Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA WIKI YA ELIMU KWA MLIPAKODI

0
0
Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam,

Wito umetolewa kwa wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika vituo ambavyo vimepangwa rasmi kwa ajili ya wiki ya elimu kwa mlipakodi itakayofanyika kuanzia kesho tarehe 5 hadi 9 Machi, mwaka huu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alisema maandalizi yamekamilika katika vituo vyote nchi nzima hivyo wananchi watumie fursa hii kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

“Maandalizi ya wiki ya elimu kwa mlipakodi yamekamilika kwa kiasi kikubwa, niwaombe tu wafanyabiashara na wananchi wote wajitokeze kwa wingi katika vituo vilivyotengwa rasmi katika kila mkoa nchi nzima kwa ajili ya kupata uelewa zaidi juu ya masuala ya kodi, kutoa malalamiko, mirejesho, changamoto pamoja na maoni mbalimbali,” alisema Kayombo.

Kayombo alifafanua kuwa katika wiki hiyo mada mbalimbali zitafundishwa kama vile ulipaji wa Kodi ya Majengo kwa njia ya kieletroniki, Mkataba wa Huduma kwa Mlipakodi ambao umeainisha haki na wajibu wa mlipakodi na viwango vya huduma wanavyopaswa kupata kutoka TRA pamoja na umuhimu wa kutoa na kudai risiti ikiwa ni pamoja na kikagua kabla ya kuondoka nayo.

“Watalaam wetu wamejipanga vizuri kutoa elimu katika kila mkoa kwenye wiki hii ya elimu kwa mlipakodi. Mada mbalimbali zitafundishwa ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wananchi kulipa kodi inavyostahili ndani ya muda utaotakiwa,” alisisitiza Kayombo. Kayombo alisema kuwa, katika wiki hiyo kutakuwa na usajili wa walipakodi wapya hivyo wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Wiki ya elimu kwa mlipakodi itakuwa inafanyika kila baada ya miezi mitatu ikiwa na lengo la kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto, kupokea mrejesho pamoja na maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi.

Mbio za Tigo Kili Half Marathon zafana mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro

0
0
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon upande wa wanaume,  Gefrey Kipchumba kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:03 kwenye uwanja wa ushirika mjini Moshi.
 Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni upande wa wanawake,  Grace Kimanzi kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:13 kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Simon Karikari wakimkabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanaume, Gefrey Kipchumba toka Kenya leo kwenye viwanja vya Chuo cha Ushirika mjini Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akiwa na mzee Joram Mollel maarufu kama BABU, mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 21 zijulikanazo kama Tigo Kili Half Marathon leo.
 Babu Joram Mollel katikati akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo, pamoja na Mkurugenzi wao Simon Karikari kwa pamoja na kauli mbiu yao TUMETISHA KAMA BABU.
Mshindi wa upande wa wanawake  mashindano ya kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon toka Kenya Grace Kimanzi (katikati) akiwa na washindi wa pili toka Tanzania Fainuna Abdi na mshindi wa tatu, Pouline Nkehenya toka Kenya, wakinyanyua mfano wa Hundi juu mara baada ya kutangazwa kushinda mbio hizo. Kushoto ni waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari leo.

TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazokwamisha mradi wa ujenzi wa gati mpya.

Prof. Marawa ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Gati mpya inayojengwa Mkoani Mtwara kwa ubia wa kampuni mbili za Kichina za China Railways Major Bridges Engineering Group Co. Ltd (CRMBEG) na China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na kubaini mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo.

“Hatuwezi kuendelea kuchelewesha mradi huu muhimu kwa wakazi wa Mtwara, wakati fedha zipo na mikataba imeshasainiwa, naiagiza TPA kuhakikisha kuwa inatatua changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi ndani ya miezi mitatu ili mradi ukamilike kwa wakati,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa na Wakandarasi wazawa chini ya usimamizi wa TPA isimamiwe kwa kuzingatia viwango na muda uliopangwa na kuahidi kurejea baada ya miezi mitatu kukagua maendeleo ya miradi hiyo.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali akiwasilisha taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Hayupo Pichani), kuhusu mapato na matumizi ya bandari hiyo, wakati Waziri huyo alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa gati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiangalia eneo ambalo linajengwa maegesho ya kawaida ya mizigo katika bandari ya Mtwara, alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari hiyo.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya mradi wa Gati katika bandari ya Mtwara. Gati hiyo yenye urefu wa mita 300 inatarajiwa kukamilika mwaka 2019 na upanuzi wake utagharimu kiasi cha shiliingi zaidi ya bilioni 100.
Mhandisi wa Bandari ya Mtwara, Eng. Twaha Msita ambaye ni (katikati), akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), ramani ya eneo la mradi wa kuegesha mizigo ya kawaida, alipokagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari ya Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Karim Mattaka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Karim Mattaka (kushoto), alipokagua maendeleo ujenzi wa gati, Mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd (kushoto), anaejenga Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50, alipokagua maendeleo ya ujenzi wake mkoani Mtwara. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoani Mtwara, Eng Dotto Chacha. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini Bw. Evod Mmanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na wakazi wa Nanguruwe Mkoani Mtwara alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha Lami.

CONGRATS MR. & MRS FELIX MREMA ON YOUR SPECIAL DAY. GOD BLESS YOU

JUKWAA LA WANAWAKE TANESCO LACHANGIA DAMU HOSPITALI YA TUMBI KIBAHA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kupitia jukwaa la wanawake wa shirika hilo leo kwa umoja wao wamekusanyika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani , Tumbi Kibaha na kujitolea Damu kwa ajili ya Wanawake wanaojifungua na majeruhi kadhaa wanaotibiwa katika Hospitali hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa Tanesco Kanda ya Pwani, Martin Maduhu amesema wafanyakazi wa shirika hilo wameamua kujitolea kwa moyo wao mara baada ya kundi la umoja wa Wanawake kufikiria kutoa mchango huo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

"Sisi tumekuwa tukiwaangazia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuakikisha kuwa wanapata umeme wa uhakika lakini tumegundua umeme bila afya auna faida hivyo kupitia jukwaa hili tumeweza kuja kujitolea damua hili iweze kuwasaidia Mama zetua mabo ujifungua hapa na kumaliza damu nyingi pamoja na majeruhi."amesema Maduhu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi amesema wazo hilo limekuja mara baada ya kushauriana na wenzao wa pwani na kuona umuhimu wa damu katika Hospitali iyo ambayo upokea watu wengi kuliko kawaida kutokana na barabara ya Morogoro kuwa na mikasa mingi ya ajali.
amesema kuw ahuo ni mwanzo tu kwa jukwaa hilo lakini wamejipanga kutoa msaada zaidi katika jamii hili kuaakikisha kuwa wao kama watanzania wanaona kila mmoja anakua kiuchumi na afya.
Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha,Dkt Briceson Kiwelu, aliwashukuru wafanyakazi hao wa Tanesco na kusema kuwa ni mara chache sana kuona kundi kubwa kama hilo linakuja kujitolea damu katika hospitali hiyo hivyo uwe uwe mwanzo na isiwe mwisho.

amesema kuwa uzuri wa damu inayotolewa na kundi kubwa la watu kutoka katika shirika hilo asilimia 70 huwa ni nzima kutokana na watu wake wengii huwa wanafika wakiwa tayari wamejitathmini na kuchangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa damu safi kwa muda mfupi.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchangiaji Damu kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco lilipoamua kujitolea kutoa Damu kwa jili ya Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoa wa pwani kama Sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
 Meneja wa Tanesco Kanda ya Pwani, Martin Maduhu akizungumza jinsi gani Tanesco inavyoweza kuwaangazia wananchi maisha yao kwa kushiriki katika utoaji damu kwa ajili ya kuwezesha wajawazito na watu wanaopata ajali waweze kupata matibabu haraka katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha,Dkt Briceson Kiwelu akitoa neno la ukaribisho kwa wafanyakazi wa Tanesco wa Dar es Salaam na Pwani waliojitokeza kwa wingi kujitolea Damu kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayo adhimishwa Marchi  8  mwaka huu
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi akiwa katika Maandalizi ya utoaji wa Damu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha.
Mmoja ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco ambaye ni Mwanachama wa Jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo akiwa katika vipimo vya awali kwa ajili ya uchangiaji damu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC

0
0
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri kupeleka wakaguzi kwenye Shule ya Sekondari Joel Bendera iliyopo Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi.

Ni kutaka kubaini ukweli kuhusu matumizi ya fedha baada ya sh. milioni 150 zilizopelekwa shuleni hapo kumalizika, kabla ya ujenzi wa mabweni mawili kumalizika, huku tena zikihitajika sh. milioni 17 kumalizia ujenzi huo.

Chatanda alibaini hilo baada ya Machi 3, 2018 kufanya ziara kata ya Kwamsisi, na kusomewa taarifa na Mkuu wa Shule hiyo Nasson Msemwa kudai sh. milioni 150 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kujenga mabweni hayo ikiwa ni pamoja na kuweka samani, fedha zake zimekwisha.

“Mheshimiwa Mbunge, Serikali ilituletea sh. milioni 230, ambapo sh. milioni 150 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana na wavulana na sh. milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya manne. Fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambapo tupo kwenye hatua za mwisho zimekwisha. Na ili tukamilishe mabweni hayo kunahitajika sh. milioni 17.

“Kwa upande wa ujenzi wa madarasa manne, bado tunakwenda vizuri, kwani pamoja na ujenzi kuwa kwenye hatua za mwisho, bado tuna sh. milioni 28” alisema Msemwa.
Mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda (wa tatu kulia) akisikiliza taarifa inayosomwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Joel Bendera Nasson Msemwa (wa pili kushoto). Hapo ndipo Chatanda aliliamsha ‘dude’ kutaka kujua kwa nini sh. milioni 150 zimeshindwa kukamilisha mabweni mawili.Yussuph Mussa, Korogwe
Madarasa mapya manne ya Shule ya Sekondari Joel Bendera, Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Halmashauri ya Mji Korogwe. Madarasa hayo ambayo yapo kwenye hatua za mwisho kukamilika, Serikali ilitenga sh. milioni 80 kujenga madarasa hayo. (Picha na Yusuph Mussa).
Moja ya mabweni yaliyopo Shule ya Sekondari Joel Bendera Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Halmashauri ya Mji Korogwe. Mabweni mawili yaliyojengwa shule hiyo, kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.PICHA ZOTE NA YUSSUPH MUSSA

MNEC SALIM ASAS AMPONGEZA MBUNGE ROSE TWEVE KUINUA UCHUMI WA WANAWAKE WILAYA YA MUFINDI.

0
0
Na Fredy Mgunda -Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 

Akingumza wakati wa baraza la UWT wilaya ya Mufindi Salim Asas alisema kuwa amefurahishwa na mkakati mbunge Rose Tweve kwa kufanikiwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kabisa ambao ndio wanastahili kuinuliwa kiuchumi kuliko wananchi ambao tayari wanauchumi mkubwa.

“Kwa kweli niwe muwazi kuwa nimefurahishwa na hiki kitu ambacho huyu mbunge anakifanya kwa kuwawezesha wananchi ambao ndio serikali ya awamu ya tano inataka kuwafikia na kuwainua kiuchumi” alisema Asas

Asas aliwata wabunge wengine kuiga mfano wa mbunge Tweve kwa kazi anayoifanya ya kuwawezesha akina mama na wananchi wengi kwa kuwa hiyo ndio inakuwa faida kwa taifa.“Naombeni wabunge wangu wote tufanye kazi kama anayoifanya mbunge Rose Tweve kwa kuwafikia wananchi wa chini ambao mara nyingi imekuwa vigumu kuwafikia kutokana na sababu mbalimbali” alisema Asas
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve akiongea mbele ya baraza kwa kuonyesha furaha yake mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas baada ya kuambiwa kuwa ataongezewa shilingi milioni kumi na nane kwa ajili ya maendeleo ya akina wanawake wa wilaya ya Mufindi
viongozi mbalimbali na wabunge wa viti maalum walihudhuria baraza hilo.

Kilimanjaro Marathon 2018 funsters huffing and puffing their way up to the finishing line

0
0
 Energetic participating in finishing up the remaining 5km of the Game

 Dr Dennis Katundu (left) and the cheering team from  the International School of Moshi and KCMC Hospital strike back on the sidelines...
 Some declare themselves winners midway
 Muscles getting hard and hot for some participants
 "....Do you really think Kichuri will be served after we are done as promised?"

SERIKALI YATOA BIL. 1.4 KUBORESHA VITUO VYA AFYA RUANGWA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya uboreshaji wa vituo vitatu vya afya katika wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Machi 04, 2018) wakati alipotembelea kata ya Mandawa kwa ajili ya kukagua mradi wa uboreshaji wa kituo cha afya cha kata hiyo.
“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”
Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. milioni 400 kwa ajili ya kituo cha Mandawa, sh. milioni 500 kituo cha Mbekenyera na sh. milioni 500 Nkowe.
Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi huo chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha kuhifadhia maiti.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.
Pia Waziri Mkuu amekabidhi gari la kutolea huduma za afya vijijini. Gari hilo linauwezo wa kutoa huduma za afya kama Zahanati. 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameshiriki katika zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya  ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Matambarare.
Amesema kata hiyo yenye vijiji vinne ilikuwa haina shule ya sekondari, hivyo kusababisha wanafunzi kutembea umbali wa kilomita tano kwenda kusoma kwenye shule za kata nyingine.
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akichanganya udongo wa tofali, wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiweka udongo wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akifyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO

0
0
Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
WATU watano wakiwemo wanawake wanne na mwanaume mmoja ambaye ni dereva basi ndogo aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE aliyetambuliwa kwa jina la Jackson Adam wamefariki dunia papo hapo baada yakugongana na basi  la  New force New lenye namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam kuelekea Tunduma na kusababisha majeruhi  ya watu wengine tisa na kulazwa  hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibisha kutokea kwa ajali hiyo  Machi 4, mwaka huu majira ya saa nne asubuhi  katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa  eneo la Lungemba – Rombo , Manispaa ya Morogoro kwa kuhusisha basi la aina ya Youtong  lenye namba za usajili T 346 DLY mali ya kampuni ya New force.
Basi hilo lilikuwa likitokea   Dar es Salaam kwenda Tunduma  na lilipofika eneo hilo liligongana uso kwa uso na basi ndogo  aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE iambayo lilikuwa likitokea kijiji cha   Mlali, katika wilaya ya Mvomero kwenda Morogoro Mjini.
Kamanda Matei alisema katika ajali hiyo  abiria  watano waliokuwa ndani ya Toyota Hiache walifariki dunia papo hapo na wengine  tisa kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Morogoro  kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hakukuwa na majeruhi kutoka  basi la New Force .
Kamanda wa Polisi wa huyo aliwataja waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa basi dogo  Jackson Adam ambaye ni mkazi wa Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro,  na wengine wanawake Georgina Aloyce (35) , Revocatha Raymond Lyimo , Mangasa Almasi  na Witness Leonard Mwamuni (26).
Pia aliwataja majeruhi waliokuwa kwenye  basi dogo ni  watoto wawili waliofiwa na mama yao katika   ajali hiyo ambao ni Catharine Mhagama (6) na Caltimei Mhangama  mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Prisca Isaya (25), Chuki Wage (40), Anthon Cletus Mhando (39) mkazi wa eneo la SUA, Innocent Emilian , Willbrod Emilian ambao ni watu wazima mapacha , Iman Amri  Salum  na kondakta wa daladala hiyo  Ally Ramadhan.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi huyo  , chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi dogo ambaye ni marehemu kutaka kulipita lori la mchanga lililokuwa mbele  yake bila kuchukua tahadhari na hivyo kugonaga na basi la Kampuni ya New Force ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mdula   Abdallah  (52) mkazi wa Dar es Salaam. Hata hivyo alisema , Polisi inamshirikia dereva  Mdula Abdallah wa Kampuni ya New Force kwa ajili ya uchunguzi zaidi  kutokana na ajali hiyo.
Alisema ,mazingira ya ajali hiyo inaonesha  huenda dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo kasi uliomsababishia ashindwe  kupunguza mwendo mara baada ya kuona  basi ndogo likilipita lori lililokuwa mbele ambapo ageweza   kunusuru ajali hiyo mbaya iliyopoteza maisha ya watu isitokee
 Askari Polisi wakishirikiana na wananchi wakiondoa mwili wa dereva wa basi dogo aina ya inayofanya safari zake Mlali- Moro Mjini baada ya kugongana na basi kubwa la New Force  namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam – Tunduma ,  eneo la Lungemba – Rombo ,Manispaa ya Morogoro katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
 Basi  la  New force New lenye namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam kuelekea  Tunduma na kuhusika katika ajali hiyo.
 Baadhi ya wananchi wa maeneo ya mitaa ya kata zilizopo Manispaa ya Morogoro  wakiangalia ajali wa basi dogo Toyota Hiache inayofanya safari zake Mlali –  Moro mjini baada ya kugongana na basi kubwa la New Force  eneo la Lungemba – Rombo , katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
 Mabaki  ya basi dogo Toyota Hiache inayofanya safari zake Mlali – Morogoro mjni kugongana na basi kubwa la New Force  eneo la Lungemba – Rombo , katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Wananchi wa kata za Manispaa ya Morogoro wakiliangalia basi kubwa la New Force namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam – Tunduma  baada ya kugongana na basi dogo Toyota Hiache namba T 962 BSE inayofanya safari zake Mlali- Moro Mjini eneo la Lungemba – Rombo ,Manispaa ya Morogoro katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI KITAIFA MKOANI DODOMA

0
0


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga (kushoto) wakiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanyamapori Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma juzi. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Wanyamapori jamii ya Paka wamo hatarini kutoweka- TUWALINDE”. (Picha na Hamza Temba-WMU).

MZOEZI YA KUIMARISHA VIUNGO KWA MAZOEZI LAINI KUTOKA KWA SENSEI RUMADHA FUNDI

0
0
"IMARISHI VIUNGO, TOA MAUMIVU KWA MAZOEZI LAINI"
 Imeandaliwa na Sensei Rumadha Fundi 
mwalimu wa Karate na Yoga wa kimataifa 

 Mwili hautofautiani na chombo au mashine, na huitaji sana kuangaliwa na kutunzwa vizuri kana kwamba jinsi mashine inavyofanyiwa matunzo ya kila siku kuwa inafanya kazi imara ipasavyo. Sawa na ujana wa mwili na nguvu, zinakuwa madhubuti ,lakini, jinsi umri unavyokua, viungo kama magoti, mgongo na miguu navyo huanza kupungua nguvu na kusababisha maumivu ya mwili nzima au baadhi ya viungo. 
 Hapo basi, mazoezi mepesi ya aina hii, ndio ufumbuzi katika kusaidia kuuweka mwili na viungo vyake katika hali ya afya njema. 
Kwa mujibu wa ushauri wa wakufunzi wa mazoezi mepesi kama haya, angalau dakika ishirini tu kabla ya kufungua kinywa asubuhi kila siku, inatofautisha sana kulinganisha na mtu anayefanya mazoezi mazito tu kama kubeba vitu vizito pekee au kutofanya mazoezi kabisa. 
 Faida kubwa ya haya mazoezi ni pamoja na utulivu wa mawazo, kumbukumbu za fikra na kimawazo, kuwa na subira na kupunguza hasira za haraka. 
 Vigezo vikuu vya mazoezi haya mepesi ni kuwa na moyo wa kujitolea katika jitihada za kila siku. Kufanya mazoezi katika mazingira ya usafi, kama vile kuepuka sehemu ya mazoezi yenye vumbi, moshi, kwa kuwa mazoezi haya hufanywa katika sakafu kavu na kutandika blanketi. 
 Mazoezi haya yanaimarisha viungo vya ndani ya mwili " Internal organs " kama vile, figo, mapafu, bandama na moyo. Nidhamu ya mazoezi ni moja ya vitu pekee vinavyo muwezesha mtu kuyafikia haya mafanikio halisi na kupata afya njema. 
 Mwisho, vyakula vyenye lishe ni muhimu sana, ikiwemo kunywa maji mengi na kupunguza au kuepuka ulaji wa mafuta mengi katika vyakula. 


MAGAZETI YA JUMATATU LEO MARCH 5,2018

MAKATIBU WAKUU 15 KUTAFUTA SULUHU ZA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ZIWA MANYARA

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akitoa neno la ukaribisho kwa Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali katika kikao cha Mawasilisho ya Taarifa ya Tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba .
Mwenyeji wa Ziara ya Makatibu Wakuu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akifanya Wasilisho la Taarifa kuhusu tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara,Maeneo ya Shoroba na Mitawanyiko ya Wanyama Tarangire -Manyara kwa Makatibu Wakuu hao.
Miongoni mwa Majengo yaliyokuwa yakitumika kama Vyoo katika Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara likionekana kuharibika baada ya maji ya Mvua yaliyoambatana na Mawe zilizonyesha miaka michache iliyopita. 
Muonekana wa majengo mengine yaliyokuwa yakitumika kama vyo kwa wageni waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara baada ya kuharibika kutokana na Maji hayo ya Mvua.

TAARIFA YA KUKARIBISHWA KATIKA SHEREHE ZA MAULID SEGEREA MWISHO

0
0
Siku ya Jumamosi 10-Machi 2018

ASALAAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU
Ungozi wa Al Madrasat Rahman na Masjid Qubah Segerea mwisho,Dar unawakumbusha waumini kuwa ile sherehe ya Maulid ya Kumswalia Mtukufu wa darja Mtume Muhammad (S.A.W) kuwa itafanyika Jumaamosi ya wiki hii tarehe 10.3.2018 Segerea Mwisho jijini Dar es salaam.

RATIBA: Kuanzia Saa 4 asubuhi maulid ya Kina mama(wanawake).
Saa 10 alahsir Wanafunzi wa Madrasa watasoma Quran 
Saa 2 usiku baada ya swalat inshaa Maulid ya jumuiya yakiongozwa na wanaume mnakaribishwa wote  kwa mawasiliano zaidi simu 071240732 au 0757608303
 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika shughuli ya Mawlid,Segerea mwisho,Dar es salaam mwaka jana
 Baadhi ya waumini wa kiislamu katika masjid Qubah,Segeres Mwisho,Dar
Jitokezeni kwa wingi katika Mawlidi,Madrsat Rahman Segerea,Mwisho,Dar.
  


WAZIRI MKUU AKABIDHI PIKIPIKI MBILI KWA JESHI LA POLISI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akikabidhi pikipiki mbili kwa Kamanda Mkoa wa Lindi, ACP. Pudensiana Protas, zilizotolewa na kampuni ya WU ZHOU Investment Company kwa Jeshi la Polisi, wakati alipo tembelea kituo hicho jana, Machi 4, 2018 , Wilayani Ruangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA

0
0
Na Munir Shemweta, Mkinga Tanga

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini uwepo ya nyumba za watanzania zilizojengwa katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya huku eneo moja la nyumba hizo likiwa upande wa Kenya.

Katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro mkoa wa Tanga mhe Mabula alijionea jinsi nyumba zilivyojengwa bila utaratibu wa kuacha umbali wa mita mia kama eneo huru.

Eneo lililoathirika zaidi na ujenzi huo, ni katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake wamejenga nyumba zao zikiwa karibu kabisa na mpaka huku baadhi yake sehemu ikiwa upande wa Tanzania na nyingine upande wa Kenya.

Hata hivyo, Naibu Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshuhudia upande wa Tanzania katika eneo la Horohoro ukiwa umezingatia umbali unaotakiwa kati ya mpaka ukilinganisha na wakenya wanaoishi kijiji cha Jua kali Lungalunga ambao wamejenga karibu kabisa na mpaka wa Tanzania.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akipita katika kichaka kuelekea katika kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa nchi hizo mbili eneo la Horohoro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akitafuta kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kwa kuchimba eneo ambalo kigingi hicho kilikuwepo katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga. Nyuma zinazoonekana nyumba zimejengwa katikati ya mpaka huo wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia baadhi ya nyumba zilizojengwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya katika kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.

ASSEMBLY COMMENCES ITS SITTING IN ARUSHA

0
0

ASSEMBLY COMMENCES ITS SITTING IN ARUSHA


East African Legislative Assembly, Arusha, March 5, 2018: The East African Legislative Assembly (EALA) resumes its Sitting in Arusha, Tanzania, this week. The Assembly convenes for the Third Meeting of the First Session of the 4th Assembly, which commences today March 5th , 2018 and runs until March 23rd, 2018.

Key items at the Sitting include the debate on the East African Community Oaths Bill, 2017. The Bill anticipates the provision for the taking and administering of Oaths in relation to the specific persons appointed to serve in the Organs or Institutions of the Community or required to take oath before giving evidence at the East African Court of Justice. 

The Bill moved by the Chair of the Council of Ministers, Rt Hon Dr Ali Kirunda Kivejinja, avers that whereas there are specific persons who are required by the Treaty like in the case of the Judges and Registrars of the East African Court of Justice if in justice matters, or an Act of the Community like in the case of EALA Members, in all other cases, oaths of allegiance are administered and taken in accordance with staff rules and regulations or by practice. 

 The Bill which sailed through the First Reading at the recent Sitting in Kampala (2nd Meeting of the First Session) therefore hopes to cure the lacuna by providing for the administration of an oath as a statute.

In addition, the Report of the EALA on the on-spot assessment (tour) of the Northern and Central Corridors shall also be tabled and debated. The report follows the recent 13-day (February 12th-23rd, 2018) assessment of the institutions, facilities and installations of the EAC programmes in the Partner States undertaken by the Assembly.

UVCCM KIGOMA WAHAMASISHWA KUBUNI MIRADI YA MAENDELEO

0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapindizi(UVCCM), Mkoa wa Kigoma wametakiwa kubuni miradi ya kimaendeleo kwa lengo la kupunguza kuomba misaada na kubwa zaidi kujiimarisha kwenye uchumi ili kuunga mkono kauli mbiu ya Uchumi wa viwanda.

Mwito huo ulitolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa MNEC, Kilumbe Ngenda aliyekuwa mgeni rasmi, Katika Baraza la Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kigoma katika uchaguzi wa wajumbe watatu wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa na kumthibitisha Katibu wa uhamasishaji na chipukizi.

Ambapo aliwataka vijana hao kubuni miradi na kuendeleza miradi waliyonayo kama jumuiya nyingine zinavyo fanya na kuwataka kuwa na miradi yao binafsi ili kupunguza tabia ya kutembea na mabakuli kuomba.
Pia ameahdi kutoa mifuko 50 ya saruji ili wabuni mradi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda na kuiboresha nyumba ya wageni ambayo ipo chini ya vijana hao iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.Aidha Mbunge kupitia Vijana mkoa huo, Zainabu Katimba, amesema yeye kama kiongozi wa vijana ameamua kutoa Sh.milioni saba kwaajili ya kuwasaidia vijana Wilaya zote kuanzisha miradi ikiwamo miradi itakayohusisha viwanda.

Pia ametoa cherehani tatu kwa kikundi cha vijana wajasiriamali cha Mwandiga na kuwataka waendelee na jitihada za kuhakikisha vijana wote wanakuwa na shughuli za kufanya na kila Wilaya wabuni miradi."Sisi viongozi tutahakikisha tunawasaidia kuwawezesha ili kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wengi,"amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Wa Kigoma, Silvia Sigura amesema wao wamejipanga kufanya siasa za uchumi na si siasa za maneno na kwa kudhihirisha hilo wmeanza harambee kwa vijana katika baraza lililofanyika na kufanikiwa kuchangisha mifuko ya saruji 130 ili kuanza kujenga vibanda 12 katika kiwanja chao.

Amesema kwa michango walioipata watahakikisha wanaanzisha miradi kwa kila wilaya na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana ili wajiajiri katika masuala ya ujasiriamali.

MABWENI MAWILI SEKONDARI YA WASICHANA KOROGWE YATEKETEA KWA MOTO

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii

MABWENI mawili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Moto huo ulianza kuunguza mabweni hayo saa tatu usiku na chanzo chake hakijajulikana.Hata hivyo inadaiwa huenda chanzo kikawa ni umeme ingawa bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa moto huo.

Akizungumza leo, kwa njia ya simu na Michuzi Blogu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ,Edward Bukombe amesema atatoa taarifa rasmi na kwa sasa yupo eneo la tukio hilo."Nipo eneo la tukio na baada ya hapo nitakupa taarifa rasmi." 
Baadhi ya wanafunzi wote waliopatwa na mshituko wa tukio hilo wakipatiwa huduma ya kwanza mara baada kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya, ambapo inaelezwa walikuwa wanafunzi zaidi ya 15 waliopelekwa katika hospitali hiyo. 


Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images