Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Meli za TPA kuongeza biashara kati ya Tanzania, Malawi

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba akizungumza wakati akipokea kwa mara ya kwanza ujio wa meli nyingine ya TPA, MV Ruvuma katika bandari ya Monkey Bay nchini Malawi.

Na Mwandishi Wetu
KUANZA safari kwa meli za mizigo za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika nchi ya Malawi kutaongeza wigo wa kibiashara kati ya nchi ya Tanzania na Malawi.

Mbali ya kuongeza zaidi wigo wa biashara kati ya nchi hizo, meli hizo – MV Njombe na MV Ruvuma pia zinatarajiwa kuimarisha uchumi wa nchi zote mbili za Tanzania na Malawi.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba wakati akipokea kwa mara ya kwanza ujio wa meli nyingine ya TPA, MV Ruvuma katika bandari ya Monkey Bay nchini Malawi.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Balozi Mashiba amesema kwamba kama bidhaa zitafika Malawi au Tanzania kwa wakati na haraka na kwa unafuu zaidi.  Mheshimiwa Balozi aliendelea kueleza lwamba watumiaji wataongezeka na wakishaongezeka basi hata uzalishaji viwandani pia unaongezeka.

Kwa  upande wa Serikali zote mbili, nazo zitanufaika kwa kutoza kodi ambayo itaongeza mapato ya nchi, pia Balozi Mashimba ameongezea kwamba kwa kuwa viwanda hivi vinatumia malighafi kutoka mashambani, hii ina maana kwamba hata wakulima nao watanufaika.

Kwa Serikali zote mbili za Tanzania na Malawi, hilo ni jambo ambalo linalitajika kabisa, ili uchumi uendelee kukua na hatimaye wananchi wote waweze kunufaika na Serikali kwa maana ya kupata ushuru na tozo mbalimbali.

Naye Kaimu Naibu Mkuu Mkurugenzi upande wa Huduma wa TPA, Bibi Francisca Muindi amesema kwamba wao kama TPA wanawakaribisha sana wafanyabiashara wa nchini Malawi na Tanzania kutumia meli zote mbili za MV Ruvuma na Mv Njombe kwani ni nafuu na za uhakika zaidi kusafirisha bidhaa.

Amesema kwamba meli hizi mbili zitakuwa zikitumika kubeba mizigo si tu ya Tanzania na mikoa inayozuunguka ziwa hilo bali pia kupeleka mzigo Malawi na Msumbiji kwa bei nafuu zaidi, ikilinganishwa na usafiri wa aina nyingine, kama vlle barabara.

Hivyo, Bibi Muindi ametoa wito kwa wafanyabiashara wa nchi zote mbili kwamba badala ya kutumia barabara kupeleka mizigo yao nchini Malawi, watumie njia ya maji kwani ni ya uhakika, nafuu na haraka zaidi.

Ama kwa hakika, TPA ilieleza kwamba kwa kutumia meli hizo itawasaidia wafanyabiashara kunufaika kutokana na unafuu na usalama wa kusafirisha mizigo na hatimaye kuongeza faida kwenye biashara zao.  Jumuia za wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi zimehamsishwa kutumia meli hizo kwa faida ya Serikali za nchi zote na vile vile kwa faida ya wafanyabiashara ili kupunguza gharama za usafirishaji; na hatimaye walaji wa mwisho kuweza kupata mahitaji yao kwa bei nafuu.

Meneja Utekelezaji wa Kampuni ya Meli ya Malawi, Capt. Francis Chilalika, kwa upande wake amesema kwamba bidhaa ambazo huwa wanasafirisha mara kwa mara kutoka Tanzania kuja nchini Malawi ni ‘Clinker’.

‘Clinker’ ndiyo bidhaa iliyoletwa na meli ya MV Ruvuma nchini Malawi pamoja na shehena ya saruji kutoka kiwanda cha Saruji cha Mbeya kuja kiwanda cha Saruji cha Larfage nchini Malawi.

Nahodha huyo wa Kampuni ya Meli ya Malawi alisema, pamoja na ‘Clinker’, bidhaa nyingine ambazo zimekuwa zikisafirishwa sana kutoka nchini Tanzania kuja Malawi ni pamoja na saruji.  

“Tumekuwa tukihudumia shehena za namna tangu mwishoni mwa mwaka 2016 hadi sasa, kama ujuavyo Malawi tuna mahitaji makubwa sana ya saruji, hivyo hii kwetu tunaiona ni kama biashara endelevu,” amesema.

Akizungumzia bandari ya Chipoka ambayo imejaa mchanga kutokana na kina cha maji kupungua, Nahodha huyo amesema kwamba wapo katika mchakato wa kuichimba bandari hiyo.

Amesema kwamba kwa sasa wanafanya utafiti kujua ukubwa wa tatizo ili kujua makadirio ya gharama za  hatimaye kuandaa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa uchimbaji huo.

Bandari ya Chipoka ndiyo iliyo katika nafasi nzuri kwa upande wa usafirisha mizigo nchini Malawi haswa kwa mizigo inayokwenda mji wa Lilongwe.

Meli ya mizigo ya MV Ruvuma ambayo imebeba zaidi ya tani 900 za shehena ya saruji na ‘clinker’ kutoka bandari ya Kiwira, mjini Mbeya, imewasili salama na mapema katika bandari ya Monkey Bay nchini Malawi. 

Hii ni mara ya kwanza kwa meli ya MV Ruvuma kuleta mzigo nchini Malawi na ni mara ya pili kwa meli za TPA kuleta shehena ya mizigo nchini humo. 

Awali meli nyingine ya mizigo ya TPA yenye uwezo wa kubeba tani 1,000 pia iitwayo MV Njombe nayo ilileta shehena ya zaidi ya tani 800 za saruji katika bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi kwa mafanikio makubwa hali iliyowavutia wafanyabiashara wengine kutumia meli ya MV Ruvuma kuleta mzigo nchini Malawi kupitia bandari ya Monkey Bay.  

DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI MAKATIBU WAKUU NA NAIBU KATIBU WAKUU

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Shaaban Seif .Balozi Mohammed  kuwa    Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais   katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha    Bibi Khadija Bakari Juma  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha    Bw.Omar Hassaan Omar   kuwa Katibu Mkuu   Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo.
[Picha na Ikulu,] 13/03/2018. 

MEYA WA MANISAA YA ILALA AFUNGA MASHINDANO YA MPIRA WA PETE YA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Vingunguti ambayo imeingia fainali katika michezo ya mpira wa pete ya mkoa wa Dar es Salaam iliyoratibiwa na (CHANEDA) kwa ajili ya kupata timu wawakilishi wa mkoa huu.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Mbagala ambapo timu hiyo nayo ilifika hatua ya fainali kwa ajili ya kupata mshinddi atakaye wakilisha Mkoa wa Dar es Salaam katika Mashindano ya Afrika Mashariki.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na Timu zote mbili kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kw atimu zilizoshiriki ligi ya mkoa wa Dar es Salaam
 Timu za Mchezo wa mpira wa Pete kwa wanaume zikimenyana wakati wa mchezo wa fainali ya mkoa wa Dar es Salaam
Mashabiki wakifatilia michezo fainali ya mpira wa pete wa Wanaume kwa mkoa wa Dar es Salaam.

SPIKA WA BUNGE AFANYA UTEUZI WA WAJUMBE WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA NDUGU IBRAHIM WEREMA JOHN

$
0
0
Ni miaka mitano sasa toka ndugu yetu kipenzi Ibrahim Werema John ututoke tarehe 13. march 2013.



 Imekua ngumu kukusahau kwani Upendo, Ucheshi, Wema na Fadhila zako kwetu bado vinaishi nasi.      


                Unakumbukwa sana na mke wako kipenzi Bi. Agatha, wazazi wako Mr.& Mrs. John Keraryo, dada yako Anna, wadogo zako Israel, Simon, Sunday, Kulwa na Doto, mkwe wako mzee Soka, sehemeji zako ndugu, jamaa na marafiki.  


                       JINA LA BWANA LIPEWE SIFA.                                AMEN

MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI

$
0
0
Na Bashir Yakub.

Inaweza kuwa nyaraka muhimu kama hati ya nyumba, mkataba wa mauziano au mkataba mwingine wowote, wosia, kadi ya gari au ya mashine yoyote,hati ya kusimamia mirathi, cheti cha ndoa au vyeti vinginevyo, na nyaraka nyingine mbalimbali.

Nyaraka hii inaweza kuwa inatakiwa sehemu muhimu kama mahakamani ili kuthibitisha shauri au kesi yako. Na inaweza ikawa ni nyaraka ambayo kuwepo kwake ndio kushinda kwako na kutokuwepo kwake ndio kushindwa kwako.

Pamoja na umuhimu wa nyaraka hii bado umeitafuta kote pa kutafuta na hukuweza kuipata. Au hukuitafuta madhali tu unajua ilishapotea au iko mikononi mwa mtu ambaye hujui alipo na hawezi kupatikana. Katika mazingira ya namna hiyo makala yataeleza vitu vichache vinavyoweza kusaidia kutoka Sura ya sita,Sheria ya Ushahidi.

1. USHAHIDI WAKO.

Kitu kikubwa kinachomsaidia mtu kushinda kesi mahakamani ni ushahidi. Kadhalika kushindwa kwako pia ni ushahidi. Ukisema hiki kiwanja au nyumba ni yangu unatakiwa kuonesha hati au mkataba wa mauziano au vyote viwili.

Ukisema hili gari ni langu kadhalika uoneshe kadi yenye jina lako ama vinginevyo. Ukisema nilikuwa na ndoa halali uoneshe cheti cha ndoa ama vinginevyo. Ukisema nilimuuzia au kununua kitu fulani uoneshe mkataba ama risiti,vivyo hivyo nk, nk.

Hakimu au Jaji si mtu ambaye anakuwa eneo la tukio na hivyo kuwa katika nafasi ya kujua nini kilitokea huko. Yeye hajui chochote kilichotokea na hivyo taarifa zote anazipata kwenu mnaoshitakiana. Kwa msingi huu yupo katika wakati mgumu kuamua nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi kwa kitu ambacho hakushuhudia na hakijui.

Kama hivi ndivyo kitu pekee cha kumuongoza hakimu/jaji huyu ambaye hakuwepo wakati mnadhulumiana, ni ushahidi wa kila mmoja atakaowasilisha. Hataangalia suraya mtu, kulia machozi kwa mtu, kuongea kwa kujiamini au kwa unyonge kwa mtu, umri wa mtu, rangi ya mtu,wala jinsia, bali ushahidi ulio uliowasilishwa na mtu.

RIDHIWANI-VITUO VYA AFYA CHALINZE HAVINA VYUMBA VYA KUHIFADHIA MAITI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,ameweka wazi kuwa vituo vya afya katika jimbo hilo vinakabiliwana na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti .

Amesema changamoto hiyo ni kubwa ambapo husababisha wananchi kupeleka maiti za ndugu zao kwenye Hospitali teule ya rufaa ya Tumbi na wilaya ya Bagamoyo ambako kuna mbali mrefu.

Aliyasema hayo mjini Chalinze,wakati akizungumza na baadhi ya wananchi,na kusema  shida kubwa inatokea hasa pale mgonjwa anapokuwa amefariki.

Ridhiwani alisema jimbo zima la Chalinze hakuna chumba cha kuhifadhia maiti kwenye vituo vyote vya afya hali ambayo imekuwa mtihani mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo .

"Hali ni mbaya kwa wenzetu wa kata ya Kibindu ambao wanapeleka maiti Hospitali ya Bwagala wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,”

"Wananchi wanaingia gharama kwenda kuhifadhi maiti sehemu nyingine ambako ni mbali na maeneo yao"

“Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya pamoja na zahanati lakini changamoto yetu kubwa ni ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti ambapo tunajitahidi kufanya njia ili kuhakikisha tunajenga chumba hicho,” alisema Ridhiwani.

Hata hivyo, Ridhiwani alisema kata ya Lugoba ambapo kuna kituo cha afya serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kujenga majengo yakiwemo wodi ya mama na mtoto, maabara, chumba cha kufanyia upasuaji mdogo kwa ajili ya akinamama na chumba cha kuhifadhia maiti.


Akielezea suala hilo ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi  Evarist Ndikilo alisema serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma za afya kwenye zahanati zake 292 na vituo vya afya 26 ambapo vituo 119 vimekarabatiwa ili kutoa huduma bora.

Alisema mbali ya hilo pia inahakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa mkubwa.

Ndikilo alieleza kwa sasa ni kunahakikishwa kunakuwa na ongezeko kutoka asilimia 73.3 hadi kufikia asilimia 85 hali ambayo amesema inawezekana kutokana na mikakati iliyowekwa ya upatikanaji wa dawa.

ECOBANK TANZANIA KUFADHILI WANAFUNZI SHULE ZA SERIKALI

$
0
0
Ecobank nchini Tanzania kuanzia mwaka huu inaanzisha mpango wa kutoa zawadi ya ufadhili kwa wasichana wanaofanya vyema katika masomo yao kwenye shule za serikali. Aidha pamoja na ufadhili huo ili kuwaweka katika hali ya kuwa na uzoefu na kazi zao wanazosomea, watakuwa wanahakikisha wakati wa likizo wanawafanyia mpango wa kujishughulisha na kazi hizo ili kuwa na uzoefu.

Hayo yamesema na Mkurugenzi Mkuu benki hiyo nchini Mwanahiba Mzee wakati wa hafla ya mchapalo iliyofanyika hoteli ya Serena kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani mwishoni mwa wiki. Alisema taasisi yake inaona umuhimu wa kumwezesha mtoto wa kike kusonga mbele kama moto wa taasisi hiyo ya kifedha unavyosema ‘press for progress’ ikimaananisha kujikita katika kutafuta maendeleo.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza kabla ya mgeni rasmi ambapo alielezea kwa undani safari ya maisha kama mwanamke wakati hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Ecobank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema mwanamke anafanyakazi nyingi hivyo ni vyema kumwandaa tangu mapema ili kujua majukumu yake kama mzalishaji mkuu kwenye familia.

Alisema kwa sasa hawajaamua wanaanzia ngazi gani za ufadhili, lakini wanataka kufanya kitu tofauti chenye kulenga kupromoti maendeleo ya mtoto wa kike kama maazimio ya Beijing yanavyotaka kufikia asilimia hamsini kwa hamsini katika ngazi za kiutendaji.

Alisema sherehe hiyo ambayo inaambatana na siku ya mwanamke duniani inasherehekewa katika nchi 33 zenye benki hiyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kibenki wa kuhakikisha kwamba wanawake wanasonga mbele kwa kuwa idadi yao ni asilimia 49.55 ya watu waliopo duniani na wanahaki ya kusaidia kukua kwa uchumi wa dunia, wa kaya na wakwao wenyewe kwa kuwezeshwa.
Mshehereshaji Babbie Kabae (kulia) akitambulisha wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Ecobank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Anasema pamoja na ukweli kuwa wanawake wameachwa nyuma kwa miaka mingi, taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha kwamba inakuwa na asilimia 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 huku hapa nchini inakaribia asilimia 49.

Alisema wakati sherehe hiyo ni kusherehekea mafanikio na kujifunza kutoka kwa wanawake waliofanya vyema, wanawake wanatakiwa kujiuliza wamesaidiaje wanawake wenzao kufikia ngazi ya juu kabisa ya uwezo walionao.

Alisema katika taasisi yake wametengeneza mpango wenye vipengele vitano vya kuhakikisha kwamba suala la jinsia linazingatiwa. Alitaja vipengele hivyo kama kushawishi fikira za jinsia katika maeneo ya kazi kuona kwamba kuna mizania. Kukabili fikira mgando dhidi ya wanawake, kuwezesha mwanamke kuonekana wazi, kushawishi kuinua wanawake kwa kutwaa huduma bora wanazozitoa na kusherehekea mafanikio ya mwanamke.
Mgeni rasmi Mwanasiasa Mkongwe nchini na mpigania haki za wanawake, Mama Getrude Mongella akitoa nasaha zake kwa wageni waalikwa na wafanyakazi wa Ecobank Tanzania (hawapo pichani) wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Ecobank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema amefurahishwa na jinsi wanawake majasiri kama Getrude Mongella walivyoweza kupigania haki za wanawake wakikabiliana na makandokando yake na kufanikisha maazimio ya Beijing ambayo yanatumika kumkomboa mwanamke.


UPANDE WA MASHITAKA WAUANDIKIA BARUA UBALOZI WA MSUMBIJI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha wa dola za Marekani 150,000 inayomkabili Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji Joyce Moshi, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wameiandikia barua nchi hiyo kuiomba msaada wa kisheria.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameeleza hayo leo,mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Wakili Wankyo amedai, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, ila wameandika barua kwenda nchini Msumbiji kuomba msaada wa kisheria (Mutual Legal Assistance) ili kufanya upelelezi wa kesi hiyo.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi March 27 mwaka 2018.

Mshtakiwa Mushi anakabiliwa na mashtaka 9, ikiwemo kughushi na utakatishaji fedha.

Inadaiwa Okbota 25,mwaka 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji, alighushi barua ikionesha kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo umeielekeza Benki ya Millennium kupeleka dola za Marekani 10,000 katika akaunti inayomilikiwa na Joyce Moshi akijua yakuwa si kweli.

Pia anadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba 25, mwaka 2016 na Aprili 12 mwaka 2017 mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma kama Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania aliiba dola za Marekani 150,000 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia inadaiwa kati ya Okbota 25, mwaka 2016 na Aprili 12, mwaka 2017 katika ofisi za ubalozi huo, Moshi alijipatia dola za Marekani 150,000.


Pia inadaiwa kati ya Oktoba 25, mwaka 2016 na Aprili 12, mwaka 2017 katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Maputo nchini Msumbiji na Benki ya Millenium BIM tawi la Julius Nyerere Maputo, alijipatia dola za Marekani 150,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la kughushi.

DC MSHAMA ATANGAZA BINGO KWA ATAKAEWAFICHUA WAUZA VIROBA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumter Mshama

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MKUU wa wilaya ya Kibaha Assumter Mshama ametoa ahadi ya fedha kiasi cha sh. 100,000 kwa mtu atakayetoa taarifa na kuwafichua wafanyabiashara wanaoendelea kuuza pombe aina ya viroba ambazo zilizopigwa marufuku na serikali .

Aidha amesema ,hata wafumbia macho wafanyabiashara wa maduka yanayouza vileo ambao hawana leseni ,kwani watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufungiwa biashara zao.

Aliyasema hayo mjini Kibaha alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye baadhi ya maduka yanayouza vileo na baa ambazo wamiliki wake wanatuhumiwa kuuza viroba.

Mshama alisema  wafanyabiashara hao wa vileo wanakiuka agizo la serikali hivyo kwa atakayebainika kuuza pombe hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Leo tumekamata viroba viwili hii inaashiria kuwa pombe hizi zipo,”

"Ninatangaza donge hilo nono ili kuleta hamasa ya ukamataji wa wauzaji wa pombe hizo ambazo ziliwaharibu hasa vijana na watu ambao walikuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na kuelemewa na ulevi," alieleza Mshama.

Mshama alieleza kwamba, kutokana na serikali kuzuia pombe hizo hali imeanza kuwa nzuri kwani vijana angalau wameachana na unywaji wa pombe hiyo na kupunguza vitendo vya kihalifu.

“Sasa tunatembea bila wasiwasi wa kuibiwa lakini kipindi cha nyuma akinamama walikuwa wakiporwa mikoba yao ama simu zao ,;"na madereva bodaboda nao wamebadilika hata ajali za bodaboda zimepungua,” alisema Mshama.

Alitoa maelekezo kuwa wamiliki wa biashara za vileo /baa hawapaswi kufungua biashara muda wa kazi .

Mshama alisema, suala hilo linapaswa lisimamiwe na watendaji wa mitaa na vijiji kwa kuwa tayari walishapewa maelekezo.

Nae mkazi wa eneo la Maili Moja, Ally Ramadhan alisema ,ili kufanikisha ukamataji wa viroba serikali inapaswa kushirikiana na wananchi kwa ajili ya kupata taarifa za wauzaji wa pombe hizo.

KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA

$
0
0
Na. Jeshi la Polisi.

Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake hapa nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari Mosi mwakani kwa lengo la kuondoa sare ambazo zimekuwa zikifanana na zinazovaliwa na askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii, Mussa Alli Mussa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa kikao kilichowakutanisha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi.

Kamishna Mussa amesema sare zilizokubaliwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na wawakilishi wa kampuni binafsi za ulinzi zinatakiwa ziwe na rangi ya bluu nyeusi (Dark blue), nyeusi pamoja na mashati meupe kulingana na mazingira ya kampuni inapofanyia ulinzi.

“Kampuni zote binafsi za ulinzi hakikisheni mnajiandaa mapema kwa kuwa muda utakapofika hakuna kampuni binafsi ya ulinzi itakayoruhusiwa kufanya kazi bila ya kutumia sare hizi ambazo zitakuwa ni utambulisho rasmi wa sekta hii binafsi ya ulinzi” Alisema Mussa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi (TAPSCOA)  Bw. Shawiniaufoo Kimuto amesema kuwepo kwa aina moja ya sare kutasaidia kuondoa mgongano uliopo hivi sasa ambapo baadhi ya kampuni zinavaa sare zinazofanana na zinazovaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Kimuto alisema jambo hilo litasaidia kufahamika kwa urahisi kwa walinzi wa kampuni binafsi na hivyo kuwa rahisi kupata msaada pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kulisaidia Jeshi la Polisi kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo wanayofanyia kazi.

Naye Julieth Rushuli kutoka kampuni binafsi ya ulinzi ya 4JY amesema Sekta binafsi ya ulinzi imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa usalama unaimarika katika maeneo yao hivyo jamii inapaswa kuwapa ushirikiano pindi wanapotekeleza majukumu yao.

DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI, MAKATIBU WAKUU NA NAIBU KATIBU WAKUU ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Joseph Abdalla Meza kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Ali Khalil Mirza kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Juma Ali Juma kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara na Viwanda katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.

DC SINYAMULE ATAKA WANAWAKE SAME WAANDALIWE KUSHIKA NAFASI ZA JUU ZA UONGOZI

$
0
0
Mwandishi wetu ,Same
MKUU wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule amesema Makundi ya wanaweke kuanzia shule ya msingi, sekondari, vyuo, wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wanasiasa, viongozi katika nyanja zote wanatakiwa kukabiliana kuhakikisha Wilaya ya Same inawaandaa wanawake kushika  nafasi nyingi zaidi za juu katika uongozi na kuwa kati ya wanawake wanaomiliki biashara kubwa nchini. 

Sinyamule amewataka Wanawake hao kuwa na kauli moja tu ya kuwa kumiliki viwanda ni haki yao.

na kuwataka kuanza kutafuta maeneo ya uwekezaji na kufikiria kukua zaidi, kuchukua hatua bila kusubiri, kushikana mkono.

"Serikali ya Wilaya imejipanga kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali kuu
yaanza kuanza kuunda mabaraza ya kata, hili yaweze kutenga maeneo ya uwekezaji vijijini na kuainisha maeneo ya wanawake, yaahidi kutoa % ya wanawake,  vijana na walemavu kwa ukamilifu. pamoja na kuanzisha soko la barabarani kukuza bidhaa za wanawake" Amesema 

Amesema wilaya  yake kwa kushirikisha wadau kujenga majengo ya kuwezesha viwanda vya wanawake na kutetea haki ya elimu kwa watoto wa kike. 

Pia amesema mimba kwa wanafunzi zinaonyesha dalili ya kupungua  kwa kipindi cha mwaka 2018 hivyo kuwatka wakzi wa Same kuwatia nguvuni wanaowapa mimba wanafunzi ili nao wapate fundisho na kuvitaka  vyombo vya ulinzi kuendelea kuwasaka wote. 

Hivyo kuwataka  wanawake Same kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Wilaya kwani wengi ni wanawake, wakiweza ni ushindi kwa wanawake wote. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Wilaya ya Same yaliyokuwa na lengo la kupinga ukatili kwa Wanawake.
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sinyamule akikagua Bidhaa za Wajasiliamali waliohudhuria katika Maonyesho ya Siku ya Wanawake Duniani.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria Kongamano la Wanawake lililokuwa likifanyika katika Wilaya hiyo katika maadhisho ya siku ya Wanawake Duniani
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sinyamule , akiwa katika picha ya Pamoja na uongozi wa Wanawake Wilaya ya Same.

MJUMBE BARAZA KUU UVCCM PWANI AAHIDI KUSHUGHULIKIA MGOGORO HIFADHI ZA BAHARI MAFIA

$
0
0
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao,akizungumza na wajumbe wa baraza la UVCCM wa Wilaya ya Mafia kuhusu kupeleka sehemu husika mgogoro wa wananchi na hifadhi ya bahari pamoja na kuwahimiza wanakipigania chama kishinde uchaguzi ujaowa serikali za mitaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Makwiro na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki.Picha Zote na Elisa Shunda.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

NA ELISA SHUNDA,MAFIA.
MJUMBE wa Baraza Kuu la Taifa Mkoa wa Pwani,Ramdhan Mlao amewahakikishia vijana wa Wilaya ya Mafia (Kisiwa) kulifanyia kazi suala la mgogoro uliopo katika ya hifadhi ya bahari na wananchi wanaoishi katika wilaya hiyo ambayo inajumuisha na visiwa vidogo vya Chole,Jibondo na Juani (Visiwa vidogo) kwa kulifikisha jambo hilo kwa viongozi wanaouhusika.

Mlao ametoa kauli hiyo leo wakati anajibu swali lililoulizwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Chole,Khamisi Musa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana CCM wilaya hiyo aliyeuliza kuhusu mgogoro wa wananchi hao kuzuiliwa kufanya shughuli za uvuvi wa samaki kwa kuwa maeneo hayo kwa sasa yamechaguliwa kuwa hifadhi za bahari kulingana na samaki aina ya Papa waliopo katika maeneo hayo.

Hivyo amesema ameyapokea malalamiko yao na kuahidi kulifikisha jambo hilo katika sehemu husika ili kusaidia vijana,wananchi hata chama chake cha CCM.

“Kwa historia tuliyoipata pamoja na nyie kutueleza hapa hili tatizo lina muda kidogo lakini pia  kuna athari kubwa kwa watu wa Mafia na pia litatuathiri sisi CCM kama hatutalifanyia ufumbuzi yakinifu ili watu hawa waweze kuishi salama katika maeneo yao upo mgogoro mkubwa baina ya hifadhi ya bahari na wananchi.

"Mgogoro huu kimsingi kama isipopazika sauti kwa viongozi kwa mustakabali mema kwa mujibu wa watu wa Mafia basi kisiwa hiki hakitakuwa salama, wenzetu hawa wa hifadhi ya bahari wanaonekana tatizo lakini suluhu si kulikimbia tatizo suluhu ni kukaa pamoja wao na nyie mnahitajiana watu wa hifadhi wanawahitaji na nyie mnawahitaji pia kwa kuwa nyie ndiyo wenye mafia yenu lakini katika bahari hii ushuru unapatikana hivyo tatizo hili ni lazima lisuluhishwe mapema” amesema Mlao.

Mbaraza Mlao amesema atayapeleka changamoto hizo kwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani ni msikivu na mchapakazi akaongeza kuwa atampelekea msisitizo kuona picha ya ukubwa wa tatizo hili kwa kuwa kati ya wahusika wa jambo hili yeye na wizara hii ni wahusika muhimu katika kulitatua mgogoro huu.

Aidha Mbaraza Mlao ameongeza kwa kueleza watahakikisha jambo hilo linapata ufumbuzi kwa kuwa kama mgogoro huo usipofanyiwa kazi vijana hao watapata shida kukinadi Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi suluhisho ni kulifanyia ufumbuzi suala hilo kwa kuwa kama wasipolitatua jambo hilo itafika wakati wananchi watawauliza kama mmeshindwa kututatulia mgogoro huu wa hifadhi za bahari tutawaamini vipi wakati jambo hili mmeshindwa kututetea.

“Lengo la dhamira yetu ni kusaidiana na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na usalama katika maeneo yao hatuwakatai ndugu zetu wa hifadhi za bahari  lakini tunataka kwenye maisha haya kila mmoja aishi kwenye eneo lake akiwa salama salmini na afurahie maisha ya uishi wa Utanzania wake tumelipokea jambo hili tunalifanyia kazi ndugu viongozi mtapata majibu juu ya jambo hili,"amesema Mlao.

VIDEO : MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiongea wakati wa baraza la (UWT) manispaa ya Iringa lililofanyika katika ukumbi wa sabasaba mkoani Iringa na kusistiza wakipewa mitaji kutoka kwenye mfuko wake wanapaswa kuutunza mtaji huo ili uongeze faida.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amewainua wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) kwa kutoa mitaji kupitia mfuko ambao ameuanzisha wa kuwainua wanawake wenye kipato kidogo.

Akizungumza nablog hii mbunge Tweve alisema kuwa lengo la kutoa mitaji hiyo ni kuwakomboa wanawake ambao wamekuwa wakisumbuka kufanya biashara ndogo ndogo ambazo ndio zimekuwa zikiendesha maisha yao.

“Mara kwa mara nimekuwa nikiwaona wanawake wengi wakiwa wanauza matunda,karaka na vitu vingine mitaani lakini mitaji yao ni midogo mno hivyo nikaamua kuanza kuwapatia mitaji kupitia mfuko wangu binafsi kwa wanawake wa wilaya ya Mufindi” alisema Tweve

Tweve alisema kuwa atahakikisha kuwa mfuko huo unakuwa mkombozi kwa wanawake wote wa mkoa wa Iringa kwa kuwa ameutengenezea malengo ambayo yameanza kuleta matunda kwenye wilaya ya mufindi na kusaidia kukuza mitaji ya wananchi na kuukuza mfuko pia.

“Matunda yameanza kupatikana kutokana nakuona faida ambayo imeanza kupatikana kwa wanawake ambao nilishawapa mitaji na mitaji hiyo imeanza kuleta faida ambapo sasa itakuwa fursa kwa wanawake wengi nao kupewa mitaji” alisema Tweve

Aidha mbunge Rose Tweve alimshukuru mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas kwa kuchangia mfuko kwa kuahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni hamsini na tatu (53,000,000) kwenye kata mia moja na sita (106) za mkoa wa Iringa.

“Kutoa kiasi ccha shilingi milioni hamsini na tatu (53,000,000) kwenye kata mia moja na sita (106) za mkoa wa Iringa sio kazi ndogo hivyo inapaswa kuzitumia pesa hizo pindi watakapo anza kutoa kama mitaji kwa wanawake wa mka wa Iringa” alisema Tweve

Lakini pia Tweve aliwaomba wanawake wanapewa mitaji hiyo kuitumia vizuri ili kuongeza faida ya mitaji yao pamoja na kuongeza idadi ya wanawake watakaopewa tena mitaji hiyo.

POLISI DAR WABAINI MWANAFUNZI ALIYEDAI KUTEKWA KUMBE ALIKUWA KWA MPENZI WAKE

$
0
0
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.


*Mambosasa asema watamchukulia hatua za kisheria, atoa onyo kali

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Abdul Nondo(24), aliyedai kutekwa  na watu wasiojulikna siku za karibuni uchunguzi wao umebaini kumbe alikwenda kwa mpenzi wake mkoani Iringa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mambosasa amefafanua Machi 6 mwaka huu ,kuanzia saa sita usiku zilianza kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwanafunzi huyo ametekwa na watu wasiojulikana na kusababisha hofu kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

Kamanda Mambosasa amesema kutokana na taarifa hizo, Polisi walianza kufuatilia ili kubaini ukweli wake ikiwa pamoja na kufungua jalada la uchunguzi lenye kumbukumbu namba DSM/KIN/CID/P.E/51/2018.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu tulipata taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, mwanafunzi huyo ameonekana mkoani Iringa katika Wilaya ya Mafinga akiwa mwenye afya njema.

"Tena anajitambua  na akiendelea na shughuli zake na wala hakuna mahali popote ambapo ametoa taarifa kwenye kituo cha Polisi kuwa amtekwa.Jeshi letu la Polisi kwa kushirikiana na wenzetu wa Iringa tulifanya uchunguzi na kubaini  Nondo hakutekwa bali alijiteka kwa lengo la kutafuta umaarufu kwa jamii,"amesema Mambosasa.

Ameongeza baada ya kuendelea na uchunguzi wao kutokana na taarifa za tukio hilo, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wamebaini mwanafunzi huyo aliyedai alitekwa kumbe alikwenda kwa mpenzi wake."Wakati tunafuatilia tukabaini mawasiliano kati yake na huyo mpenzi wake ya mara kwa mara wakati akiwa njiani akielekea Iringa,"amesema Mambosasa.

Amefafanua Polisi pamoja na kuchunguza mambo mbalimbali kuhusu mwanafunzi huyo walitumia utaalamu wao kufuatilia mawasiliano yake kwa kipindi ambacho anadai alikuwa ametekwa lakini walichoona alikuwa anawasiliana zaidi na mpenzi wake.

Pia amesema hata baada ya mwanafunzi kupelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa alipimwa na kubaini hakuna aina yoyote ya kinywaji ambacho alipewa wala hakuwa amepewa dawa za usingizi."Hakuna na majeraha ya aina yoyote kwenye mwili wake,"amesisitiza Mambosasa na kuongeza "Uchunguzi umebaini alikuwa kwa mpenzi wake na alimua kutoa taarifa hizo kwa lengo la kujitafutia umaarufu kwa umma".

Kutokana na mazingira hayo Mambosasa amesema kwa kuwa mwanafunzi huyo hakuwa ametekwa watamchukulia hatua za kisheria kama wahalifu wengine huku akitoa onyo kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam halitavumilia mtu anayejitafutia umaarufu kwa njia ya aina hiyo na nyingine zinazofanana na hiyo.

Hiki ndio kikosi cha Yanga kuelekea Botswana

$
0
0
KIKOSI Cha Mabingwa wa soka nchini na ambao wapo  kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara, Yanga SC , kimeondoka leo saa 10:15 alfajiri  kikielekea Nchini Botswana  kuwafuata Township Rollers ukiwa ni mchezo wa marudiano wa  michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Wachezaji 20 na viongozi 11 pamoja na wengine 8 ambao ni benchi la ufundi ambao wapo katika kikosi kamili cha msafara huo.


Ambapo katika mchezo uliopita uliokuwa wa aina yake kati ya timu hizo mbili ambao mtanange huo uliomalizika kwa dakika 90  na  Yanga alichezeshwa Makhirikhiri na kulazwa chali kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 

Katika Mchezo huo wa marudiano  wakilishi kutoka Tanzania Yanga anakabiliwa na kibarua kizito kwa kutakiwa kupata ushindi mnene ili kusonga mbele  na michuano hiyo. 

Mtanange huo wa  marudiano wa vuta nikuvute kati ya Mabingwa wa Tanzania bara Yanga dhidiTownship Rollers  utarindima huko Nchini Botswana tarehe 17 machi mwaka huu ikiwa kila timu ikihitaji  ushindi mnono ili kusonga mbele zaidi.

MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 81

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MFANYABISHARA Timotheo Wandiba amehukumiwa kifungo cha miaka 81 jela  baada ya kupatikana  na hatia katika mashtaka 27 yaliyokuwa yakimkabili ya kujipatia Sh.bilioni 2.1 kwa njia udanganyifu.

Aidha, Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa Dickson Okololo na Simon Efrem  waliokuwa wakishtakiwa na Wandiba baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri, kwa niaba ya Hakimu Joyce Minde aliyeandika hukumu hiyo,  amesema upande wa mashtaka kupitia  mashahidi 14 imethibitisha makosa yote 82, kuwa mshtakiwa alitenda kosa.

Katika makosa hayo 82, mashtaka 27 ni ya kughushi, 27 ya kutoa nyaraka za uongo, 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na Moja la utakatishaji fedha.

Hakimu Mashauri amesema Mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa Wandiba katika makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, baada ya kuridhishwa na ushahidi  uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka.

Hakimu Mashauri amesema katika makosa hayo 27,  katika kila kosa mshtakiwa Wandiba atatumikia kifungo cha  miaka 3 jela, mbapo jumla itakuwa ni miaka 81,  lakini vifungo hivyo vitaenda kwa pamoja, hivyo  atatumikia kifungo cha miaka mitatu tu gerezani.

Aidha Hakimu Mashauri amesema Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa Okololo na Efrem katika makosa mengine yote baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuyathibitisha pasipo kuacha shaka yoyote.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambalo limemtia hatiani Wandiba, inadaiwa kati ya Desemba 3, mwaka 2012  na Februari 5,mwaka 2013, Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia Sh.119,039,398.96  kutoka Benki ya Africa (BoA) kwa njia ya udanganyifu.

Pia wanadaiwa kughushi fomu za makubaliano ya kuhamisha fedha kutoka Benki ya BOA ikionyesha akaunti ya Sogea Sauthom imeiomba benki hiyo kuilipa akaunti ya Tracom Sh 2,119,039,398.96.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, inadaiwa walilitenda kati ya Desemba 4, 2012 na Aprili 30, mwaka 2014 walijipatia Sh.2,119,039,398.96 kutoka akaunti ya Sogea Sauthom katika benki ya (BoA) kwenda akaunti ya Tracom NMB tawi la Ban House wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu la kosa la kughushi.

Hata hivyo, upande wa mashtaka umesema haujaridhishwa na uamuzi uliotolewa na mahakama na watakata rufaa.

UTARATIBU WA KUPATA ANKARA YA MALIPO KWA JIA YA SIMU

MATUMIZI DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME SASA RUKSA, WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA KADHIA HIYO

$
0
0

Said Mwishehe,Globu ya jamii 
 WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imetaja baadhi ya sababu zinazochangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa wanaume wengi nchini. 
 Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amesema utafiti wa kisayansi duniani unaonesha kuwapo kwa tatizo la nguvu za kiume. 
 Amefafanunua kwa Tanzania hakuna utafiti rasmi ambao umefanyika kubaini tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume nchini kwetu na kueleza ipo haja ya kufanya angalau utafiti ili kubaini udogo au ukubwa wa tatizo hilo. 
 Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ni ulaji wa vyakula vya mafuta, kutofanya mazoezi, matumizi ya ulevi wa pombe pamoja na uvutaji sigara. 
 "Hizo ni miongoni mwasababu ambazo kwa kiasi kikubwa zinaweza kusababisha mwanaume kuwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume.Hivyo tunashauri kwenye chakula ule chakula bora na si bora chakula,"amesema Dk.Ndugulile. 
 Ameeleza Serikali haijawekeza kwenye afya ya uzazi kwa wanaume bali imejikita zaidi kwenye afya ya uzazi kwa wanawake. 
 Ameweka wazi ukiangalia takwimu ya uzazi na akina mama kujifungua Tanzania haina shida lakini taarifa za kisayansi duniani zinaeleza kuna tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume duniani. 
 Dk.Ndugulile amesema kwenye aina ya dawa tano ambazo zimesajiliwa na Baraza la tiba asili na tiba mbadala kuna dawa inaitwa Ujana ambayo inahusika na mambo hayo ya upungufu wa nguvu za kiume. 
 Pia amesema tayari Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), nayo kuna dawa wanaendelea kuifanyia utafiti na watakapokamilisha itaingia kwenye matumizi.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images