Hoteli hiyo iliyopo maeneo maarufu ya Stone Town tayari imeshaweza kusaidia huduma za kijamii kama kufungua vituo viwili vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kituo cha kulea wazee wasiojiweza, elimu, maji na michezo hususani mpira wa miguu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utambulisho huo, Nicolas Credo amesema kuwa mbali na kuwasaidia vijana katika masuala ya hoteli ambapo tayari ameshafanya mazungumzo na Waziri wa Utalii Zanzibar Mahmoud Kombo kwa ajili ya kuweza kusaidia vijana ambapo kiutalaamu yeye ana Shahada mbili za masuala ya vyakula na uendeshaji hoteli kutoka chuo kikuu cha hoteli kilichopo Nice nchini Ufaransa pia Shahada ya uzamili ya uendeshaji wa hoteli kutoka katika chuo kikuu cha E Cornel. 

Cedro amesema kuwa atatumia uzoefu wa elimu, ujuzi wa lugha pamoja na ubunifu katika kujenga sifa na ubora wa hoteli hiyo na pia kwa wafanyakazi wake kwani akiwa kijana wa miaka 17 aliweza kuanza kuanza kazi ya upishi na pia anatambua umuhimu wa kuibua na kulea vipaji vya vijana na hivyo anategemea kushiriki katika shughuli za kijamii akiwa Zanzibar kwa kushirikiana na shule mbali mbali za kisiwani hapo za mapishi ili kusaidia vijana wenye vipaji vya upishi waweze kupata ujuzi wa kimataifa alio nao na hivyo waweze kujiendeleza katika fani hiyo na kuitumia kama njia ya kujiinua kiuchumi.

Amesema akiwa kama Meneja wa hoteli ya Park Hyatt Zanzibar na Cedro na timu yake kwa pamoja wana lengo kuu la kuipandisha hoteli hiyo kuwa katika viwango vya juu zaidi na hivyo kuchangia katika juhudi za taifa za kuhamasisha utalii nchini ikiwemo kisiwani humo kwa kushirikiana na hoteli zilizopo Italy na Ufaransa.

“Napenda kufanya kazi katika bara la Afrika na hasa katika kisiwa cha Zanzibar. Ni mahali ambapo kuna mazingira mazuri na watu wenye upendo. Nimeshafanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka mitatu sasa katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, Melia Zanzibar na sasa hapa Park Hyatt Zanzibar. Nimesikia furaha kubwa sana kupata nafasi hii ya kuendesha hoteli hii na nategemea kutumia ujuzi na uzoefu wangu ili kuleta ladha ya kipekee katika chakula na pia huduma tutakazowapatia wateja wetu,” alisema Cedro.

Naye Meneja wa Masoko wa Park Hyatt Zanzibar  Milvas Burnice amesema kuwa ujio wa Cedro utakuja kuwa na manufaa sana kwani ni moja kati ya watu ambao wameshafanya kazi katika hotel za Hyatt ana ana ubunifu wa hali ya juu ukiachilia mbali baadhi ya vitu ambavyo mmiliki wa hotel hizo anataka vifanywe. 
Baada ya kumaliza kaz leo narejea hom kulea. Namsubir mtt atoke shule sa 10 kwahy kaz yang ndo hyo na nyingne natuma pia

DC TEMEKE AHIMIZA WAUMINI DINI YA KIISLAMU KUDUMISHA UMOJA NA AMANI

$
0
0
Mkuu wa wilaya Temeke Felix Lyaniva
Walimu wa Madrassa waliohudhuria kikao hicho

Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Felix Lyaniva amewashauri waumini wa dini ya Kiislamu kuepuka migogoro na badala yake waimarishe umoja na udugu ili kudumisha amani iliyopo katika nchi yetu iendelee kudumu. 

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu wa madrassa mbalimbali zilizopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata), Wilaya ya Temeke uliofanyika katika Chuo cha Ualimu (DUCE).

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Da es Salaam Alhadi Mussa Salim amewataka waumini wa Kiislamu kufuata kauli mbiu ya baraza hilo inayosema "Walimu, tujitambue, tubadilike na tuache mazoea" na kufafanua ili kutengeneza jamii yenye maadili mema na uadilifu kwa jamii ya kiislamu na Mkoa kiujumla. 

Pia amewasisitiza walimu wa madrassa kuwafundisha wanafunzi wao yaliyo mema na kutengeneza mtaala mmoja wa kufundishia masomo ya dini ya kiislamu.Pamoja hayo wananchi wa Wilaya Temeke wanatakiwa kudumisha ulinzi na usalama wa wilaya yao."Kwani jamii yoyote yenye amani na utulivu ndio huchochea maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla,"amesema.

AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii.
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC kesho wanatarajia kuanza rasmi mazoezi ili 
kujiandaa zaidi na michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho (ASFC) 

 ambapo watavaana na Mtibwa Sugar katika mchezo huo wa mtoano.

Mchezo huo utakuwa ni wa vuta nikuvute ikiwa kila timu ikihitaji kupata matokeo mazuri ili kusonga mbele zaidi.  Mchezo huo utarindima katika 
dimba la Uwanja Wa Azam Complex Chamazi Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam huku Azam akimkaribisha Mtibwa Sugar .

Ofisa Habari  Azam FC Jaffary Iddy amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa baada ya kumaliza mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mbao FC ambapo walipata ushindi wa mabao 2-1, kikosi kilikuwa kwenye mapumziko na kesho kinaaanza mazoezi rasmi ili kukabiliana  na mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa sugar.

Ambapo katika mtanange huo ataeibuka kidedea ndiyo ataingia Nusu Fainali ambapo Jaffary amesema wanatarajia mchezo kuwa mgumu  kwa pande zote mbili kuwa na morali ya kupata ushindi wa aina yoyote ili kutinga fainali na  kusonga mbele.

 "Mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili tunafahamu timu ya Mtibwa na ikiwa kila kikosi kinahitaji ushindi ili kuendelea na mashindano ukizingatia katika mchezo huo lazima mmoja atoke na mwengine asonge mpaka kufikia kilele na kupata mshindi ambaye atakuwa ni muakilishi wa Nchi  kombe la shirikisho Barani Afrika,"amesema Jaffary. 

Ameongezea  vijana wapo vizuri  isipokuwa katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao Danile Amor(Ghana)na  Yakubuku Mohamedi ambao ni majeruhi pamoja na Yahya Zayd aliyeitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.

USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA

$
0
0
*Ni kwa ajili ya kupata kazi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta Tanzania-Uganda

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaESA) umetangaza kuanza kwa mchakato wa utambuzi wa Watanzania wenye taaluma na ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi ambapo mwisho wa usajili ni Machi 30 mwaka huu.

Mchakato wa utambuzi huo ni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga nchini.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Boniface Chandaruba amesema kuwa ili kuhakikisha Watanzania wengi wananuifaka na fursa za ajira zitokanazo na mradi wa bomba la mafuta TaESA imepewa jukumu la kuhamasisha wote wenye taaluma na ujuzi nchini katika sekta ya mafuta na gesi wajitokeze.

“Hivyo tunaomba Watanzania wenye sifa kuja kujisajili TaESA ili waweze kuingizwa kwenye kanzidata ya Wakala kwa lengo la kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi wa ujenzi wa bomba hilo.

“Usajili huu unafanyika bure ,hivyo tunasisitiza hakuna gharama yoyote itakayotozwa kwa Mtanzania yeyote atakayehitaji kusajiliwa.Maelezo ya kina kuhusu aina ya fursa za ajira zinazotegemewa kutolewa yanapatikana katika tovuti ya Wakala ya www.taesa.go.tz,”amesema .

Chandaruba amesema mchakato wa usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalum ambazo zinapatikana kupitia tovuti ya Wakala au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizopo Dar es Salaam,Arusha, Dodoma na Mwanza.Pia amesema fumu hizo zinapatikana kwa barua pepe eacop@taesa.go.tz na kwamba mchakato wa usajili unatarajia kumalizika Machi 30 mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TaESA Boniface Chandaruba

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI ATENGULIWA

$
0
0
Aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Marekani Tillerson Rex 

Na Ripota Wetu
RAIS  wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Nje nchini humo Tillerson Rex na nafasi yake kuchukuliwa na Mike Pompeo.

Kupitia ukurasa wake wake Twitter Trump amesema Waziri Mteule wa Mambo ya Nje atafanya kazi nzuri na Tillerson hajui sababu ya yeye kuondolewa katika nafasi hiyo licha ya vyombo mbalimbali kuripoti kuwa ni sababu binafsi baina yake na Rais huyo.

Ikumbukwe tangu Trump aingie madarakani viongozi wengi wameachia ngazi zao wakiwemo washauri na viongozi wa masuala ya ulinzi na usalama katika ikulu ya marekani.

Waziri mteule Mike pompeo kabla ya uteuzi huu alikua Mkurugenzi wa Shirika la ujasusi nchini Marekani na ifahamike kwamba uteuzi huu umekuja katika kipindi cha maandalizi ya mkutano baina ya Donald Trump na Rais wa korea kaskazini Kim Jong Un aliyeomba kukutana na Trump mapema Mei mwaka huu.

POLEPOLE AWASHAURI WARATIBU TASAF KUSHIRIKISHA WATALAAM WA ARDHI ILI KUWA NA MIRADI ENDELEVU

$
0
0

 Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amewashauri Wasimamizi na waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini( TASAF) kushirikiana na viongozi wa vijiji na wataalamu wa aridhi kuanzishisha miradi itakayokuwa endelevu ambayo itakawaondoa haraka wanufaika wa mfuko huo.

Polepole ametoa kauli hiyo jana akiwa kwenye ziara yake ya mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea wanufaika wa TASAF katika Kijijji cha Nyabitaka wilayani Kibondo mkoani Kigoma.Alipata nafasi ya Shamba darasa lenye hekari mbili la kilimo cha mseto kinachosimamiwa na wanufaika hao.

Polepole amewashauri waratibu wa TASAF kushirikiana na watalaamu wa aridhi na viongozi wa vijiji kutenga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya wanufaika badala ya kuwapatia Sh.40,000 kwa kila mwezi.

"Wasikisimamiwa vema kwenye kilimo watapiga hatua za kimaendeleo haraka zaidi na baada ya mwaka mmoja wanafuika hao hawatakuwa masikini tena.Hivyo ni vema mkaangalia mbinu sahihi za kuwaondoa wanufaika hawa kwenye umasikini,"amesema Polepole.

Amesema Serikali ya CCM imeandaa mpango huu wa maendeleo kwa ajili ya kunusuru kaya masikini na lengo ikiwa ni kuwainua watu watoke kwenye umasikini uliopitiliza na kufafanua mwaka 2025 mpango huo wa TASAF utakwisha endapo utamalizika na wananchi hawajapatiwa miradi ya kujikwamua na umasikini itakuwa haijasaidia chochote.

Amewaahidi wananchi wilayani Kibondo kuwa Serikali ya Awamu ya tano ya CCM itatoa Sh.milioni 52 kwa ajili ya wananchi wakopeshwe kwa lengo la kuwaondoa kwenye umasikini na kuwaomba watendaji na wenyeviti wa vijiji kuandaa utaratibu bora wa kuwakopesha Wananchi hao kwa utaratibu mzuri.

Kwa upande wa Mratibu wa TASAF mkoani Kigoma Jailos Pilla aMEsema utaratibu wa mfuko huo ni kuwa Wanufaika kubuni mradi wa maendeleo.Hivyo baada ya kubuni mradi na kuwezeshwa na TASAF baadae mradi unakuwa mali ya Serikali ya kijiji.

Amesema kila mnufaika anatakiwa kujifunza kupitia miradi hiyo inayoanzishwa ili aweze kuanzisha nyumbani kwake ili ajikwamue katika umasikini.Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Lucia Mihayo amesema fedha alizozipata alizitumia kununa tofali na bati na mpaka sasa ameanza ujenzi wa nyumba ya bati ili aishi vizuri yeye na familia yake.

MWANAJESHI ANAYETUHUMIWA KUUMUA MWANAJESHI MWENZAKE AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU AKIWA KWENYE GARI YA WAGONJWA

$
0
0
 Mwanajeshi MT  Private Ramadhan Mlaku (28) akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu tuhuma za mauaji ya askari mwenzake MT 79512 SGT Saimon Munyama.
Mwanajeshi MT  Private Ramadhan Mlaku (28) akisaidiwa kushuka katika gari la wagonjwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu tuhuma za mauaji ya askari mwenzake MT 79512 SGT Saimon Munyama.

Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.
MWANAJESHI MT  Private Ramadhan Mlaku (28) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa juu ya kitanda cha wagonjwa kujibu tuhuma za mauaji ya askari mwenzake MT 79512 SGT Saimon Munyama.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo, saa tano asubuhi akiwa na katika gari la kubebea wagonjwa ambapo alikaa kwenye gari hilo kwa takribani saa moja hadi pale ilipotimu saa sita mchana akashushwa akiwa ndani ya gari akiwa amebebwa kwenye kitanda cha wagonjwa na kupelekwa katika chumba cha Mawakili wa Serikali ambapo alisomewa shtaka lake la mauaji linalomkabili.

Akisomewa shtaka na  Wakili wa Serikali, Mosii Kaima mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba imedaiwa Oktoba 30, mwaka jana mshtakiwa Mlaku ambaye ni Mwanajeshi wa Kambi ya Jeshi la Makongo, akiwa Makao Mkuu ya JWTZ Upanga Ilala Dar es Salaam alimuua askari mwenzie MT 79512 SGT Munyama.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu  chochote mahakamani hapo kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi za mauaji ambazo kwa kawaida zinasikilizwa Mahakama kuu.

Aidha mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kuwa kosa la mauaji linalomkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika huku Hakimu Simba akiutaka upande wa mashtaka kujitahidi kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo mapema.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kusomewa shtaka lake,  mshtakiwa huyo alipandishwa tena katika gari la Jeshi la wagonjwa ambalo lilimleta mahakamani hapo kwa ajili ya kupelekwa mahabusu.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA

$
0
0
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA KM 422 KATIKA ENEO LA IHUMWA NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika uwekaji wa jiwe la msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ya umeme kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa,  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wabunge waliofika kwenye uzinduzi wa Reli hiyo ya Kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Reli hio ya Kisasa katika eneo la Ihumwa Stesheni mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru madereva wa magari yatakayofanya kazi ya ujenzi wa reli hiyo ya kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.
 Sehemu ya wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.
  Treni ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika eneo la Ihumwa Stesheni kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi huo wa Reli ya kisasa ya umeme kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli PICHA NA IKULU

SEKRETARIETI YA TFF YAMPELEKA MICHAEL WAMBURA KAMATI YA MAADILI

$
0
0
KAMATI ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF inakutana leo Jumatano Machi 14,2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura aliyefikishwa kwenye kamati hiyo kwa masuala ya kimaadili.

Shauri hilo la Wambura limefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.

Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.

Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili baadaye leo na ana hiyari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo,kutuma kwa maandishi,kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.

Makosa anayoshtakiwa Wambura ni
1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013

2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013

3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)


AMMY NINJE KOCHA NGORONGORO HEROES
KOCHA Ammy Ninje ameteuliwa kuwa Kocha wa muda wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes)

Ninje atakiongoza kikosi hicho kwakuwa Kim Poulsen na Oscar Mirambo wamebaki na majukumu na kikosi cha Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys kinachojiandaa na mashindano ya Cecafa yatakayoanza Aprili 1-15,2018 nchini Burundi.

Kocha Ninje atakiongoza kikosi cha Ngorongoro Heroes kuanzia kwenye mechi zake za Kirafiki za Kimataifa dhidi ya Morocco Machi 17,2018,dhidi ya Msumbuji Machi 21,2018 na mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Vijana chini ya miaka 20 dhidi ya DR Congo zote zikichezwa Uwanja wa Taifa.

Mshindi kati ya Tanzania na DR Congo atakwenda kucheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa mwezi Mei.

Awali Ninje alikuwa kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya wakubwa Taifa Stars ambapo pia alikuwa kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika nchini Kenya.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF.

WATU NANE WANASHIKILIWA NA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI NYAMAGANA.

$
0
0
KWAMBA TAREHE 13.03.2018 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI KATIKA MTAA WA MABATINI KUSINI KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU NANE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.DEUS LUCAS, MIAKA 52, DIWANI WA KATA YA MABATINI - CHADEMA, 2. DANIEL MONGO, MIAKA 46, MWENYEKITI CHADEMA TAWI LA KILOLELI B”, 3. LAURENCE CHILO, MIAKA 21, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI, 4.LAMECK KAUNDA, MIAKA 38, MKAZI WA KILOLELI B, 5.JACKSON MADEBE, MIAKA 44, MKAZI WA MTAA WA MWANANCHI, 6.BI SECILIA BUTUKO, MIAKA 4O, MKAZI WA MTAA BUGARIKA, 7.MWITA SAGALI, MIAKA 38, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA NA 8.SELEMAN GABRIEL, MIAKA 45, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA TOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU LIPO KUNDI LA WATU KATI YA 200 NA 500, WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) WAMEKUSANYIKA KATIKA NYUMBA ALIPOPANGA BWANA LAURENCE CHILO, HUKU WAKIWA WAMEFUNGA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA SPIKA ZA MATANGAZO. HUKU WANACHAMA  HAO WA CHADEMA WAKIDAI KUWA WAMEKWENDA KUMUHANI MWANACHAMA MWENZAO BWANA LAURENCE CHILO ALIYEPATWA NA MSIBA WA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI MIEZI SITA ILIYOPITA KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KISHA KWENDA KUZIKA NYUMBANI KWAO UTEGI WILAYANI TARIME MKOANI MARA MWAKA JANA.

AIDHA BADAE ILIDAIWA KUWA JAMBO LILILOKUWA LIKIENDELEA KATIKA KIKAO HICHO NI UGAWAJI WA KADI ZA CHAMA, KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA NA KUTOA HOTUBA. ASKARI WALIFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO KISHA KUWAITA VIONGOZI NA  KUONGEA NAO ILI KUWEZA KUFAHAMU UHALALI WA KIKAO HICHO NDIPO GHAFLA WALIANZA KURUSHA MAWE KWA ASKARI. ASKARI WALIWEZA KUJIHAMI VIZURI KISHA WALIFYATUA MABOMU YA MACHOZI HEWANI KUWATAWANYA NA BAADAE WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WAFUASI NANE TAJWA HAPO JUU  WA CHAMA HICHO.

KATIKA ENEO LA TUKIO KUMEPATIKANA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, KADI ZA CHADEMA ZILIZOANDIKWA MAJINA NUSU, KADI ZA CHADEMA AMBAZO HAZIJAANDIKWA MAJINA NA KADI ZILIZOANDIKWA MAJINA, MIHURI MIWILI, KARATASI TATU ZENYE MAJINA YA MAHUDHURIO NA T-SHIRT ZENYE NEMBO YA CHADEMA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMNI. UFATILIAJI WA KUHAKIKISHA MJI UNAKUWA SHWARI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA ONYO KWA VIONGOZI WA SIASA NA WANACHAMA WAO KWA UJUMLA AKIWATAKA KUACHA TABIA  ZA HOVYO AMBAZO ZIPO KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI ZENYE LENGO LA KUONDOA UTULIVU KATIKA MKOA WETU.

 KWANI SUALA HILO HALIKUBALIKI NA TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI. PIA EMEOMBA WANANCHI WAELEWE KUWA AMANI NA UTULIVU NA USALAMA MKOANI KWENTU NA NCHI YETU KWA UJUMLA NI JAMBO LA MSINGI.

 BILA UTULIVU, AMANI NA USALAMA HAKUTAKUWEPO NA SHUGHULI YEYOTE YA MAENDELEO ITAKAYOFANYIKA KWA HIYO TUEPUKE WALE WOTE WANAOSHAWISHI VURUGU/FUJO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU WA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

KILIMANJARO SAR LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA HOSPTALI YA ST JOSEPH KUTOA HUDUMA KWA WATALII WALIOPATA MATATIZO MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .

SEKTA ya Utalii nchini imepata suluhu ya Changamoto ya muda mrefu ya utoaji wa msaada wa kitabibu, utafutaji na uokoaji wa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru .

Changamoto hiyo inafika kikomo rasmi baada ya kampuni ya Kilimanjaro SAR kuzindua Kliniki ya kwanza Afrika ya magonjwa yatokanayo na muinuko wa juu pamoja na utumiaji wa Helkopta kwa ajili ya uokoaji katika Hifadhi za Mlima Kilimanjarona Mlima Meru.

Mbali na uzinduzi huo Kilimanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi ,kuanza kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa watakao pata matatizo wakati wa kupanda Milima hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni ya Kilimanjaro SAR na Hospitali ya St Joseph ,Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba aliyekuwa mgeni rasmi amesema hii ni fursa mpya kwa sekta ya Utalii kuutangaza vyema Mlima Kilimanjaro.

Huduma hii ya kwanza kutolewa barani Afrika inaiweka Tanzania katika nafasi ya pili katika Ramani ya Dunia, kuwa  na kliniki ya kipekee katika utoaji wa huduma kwa wapanda Mlima na kwamba kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuongeza idadi ya Watalii. 

Hata hivyo kuanza kwa huduma hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini ,bado ipo changamoto ya matumizi ya uwanja mdogo wa ndege wa Moshi hali inayowalazimu kutumia uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Ulbanie Lyimo ni mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph akaeleza faida itakayopatikana kutokana na kuingia makubaliano na kampuni hiyo ya Uokoaji ya Kilimanjaro SAR kuongeza maarifa katika utoaji wa matibabu kutoka kwa madaktari wa kigeni watakao hudumia wagonjwa wa Mlimani.

Kuanza kwa kliniki hii ni msaada kwa maiha ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro na Meru ikizingatiwa asilimia 75 ya magonjwa uwapo mlimani yanatokana na mbadiliko ya Hali ya Hewa kulingana na urefu wa Mlima.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun akitia saini makubaliano ya Mashirikiano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi kuhusu uanzishwaji wa Kliniki ya utoaji matibabu kwa Wagonjwa wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (aliyesimama kulia) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Amour Abdallah.

Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Kippi Warioba na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini .

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

VILABU LIGI KUU VYASHAURIWA KUWEKEZA KWA KUWA NA TIMU ZA WACHEZAJI WA UNDER 20

$
0
0
Na Agnes Francis,Globu ya jamii

VILABU vya soka vinavyoshiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara vimeshauriwa kuhakikisha wanawekeza kwenye timu za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (Under 20). 

Kwani kuna umuhimu mkubwa kwa vilabu hivyo kuwekeza kwa wachezaji wenye umri huo.Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga ambapo amesisitiza ni muhimu kwa vilabu kuwa na timu za Under 20.

Ameipongeza timu ya Mbao ambayo imeonesha kuwekeza katika Academy ya vijana wanasoka under 20 na amewataka timu zingine kuiga mfano huo."Naipongeza timu ya Mbao kwa kuwa na utamaduni wa kuhakikisha timu ya wachezaji wenye chini ya miaka 20 wanaisimamia vema.

" Mbao kwenye mechi zao nyingi wanatembea na wachezaji wao wa Under 20 na kwenye mechi za kirafiki wamekuwa wakiwatumia na lengo nikuwajengea uwezo na uzoefu mapema,"amesema Jaffary Idd Maganga.Ameongeza wakati Mbao inawekeza kwa wachezaji vijana kwa vitendo,vilabu vingine bado havijaamua kuandaa wachezaji kupitia wachezaji wenye umri mdogo walionao.

Amefafanua vilabu vingi wanaandaa timu za Under 20 pindi wanapoona kuna mashindano mbeleni ndio utaona wanaandaa vijana."Na hili si jambo Zuri, tuwe na utamaduni wa kuanzisha Academy katika vilabu vyetu," amesisitiza Jaffary. 

Amesema timu yao imefanikiwa kutoa wacheza watano kuungana na kikosi cha Timu ya Taifa vijana chini ya umri wa miaka 20 (Under 20). "Mwalimu wa kikosi cha Timu ya Taifa chini ya Umri miaka 20 (under20) Salum Mayanja ameona uwezo wa vijana wetu walivyo na uwezo wa hali ya juu mpaka imemfanya kuita vijana 5 kutoka kwenye Academy yetu kujiunga na kikosi hicho.

"Vijana hao ni Rajab Odasi, Paulo Peter, Mohammed Mussa, Osca Masai pamoja na Lusajo Mwaikenda,"amesema Jaffary
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images