Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MTI WA MBUYU ULIOISHI KWA ZAIDI YA MIAKA 100 WAANGUKA MAENEO YA OCEAN ROAD JIJINI DAR

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
KISHINDO kikubwa kimesikika katika maeneo ya barabara ya Chimala karibu na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam baada ya mti wa mbuyu uliopo ndani ya uzio wa hospitali hiyo unaodaiwa kuishi zaidi ya miaka 100 kuanguka.
Mbuyu huo umeanguka leo majira ya saa kumi alasiri na kusababisha kukatika kwa nishati ya umeme katika maeneo hayo ya hospitali ya Ocean Road, na pia umesababisha pia sehemu ya uzio wa hospitali hiyo kuvunjika.
Hata hivyo licha kuanguka na kufunga barabara ambayo imekuwa mara nyingi ikitumika kupitisha magari ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali, wakati huo hakukua na gari ya aina yoyote iliyokuwa inapita. Hivyo hakukuwa na madhara zaidi ya kubomolewa kwa uzio wa Hispitali ya Ocean Road.
Baadhi ya mashuhuda wakati mbuyu huo unaanguka wamedai kabla ya kuuanguka ulianza upepo mkali ulioutikisa.Pia inaelezwa dalili za kuanguka kwa Mbuyu huo ulianza tangu jana mchana baada ya kupiga radi wakati wa  mvua kubwa iliyonyesha. Baada ya radi hiyo waliabini mzizi wa Mbuyu huo kukatika na matokeo yake ukawa umeelemewa na hivyo ilipofika leo tisa Alasiri ndipo ukaanguka. 
Mafundi wa Umeme wa Tanesco wa kikosi cha dharura walifika na kuerekebisha mambo chap chap, na kuwezesha umeme kuendelea kuwaka baada ya kuuzima kwa muda.
Mashuhuda hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao wamedai walishtuka baada ya kusikia kishindo kikubwa wakati Mbuyu ukiwa  unaanguka na kusababisha mlipuko mkubwa wa umeme kutokana na  kukatika kwa nyaza za umeme zinazopita eneo hilo.
"Tunashukuru Mungu maana licha ya ukubwa wa mbuyu huu wakati unaanguka hakukuwa na mtu yoyote aliyekuwa anapita barabarani eneo hilo bali kuna gari moja ndogo ndiyo ilikuwa inapita lakini hata hivyo baada ya kupita eneo hilo ndipo mbuyu ukaanguka.
"Hivyo hakuna madhara yoyote ambayo yametokea zaidi ya kukatika umeme na sehemu ya uzio wa ukuta wa Ocean Road kubomoka,"amesema mmoja wa mashuhuda wakati anaielezea Michuzi Blogu ambayo waandishi wake walifika eneo la tukio kushuhudia kuanguka kwa mti huo unaodaiwa kuishi miaka zaidi ya 100.
 Mti wa Mbuyu wenye miaka zaidi ya 100 ukiwa umeanguka na kufunga barababra ya Chimala na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara pamoja na nishati ya Umeme leo  karibu na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi wakiangalia Mbuyu ulioanguka kufunga mawasiliano ya barabara inayotumiwa na viongozi wa wakuu wa serikalini ulioanguka leo jijini Dar es Salaam.

Mafundi wa Umeme wa Tanesco wakiwa katika eneo ulioanguka Mbuyu ambao ulifanya hitilafu ya nyaya za umeme leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka)

Kumbilamoto afunga michezo ya mpira wa pete ya mkoa wa Dar es Salaam

$
0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Vingunguti ambayo imeingia fainali katika michezo ya mpira wa pete ya mkoa wa Dar es Salaam iliyoratibiwa na (CHANEDA) kwa ajili ya kupata timu wawakilishi wa mkoa huu.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Mbagala ambapo timu hiyo nayo ilifika hatua ya fainali kwa ajili ya kupata mshinddi atakaye wakilisha Mkoa wa Dar es Salaam katika Mashindano ya Afrika Mashariki.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na Timu zote mbili kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kw atimu zilizoshiriki ligi ya mkoa wa Dar es Salaam
 Timu za Mchezo wa mpira wa Pete kwa wanaume zikimenyana wakati wa mchezo wa fainali ya mkoa wa Dar es Salaam
Mashabiki wakifatilia michezo fainali ya mpira wa pete wa Wanaume kwa mkoa wa Dar es Salaam.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. MPANGO AWASILISHA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI 2018/2019

$
0
0

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango  (Mb)   akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma.
 Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango  (Mb)  (katikati) akisikiliza jambo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni, nje ya Bunge baada ya mawasilisho ya Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma.
Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni (kushoto) akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) baada ya kuwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango

Habari za UN: Ukatili na unyanyasaji wa kingono marufuku UN - Ripoti, na mengineyo

VOA Swahili: Duniani Leo 13th March 2018

UN YAJITOSA KUWASAIDIA MAAFISA HABARI WA SERIKALI

$
0
0
Na.Vero.Ignatus Arusha.
Umoja wa mataifa umekubali kuingia makubaliano na Serikali ya Tanzania kupitia chama cha maafisa habari na mawasiliano na wa Serikali na uhusiani TAGCO katika sekta ya habari ambapo mkataba huo utatoa nafasi kwa wanahabari kutembelea na kuitangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.
Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amesema UN ni mshiriki mwenza wa maswala ya maendeleo kwahiyo kwao mkutano kama huo ni muhimu ambapo shirika la maendeleo la umoja wa Kimataifa (UNDP) ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa malengo ya dunia kwa miaka miwili iliopita ili kufanikisha malengo hayo kwa miaka 13 ijayo.
Amesema kuwa Umoja wa Mataifa kupitia wanamawasiliano wake kwa kushirikiana na serikali wanaweza kuijua Tanzania ya viwanda Tanzania ya maendeleo ,hivyo basi wataonyesha matokeo chanya yanayofanywa na serikali ambapo wapo tayari kufanikisha malengo yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti chama cha maafisa wa habari na mawasilianao na uhusiano serikalini Pascal Shelutete amesema kusainiwa kwa mkataba huo kutatoa fursa ya malengo yaliopo baina ya serikali ya Tanzania na umoja wa mataifa yanatekelezwa kwa wakati huku
Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ambapo pia ni msemaji mkuu wa serikali Dkt Hasan Abbas amesema mkataba huo na utawawezesha maafisa habari kutekeleza kwa haraka malengo 17 ya milenia .Dkt Abbas amesema kuwa  kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa inaandaaa mradi wa maendeleo inayotekelezwa chini ya malengo ya mileniamu

Amesema hata hivyo wapo katika hatua za awali a mazungumzo na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDPj).ambapo mradi huo utakuwa na manufaa kwa waandishi wa habari na serikali itaona ile miradi ambayo ilikuwa haijulikani na wananchi sasa itaonekana  kwa ushirikiano huu utaibua miradi hiyo.

Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez
Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa Simba katika Kituo cha Kimataifa AICC Jijiji Arusha.

MALIKIA WA NYIMBO ZA INJILI ROSE MUHANDO ATHIBITISHA KUZINDUA ALBAMU YAKE MPYA TAMASHA LA PASAKA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Malkia wa nyimbo za Injili hapa nchini,Rose Muhando ametihitisha kushiriki  tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Aprili 2 kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi Mkoani Simiyu. 

Akizungumza hivi karibuni wakati wa maandalizi yake,Rose Muhando amesema yuko tayari kwa kazi ya kuburudisha katika tamasha hilo ambapo pia atazindua albam yake yenye jumla ya nyimbo saba,itakayojulikana kwa kwa jina la “Usivunjike Moyo” .

Katika Tamasha hilo Kiingilio kimepangwa kuwa, watu wazima ni  shilingi Elfu 5000 na watoto itakuwa ni shilingi 2000 na Kiingilio katika tamasha la Pasaka mkoani Simiyu watu wazima itakuwa ni shilingi 3000 na watoto ni shilingi 2000.

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA BALOZI WA UFARANSA NA MKURUGENZI MKAZI WFP

$
0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ufaransa nchini Mhe. Frederic Clavier ambaye aliongozana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Emmanuel Baudran.

Katika mazungumzo hayo ambayo yamefanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Clavier amewasilisha salaam za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kusema “Rais wa Ufaransa ana uhakika na Tanzania ijayo na anaunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli”

Balozi huyo mpya wa Ufaransa nchini ambaye amekutana na kuzungumza na Mheshimiwa Makamu wa Rais aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika masuala mbali mbali ya Kimataifa na kusema “Tanzania ni nchi yenye utulivu na Amani kitu ambacho kinaipa taswira nzuri Umoja wa Mataifa”.

Mhe. Balozi amemjulisha Makamu wa Rais kwamba Ufaransa imekusudia kuimarisha uhusiano zaidi na Tanzania wa Uchumi na Siasa na kuanzisha majadiliano mbali mbali katika masuala ya Mazingira,Mabadiliko ya Tabia Nchi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Frédéric CLAVIER aliyemtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Frédéric CLAVIER ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani(WFP) hapa nchini Bw. Michael Dunford ambaye alifika ofisni kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani(WFP) hapa nchini Bw. Michael Dunford ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU GEITA

$
0
0
Na Joel Maduka,Geita

Mkoa wa Geita unatarajia kunufaika na mradi kabambe wa usambazaji umeme vijijini REA awamu ya Tatu kwa kuongeza shughuli za kiuchumi kwa wananchi kutokana na vitongoji 220, vijiji 372 na Kata 499 ambazo zinatarajia kunuifaika na Nishati ya Umeme.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta amesema Mradi huo kwa mzunguko wa kwanza utaunganisha wateja wapatao 12,944 na hivyo kukamilika kwa Mradi huo utafanya umeme kuongezeka kwa Asilimia 51 kwa wateja waliopo sasa.

“Mategemeo yetu ni kwamba mzunguko wa pili ambao unatarajia kuanza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2020 na 2021 utafanya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita kupata umeme kwa asilimia mia moja” Alisema Ruweta.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kujua kuwa hakuna fidia ambazo watalipwa kutokana na mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA baada ya kufika kwenye ofisi yake . 
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita, 
Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda akimashukuru Mkuu wa Mkoa baada ya kutembelea miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwenye Wilaya za Bukombe pamoja na Chato. 
Meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta ,Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya Tatu kwenye baadhi ya maeneo. 

Barclays Tanzania marks the International Women's Day

$
0
0
 Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (right), addresses some of the bank’s female staff during the function to mark the International Women’s Day in Dar es Salaam over the weekend.
 Barclays Bank CIB Sales, Naomi Mafwiri Rhubera (left), gives a testimony during a function hosted by Barclays for its female staff members to observe this year’s International Women’s Day in Dar es Salaam last weekend.
 Jubilation soars as some Barclays female staff members cut a cake during the ceremony to commemorate the International Women’s Day in Dar es Salaam over the weekend.

 A cross section of Barclays Bank Tanzania workers who took part in the ceremony.
 Barclays Bank Tanzania Citizenship Manager, Hellen Siria (right,) gives a word of encouragement to her fellow workmates at a function hosted by Barclays in Dar es Salaam last week.
It is time to take the festive mood to the dancing floor during the function hosted by Barclays for its female staff in celebration of the International Women’s Day in Dar es Salaam last week,

KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA WA MAPATO TANZANIA AKUTANA NA MAKAMU KAMISHNA WA IDARA YA FORODHA KOREA

$
0
0


  TRA 8
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akisisitiza jambo wakati alipokutana na Makamu Kamishna wa Idara ya Huduma za Forodha Korea, Roh Suk-Hwan (kushoto) pamoja na ujumbe wake jijini Dar es Salaam ili kujadili maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Idara hiyo, ikiwemo Mfumo wa Uondoshaji Mizigo Bandarini (TANCIS) na dirisha moja (Single Window System).  

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

DC SINYAMULE AAGIZA MTENDAJI KATA YA BOMBO AWEKWE NDANI SAA NANE

$
0
0
Na Ripota wetu, Same

Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule ameagiza wa Kata ya Bombo awekwe ndani chini ya ulinzi mkali kwa saa 8 kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari Bombo na kumtaka apewa siku 2 kuleta maelezo kwa nini asichukuliwe hatua.

Dc Sinyamule, amefikia uamuzi huo mara baada ya wataalamu wa kutaka hela za kujenga bweni la Shule ya sekondari ya Bombo zihamishiwe shule nyingine kutokana na wananachi wa kata ya Bombo kutotoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha ujenzi wa bweni hilo unakamilka.

"Fedha za serikali ( P4R) zilipelekwa tangu mapema 2017 na mradi ulitakiwa kuisha Nov. 2017 na Ikitegemewa kuwa kuanzia hapo ujenzi wa bweni uanze na mpaka leo nimefika hapa March 2018 bado hata msingi haujakamilika kujengwa na kutoa sababu zisizo na tija.

Mtendaji huyu ameshindw akusimamia Vizuri majukumu yake ya kuhamasisha watu kushiriki katika miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa bweni la shule hii ambayo serikali ilishatoa fedha kilichotakiwa ni nguvu ya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akikagua Msingi wa Bweni la Shule ya Sekondari Bombo Wialayani hapo ambao umekwama tangu 2017 kutokana na Wananchi kushindw akujitokeza kuchangia ujenzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akikagua, akiwa ameongozana na Wataalamu kutoka Wilayani kukagua Madarasa yaliyojengwa tangu 2017 bila kukamilika.

TAZAMA JINSI SIMU YA MKONONI INAVYOBADILISHA MAISHA YA MAELFU NCHINI TANZANIA.

$
0
0
Je wajua yakuwa unaweza baadilisha maisha na mtandao wa simu? Hebu angalia video hii kujua wengine wamefanyaje?




KIWANDA CHA CHUMVI KUNUFAISHA HANANG

$
0
0
Wananchi wanaozunguka mgodi wa madini ya chumvi ya Gendabi Wilayani Hanang' wanatarajia kunufaika na rasilimali hiyo, baada ya Serikali kupata mwekezaji atakayejenga kiwanda cha chumvi eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza jana kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano wilayani humo alisema atawachukulia hatua kali wanasiasa watakaokwamisha mradi huo. Mnyeti alisema wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia matatizo ya wananchi kuwa fursa hivyo hawezi kukubali wakwamishe mradi huo mkubwa wenye faida kwa jamii.

"Nimesikia hapa kuna baadhi ya wanasiasa wanatumia shida za watu kujinufaisha kisiasa, sasa nikimkuta anapinga hili nitamshughulikia bila kujali chama chake,," alisema Mnyeti. Alisema kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji hivyo wananchi wa eneo hilo wajiandae kunufaika kiuchumi kwa kuchimba chumvi kwa wingi na kuuza kiwandani hapo.

"Haya ndiyo maendeleo tunayosema siyo siasa za maji taka kwani chumvi itakuwa na thamani kubwa tofauti na hivi sasa kwani kiwanda kitawanufaisha," alisema Mnyeti. Aliwataka wananchi wa eneo hilo kujiweka tayari na uwekezaji huo ili kuhakikisha uzalishaji unafanyika wa kutosha kwani soko la uhakiki litakuwepo kwa kadiri watakavyofanya uzalishaji.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akiangalia kiatu kilichotengenezwa na kikundi cha Datoga cha Wilayani Hanang kinachotengenezwa vifaa vinavyotokana usindikaji wa ngozi.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akipokea heshima kutoka kwa skauti mara baada ya kuwasili Wilayani Hanang jana alipoanza ziara ya siku tano, ya kutembelea wilaya hiyo kwa kuzungumza na wananchi, kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero zao. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, (kushoto) akizungumza jana kwenye eneo la kuhifadhi dawa baada ya kukagua mazingira ya hospitali ya Wilaya ya Hanang kwenye ziara yake ya siku tano.  



DKT . HASSAN ABASS AZINDUA TOVUTI YA MISA TANZANIA, JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto) wakizindua rasmi Tovuti ya MISA Tanzania inayopatikana hapa www.tanzania.misa.org
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto)pamoja na wadau mbalimbali ambao hawapo pichani wakipata maelezo kuhusiana na Tovuti ya MISA Tanzania kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa
Sengiyumva ambaye hayupo pichani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva(kulia) kulia akiendelea kutoa maelezo mbali mbali na vitu ambavyo vinapatikana katika Tovuti ya MISA Tanzania 
 Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Tovuti ya MISA Tanzania Jijini Arusha.

UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo

$
0
0
UMOJA wa Mataifa umeingia makubaliano ya kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa habari za maendeleo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO).

Makubaliano hayo yamelenga kuimarisha upatikanaji na utoaji habari wa pamoja kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa serikali na malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.

Kwa mujibu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez  makubaliano hayo yatachagiza kupatikana kwa habari kuhusiana na utekelezaji  wa malengo ya maendeleo endelevu unaokwenda sambamba na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa Tanzania.

Akizungumzia malengo hayo kwa maofisa wa mawasiliano wa serikali wanaokutana mjini Arusha kwa semina ya wiki moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya TAGCO na Wizara ya Habari na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa, alisisitiza kuwa malengo hayo yanahitaji kuwasilishwa kwa wananchi na pia kupigiwa chapuo.
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akiwasilisha mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Ofisa Habari wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru akiuliza namna ambavyo mapambano dhidi ya rushwa yanavyoweza kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi (kulia) wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
 Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Maelezo Dk. Hassan Abbas akizungumza  na waandishi wa habari nje wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano ikiwasilishwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez hayupo pichani katika mkutano huo wa 14 unaoendelea jijini Arusha.

MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA YA KIWANGONA UKOMO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2018/19

IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII YAJIPANGA KIMKAKATI KUFANIKISHA MALENGO YA UTENDAJI

$
0
0
Na mwandishi wetu - WAMJJW, Dodoma 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii) imeendesha Mafunzo ya siku mbili kwa ajili ya kuimarisha utendaji na kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi, weledi na uadilifu katika Wizara hiyo.  
Mafunzo hayo siku mbili yanaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma yamejumuisha wajumbe wa Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa Ndani ya Wizara hiyo. Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ni Bwa. Alphonce Muro na Bw. Athanas Pius kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, katika Ofisi ya Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesisitizwa kuzingatia utatu (Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa ndani) katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakiki, kusimamia na kudhibiti utendaji mahali pa kazi ili kuongeza thamani ya huduma na kazi za kila upande katika kufanikisha malengo ya Wizara. Akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo mwezeshaji alisema, 
“Uhusiano na mawasiliano kati ya watendaji hao ni muhimu katika kufanikisha maelengo ya Wizara”.. amesema Bw. A. Muro  
Imeelezwa kuwa kila upande una wajibu wa msingi katika kuchangia kufikiwa kwa malengo ya Wizara, washiriki wamesisitizwa kuwa na mawasilino na kushirikiana katika kupokea na kutekeleza ushauri wa kitaalam unaotolewa na maafisa wa kitengo cha Ugaguzi na Kamati ya Ukaguzi wa Ndani kwa lengo la kuboresha utendaji na usimamizi.
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya uimarishaji na uboreshaji wa utendaji kazi mahali pa kazi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango- Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Alphonce Muro (aliyesimama) akitoa mada kwa wajumbe wa Menjimenti, Kamati ya Ukaguzi na Maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya  Jamii) wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma.    
 Baadhi ya washiriki wa Mafunzo Mkakati ya kuimarisha na kuboresha wa utendaji kazi mahali pa kazi katika Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya  Jamii) wakifuatilia mada ya majukumu ya Kamti ya Ukaguzi mahali pa akzi kutoka kwa mmoja wa wawezeshaji wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma.  
 Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marece Katemba (katikati) akifuatilia kwa makini mafunzo ya uimarishaji na uboreshaji wa utendaji kazi mahali pa kazi, wengine Bi. Georgina Edmundi Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara (kushoto) na Bi. Josephina Rusatila Mjumbe wa Kamati (kulia) wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.  
Mwezeshaji wa Mafunzo ya uimarishaji na uboreshaji wa utendaji kazi mahali pa kazi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango- Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Athanas Pius (aliyesimama) akitoa mada kwa wajumbe wa Menjimenti, Kamati ya Ukaguzi na Maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya  Jamii) wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma.    

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MADAKTARI WA CHAMA CHA MADAKTARI WA AFYA KINYWA,MENO WATOA HUDUMA YA AFYA BUHANGIJA SHINYANGA

$
0
0
Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr, Rashid Mfaume (wa tatu kushoto) akifungua  shughuli za uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno kwa watoto waliopo katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, Mkoani Shinyanga katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, Ambapo Kitaifa yatafanyika Machi 20, 2018,Tarime Mkoani Mara . Kuanzia kushoto ni Kiongozi wa msafara huo ambaye pia ni Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Arnold Mtenga, Mwalimu msaidizi wa kituo hicho, Mohamed Makana na kushoto kwa mgeni rasmi ni Daktari wa Meno Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya. (Picha na Khamis Mussa ) 
Mlezi Jackson Leonard (kushoto) na Mlezi Flora Kankutebe wakifatilia jambo wakati watoto hao walipokuwa wakifanyiwa uchunguzi huku watoto wendine wakiwa katika msitari wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Mwalimu msaidizi wa kituo hicho, Mohamed Makana akiwakaribisha wageni na kutoa utangulizi wa kituo hicho
Dakt. Bingwa wa Magonjwa ya Kinywa na Meno kwa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr, Conrad Mselle akionyesha kwa mfano namna nzuri ya upigaji mswaki kwa Zephania Bahebe mmoja kati ya watoto wanaoishi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, Mkoani Shinyanga katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, Ambapo Kitaifa yatafanyika Machi 20, 2018,Tarime Mkoani Mara.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images