Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

MGUNDUZI MADINI YA TANZANITE AOMBA MSAADA KWA RAIS MAGUFULI


MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO MARCH 3,2018

UONGOZI ACT WAZALENDO WATANGAZA KUJITOA KATIKA CHAMA HICHO

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Uongozi wa wa Chama Cha Act Wazalendo wa mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na katibu wao Ernest Kalumuna  wameamua kujitoa katika chama hicho na kujiunga na Chama cha mapinduzi kufuata uzalendo unaonyeshwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo aliyekuwa katibu wa Chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, Ernest Kalumuna amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya Chama chao kilichokuwa kinajisibu kwa misingi ya uzalendo na kushindw akufuata misingi hiyo hasa kwa kiongozi mku wa Chama.

"Tumeshutushwa zaidi na kauli za karibu za kiongozi wa chama chetu ndugu Zitto Kabwe kuhamasisha Viongozi wa Chadema wakae na kufanya maamuzi ambayo anadai sisi tutawaunga mkono huku akimalizia kusema kuwa serikali hii ni rahisi sana kuiangusha  kwa hiyo ni ishara ya juu sana kwa kuona kiongozi wenu wa kisiasa kufirisika"amesema.

Amesema wajumbe wa kamati kuu wakilalamika na wengine wakihama chama kwa sababu hakuna tena kamati  kuu siku hizi lakini kuna kakikundi ka wapambe wake ambao badala ya kujenga wanabomoa.

Alimaliza kwa kusema kuwa wao kama wanasiasa mahiri hawezi kuendelea kuwa kwenye kikundi cha namna hii: "Hivyo kwa pamoja tunatangaza  kujivua  uanachama wa ACT Wazalendo  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili tufanye Siasa za kweli  za kurudisha nch yetu kwenye misingi ya kuasisiwa kwake", alisema.

RC MAKONDA AMKABIDHI AHMED TIKETI ZA NDEGE KWENDA CHINA KWA MATIBABU

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA YATOA ONYO KALI KWA MATAPELI WA BIMA.

$
0
0

Na.   Vero Ignatus, Dodoma.

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imetoa onyo kali kwa watu wanaowatapeli wananchi kwa kuwauzia bima za kugushi na hivyo kuwasababishia hasara na kuikosesha Serikali mapato,Matapeli hao ambao wengi wao hawana leseni za kufanya biashara ya Bima wametakiwa kuacha mara moja wizi huo kwani mkono wa sheria unawasaka ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wa bima katika Vyombo vya moto lililofanyika Mjini Dodoma ,Bibi Stella Guli Rutaguza amesema jumla ya magari 586 yalifanyiwa ukaguzi, ambapo  wamebaini  magari 25, pikipiki za miguu mitatu 5(bajaj) pikipiki za miguu miwili 2 yakiwa na Bima za kugushi huku magari mengine 19 yakiwa hayana bima.

 Rutaguza amesema kuwa wamefaminikiwa kuwakamata watu Wawili ambao wanatuhumiwa kujihusisha na kuuza bima za kugushi kwa wananchi na tayari wako mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Bibi Stella Rutaguza amesema zoezi la kuwasaka watu wanaouza bima feki kwa na kuwaibia wananchi na Serikali ni endelevu hapa Dodoma na Nchi nzima kwa ujumla.

"Tunataka kukomesha tabia hii chafu kwenye Soko la Bima", hivyo tunawataka vishoka wa Bima popote walipo watafute kazi halali ya kufanya maana Mamlaka ya Usimamizi wa Bima haitawafumbia macho na mkono wa sheria hawataukwepa", alisema Rutaguza.

Amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kutokuibiwa na matapeli hawa wa Bima kwa kununua Bima kwenye ofisi zilizosajiliwa na kupewa Leseni na Serikali kwa ajili ya kufanya biashara ya Bima na kuacha kununua Bima kiholela mitaani kwa watu wasiofahamika.
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima(TIRA) Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza.Picha na Vero Ignatus Blog.
Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA)  kanda ya kati ,Adamu Maneno (katikati)akihakiki stika ya bima kama ni halali au feki stendi ya  Hiace jamatini Dodoma,kulia kwake ni PC Majenga,kushoto kwake ni Liberath wakala wa bima mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Afisa mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Kati Rojas Msagati (katikati)akiwa anahakiki moja ya gari katika stendi ya jamatini Dodoma ,kulia.kwake ni WP 4079CPL Karitas.Picha na Vero Ignatus Blog.

TUTAENDELEZA UTALII WA PICHA KATIKA PORI LA AKIBA BURIGI - DK. KIGWANGALLA

$
0
0
Baadhi ya Twiga wanaopatikana katika Pori la Akiba Burigi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Malmlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata kuhusu mipango mbalimbali ya mamlaka hiyo kuendeleza utalii katika Pori la Akiba Burigi alipotembelea pori hilo jana mkoani Kagera.
Ndege aina mbalimbali pia ni kivutio katika pori hilo.
Viboko nao wanapatikana katika pori hilo ndani ya ziwa Burigi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti baada ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.

HABARI  ZAIDI BOFYA HAPA

MAVUNDE AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 35 KIWANDA CHA NYUZI CHA PPTL KILICHOKO MKOANI TANGA KWA UKIUKWAJI WA SHERIA

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amekitoza faini ya shilinhgi milioni 35 (milioni thelathini na tano), kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko eneo la Kange Mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Mavunde alichukua uamuzi huo, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo Machi 2, 2018 ili kubaini waajiri ambao hawatekeelzi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

Naibu Waziri Mavunde, alikuta wafanyakazi wa kiwanda hicho ambacho kina mashine nyingi na kutokana na mfumo wa utendaji kazi wake, kinatoa kelelenyingi hawakuvaa vifaa vya kujikinga na madhara kazini, (protective gears).

Mhe. Mavunde aliwakuta baadhi yao wakiwa wamevaa kandambiloi, wengine hawana vifaa vya kuziba masikio kujihami na kelele, pamoja na vifaa vingine. Hatua hiyo ilimkasirisha Mhe. Navu Waziri na kumuagiza Afisa wa OSHA, kuchukua hatua mara moja ambapo kiwanda hicho kilitozwa faini ya shilingi milioni 35 kwa kukiuka Sheria ya ajira na mahusiano kazini ambapo pamoja na mambo mengine inasisitioza usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi kuvaa vifaa vya kujihami.

Aidha Mhe. Mavunde ambaye kabla ya kufika Mkoani Tanga, alitembelea mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kilimanjaro, ameuagiza uongozi wa kiwanda hivho kuondoa kasoro hizo mara moja.Sambamba na hilo, Mhe. Mavunde amesema, serikali haitabadili msimamo wake wa kuwafikisha mahakamani waajiri wote ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) kwani kwa kutofanya hivyo wanakabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo kupelekwa mahakamani ambapo mwajiri atakayepatikana na hatia atalazimika kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi Milioni 50,000, (Milioni Hamsini), au kifungo kisichopungua miaka mitano (5) au vyote kwa pamoja.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya  kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018. 

Naibu Waziri akitembelea kiwanda hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018.
Nabu Waziri Mavunde, akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, wakati walipotembelea kiwanda bhicho cha PPTL.

JUKWAA LA WANAWAKE SOMANGILA, KIGAMBONI, LAZINDULIWA

$
0
0

Na Bashir Nkoromo, Kigamboni.

Wanawake wajasiariliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi.


Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.



Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Dege katika Kata hiyo  Angela alisema mbali na na bidhaa bora kuhamasisha wanunuzi na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi boa bidhaa hizo zinaweza kumudu ushindani katika soko.



Alivishauri vikundi vya Wanawake wajasiriamali kwenda kuomba mikopo kwenye Benki ya Wanawake Tanzania ambayo alisema ni benki yenye mikopo ya riba nafuu.



Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mapema mwezi huu.

 Wanawake wa vikundi vya Wajasiriamali wakiandamana kutoka kwenye Ofisi yao kwenda kwenye uwanja wa Dege, kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, leo
 Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akisoma moja ya mabango waliyokuwa nayo Wanawake Wajasiliamali walipowasili Uwanjani kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila.

 Angel Akilimali akitazama mkeka uliotengenezwa na Mwanamke Mjasiriamali Jawa Maulidi (kushoto)
 Angel Akilimali (kushoto) akimuuliza Mwanamke Mjasiriamali jinsi anavyotengeneza bidhaa zake.
 Angel Akilimali na Diwani Chichi wakinywa togwa kwenye banda la maonyesho la Mwanamke Mjasiriamali, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni. 


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

:RC RUVUMA AWAONYA WATAKAO KWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo katika kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME, alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha MTYENGIMBOLE katika halimashauri ya MADABA, ambapo serikali imetoa shilingi milioni mia tano kwa ajili ya kituo hicho.

Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo katika kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ili kuleta maendeleo kwa wananchi.Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME, alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha MTYENGIMBOLE katika halimashauri ya MADABA, ambapo serikali imetoa shilingi milioni mia tano kwa ajili ya kituo hicho.

Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo katika kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ili kuleta maendeleo kwa wananchi.Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME, alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha MTYENGIMBOLE katika halimashauri ya MADABA, ambapo serikali imetoa shilingi milioni mia tano kwa ajili ya kituo hicho.

Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo katika kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ili kuleta maendeleo kwa wananchi.Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME, alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha MTYENGIMBOLE katika halimashauri ya MADABA, ambapo serikali imetoa shilingi milioni mia tano kwa ajili ya kituo hicho.

DKT MWIGULU AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba  ametembelea kukagua ujenzi wa nyumba za polisi wilaya ya Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto uliyotokea mwaka jana umefikiaje mpaka sasa na kuridhika na hatua iliyofikia.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
Nyumba za askari polisi ambazo ni za kisasa kabisa zikiwa tayari ,nyumba hizo zimejengwa kufuatia hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huo uanze mara moja

Dkt mwigulu amesema ameridhika na hatua iliyofikia ya ujenzi wa nyumba za askari polisi ambazo ni za kisasa kabisa na kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huu uanze mara moja, pia mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewashukuru Wafanyabiashara wa Arusha kusaidia ujenzi wa nyumba hizo mpaka sasa ulipo kamilika, kwani walichukua hatua mapema tu pale moto ulipotokea.

"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba hapa ndipo ninapokaa, hili ni jambo jema ,kama Waziri namshukuru sana Rais Dkt Magufuli,na kwa hakika jambo hili litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanayoifanya" ,alisema Dkt Mwigulu.

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru waziri Mwigulu kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo na kufikia hapo kwani kama Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya ndani amekuwa karibu nao sana na kukagua kila hatua inayofikiwa.
RC Gambo ameongeza kusema kuwa kwasasa wamemuomba waziri Mwigulu awasaidie gari la polisi katika kituo cha polisi murieti na amekubali kuwasaidia kuwaletea gari ili kusaidia kupunguza matukio ya kiharifu maeneo hayo kwani kwasasa mji huo watu wengi wanaishi maeneo hayo na askari wanategemea gari linalotoka kituo kikuu cha polisi Arusha.

RPC MWANZA AWASISITIZA ASKARI KUEPUKA UBAMBIKAJI KESI

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi amewasisitiza askari kuepuka ubambikaji kesi kwa wananchi, rushwa na ubabaishaji pia akiwataka askari kufanya kazi kwa utii, nidhamu na maadili kama ambavyo Jeshi la Polisi Tanzania linavyoelekeza. Hayo yamejiri tarehe 28/02/2018 wakati Kamanda Msangi alipokutana na askari wa Wilaya ya Sengerema katika ukaguzi anaoendelea kuufanya katika Wilaya na Vikosi vyote hapa Mkoani Mwanza.

Amewataka askari kukomesha vitendo vya ubabaishaji kwa wananchi na ubambikaji kesi kama vipo, mfano kesi ya madai inabadilishwa kuwa kesi ya jinai jambo ambalo linanyima haki wananchi na kuchafua sifa nzuri ya Jeshi la Polisi. Hivyo ubabaishaji wa aina hiyo uepukwe na yeyote atakaye bainika anafanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hilo Kamanda Msangi amewataka askari wa kila kitengo kusimama vyema katika nafasi zao, ambapo alisema kila askari akiwa vizuri katika utendaji kazi hakutakuwa na malalamiko yeyote toka kwa wananchi hivyo ni jukumu la kila askari kuhakikisha dhamana aliyopewa na serikali ya kulinda wananchi pamoja na mali zao  anaisimamia vizuri bila ubabaishaji wa aina yeyote ile.
Pia aliwataka askari wawe na utaratibu mzuri wa upokeaji, utunzaji na uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi, kwani katika baadhi ya vituo vya Polisi lipo tatizo la utunzaji wa vielelezo hivyo hataki kuona tatizo hilo linaendelea kuwepo. Vilelele aliwataka Maofisa wa Polisi wa Wilayani hapo kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria za uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi.

Hata hivyo alisema hategemei kuona mlundikano wa vielelezo katika vituo vya Polisi ambavyo vimekaa vituoni mwaka mmoja au zaidi. Kwani madhara yake vinaweza kuharibika, kupoteza ubora au kupotea alafu baadae liwe deni kwa Jeshi. Hivyo aliwataka askari kutekeleza maamuzi ya mahakama haraka juu ya uondoshaji wa kielelezo/vielelezo baada ya kesi kumalizika mahakamani.

Kwa upande wa upelelezi alisema kumekuwa na tatizo la kuchelewesha upelelezi wa kesi nyingi. Jambo ambalo linawanyima wananchi haki. Hivyo alimtaka Mkuu wa Upelelezi Wilayani hapo kushughulikia suala hilo mapema lisiwepo katika himaya yake ili haki ipatikane haraka bila uonevu wa aina yeyote.

Pia aliwapongeza askari wa Wilaya hiyo kwa utendaji mzuri wa kudhibiti uhalifu, aliwataka waongeze juhudi kwa yale maeneo yenye vibaka na uhalifu mwingine mdogomdogo kwani anaamini wanaweza. Ushirikiano ulipo na Viongozi wa ulinzi na usalama Wilaya, Wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama udumishwe ili Sengerema iwe salama zaidi kwani amani ikiwepo maendeleo yatapatikana zaidi.

Imeandaliwa na Oscar Msuya, Mwandishi wa Polisi Mwanza.

HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali Mkoani humo haijawakataa wadau wa Afya kutoka katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa wanaofanya kazi mbalimbali  katika  kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye Sekta ya Afya, bali inatambua mchango wao na inawaomba kufanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa kwenye Sekta ya Afya.

Mtaka ameyasema hayo katika mazungumzo maalum na waandishi wa Habari wakati alipokuwa akifafanua kauli aliyoitoa katika kikao kilichofanyika Februari 25 na 26 Mjini Bariadi kati ya Viongozi wa Mkoa huo na Wadau Afya mkoani humo ya kuwataka kuelekeza zaidi fedha zao katika kujibu mahitaji ya wananchi kwenye Afya badala ya semina na mafunzo kwa watumishi.

Amesema Serikali inatambua mchango wa Mashirika na wadau wa Afya Mkoani humo kutokana na mambo waliyoyafanya kuunga mkono Serikali kutatatua changamoto mbalimbali za Sekta ya Afya, ikiwa ni pamoja na kutoa magari, kujenga majengo ya upasuaji katika baadhi ya Vituo vya Afya na kuwajengea uwezo watumishi wa afya.
Ameongeza kuwa pamoja na michango hiyo Mashirika mengi yanayofanya kazi Mkoani Simiyu katika Sekta ya Afya yameonekana kujikita zaidi katika kutoa fedha nyingi kwa ajili ya semina na mafunzo kwa watumishi wa Afya , badala ya kusaidia katika kutatua changamoto ambazo ni vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa pia katika Sekta ya Afya.
Aidha. Mtaka amebainisha kuwa Vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa  katika Sekta ya Afya ni pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Afya ambayo ni majengo ya zahanati, vituo vya afya, vyumba vya upasuaji, hospitali), Vifaa pamoja na vifaa tiba,  ambapo alieleza kuwa Mkoa huo una upungufu wa Hospitali ya Mkoa, Hospitali mbili za Wilaya, Vituo vya Afya 112 na Zahanati 291.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Machi O2, 2018 Mjini Bariadi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WAKANDARASI WOTE WALIOHUJUMU MIRADI YA MAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameitaka Bodi ya Usajili ya Wakandarasi nchini (CRB) kuwachukulia hatua kali wakandarasi wote walioihujumu Serikali katika miradi ya maji inayotekelezwa nchini.
Naibu Waziri Aweso ametoa tamko hilo mara baada ya kufanya kikao na bodi hiyo na kutaka ufanyike uchunguzi wa kwa miradi yote ambayo utekelezaji wake umegibikwa na utata na wakandarasi wote watakaobainika kutekeleza miradi hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesema hatuwezi kufika popote tukiendelea kuwalea wakandarasi wasio na uwezo ambao wamekuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji, hatutawaendekeza tena wakandarasi wa aina hii, kwa kuwa wamekuwa chanzo cha kukwamisha juhudi za Serikali katika kuiletea nchi maendelo.
‘‘Naomba mfanye uchunguzi wa kina katika miradi yote ya maji iliyohujumiwa nchini, wizara yangu itawapa ushirikiano wa kutosha ili tuweze kuwabaini wakandarasi waliohusika na ikithibitika kuwa ni kweli wachukuliwe hatua kali na ikibidi wafutiwe usajili kabisa’’, alisema Aweso.
Hata hivyo, amesema wako pamoja na wakandarasi wazawa na watarajie ushirikiano wa dhati kutoka kwa Serikali. Tutawapa kipaumbele wakandarasi wazalendo kwenye miradi ya Serikali na walio waaminifu tutawapa kazi zaidi, tutasimamia na kuhakikisha fedha zao zinalipwa kwa wakati ili watimize majikumu yao kwa ufanisi.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza katika kikao cha pamoja na Wakurugenzi wa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB) katika ofisi za bodi hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CRB, Joseph Tango na wajumbe wengine wa CRB.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia bomba la maji lililopo kwenye karakana ya Bohari Kuu ya Maji, nyuma yake ni Boharia Mkuu, Crepin Bulamu.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye karakana ya Bohari Kuu ya Maji iliyopo Boko, jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wasanii wa Filamu Nchini Waaswa Kuzingatia Maadili

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo akionyesha Leseni inayotolewa na bodi hiyo kwa ajili ya waendeshaji wa vibanda vya kuonyeshea filamu wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha Bi. Irene Ngao na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Gasper Tesha.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo akiwasilisha mada  wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
  Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo na kulia ni Afisa Utamduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
 Katibu wa Umoja wa Wasanii wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Mkoa wa Arusha (TDFA), Said Mohamed Gogola akichangia mada wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo (waliokaa kwenye viti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo (kulia) akiagana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Hargeney Chitukuro mara baada ya kumaliza kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.

MABINGWA TIMU YA IRINGA UNITED KUUWAKISHA MKOA WA IRINGA KWENYE LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

$
0
0

Na Fredy Mgunda,Iringa.

TIMU ya Soka ya Iringa United imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Mkoa wa Iringa baada ya kuibuka na ushindi penati 3 - 1 dhidi ya Mtwivila Fc.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Samora timu ya Mtwivila Fc walikuwa wa kwanza kupata bao dk 8 kupitia kwa mshambuliaji hatari David Mwanga baada uzembe wa golikipa wa Iringa United Nelly Mkakilwa kuponyokwa na mpira na kumpita tobo.

Mchezo huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila walikuwa wakiongoza bao 1.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha kufika fainali ya ligi ya Mkoa kwa Mtwivila wakitaka kuongeza huku Iringa wakitaka kurudisha.Mchezaji bora wa mechi ya nusu fainali Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya kusawazisha goli katika dk 76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana.

Mara ya dakika 90 kumalizika ndipo hatua za kupigiana matuta ilipowadia ambapo timu ya Mtwivila fc ilikosa penati 3 na Iringa United kupata penati 3 dhidi ya 1. Kutokana na ushindi huo timu ya Iringa United imejinyakulia jezi seti moja, mipira miwili huku timu ya Mtwivila wakiondoka na jezi na mpira mmoja.Mchezaji bora wa mashindano hayo aliibuka Razack Kibuga wa Iringa United aliyeondoka na zawadi ya sh.100,000 na cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa United aliyepata sh.50000


Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi kombe kampteni wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja 
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja 
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi mchezaji bora wa mashindano Razack Kibuga ambaye ametoka katika timu ya Iringa United


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAHLISO YATOA TAMKO WANAFUNZI WANAOTAKA MWIGULU AJIUZULU KWA KIFO CHA AKWILINA.

$
0
0

JUMUIYA YA TAASISI ZA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA
(TAHLISO)OFISI YA MWENYEKITI TAHLISO

Ndugu waandishi wa habari tunawashukuru sana kwa kukubali wito wetu wa kuja kujumuika pamoja na sisi. Leo tarehe 3/3/2018 tumekuta na viongozi wa vyuo vikuu nchi nzima kwa ajili yakujadili changamoto zinazotukabili. Kikao hiki ni cha TAHLISO BarazaKuu (SENATE) kinacho husisha Maraisi wa serikali za wanafunzi wa VyuoVikuunchini.
Tunatambuakwambakunakifo cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina Akwilini,mwanafunziwachuo cha NIT kilichotokea mwezi wa pili. Tunawashukuruwanafunziwenzetukwautulivumkubwanamshikamanowaliouoneshatangumsibaulipotokea, wakatiwakipindi cha majonzihadikufikiasasa.
TunamshukuruMhe.Raisi wa Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuingilia kati suala hili na kuagiza uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kuhusika na kifo cha AkwilinaAkwilini. 
VileviletunaishukuruWizarayaElimu, Sayansi na Teknolojia kwa ukaribu waliouonesha katika kipindi chote cha msiba.Tunaomba wanafunzi waendelee kuwa watulivu wakati maagizo yaMh. Raisi yakitekelezwa.
Aidha tunapenda jamiii tambue kuwa TAHLISO ndio chombo kikuu cha kuwasemea wanafunzi wote nchi nzima Tanzania na sio kikundi kingine chochote kile. 
Vipovikundivingivimejitokezanakutoamatamkombalimbalibaadayakifohikikutokea, vikundivinginevikaendambali Zaidi kwakuwataka baadhiya watendajiwa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo yaNdani kujiuzulu jambo ambalo linaashiria vikundi hivyo kuongozwa ama kutumika namakundiyakisiasa, haiwezekani kutaka watendajiwa Serikali wajiuzulu wakati uchunguzi bado unafanyika na matokeoya uchunguzi huo bado hayajatoka.

Mwenyekiti wa Tahlisi George Albert  Mnali  wa pili kutoka kulia akizungumza na baraza Kuu la Senate leo  kushoto ni Katibu Mkuu wa Tahliso John Mboya kulia ni Katibu wa Baraza hilo Faidhaa Msangi na kulia ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Rais wa Chuo cha Zanzibar University.
 Sehemu ya Marais wa Vyuo Vikuu nchini wakiwa kwenye mkutano huo
Jambo la kusikitisha Zaidi kuna baadhi ya vikundi vimejitangaza kwamba vinaungwa mkono na Maraisi waVyuoVikuu jambo ambalo sio la kweli, Marais wote waVyuo Vikuu tuko hapa Dodoma tunaendelea na vikao vyetu vya kujadili changamoto zinazowakabili wanafunziwa VyuoVikuu.
Tunatoa wito kwa vikundi vyote vinavyojihusisha nakutumia mwamvuliwa Marais waVyuoVikuu kama kinga yao ili kuu hadaaUmma kwamba wanaungwa Mkono, vikundi hivyo viache tabia hiyo vinginevyo tutawachukulia hatua za kinidhamu.
TAHLISO tunasubirimatokeoya Uchunguzi unaofanyika juu ya kifo cha Akwilina na tunaimani wahusika wote watachukuliwa hatua kali zakisheria. 
Tunawaombawanafunzi wote tuendelee kuwa watulivu wakati tukisubiri matokeo hayo na kujiepusha na maandamano na vitendo vyovyot e vitakavyo sababisha uvunjifu wa Amani nakuleta mgawanyo miongoni mwawanafunzi. 
Hata hivyo namna bora yakufikisha hoja nikutumia njia ya majadiliano kama wasomi badala ya kutumia nguvu ama maandamano kwakutofuata taratibu na madhara yake ni kusababisha vuruguzi sizotakiwa na hatimaye kuhatarisha usalama na hivyo kuathiri jamii kwaujumla wake.
Vurugu zozote zitokanazo kwakutozingatia taratibu zinaweza kudhorotesha shughuli za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Uchumiwa Taifa letu. Vile vile zinapoteza mvuto kwawawekezaji wanje na wandani, ikiwemo shughuli za utalii nchini ambazo zinachangia pato la Taifa letu. 
Athariza Vurugu na kukosekana kwa amani zipo wazi natunaziona kwa nchi nyingine zikiwemo baadhi ya nchi jirani zetu ambao wamekua wakimbizi nchini kwetu kila siku.
Tunaona kuwa kama wanataaluma tunajukumu kubwa la kuelimisha jamii na kuwamfano bora wakutumia njia za majadiliano katika kujenga hoja zetu ilizitatuliwe kuliko kutumia njia ya maandamano au vurugu zisizo na ulazimawowote.

Taasisi hii ndio yenye dhamana ya kutetea nakusimamia maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo na vyuovikuu Tanzania na si vinginevyo.
………………………………….
GEORGE ALBERT MNALI
MWENYEKITI TAHLISO

MSIUZE UFUTA WENU MASHAMBANI PELEKENI MINADANI-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa ufuta katika mikoa inayolima zao hilo nchini kuuza kwa kutumia njia ya minada na si mashambani.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Machi 03, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Nachihungo, Narungombe na Chikwale.Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi amesema ili wakulima waweze kupata tija ni vema wakauza ufuta wao kwa kupitia minada kama inavyofanyika katika zao la korosho

“Usikubali kumuuzia mtu yeyote ufuta wako ukiwa shambani kwa sababu bei atakayonunulia ni ndogo kulinganisha na soko, naamini ufuta wote ukiuzwa katika minada mtaona faida.”Kufuatia agizo hilo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue aandae utaratibu wa maeneo ya kukusanyia ufuta na kufanyia minada.

Amesema ufuta unaolimwa nchini ni bora na unapendwa sana duniani hivyo wasiwe na wasiwasi. Baadhi ya Mikoa inayolima ufuta kwa wingi ni Lindi, Pwani, Dodoma, Manyara, Kigoma na Singida.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema vijiji vote visivyokuwa na umeme nchini vikiwemo vya wilaya ya Ruangwa vitaunganishiwa katika REA awamu ya tatu.

Amesema wananchi waendelee kuwa na subira kwa sababu tayari mkandarasi ameshaanza kazi ya kuunganisha umeme katika vijiji vingine vya wilaya hiyo na atafika kwenye maeneo yao.Alibainisha kuwa mkakati wa Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wote nchini waunganishiwa nishati ya umeme kwenye majumba yao, hivyo waendelee kuwa na subira na kushirikiana na Serikali yao.
 
Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama alisema, “Huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo vijiji vyote vitapata maji”.Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kote nchini kutunza vyanzo vya maji ili kuliepusha taifa kugeuka jangwa pia miradi inayoletwa na Serikali iwe endelevu.

Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akisalimiana na Diwani wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akisalimiana na Diwani wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na mzee Omar Issa, katika Kata ya Narungombe, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni, katikati ni mzee Mussa Lambamba. Machi,5 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee Omar Issa kulia na mzee Mussa Lambamba katikati, katika Kata ya Narungombe, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni, katikati ni mzee Mussa Lambamba. Machi,5 2018,.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MBUNGE LUCY MAYENGA AMWAGA MABATI UJENZI WA ZAHANATI KATA YA CHADEMA KITANGIRI

$
0
0
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) ametoa msaada wa mabati 128 kwa ajili ya kuezeka zahanati ya Kitangiri iliyopo katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga ambayo ipo kwenye hatua ya upauaji. 

Akizungungumza wakati wa kukabidhi mabati hayo, Mhe. Mayenga juzi alisema uamuzi wa kusaidia hatua hiyo unatokana na ari aliyonayo ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila kusafiri umbali mrefu.

"Mheshimiwa diwani wa kata ya Kitangiri wewe ni Chadema lakini nimefarijika umehudhuria zoezi hili la makabidhiano, hii inaonesha dhamira ya kutekeleza ilani yetu ya CCM na unamuunga kwa dhati mheshimiwa rais wetu katika jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa" alisema Mhe. Mayenga.

Aidha Mayenga alibainisha kuwa maendeleo hayana itikadi za vyama vya siasa,dini wala rangi hivyo kuwaomba wananchi kushirikiana katika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itamnufaisha kila mtu.

"Tunataka zahanati hii ikamilike ili wananchi wapate huduma bora za afya,niwakumbushe tu kuwa ugonjwa huwa hauangalii kwamba wewe ni CCM,Chadema au ACT Wazalendo ama chama chochote kile, naomba tuweke pembeni itikadi za vyama kwenye masuala ya maendeleo",aliongeza.

Mbunge huyo pia aliahidi kusaidia kununua magodoro yote katika zahanati hiyo pindi itakapokamilika.Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Omar Ngunila (Chadema) alisema amefarijika kwa kata yake kupata msaada huo kwani zahanati hiyo ikikamilika itasaidia kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kitangiri Mohammed Mulabo (CCM) alisema alilazimika kumuomba mbunge Lucy Mayenga msaada wa mabati kutokana na changamoto ya umbali wa kupata huduma wanayoipata wananchi wake.

Alisema kata hiyo yenye zaidi ya wakazi 13,000 wananchi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hivyo wengine kulazimika kwenda zahanati binafsi kupata huduma."Mheshimiwa Mayenga leo umetukomboa kwa msaada huu naomba mkurugenzi wa halmashauri amalize haraka hatua zilizobaki ili zahanati ifanye kazi",aliongeza.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 128 kwa ajili ya ujenzi wa zanahati ya Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akishikana mkono na mwenyekiti wa mtaa wa Kitangiri Mohammed Mulabo (CCM) wakati wa kukabidhi mabati katika zanahati ya Kitangiri. Aliyevaa nguo nyeupe kulia ni diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Omar Ngunila (Chadema).
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akiendelea kukabidhi mabati hayo.
Zoezi la makabidhiano likiendelea

SIMBA YATAJA KIINGILIO CHA MECHI YAO DHIDI YA AL-MASRY MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO

$
0
0
Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya klabu ya Al Masry kutoka nchini Misri siku ya Jumatano ya tarehe 7/3/2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza mishale ya saa 12 kamili jioni, Aidha viingilio katika mchezo huo vinataraji kuwa katika bei zifuatavyo;-
VIP A – Tsh 20000
VIP B – Tsh 15000

III. Mzunguko/Orange – Tsh 5000.

Tiketi za kuingilia uwanjani siku hiyo zitaanza kuuzwa siku ya Jumatatu kwa mawakala wa Selcom na vituo vitakavyotangazwa hapo baadae.

Klabu inawaomba mashabiki na wapenzi wa klabu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangilia timu yao itakapokuwa inacheza, aidha inawakumbusha kununua tiketi za mechi hiyo kwa wakati.

Katika hatua nyingine,Klabu ya Al Masri inataraji kuwasili nchini siku ya Kesho Jumapili majira ya saa 12 jioni,na itafanya mazoezi siku ya Jumatatu jioni katika Uwanja Taifa.

Pia,waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Afrika kusini wanatarji kuwasili nchini siku ya Jumatatu saa 10 jioni.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club,
Haji S. Manara
3/3/2018
Simba Nguvu Moja..!!!
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images