Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV GOSSIP: SHILOLE APONZWA NA MILIONI 3, ROMA MIEZI 6 BENCHI..


CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
TASNIA ya Habari ni sekta muhimu inayoziwezesha Serikali mbali mbali Duniani kuimarisha dhana ya Demokrasia kupitia matangazo na taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Chama tawala, miongozo na mipango ya maendeleo ili wananchi wajue uwajibikaji wa serikali yao na kupima uhalisia wa sera zinazotekelezwa kama zinakidhi mahitaji yao.
Maelezo hayo yametolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi. Catherine Peter Nao katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo Zanzibar, aliwaagiza viongozi na watendaji wa Chama na Serikali kupanga utaratibu wa   kuzungumza na vyombo vya Habari mara kwa mara  ili waweze kuwaeleza wananchi utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika taasisi zao.
Catherine alisema kiongozi yeyote mwenye dhamana ya kutoa taarifa za Chama ama Serikali atakayekataa kuzungumza na vyombo vya habari atakuwa anaenda kinyume na falsafa ya CCM mpya na Tanzania mpya inayotaka Chama kirudi mikononi mwa wananchi kwa kuanza na hatua ya kuwapatia taarifa sahihi zinazohusu masuala ya maendeleo.
Alisema kiongozi anayetekeleza wajibu wake vizuri hawezi kuwa na hofu ya kuzungumza na vyombo vya habari, hivyo ni lazima watumishi hao wa umma kukubali mabadiliko ya zama mpya za utandawazi zinazotoa fursa ya wananchi kuhoji na kudadisi viongozi waliowapa dhamana nini wamefakanya katika maeneo yao.
“Serikali ya Mapiunduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein imefanya mambo mengi mazuri lakini cha kusikitisha wananchi wengi hawajui serikali yao nini inafanya kutokana na baadhi ya Viongozi wenye dhamana ya kuzungumza wapo kimya”, alisema Catherine.
 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao akizungumza mara baada ya kuwasili katika studio za Chuchu FM iliyopo Mlandege Zanzibar.
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao akizungumza mara baada ya kuwasili katika studio za Swahiba Fm iliyopo Mbweni  Zanzibar.
 Mhariri wa Zanzibar leo Juma Khamis (aliyesimama akizungumza mwenye shati la mistari) akiwatambulisha wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar waliokuwepo katika Chumba cha Habari baada ya kutembelewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao.
 Mkurugenzi wa Swahiba Fm, Maalim Kassim Mohamed Kassim(kulia) akizungumza na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao mara baada ya kuwasili katika Kituo cha radio hiyo kwa ajili ya kujitambulisha.
MKUU wa Waandishi wa habari Zanzibar leo Ndugu Mwantanga Ame (kulia) awakionyeshwa machapisho mbali mbali ya Gazeti la Zanzibar leo Toleo la No.5804 la Machi 1, 2018 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao (kushoto) na Katibu msaidizi wa Idara hiyo Daud Ismail Juma(wa pili kushoto).

INTRODUCING NEW SINGLE "KILANGA" BY STANREX

SIMBA NA STAND KUCHEZA UWANJA WA TAIFA KESHO, DROO KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUFANYIKA KESHO

$
0
0
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa 19 inaendelea kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya Shinyanga Mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa. Mwamuzi wa katikati Florentina Zabron kutokea Dodoma ,Mwamuzi msaidizi namba moja Ferdinand Chacha wa Mwanza,mwamuzi msaidizi namba mbili Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza,mwamuzi wa akiba Gelmina Simon wa Dar es Salaam na kamishna wa mechi anatoka Arusha,Peter Temu.
Wakati huo huo, droo ya Kombe la Shirikisho la Azam inafanyika kesho Ijumaa Machi 2, 2018 saa 5 asubuhi Makao Makuu ya Azam Tv wadhamini wa mashindano hayo. Droo hiyo itahusisha timu nane(8) zilizofanikiwa kufuzu hatua hiyo ya Nane bora. Timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Young Africans na Azam FC za Dar es Salaam,Singida United ya Singida,Njombe Mji ya Njombe,Mtibwa Sugar ya Morogoro,Tanzania Prisons ya Mbeya,Stand United ya Shinyanga na JKT Tanzania ya Dar es Salaam.

HALMASHAURI UBUNGO,YAPITISHA BAJETI YA BILLIONI 98.2/- MWAKA 2018/2019

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam limepitisha makadirio ya mapato kwa mwaka 2018/2019

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa Mwaka 2018/2019 imekadiria kutumia fedha Sh. 98,238,193,600 ambapo katika fedha hizo Sh. 76,607,163,700 ni matumizi ya kawaida na mishahara ambayo sawa na asilimia 78 ya Bajeti yote .Wakati Sh 21,631,029,900 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo sawa na asilimia 22 ya bajeti yote.

Akizungumzia makadirio hayo Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob amesena wamekidhi kigezo cha kutenga asilimia 60 ya fedha za mapato ya ndani katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ambayo ni Sh.12,600,760,400.00 na Sh. 8,498,717,600 sawa na asilimia 40 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na nishahara.

Akifafanu zaidi wakati anasoma bajeti hiyo Jacob amesoma vipaumbele 17 vya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019.Ametaja vipaumbele hivyo ni ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Sh bilioni 3, uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji mapato ya ndani,kukusanya Sh.bilioni 25.7

Pia miradi ya maendeleo imetengewa fedha kiasi cha Sh.billioni 21.6 wakati kipaumbele cha nne kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kununua dawa na vifaa tiba Sh.bilioni 8.2.Jacob ametaja kipaumbele cha tano ni kupandisha maslahi ya wajumbe Serikali za Mitaa kutoka sh. 5000 kwa mwezi mpaka sh 20,000 kwa mwezi.

SERIKALI KUTOA KIBANO KWA WATENDAJI WANAOHUJUMU FEDHA ZA SERIKALI.

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amefunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara ambapo amewaasa washiriki hao kutumia fedha za Serikali kwa kufuata sheria.

Mheshimiwa Ndalichako alisema Wizara ya Elimu itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais,TAMISEMI kwa kuwaadhibu wale wote wanaoenda kinyume na matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Elimu bila ya kuzingatia sheriaa na miongozo ya utekelezaji wake.

“Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya RAis TAMISEMI itawachukulia hatua Wale wote wataokula fedha za miradi na hawatopelekewa pesa za miradi mingine hadi wakamilishe miradi ambayo haijakamilika na kutoa mchanganua wa matumizi yake,”Amesema

Ndalichako alihamasisha uzingatiaji wa taratibu za fedha kwani Viongozi wa ngazi ya juu hususani Mawaziri wamekua wakijibu tuhuma za ubadhilifu wa fedha kwa wakaguzi wakati hawakuchukua fedha hizo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kikai kazi kilichofungwa jana cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.

MBUNGE LUCY MAYENGA AKUTANA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO MJINI SHINYANGA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga (CCM) amefanya ziara ya kukutana na akina mama wafanyabiashara ndogo ndogo zaidi ya 250 wanaofanya shughuli zao katika Soko Kuu, Mtaa wa Sukari na Nguzo Nane mjini Shinyanga kwa lengo la kusikiliza shida zao na kujadili namna ya kuboresha biashara zao.

Mhe. Mayenga amefanya ziara hiyo leo Alhamis Machi 1,2018 akiwa ameambatana na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga,Octavina Kiwone, Afisa Biashara wa Manispaa hiyo,Sunday Deogratius, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shumbuu Katambi na madiwani wa viti maalum Zuhura Waziri na Mariam Nyangaka.

Alisema lengo la kukutana na akina mama hao ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji na mazingira yasiyo rafiki ni kutoa elimu na kubadilishana mawazo kuhusu ya namna ya kuondoka katika hali waliyonayo ili wapige hatua kimaendeleo.

“Nimeanzisha utaratibu huu wa kukutana na akina mama bila kujali itikadi za vyama vya siasa,dini wala rangi kwani maendeleo hayaangalii mambo haya, wanawake wana nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii hivyo lazima tushirikiane na tujumuike pamoja kumaliza changamoto zinazowakabili ili tujikwamue kiuchumi”,alieleza.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga (CCM) akizungumza na akina mama wanaofanya biashara zao katika Soko Kuu Mjini Shinyanga waliokutana naye katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Machi 1,2018 kwa ajili ya kutoa elimu na kubadilishana nao mawazo namna ya kuboresha biashara wanazofanya - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga akizungumza na akina mama zaidi ya 100 wanaofanya biashara zao katika Soko Kuu mjini Shinyanga.
Mfanyabiashara katika Soko Kuu Mjini Shinyanga,Winfrida Rwehumbiza akimshukuru Mbunge Lucy Mayenga kwa kuwafikia akina mama wafanyabiashara wenye mitaji midogo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga akizungumza na wafanyabiashara katika Mtaa wa Sukari mjini Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga,Octavina Kiwone akitoa elimu ya vikundi kwa wafanyabiashara wa mbogamboga katika mtaa wa Sukari mjini Shinyanga

Mahakama Kinondoni yamuhumuku msanii Shilole kulipa milioni 14 ndani ya wiki moja

$
0
0
MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya utapeli kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo.

Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imethibitika kuwa Shilole alipatiwa kiasi cha fedha Tsh. Milioni tatu kutoka kwa muandaaji wa tamasha hilo Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mton-Kijichi jijini Dar es Salaam.

Mbele ya mahakama imethibitisha kuwa Shilole alipokea fedha hizo lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana.

Kutokana na kitendo hicho, mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo hivyo kumsababishia mwandaaji hasara ya Milioni 14 ambazo mahaakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji.

Baada ya tukio hilo, Mary alifungua kesi mahakamani hapo akiomba kulipwa kiasi hicho cha fedha kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na Shilole kushindwa kufika lakini msanii huyo anadaiwa kupuuza wito wa mahakama.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P. Mshingwa amesema Shilole amekuwa akitumiwa wito mara kwa mara na mahakama afike kusikiliza kesi yake lakini amekuwa akikaidi kufanya hivyo hadi mahakama ilipomuandikia wito mwingine kwenye Gazeti la Uhuru lakini hakufika pia.

Shilole aliambatana mahakamani hapo na mumewe, Uchebe, na wakili wake ambapo mahakama imemuamuru azilipe pesa hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa.

WANANCHI MADABA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUWALETEA FEDHA ZA MRADI UJENZI KITUO CHA AFYA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Christina Mndeme akifuatilia maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Mtiangimbole kilichopo katika Halmashauri ya Madaba ambapo jumla ya sh. Milioni 500 zimetolewa na Serikali ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya. Wananchi wamemshukuru Mhe Rais kwa kuwaletea fedha za mradi huo .RC amewataka viongozi na mafundi kuweka uzalando na kujiepusha na ufanganyifu na amewataka watalaamu kukamilisha mradi huo kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu kwa matokeo chanya.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 01.03.2018

MAGAZETI YA IJUMAA LEO MARCH 2,2018

MBUNGE MGIMWA ATOA VIFAA VYA UJENZI JIMBONI MWAKE

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJLIWA AWEKA JIWE LA MSINGI ZAHANATI MBECHA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkewe Mary Majaliwa, wakiwasalimia watoto wa shule ya msingi Mbecha, katika kijiji cha Mbecha Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani humo kwa ziara ya kikazi jimboni, Machi 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Zahanati, iliyopo katika kijiji cha Mbecha Wilayani Ruangwa, iliyojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya African Relief Organization, wa kwanza kushoto ni Sheikh Abdallah Ndauga (wapili kushoto) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya African Relief Organization Sheikh Ibrahim Yusuf, na kulia ni mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, Machi 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya African Relief Organization Sheikh Ibrahim Yusuf, iliyojenga Zahanatiiliyopo katika kijiji cha Mbecha Wilayani Ruangwa, Machi 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia mtoto Shafii Khamis, katika kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nanganga Wilayani Ruangwa, Machi 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nanganga Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi jimboni, Machi 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, katika kijiji cha Mchenganyumba Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara Februari 28, 2018, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAAGIZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI WA KIGENI KATIKA KISIWA CHA IZINGA MKOANI KAGERA

$
0
0

.........................................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA  kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe kufanya Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa nchi jirani wanaodaiwa kulima na kufiga ndani kisiwa cha Izinga kilichopo ndani ya Pori la Akiba la Kimisi mkoani Kagera.

Ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake wilayani Karagwe mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kupokea taarifa na malalamiko ya kukamatwa kwa mifugo ya Watanzania ndani ya kisiwa cha Mubali huku kukiwepo mazao yanayodaiwa kulimwa na wananchi wa Rwanda katika kisiwa kingine cha Izinga.

“Ndani ya siku saba hicho kisiwa cha Zinga msafishe kila kitu, Mkuu wa Wilaya msaidie mtengeneze kikosi kiende kule kitoe takataka zote zilizoko kule, inakua ngumu kuadministrate (kutawala) wengine wa kwetu tunawatoa alafu wa nchi nyingine wamekaa, unatawalaje?”. Aliuliza kwa mshangao Dk. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha mpaka wa Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. Kulia ni Mkuu wa Karagwe, Godfrey Mheluka na Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (kulia kwake).
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lut. Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Article 4

$
0
0
CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA, KILICHOPO USA-RIVER, ARUSHA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA 2018/2019 KAMA IFUATAVYO:


ASTASHAHADA (CERTIFICATE)

1.      Astashahada (Certificate) ya ICT (mwaka 1)

2.      Astashahada (Certificate) ya Usimamizi wa Biashara/ Business Administration (mwaka 1)

3.      Astashahada (Certificate) ya Uhasibu (Accounting) (mwaka 1)

4.      Astashahada (Certificate) ya Sheria/Certificate in Law (mwaka 1)



Sifa zinazohitajika:

·        Mwombaji awe na ufaulu wa kuanzia alama “D” katika masomo manne.

AU

·        Ufaulu wa kiwango cha ‘subsidiary’ kwa Kidato cha 6

KOZI ZA STASHAHADA (ORDINARY DIPLOMA)

5.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5 & 6) katika ICT (miaka 2)

6.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5& 6) Usimamizi wa Biashara/Business Administration (miaka 2)

7.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5 & 6) katika Uhasibu/Accounting (miaka 2)

8.      Stashahada ya Sheria /Diploma in Laws (mika 2)

Sifa zinazohitajika:

·        Mwombaji awe na Cheti cha NTA Level 4 kutoka chuo kinachotambulika na NACTE

AU

·        Ufaulu kwa kiwango cha “Principle” moja (1) na “Subsidiary” moja (1) kidato cha Sita (A-Level)



NB: Nakala za vyeti vya nje viambatane na Fomu ya uthibitisho wa tathmini toka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

 

Maombi yafanyike kupitia mtandao wa chuo“ONLINE APPLICATION”katika tovuti ya chuo, yaani: www.makumira.ac.tz



AU

Chuoni, Tumaini University Makumira, Ofisi ya Msajili.



Mwisho wa maombi kupokelewa ni tarehe 30/03/2018.



Msajili,

Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira,

S. L. P. 55, Usa River, Arusha

Simu:  027 254 1034

Simu za Mkononi: 0753 293986 au 0753 008084


TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

TUME ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS), inatarajia kuanza kampeni za kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kujua afya zao kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.
Aidha imeeleza ,kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.

Pamoja na hayo ,kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS ,Leonard Maboko aliyaeleza hayo mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .

Alisema ,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .Maboko alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa vifo vinavyotokana na virusi hivyo .

Alielezea ,wanaandaa kampeni hizo kutokana na takwimu za utafiti wa viashiria vya ukimwi ya mwaka 2016/2017 inayoonyesha idadi ya watu wanaopima na wanaogundulika kuambukizwa wanaoanza kutumia dawa ni wanawake kuliko wanaume.
Mratibu wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi ,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa pichani .(picha na Mwamvua Mwinyi)

Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS ) ,Leonard Maboko akizungumza jambo ,mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .(picha na Mwamvua Mwinyi).


Ziara ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoani Njombe.

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipomtembelea ofisini kwake kupata taarifa ya Viwanda na uwekezaji katika mkoa huo, leo tarehe 1 Machi, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bibi. Ruth Blasio Msafiri walipofika ofisi za SIDO Mkoa wa Njombe kuona utendaji wake.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akikagua eneo litakalojengwa majengo makubwa kwa ajili ya wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo, Mkoani Njombe leo tarehe 1 Machi, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akimsikiliza meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Njombe kuhusu utaratibu wanaotumia katika kupima mizigo ya wakulima na wafanyabiashara mkoani Njombe.
Muonekano wa Kiwanda cha kuchakata Chai cha Unilever kilichopo mkoani Njombe ambacho kipo katika hatua za mwisho kukamilika kwa ujenzi wake.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akikagua uenzi wa kiwanda cha Chai cha Unilever, Mkoani Njombe leo tarehe 1 Machi, 2018.
Wadau na wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe waliokusanyika kumsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Hayupo pichani) na baadae kuuliza maswali kutokana na changamoto wanazokutana nazo na kupatiwa majibu.

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YAZIDI KUNOGA,WAIMBAJI WAZIDI KUMIMINIKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza mapema jana mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar kuhusiana na  maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018  litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
 
Msama ameanza kuwatangaza baadhi ya waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo ambalo limekuwa likiwavutia waimbaji wengi kila linapoanza kuandaliwa na hatimaye kukamilika,Msama amemtaja mwimbaji mahiri jukwaani Boniface Mwaiteje,Christina Shusho,Rose Muhando ambaye atazindua albamu yake mpya siku hiyo, na wengineo ambao wanaendelea kujiunga kuhakikisha tamasha hilo linafana. Pichani kulia ni mwimbaji Paul Clement pamoja na Beatrice Mwaipaja,ambao walitambulishwa rasmi hapo jana.
Beatrice Mwaipaja akifafanua zaidi namna ambayo ananendelea kujiandaa na maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa kushoto ni Mwimbaji mwenzake Paul Clement.
 Mwimbaji Paul Clement akizungumza kuhusu maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa, kulia ni Mwimbaji mwenzake Beatrice Mwaipaja .

SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 11.4 KUBORESHA WAKALA WA NDEGE ZAKE

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuboresha Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Ndege za Serikali ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali ambapo alizungumza na Menejimenti na wafanyakazi na kuwaeleza kuwa Serikali imejipanga kuboresha Wakala hiyo

Mhandisi Nditiye alisema kuwa azma ya Serikali ya Awamo ya Tano inayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinafanya kazi zake kwa weledi na uadilifu ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi. 

“Serikali inatambua umuhimu wa Wakala hii na ina imani kubwa nanyi katika kuhakikisha kuwa mnafanya kazi zenu za kusafirisha viongozi kwa usalama na kwa uhakika ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na tayari ina nia ya kuboresha taasisi hii”, amesema Mhandisi Nditiye.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea na wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Anayemsikiliza ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bwana Tito Kasambala
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bwana Richard Mayongela (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Wakala wa Ndege za Serikali
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali inayosafirisha viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali wakati wa ziara yake kwa Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Mhandisi Bernard Mayila akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akifanya ukaguzi ndani ya ndege mojawapo inayosafirisha viongozi wa ngazi za juu wa Serikali wakati wa ziara yake alipotembelea Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka baada ya kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali wakati wa ziara yake kwenye Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.


‘TUTAIFANYIA MABADILIKO MAKUBWA TUME YA UMWAGILIAJI’-AWESO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema wizara yake itaifanyia mabadiliko makubwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutokana na udhaifu mkubwa aliougundua kiutendaji, hali inayosababisha kutotimiza majukumu yake kwa ufanisi.

Naibu Waziri Aweso amesema kuwa tume hiyo kwa muda mrefu imekuwa haifanyi kazi yake vizuri na imembidi afike katika tume hiyo ili kufahamu undani wa tatizo hilo, kwa kuwa Serikali imeazimia kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula na kuunga juhudi za kuinua uchumi wa viwanda nchini.

‘‘Tuna zaidi ya hekta milioni 29.4 za ardhi kwa ajili ya kilimo, lakini hekta 468,000 sawa na asilimia 24 pekee ndio zimeendelezwa, hii manake bado tuko nyuma sana katika uzalishaji wa chakula pamoja na kuwa na eneo kubwa. Hili ni tatizo ambalo wizara italichukulia hatua za haraka’’, alisema Naibu Waziri.

Aliendelea kusema kuwa kuna haja ya kuipa nguvu sekta ya umwagiliaji kwa kuwa dhana ya uchumi wa viwanda inategemea sana kilimo cha umwagiliaji na sio kutegemea msimu wa mvua, ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakikidhi mahitaji ya taifa.

‘‘Sijaridhishwa kabisa na utendaji wa Tume ya Umwagiliaji na kuna tatizo katika menejimenti yenu na kusababisha utendaji mbovu, mabadiliko makubwa yanahitajika ili kuleta ufanisi wa tume hii ili tuanze kuona tija katika sekta ya umwagiliaji,’’ alisema Aweso.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji, Mhandisi Seth Luswema amesema kuwa amefarijika na ujio wa Naibu Waziri kwa kuwa hawajawahi kuwa na kikao ambacho wameweza kueleza changamoto zao, na kukiri kuwa kuna kasoro nyingi za kurekebisha kiutendaji ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao kilichofanyika katika ofisi za tume hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandis Seth Luswema akitoa ripoti ya kuhusu sekta ya umwagiliaji kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika kikao na watumishi wa tume hiyo.
Sehemu ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliohudhuria katika kikao na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images