Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

MNEC SALIM ASAS BADO ANAUMIZWA NA USHINDI WA MBUNGE MSIGWA WA MWAKA 2015

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni jambo ambalo hakulitegemea.
Akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa  ya Iringa Asas alisema kuwa usaliti uliofanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado anakumbuka mara kwa mara.

“Naombeni niongee ukweli kitendo kilichofanywa na wanaCCM wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu” alisema Asas

Asas alisema kuwa uchaguzi huo kulikuwa na wanaCCM wengi ambao mchana walikuwa CCM  na usikuwa walikuwa kwa wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea kushindwa kila siku.

“Unakuta rasilimali zilizokuwa zinatolewa na  CCM zote zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha,sasa hicho kitu ndio ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas.

Asas aliutaka umoja wa wanawake (UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa kishindo kwa kutumia umoja wao.
“Nawaombe muutunze umoja huu ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa inafanyika katika manispaa ya Iringa.
“Ndugu MNEC kwa kweli tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo.
“Mheshimiwa MNEC umoja ambao tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas  akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwabado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015 
 Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakinimjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015

INTRODUCING "AHSANTE" OFFICIAL MUSIC VIDEO BY DRAGON🐉

RC SHIGELLA:WANAWAKE WANA MCHANGO MKUBWA KWA JAMII

$
0
0

 Sehemu ya wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange Jijini Tanga
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akipokea maandamano ya wanawake wakati wa maadhimisho ya siku yao kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa benki ya Amana wakati alipotembelea banda lao kwenye maadhimisho hayo wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (Ras) Mhandisi Zena Saidi

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wanawake

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika maadhimisho hayo.  Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Introducing Wimbo Mpya “Huku” ni Gqom ya Kiswahili

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO MARCH 11,2018

HOTUBA YA MHE DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA BARABARA YA ISAKA USHIROMBO

‘OLE WENU WEZI WA MAJI’-NAIBU WAZIRI AWESO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ametoa onyo kali kwa wezi wa maji na wahujumu wa miundombinu ya maji na kuwataka waache tabia hiyo mara moja kwa kuwa Serikali imechoka kuingia gharama kubwa za utekelezaji wa miradi ya maji na kuhujumiwa.
Hayo yamesemwa wakati alipotembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) wakati akizungumza na Bodi, menejimenti na watumishi wa mamlaka hiyo inayotoa huduma ya maji kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Aweso amesema wizara itaanzisha kampeni kabambe nchi nzima ya kubaini mtandao mzima na wale wote wanaoihujumu Serikali kwa wizi wa maji na miundombinu yake na kuziagiza mamlaka zote nchini kuweka mikakati mizuri ya kudhibiti tabia hiyo.
Amesema miradi ya maji imegharimu fedha nyingi sana ili kuwanufaisha wananchi wote kwa kufuata taratibu za kupata huduma hiyo kihalali na si kinyume na taratibu, akisisitiza kuwa ni haki ya mwananchi kupata maji lakini pia ana wajibu wa kuitunza miundombinu ya maji ili itoe huduma ya uhakika na endelevu.
‘‘Ninatangaza vita na wezi wa maji na wahujumu wa miundombinu ya maji, ole wenu wenye tabia hiyo maana tumechoka kwa kuwa inaturudisha sana nyuma kimaendeleo na nitalivalia njuga suala hili mpaka likome’’, amesisitiza Aweso.
Aidha, Naibu Waziri Aweso ametembelea mradi wa Hoza Salala uliopo Kijiji cha Kibati, wilayani Mvomero, mradi uliokuwa umegubikwa na tuhuma za ufisadi ambapo ameivunja Bodi ya Maji ya mradi huo na kuagiza iundwe mpya baada ya kugundua matumizi mabaya ya fedha kwa wajumbe wa kamati ya bodi.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, Mhandisi Nicholaus Angumbwike kwenye mtambo mpya wa kusafisha na kutibu maji wa Mambogo, Morogoro.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, Mhandisi Nicholaus Angumbwike alipotembelea Bwawa la Mindu, Morogoro.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Sadiq Morad wakiwa kwenye eneo la mradi wa Hoza Salala, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibati, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU

$
0
0

Na Ripota Wetu,Tanganyika

SHILINGI zaidi ya milioni 152 zimetolewa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu  Raphael Mhuga akihutubia wadau wa elimu pamoja na mambo mengine walikutana kwa ajili ya kuchangishana fedha hizo wenye lengo la kusaidia maendeleo ya elimu kwa shule za msingi na sekondari.

Meja Jenerali Mstaafu Muhaga ambaye aliyekiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda Mjini,ametoa mwito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuleta maendeleo.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tangayika Salehe Muhando amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

Mhando ameonya mara kadhaa kuhusu uadilifu katika matumizi ya fedha za umma akifafanua maendeleo hayawezi kuja kama ndoto tu bali uthabiti katika katika kutenda na usimamiaji.Pia Mhando akizungumza mbele ya wadau wa Elimu katika ukumbi wa Idala ya Maji mkoani Katavi amewahakikishia kuwa michango ambayo imetolewa itasimamia wa vema na kutumika kwenye malengo yaliyokusudiwa.


Naye Mbunge wa Jmbo la Mpanda vijijini Suleimani Kakoso ameachangia komputa kwa shule za sekondari,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu, nakuzishauri halmashauri mkoani Katavi kuwashirikisha wadau wa maendeleo walioko ndani na nje ya halmashauri zao ili washiriki kuleta maendeleo katika elimu na nyanja mbali mbali.

Wadau wa elimu ambao wameshiriki wanatoka taasisi za kifedha,wafanyabiashara,madiwani halmashauri ya wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara wilayani Tanganyika,wakulima, pamoja na watu binafsi.

Baadhi ya vitu vilivyochangwa na wadau hao mbali ya fedha ni kompyuta 24 zenye thamani ya Sh.milioni 48,mifuko ya saruji 2281 yenye thamani ya Sh.milioni 41,058,000,vitanda dabodeka 25 vyenye thamani ya Sh. 5,000,000
Malumalu box 200 yenye thamani ya Sh.milioni 5 na 
Bando za bati 1530 zenye thamani ya Sh.30,400,000.

Pia fedha  taslimu Sh.400,000,fedha za ahadi Sh.milioni 17.4,kokoto kubwa tani 14 zenye thamani ya Sh.520,000 na Kokoto Vumbi tan 14 ambazo thamani yake ni Sh.160,000.Mpango huu unatarajiwa kuleta tija kwa ustawi wa elimu katika wilaya hiyo yenye takribani kata 15.
Mkuu wa Wilaya ya Tangayika Salehe Muhando 

MWENYEKITI UWT AMZUNGUMZIA MWANAFUNZI CHUO KIKUU DAR ANAYEDAI AMETEKWA

$
0
0

*Amtaka aache kutafuta kiki kwa staili hiyo,awapa somo vijana wa kitanzania


Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) Gaudentia Kabaka amewataka vijana wote nchini kuacha tabia ya kuichafua Serikali kwa kujifanya wanatekwa kwani madhara yake ni makubwa.

Amesema vijana wa kitanzania wanatakiwa kusoma kwa bidii ili waweze kuisaidia nchi yao katika kuleta maendeleo badala ya kutafuta kiki za kitoto.

Kabaka ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumzia madai ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Abdul Nondo ambaye alitoa taarifa kudai ametekwa na kisha kwenda kutelekezwa mkoani Iringa.

Hata hivyo wakati mwanafunzi huyo akitangaza kutekwa wapo baadhi ya watu waliosafiri naye kutoka Dar es Salaam hadi Iringa kwa kutumia basi la New Force wameelezea namna alivyokuwa amesafiri kwa kujificha ficha uso kwa kujifunika na shuka la kimasai.

Hivyo Kabaka akizungumzia madai ya mwanafunzi huyo amesema ni kitendo kibaya sana mwanafunzi kudai ametekwa wakati anajua anachokifanya na inaonesha hakuwa na nia njema na Serikali.Amesema kuwa amefuatilia taarifa mbalimbali zinazomhusu Nondo na kwa sehemu kubwa zinaonesha alichokifanya ni kutafuta kiki bila kujua madhara yake na anataka kuuaminisha umma kuwa ametekwa na Serikali.Kabaka amemzungumzia hayo baada ya waandishi wa habari kutaka kupata kauli ya UWT kuhusu kitendo alichofanya mwanafunzi huyo na wao kama wazazi wanalichukuliaje.

Hivyo akasema kama wanawake wa Tanzania ambao pia ni wazazi,walezi na wakati mwingine ndio bibi wamesikitishwa na madai ya kijana huyo."Kwanza najaribu kuangalia baada ya kutangaza ametekwa wazazi wake walikuwa kwenye hali gani.Kwa vyovyote walikuwa katika wakati mgumu na hata mimi binafsi niliumia maana najua uchungu wa mtoto.

" Alichokifanya ni kutafuta kiki vijana wa siku hizi kama mbavyo mnasema wenyewe.Kwetu sisi UWT tunaamini kijana anayetaka kutafuta kiki yenye heshima ni kusoma kwa bidii na akihitimu masomo yake awe msaada kwa nchi katika kuleta maendeleo,"amesema.Kabaka amesema vijana ni wakati wa kutambua taifa linawategemea katika kuleta maendeleo hivyo badala ya kujikita kwenye mambo yasiyo na tija wakawekeza nguvu zao katika kusaidia nchi kusonga mbele kimaendeleo.

SORING WOMEN INTERNATIONAL WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2018

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Wanawake wanaweza kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii ikiwa watasimama imara kwa pamoja na kuwezesha wenzao ambao hawana elimu ya kutosha.

Hayo yamesemwa na mapema leo Machi 10, 2018 na Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi wakati akizungumza katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wanawake wanaweza kufanya mabadiliko kwa kila mmoja kuwa imara na kuamsha wanawake wengine ambao hawajafikiwa na fursa zikiwemo cha uchumi au za ubunifu za kuweza

Marsha amasema kuwa kuadhimisha siku ya wanawake lazima kulete mabadiliko sio kuadhimisha tu halafu hakuna matokeo chanya yanayoonekana kwa wanawake tutakuwa hatujatenda haki katika kujipambanua ili kuweza kufikia malengo kwa wale wale walioasisi.
Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi akizungumza wakati wa mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2018 aliyoandaa jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri, Ali Masoud 'Masoud Kipanya'  (katikati) akiwa katika moja waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke katika maadhimisho ya siku wanawake Duniani  leo jijini Dar es Salaam. Kutoka ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura, na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soring Women International, Luphurise Lema (kushoto).
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura (katikati) akichangia mada ya nafasi ya mwanamke katika jamii katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mchoraji wa Katuni na Mtangazaji wa Clouds Radio/TV, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (kushoto)  na Mratibu wa UN Global Compact Network  Tanzania, Emmanuel Nnko (kulia) na Dk. Florence Temu kutoka AMREF (wa kwanza kulia).
 Mchangiaji wa Shirika la AMREF, Dk. Florence Temu akichangia mada katika siku wanawake duniani.
 Mratibu wa UN Global Compact Network  Tanzania, Emmanuel Nnko akichangia mada katika siku wanawake duniani.
Waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke wakiwa katika picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA CHUMA NA PLASTIKI KAHAMA MKOANI SHINYANGA, AZUNGUMZA NA WANANCHI WA TINDE NA IGUNGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kagongwa Kahama mkoani Shinyanga wakati akielekea mkoani Singida 
 Wananchi wa Kagongwa Kahama mkoani Shinyanga wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika eneo hilo wakati akielekea mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha Kahama Oil mills kilichopo Kahama mkoani Shinyanga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda cha Kahama Oil mills kilichopo Kahama mkoani Shinyanga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekalia moja ya kiti kilichotengenezwa na kiwanda cha Kahama Oil mills wakati akikagua bidhaa zinazo tengenezwa kiwandani hapo Kahama mkoani Shinyanga. Pembeni yake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telak.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya mabomba ya plastik yanayo tengenezwa katika kiwanda hicho cha Kahama Oil mills kilichopo Kahama mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha  Kahama Oil mills mara baada ya kukifungua.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Tinde mkoani Shinyanga wakati akielekea mkoani Singida. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Igunga mkoani Tabora wakati akielekea mkoani Singida. PICHA NA IKULU

TANZIA: Munga Shabani Mtengeti afariki dunia

$
0
0
Bi Mwatumu Jasmine Malale wa Regent Estate Mikocheni Dar es Salaam anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Munga Shabani Mtengeti kilichotokea nyumbani kwake Mlingotini Close Regent Estate jijini Dar es salaam  jana tarehe 10/03/2018. 
Mazishi yanatarajia kufanyika siku ya Jumanne baada ya salatul dhuhur nyumbani kwake Bi. Mwatumu Jasmine Malale. Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. 

Inna lillahi wa inna illahi rajiun

TRENI YA ABIRIA RELI YA KATI YA LEO KUONDOKA DAR ES SALAAM KESHO

KUBENEA AWASILISHA MUSWADA WA KUTAKA MABADILIKO YA KATIBA BUNGENI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Ubungo Mhe. Saed Kubenea, amewasilisha bungeni hoja binafsi, kutaka kufanyika mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ili kuruhusu kuundwa kwa “Tume Huru ya Uchaguzi.
Kubenea ambaye leo amewaita Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuwaeleza kwanini ameamua kupeleka muswada huo katika bunge hili linaloanza Aprili 1, 2018.
 Mhe. Kubenea amesema, uchaguzi huru na haki hauwezi kufanyika nchini bila kuwapo na chombo huru cha kusimamia na kuendesha chaguzi hizo.
“Hoja kwamba NEC siyo chombo huru, siyo maneno yangu pekee. Haya yameelezwa vizuri na wanazuoni mbalimbali, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali ambayo iliundwa na Rais wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mwaka 1991.tume hii ya Jaji Nyalali ndio iliyokuja kupendekeza kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi nchini,’’Amesema Kubenea.
 Aliongeza kuwa mwaka 1999, Tume iliyoundwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuratibu maoni ya wananchi kuhusu Katiba ilipigilia msumali mwingine kuhusu muundo wa sasa wa NEC iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga.
Kwenye ripoti ya Jaji Kisanga alisema “hatua ya wajumbe wa Tume kuteuliwa na Rais ambaye pia aweza kuwa kiongozi wa chama cha siasa kinachotawala, katika utendaji wao wa kazi ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika au watakuwa wanalipa fadhila 
 Mbunge wa Ubungo Mhe. Saeed Kubenea akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Hoja yake aliyowasilisha bungeni kutaka iundwe  tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
 Mbunge wa Bukoba Mjini  Mhe. Willfred Rwakatale, akichangia jambo wakati Kubenea alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuwasilisha hoja ya kuwepo kwa tume huru ya Uchaguzi.
 Mbunge wa Moshi Vijini Mhe. Antony Komu  akichangia jambo baada ya Kubenea kuzungumza na Waandishi wa Habari juu kuwasilisha Hoja Binafsi.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioudhuria Mkutano huo 

TANO LADIES YASHEREHEKEA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE BURTONSVILLE, MARYLAND, MAREKANI

$
0
0

Meza kuu toka kushoto ni Janet Kisyombe, Harriet Shangarai, Dr. Sylvia Dasi ambaye ndio mwanzilishi wa Color of Roses Foundation na mwaka 2015 alishiriki na kujitolea kwenda Tanzania kutoa huduma za afya chini ya shirika lisilo la Kiserikali la African Women Cancer Awareness Associatiation na kulia ni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Mhe. Liberata Mulamula ambaye kwa sasa ni Acting Director Institute for African Studies Chuo Kikuu cha George Washington kilichopo Washington, DC, nchini Marekani. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production chini ya udhamini wa Kilimanjaro Studio.

Hawa ndio Tano Ladies walioratibu siku ya kimataifa ya wanawake iliyoadhimishwa rasmi March 8, 2018 Duniani kote na Tano Ladies wao kuisherehekea siku hiyo Jumamosi March 10, 2018 Brtonsville, Maryland na kuhudhuriwa na wanaDMV. Kutoka kushaoto ni Tuma Kaisi Katule, Iska J Kauga, Asha Nyang'anyi, Justa Mtalemwa na Asha Hariz walipokua wakijitambulisha., 

Tano Ladies wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wao.

 Vikundi mbalimbali vya watoto wakitumbuiza kwenye sherehe ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake Duniani.
.
Kushoto ni Dj Maryam White katika picha ya pamoja na mdogo wake.
Wahudhuriaji wakifuatilia kinachoendelea katika siki ya kimataifa ya wanawake iliyoratibiwa na Tano Ladies siku ya Jumamosi March 10, 2018 Burtonsville, Maryland nchini Marekani.


Prof. Palamagamba Kabudi akutana na watendaji wa Wizara na Taasisi zinazounda sekta ya Sheria nchini

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali imefanyia mabadiliko Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuanzisha Ofisi nyingine mbili mpya kwa lengo la kuongeza Tija na Ufanisi katika utendaji kazi.
Prof Kabudi alikuwa akizungumza na watendaji wa Wizara na Taasisi zinazounda sekta ya Sheria nchini makao makuu ya Wizara mjini Dodoma ambao wanakutana mjini humo kujadili na kuandaa makadirio ya Bajeti ya Wizara na Taasisi zake.
Prof. Kabudi amesema  uundwaji wa Ofisi mbili mpya za Ofisi ya Taifa ya Mashitaka  na Ofisi ya Wakili Mkuu unafanya sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kubaki na jukumu lake la msingi la kuishauri Serikali katika masuala yote ya kisheria, kufanyia uhakiki mikataba ya kitaifa na kimataifa na kuratibu wanasheria wote walioko katika Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka, Mashirika ya Umma na Serikali za Mitaa.
Amesema Ofisi ya Taifa ya Mashitaka sasa itajikita katika uendeshaji wa mashitaka ya jinai mahakamani  ikiwa na wanasheria wake wakati Ofisi ya Wakili Mkuu kupitia wanasheria wake itajikita katika uendeshaji  wa mashitaka ya madai ya kitaifa na kimataifa, utatuzi wa migogoro kitaifa na kimataifa na ushughulikiaji wa mikataba ya kitaifa na kimataifa ambayo taasisi za umma zinaingia kwa niaba ya nchi.
amewataka watumishi wa umma  ambao ni wanasheria kuwa tayari na kujipanga kutokana na mabadiliko hayo ambayo yatasababisha uhamisho wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ili kuyatekeleza kwa vitendo yale yote yanayotarajiwa kupatikana baada ya mabadiliko hayo.
Amesema serikali imefikia uamuzi huo ili kuweza kufanikisha azma ya kuwaweka pamoja wanasheria wote na kuwaratibu ili kujua nani yuko wapi na anafanya nini n a kuongeza kuwa wanasheria hao sasa watawajibika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atakuwa na jukumu la kumpeleka mwanasheria yoyote atakayemuona anafaa kufanikisha jambo jema la Serikali.
“Wakuu wa Idara na Vitengo vya Sherioa katika mashirika makubwa ya umma na ambayo Serikali imetoa mabuiloni ya fedha zake ili kuyaendesha wataangaliwa na mwanasheria mkuu na kama akionekana hakamilishi lengo la kuwepo katika ofisi husika basi mara moja atapelekwa mwingine mwenye uwezo wa kuisadia Serikali,” alisema Prof Kabudi.
Akizungumza katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Alderaus Kilangi amewataka watendaji wa ndani ya Sekta ya Sheria kufanya kazi kama timu moja ili kuweza kurejesha imani ya wananchi kwa wataalamu wa sekta hiyo ambayo inapaswa kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
“Niwaombe wanasheria wenzangu tuwe timu moja na tufanye kazi zetu kwa weledi na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha maendeleo ya kweli ya nchi yanafikiwa, ni kweli  kama sekta tulianza kupoteza mwelekeo, tuyachukulie maboresho haya ya miundo ya Ofisi zetu kama chachu ya kuleta tija na ufanisi katika kazi zetu,” alisisitiza
Mkutano huo ulihudhuriwa na watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Tanzania, ofisi ya Mwendesha Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria,Wakala wa Ufilisi na udhamini (RITA), Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo( Law School)Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto    
 Watendaji wa Wizara na Taasisi za Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikilizza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudialipokuwa akizungumza nao mjini Dodoma
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi  akisisitiza jambo wakati alipozungumza na watendaji wa Wizara  na Taasisi zake

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dkt. Adelardus Kilangi akizungumza katika kikao cha watendaji wa Wizara na taasisi zake
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini Bw. Biswalo Mganga akizungumza jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dkt. Adelardus Kilangi baada ya kumalizika kwa kikao cha watendaji wa Wizara na taasisi zake kilichofanyika jana mjini Dodoma.

Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe.

$
0
0
Na Richard Mwaikenda

Tangazo la uuzaji wa mananasi limetolewa na Mkurugenzi Mtandaji wa Mkikita, Adam 
Ngamange, ambaye hivi karibuni ameingia mkataba wa kuuza matunda hayo ndani na nje ya nchi.



Ngamange amewakaribisha Ofisi za Mkikita Dar es Salaam, wadau wenye maeneo ya kuuzia ili wapate utaratibu wa kununua jumla na kuyauza rejareja.

Bei ya mananasi hayo yaliyolimwa ki-organic kila moja huuzwa kwa bei ya kutupa ya sh. 1,200 itakayomwezesha muuza rejareja kupata faida kubwa.
Huduma hii inatarajiwa kuanza Machi 20 jijini Dar es Salaam, ambapo Mkikita imeingia mkataba wa kila wiki kuingiza sokoni nanasi 20,000.

"Hii ni fursa ya kuongeza kipato kwa wanaopenda kuwa wasambazaji na wenye mahoteli. Huu ndiyo mwanzo wa viwanda mkoani Njombe. Ungana na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania kuhamasisha kilimo mkataba," amesema Ngamange.

MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO

$
0
0


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kada wake marehemu Mzee Abdulrazaq Mussa Simai 'Kwacha' aliyefariki  leo Machi 11,20118.

Mzee  Abdulrazaq  amefariki katika  Hospitali ya Kuu ya Taifa ya Muhimbili, iliyopo  Jijini Dar es salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika Salamu hizo Dk. Mabodi amesema CCM imepokea taarifa ya kifo hicho kwa mshutuko mkubwa na uzuni ya hali ya juu, kutokana na  marehemu Abdulrazaq alikuwa mwadilifu kwa Chama chake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote wa uhai wake, na amemtaja kuwa ni miongoni mwa Wana ASP aliyeyalinda na kuyathamini Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo.

Kupitia salamu hizo Dk. Mabodi amewaomba  familia ya marehemu, Wanachama, Viongozi na Watendaji wote wa CCM, Marafiki, Ndugu  na Jamaa wote walioguswa na msiba huu kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu  na kuendelea  kumuombea dua.

Enzi za uhai wake Abdulrazaq amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ikiwemo Katibu Maalumu wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.

Marehemu amezikwa leo katika kijiji cha Paje wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, amefariki akiwa na umri wa miaka 98 ameacha watoto watano  na  kizuka mmoja.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili leo katika maziko ya MarehemuMzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM   katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali leo katika kumswalia  Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM   katika  Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka udongo kaburini wakati wa maziko ya  Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) baada ya kumswalia katika  Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
 Maelfu ya Wananchi kutoka sehemu mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara walijumuika katika maziko ya Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha)  yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje   Wilaya ya Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ( kulia) alifika kuwapa mkono wa pole Wanafamilia ya   Marehemu  Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM  Nyumbani kwao baada ya mazishi yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja. Picha na Ikulu.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA KUSINDIKA NA KUZALISHA MAFUTA YA ALIZETI CHA MOUNT MERU MILLERS KILICHOPO MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria ufunguzi wa  kiwanda kikubwa cha Kusindika na kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers kilichopo mkoani Singida. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu tisini za mafuta ya alizeti kwa mwaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda hicho kikubwa cha kusindika Alizeti cha Mount meru millers kilichopo mkoani Singida. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba, mmiliki wa Kiwanda hicho Atul Mittal mwenye nguo nyeupe na  Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenda kukagua shughuli mbalimbali za kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti kilichopo mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na viongozi wa Kidini kutoka Singida mara baada ya kufungua kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Atul Mittal mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti mkoani Singida. PICHA NA IKULU

Introducing "WASHA" by Silvabel

Viewing all 109973 articles
Browse latest View live


Latest Images