Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

MADIWANI NAMTUMBO WAMKATAA MKUU WA WILAYA HIYO,WAMUOMBA RAIS AMWAMISHE

$
0
0
Balaza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya NAMTUMBO mkoani RUVUMA, limefikia maamuzi ya kumkataa mkuu wa wilaya hiyo LUCKNESS AMLIMA na kumuomba rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko kwa kumuondoa ili kuharakisha shughuli mbali mbali za maendeleo katika wilaya hiyo ambazo zimekwama kutokana na migongano na migogoro ya mara kwa mara baina yake na viongozi mbalimbali wa kisiasa katika halmashauri hiyo wakiwemo madiwani na wananchi.

UZINDUZI WA KAMPENI KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI WILAYANI CHAMWINO MKOANI DODOMA

CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0
Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .

Mhe. Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.“Tutaendeleza Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema Mhe. Chidawali.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki mapambano dhidi tatizo hili.
Diwani wa Kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Peter Elia Chidawali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo ‘Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima’ Wilayani Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja akitambulisha Kampeni ya Kitaifa ya Kuzuia Mimba za Utotoni kwa wanafunzi wa shule sambamba na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatil idhidi ya Wanawake na watoto katika Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala akiwaasa watoto wa kike kujitambua na kujilinda dhidi ya mimba za utotoni ili kupata haki ya kuendelezwa na kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia mimba za utotoni Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisikiliza ushauri wa malezi na makuzi kutoka kwa wataalamu jinsia ili kuwawezesha kupambana na mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.

KUNDI LINALOJIITA "WAKOREA" LAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA UHALIFU MJINI MBEYA

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu maarufu kama "Wakorea".
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya Operesheni maalum pamoja na misako katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya. Operesheni hii ililenga kukamata wahalifu mbalimbali likiwemo kundi la vijana wanaojiita "Wakorea" ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Operesheni hii imefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambayo ni Ivumwe, Mwakibete, Mwambene, Mama John, Ilomba, Mafiati, Makunguru, Iyela na Isyesye.
Katika Operesheni hii maalum, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita kwa  tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-

KELVIN RAPHAEL [22] Mwakibete Bomba mbili ambaye ndiye kiongozi wa kundi hili la uhalifu @ Wakorea.
CLEMENCE CHRISTOPHER @ MWAKALINGA [23] Mkazi wa Mwakibete Viwandani.
CHARLES MWASUMBI [21] Mkazi wa Mwakibete
EDGA EDWARD [20] Makondeko Mwakibete
IPYANS NDUNGURU [21] Mkazi wa Mwakibete
ADEN MWALUKASA [35] Mkazi wa Mwakibete

Pia katika Operesheni hii maalum ya kuwasaka vijana wanaojihusisha na uhalifu hapa Jijini Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana watatu [03] kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji nyakati za usiku na mchana. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-
GODFREY JOSEPH @ MHENGA [20] Mkazi wa Ilemi Mapelele
GODFREY PAUL @ MWAKASAJE [39] Mkazi wa Ilemi Mapelele
MTEMI YAHAYA @ MWASANGA [42] Mkazi wa Uyole

Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali walivyokuwa wakivitumia kuvunjia ambavyo ni:-
Bisibisi – 03
Nyundo – 01
Mkasi – 01
Aidha watuhumiwa hao walikutwa na mali mbalimbali za wizi:-
Flat Screen aina ya Home base
Flat Screen aina ya Samsung
TV ya kawaida aina ya Home base
Sub Woofer 01
Deck 03 aina ya Singsung 02 na Fusion 01.

Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane [08] kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.

Pia watuhumiwa kumi na mbili [12] ambao walikamatwa hivi karibuni katika Operesheni/Misako iliyofanyika huko katika maeneo ya Ilemi, Juhudi, Makunguru na Mwenge hapa Jijini Mbeya ambao kesi zao zinaendelea katika Mahakama ya Mwanzo Iyunga
Watuhumiwa wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya Upelelezi kukamilika.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato. Aidha anatoa onyo kali wafanyabiashara ya vilezi kufuata sheria na taratibu za biashara yao ikiwa ni pamoja na kufungua na kufunga sehemu zao za biashara muda sahihi kwa mujibu wa sheria.

BITEKO: TUFANYE SIASA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

$
0
0

Na Mathias Canal, Geita

Wanasiasa hasa wasomi na wale wenye ushawishi mkubwa nchini wametakiwa kuacha kulalamika na kutoa kauli ambazo hazitawasaidia wananchi katika kuwatatulia matatizo na kero zao bali waungane na serikali katika juhudi zinazoonekana za kuleta maendeleo. 

Rai hiyo imetolea na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo akiwa katika ziara ya kijimbo ya siku nne.

Mhe Biteko amesema baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa wakitumia muda mwingi kueleza matatizo na kero za wananchi bila ya kuonyesha suluhisho au kusaidia kutatua kero hizo jambo ambalo halimsaidii mwananchi kwa namna yoyote.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Pamoja na mvua kunyesha lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakifatilia kwa karibu na umakini mkubwa mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara juu ya namna bora ya kuwa na mafanikio kama Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, Jana 3 Machi 2018.

SEED trust yapokea vitabu1000 vya Malengo ya Dunia kwa wasioona

$
0
0

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo na Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju (wa pili kushoto) sehemu ya nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Bodi ya SEED Trust Tanzania, Mh. Stephen Mashishanga (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa SEED Trust Tanzania, Mh. Margaret Mkanga (kushoto) na Meneja Programu wa SEED Trust Tanzania, Peter Mwita (kulia).

Umoja wa Mataifa umetoa nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia vilivyochapishwa kwa herufi nundu (braille)(hizi ni herufi zilizovimbishwa na ambazo watu wasioona au wenye uoni hafifu husoma kwa kugusa na kidole) kwa taasisi ya Seed Trust Tanzania katika jitihada za kuwafikia wasioona. Kuna takribani watu milioni 39 wasioona na wenye uoni hafifu kote duniani leo; miongoni mwao takribani milioni 5.8 wako Afrika. Nchini Tanzania, kuna taarifa kwamba takribani asilimia 1.2 ya watu wenye ulemavu huu walitoa taarifa kwamba wana matatizo ya kuona.
 
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumzia kuhusu Umoja wa Mataifa kuwafikia watu wenye ulemavu katika kuhakikisha taarifa za Malengo ya Dunia zinawafikia watu wote wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo na Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju, akitoa salamu za serikali na kupongeza juhudi za Umoja wa Mataifa kuwafikia wenye ulemavu kwa kutoa nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za UN ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo ya Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju.Akizungumzia juhudi za UN kuwafikia wenye ulemavu, Mh. Amonalisema: “Lengo la 4 la Malengo ya Dunia linahusu elimu bora iliyo jumuishi na usawa wenye haki na kuhamasisha upatikanaji wa fursa za kujifunza za kudumu kwa wote. Lengo la 10 linahusu kuhakikisha kupungua kwa tofauti ndani na kati ya nchi nanchi.

Lengo la 17linahusu kuimarisha njia za utekelezaji na kuhuisha ushirika duniani ili kufikia Maendeleo Endelevu. Shabaha hizi kwa namna ya pekee zinataja ulemavu kama kitu kitakachosaidia kuhakikisha ushirikishwaji na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika utekelezaji, usimamizi na tathmini ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ujumuishwaji kwa hakika utahakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma. Kujumuishwa kwa watu wenye ulemavu kunatoa fursa kwao kushiriki na kutoa dukuduku zao pia.
Mwenyekiti wa Bodi ya SEED Trust Tanzania, Mh. Stephen Mashishanga akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO MARCH 4,2018

UDHAMINI WA BACHELOR DEGREE UGHAIBUNI


WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA ZIARANI MTWARA

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage  amekabidhi mradi wa SIDO kujenga Industrial sheds kwa Mkandarasi SUMA JKT. Katika Makabidhiano hayo Waziri Mwijage ametoa miezi 2 kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa majengo hayo. Mradi huo unakadiriwa kugharimu zaidi ya sh. Milioni 200,ambapo majengo yatajengwa ndani ya eneo la SIDO Mtwara lenye ukubwa wa hekta 8.

INTRODUCING "SAULA" BY SUPER NYAMWELA

$
0
0

Brand New Video from Tanzanian Artist/Dancer called SUPER NYAMWELA, Song name SAULA.
Video Directed by O-Key
Social media:
Instagram: @nyamwelasuper
Facebook: Super Nyamwela


DSM KUANZA KUTUMIA GESI MATUMIZI YA NYUMBANI

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amelitaka na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) kuharakisha uunganishaji wa huduma ya gesi asilia katika baadhi ya nyumba za wananchi kwenye maeneo ya jiji la Dar Es Salaam kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Dkt.Kalemani aliyasema hayo ofisini kwake mkoani Dodoma alipokutana na watendaji wa TPDC kwa lengo la kujadili suala la usambazaji wa Gesi asilia katika nyumba za Wananchi pamoja na bei watakayouziwa wananchi hao.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Kalemani aliwataka TPDC kuunganisha nyumba kuanzia Hamsini( 50) na kuendelea, na huduma ya gesi asilia katika maeneo la Mwenge na Mikocheni, kwa kuwa tayari miundombinu ya bomba la gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani imepita maeneo hayo.

Wakizungumzia suala la bei ya kuwauzia wateja, Dkt. Kalemani alisema kuwa pamoja na mambo mengine Gesi hiyo itauzwa kwa Wananchi kwa pungufu ya 40% ya bei ya mitungi ya gesi itayokuwa sokoni kwa wakati huo.

" Hii ni gesi yetu na bomba ni la kwetu vyote vinapatikana hapahapa nchini, ni vyema iuzwe kwa bei ya chini zaidi ya ile iliyopo sokoni kwa sasa, ili kila mwananchi aweze kumudu gharama zake pia ni rafiki wa mazingira, itasaidia kupunguza matumizi ya mkaa na kulinda misitu yetu", alisema Dkt. Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na watendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) ,na watendaji wa Wizara ya Nishati, kuhusua suala la usambazaji wa gesi asilia katika nyumba za wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ofisini kwake mkoani Dodoma
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( kushoto)na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba( kulia) wakizungumza kuhus suala la usambazaji wa gesi asilia katika nyumba za wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

MKATABA WA MAKUBALIANO KUTEKELEZA MRADI WA MAJI WILAYANI LUSHOTO

$
0
0


  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares na Mkandarasi Justice Kato  kutoka kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambaye atatakeleza mradi wa maji wilayani Lushoto mbao utagharimu milioni 700 wakionyesha hati za makubaliano mara baada ya kusaini mkataba
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares akizungumza wakati wa utiliaji saini wa makubaliano hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza wakati wa utiliaji saini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa maji wilayani Lushoto kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares

CHUMVI, CHOKAA ZINAWEZA KUITAJIRISHA KIGOMA - NYONGO

$
0
0

Na Veronica Simba – Kigoma 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, amesema kwamba ikiwa wananchi wa Kigoma watatumia vyema fursa za upatikanaji wa Madini ya Chumvi na Chokaa, zilizopo katika Mkoa huo, wanaweza kutajirika. 

Akihitimisha ziara yake katika Mkoa huo, jana Machi 3, baada ya kutembelea Migodi mbalimbali ya Madini ya Chokaa na Chumvi, Nyongo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa upatikanaji wa Chumvi na Chokaa ni neema kwa wananchi hao kutokana na uhitaji wake mkubwa katika maisha ya kila siku. 

“Ni fursa kubwa sana kwa wananchi wa Kigoma. Wasidhani kwamba fursa iliyopo hapa ni ya uvuvi na mawese peke yake; wanaweza kuwa matajiri wakubwa kupitia Madini ya Chokaa na Chumvi.” 

Akifafanua zaidi, Nyongo alisema kuwa, katika siku mbili za ziara yake mkoani Kigoma, ameshuhudia maeneo mengi yenye Chokaa ya kutosha na kwamba uzalishaji wake ni rahisi sana kwani kinachohitajika ni kuyachoma mawe husika na kusaga; basi. 

Akizungumzia upande wa Chumvi, alisema kuwa, Mgodi wa kuzalisha Chumvi wa Nyanza, uliopo Uvinza unafanya kazi nzuri katika uzalishaji lakini kwa bahati mbaya asilimia 70 ya bidhaa wanayozalisha, huiuza nje ya nchi hususan katika nchi jirani za Kongo na Burundi. 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu. 
Mmoja wa wafanyakazi katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza, ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), akifunga Mifuko ya Chumvi tayari kupelekwa Sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), Mgodini hapo, Machi 3 Mwaka huu.
Shughuli za uchakataji chumvi zikiendelea katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mine), siku Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), alipotembelea Mgodi huo akiwa katika ziara ya kazi, Machi 3 Mwaka huu.

Introducing "Furaha Yangu" by Farida Music, CBH & Teacher Oliver - Official Video

$
0
0
Introducing to you a young Tanzanian talented girl Farida Saidi Katungaye named Farida Music. Her talent was found and is being trained by a Traditional Musician Teacher Oliver who is now living in Germany in 2014 in Hamburg Germany in a Concert Theater named ZU HAUSE played by Teacher Oliver with his team, CBH as a special guest appearance was able to recognize Faridaz talent. 
Since CBH and Teacher Oliver are friends, CBH approached Teacher Oliver for a music project, three of them together (Farida Music, CBH, & Teacher Oliver). 
A lot happened with their busy schedule but end of 2017 they were able to settle for a studio session. 2018 now the first project CBH & Teacher Oliver Introducing Farida Music is out. Farida Music, CBH & Teacher Oliver - Furaha Yangu. 
Songwriter Teacher Oliver & CBH. The Song was recorded in G Records under producer KGT Shadeed. The video was shot in two countries Tanzania and Germany. Directed By Joowzey in Tanzania and Franziska Muller in Germany. Furaha Yangu is a song based on love and dedicated to all beloved ones ( Lovers, Family & Friends) both sides Male and Female. 
The song is a voice of a woman crying out for her love after the lonely days. Furaha Yangu is based on long distance love or relationships and It doesn't matter how far or close your beloved one is, If you can't see him or her easily then this is the song for you. 
Send a clear Message by dedicating this song to all the people you love with long distance. Few worlds but very powerfully to make them hear your pain. What is more important than being together? Money?Life? Wealth or Happiness? Enjoy the good Music

BODI YA MFUKO WA FIDIA YA ARDHI YAZINDULIWA

$
0
0
Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi imezinduliwa rasmi mjini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi.

Akizindua Mfuko huo kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi; Naibu Katibu Mkuu; Dkt. Moses Kusiluka alisema, Mfuko wa Fidia ya Ardhi umeanzishwa kwa mujibu wa Kanuni zilizoundwa chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 kwa lengo la kuondoa kero za ulipaji wa fidia katika utwaaji wa Ardhi. 

Kuundwa kwa Mfuko huu ni hatua mojawapo muhimu sana katika kuiwezesha Serikali kutekeleza kwa ufanisi zaidi matakwa ya Sera ya Ardhi na sheria zake, hususan katika ulipaji wa fidia pindi ardhi inapotwaaliwa kwa manufaa ya umma.

Dkt. Kusiluka alisema; Bodi hii inatarajiwa kufanya kazi kwa karibu sana na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Mthamini Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Alisema; “Mkitekeleza majukumu yenu kwa ufanisi mtaisadia sana Serikali kukidhi matarajio ya wananchi katika kuwaletea maendeleo na kuwaondolea kero. Hivyo, ni imani yangu kwamba mtatumia weledi wenu katika kutekeleza majukumu yenu”.

Aidha, Dkt. Kusiluka alitoa wito kwa taasisi zote kuhakikisha kuwa mipango yote ya utwaaji wa ardhi inazingatia matakwa ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo. Aliendelea kusema kuwa ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi zake zote zitafanya kazi kwa karibu na Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.

Naye, mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko; Bwn. Martin Madekwe alisema kuwa anashukuru kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti katika Bodi hiyo na kuwa anatambua kuwa Bodi anayoiongoza inategemewa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu Mkuu. Alisema; “ Bodi tumejipanga kufanya kazi kwa ufanisi, uwazi, ueledi na uadilifu na tutajitahidi kuzingatia kuwa wale wote wapaswao kufidiwa, wanafidiwa ipaswavyo”.

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi, inaoongozwa na Mwenyekiti Madekwe, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Katibu wake ni; Grace Gulinja, ambaye ni Afisa Ardhi Mkuu katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akisoma Hotuba ya Waziri wa Ardhi; Mhe. William Lukuvi akiwa amemwakilisha katika Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi ( Mijini), Paul Luge na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo; Bwn. Martin Madekwe.
Wajumbe wa Mkutano wa Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe.William Lukuvi katika Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
Kanali Mstaafu; Joseph Simbakalia, aliyewahikuwa Mkuu wa Mkoa Kigoma, mmoja wa wajumbe katika Mkutano wa Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi akionekana kwa karibu akifuatilia kwa Makini Hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi katika Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.


TRA YAWAPA SOMO WANAHABARI JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo (aliyesimama mbele) akiwaelimisha baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina Maalum iliyohusu masuala ya kodi hususani katika matumizi ya mashine za Kielektriniki za kutolea Risiti (EFD), masuala ya utoaji taarifa ya fedha mpakani pamoja na masuala ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 5 - 9 Machi, 2018.
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , Bibi Diana Masalla (aliyesimama mbele) akiwaelimisha baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina Maalum iliyohusu masuala ya kodi hususani katika matumizi ya mashine za Kielektriniki za kutolea Risiti (EFD), masuala ya utoaji taarifa ya fedha mpakani pamoja na masuala ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 5 - 9 Machi, 2018. 
Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa baadhi ya Watendaji wa Mamlaka hiyo (hawapo pichani) katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), 3 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-SPRO-TRA HQ)

INTRODUCING "CAROLA" (OFFICIAL VIDEO) BY THE MAFIK

LIVE: AIRPOT! Kijana Ahmed Albaity Akisafiri Kwenda China

WAZIRI UMMY AIKABIDHI TIMU YA COASTAL UNION KIWANJA,AWAHIDI NEEMA

$
0
0


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameipongeza Kampuni ya City Plan kwa kuunga mkono juhudi zao za kutaka kuimarisha klabu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kwa kuisaidia kupata kiwanja chao eneo la Maweni Jijini Tanga.

Hatua hiyo inatokana na viongozi kufanya kazi kubwa wakishirikiana na wadau kuhakikisha wanapambana ili kuiwezesha timu hiyo kurudi kucheza michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kucheza madaraja ya chini kwa kipindi.

Kiwanja hicho ambacho kina ukubwa wa square mita 7632 kipo Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambacho kina gharimu kiasi cha sh.milioni 38 kimepatikana baada ya kuwepo kwa juhudi kubwa za Waziri Ummy kuiomba kampuni hiyo kuisaidia timu hiyo eneo lake la kiwanja.

Kukabidhiwa kwa kiwanja hicho inafungua ukurasa mwengine wa mafanikio kwa timu hiyo kongwe hapa nchini.Akizungumza leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya kiwanja hicho, Waziri Ummy alisema kitendo cha kampuni hiyo kutoa eneo hilo kimesaidia mipango iliyokuwa nayo timu hiyo kuanza kwenda vema huku wakijipanga kwa hatua nyengine.

Alisema suala hilo linatokana na mshikamano uliopo baina ya viongozi waliopo wakiwemo wapenzi, mashabiki na wanachama huku wakiwataka kuuendeleza ili kuweza kupata mafanikio makubwa siku zijazo kwenye michuano ya ligi kuu.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga katika akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Coastal Union wakati akipokwenda kuwakabidhi kiwanja eneo la Maweni Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni Jijini Tanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu ya Coastal Union akizungumza katika halfa hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga (TRFA) Saidi Soud kushoto akiteta jambo na Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika halfa hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa TRFA Saidi Soud na Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto.

MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA

$
0
0
Na,Joel Maduka,Geita.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni 13.2 ,mifuko ya seruji 70 na mabanti ya kisasa 131 kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwenye kanisa la AIC Kalangalala Wilayani Geita.

MNEC wa mkoa huo Iddi ameendesha harambee hiyo siku ya leo kwenye ibada ambayo ilikuwa imeandaliwa na idara ya wanawake wa kanisa la AIC Kalangalala kwaajili ya changizo la umaliziaji wa madarasa ya kujifunzia watoto kanisani hapo.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wa kanisa hilo,Bi Justina Yuda ameeleza mahitaji ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwa awamu ya pili yanatarajia kugharimu kiasi cha Tsh 19,185,000 na kwamba fedha hiyo itasaidia kuezeka,kuweka dali kwenye madarasa pamoja na kuweka frame za madirisha ,milango na mageti ya milango.

Katika harambee hiyo MNEC Iddi milioni 1 papo hapo,mifuko 20 ya seruji na mabati 13 huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo iliweza kusaidia kupatikana kiasi cha sh,milioni 12.2 hivyo kupelekea kupatikana kwa jumla ya kiasi cha sh,milioni 13.2 ambazo zitatumika kujenga madarasa ya kujifunzi watoto.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,akiendesha Harambee ya umaliziaji wa ujenzi wa madarasa kwenye kanisa la AIC Kalangalala. 
Mch,John Masanyiwa akisoma kiasi ambacho kimepatikana kwenye harambee hiyo ya kanisa. 
Madarasa ambayo yamejengwa kwaajili ya watoto wa kanisa la AIC Kalangalala. 
Mgeni Rasmi pamoja na mchungaji na viongozi wa kanisa la AIC Kalangalala wakikagua baadhi ya majengo ambayo yamekwishakujengwa. 

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images