Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

WAZIRI UMMY MWALIMU, BALOZI WA PALESTINA WAINGIA MAKUBALIANO KUSHIRIKIANA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim pamoja na Balozi wa Taifa la Palestina nchini Tanzania Hazem Shabat wametia saini ya mkataba wa ushirikiano kwenye sekta ya afya.
Kupitia mkataba huo Taifa la Palestina pia litasaidia katika kuleta madaktari kwa ajili ya kutibu magonjwa yakiwamo ya uti wa mgongo ambapo madaktari wao na wa Tanzania watafanya kazi pamoja ya kutoa huduma za afya.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri Mwalim amesema kuwa wanatambua kuna changamoto katika kutibu baadhi ya magonjwa nchini, hivyo madaktari bingwa wa Palestina na madaktari bingwa waliopo nchini watatumia fursa ya mkataba huo wa ushirikiano katika kutoa huduma za tiba kwa Watanzania.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano,chini ya Rais, Dk.John Magufuli imekuwa na jitihada  mbalimbali za kuboresha sekta ya afya lakini mkataba uliotiwa saini leo unatoa fursa ya kuimairisha pia utoaji wa chanjo na dawa.
Amesema mkataba huo umejikita kwenye maeneo mbalimbali na baadhi ni kusaidia katika kutoa huduma za afya, kusaidia upatikanaji wa dawa, kuimarisha eneo la Tehama ili kuboresha huduma hasa kwa kuzingatia teknolojia ya habari na mawasiliano itasaidia kuimarisha mfumo wa kutunza kumbukumbu za sekta ya afya.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimuakibadilishana mikataba na Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania baada ya kutiliana saini kwa ajili ya  ushirikiano kati ya Tanzania na Palestina katika sekta ya afya, Hafla ya kutiliana saini imefanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Kwanza wa Balozi wa Palestina Derar Ghannam.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimuakizungumza na mara baada ya kusaiini mikataba ya ushirikiano katika sekta ya Afya  kati ya Tanzania na Palestina kushoto ni Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania.
 Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mikataba hiyo, Kulia ni Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  na Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mikataba hiyo kushoto ni Msaidizi wa Kwanza wa Balozi wa Palestina Derar Ghannam.
Baadhi ya maofiza kutoka wizaya ya Afya wakiwa katika hafla hiyo.


Rayvanny Performing Live In Chicago Saturday March 24th, 2018

$
0
0
Tanzanian recording artist Rayvanny will be performing Live In Chicago @ JC Martini Club, 3124 N Central Ave, Chicago, IL.
Doors open at 9.00p.m.
Showtime 11.30p.m [No African Timing] !!!!
Early Bird Tickets on sale now for only $25.

WACHIMBAJI MADINI KIGOMA WAELEZA CHANGAMOTO ZAO KWA NAIBU WAZIRI NYONGO

$
0
0
Na Veronica Simba – Kigoma
Wachimbaji wa Madini wadogo wa Mkoa wa Kigoma, wamemweleza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao na kumwomba awasaidie kuzitatua.
Walimweleza changamoto hizo katika kikao maalum, Machi 3 mwaka huu, wakati Naibu Waziri alipowatembelea akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo.
Miongoni mwa changamoto kubwa waliyoitaja ni kuhusu vibali vya kusafirisha madini ghafi nje ya nchi; ambapo Naibu Waziri aliwataka kuwa wavumilivu kwani Serikali inakamilisha mchakato wa kuandaa Mwongozo maalum utakaopambanua kila aina ya madini yaliyo nchini na yanapaswa kusafirishwa yakiwa katika hali gani. 
“Unajua, Madini yanatofautiana, na uchakataji wake unatofautiana. Hivyo tumeona tuandae Mwongozo utakaoondoa mkanganyiko huo na kuwarahisishia kujua Madini gani yanapaswa kuongezewa thamani kwa kiwango kipi ili uruhusiwe kuyasafirisha nje ya nchi.”
Alisema kuwa, Mwongozo huo utatolewa hivi karibuni na hivyo Serikali itaanza tena kutoa vibali vya usafirishaji Madini nje ya nchi.
Vilevile, wachimbaji hao walitaja changamoto nyingine kuwa ni upatikanaji wa Ruzuku ambapo pamoja na kulalamikia Serikali kusimamisha zoezi hilo, lakini pia walidai kuwa wakati ikitolewa, wahusika hawakutenda haki.
“Wasiokuwa na vigezo ndiyo walikuwa wakipatiwa Ruzuku ilhali wenye vigezo wakinyimwa,” walilalamika.
Akizungumzia suala hilo, Naibu Waziri aliwaeleza kuwa Serikali iliamua kusimamisha kwa muda zoezi la utoaji Ruzuku kutokana na kugundua udhaifu katika zoezi husika ikiwemo baadhi ya wanufaika kutumia Ruzuku waliyopewa kwa mambo yao binafsi tofauti na masharti yake. Hata hivyo, alisema kuwa Ruzuku itaanza kutolewa tena baada ya Serikali kujiridhisha kuwa itatumika vema.
Kuhusu suala la wenye vigezo kunyimwa Ruzuku na wasio na vigezo kupatiwa; Naibu Waziri alisema Serikali itafuatilia na kuchunguza kwa ukaribu ili kuwabaini watumishi wa umma na wengine wanaoshirikiana nao katika kupindisha utaratibu uliowekwa kwa sababu wanaozijua wao. 
“Tukiwabaini tutawachukulia hatua kali za kisheria. Nanyi tunawaomba mtuletee aina yoyote ya ushahidi unaoweza kutusaidia kuthibitisha madai yenu ili kwa pamoja tukomeshe tatizo hilo.”
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji madini wadogo wa Mkoa wa Kigoma, wakati wa ziara yake ya kazi mkoani humo, Machi 3 Mwaka huu.
 Katibu wa Kikundi cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Kigoma, Iddi Lugundana, akisoma Risala ya Kikundi hicho mbele ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), wakati alipowatembelea na kuzungumza nao, akiwa katika ziara ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, wakikagua Kiwanda cha Kuchakata Chokaa kinachomilikiwa na Kikundi cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Kigoma, kilichopo Eneo la Simbo, Machi 3 Mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA 2018/2019

$
0
0

CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA, KILICHOPO USA-RIVER, ARUSHA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA 2018/2019 KAMA IFUATAVYO:


ASTASHAHADA (CERTIFICATE)


1.      Astashahada (Certificate) ya ICT (mwaka 1)

2.      Astashahada (Certificate) ya Usimamizi wa Biashara/ Business Administration (mwaka 1)

3.      Astashahada (Certificate) ya Uhasibu (Accounting) (mwaka 1)

4.      Astashahada (Certificate) ya Sheria/Certificate in Law (mwaka 1)


Sifa zinazohitajika:

·        Mwombaji awe na ufaulu wa kuanzia alama “D” katika masomo manne.

AU

·        Ufaulu wa kiwango cha ‘subsidiary’ kwa Kidato cha 6

KOZI ZA STASHAHADA (ORDINARY DIPLOMA)

5.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5 & 6) katika ICT (miaka 2)

6.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5& 6) Usimamizi wa Biashara/Business Administration (miaka 2)

7.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5 & 6) katika Uhasibu/Accounting (miaka 2)

8.      Stashahada ya Sheria /Diploma in Laws (mika 2)

Sifa zinazohitajika:

·        Mwombaji awe na Cheti cha NTA Level 4 kutoka chuo kinachotambulika na NACTE

AU

·        Ufaulu kwa kiwango cha “Principle” moja (1) na “Subsidiary” moja (1) kidato cha Sita (A-Level)

 

NB: Nakala za vyeti vya nje viambatane na Fomu ya uthibitisho wa tathmini toka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

 

 
Maombi yafanyike kupitia mtandao wa chuo“ONLINE APPLICATION” katika tovuti ya chuo, yaani: www.makumira.ac.tz


AU

Chuoni, Tumaini University Makumira, Ofisi ya Msajili.

 

Mwisho wa maombi kupokelewa ni tarehe 30/03/2018.

Msajili,

Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira,

S. L. P. 55, Usa River, Arusha

Simu:  027 254 1034

Simu za Mkononi: 0753 293986 au 0753 008084


UAMUZI PINGAMIZI LA AWALI LA JAMHURI DHIDI RUGEMALILA KUJUKIKANA KARIBUNI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

UAMUZI dhid ya pingamizi la awali lililowasilishwa na Jamuhuri katika Mahakama ya Rufaa kupinga maombi yaliyowasilishwa na mfanyabiashara James Rugemarila kupinga kukataliwa kupewa dhamana Mahakama kuu kujulikana hivi karibuni.

Jopo la majaji linaloongozwa na mwenyekiti, Bernad Luanda,Batueli MMimilla na Gerald Ndika limesema litatoa uamuzi tarehe itakayopangwa na pande zote mbili zitajulishwa.

Katika maombi hàyo, upande wa Jamuhuri unawakilishwa na Zainabu Mango,Peter Maugo na Tumain Kweka ambapo Rugemarila alijiwakilisha mwenyewe.

Katika maombi hayo Rugemarila anaiomba Mahakama ya Rufaa imruhusu kufanya mabadiliko ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa.Pia anaomba kumuunganisha mshtakiwa mwenzake katika kesi ya Economic, Harbinder Seth kama mtu muhimu katika maombi hayo na anaomba wapatiwe dhamana wakati rufaa yao inaendelea kusikilizwa. 

Upande wa Jamuhuri uliwasilisha pingamizi la awali na kupinga maombi hayo kwa madai yameletwa chini ya kifungu kisicho sahihi.Kwani hakielekezi maombi hayo ni ya jinai au madai na kuiomba Mahakama iyatupilie mbali baada ya kusikiliza pingamizi hilo.

Mahakama imesema itawataarifu wahusika tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huo.Baada ya kusema hayo Rugemarila aliiomba Mahakama itupilie mbali pingamizi la Jamuhuri kwasababu pingamizi hilo limeletwa kwa kanuni isiyo sahihi.Alidai pingamizi hilo halina ufafanuzi kuhusu sababu za pingamizi na kuiomba Mahakama itupilie mbali na ataeleza kwanini amemuunganisha Seth kama mtu muhimu.   

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh, bilion 309

MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

JESHI la polisi mkoani Pwani, limetoa siku saba kwa madereva pikipiki (bodaboda) ambao walitelekeza pikipiki zao katika vituo mbalimbali vya polisi, kwenda kuzichukua baada ya kusamehewa na jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani humo, (ASP) Jonathan Shanna ,alisema jeshi hilo liliwahi kuendesha zoezi la ukamataji wa pikipiki kwa makosa mbalimbali ambapo baadhi ya madereva walizitelekeza pikipiki hizo hadi sasa.

Hata hivyo alisema ,pikipiki zilizohusika kubeba bangi ,madawa ya kulevya na kutumika kufanya uhalifu hazitatolewa .Alisema wamejiwekea mikakati ya kukabiliana na ajali mwaka huu,kwa kutoa mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.

Shanna alieleza, watahakikisha wanasimamia elimu hiyo iweze kutolewa kwa madereva hao kwenye vijiwe vyao mitaani kwa kutumia askari waliopangwa kwa kila kata.Pamoja na hayo, watakuwa wanafanya operesheni za mara kwa mara ili kuwakamata wale madereva bodaboda watakaokuwa hawataki kutii sheria bila shuruti kwa kuwachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani ili kupunguza ajali na vifo kwa waendesha pikipiki.

Shanna alifafanua,wanatarajia kufanya misako kwa magari aina ya Noah yanayozidisha abiria kupita kiasi na magari yanayobeba wanafunzi ambayo hayana ubora .“Tutawachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani madereva na wamiliki wa magari hayo,yatakayokiuka sheria za usalama barabarani”alisema Shanna.

Shanna hakusita kutoa ushauri kwa mamlaka nyingine ikiwemo wakala wa barabara TANROADS, TARURA, kuwa waongeze juhudi katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kuweka alama za barabarani na kuziba mashimo.

ARUSHA WAENDELEA KUFANYA BIASHARA YA FILAMU ZISIZOFUATA TARATIBU NA SHERIA ZA NCHI

ALIYOYAZUNGUMZA MSEMAJI WA SERIKALI MJINI DODOMA LEO


Profesa Mubofu Makamu Mkuu wa Chuo Mpya UDOM.

$
0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO   
         
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa ametangaza uteuzi wa  Profesa Egid Beatus Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Idris Suleiman Kikula.

Uteuzi huo umetangazwa rasmi leo tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi   ya Mkuu wa UDOM, Mhe. Benjamin Mkapa.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Mubofu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kabla ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.

Profesa Idris Kikula ni miongoni mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani  na nje ya nchi kitaaluma kwa kushiriki katika tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii

Ameshiriki katika tafiti hizo kwa kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa nchini  kama REPOA, pamoja na taasisi ya UONGOZI.

UDOM ndio chuo kikuu pekee chenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi hapa nchini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 40,000, pia kina eneo la ukubwa wa hekari zaidi ya 6000.

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA 2018 YAZIDI KUNOGA,WAIMBAJI WAENDELEA KUTAMBULISHWA

$
0
0
Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki kwao.

Maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018 yameendelea kunoga huku waimbaji mbali mbali wakiendelea kutambulishwa.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, RainFred Masako wakati akimtambulisha mwimbaji wa nyimbo za injili Martha Baraka.

Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki kwao.

Kwa upande wake mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Martha Baraka amesema kuwa yupo tayari kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kwa vile amejiandaa vyema."Tunaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa mjitokeze kwa wingi kuhudhuria Tamasha hilo ambalo nitaungana na waimbaji wenzangu kutoa burudani ya kukata na shoka," amesema Martha Baraka.

Tamasha hili linatarajiwa kufanyika Aprili 1-2, 2018 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Uwanja wa Halmashauri mkoani Simiyu,ambapo Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhando atazindua albamu yake mpya.

Waimbaji ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki ni Christopher Mwahangila, Jessica BM Honore. Wengini ni Solomoni Mukubwwa, Danny M- Kenya na Ephraim Sekeleti.

 Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili Martha Baraka akieleza namna alivyojiandaa katika tamasha la pasaka 2018,mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani).Kushoto ni Meneja wa Msama Promotions Ltd,Jimmy Charles
Mmoja wa waratibu wa tamasha la Pasaka 2018, RainFred Masako akimkaribisha na kumtambulisha mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili Martha Baraka mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar

UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu, UNAMID.

Umoja wa mataifa UN umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Mkuu wake wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufuatia jitihada zao za kudumisha amani ndani na Nje ya Nchi hiyo.

Hayo yalibainishwa na mwakilishi Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Watoto (Special Representative of Secretary general of Child Abuse and AA) Profesa Virginia Gamba wakati wa Ziara yake kikazi katika Maeneo ya vjiji vya Shangilitobaya Jimboni Darfur nchini Sudan hivi Karibuni.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo zinazopaswa kutiliwa mfano lakini yote hiyo inatokana na umadhubuti wa Serikali yake, na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa mchango wake katika kushughulikia mambo ya msingi katika kudumisha Amani.

“Sina budi kuipongeza Serikali chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao ni wa kutukuka Afrika nzima katika kuleta Amani kwani bila Amani hakuna maendeleo hivyo maendeleo yanayotarjiwa Tanzania ytapatikana kwa sababu ya Amani” Alisema Profesa Virginia.

Aliongeza kuwa kutokana na kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote kujiletea maendeleo haraka na kuwataka kuendeleza jitihada hizo kwa kuwalinda watoto ambao ni nusu ya Idadi ya watu Duniani hivyo wakilindwa Watoto Dunia itakuwa salama.

“ Najivunia Tanzania naweza kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa sababu nyingine ni kutokana na Umahiri wao katika Amani ikiwemo jeshi lake la Ulinzi limekuwa Msaada mkubwa katika kuleta Amani kupitia Umoja wa Mataifa” Alisema Profesa Virginia.
Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya Jirani na Mlima Mawe Khor Abeche Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Shangilitobaya Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Msafara Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya kijiji cha Shardai Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

MICHANGO NA MAFAO YA WANACHAMA KATIKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII IKO SALAMA.

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
Kama mnavyofahamu Serikali inaendelea na Mchakato wa kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada ya Sheria kupita Bungeni. Hivi karibuni kumeibuka taarifa ambazo si sahihi kuhusiana na usalama wa michango na mafao ya Wanachama. Taarifa hizi zimepelekea baadhi ya Wanachama na Wastaafu kuwa na wasiwasi kuhusu hatma ya michango na mafao yao. 

Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi Wanachama na Wastaafu wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwa mafao na michango yao iko salama. Waajiri wanapaswa kuendelea kupeleka michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii husika. Vile vile Wanachama na Wastaafu waendelee kufuatilia mafao yao katika Mifuko kama kawaida hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Dar es Salaam
05/03/2018

Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII

$
0
0
Na Zuena Msuya, Dodoma.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewateua Wahandisi Saba(7) kutoka Wizara ya Nishati watakaoshirikiana na wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa REA III katika kila Kanda ili kuboresha na kurahisisha utekelezaji wa Mradi huo kwa ufanisi.

Dkt. Kalemani alifanya uteuzi huo baada ya kufanya mkutano na Wadau mbalimbali wanaotekeleza Mradi wa REA III wakiwemo, Wakandarasi,  Wawekezaji wenye Viwanda vya kutengeneza miundombinu ya umeme kama vile Trasfoma, Mita, pamoja na nyaya za umeme , Mameneja wa Kanda, na Wahandisi wanaosimamia Mradi ya REA III nchi nzima.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina ulipo Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu pamoja na changamoto zinazojitokeza  katika utekelezaji wa Mradi huo.

Dkt.Kalenani alisema Wahandisi walioteuliwa watashirikiana na Wakandarasi wa REA III kutafanya kazi mbalimbali pamoja na kuwa na mpango kazi wa kila wiki wa kila Mkandarasi katika eneo husika ili kusisimamia kwa ukaribu utekelezaji wake. 

Pia watarahisisha mawasiliano yamoja kwa moja kutoka kwa wakandarasi hao na Wizara ya Nishati  ili kufahamu hatua waliofikia na changamoto watakazokuwa wakikabiliana nazo kwa Lengo la kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( katikati) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua( kulia) wakisikiliza maoni ya wadau wanaotekeleza mradi wa REA III katika ukumbi wa hazina wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika mkoani Dodoma.

Washiriki wa mkutano wa wadau wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
Watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakimsikiliza waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani( hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaotekeleza mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.

MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE

$
0
0


Na Yusuph Mussa, Korogwe.

BWENI la Mapinduzi la wanafunzi wa kidato cha pili na nne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe limeteketea kwa moto, huku mali zote za wanafunzi ikiwemo fedha zimeungua.

Moto huo ulioanza 3.15 usiku jana Machi 4, 2018, uliwakuta wanafunzi 43 wa bweni hilo wote wakiwa darasani (prepo), hivyo mali zao zote kuanzia vitanda 19 vya kulala wanafunzi wawili wawili na vitanda vitano vya kulala mtu mmoja vimeteketea kwa moto.

Akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Rehema Bwasi, alisema mali nyingine zilizoteketea ni magodoro 43, ambapo kati yao 26 ni ya shule na 17 ya wanafunzi. Pia vyandarua 43, shuka 86, blanketi 43, masanduku ya bati 43, mabegi 43 na fedha taslimu za wanafunzi mmoja mmoja sh. 336,500.

"Vitu vingine vilivyoungua ni pamoja na nguo za wanafunzi, miswaki, sabuni, vikombe, sahani pamoja na vitabu vya wanafunzi na vya shule. Ila tathmini inaendelea ili kuweza kujua hasara iliyotokana na moto huo" alisema.

Bwasi alisema kutokana na kadhia hiyo, baadhi ya wanafunzi walipata mshtuko, huku wengine wakiwa na magonjwa mbalimbali kama pumu na kifua, hivyo wanafunzi 41 walipelekwa Hospitali ya Wilaya na saba Zahanati ya Majengo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela(mwenye shati jeupe) akiangalia athari zilizosababishwa na moto ulioteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Wilaya ya Korogwe. moto huo ulizuka usiku wa kuamkia leo, juu pichani akiwa ndani ya Bweni hilo linaloitwa Mapinduzi lililoteketea kwa moto. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Anisia Mauka. (Picha zote na Yusuph Mussa)
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Machi 5, 2018 alifika Wilaya ya Korogwe kuangalia athari za moto Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Pichani akimfariji mmoja wa wanafunzi waliopata mkasa wa kuunguliwa na bweni la shule hiyo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Machi 5, 2018 alifika Wilaya ya Korogwe kuangalia athari za moto Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Pichani akimfariji mmoja wa wanafunzi waliopata mkasa wa kuunguliwa na bweni la shule hiyo. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said.
Bweni la Mapinduzi la Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe ambalo limeteketea kabisa kwa moto jana usiku Machi 4, 2018. Bweni hilo walikuwa wanalala wanafunzi 43 wa kidato cha pili na nne.

AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa kutoa huduma bora za smartphone leo imetangaza uhuru wa mawasiliano kwa kuzindua huduma kabambe ya kipekee kwa wateja wake wanaopiga simu na kutuma sms kwenda mitandao yote nchini. 

Taarifa iliyotolewa na Airtel leo imesema bando za uhuru zinakuja baada ya serikali hivi karibuni kuweka punguzo kubwa la gharama za kuunganisha simu zinazokwenda mitandao mingine (interconnection rate) na hivyo Airtel kuona vyema kuwapa wateja wake fursa ya kufurahia punguzo hilo kupitia huduma yake itakayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Wateja wote watapiga na kutuma sms mtandao wowote nchini baada ya kujinunulia bando nafuu ya shilingi 1000 au bando mpya ya shilingi 600 tu.

 ‘Yatosha Mitandao Yote’ ni bando bora kuliko zote nchini zinazowawezesha wateja wa Airtel kujipatia vifurushi vyenye muda wa maongezi mara mbili zaidi ya  ilivyokuwa awali. Mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24, hapo awali kifurushi hiki cha shilingi 1000 mteja alipata dakika 25 tu. 

Vilevile kwa kifurushi kipya kimeongezwa faida ili kumpa mteja dakika 16, 2MB na 50 sms  kwenda mitando yote kwa shilingi 600 tu. Zaidi ya hapo wataendelea kujipatia vifurushi nafuu kwa SIKU, WIKI, MWEZI kwa kujiunga baada ya kununua vocha kwa kupiga *149*99# kisha chagua YATOSHA MITANDAO YOTE au kujiunga kupitia huduma ya Airtel Money na kufurahia Uhuru wa kuongea.

Akiongea jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindua wa Yatosha Mitandao Yote, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa “wateja wanabaki kuwa ndio nguzo kuu yetu kwenye biashara, ni furaha kubwa kwetu kuzindua huduma ya Yatosha Mitandao Yote ambayo itawapa wateja wa Airtel unafuu zaidi na uhuru  wa kutumia huduma za mawasiliano. Tunaendelea kufanya utafiti kufahamu mahitaji ya wateja pamoja na kuongeza ubunifu ili kuleta huduma nafuu zaidi ”
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania, Sunil Colaso(katikati), Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano(kulia) na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon, wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Sunil Colaso.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


BARAZA LA MADIWANI NA MBUNGE CHALINZE WACHARUKIA WAPIGAJI KWENYE VIZUIA VYA USHURU

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze.

MADIWANI wa Halmashauri ya Chalinze, pamoja na mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wamewasimamisha wakusanyaji wa ushuru kwenye baadhi ya vizuia, kutokana na kudaiwa kujihusisha na wizi na upotevu wa vifaa  ili kupisha uchunguzi .

Pia, wameitaka halmashauri hiyo kutumia walinzi wenye silaha kwenye vizuia vikubwa vya ukusanyaji ushuru ikiwemo wa kokoto ili kukabiliana na wizi unaotokea mara kwa mara.

Maamuzi hayo ,yamefanyika baada ya madiwani hao kulalamikia wizi na hujuma zinazofanywa na wakusanyaji kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.

Ridhiwani alisema ,kizuia cha Lugoba ni kero sanjali na Mpaji ,Mbwewe na Lunga ambapo kizuizi cha Lugoba kimeshavamiwa zaidi ya mara moja na matukio hayo yanaendelea kujitokeza hivyo wahusika lazima wachunguzwe.

“Mashine za ukusanyaji wa mapato zinaibiwa kirahisi rahisi ,hakuna kinachoendelea hivyo mchezo huu unavyoendelea halmashauri inapata hasara ”alifafanua Ridhiwani.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatim akuzungumza jambo wakati wa baraza la madiwani la Chalinze lililofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Chalinze
Mbunge jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akuzungumza jambo wakati wa baraza la madiwani la Chalinze lililofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Chalinze.
 Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,wakionekana pichani kusikiliza kwa makini jambo wakati wa baraza la madiwani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKURUGENZI MKUU TCAA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA CANSO KANDA YA AFRIKA Yahoo / Inbox

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege (CANSO)akichukua wadhifa huo kutoka kwa Thabani Mthiyane wa Afrika Kusini aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka sita.

 Bwana Johari ambaye atakuwa kwenye wadhifa huo kwa miaka mitatu, amechanguliwa tarehe 5 Machi 2018 katika mkutano wa CANSO unaofanyika Madrid Hispania na anatarajiwa kuthibitishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa CANSO uliopangwa kufanyika mwezi Juni Bangkok, Thailand. Kutokana na uteuzi huo, Bwana Johari anakuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya CANSO (EXCOM) ambacho ndicho chombo cha juu cha usimamizi wa shughuli za shirikisho hilo. Bwana Mthiyane anatarajiwa kukabidhi majukumu ya mwenyekiti wa CANSO Afrika kwa Johari baina ya mwezi Machi na Juni 2018.

 Tunapenda kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TCAA na kumtakia mafanikio katika majukumu haya mapya CANSO ni Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege za Kiraia Duniani. Wanachama wa CANSO wanatoa huduma hizo kwa asilimia 85 kote duniani. Wanachama wa shirikisho wanabadilishana taarifa na kuandaa sera zinazolenga kuboresha huduma za anga na uongozaji ndege.

IMETOLEWA NA OFISI YA HABARI MAMLAKA YA USAIFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)

MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Philipo Mangula amewataka Watanzania kujenga na kuilinda amani nchini na kushangazwa na viongozi wa dini wanaobariki chuki kuwa wanamkosea Mungu.

Pia aliwaonya wanasiasa wanaochochea chuki na kusababisha vurugu na kuwashauri waache kwa kuwa siasa ni uvumilivu na kuumiliana.
Mangula alitoa kauli hiyo jana mjini Musoma alipozungumza na viongozi na wana wana chama wa CCM kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama mjini humo.

Alisema kuwa turufu kubwa iliyobaki kwa CCM na watanzania ni amani iliyodumu nchini kwa miaka dahari na hivyo wakati wote wazungumzie taratibu na kutunza amani ya nchi ili kue[uka machafuko vurugu na migogoro inayosababishwa na kuchochewa na wanasiasa.

“Siasa ni kuvumiliana na uvumilivu ndiyo hujenga umoja.Wanasiasa wanapoleta vurugu  wajue wanaoumia ni watoto na wanawake na hivyo tuache chuki tujenge amani ya nchi yetu bila kufanya hivyo hatuwezi kupata maendeleo,”alisema Mangula na kuongeza kuwa;“Nashangaa na kushitushwa na viongozi wa dini wanapojiingiza na kubariki chuki, wanamkosea Mungu.

Machafuko yakishatokea hakuna atakayesalimika kwa kusema mimi ni kiongozi wa dini."Alieleza kuwa kazi ya serikali ni kuwajengea nyumba bali  mazingira mazuri wananchi ili wajijenge na kujifanyia maendeleo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philipo Mangula akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Mara jana alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.Kushoto bi Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara Samuel Kiboye Namba Tatu na wa pili kutoka kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ( NEC) Mkoa wa Mara Christopher Gachuma. Picha zote na Baltazar Mashaka.
 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye Namba Tatu (kulia), akizungumza na baadhi ya viongozi na wana CCM waliojitokez kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philipo Mangula wa pili kutoka kushoto.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BARAZA la Madiwani Manispaa ya Ilala imepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 katika mwaka fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwanduga amesema kuwa bajeti hiyo katika sehemu kubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Mwanduga amesema kuwa fedha hizo zitapatikana katika makundi mawili ya ruzuku pamoja na vyanzo vya ndani ambapo hakuna mwananchi atakayeonewa katika bajeti hiyo.

Amesema kuwa chanzo cha mapato ya ndani ni wanatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 ambapo na fedha nyingine zitakuwa ni za ruzuku.Mwanduga amesema kuwa kila diwani anataka kuwa na mradi katika kata yake lakini haiwezikani kutokana na uwezo wa manispaa.

Amesema kuwa bajeti hiyo itatekelezeka ni pamoja na kuwa na vyanzo hivyo viwili vya ruzuku na mapato ya ndani na asilimia 60 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika kutekeleza miradi.

Aidha amesema kuwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya elimu bure kwa manispaa imethubu ikiwa ni pamoja na kujenga shule nne pamoja na kufanya ukarabati kwa bajeti iliyoishia 2018.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza wakati wa Kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Anatoglo 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,Ando Mwankuga akiwaeleza Madiwani jinsi mipango na miradi ya Maendeleo katika kata ya Segera itakavyoendeshwa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akiwasilisha makadilio ya bajeti ya Mwaka 2018/ 2019.
Wabunge wa jimbo la Ilala na Segerea , Azzan Zungu na Bonnah Kaluwa wakisoma kwa makini makblasha ya bajeti ya Manispaa ya Ilala.


AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE

$
0
0
Akina mama zaidi ya 200 wa kijiji cha Jomu kata ya Tinde mkoani Shinyanga wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hamad Hilal (CCM) wameadhimisha wiki ya Wanawake Duniani kwa kushiriki ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi na watoto katika kituo cha afya Tinde kwa kujitolea kusomba maji.

Akina mama hao wamejitolea kusomba maji kutoka katika bwawa la Tinde hadi katika kituo hicho cha afya leo Jumatatu Machi 5,2018 siku ambayo mafundi ujenzi wamemwaga jamvi katika jengo hilo la wodi ya wazazi na watoto.

Ujenzi wa jengo hilo unaoendelea ni miongoni mwa majengo yanayojengwa katika kituo hicho ambapo majengo mengine ni jengo la upasuaji,wodi ya wazazi,chumba cha kuhifadhia maiti,maabara na nyumba ya mtumishi ambayo kwa pamoja yatagharimu shilingi milioni 400 zilizotengwa na serikali.

Akizungumza kituoni hapo,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad aliwashukuru akina mama hao kujitokeza kusaidia katika ujenzi huo ambao kukamilika kwa jengo hilo kutaondoa adha wanayopata akina mama pindi wanapofika katika kituo hicho kupata huduma za afya. 

“Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga tumepata shilingi milioni 900 kwa ajili ya vituo viwili ya afya vya Samuye na Tinde naishukuru sana serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli na wasaidizi wake akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jafokwa kuweka kipaumbele huduma ya mama na mtoto”,alieleza.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi na watoto katika kituo cha afya Tinde
Wa tano kutoka kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hamad Hilal (CCM) akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wenzake wakazi wa kijiji cha Jomu wakishiriki ujenzi wa jengo la wazazi na watoto kituo cha afya Tinde
Akina mama wakiwa wamebeba ndoo za maji
Zoezi la kusomba maji likiendelea.

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images