Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live

Mjumbe wa Baraza la Biashara la Ubeligiji na Luxembourg Bwana Christian Verbrugghe amtembelea Balozi Dr Kamala ofisini kwake Brussels

$
0
0
Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Biashara la Ubelgiji na Luxembourg Bwana Christian Verbrugghe (aliyeshika kabrasha) akimweleza Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Kamala maandalizi ya ziara ya  Wafanyabiashara na Wawekezaji  wa Ubelgiji na Luxembourg inayotarajiwa kufanyika Tanzania. Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kwa kushirikiana na Taasisi ya Uwekezaji ya Ubelgiji, Taasisi ya Uwekezaji Tanzania na Baraza la Wafanyabiashara la Ubelgiji na Luxembourg wanaadaa ziara hiyo.

DSTV sasa kuja na mambo mapya katika kipindi cha msimu wa soka

$
0
0
 Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Ronald Baraka Shelukindo (kulia) akitoa maenezo ya huduma mbali mbali zinazorushwa na Televisheni yao ya DStv pamoja na huduma ya soka katika msimu mpya wa ligi mbali mbali Duniani mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kwenye ukumbi wa Mikutano ya Hoteli ya New Afrika,jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Furaha Samalu,Meneja Mauzo,Salum Salum pamoja na Meneja Uhusiaono wa Kampuni hiyo,Barbara Kambogi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu (kushoto) akifafanua jambo mbele ya mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kwenye ukumbi wa Mikutano ya Hoteli ya New Afrika,jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiaono wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akieleza ubora wa huduma hivo mpya.
Sehemu ya Waandishi wa Habar toka vyombo mbali mbali wakifuatilia mkutano huo.

Mama Kikwete awataka wanawake nchini kuishi maisha ya upendo

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo

Wanawake nchini wametakiwa kuishi maisha ya upendo, umoja na mshikamano bila ya kuangalia itikadi zao za dini na vyama vya siasa hatua itakayosaidia kuimarisha hali ya amani na utulivu.

Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya wanawake viongozi na wake wa viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam .

Mama Kikwete alisema hakuna dini hata moja inayowafundisha watu kuishi maisha ya chuki bali dini zote zinasisitiza kuishi kwa amani, umoja, na upendo jambo ambalo litamfanya binadamu aweze kumfikia Mwenyezi Mungu.

“Bila ya kuangalia itikadi zetu tulizonazo, sisi kama viongozi na wake wa viongozi tutumie nafasi tuliyonayo kuzungumza kwa vitendo maneno matatu ya upendo, amani na mshikamo ili jamii yetu iweze kuiga mfano kutoka kwetu”, alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Rose Migiro alimshukuru Mama Kikwete kwa ajili ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao ambayo imewafanya waweze kukutana kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo.

Dk. Migiro alisema kuwa hivi sasa watu wote wanatakiwa kuliombea taifa amani na salama pia Mwenyezi Mungu awajalie viongozi wote busara, afya njema na mshikamoano ili waweze kuongoza watu vizuri na kwa amani.

Waziri Nagu atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Maonesho ya Wakulima NaneNane mjini Dodoma leo

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (MB) Kulia akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Palangyo wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu leo katika Maonesho ya Wakulima NaneNane yanayoendelea Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (MB) akisoma Mwongozo wa Ufuatiliaji Tathmini na Utoaji Taarifa za masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi uliondaliwa na Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu leo, kulia ni Bw. Girson L. Ntimba Mchumi Mwandamizi Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji. Picha zote na Waziri Mkuu

TAARIFA YA SIKUKUU YA EID TOKA JESHI LA POLISI

$
0
0
Ndugu Wanahabari,

Jeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.

Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.

Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Aidha, wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, wanatakiwa kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Wananchi wanatakiwa kuwa makini hususani watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu na pale inapobidi watoe taarifa kwa majirani zao. Wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

Vilevile, Jeshi la Polisi linawatahadhalisha wananchi kuwa makini na matapeli yanayotumia majina ya viongozi, watu maarufu na wafanyabiashara wakubwa ili kujipatia pesa na vitu mbalimbali. Matapeli hao wamekuwa wakitumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi kupata taarifa za mtu binafsi hatimae mtu huyo kuibiwa.

Ndugu wanahabari,
Kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo, pamoja na watu wote wanaoingia ama kuishi na kufanya shughuli hapa nchini bila kufuata utaratibu (wahamiaji haramu) kutakiwa kuondoka au kuharalisha ukaazi wao, Jeshi la Polisi linawataka watu hao kuendelea kutekeleza agizo hilo la Serikali kabla ya Operesheni kabambe kuanza itakayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama.

Aidha, baadhi ya watu hao tayari wamekwishasalimisha silaha wanazozimiliki kinyume cha sheria na pia baadhi ya wahamiaji haramu wameanza kuondoka hususani katika mikoa ya Kagera na Kigoma. Hiyo ni hatua nzuri, tunawataka wale wote ambao bado hawajatekeleza agizo hilo, waendelee kufanya hivyo haraka kabla ya muda wa msamaha kumalizika.

Mwisho, napenda kuwahakikishia wananchi kwamba, Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi na hivyo halitawajibika kumwonea huruma ama upendeleo mtu yeyote atakayeenda kinyume na sheria.

NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID –EL-FITR

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

TAZARA MAJANGA TENA: WAFANYAKAZI WADAI MSHAHARA WA MIEZI 3, WAGOMA KWA SAA KADHAA, WATANGAZA KWENDA KWA WAZIRI MKUU

$
0
0
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo wamefanya mgomo wa saa chache kushinikiza Menejimenti iwalipe mshahara wao wa miezi mitatu. 
 Wakizungumza wakati wa mkutano wao wa kujadili matatizo yao ikiwemo na hatma ya malipo ya mshahara wao wafanyakazi hao wamesema hawawezi tena kuendelea na kazi kwani kwa sasa wana njaa ya miezi mitatu na hivyo kuitaka Menejimenti kuwalipa kwanza mishahara yao na ndipo waendele na kazi. 
 Kwa upande wake Menejimenti imewataka wafanyakazi hao kuvumilia kwani tatizo lao linashughulikiwa. Hata hivyo wafanyakazi hao wameazimia kwenda kwa Waziri Mkuu  kuwasilisha suala lao.
Mmoja wa wafanyakazi wa TAZARA, Charles Sumai akiongea kwa hasira wakati wa mkutano wao huo.
Sehemu ya abiria wanaosafiri kwa treni ya TAZARA wakiwa nje ya kituo na mizigo yao baada ya safari ya reni iliyokuwa iwe saa 9.50 kuahirishwa mpaka saa 2 usiku kufuatia sakata hilo leo.
Sehemu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wakiwa kwenye mkutano wao kujadili matatizo mbalimbali ikiwemo hatma yao ya kutolipwa mshahara wa miezi mitatu kuanzi Mei, juni na Julai. Mkutamo huo ulifanyika kwenye ofisi za TAZARA, Dar es Salaam leo mchana.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha baraza la Mawaziri kilichofanyika ikulu jijini Da es Salaam leo.Wapili Kulia ni Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na watatu kulia ni Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue.(Picha na Freddy Maro).

BENKI YA KCB YATOA MISAADA YENYE THAMANI YA SHILINGI TSH 7,200,000 KWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA, YAAHIDI KUFANYA MAKUBWA SEKTA YA ELIMU NCHINI

$
0
0
KCB Bank Tanzania, imekabidhi vifaa vya hospitali ambavyo ni oxygen flow meters venye thamani ya Tsh. 7,200,000/= kwa uongozi wa hospitali ya Mwananyamala 
Huu ni mwaka wa pili mfululizo ambako benki ya KCB inatoa misaada kwa hospitali ya Mwananyamala. Mwaka jana tulitoa vitanda 65 vikiwemo 60 na loka zake kwa ajili ya wadi ya kinamama na vitano kwa ajili ya kujifungulia (delivery beds) vyote kwa ujumla vikiwa na thamani ya Sh. 45,000,000. 
 Hii ni kawaida ya KCB bank kutembelea vituo vyote ambavyo imepeleka misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada husika. Ni matunzo na matumizi mazuri ya vifaa vinavyotolewa, yatakayoifanya benki ya KCB iongeze msaada au misaada kituo chochote kilichokwishasaidiwa, vivyo hivyo itakua hospitali ya Mwananyamala. 
Tathmini ya mwaka jana inaonyesha benki ya KCB ilitoa misaada yenye jumla ya thamani ya Tsh 362,545,000/= katika mchakato ufuatao:
 • Tsh. 145,024,000- Sekta ya Afya 
• Tsh. 130,000,000- Sekta ya Elimu 
 • Tsh.73,521,000- Mafunzo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs)
 • Tsh. 14,000,000 - Sekta isiyo rasmi (jamii yenye shida mbalimbali kama vyakula, maafa n.k) Mwaka huu KCB imetenga kiasi kikubwa zaidi cha fedha kwaajili ya kusaidia jamii inayotuzunguka katika sekta zilizotajwa hapo juu na mazingira nchini. Mikoa itakayofaidika ni pamoja na Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba vya kuwekea mgonjwa gesi, vilivyotolewa na benki ya KCB kwa hospitali hiyo, Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
 Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), moja ya vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk.Sophinias Ngonyani, akiangalia moja ya vifaa tiba vya kumwekea mgonjwa gesi, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye (katikati), vifaa vilivyotolewa na benki hiyo kwa hospitali hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa,akimkabidhi moja ya boksi lenye vifaa vya kumwekea mgonjwa gesi, Mkuu wa Bima ya Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Merina Nkullua, vilivyotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oysterbay, Gladys Mhina, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya benki ya KCB, kuchangia madawati inayoitwa 'Buy 10 Get 90, ambayo benki hiyo itanunua madawati 90 na shule husika kutakiwa kununua madawati 10. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa
na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB,Christina Manyenye.

Dhana 10 Potofu Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

$
0
0
Na Mdau, Mwanakwerekwe
 Kuna tishio kubwa dhidi ya Muungano wetu.  Tishio hilo liko zaidi kwenye dhana kuliko udhaifu wa dhamira ya Muungano wenyewe. Tishio hilo limedhihirika katika kipindi hiki cha Mchakato wa Kuandaa Katiba Mpya ya nchi yetu.

Mjadala wa rasimu ya Katiba mpya umetawaliwa kwa kiasi kikubwa na agenda ya Muungano.  Yamejitokeza makundi yenye mitazamo tofauti juu ya Muungano. Wako wanaoutaka uendelee, wako wasioutaka, wako wanaotaka urekebishwe, ilihali kuna kugongana kwa fikra.

UNITED NATIONS CHILDREN`S FUND (UNICEF) PUBLIC AUCTION IN ZANZIBAR

$
0
0

UNIVERSAL AUCTION CENTRE under instructions received from UNICEF we shall sell Suzuki motorcycle &  Office Furniture   by public auction on Wednesday  7 , August, 2013 commencing at 10.00 am. The auction will take place at  Zanzibar Kinanzini,  ZSTS building  floor 3  Malawi road near BOT building .

ITEMS TO BE SOLD:Suzuki motorcycle  TF125, Office  Desk/Chairs, Computer table,  Book shelf, Facsimile m/c, Computer sets, Printer,  Shredder m/c  Etc.


All items may be inspected at UN Vehicles parking, Kinanzini Zanzibar on 5th  to 6th August, 2013 from 10.00 hrs. to 16.00 hrs.


AUCTION CONDITIONS:

  1. The winning bidder for furniture has to make full payments to cashier immediately.


  1. All items are sold on” as where is” basis with no guarantee.


  1. Duty and all Taxes are the responsibility of the buyer.


  1. Bidder will remove the items after all payments and duty.


  1. UNICEF reserves the right to reject any and all bids for any reason whatsoever.


For further information contact:

UNIVERSAL AUCTION CENTRE,          OR: UNICEF OFFICE, ZANZIBAR

Nkrumah Street Opp. CO- CABS                            MOB: 0787600118/0774440005

TEL: 2128027, 0754 284 926,                         Email: sabali@unicef.org

Email:universalauction@hotmail.com                  ZANZIBAR.      


DAR ES SALAAM.                                            

jokate ndani ya mkasi na salama jabir pale pale amaya

MKOA WA VYUO VYA ELIMU YA JUU CCM WAFANYA KUBWA LA WASOMI WA VYUO VIKUU KUJADILI RASIMU YA KATIBA,GESI

$
0
0
 Sehemu ya Vijana wa Vyuo Vikuu walioshiriki Kongamano la kujadili Rasimu ya Katiba Mpya na Rasilimali za nchi yetu.
 Baadhi ya Mafisa wa Mkoa wa Vyuo Vya Elimu ya Juu CCM wakiwa na mgeni rasmi wa Kongamano,Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo,katika ukumbi wa Riverside,Ubungo.
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano wakifuatilia kwa makini hotuba ya Profesa Muhongo alipokuwa akichambua masuala ya gesi na uchumi.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali nchini wakichukua habari za Kongamano la Kujadili rasimu ya Katiba mpya na rasilimali lililofanyika katika ukumbi wa  Riverside Ubungo, ambalo liliratibiwa na Mkoa wa Vyuo Vya Elimu ya Juu CCM tarehe 5 Agosti 2013. 

KISOMO CHA KUWAREHEMU NDUGU ZETU WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI DMV

$
0
0

Nyarugusu wakishirikiana na Kruu nzima ya Kijiwe cha Ughaibuni wanawakaribisha watu wote kwenye kisomo cha kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki na chai ya pamoja siku ya Alhamisi Aug 8, 2013 baada ya Swala ya Eid. 

Address ni 
6200 Ager Road, 
Hyattsville, MD 20782

Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.

Kwa taarifa zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na Makeo 301 318 3419
Choteka 301 779 8799

KARIBU

SHINE A LIGHT'S 2013 RAMADHAN PROGRAM

$
0
0
This is a group founded by KCMC (Kilimanjaro Christian Medical College)students in June 2010 aimed at helping children who are less fortunate (orphans ,street children etc ) achieve their dreams, have a chance at life and a bright future . 
email us at sal.kcmc@gmail.com or visit us at www.shine-a-light.org 
 SHINE A LIGHT FUNDRAISED OVER THE COURSE OF RAMADHAN TO GET OPRHANAGE CENTERS AROUND TANZANIA BASIC FOODSTUFF(RICE ,BEANS ,SUGAR,SALT ,FLOUR ETC) ! 
 662,000 Tshs was raised 
 Centers touched include : -Umra orphanage center, Dar es Salaam -Al huda orphanage center Kaloleni Pasua, Moshi -Al Swabirina orphanage ,Mbeya -Binti Maringo center , Mwanza 
 Shine A Light would like to thank everyone who contributed in making this a success and would like to wish everyone a very blessed forthcoming 
EID EL FITR!!!!
MEMBERS OF SHINE A LIGHT IN DAR ES SALAAM AFTER HANDING OVER FOODSTUFF AT UMRA ORPHANAGE CENTER  AT MAGOMENI DAR ES SALAAM
MEMBERS OF SHINE A LIGHT IN MBEYA HANDING OVER FOODSTUFF TO AL SWABRINA OPRHANAGE CENTER IN MBEYA
MEMBERS OF SHINE A LIGHT IN MOSHI HANDING OVER  THE  FOODSTUFF AT AL HUDA ORPHANAGE CENTER AT PASUA MOSHI
SHINE A LIGHT HANDING OVER FOODSTUFF AT THE BINTI MARINGO CENTER IN MWANZA 

PPF KANDA YA KINONDONI YAFUTARISHA WATOTO WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA NEW LIFE ORPHANAGE, KIGOGO JIJINI DAR

$
0
0
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Zahra Kayugwa, akigawa uji kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha New Orphanage, Kigogo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Upendo Mazzuki, akigawa uji kwa watoto.
Watoto pamoja na walezo wa kituo cha kulea watoto yatima cha New Orphanage wakifuturu pamoja na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Afisa wa Mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni, John Nyalusi, akiwapa chakula watoto wakati wa futari.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Zainab Ndullah (Kushoto) na Nelu Mwalugaja, wakigawa chakula.

BENKI YA FBME yatoa misaada kisiwa cha Tumbatu

$
0
0

 Mkurugenzi wa uendeshaji wa benki ya FBME, Nassor Dachi (kulia) akikabidhi sadaka ya chakula kwa Bi Kazija Haji huko kisiwa cha Tumbatu Zanzibar jana.
picha na Martin kabemba.
Mfanyakazi wa benki ya FBME tawi la zanzibar, Abubakar saleh (kulia) akikabidhi sadaka ya chakula kwa bi mizaNyange huko Tumbatu jana. Msaada huo umetolewa na benki hiyo.

Wandishi wa habari kutoka ZBC Television Zanzibar, Saleh Masoud (kushoto) Abdalla Masangu wa Zanzibar leo na Munir Zakaria wa Chanel Ten (kulia) wakiwa katika msafara wa kutembelea kisiwa kidogo cha Tumbatu kutoa msaada wa sadaka pamoja na benki ya FBME tawi la zanzibar. Picha na Martin kabemba

TANZANIA YASHAURIWA KUANZISHA kampuni maalumu itakayoshughulikia maendeleo ya chanzo cha umeme cha Jotoardhi (Geothermal)

$
0
0
Serikali ya Tanzania imeshauriwa kuanzisha kampuni maalumu itakayoshughulikia maendeleo ya chanzo cha umeme cha Jotoardhi (Geothermal). Ushauri huo ulitolewa na Serikali ya Kenya kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli ya nchini humu, Mhandisi Joseph Njoroge alipokutana na Ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ya Tanzania wakati wa ziara ya mafunzo ya jotoardhi, jijini Nairobi. 
Katibu Mkuu huyo alisema serikali ya Kenya kwa kuchukulia umuhimu wa chanzo hicho, iliamua kuanzisha kampuni inayojishughulisha na uendelezaji wa jotoardhi nchini humu ambayo inajulikana kwa jina la Geothermal Development Company (GDC). 
“Sisi tumeanzisha kampuni hii ambayo kazi yake ni kuendeleza chanzo hiki cha umeme ambacho gharama ya umeme wake ni nafuu ikilinganishwa na gharama ya umeme wa vyanzo vingine” alisema. Alishauri serikali ya Tanzania kushirikiana na sekta binafsi ili kuweza kuwa na uchimbaji wenye tija wa chanzo hicho ambacho gharama yake kubwa ni katika uchimbaji. 
 Aidha, alisema serikali ya Kenya inashirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha chanzo hicho kinaendelezwa. 
“Gharama za kuchimba ni kubwa sana takribani dola za kimarekani milioni 4.2 zinatumika katika uchimbaji pekee hapo bado gharama nyingine hiyo ni kuchimba tu” alisema 
Alisema serikali ya Kenya imekuwa na ushirikiano wa karibu na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya kupata fedha za utafiti wa awali wa kisayansi na fedha kwa ajili ya uchimbaji. Alisisitiza bila sekta binafsi maendeleo ya nishati hayawezi kufikiwa. 
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Tanzania, Eliakim Maswi alisema ni wakati muafaka kwa Tanzania kushirikiana na nchi zingine za Afrika Mashariki ili kuendeleza rasilimali zinazopatikana katika nchi hizo. 
Alisema serikali ya Tanzania imeamua kujifunza uendelezaji wa jotoardhi kutoka Kenya kwaajili ya kuzalisha nishati ya umeme kwa kuwa nchi hii imepiga hatua ikilinganishwa na nchi nyingine za jirani. 
“Afrika Mashariki tuwe mfano wa kuigwa, tushirikiane katika kuendeleza rasilimali zilizopo nchini mwetu kwa manufaa ya umma” alisema. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Tanzania, Victor Mwambalaswa alisema serikali ya Tanzania imeonesha dhamira ya kweli katika kuendeleza jotoardhi. 
“Tumekuja hapa kwa lengo kuu moja ambalo ni kujifunza masuala ya uendelezaji wa jotoardhi ili nasi tuweze kunufaika na chanzo hiki cha kuzalisha umeme” alisema. 
Katibu Mkuu Maswi alisema ziara hiyo ya mafunzo imekuja baada ya Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kutembelea maeneo ambayo umeme wa jotoardhi unazalishwa na kuahidi kuleta wataalamu kutoka nchini Tanzania ili kujifunza. Alisema Serikali ya Tanzania ina nia ya dhati kuhakikisha wananchi wake wanapata umeme wa uhakika na wabei nafuu huku ziada inayopatikana inauzwa nchi nyingine.

 Mafunzo yanaendelea: Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa kwanza kushoto) akisikiliza mada iliyokuwa ikitolewa kuhusu uendelezaji wa chanzo cha umeme cha jotoardhi. Anaemfuatia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi GDC) Kenya, Silas Simiyu. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Tanzania, Mhandisi Hosea Mabise na anayemfuatia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Victor Mwambalaswa

Baadhi ya wabunge wakifuatilia mafunzo ya Jotoardhi yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (GDC) ya Kenya, Silas Masinde Simiyu (hayupo pichani). Kulia ni Mhe. Peter Kafumu, mbunge wa Igunga na kushoto ni Mhe. Riziki Said, Mbunge wa Lindi Viti Maalumu.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ya Tanzania, Mhe Victor Mwambalaswa wakati wa mafunzo ya uendelezaji wa chanzo cha umeme cha jotoardhi yaliyofanyikia jijini Nairobi nchini Kenya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akihutubia wabunge na wataalamu wa chanzo cha umeme cha jotoardhi  (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya uendelezaji wa chanzo hicho yaliyofanyikia jijini Nairobi, Kenya. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Kenya (GDC), Silas Simiyu. 

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Last Night A DJ Saved My Life' ya bendi ya Indeep ilipagawisha sana enzi hizo

New Arrivals! Wahi dukani Vazi

J&M VIRGO YAJA NA OFA YA SIKUKUU YA IDD

$
0
0
 KATIKA KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL-FITR,DUKA LAKO LA VIWALO VIKALI JIJINI DAR ES SALAAM LIFAHAMIKALO KAMA J&M VIRGO,LINAKUPATIA PUNGUZO LA BEI WEWE MTEJA WAKE ILI UWEZE KUTOKA NA VITU VIKALI VYA KUTINGA SIKU YA IDD EL-FITR.

HIVYO FIKA DUKANI KWAO PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA,JENGO LA C&G PLAZA KUJICHUKULIA PAMBA KALI,MOKA ZA KISASA NA MICHUCHUMIO MIKALI KWA KINA DADA PAMOJA NA MIKOBA.

KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO

 MAGAUNI YA KILEO KWA KINA DADA NA KINA MAMA
 SANDROZ KALI KWA KINA BABA KWA AJILI YA KUVALIA KANZU WAKATI WA KWENDA KWENYE SWALA YA EID EL - FITR.
MICHUCHUMIO NDIO USISEME KWA KINA DADA.
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live




Latest Images