Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

WAZIRI KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA KUPISHA UCHUNGUZI KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJANGILI


ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

APRILI Moja katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza,macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa uwanjani hapo.Kwanini jibu ni moja tu kutakuwa na Tamasha la Pasaka.

Tamasha la Pasaka ambalo limekuwa likiandaliwa na Msama Promotion kila mwaka na kufanyika siku ya Sikuu ya Pasaka.Ni tamasha ambalo limekuwa likiwaweka Watanzania pamoja.

Ni tamasha ambalo msingi wake mkubwa ni kudumisha upendo na mshikamano kwa Watanzania na kila mwaka kumekuwa na kauli mbiu kuhusu tamasha hilo.Kwa kukumbusha tu kauli mbiu kwenye tamasha la Pasaka kwa mwaka jana ilikuwa inasema hivi "Umoja na upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu" ...na lilifanyika jijini Dar es Salaam, Mwanza na mikoa mingine kwa siku tofauti .

Tamasha la Pasaka la mwaka huu ambalo sasa linafanyika Mwanza kwa mara ya kwanza kauli mbiu yake inasema “UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU” na sababu kubwa ni kwamba Msama Promotion inataka kuwahubiria injili ya Amani na Upendo wakazi wa Kanda ya Ziwana na Vitongoji vyake.

Ukweli ni kwamba msingi mkuu wa Tamasha la Pasaka ni kutumia tamasha hilo kwa ajili ya kuabudu na kumtukuza Mungu.Hivyo ni tamasha ambalo linahusisha zaidi waimbaji wa nyimbo za Injili huku waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi Maaskofu na wachungaji wakitoa jumbe nyingi za kuhumiza Upendo, Amani na Utulivu kwa watanzania.

Kampuni ya Msama Promotioni kupitia Mkurugenzi wake Alex Msama imekuwa ikifanya jitihada za kuhakikisha wanaohudhuria tamasha hilo wanaburudika kutokana na aina ya waimbaji ambao hupata nafasi ya kutumbuiza kwa kuimba nyimbo za Injili katika tamasha hilo.

Waimbaji wengi maarufu wa muziki huo kutoka ndani na nje ya Tanzania wamekuwa wakishiriki kila mwaka kwenye Tamasha la Pasaka.Tamasha ambalo mwaka huu ni la 18 tangu kuanzishwa kwake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu huku akiwatangaza baadhi ya waimbaji katika tamasha hilo kushoto ni mwimbaji Beatrice Mwaipaja na kulia ni Mwimbaji Paul Clement.
Beatrice Mwaipaja kushoto na Mwimbaji Paul Clement. wakizungumza na waandishiwa habari kuhusu maandalizia ya Tamasha la Pasaka.


MAHUSIANO KAZINI YANAKUFANYA USIJIAMINI -ANNA MAKINDA

0
0
Imeelezwa kuwa mashirika mengi yamekuwa yakianguka na kukosa mweelekeo kwa sabababu ya washirika wake kuwa na mahusiano ya mapenzi wao kwa wao wawapo kazini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Wa bodi Wa mfuko wa Taifa Wa bima ya afya NHIF  Spika  wa bunge mstaafu Anne Makinda wakati Wa sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake iliyofanywa na shirika hilo ofsini kwao jijini Dar es salaam.

Akizungumza na watumishi Wa NHIF Makinda amesema kuwa na mahusiano kazini yanakufanya usijiamini uwapo kazini."Ukiwa na mahusiano na bosi wako hata kama utafanya Kazi kwa juhudi na kupandishwa cheo itaonekana kama umepanda kwa sababu mahusiano mliyokuwa nayo,"alisema Makinda.

Makinda amewaasa wafanyakazi wa NHIF wafanye Kazi kwa uaminifu na waache makandokando.Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa NHIFA Bernard Konga amesema shirika lao linasimamia suala zima la usawa wa kijinsia na watahakikisha wanawake wenye sifa wanapanda cheo.

Aidha Rose Gabriel ambae ni Mwenyekiti wa akina mama NHIF ametoa rai kwa wanawake kusherekea siku ya wanawake kwa kudumisha Umoja na mshikikamano.Amesema unapokuwa kazini masuala ya mahusiano uachane nayo na kufanya kazi kwa waminifu pamoja na kujituma kwa bidii.


Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu,Anne Makinda akizungumza na wanawake wa Mfuo huo leo jijin Dar es Salaam wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza machache katika leo jijin Dar es Salaam wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda akikata keki leo wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe,Anne Makinda akimlisha keki Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
 Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu Anne Makinda akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Taarifa kwa Umma

Dkt.Abbas apongeza utafiti uliofanywa na Misatan kwa kushirikiana na CPESA

0
0
Na.Vero Ignatus Arusha.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema Maafisa Mawasiliano serikalini bado wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa mabosi wao, ikiwano wengine kutokutaka habari zao zisikike kwenye vyombo vya habari.

Dkt.Abbas aliyasema hayo jana mjini hapa wakati mapitio ya ripoti ya upatikanaji wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.

Alisema kupitia ripoti hiyo aliyoiunga mkono na kuisoma vyema atahakikisha maofisa mawasiliano zaidi ya 300 wanaokutana mjini Arusha wanapata utafiti huo."Nimesoma utafiti huu, kurasa zote upo vizuri, niwaombe muendelee kufanya tafiti kama hizi kwani ni chakula kwetu," alisema Dkt. Abbas.

Akizungumzia utafiti uliofanywa katika mikoa 7 na MISATAN Wakili wa mahakama kuu James Marenga amesema ofisi za halmashauri ya mikoa ya Arusha na kigoma ,walau ndiyo zimeonekana ndiyo wanafanaya vizuri katika kuwa wazi katika utoaji wa taarifa kuliko ofisi za mikoa.

Dodoma manispaa,halmashauri ya Jiji la mbeya,Kigoma ofisi ya mkuu Arusha, ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza hakukuwa na ushirikiano,vilevile mkoa wa Mtwara hakukuwa na ushirikiano ,Dar ni katika halmashari ya Jiji,Kwahiyo Utafiti huo ulikuwa umegawanya utoaji  wa taarifa kwa ofisi za mkuu wa mikoa na ofisi za halmashauri au za Majiji katika mikoa iliyochaguliwa.

Moja ya mapendekezo yaliyotolewa baada ya utafiti huo vitengo vya watoa taarifa vinaimarishwa kama inavyotakiwa  katika sheria ya haki  kupata taarifa ya mwaka 2016.Vilevile utafiti huo unasisitiza kuwepo na uwazi katika utoaji wa taarifa haswa kwenye taasisi za serikali.

Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku moja uliofanyika Jijini Arusha ,ulioandaliwa na MISATAN kwa kushorikiana na CIPESA.
Wakili wa Mahakama Kuu Janes Marenga akifafanua jambo katika mkutano wa siki moja uliaondalowa na Misatan na kufanyika Jiiini Arusha.

Mwenyekiti wa MISATAN Salome Kitomari akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Jijini Arusha
Baadhi ya wadau mbàlimbali pamoja na waandishi walioshiriki katika mkutano huo Jijini Arusha.

JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26

0
0

Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama cha MAANDAAMANO UDP,John Cheyo amewataka wanaotaka kufanya maandamano Aprili 26 mwaka huu kuacha kwani yatasababisha uvunjifu wa amani nchini.

Cheyo ameamua kuvunja ukimya na hatimaye kukemea wanaotaka kufanya maandamano ambapo amesisitiza na bora wakaacha kufanya.

Kauli ya Cheyo ambayo ameitoa leo inakuja wakati ambao viongozi mbalimbali akiwamo Rais John Magufuli na Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro, wakitoa kauli za kuwataka wanaotaka kuandamana siku hiyo kuacha mara moja na iwapo watafanya hivyo watasimulia watakachokipata kwa waliwatuma.

 Mwekyekiti huyo, amesema haki haipimwi kwa kuruhusiwa kufanya maandamano au mikutano ya hadhara.“Watanzania tutangulize masilahi ya nchi mbele, amani ndio kila Kitu, tusiruhusu wanaotaka kuvuruga amani, hakuna mahali pazuri pakuishi kama Tanzania."Juzi wenzetu wakenya Rais Uhuru na Odinga walikutana wakasema hakuna zaidi ya Kenya na kukubaliana kudumisha amani.

"Sasa hivi kuna viashiria vya watu kuchoka kuishi kwa amani, vita ya namna hii haifai, nataka utulivu kama huu tulionao watanzania uendelee ili watu waweze kufanya kazi za kujenga Taifa, tuache hofu kwamba hapa hapakaliki,” amsema Cheyo.Aidha amewataka wanaolalamika kwamba sheria zinavunjwa waende mahakamani kulalamika na  maandamani si chochote bali uchonganishi.

Pia amewataka viongozi wa dini kuwa wapatanishi kama vitabu vya dini vinavyowatambulisha badala ya kuchochea wananchi wananchi kuvunja sheria kwa kisingizio cha kudai haki.“Kila kitu kinaachofanywa kwa kupitiaa siasa kisiwe kizingizio kwa mambo mengine, viongozi wengine wafanye kama vile ambavyo wamekuwa wakifanya kipindi cha nyuma, wasiwe chanzo cha watu kufarakana,” amesema Cheyo.

Kuhusu viongozi waandamizi wa Serikali kufanya urasimu kwenye baadhi ya mambo na kukwamisha maendeleo alisema viongozi lazima watambue nchi hii inahitaji maendeleo na hivyo hakuna sababu ya kukwamisha mambo.

KUWAIT YAZINDUA KISIMA CHA 61 KATIKA WILAYA YA KIGAMBONI

0
0
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe, Jasem Al-Najem azindua kisima cha 61 katika shule ya msingi ya Gezaulole, Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam machi 7, 2018, Ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa ''Kisima cha Maji katika kila Shule''.

Ulio anzishwa na Ubalozi wa Kuwati mwishoni mwa mwaka 2016, Hafla ya uzinduzi wa kisim hicho kilihudhuliw na Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Maziku Luhemeg, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Gezaulole, Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shabani pamoja na walimu na wanafunzi wa shule hiyo,kilicho zindiuliwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem.

Ambapo kitanufaisha shule ya Msingi ya Gezaulole iliyoanzishwa mwaka 1962 yenye wanafunzi 868 na madarasa kumi na shule jirani ya Sekondari ya Ibnu Rushyyenye wanafunzi 250 iliyo anzishwa mwaka 2007.

Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh. Jasem Al-Najem katika hotuba yake baada ya uzinduzi huo amesema kuwa Ubalozi wa nchini mwake umeanzisha mradi wa "Kisima cha Maji" ilikuitikia wito na kuunga mkono sera ya Rais wa Tanzania, Mh. Jonh Magufuli ya kutoa Elimu bure .Balozi Mhe, Jasem Al-Najem ameeleza kuwa kuwa atashirikiana na viongozi wa eneo hilo katika kutatua changamoto zitakazo kabiliana na shule hiyo,

Aidha aliahidi kuwapatia wanafunzi wa shule hiyo, madaftari , , mikoba na vifaa vya kuhifadhia maji kwa kila darasa ili wanafunzi wasihangaike kuchukua maji katika kisima mara kwa mara huku akiwataka wanafunzi hao kujihimu katika masomo yao ili wawe mdaktari, wanahabari, walimu.

Diwani Sumangila kwa upande wake Francis Chichi ameishukuru Kuwait kwa kuwachimbia kisima cha maji katika shule hiyo huku akimuomba Balozi, Jasem Al-Najem kusaidia Kata yake gari la kubebea wagonjwa ili kuwaondolea akina mama wajawzito na watu wazima ambao hulazimika kutembea masafa marefu kufika Hospitali na katika vituo vya Afya ambapo baadhi yao wakati mwingine hulazimika kukodi Pikipiki ili kufika huko, jambo ambalo linahatarisha uhai wao.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akizindua kisima cha maji katika shule Gezaulole. akiwa na mwalimu Mkuu Maryam Shaban (wa tatu kulia), na Sheikh Kaporo ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa kisima wa kwanza kushoto 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem akihutubia baada ya uzinduzi wa kisima, kulia kwake ni Diwani wa Sumangila Fransis Chichi na kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu Waryam Shabani.
Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi akizungumza jmbo mara baad ya Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem kuzindua kisima 
Wanafunzi wakiwa wamebeba vifaa maalumu vya kuhifadhi maji vilivyotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait Nchini
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh.Jasem Al-Najem akiwa amekaa na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya Gezaulole ambapo amewaahidi kuwapati mdftari na mikoba

MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

0
0
NA ELISA SHUNDA,MAFIA .


VIONGOZI wanaounda Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mafia wametakiwa kujitoa kwa nguvu,mali na rasilimali zao katika kukitumikia chama hicho na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu 2020 ili CCM katika wilaya hiyo kiibuke na ushindi wa kishindo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Charangwa Selemani Makwiro wakati alipofanya ziara wilayani humo leo ambapo katika kuhakikisha vijana wa wilaya hiyo wananufaika na serikali ya Dk.John Pombe Magufuli amepata fursa ya kutembelea ofisi ya wilaya na halmashauri ambapo amekutana na uongozi na kupewa maelezo ya mnufaiko wa vijana wa Mafia katika asilimia 4% ya mikopo na miradi inayotolewa na uongozi huo kwa vijana hao.

Mwenyekiti Makwiro amewaeleza vijana hao kuwa wao ndiyo nguvu ya chama na kuwataka kusimama ngangari kama viongozi na vijana wa CCM kwa kutumia nguvu,mali,akili na rasilimali zao zote katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwakani wa serikali za mitaa ambapo ndiyo msingi wa ushindi wa uchaguzi mkuu wa madiwani,ubunge na urais hivyo ni jukumu lao vijana kukipigania chama katika maandalizi ya uchaguzi huo.

“nimefarijika siku ya leo kukutana na viongozi na vijana wa CCM wa Wilaya hii ya Mafia napenda kuwausia na kuwakumbusha vijana wenzangu mmeomba nafasi za uongozi kwenye maeneo yenu hivyo basi unapoomba nafasi katika chama hiki usitarajie labda kuna hela utapata au uwe kibaraka wa kiongozi Fulani ili maisha yako yaendelee hapana umeomba nafasi ya uongozi kwa ajili ya kuwatumikia vijana wenzako ni jukumu lako kama kiongozi sasa kutumia nguvu zako,akili,mali na rasilimali katika kukitumikia chama hiki;

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Picha zote na Elisa Shunda
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia,Gilbert Sandagula akitoa ufafanuzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri kwa ujumla jinsi inavyosaidia vijana wa wilaya hiyo kunufaika na mikopo na miradi mbalimbali inayotolewa na ofisi hizo kwa vijana.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akiulizia mambo mbalimbali yahusuyo vijana wa Wilaya ya Mafia kwa uongozi wa wilaya hiyo ofisini hapo.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango,akizungumza wakati Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao walipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia kupokea taarifa ya usaidizi wa ofisi hiyo katika kuwasaidia vijana wa wilaya hiyo kwenye mikopo ya asilimia 4%.



CRDB-MLIMANI CITY WASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA ZAWADI KWENYE WODI LA WALIOJIFUNGUA KWA UPASUAJI NA

0
0
WAFANYAKAZI wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam waadhimisha siku ya wanawake kwa kutoa zawadi katika wodi la wanawake waliojifungua kwa upasuaji pamoja na wenye kifafa cha mimba katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Saalaam.

Akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Malimani City, Adelpghina Barongo amasema kuwa wanawake wananchango mkubwa sana ndio maana wameona umhimu wa kutoa zawadi kwenye wodi hiyo kwana wanawake pia ndio wanaopata changamoto mbalimbali.

"Wanawake wanamchango mkubwa pia ndio wanaopata chamgamoto mbalimbali ndio maana tumeota tuwae zawadi japo kidogo wa akinamama ambao wapo hospitali"

Ametoa wito kwa akinamama waliopo hospitali kufungua akaunti kwaajili ya kujiwekea akiba kwani akaunti ya Malkia ni sawa na kibubu chenye dhamana pamoja na faida.

"Wanawake tujifunze kuweka akiba benki kuweka ndani hii haina ulizi wa pesa kutokana na majamga mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza kama moto na wizi  akauti hii inaulizi tosha na madhibuti"Amesema Adelphina.

Benki ya CRDB yenye kauli mbiu ya siku ya Mwanamke Tanzania isemayo "Mwanamk na Malkia akaunti"  pia kauli mbiu ya Kitaifa ni Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”. hii inawaa nguvu benki hiyo kuendelea kuwaangalia wanawake kwa jicho la karibu zaidi kwani wanajua mchango wa mwanamke kwa jamii.




 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlima city wakiwa katika hospitali ya Mwananyamala wakiwa tayari kutoa msaada katikawodi ya wanawake waliojifungua kwa upasuaji na wenye kifafa cha mimba katika hospitali  hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuwajali wanawake na watoto kuadhimisha siku ya wananwake duniani ambayo hufanyika Machi nane kila mwaka.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja leo.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya Mwananyamala wodi ya wanawake waliojifungua kwa upasuaji pamoja na wenye kifafa cha mimba.
 Picha ya pamoja wafanyakazi wanawake wa benkiya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Adelphina Barongo akimkabidhi zawadi mteja wa tawi hilo na Malkia, Witnes Masawe ikiwa ni kwaajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.

FUATILIA LIVE: Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini, Mkoani Arusha

MWENYEKITI,MTENDAJI WA KIJIJI WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUWAKODISHIA MASHAMBA RAIA WA BURUNDI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilayani Kakonko mkoani Kigoma inawashikilia Mwenyekiti na Mtendaji wa Kijiji cha Kikurazo pamoja na Warundi watano kwa kosa la kuwakodisha warundi mashamba zaidi ya Hekari 100 ambayo ni mali ya Kijiji hicho.

Viongozi hao na RAIA hao wa Burundi wanashililiwa baada ya oparesheni iliyofanywa na Kamati hiyo katika kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kukagua usalama wa mipaka ya Tanzania.
Akiizungumzia operesheni hiyo jana, Mkuu wa Wilaya ya kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wependa maendeleo kuwa kuna baadhi ya wananchi kutoka Burundi katika eneo la Kumuka wanakuja katika mpaka wa Tanzania katika Kijiji cha Kikurazo.

Ameongeza wanapofika kijijini hapo hukodishiwa maeneo hayo ambapo wamekuta wamelima Mihogo, Mahindi na Karanga wakati wananchi baadhi wanakosa maeneo ya kulimia.Amesema kuwa wao kama viongozi wa wilaya waliamua kufika Katika eneo hilo na kukuta kuna mshamba zaidi ya hekari 100 zinazolimwa na Warundi kwa kukodishiwa na viongozi wa Kijiji kwa Sh. 40000 hadi Sh.60,000 kwa hekari moja ilikujipatia fedha hizo.

"Baada ya kukuta hali hiyo waliamua kumkamata Mwenyekiti wa Kijiji na Mtendaji pamoja ma baadhi ya Warundi waliokuwa katika mashamba hayo na wanaendelea na mahojiano na jeshi la polisi baada ya hapo watawafikisha mahakamani," amesema.Ameongeza walipofika mpakani kuangalia usalama wa mpaka wetu wameukuta mpaka uko salama na wamefanya oparesheni na kubaini Warundi wanalima kwenye ardhi ya Tanzania.
*Na baada ya mahojiano wamekili kabisa wanalima na wamekodishiwa na viongozi nipende kuwaambia Warundi na viongozi wa vijiji wasiifanye Tanzania kama shamba la bibi, wananchi wetu na wao wanahitaji kulima na tutahakikisha hakuna Mrundi yeyote atakae vuna mazao hayo.

"Na tutahakikisha mazao hayo yanavunwa na wananchi wetu hatuko tayari kuona nchi yetu inaingia uhasama na nchi jirani kwaajili ya baadhi ya viongozi wasio waaminifu", amesema Kanali Ndagala.Aidha amewataka viongozi na wananchi wa mipakani kuacha tabia ya kuwakodishia wananchi wa Burundi mashamba kwa kuwa ni kosa kisheria na kwa watakao bainika watafikishwa mahakamani," amesisitiza.

Pia amesena oparesheni hiyo ni muendelezo wa oparesheni zingine kwakuwa suala hilo linaweza kusababisha kupelekea uvunjifu wa amani kutokana na miingiliano huo wa mipaka na kusababisha mipaka ya nchi kuibiwa na wageni.Mtendaji was Kijiji cha Kikurazo Merikiadesi Evarist amekiri ni kweli maeneo hayo yamevamiwa na Warundi na baadhi ya wananchi hawana maeneo ya kulimia.
Amesema yeye kama mtendaji wa kijiji hajahusika na suala hilo na ameaminiwa kuwa mtendaji wa kijiji hicho kwa muda wa miezi sita iliyopita, hivyo hakuwa anafahamu chochote kinachoendelea katika maeneo hayo.

Mwenyekiti was kijiji hicho Enosi Rwanika amesema baadhi ya wananchi ambao ndio wamiliki wa mashamba hayo wamekuwa wakiwakodishia raia hao kutoka Burundi.Amesema mwaka 2017 waliweka utaratibu wa Kuhakikisha wananchi wanagawiwa maeneo kwaajili ya shughuli za kilimo, baadhi walichukua na wengine hawakuweza kujitokeza.

"Ambao hawakujitokeza ndio hao wanaolalamika hawana maeneo ya kufanyia kilimo na waliochukua baaadhi yao wanawakodishia Warundi mashamba," amesem

DKT.MWIGULU AAGIZA WANAOPANGA MIPANGO YA MAANDAMANO WAKAMATWE

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya Aprili 26 mwaka huu.

Dk.Mwigulu ametoa maelekezo hayo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dk.John Magufuli aliyopo mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo jana amezindua kiwanda cha Alizeti mkoani humo.Amesema lengo la maandamano hayo ni kutaka kuchafua taaswira ya nchi na tayari ameshatoa maelekezo kwa IGP Sirro.

"Njama hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma." Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu  ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Dk.Mwigulu.

Pamoja na hayo, Dk.Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa. Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?

"Watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana,"amesisitiza.Pia Dk.Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.

"Ikitokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atakuwa nala kuajibika kwasababu watu wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania",amesisitiza Dk. Mwigulu.

Kwa upande mwingine, amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu Taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.

Taasisi za elimu ya juu ziimarishe madawati ya mikopo

0
0
Viongozi wa taasisi za elimu ya juu nchini ambazo wanafunzi wake wanapokea fedha za mikopo kutoka Serikalini kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafuzi wa Elimu ya Juu (HESLB) zimetakiwa kuwawezesha maafisa wanaosimamia madawati ya mikopo katika taasisi hizo ili watoe hudima bora kwa wanafunzi.

Akifunga kikao kazi cha siku mbili kati ya Menejimenti ya HESLB na maafisa wanaosimamia madawati mikopo kutoka taasisi za elimu ya juu zaidi ya 70 mwishoni mwa wiki mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha maafisa wao wana vitendea kazi vya uhakika na wanapata ushirikiano wa kutosha.

Madawati hayo ya mikopo yalianzishwa mwaka 2011 katika taasisi zote za elimu ya juu kufuatia maelekezo ya Serikali ili kuongeza ufanisi katika kusimamia shughuli za utoaji mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi.  
“Kila mdau kwenye utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ana wajibu wake, Serikali inatoa fedha kwa wakati na menejimenti za taasisi za elimu ya juu ni wajibu wao ni kuimarisha wadawati ya mikopo yanayowahudumia wanafunzi kwa kuwawezesha ili ninyi maafisa mnayoyasimamia mtoe huduma nzuri kwa wanafunzi … mpewe ushirikiano na vitendea kazi,” alisema Dkt. Akwilapo wakati akifunga kikao kazi hicho kilichofanyika Alhamisi na Ijumaa ya wiki iliyopita (Machi 8-9, 2018).

Dkt. Akwilapo aliwakumbusha maafisa hao kuwa wao ndiyo watu wanaokutana na wanafunzi kwa mara ya kwanza huko vyuoni na kwamba ni muhimu wakatoa huduma bora kama Serikali ilivyotarajia wakati inatoa maelekezo ya kuanzishwa kwa madawati hayo.

Pamoja na kuimarisha madawati ya mikopo, Katibu Mkuu pia amazitaka taasisi kuhakikisha fedha za mikopo ya wanafunzi zinazopelekwa vyuoni zinawafikia wanafunzi kwa wakati kama ilivyokusudiwa na pale ambapo mwanafunzi hayupo chuoni, zirejeshwe kwa Bodi ya Mikopo haraka kama miongozo inavyotaka.
Lengo la kikao kazi

Akizungumza kabla ya Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alisema HESLB huandaa kikao kazi kama hicho mara moja kila mwaka ili kujadiliana kwa pamoja kuhusu utendaji kazi wetu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wanafunzi na wadau wengine.

NAIROBI TO HOST ACADEMIA-PUBLIC-PRIVATE PARTNERSHIP (APPP) FORUM AND EXHIBITIONS 2018

0
0
The Inter-University Council for East Africa, Kampala, Uganda, 12th March 2018:The Inter-University Council for East Africa (IUCEA), the East African Business Council (EABC), the East African Science and Technology Commission (EASTECO), and the East African Development Bank (EADB) are jointly organizing the Academia-Public-Private Partnership (APPP) Forum and Exhibitions 2018.

The forum’s theme is The East African Common Higher Education Area: Opportunities for Industrialization through Academia-Public-Private Partnerships. The forum seeks to explore the status and potential for linkage between the three sectors in utilizing opportunities brought about by the East African Community (EAC) Common Market Protocol. The forum will take place at Catholic University of East Africa in Nairobi, Kenya on 21st to 22nd March 2018.

The APPP focuses on (i) enhancing linkage between the academia, research institutions, and public and private sector enterprises; (ii) promoting the utilization of higher education research output and innovations by the private sector/business community; (iii) promoting consultative engagement in curriculum and research development and implementation and (iv), jointly organizing dialogue forums and exhibitions. The pioneer Forum organizers – IUCEA and EABC were joined by EADB in 2013 and EASTECO in 2017.

The key themes of discussion will include Science, Technology and Innovation (STI) as a catalyst for transformation of the production systems and outputs, contribution of medium, small and macro enterprises (MSMEs) to ensure optimization of productive potential for sustainable economic growth; education ecosystems for knowledge management and information sharing within the EAC industrialization processes; role of centers-of-excellence initiatives in the EAC Partner States in industrialization; and the role of media and creative arts in promoting APPP and EAC integration.

The plenary and breakaway sessions will be run in parallel with exhibitions, in which products, systems and services emanating from research and innovations from universities, research institutions and the private sector will be showcased as a way of promoting and enhancing academia-public-private partnerships.

“Academic-Industry linkages have become critically important at this stage when we know that the convergence between academic, public and private institutions both productive and service providers can drive innovative development,” said Prof. Alexandre Lyambabaje, Executive Secretary, IUCEA.  “Whereas publication of research findings in peer-reviewed journals is good, translating these research findings into innovative products and services that can be commercialized and used in everyday life is greater,” he said.

He encouraged academics, researchers, innovators, students, SMEs and all interested members of the public to attend the forum for sharing experiences and use the forum as opportunity for learning.

Registration for the Forum and Exhibitions

The Forum which has been in place since 2011, is open to all stakeholders in East Africa and beyond from the academia, public and private sectors, higher education institutions, Africa Centers of Excellence (ACEs), employers, manufacturers and other players in the wide industry value chain and business community in general, national commissions and councils for higher education and national commissions and councils for science and technology as well as organizations responsible for research, development and industrialization and the media. To register to participate as an exhibitor, visit the website www.iucea.org/forum.  Deadline for registration is 5th March 2018.

DC Nyamagana aipongeza Airtel na kusisitiza uaminifu kwa mawakala wa mitandao ya simu

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha ameipongeza Artel Tanzania kwa juhudi zake za kupeleka huduma kwa wateja huku pia akitoa onyo kwa Mawakala wa Mitandao ya simu kuacha hila na udanganyifu kwa wateja ili kujenga imani ya mitandao hiyo kwa Jamii.

Bi Tesha amebainisha hayo wakati akifungua moja ya maduka ya kisasa ya kutolea huduma ya kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel eneo la Nyegezi,jirani na kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbalimbali nchini. “Wananchi wetu wamelizwa sana kutokana na mawakala kutokuwa waamifu na waadilifu,Ukweli Serikali haitawafumbia machi kuona wananchi wanaibiwa” …Alisema Mama Tesha

Mama Tesha amewaomba wananchi wa kata 18 za wilaya ya Nyamagana kuyatumia maduka yanayofunguliwa na Airtel kupata huduma za ukakika zilizosogezwa katika maeneo yao na kuwafichua mawakala wasio waaminifu.

Aidha amewaomba wananchi kusajili laini zao za simu kwa kutumia vitambulisho vinavyokulika kiserikali ili kupunguza uhalifu wa kimtandao ambao umeshamiri katika maeneo mbalimbali nchini. Meneja Miradi ya Airtel Kanda ya Ziwa Joseph Mushi amesema kufunguliwa kwa duka hilo ni mwendelezo wa kampuni yake kusogeza huduma karibu kwa wateja badala ya kuzifuata kwenye maduka makubwa mijini.

“Duka hili la kisasa ni moja ya maduka 27 ya kanda ya ziwa,na nila 13 mkoani Mwanza litatoa huduma zote zinazopatikana kwenye maduka makubwa,na hakuna kuwa na upungufu wa kutoa fedh.alisema Mushi.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Nyegezi Charles Muso mbali nae aliipongeza Airtel kwa kuboresha huduma zake pamoja na kuwashauri wananchi walioko pembezoni kulitumia duka hilo kupata huduma za kimtadao. “Ukweli duka hili sasa litawafanya wananchi waliokuwa wakitumia nauli zao kufuata huduma mjini karibu kilometa 15 sasa wamepata mkombozi..alisema Muso.

Jumla ya mikoa 10 imezindua maduka ya kisasa ka ajili ya kusogeza huduma karibu kwa wateja, mikoa hiyo ni pamoja Morogoro,Pwani,Mwanza,Kagera,Kigoma,Mara Dodoma,Singida,Pwani na Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha (katikati aliyeshika mkasi) akiwa pamoja na Meneja Miradi ya Airtel Kanda ya Ziwa Joseph Mushi (mwenye tshirt nyekundu) pamoja na wadau wengine muhimu tayari kukata utepe ili kuzindua duka la Wakala wa huduma za kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel,eneo la Nyegezi, jirani na kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi ya Airtel Kanda ya Ziwa Joseph Mushi, ambaye amefunguka kwa kusema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo ni mwendelezo wa kampuni yake kusogeza huduma karibu kwa wateja badala ya kuzifuata kwenye maduka makubwa mijini.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha akisalimiana na baadhi ya wateja.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha amekuwa mteja wa kwanza kupatiwa huduma mara baada ya kufanya uzinduzi wa duka hilo la Wakala wa huduma za kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel, lililoko katika eneo la Nyegezi, jirani na kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbalimbali nchini.

WAKULIMA 2000 WAONGEZA KIPATO KWA UJENZI WA DARAJA LA MIVARF

0
0
Wakulima 2000 kutoka  vijiji sita vya Kata ya Kiru Wilayani Babati wameongeza kipato kutokana na ujenzi wa daraja lililojengwa na Mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za kifedha Vijijini (MIVARF),  ikiwa ni sehemu ya malengo ya mradi huo katika kuongeza kipato nchini hususan  maeneo ya vijijini.

Wakulima hao wa Kata ya Kiru, inayojumuisha kaya 306, walishindwa kuongeza kipato kwa takribani  miaka 38,  tangu mwaka 1978, baada ya Daraja walilokuwa wanatumia kusombwa na Mafuriko hadi mwaka 2016, Serikali kupitia Mradi wa MIVARF ilipojenga  Daraja hilo ambalo limeanza kutumika sasa na  kuchochea shughuli zao za  kiuchumi .

Akiongea  na timu ya  wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na  Mradi  wa MIVARF mara baada ya kutembelea Kijiji cha Masware lilipojengwa Daraja hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Hamis Malinga amesema, Serikali kupitia Mradi wa MIVARF imeweza kuchochea uwekezaji katika kata hiyo

“Kiwanda cha Sukari cha Manyara kimeweza kuongeza uzalishaji kutoka tani 15 hadi 30 kwa siku kutokana na ujenzi wa daraja la kijiji cha Masware ambalo limesaidia kuboresha biashara baina ya vijiji na kuongeza kipato kwa wananchi. Aidha, Usafirishaji wa mazao na bidhaa ulikuwa wa gharama kubwa sana lakini kwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mradi huu tumeweza kuona maendeleo makubwa katika Vijiji hivi”, alisema Mkurugenzi Malinga.

Kwa upande wa wakulima wa kijiji  cha Masware wamesema ujenzi wa Daraja hilo umeongeza kipato chao kwani wanaweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi pamoja na vijana wamepata ajira kupitia usafiri wa pikipiki maarufu kama “bodaboda”  unaotumiwa kusafirisha abiria

“Tangu ujenzi wa daraja hili tumeweza kupeleka mazaoyetu katika soko tunalotaka ambapo awali haikuwa rahisi, wakulima walikuwa wanalanguliwa gunia moja la mahindi lilikuwa likiuzwa kuanzia shilingi elfu 20,000 hadi 30,000 lakini kwa ujenzi wa daraja hili wananchi wanaweza kuuza mahindi kuanzia elfu 50,000 hadi 60,000 kwa gunia moja” amesema Aboubakar  Mohamed.

Naye Mkulima wa Kijiji hicho Zena Mpinga ameeleza  kuwa, “kabla ya ujenzi wa daraja hilo wanawake na wamama wajawazito walikuwa wakisafiri kwa shida na kwa gharama kubwa sana ambapo ukisafiri kwa kutumia pikipiki maarufu kama “bodaboda” ilikuwa ni shilingi elfu 10,000 kutokana na ukosefu wa kivuko imara na bora na kulazimu kuzunguka na pikipiki kijiji jirani ila kwa sasa usafiri wa bodaboda ni shilingi elfu 2000 hadi 3000 tu inakufikisha na kuweza kukamilisha mahitaji yako kwa wakati.

Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kutekelezwa katika Halmashauri 76 za Tanzania Bara na Zanzibar, ikiwa  imegharamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (IFAD) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (ADB) kwa kushirikiana na  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muonekano wa Daraja la Masware lililopo katika kijiji cha Masware Kata ya Kiru Wilayani Babati, daraja hilo limejengwa na Mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za kifedha Vijijini (MIVARF).

Why Tanzania Should Turn Natural Gas Into Diesel

0
0
If you are skeptical, technology has made it possible to convert natural gas and coal into high-quality liquid transportation fuel such as diesel, kerosene, lubricants oil and jet fuel just to mention a few. This technology is known as Gas-To-Liquid (GTL).

Gas-To-Liquid (GTL) has been around for years. It enacted in the 1920s by the German scientists named Franz Fischer and Hans Trapsch when they had figure out the best way to convert coal into oil materials like diesel and kerosene. The technology become the most important source of energy in German that provides fuel to keep transportation going in the country.

Gas-To-Liquid (GTL) worked dramatically not only with coal and natural gas, applying heat and pressure and convert natural gas into oil products such as diesel, engine oil and so on.
With no oil but huge quantities of natural gas assets, it is a reasonable option for Tanzania to give the gas-to-liquid technology a chance.

Tanzania does not produce oil, is a net importer of the oil-related product such as diesel, lubricant oil.
With huge gas reserves in the country (about 57 trillion cubic feet of gas gross recovered). Transforming natural gas into transportation fuel is the best way to sustain our oil-reliant way of life. The gas-to-liquid process will help Tanzania to become self-sufficient and reduce or stop relying on importing the transportation fuel from the foreign country.

And use our natural gas rather than buying the fuel from other countries. It will help Tanzanians, consumers, to buy cheap fuel at the pump. Another reason to encourage the use of the gas-to-liquid process is the liquid fuels derived from the technology has fewer impurities such as sulfur and Nitrogen, than fuel made from crude oil. Because it derived from the cleanest fossil fuel-natural gas.

Tanzania should look up to South Africa.
Tanzania has to learn from South Africa and follow in its footsteps. When state-owned south Africa coal, oil, and gas corp(ltd) created in the 1950s, South Africa had little oil, but great volume of coal. To come out ahead, they converted coal into liquid fuels that power cars. aircraft, and tankers.
Five years later, It was pumped the first coal derived from oil. Today, South Africa supply 29% of the country transportation fuel.

Also Read.    Tanzania's Thirst For Gas Many Multinational Oil Companies Are Looking At The Gas -To -Liquid Technology. The gas-to- liquid process increases popularity day by the day. Many companies such as Exxon Mobil, BP, Conoco and Royal Dutch Shell Plc have examined the technology for quite some time. And they built gas-to-liquid plants in several regions.
In 2014, Shell signed an agreement to carry out a feasibility study for the gas-to-liquid plant in Mozambique. And now Shell is constructing $19 gas-to-liquid plant in Qatar.

How The Gas-To-Liquid Technology Work.
Natural gas is extracted from the ground, afterward, they add oxygen to the extracted natural gas.
This form combination of hydrogen monoxide, hydrogen, and carbon dioxide.
With the presence of catalyst often cobalt, it subjected to high pressure and temperature.
Cobalt is used as a catalyst to speed up the reaction.

This led to the production of wax. To turn into usable form wax processed at the refinery where heat and pressure is used to split the hydrocarbon into various oil-related products,

By Hussein Boffu
Hussein.boffu@tanzaniapetroleum.com
+255655376543

FIRE KLABU ZITUMIKE KUZUIA MAJANGA YA MOTO SHULENI - ZIMAMOTO

0
0
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Emmanuel Kibona akitoa elimu ya Kinga na Tahadhari Dhidi ya Majanga ya moto kwa Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Secondari Azania (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Na Nasibu Mgosso. 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ndicho chombo chenye jukumu la kuzuia na kukabiliana na majanga mbalimbali kama mafuriko , Tetemeko la Ardhi, ajali za vyombo vya usafiri na usafirishaji, kuporomoka kwa majengo, migodi, pamoja na matukio ya moto.

Mara kwa mara, majanga ya moto yamekuwa yakitokea katika jamii yetu kwa sababu moto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Utafiti umethibitisha kwamba, vyanzo vingi vya moto ni sisi wenyewe (binadamu) kutokana na uzembe, hujuma au kutokukuwa na elimu ya Tahadhali na Kinga Dhidi ya Moto.

Aidha, matukio ya moto yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika shule za bweni hapa nchini hususani shule za sekondari, na kusababisha uharibifu wa miundo mbinu kama vile Mali, majengo na wakati mwingine majeraha au vifo kwa wanafunzi wetu na kuleta simanzi na sintofahamu kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla .
Picha ni sehemu ya bweni iliyoathirika na moto na kuteketeza mali za Wanafunzi.

Uchunguzi wa moto (Fire Investigation) umebaini sababu za matukio hayo ni matumizi mabaya ya umeme yanayofanywa na wanafunzi kwa kujiunganishia nyaya za umeme wenyewe bila kuwa na weledi iliwapate sehemu za kuchaji simu na heater za kuchemshia maji kwa kificho kwa sababu Wanafunzi hawaruhusiwi kuwa na simu wala heater pindi wanapokuwa shuleni.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

DC TABORA AHIMIZA MATUMIZI YA DAWA ZA KUUWA WADUDU KWA WAKULIMA

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Nzega. Mkuu wa Mkoa huyo alikuwa katika ziara maalumu ya kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali katika mashamba ya wakulima wa pamba katika sehemu mbalimbali Wilayani humo.
 Mshauri wa Masuala ya Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage (mwenye shati nyeupe) akitoa kwa wakulima namna ya kuwatambua wadudu mbalimbali waharibifu wa zao la pamba katika Kijiji cha Mogwa Wilayani Nzega wakati wa  ziara maalumu ya Mkuu wa Mkoa huo kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali kuua wadudu katika mashamba ya wakulima katika sehemu mbalimbali Wilayani Nzega.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa elimu Wilayani Nzega  juu ya matumizi ya dawa ya kuua wadudu waharibifu wa pamba aina ya Dudu -All 450EC wakati wa mwendelezo wa kampeni yake ya kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya viuawadudu.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia ) na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (kushoto) wakigagua shamba la Mkulima wa pamba katika kijiji cha Chamwabo wilayani Nzega ambalo lilikuwa limeathiriwa na juu na wadudu waharibifu lakini hivi limeanza kuanza matunda mapya ya pamba(vitumba).  
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) akitoa elimu kwa wakulima wa pamba wa Kijiji cha Budushi wilayani Nzega juu ya matumizi sahihi ya aina mbalimbali ya dawa za kuua wadudu wa zao la pamba. Wengine ni Afisa Ugani Kata ya Kitangili Halima Chezue(wa pili kulia), Mtendaji wa Kijiji cha Budushi Ndimiyake Noah (wa pili kutoka kushoto) na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitangili Jesca Kaaya(kushoto)
 Miongoni pamba ambayo imetunzwa vizuri na kupuliziwa dawa vizuri ya kuua wadudu waharibifu katika shamba la Mkulima wa Kijiji cha Budushi Christina Bundala kama inavyoonekana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Saving maize in Tanzania with nuclear techniques

0
0

Hundreds of hectares of prime maize cultivation areas in Tanzania have in recent years been invaded by so called army worms or maize leaf worms, which pose serious danger to crops. In late 2017 more than 7,500 acres of maize had been destroyed according to the Mwanza Regional Agricultural Officer, Innocent Keya.

Agriculture in Tanzania plays one of the leading roles in the economy, contributing nearly 30% of GDP and more than 50% of the country’s employment and the sector is on the rise.According to the World Bank’s crop production index, Tanzania’s crop production rose by 44% during 2008–2013, far exceeding Sub-Saharan Africa’s total average growth rate of 18%. 
Among the crops, maize has a special place in terms of ensuring food security. Tanzania is listed inthe top 25 countries that take leading positions in cultivating maize. 

Maize is one of the most important crops in Tanzania, and accounts for more than 40% of all cultivated lands. The production of maize accounts for more than 70 % of the cereal produced in the country.
It’s estimated that between 85 to 90% of Tanzania’s population, about 50 million people, consume 90% of the maize production. The rest is exported mainly to neighboring countries. Most of the maize (80 %) is produced by small scale farmers and is grown both for subsistence and as a cash crop.
To guarantee future crop yields and food security maize seeds and plants should be protected.

In order to prevent these disastrous effects from insects, there are traditional and unconventional methods. Farmers can use huge amounts of pesticides, which have a negative impact on the environment and result in the development of resistance against pesticides among various insect species. Alternatively there is an option of using nuclear science to deal with these harmful pests, this while not affecting soil and environment. 

The International Atomic Energy Agency (IAEA) is using nuclear science to develop environmentally-friendly alternatives for pest control. The IAEA and the Food and Agriculture Organisation (FAO) are jointly sponsoring projects and conducting research on control of insect and pests using ionizing radiations. They have placed considerable emphasis on the Sterile Insect Technique (SIT) to effectively deal with insect pests such as army worms. 
SIT involves rearing large populations of insects that are sterilized through irradiation (gamma or X-rays), and introducing them into natural populations.

 The SIT technique is environmentally-friendly, and has proved an effective means of pest management even where mass application of pesticides have previously failed. Another benefit of this technique is that unlike pesticides which kill important harmless insects such as bees, SIT is able to target an individual insect while posing no threat to others.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images