Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

Mbunge Mabula apambana kuondoa kero tatizo la Maji Shule za Msingi.

0
0
Mhe Stanislaus Mabula Leo amemkabidhi tenki kubwa la maji Diwani mteule Kata ya Isamilo Mhe Charlse Nyamasiriri linaloweza kuhifadhi lita 10000 za maji kwa ajili ya shule ya Secondari ya Ole Njoolay iliyopo Kata ya Isamilo. Hii ni sehemu ya ya utekelezaji wa mkakati wa kuondoka kero za tatizo la maji katika shule za msingi na sekondari Jiji la Mwanza.

Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini za mbunge Jimbo la Nyamagana.
Mwanza kwanza, Tukutane kazini
Tulianza na Mungu, tutaendelea na Mungu

Imetolewa na,
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿 @ Mwanza.

TGNP Mtandao wakutanisha madiwani 20 kujadili kushirikiana

0
0
Zaidi ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Madiwani hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime (Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).

Madiwani hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi unaotekelezwa katika eneo hilo.

Pamoja na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.

Wakiwa kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.Eneo hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.
Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

YANGA TENA UGENINI DHIDI YA SINGIDA UNITED KOMBE LA FA

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Droo ya upangaji wa ratiba ya michezo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam sports Federation Cup (ASFC) imefanyika mapema mda huu na kila timu kumfahamu mpinzani wake.

Droo hiyo iliyokuwa inachezwa moja kwa moja na kituo cha Azam Tv imekamilika kwa Singida United kuwa mwenyeji wa Yanga katika uwanja wa Namfua Mkoani Singida.

Michezo mingine ni Tanzania Prisons wakiwakaribisha JKT
 Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya huku Azam wakiwa wenyeji dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo wa nne Stand United watavaana na Njombe Mji kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Tigo Pesa to offer Masterpass QR in Tanzania

0
0
With over 40 million mobile users in Tanzania, there is a real opportunity to use technology to financially connect those not yet included. Tigo Tanzania, Mastercard and leading local fintech Selcom have partnered to introduce Masterpass QR on Tigo’s Mobile Financial Services platform, called Tigo Pesa. 

Almost seven million registered wallet holders of the Tigo Pesa solution will be able to securely pay for goods and services before the end of the second quarter of 2018. By simply scanning a Quick Response (QR) code at merchants via their Tigo Pesa app using their smart phone, they will be able to pay more quickly than ever before. Feature phone users can use the USSD menu and simply type in a unique merchant code available under the merchant’s QR code.

The partnership announcement during the Mobile World Congress marks the launch of the country’s first truly global interoperable QR payment solution, allowing payments by both mobile money users and banked consumers at locations displaying the Masterpass QR logo.

“Tigo Pesa is not only a payments enabler,” said Simon Karikari, Managing Director at Tigo Tanzania. “It is a platform where customers can perform a full range of financial services, where Masterpass is a strong addition to the range of products and services our customers can enjoy in their daily lives.”

Tanzania has made great strides in financially including its citizens in the past decade: the percentage of Tanzanians formally part of the economy was positioned at only 15.8 percent in 2009, but that number has jumped to over 65 percent in the last year, driven largely by the introduction of easily accessible mobile solutions such as Tigo Pesa.

Raghav Prasad, Division President for Sub-Saharan Africa, Mastercard said, “Findings released in the 2017 FinScope Tanzania report further indicate that one of the main drivers of access to financial services in Tanzania has been the adoption of digital financial services. A trend we are seeing across the continent, and in emerging markets globally.”

He went on to add that with over 85 percent of retail transactions still being done in cash in Africa, accessible and secure payment solutions are key to bridging the gap. This is further reinforced by local research which reveals that 89 percent of consumers are still receiving income and making payments in cash. “We need to urgently action the shift from cash to smarter digital solutions, and Tigo Pesa enabling Masterpass QR payments is allowing this goal to become a reality.”

Tigo is a strong brand in the Tanzania market, with our mobile financial services platform, Tigo Pesa, as a powerful driver to achieve financial inclusion across Tanzania. With the addition of Mastercard’s Masterpass QR solution we are not only able to further strengthen our offering and ensure secure payments for all users, but also to bring much faster and more convenient payments to the fingertips of our customers. We have a vested stake in ensuring the country’s prosperity and that of its people, where partnership will be critical to achieving this goal and introducing more efficient ways for consumers to engage with the world around them,” concluded Simon Karikari, Managing Director at Tigo Tanzania.

Waziri wa Mwijage afanya ziara Mkoani Njombe

0
0
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipomtembelea ofisini kwake kupata taarifa ya Viwanda na uwekezaji katika mkoa huo, tarehe 1 Machi, 2018.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bibi. Ruth Blasio Msafiri walipofika ofisi za SIDO Mkoa wa Njombe kuona utendaji wake.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akikagua eneo litakalojengwa majengo makubwa kwa ajili ya wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo, Mkoani Njombe tarehe 1 Machi, 2018.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akimsikiliza meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Njombe kuhusu utaratibu wanaotumia katika kupima mizigo ya wakulima na wafanyabiashara mkoani Njombe.
 Muonekano wa Kiwanda cha kuchakata Chai cha Unilever kilichopo mkoani Njombe ambacho kipo katika hatua za mwisho kukamilika kwa ujenzi wake.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano na wafanyabiashara kujadili changamoto zianazowakabili wafanyabiashara katika mkoa wa Njombe Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bibi. Ruth Blasio Msafiri. 
Wadau na wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe waliokusanyika kumsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Hayupo pichani) na baadae kuuliza maswali kutokana na changamoto wanazokutana nazo na kupatiwa majibu.

NYONGO ATAKA MADINI YA NICKEL YAONGEZWE THAMANI NCHINI

0
0
Na Veronica Simba – Ngara
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali itaboresha mazingira ya uwekezaji wa Madini ya Nickel yanayopatikana Ngara mkoani Kagera lakini pia itahakikisha wawekezaji wanayaongezea thamani Madini hayo hapa nchini kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi ili kuleta tija zaidi.
Aliyasema hayo jana, Machi Mosi alipotembelea Mradi wa Uwekezaji wa Madini ya Nickel wa Kabanga, uliopo wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera, akiwa katika ziara ya kazi.
“Sisi kama Serikali tutahakikisha tunawaletea wawekezaji miundombinu ya Barabara, Reli na Umeme ili kuwajengea mazingira rafiki ya uzalishaji lakini kwa upande wao tunataka kuona uwekezaji makini; wachimbe na kuongeza thamani ya madini hayo hapa nchini. Badala ya kutoa Nickel kama malighafi, watoe bidhaa zinazotokana na Nickel.”
Alisema kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha Madini hayo muhimu, ambayo kwa sasa Soko lake Duniani limeanza kupanda, yanalinufaisha Taifa kwa kiwango kinachostahili.
Akifafanua, Naibu Waziri alisema kuwa, Nickel ikiongezewa thamani hapa nchini, miundombinu ya Reli, Umeme na Barabara ikaboreshwa; kutakuwa na uhakika wa kuuza Madini hayo kwa bei nzuri na kuleta ushindani kwenye Soko la Dunia.
Meneja Mkazi wa Mradi wa Kabanga Nickel, Andrew Msola akiwasilisha Taarifa ya Utendaji kazi wa Mradi huo kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe aliofuatana nao, alipotembelea na kukagua Mradi huo akiwa katika ziara ya kazi, Machi Mosi mwaka huu.
Sehemu ya shehena ya Madini ya Nickel kama ilivyokutwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), katika Mradi wa Kabanga Nickel, Wilayani Ngara Mkoa wa Kagera, Machi Mosi mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukagua Mradi wa Kabanga Nickel uliopo Wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera, Machi Mosi mwaka huu akiwa katika ziara ya kazi.

Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure

0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaosomea Shahada ya Ualimu wameunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika  Utoaji wa Elimu Msingi bila malipo kwa kujitolea kwenda kufundisha katika shule za msingi na Sekondari zilizoko katika maeneo yao wakati wa Likizo.

Akizindua mpango huo wa kujitolea kwa wanafunzi walimu zaidi ya 500 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka wanafunzi hao kuwa mfano ya kuigwa kwenye shule watakazoenda kufundisha ili kuipa heshima zaidi programu hii iweze kuwavutia walimu wengine zaidi.

Alisema kuwa mnapofika mashuleni mkawe mfano bora kwa wadogo zenu, mkaonyeshe uwezo wenu katika kufundisha na kuwafikishia yale muhimu katika masomo yao, mkaonyeshe Umahiri katika Taaluma yenu ndipo kujitoa kwenu kutaheshimiwa na kuthaminiwa na jamii nzima ya watanzania.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (aliyesimama) akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua programu ya wanafunzi walimu kutoka Chuo Kikuu cHa Dodoma wanaokwenda kujitolea kwenye shule za Sekondari na Msingi zilizo karibu na maeneo wanayoishi.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Pro.Davis Mwamfupe akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua program ya wanafunzi walimu wa UDOM wanaokwenda kujitolea kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
 Mratibu wa program ya kujitolea kwa Wanafunzi Walimu Dr. Ombeni Msuya ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma akielelezea namna walivyojipanga kusimamia program hiyo.
 Mwenyekiti wa Wanafunzi Walimu wanaokwenda kujitolea akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyopo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kabla ya uzinduzi wa program maalumu ya kwenda kujitolea kwenye Shule za msingi na sekondari.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Azam FC, Mtibwa Sugar Uso kwa uso FA.

0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii 
Kikosi cha AzamFc kukutana na Mtibwa sugar robo fainali ya Michuano  Kombe la Shirikisho  la Azam Sports  Federation Cup (ASFC). 

Ambapo Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati AzamFc watawakaribisha Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi

Akizungumza ofisini kwake leo Jijini Dar es salaam Ofisa Habari AzamFc Jaffary Maganga amesema kuwa wanasubiri tarehe ya mchezo huo  ambayo Bado haijatajwa. 

"Tunasubiri tu tarehe ya mchezo  ili kujua  mandalizi  yetu yanakwenda vipi na ukizingatia kikosi ni kigumu,  wana wachezaji wenye uwezo mkubwa  na Mwalimu  wao ni mzuri ila tutaakikisha tunalinda ushindi wa kuchezea  nyumbani ikiwa kila Timu Ina presha ya kutaka kusonga mbele zaidi ukizingatia ni mashindano ya mtoano ambapo ukifungwa unatolewa kwenye Michuano hiyo"amesema Jaffary.  

Maganga amemalizia  kuwa mashindano hayo yenye heshima kubwa  ambapo mshindi  wa michuano hiyo hupata nafasi ya kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa  na kuiwakilisha Nchi.
Ofisa Habari Azam Fc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza ofisini kwake leo Jijini Dar es salaam kuhusu mchezo wao dhidi ya Mtibwa sugar katika droo iliyochezeshwa ya robo Fainali ya mashindano ya kombe la shirikisho  Azam  sports federation cup   (ASFC).

DKT. MPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI WA UCHUMI WA BENKI YA DUNIA

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo katika ofisi za  Wizara ya Fedha na Mipango Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli  katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maedeleo hapa nchini.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha  kati ya asilimia 6-7 kwa muda na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa  pomaja na nia ya  kuendeleza mafanikio mazuri yaliyopatikana katika awamu za Serikali zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi imara kwa kuendeleza viwanda na kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia wawekezaji wa ndani na wale wa nje   kuja kuwekeza nchini , kujenga miundombinu  ya barabara, reli, umeme , viwanja vya ndege na kuongeza uwekezaji katika utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji.
 Mkurugenzi wa Uchumi Jumla, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo akifafanua jambo katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na ujumbe wa Mkurugenzi wa Uchumi jumla, Biashara na Uwekezaji (hawapo pichani), katika kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James akisisitiza jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na Mkurugenzi wa Uchumi Jumla, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bi. Bella Bird na Mkurugenzi wa Uchumi, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo, mara baada ya kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

DAKTARI Bingwa mwandamizi wa upasuaji mifupa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI), Paul Marealle amesema tayari wamemfanyia upasuaji Martha Malambi (25)ambaye amenusurika kufa baada ya kupambana na mamba katika mto Mgeta uliopo Dakawa mkoani Morogoro.

Martha alifikishwa MOI kwa ajili ya matibabu zaidi kabla ya kufanyiwa upasuaji huo leo asubuhi, alianza kupatiwa matibabu mengine ya kutibu majereha yaliyopo mwilini yaliyotokana na meno ya mamba wakati anapambana kuokoa maisha yake.

Akizungumza na Michuzi Blogu leo, Dk.Marealle amesema tayari Martha amefanyiwa upasuaji na sasa anaendelea vizuri.

Dk. Marealle amesema Martha alipata jeraha kubwa la kuvunjika mfupa wa paja la mguu wa kulia,hivyo pamoja na tiba nyingine wamemfanyia upasuaji na kumuwekea chuma ndani ya paja.

"Mgonjwa anaendelea vizuri , tumefanikiwa kumfanyia upasuaji na amerudishwa wodini kwa ajili ya mapumziko na uangalizi zaidi.Kwa kuwa upasuaji umefanyika ataruhusiwa ndani ya siku mbili hizi,"amesema Dk.Marealle.

Martha ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Ukutu huko Dakawa mkoani Morogoro,akielezea tukio hilo kwa kifupi anasema kinachomuuma zaidi mbali ya yeye kujeruhiwa ni mtoto wake wa mwaka mmoja Godfrey David amefariki wakati wa tukio hilo na maiti yake imesombwa na maji.

Amesema akiwa mtoni alikoenda kuteka maji, wakati anajiandaa kuondoka mtoni, ghafla alitokea mamba mkubwa na kisha kuvuta mguu na kumtupia kwenye kina kirefu cha maji.

Wakati anahangaika kujiokoa ndipo mtoto wake alipokunywa maji mengi na kumsababisha kifo na maiti yake imesombwa na maji. Kwani alikuwa amembeba mgongoni na hivyo kanga ilifunguka na mtoto kwenda na maji.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KWANZA WA GLOBAL DRYLAND ALLIANCE ULIOFANYIKA QATAR

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017 unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa. 
Kikao hicho kilizinduliwa rasmi na mwenyewe wa mkutano huo Mhe. Mohammed bin Abdullah Al Rumaihi Waziri wa Manispa na Mazingira wa Qatar. Na baadae kuendeshwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja huo ambae pia ni Waziri wa Kilimo wa Benin. 
Balozi Fatma M. Rajab akifuatilia mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance Tanzania ambapo alimwakilisha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo umefanyika Kwenye Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Doha, Qatar. 
Mkutano ukiendelea. 
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Global Dryland Alliance mjini Doha. 

HALMASHAURI YA MJI GEITA YAPITISHA BILIONI 44.9 MWAKA WA FEDHA 2018/19

0
0
Na,Consolata Evarist,Geita

Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita,Wilayani Halmashauri ya Mji Geita limepitisha makadirio ya bajeti ya matumizi ya ya mwaka wa fedha 2018/2019 kiasi cha shilingi Bilioni 44,983,764,197.00 katika shughuli mbalimbali za Halmashauri. 

Kati ya Fedha hizo Jumla ya Tsh 15,585,248,344.00 ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ikiwa ni Mapato ya Ndani, Ruzuku ya Serikali na Wahisani mbalimbali. Tshs. 4,765,976,688.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikali kuu na Mapato ya ndani na Tshs. 24,632, 539,165.00 kwa ajili ya mishahara.

Aidha Halmashauri imekisia kukusanya Jumla ya Tsh 5,114,157,735.00 toka vyanzo vya ndani ambayo fedha hii imejumuishwa katika jumla ya Bajeti ya mwaka 2018/2019. Jumla ya Tsh. 3,030,016,641.00 sawa na 60% zimetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Akiongeza katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita kwenye kikoa cha kupitisha bajeti ya Mwaka wa fedha 2018/2019,Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali alisema Bajeti hyo imezingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa kuandaa Bajeti uliotolewa na Wizara ya Fedha Mwezi, Novemba 2016, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030); Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, Mpango wa Pili wa miaka Mitano (FDYPII) 2016/17-2020/21 na Lengo likiwa ni kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2030.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly Akizungumza wakati wa kikao cha kupitisha Bajeti ya fedha ya mwaka 2018/19. 
Baadhi ya watumishi na wakuu wa idara wakiwa kwenye Kikao cha kupitisha Bajeti ya fedha ya mwaka 2018/19. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita Mheshimiwa Leonard Kiganga Bugomola,akizungumza wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19. 
Meza kuu ikiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali na chama cha mapinduzi.


WAFADHILI WARIDHISHWA MAENDELEO YA MRADI MAJARIBIO WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KWA WATOTO WALIO NA FURSA NDOGO

0
0
Wadau wa mradi wa miaka mitano wenye lengo la kutumia teknolojia ya kisasa kuwawezesha watoto waliona fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) wameeleza kuridhishwa kwao na maendeleo ya majaribio hayo. 

Wadau ambao walikuwa na ziara ya siku moja kutembelea vijiji mbalimbali vya nradi huo katika wilaya za Muheza na Pangani wadau aho ambao walikuwa pamoja na Mwakilishi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Tanzania, Michael Dunford, Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya Kanda ya Afrika Mashariki, Anne Ndong-Jatta wakiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said.

Wakitoa maoni wakati wakipewa maelezo walisema ni wazi mradi umeanza kuonyesha uwezo wa teknolojia kuamsha ari ya kujifunza na kusoma.Taarufa za awali za mradi na ushuhuda tuliouona inaonyesha kuwa mpango huu wa kiteknolojia una uwezo wa kuwasha mwamko wa elimu miongoni mwa watoto na wazazi na unapaswa kutiliwa maanani,” alieleza Mhandisi Said wakat wa ziara hiyo. 
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiwaonyesha mmoja ya sehemu zinazotunzwa tablets ambazo zinatumiwa kufundishia wanafunzi akiwa na wafadhili wa mradi huo
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akiwaongoza wafadhili wa mradi huo kutembelea maeneo mbalimbali unapotekelezwa wilayani Pangani 
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akiwa na wafadhili wa mradi huo wakiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kutumia teknolojia ya Tablets
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiteta jambo na wafadhili wa mradi huo .




MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA

0
0
Na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhi tiketi za ndege za watu wanne kwa ajili ya safari ya matibabu ya kijana Ahmed Albaity ambaye ambaye anakwenda kutibiwa nchini China kwenye Hospitali ya Beijing.

Albaity amekuwa akiteseka kwa zaidi ya miaka 10 akiwa kitandani kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu lakini leo hii Makonda amefanikisha ndoto yake ya kumkabidhi tiketi kwa ajili kwenda nchi humo akatibiwe.
Makonda mbali ya kukabidhi tiketi, pia amejitolea kugharamia fedha za matibabu na malazi na alitoa ahadi ya kumsaidia Albaity wakati wa mchakato wa upimaji afya bure kwenye meli ya Jeshi la China mwishoni mwa mwaka jana baada ya kugundulika kijana huyo anahitaji matibabu maalumu ambayo yanapatikana katika nchi ya China tu.

Hali hiyo ilimfanya Makonda kutokwa na machozi na kuahidi kumpeleka China akatibiwe kwa gharama yoyote ili maumivu na mateso anayoyapata yafike mwisho.Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu dola za Marekani 26,000 sawa na Sh.milioni 52.

Akizungumza leo baada ya kukabidhi tiketi hizo,Makonda amesema Albaity atasafiri nchini China siku ya Jumapili akiongozana na watu wengine watatu wa kumsaidia ambapo gharama zake ni zaidi ya Sh.milioni 100.Makonda amesema shauku yake ni kugusa maisha ya kila mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema ahsante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu na kuongeza "Ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu.
"Na katika hilo watu wote watakuwa sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao na tunachokifanya ni sehemu ya utumishi wetu.Niwashukuru wote waliochangia kwa ajili ya kusaidia kufanikisha matibabu haya,"amesema Makonda.

Ametoa mwito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Albaity ili apone na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.Kwa upande wa Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu. 

"Wakati naomba watu wanichangie wapo watu waliokuwa wananivunja moyo kwa kuniambia siwezi kupona lakini Makonda ameonesha moyo wa kipekee,"amesema.

JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO .

0
0
Na John Nditi, Morogoro
WANANCHI wa mitaa ya Kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro  wameondokana na adha ya kutopata uhakika maji safi na salama baada kujengwa kituo cha kuchota maji ya bomba kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Waislamu Waahamadiyya  chini ya mradi wake wa Taasisi ya International Association of Ahmadi Architects and Engineers (I.A.A.A.E).

Mkuu wa Chuo cha Ahmadiyya Muslim Jama’at Tanzania, Sheikh Abid Mahmood Bhatti alisema hayo  kabla ya kukaribishwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe , kuzindua mradi wa maji  uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’  katika kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro na jirani zake .

Alisema , Jumuiya hiyo pamoja na kuwa ni taasisi ya kidini , inayo mipango mbalimbali ya kutoa huduma za kijamii zikiwemo katika sekta ya afya, elimu , umeme wa soka na maji.

“ Mradi huu  ulianzishwa mwaka jana baada ya kupitishwa na Hadharat Khalifa tul Masih  kiongozi mkuu wa Jumuiya  ya waislamu waahmadiyya duniani kupitia taasisi ya IAAAE” alisema Bhatti.

Mkuu wa Chuo alisema , jamii ya Kihonda Maghorofani  iliyopo karibu na taasisi hiyo wanaweza kuchota maji lita zisizopungua 10,000 kwa siku kwa ajili ya matumizi ya nyumbani .
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kulia ) akifungua koki ya maji wa ajili ya kujaza ndoo  mara baada ya kuzindua  mradi wa maji  uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro  ambayo yanawanufaisha  wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro .
 Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania , Tahir Mahmood Chaudhary Sahib ( kulia) akimtwisha  ndoo ya maji  mkazi wa Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro,   Winifrida Laizer , mara baada ya  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani)  kuzindua mradi wa maji  uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni katika kituo cha Jumuiya hiyo  eneo la Kihonda Maghorofani .
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kulia )akikata utepe kuashiria  kuzindua  mradi wa maji  uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro  ambayo yanawanufaisha  wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro  na ( wa kwanza kulia ) ni  Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania , Tahir Mahmood Chaudhary Sahib.
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wapili kulia ) akioneshwa kisima cha maji  na  mkuu wa Chuo cha Ahmadiyya Morogoro , Sheikh Abid Mohmood Bhatti ( kushoto) kabla ya  kuzindua  mradi wa maji  uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro  ambayo yanawanufaisha  wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro.
 Baadhi ya wakazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani ,  Manispaa ya Morogoro  wakichota maji safi na salama ya  bomba  mara baada ya  Mkuu wa mkoa , Dk Kebwe Stephen Kebwe , kuzindua  mradi wa maji  uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Internatioal Association of Ahmadi Architects and Engineers (I.A.A.A.E) Akram Ahmadi Sahib ( kulia) akiwa ameongozana na mmoja wa viongozi wa Ahmadiyya Muslimu Missionaries Training Centre iliyopo kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro wakitoa kuangalia mtambo wa kusukuma maji kwa kutumia umeme wa jua. (Picha na John Nditi).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIA WA CHINA ALIPA MILIONI 110/- KUKWEPA KWENDA JELA MIAKA 20

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Raia wa China, Liu Xiu Feng kutumikia kifungu cha miaka 20 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 110 baada ya kukiri kosa la kukutwa na meno ya Simba mawili.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kueleza mshtakiwa huyo amekiri kosa.

Hakimu Shaidi amesema kutokana na mshtakiwa huyo kukiri kosa Mahakama inamuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani ama kulipa faini ya sh.milioni 110."Mahakama inakuhukimi kutumikia kifungo cha miaka 20 jela ama ulipe faini ya Sh.milioni 110," amesema Hakimu Shaidi.

Baada ya kutolewa hukumu hiyo, mshtakiwa Feng aliepuka kwenda jela baada ya kulipa faini hiyo ya Sh.milioni 110.

Raia huyo wa China alikuwa akikabiliwa na kosa la kukutwa na meno mawili ya Simba katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).Alikutwa na meno hayo Februari 7,mwaka 2018 ambapo yanathamani ya Sh.milioni 11, 029,900.

AZAM FC KESHO KUIKARIBISHA SINGIDA UNITED CHAMAZI

0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC kesho itawakaribisha Singida United ya mkoani Singida kwenye mchezo wa raundi ya pili ya michuano wa kuania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utachezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam saa moja usiku ambapo AzamFc watakuwa wenyeji wa Singinda United katika mchezo huo.

Akizungumza leo Dar es Salaam,Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema mchezo huo ni mgumu ukizingatia na kikosi cha Singida kipo vizuri ila watahakikisha watapambana ili kushinda mchezo huo. 

"Kikubwa sisi kwetu ni kupambana ukizingatia timu zote mbili zina upinzani wa hali ya juu na kila mmoja anataka kuibuka kidedea katika mchezo huo na ukizingatia Ligi inaelekea mwishoni"amesema Jaffary.

Amesema nyota wao wa kimataifa Daniel Amor ataukosa mtanange huo pamoja na Waziri Junior aliyefanyiwa upasuaji wa paja kwa sasa anayefanya mazoezi madogo madogo na kuongeza Nahodha wa kikosi hicho Himidi Mau yupo fiti na kesho atacheza mechi ya kesho dhidi ya Singida united. 

"Mchezaji wetu Himidi Mau alianza mazoezi na wenzake wiki yote hii na anaendelea vizuri, kurejea kwa kiungo huyo katika kikosi kutaleta morali katika timu na imezidi kuongeza nguvu na tutapambana katika Uwanja wetu wa Nyumbani katika kuhakikisha tunapata pointi 3,"amesema Jaffary.

UHABA MADARASA WASABABISHA WANAFUNZI 346 KIDATO CHA KWANZA KUSHINDWA KURIPOTI SHULE WILAYANI KAKONKO

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

JUMLA ya wanafunzi 346 wa kidato cha kwanza wilayani Kakonko mkoani Kigoma,wameshindwa kuripoti shuleni kutokana na shule walizopangiwa kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Hali iliyo walazimu viongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na wananchi kujenga vyumba viwili kwa kila shule.

Akitoa takwimu hizo jana katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko ya kutembelea ujenzi wa vyumba hivyo, Ofisa elimu sekondari wilayani humo Clouds Nzabayanga amesema miongoni mwa wanafunzi 1714 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza walishindwa kuripoti ni 346.

Amefafanua wanafunzi hao waliopangiwa katika shule ya Kanyonza, Muhange na Gwanumpu.Amesema katika shule ya Kanyonza kuna wanafunzi 78, Muhange 97 na Gwanumpu 171 ambao bado hawajapewa barua zao za kujiunga shuleni hapo hadi hapo shule hizo zitakapo kamilisha ujenzi wa madarasa hayo.

Ameongeza kila shule inatakiwa kujenga madarasa mawili kwa nguvu za wananchi na Serikali kuchangia mabati pamoja na ukarabati wa vyumba hivyo.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,amewapongeza Watendaji wa kijiji pamoja na Wenyeviti wa kijiji kwa juhudi kubwa walizozionesha za kuwashawishi wananchi kujitoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Amesema wameonesha namna ambavyo wanataka iliwanafunzi waanze kupata elimu kama wengine, na kumuagiza mkurugenzi kutoa fedha za mabati na ukarabati ili wanafunzi wapewe barua zao na waanze kuripoti shuleni.
Mkuu huyo alisema Serikali inatamani kuona kila mtoto anapata elimu lakini lazima wazazi wajitoe kutatua changamoto zinazo jitokeza kwakuwa Serikali haiwezi kufanya kila kitu na kutatua changamoto zingine na kuwaagiza Wenyeviti kupita kuchangisha fedha na michango mingine kwa wananchi ili watoto wao wapate elimu.

Ameahidi kuchangia bati 30 katika shule ya Kanyonza na bati 20 kwa shule ya Gwanumpu ambazo zimekwisha kamilisha ujenzi wa vyumba hivyo kwa kiasi na kuwataka walimu na wenyeviti kushirikiana kukamilisha madarasa mawili katika shule ya Muhange.


STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU

0
0

Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii.

STAND United yapunguza spidi ya Simba!Ndio kauli ambayo unaweza kuitumia baada ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba kushindwa kufurukuta mbele ya wapiga debe wa Shinyanga Stand United kwa kukubali sare ya goli 3-3 katika mchezo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliopigwa ndani ya dimba la Uwanja wa Taifa ulichukua dakika 6 timu ya Simba kuandika goli la kuongoza kupitia kwa beki wake Asante Kwasi aliyemalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Stand United.

Dakika ya 23, Laudit Mavugo anashindilia msumari wa pili na kufanya usomeke 2-0 ila matokeo hayo hayakudumu ambapo katika dakika ya 36 mchezaji wa Stand United Tariq anamalizia krosi kwa kichwa na kumimina mpira wavuni na matokeo kuwa 2-1.

Baada ya dakika 5 ikiwa ni dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza Stand United walisawazisha kupitia kwa Lulambo na matokei kuwa 2-2 mpaka mapumziko.Kipindi cha pili,kilianza kwa kasi na kila timu kusoma mchezo wa mwenzake ambapo Simba walitangulia kupata goli la 3 dakika ya 61 kupitia kwa Nicolaus Gyan.

Hata hivyo kasi ya wachezaji wa Stand United na dakika 6 baadaye mchezaji wa Stand United raia wa Burundi Bigiriama aliisawazishia timu yake na matokeo kuwa 3-3 mpaka kipyenga cha mwisho.Baada ya matokeo hayo Simba anaendelea kukaa kileleni kwa alama 46 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 40 wakiwa wamecheza michezo 19.

Matokeo ya Simba na Stand United yameonekana kuwafurahisha zaidi mashabiki na wapenzi wa Yanga kwani alama za Simba kukaa kileleni zimezidi kupungua.

ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20

0
0
Na Karama Kenyunko,Blogu ya jamii

ALIYEKUWA mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ),Ex MT 66807 na wenzake watatu wamehukumiwa kwenda jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno ya Tembo yenye thamani ya Sh.198.

Hukumu hiyo imesomwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi  Kasonde.Watuhumiwa wengine waliohukumiwa kifungo hicho ni Bakari na Shafii Muhibu Muhibu.

 Hata hivyo, Mahakama imemuachia huru Asha Hassan Ulaya, aliyekuwa akishtakiwa na wenzake hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka bila ya kuacha shaka yoyote kuwa naye alihusika kwenye tukio hilo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kasonde amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake nane wameweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao watatu pasipo kuacha shaka yoyote kuwa wametenda kosa.

"Mahakama inawahukumu washtakiwa wote watatu kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja kwenye shtaka la kwanza na vilevile shtaka la pili miaka 20,"amesema Hakimu Kasonde.Pia Mahakama imeamuru meno ya Tembo yarudishwe kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori na gari aina ya Suzuki waliyokamatwa washtakiwa waliyotumia kubebea meno hayo itaifishwe na Serikali.

Katika hati ya mashtaka, inadaiwa, Juni 2, mwaka 2016 huko Mbagala Kibondemaji wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote walikamatwa na vipande 10 vya meno ya Tembo.Pia washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kukubali kisafirisha meno hayo ya Tembo yenye thamani ya Sh. milioni 198,mali ya Serikaliya Tanzania.

Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na nyara hizo za Serikali bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wanyama pori.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images