Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

Mshindi wa Kampeni ya Malengo ya NBC wa Dar aondoka na kirikuu yake.

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theoblad Sabi (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kabla hajakabidhi zawadi ya gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ yenye thamani za zaidia ya shs miliono 30 kwa mshindi wa kampeni ya Malengo ya NBC, Fatuma Saidi Ramadhani (kulia). Alisema moja na malengo la kapeni hiyo ni kuhamasisha wateja na wasio wateja kujiwekea akiba katika benki hiyo ili kutimiza malengo. 
 Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni ya Malengo ya NBC, Fatuma Saidi Ramadhani akihojiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akikabidhi  kadi ya gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’  kwa Fatuma Saidi Ramadhani,  mmoja wa  washindi  sita wa kampeni ya  Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam jana. Anayeangalia ni Mkurugemnzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Filbert Mponzi. Kampeni hiyo ilidumu wa muda wa miezi mitatu.
Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni yas Malengo ya NBC, Fatuma Saidi Ramadhani (katikati), akionyesha kadi ya gari lake baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto).  Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Filbert Mponzi na baadhi ya familia ya mshindi huyo.  

DED Kishapu asisitiza uwajibikaji kwa walimu

$
0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga amesisitiza uwajibikaji kwa walimu ili kuleta ufanisi mkubwa katika sekta ya elimu.

Magoiga alitoa msisitizo huo wakati akikabidhi vyumba viwili vya madarasa kwa shule ya sekondari Maganzo wilayani humo vilivyokamilika vyenye thamani ya sh. milioni 19.4.Vyumba hivyo ni sehemu ya mradi uliotekelezwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na fedha ambazo zilitolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Alisema kuwa endapo walimu hao watawajibika ipasavyo wanafunzi watafanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuleta sifa nzuri katika shule pamoja na wilaya nzima kwa ujumla.Mkurugenzi Mtendaji aliongeza kwa kusema kuwa kampeni ya kufuta ziro yaani sifuri inayoendelea itaweza kupata mafanikio makubwa kama walimu watajituma katika kufundisha vizuri.

Aidha aliwataka wanafunzi kujituma na kutumia fursa ya kuwepo shuleni kwa ajili ya kusoma kwa bidii na kufaulu masomo yao hivyo kuweza kuwa watalaamu wa baadaye kwa manufaa ya jamii.

Itakumbukwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ilipata ufadhili wa fedha TEA jumla ya sh. milioni 70.5 kati y ash. milioni 141 kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa miundombinu katika shule hiyo.
Kwa kutumia fedha hizo pamoja na kushirikisha nguvu za wananchi inaendelea na ujenzi wa nyumba ya walimu sita, choo cha matundu 2 cha walimu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mwenye tai) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Maganzo wakati alipozindua vyumba vya madarasa vilivyokamilika.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akifungua moja ya vyumba vya madarasa vilivyomalika ujenzi wake wakati akivikabidhi kwenye shule ya sekondari Maganzo.
 Walimu, wajumbe wa bodi ya shule na wanafunzi (hawapo pichani) wa shule ya sekondari  Maganzo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (aliyesimama) wakati alipozungumza alipowakabidhi vyumba vya madarasa.
 Sehemu ya jengo lenye chumba cha darasa la shule ya sekondari Maganzo lililokamilika ujenzi wake na kukabidhiwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKURUGENZI WA UNIDO AWASILI TANZANIA KUUNGA MKONO MAENDELEO YA VIWANDA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Blogu ya Jamii
Serikali imesema kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) limekubali kushirikiana na serikali ya Tanzania katika ukuzaji na uendelezwaji wa viwanda nchini.

Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akimpokea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), LI Yong.

Mwijage amesema kwamba katika muda mfupi aliozungumza na Mkurugenzi huyo amesema kwamba yuko tayari kushirikiana na Tanzania katika ukuaji wa viwanda nchini na kuitangaza nchi yetu kimataifa ili kuvutia wawekezaji.

Mwijage amesema kuwa UNIDO imefanya vizuri katika nchi mbalimbali hivyo alichokifanya katika nchi zingine ndicho atakachokifanya Tanzania katika maendeleo ya viwanda vya kuzalisha bidhaa bora na sio mali ghafi.

Amesema kuwa ujio wa bosi wa UNIDO ni sehemu ya kutangaza bidhaa kuweza kupata masoko nje ya nchi na sio wakati wa sasa kupeleka mali ghafi.

Mwijage amesema katika kipaumbele kilichopo ni kuweka viwanda vya kutengeneza mafuta ya kula pamoja na viwanda vya nguo ambapo mali ghafi zote zinapatikana nchini.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, LI Yong amesema kuwa katika ziara hiyo kuna vitu vingi atajifunza kwa nchi ya Tanzania kwa hatua iliyofikiwa katika uendelezwaji Viwanda.

Katika ziara hiyo atafanya mazungumzo na Viongozi wakuu wa Serikali kwa Tanzania bara na Zanzibar pia kufanya mazungumzo na Sekta binafsi nchini ikiwa ni sehemu ya kusukuma maendeleo ya viwanda kwa kasi.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, leo tarehe 7 Machi, 2018 jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watendaji wa UNIDO pamoja na watendaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya nje, ushirikiano wa kikanda na kimataifa wakimpokea Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, LI Yong(kushoto) mara baada ya kuwasili.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage(kushoto)  akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, LI Yong(kulia) mara baada ya kuwasili nchini leo.

WAZIRI UMMY KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI RUKWA

WAZIRI UMMY AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI ILEJE, AFUNGUA KITUO CHA AFYA NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

$
0
0

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akitoa udongo wakati wa  uchimbaji wa msingi katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mtura kilicho katika kata ya Lubanda Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akielekea eneo la gari lililokwama kutokana na changamoto ya Barabara, wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Kheri Kagya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje na watumishi wa Serikali (hawapo kwenye picha) wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.
 Wananchi wa kata ya Lubanda katika kijiji cha Mtura wilaya ya Ileje wakimsalimia Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu

SERIKALI YATENGA BILIONI TATU UJENZI WA BARABARA YA MUHEZA-AMANNI MKOAN TANGA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Tanga

SERIKALI imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 39 kutoka mjini Muheza hadi Amani wilayani humo, kwa kiwango cha lami. 

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbalo alisema fedha hizo zimetengwa kama utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwaka jana kwamba barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami. 

Ndumbalo alisema nia ya serikali ni kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na fedha zilizotengwa zinatokana na bajeti ya Mwaka huu."Tayari serikali imetenga fedha hizo na wiki iliyopita Naibu Waziri wa Ujenzi (Elias Kuandika) tulimpeleka Muheza na pia amewahakikishia wananchi kwamba barabara hiyo tayari imetengewa fedha hizo," alisema Ndumbalo. 

Meneja huyo alisema kuwa wanachosubiri kwa sasa ni kupewa maagizo na wizara kuhusu ama kutangaza zabuni ili ujenzi uanze au vinginevyo kwa kuwa tayari wamemaliza kazi ya upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa barabara hiyo tangu mwaka jana. 

Ndumbalo alisema kwamba mkoa wa Tanga una kilomita zipatazo 327 za barabara kuu na kilomita 171 za barabara za vijijini zilizojengwa kwa kiwango cha lami, hivyo kujengwa kwa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa Kwa wananchi hasa wanaoishi tarafa ya Amani ambayo jiografia yake ni ya milima.

Barabara hiyo ambayo ilikuwa haipitiki kwa uraisi Mwaka 2011 Rais Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi aliipatia fedha ambazo zilitumika kujenga zege Kwenye maeneo yenye kona kali na hatarishi, kiasi ilipunguza adha ya magari kukwama na sasa ikijengwa lami itasaidia wananchi wa tarafa hiyo ambao ni wakulima wa viungo vya chai na Chakula na wauzaji wakubwa wa vipepeo nje.

Meneja wa Wakala wa barabara mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbalo

UVCCM KIGOMA WAMLILIA KABOROU

$
0
0
Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma


Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoani Kigoma umepokea kwa masikitiko na huzuni taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa Kigoma Dk Walid Amani Kaborou aliyefariki usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Katika salamu za rambirambi toka Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Kigoma Sylivia Sigula kwenda kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa kigoma Ammandus Nzamba , UVCCM wameelezea kusikitishwa kwao na kifo cha kiongozi huyo mkoani humo.

Sylivia amemuomba Mwenyekiti wa ccm mkoa kigoma awafikishie salamu zao za zarambirambi na mkono wa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu na jamaa na kuwataka wawe na moyo wa subira na ustahamilivi kwa wakati huu

Aidha Mwenyekiti huyo wa UVCCM amemtaja marehemu Dk kabourou katika maisha yake amekuwa kiongozi aliyetawaliwa na busara, hekima, maarifa mapana na mwenye upeo mkubwa katika medani za siasa na historia ambapo mara zote amekuwa zaidi ya mwalimu kwa vijana.

"Chama chetu kimepoteza kiongozi wake bora, msikivu na mjuzi katika masuala ya siasa na maendeleo ya demokrasia .Tunamuomba mungu mtukufu ampokee, amsaheme dhambi zake na amuweka mahali pema peponi"Alieleza Sylivia kwenye tanzia yake kwenda kwa Mwenyeliti wa CCM Mkoa Kigoma .

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amesema jumuia yake mkoani humo itaendelea kujifunza mambo yote mema na mazuri yaliokuwa yakifanywa na Dk Kabourou wakati wa uhai wake na jinsi alivyokuwa mahiri katika kujenga hoja na kujibu mapigo ya kisiasa .

Sylivia ameeleza mwili wa marehemu Dr. Walid Kabourou utasafirishwa kutoka dar es salaam kuelekea kigoma kesho saa nne asubuhi. Mazishi yamategemewa kufanyika Tarehe 9 Machi 2018, siku ya Ijumaa, katika msafa wa makaburi ya Kipampa shule ya ujiji. Mwenyekiti anawaomba wanakigoma na wanaccm kwa ujumla tushiriki kwa pamoja katika kumpumzisha mzee wetu katika nyumba yake ya milele. Msiba utakua nyumbani kwa marehemu huko Bagwe, Kigoma Mjini.

Inna lilahi wa Inna Ileiyhi Rajiun .
Imetolewa na,
Mwenyekit wa vijana mkoa wa kigoma.

MBUNGE AZINDUA MRADI USAMBAZAJI MBEGU ZA VIAZI LISHE

$
0
0

Na Allan Ntana, Urambo

MBUNGE wa jimbo la Urambo Mkoani Tabora Magreth Sitta amezindua mradi wa ugawaji na usambazaji mbegu za zao la viazi lishe linalosimamiwa na Mradi wa ‘Sambaza Marando Fasta’ wilayani humo.

Akikabidhi mbegu hizo jana Sitta alisema mradi huo unaoratibiwa na Shirika la ANSAF la jijini Dar es salaam ni muhimu sana kwa sababu ya urahisi wake na manufaa makubwa watakayopata wananchi kwa kuzalisha zao la viazi lishe.Alisema semina iliyotolewa na Shirika hilo bungeni mjini Dodoma ilimhamasisha kuleta mradi huo kwa wananchi wake jimboni na mwezi Desemba mwaka jana alianzisha shamba la zao hilo lenye ukubwa wa ekari 2 ili kuzalisha mbegu hizo.

‘Nawashukuru sana ANSAF na Kituo cha Utafiti wa Mazao Ukiriguru kwa kufanikisha mradi huu hapa Urambo, sasa mbegu zipo tayari na leo tunazigawa bure kwa vikundi vya wakulima wa kata zote 18 jimboni kwangu’, alisema.Alisema atahakikisha mbegu hizo zinazalishwa kwa wingi na kusambazwa katika vijiji vyote jimboni kwake na wilayani nyingine za mkoa huo ili zao la viazi lizalishwa kwa wingi sana katika mkoa huo ili kumwinua kiuchumi mwananchi.

Afisa Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru cha jijini Mwanza Rahila Amour aliwataka wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani kuchangamkia mradi huo kwa kuwa una faida nyingi na mbegu zinapatikana kwa urahisi mno, alibainisha mbegu zilizopo kuwa ni Kabode, Kakamega na Mataya.Alisema Mradi huo unafadhiriwa na Shirika la Bill and Melinda Gates Foundation la nchini Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya ANSAF ya jijini DSM, Wizara ya Kilimo na Chakula na Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Ukiriguru-Mwanza.

Mtafiti Mwenza kutoka Kituo cha Ukiriguru Eric Chang’a alisema zao la viazi ni muhimu sana kwa sababu ni lishe nzuri (chakula), linaongeza mapato na ni kinga dhidi ya upofu, hivyo akawataka wananchi wengi zaidi kuchukua mbegu hizo.Alisema mbegu hiyo imefanyiwa utafiti wa kina na Wataalamu wa Ukiriguru na kujiridhisha kuwa ni mbegu bora inayopaswa kulimwa na wakulima wote hapa nchini kwa kuwa inachukua muda mfupi sana takribani miezi 3-4kutoa viazi.

Baadhi ya Madiwani waliokuwepo katika tukio hilo Elizabet Mkwenda na Blandina Magupa walimpongeza mbunge wao kwa kuleta mradi huo na kuamua kuzalisha mbegu na kuzigawa bure kwa wananchi wake.Shughuli ya uzinduzi wa Mradi huo ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Kanda wa Kituo cha Utafiti Ukirigiru Dr Everine Lukonge, Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora, Wataalamu Watafiti kutoka Ukiriguru, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa na mwenzake wa wilaya na viongozi wa UWT wilaya.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Vikundi wa Wakulima kutoka kata 18 za wilaya hiyo baada ya kuwakabidhi mbegu za viazi ili wakazismabaze. Picha na Allan K

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

Kauli Mbiu: Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini. 

Leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mimi kama mwanamke na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini. 

· Serikali inayo Sera ya kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi. 

· Sera ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni. 

· Kuboreshwa kwa huduma za kijamii kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo. 

· Usambazaji umeme vijijini kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato. 

· Uwezeshaji wa Wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za halmashauri kumewawezesha wanawake wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato . 

· Serikali kuendelea kuhimiza taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo. 

· Kurasimisha vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo. 

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 8, 2018

SERIKALI YAFUNGA KIWANDA KWA SIKU 14 NA KUVITOZA FAINI YA JUMLA YA SH. MILIONI 40.8 VINGINE VITATU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SERIKALI imesitisha shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba), cha TASIPA kilichoko jijini Dar es Salaam kwa siku 14 kuanzia leo Machi 7, 2018 baada ya kubainika kuwa kiwanda hicho kinahatarisha maisha ya wafanyakazi wake.

Sambamba na hilo, kiwanda hicho pia kimetozwa faini ya shilingi milioni 18 kwa kukiuka sheria ya usalama na afya mahala pa kazi. Aidha Mhe. Mavunde pia amevitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 22.8 viwanda vya Hengji Investment, ambacho pia kinatengeenza viroba (mifuko ya nailoni), na kiwanda kingine cha kutengeneneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited kwa makosa mbalimbali ya kukiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini.

“Katika kukagua Sheria za usalama na afya mahala pa kazi, tumebaini kuwa mazingira ya kiwanda hiki cha TASIPA ni hatarishi mno kwa mfanyakazi kufanya kazi na tayari watu wa OSHA walikwishafika hapa na kutoa maelekezo, lakini hakuna kilichofanyika.” Alisema Mhe. Mavunde.

Naibu Waziri pia aliagiza kuwa muajiri huyo kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wote kwa mujibu wa sheria namba 6 ya mwaka 2004 na mikataba iwe imekamilika n dani ya siku 14 na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi ili aipitie.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited leo Machi 7, 2018, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
Kwa mujibu wa sharia ya usalama mahala pa kazi mfanyakazi huyu alipaswa kuvaa mask na gloves. hapa ni kiwanda cha TASUPA kinachotengeneza mifuko ya nailoni (viroba)
Naibu Waziri Mvunde akishuhudia ukiukwaji wa sharia ya usalama mahala pa kazi kiwanda cha TASUPA
Naibu Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).

NIDA KUZINDUA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KIGOMA, RUKWA NA KATAVI

$
0
0
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)  inatarajia kuzindua usajili na utoaji wa  vitambulisho hivyo katika mikoa mitatu ya Katavi, Kigoma na Rukwa.

Pia  NIDA  kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini , imeanza  kuwasajili watu wote watakaoishi, kufanya kazi au biashara ndani ya eneo lililozungushiwa ukuta lenye madini ya TANZANITE huko Mererani mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, leo, Kaimu Ofisa Uhusiano  wa NIDA,  Rose Joseph, alisema   mpaka sasa mamlaka hiyo imaendelea  na  usajili na utoaji vitambulisho vya  uraia  katika mikoa 20.

“Hivi karibuni tutafanya uzinduzi katika mikoa mitatu iliyobaki ambayo ni Kigoma,  Rukwa na Katavi . Wananchi katika mikoa hii watakuwa na muda wa miezi mitatu wa kujisajili,  na hivyo  tutakuwa  tumeifikia nchi nzima,”alisema Rose.Ofisa huyo alisema  pia NIDA taangu Novemba   mwaka uliopita  ilianza  usajili wa mkupuo katika mikoa mbalimbali   na muda ulikuwa ukiongezwa  kadri ilivyokuwa uinaruhusu.

“Tayari baadhi ya mikoa imemaliza kazi ya kusajili  kwa mkupuo ikiwemo mikoa ya Mara na Iringa,”.alieleza  Rose.Alisema  katika kazi hiyo ya usajili NIDA kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji  wanapeleka  maofisa hadi  ngazi ya kata na vijiji,  ili  kuhakikisha  kazi hiyo inakwenda kwa mchujo sahihi na wale wote wanaosajiliwa wawe na sifa  na vigezo kuwa raia  wa Tanzania. “Tunasajili  vitambulisho vya aina tatu ambavyo ni vya uraia, mkimbizi na mgeni na kumekuwa na ufanisi mkubwa,”alifafanua ofisa  uhusiano huyo.
Kaimu Ofisa Uhusiano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Rose Joseph akielezea mikakati ya kuzindua usajili wa vitambulisho Kigoma, Rukwa na Katavi sambamba na ndani ya mgodi wa Tanzanite.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

RAIS WA TFF NDUGU KARIA ATUMA SALAMU ZA POLE CYPRUS

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za pole kwa Chama cha Mpira wa Miguu Cyprus kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Rais wa FA Costakis Koutsokoumnis.

Rais wa TFF Ndugu Karia amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wakongwe wa mpira wa Miguu.

“ Koutsokoumnis alikuwa muhimiri mkubwa kwa soka la Cyprus na amefariki katika wakati ambao Cyprus na mpira kiujumla ulikuwa unamuhitaji,nimesikitishwa na kifo chake na ninatoa pole kwa familia yake,FA ya Cyprus,FIFA na familia ya soka kwa ujumla” Alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Mpaka mauti yanamkuta Koutsokoumnis alikuwa ndio Rais wa FA ya Cyprus na amekuwa kwenye kamati mbalimbali za FIFA akiwa Makamu Mwenyekiti na alianza kutumikia soka la Cyprus tokea mwaka 1990.

Amewahi kuwa Makamu wa Rais wa FA ya Cyprus kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa FA hiyo mwaka 2001 nafasi aliyoitumikia mpaka mauti yanamkuta.

Koutsokoumnis amefariki Machi 5, 2018 akiwa na miaka 61 baada ya miezi kadhaa ya kupigana kupona ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua.

MIRADI YA AJIRA YA MUDA INAYOTEKELEZWA NA TASAF WILAYA YA BUKOMBE,GEITA YAWANUFAISHA WANANCH KIUCHUMI.

$
0
0
NA ESTOM SANGA-GEITA.

Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wameipongeza serikali kwa kuanzisha utaratibu wa miradi ya Ajira ya Muda huo ambao wamesema licha ya kuinua kipato chao lakini pia unawaongezea hamasa ya kushiriki katika kazi za maendeleo kwenye maeneo yao.

Chini ya Utaratibu huo wa Ajira ya Muda,Walengwa wanaotoka katika Kaya Maskini huibua miradi,kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya Serikali kupitia TASAF kuongeza kipato na ujuzi cha Kaya za Walengwa.

Kupitia utaratibu huu wa ajira ya muda,walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya ya Bukombe wametekeleza miradi kadhaa ikiwemo kilimo bora cha pamba, uchimbaji wa malambo ya maji na upandaji wa miti.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Malighasi katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe ,Samweli Nyelu amewaambia Waandishi wa habari wanaotembelea mkoa wa Geita kujifunza namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusu Kaya Maskini kuwa wananchi wananufaika na huduma ya malambo ya maji yaliyochimbwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda na kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la uhaba wa maji kwao na mifugo yao lililokuwa linawakabili kabla ya kuanza kwa Mpango hu.

Baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Malighasi katika halmashauri ya wilaya ya Mbogwe wakiwa katika shamba la Pamba walilolilima kwa utaratibu wa Ajira ya Muda kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakitoa maelezo kwa Waandishi wa habari namna walivyoshiriki kazi ya ajira ya muda kwa kulima hekari tatu za pamba.
Mojawapo ya malambo yaliyochimbwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Waandishi wa habari wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Malighasi halmashauri ya wilaya ya Bukombe ,Samweli Nyeli kazi ya uchimbaji wa lambo ilivyofanywa na Walengwa wa TASAF na jinsi inavyowanufaisha wananchi wote kijijini hapo.
Ng’ombe wakinywa maji kwenye lambo lililochimbwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda katika moja ya vijiji vya halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

TANZIA: DKT AMAN WALID KABUROU

$
0
0
Inna lillah wainna Illah rajiun.Poleni wana Ujiji poleni wana Kigoma poleni wana CCM na poleni Watanzania.

Ilikuwa alfajiri ya leo saa 12.37 asubuhi nilipopokea simu kutoka rafiki na ndugu yangu Ahmed Maaruf Byemba almaarufu Yaounde. Alianza na kauli niliyoanza nayo hapo juu. 

Nikajua yametimia kwani ndugu yangu huyo anamuuguza mdogo wake kule Dodoma hivyo nikaelewa mgonjwa wake amefariki. Haikuwa hivyo bali alikuwa ananifahamisha kuwa Dk. Aman Walid Kaburou hatunae tena.

Niliduwa japo sikushangaa kwani taarifa za ugonjwa nilikuwanazo na hata taarifa za kupekekwa Muhimbili kutokea hospitali ya Maweni Kigoma nilikuwanazo na ndio maana sikushangaa. Ila niliduwaa kutokana na ninavyomfahamu Dk Kaburou. Nina historia nae.

Baada ya kupata maelezo toka kwa ndugu Yaounde nakuondokana na mduwao uliokuwa umenipata niliendelea kupata simu kuhusiana na kufariki kwa Dk Kabourou kutoka kwa ndugu wengine, hususan wana Ujiji.

Kifo cha Dk Aman Walid Kabourou kimenirejesha kifikra zaidi ya miaka 68 tokea sasa tukiwa watoto hadi kipindi cha kuanza elimu ya msingi. Mimi nilikisoma Ujiji Government Town School na Aman akiwa Kipampa Lower Primary School.

Sote tulikutana Kipampa Middle School mwaka 1962.Tulisoma hapo kwa miaka minne hadi tulipohitimu darasa la nane mwaka 1965 na kujiunga na elimu ya sekondari pale Livingstone College mwaka 1966.

Kifo cha Dk Kabourou kimenikumbusha mikimiki ya pale Livingstone hadi kusababisha kukatiza masomo tukiwa tumehitimu kidato cha tatu tu. Hapa leo sio mahala pa kuelezea hiyo mikimiki bali kumuomboleza Dk Aman Kabourou.

GGM NA SERIKALI GEITA YATILIANA SAINI MAKUBALIANO FEDHA HUDUMA ZA JAMII.

$
0
0
NA JOEL MADUKA-GEITA.

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGM) pamoja na Halmashauri mbili za Wilaya na Mji wa Geita zimetia saini ya Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja kuhusu Matumizi ya fedha za Huduma za Jamii zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa mwaka 2018.

Saini ya Makubaliano hayo inafuatia kutokana na marekebisho ya Sheria Mpya ya Madini iliyopitishwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kufanya mageuzi kwenye utekelezaji wa Fedha za Miradi ya Huduma za Jamii baina ya Kampuni za Uchimbaji Madini na Jamii kwenye eneo husika. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema Serikali mkoani humo imekusudia kuanzisha miradi mipya ikiwemo kiwanda cha sukari kutokana na mapato yanayotolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM baada ya kuingia mkataba upya na halmashauri ya mji na wilaya ya Geita.

Aliongeza kuwa fedha zilizokwisha kutolewa na GGM kwa mwaka huu ni Bilioni tisa pointi mbili (B 9.2) ambapo fedha hizo zitatumika kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wawezesha wananchi kujikwamua na umasikini, ikiwemo kiwanda cha sukari ,afya elimu na mazingira.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakikabiana hati ya makubaliano ya miradi ya jamii na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso baada ya zoezi la Saini ya Makubaliano. 
Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri mbili ya mji na wilaya ya Geita wakisaini makubaliano.(katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso. 
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi aweka saini kwenye hati ya makubaliano ya miradi kwenye halmashauri mbili ya mji na wilaya. 
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola. 
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga.


SHUWASA YATOA ELIMU YA MAJI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imeendesha semina kwa wanawake wa manispaa ya Shinyanga kuwapa elimu kuhusu utoaji huduma ya maji safi na usafi wa mazingira.

Mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika leo (jana) Jumatano Machi 7,2018 katika ukumbi wa Shinyanga Vijana Centre Mjini Shinyanga alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.

Akifungua semina hiyo,Matiro aliushukuru uongozi wa SHUWASA kwa kuthamini umuhimu wa akina mama katika jamii akieleza kuwa akina mama ni muhimili mkubwa katika malezi ya familia na jamii lakini pia ndiyo walengwa wakubwa wa huduma ya maji katika maisha ya kila siku.

"Kwa kuzingatia kauli mbiu ya kitaifa ya mwaka huu inayosema 'Kuelekea uchumi wa viwanda: Tuimarishe usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake vijijini',ni dhahiri kuwa taifa limetambua nafasi ya mwanamke katika jamii,SHUWASA nawashukuru kwa kuwapa kipaumbele akinamama katika uendelezaji na usimamizi wa mipango na mikakati ya huduma ya maji safi",alisema.

"Akina mama ni nguzo muhimu sana katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za maji kwani huduma ikiwa dhaifu,waathirika wakubwa wa hali hiyo ni akina mama na watoto hivyo ni vyema wadau wote tukashirikiana kutatua changamoto zinazojitokeza",aliongeza Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua semina ya wanawake wa Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA kama moja ya matukio ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Akina mama wa Manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Joyce Egina akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa semina hiyo, Ziphora Pangani (Mkuu wa wilaya mstaafu) akiongoza kipindi cha majadiliano wakati wa semina.

TARURA KUIFANYIA MATENGENEZOBARABARA YENYE UREFU WA KILOMETA 241.71 RUKWA

$
0
0
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mkoani Rukwa wamesaini mikataba na wakandarasi 18 wa hapa nchini ili kufanyia matengenezo ya barabara za urefu wa kilometa 241.7 mkoani humo zitakazogharimu shilingi Bilioni 2.8.

Kati ya urefu huo barabara za kiwango cha lami kitakuwa ni km 1, changarawe km 77.91, udongo km 163.8 na kuweka alama za barabarani 123, ambapo pia kuna jumla ya vivuko 66 vitakavyotengenezwa vikiwa ni “drifts” 1 na makalavati ya aina mbalimbali 65.

Katika kutekeleza hilo TARURA ilizingazia kutoa kipaumbele kwa wakandarasi waliomo Mkoani Rukwa, na kati ya wakandarasi 18, 12 ni wakandarasi wa mkoa wa Rukwa ambao wanafanya asilimia 67 ya wakandarasi wote.

Awali akitoa hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa Benard Makali ameasa kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa kazi zinazofanyika ili zifanyike kwa kiwango kinachokubalika na kuhakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kuwawezesha wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati.

“Serikali iko macho na haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atakayebainika kuwa ameenda kinyume na matarajio ya serikali hii ya awamu ya Tano na kuuchafua Wakala huu na Serikali kwa ujumla kwa vitendo visivyo vya kimaadili.” Makali alisisitiza.
 Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali akikabidhi mmoja wa mkataba kwa mmoja wa Wakandarasi hao Luis Mamba muda mfupi baada ya kusaini mikataba hiyo. 
  Mwanasheria wa TARURA Mkoa wa Rukwa, Jery Simon akisaini miongoni mwa mikataba 18 iliyosainiwa na kukabidhiwa kwa wakandarasi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


BITEKO AIPONGEZA KAMPUNI YA MZAWA YA NYAMIGOGO

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameipongeza Kampuni ya Mzawa ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd inayojishughulisha na uchenjuaji dhahabu kwa kuthubutu kuanzisha mradi huo na aliahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kuona manufaa zaidi yakipatikana.

Alitoa pongezi hizo Machi 6, 2018 alipofanya ziara kwenye mgodi huo uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita ili kujionea shughuli ziazoendelea sambamba na kuzungumza na watendaji wake.

Biteko aliitaka kampuni hiyo kuendelea kufuata maelekezo ya Serikali ikiwemo kufuata sheria, kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali sanjari na kutunza takwimu za uendeshaji wa shughuli zao kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

Mara baada ya kupokea taarifa ya mgodi huo, Biteko aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi huo ikiwemo suala la maeneo ya uchimbaji na upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme.

“Suala la umeme nitalifikisha; tunahitaji kuona maendeleo. Tunahakikisha tunaandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji wote wa ndani na nje,”  alisema Biteko.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akikagua eneo linalojengwa mitambo ya kusagia mawe kwa ajili ya kuchenjua dhahabu katika mgodi wa Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) alipofanya ziara kwenye mradi wa kuchenjua dhahabu wa Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hussein Amar.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd Hussein Amar (kushoto) akielezea mtambo wa kuchenjulia dhahabu wakati wa ziara yake kwenye mradi wa kuchenjua dhahabu wa kampuni hiyo.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) alipofanya ziara kwenye mradi wa kuchenjua dhahabu wa Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hussein Amar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images