Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO

0
0
Na Rhoda Ezekieli, Kigoma

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameikataa miradi minne ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni mbili iliyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2012.

Miradi hiyo inafadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na ikiwa chini ya uangalizi wa Wilaya ya Kibondo ambayo mpaka sasa bado haijakamilika.

Madiwani hao wameitaja miradi hiyo ni wa maji Nyagwijima, Kiduduye, Katanga na Muhange ambayo imetekelezwa kwa muda mrefu licha ya fedha zote zilishatolewa lakini haikamiliki na sasa wamechoka kupewa majibu ya kuahidiwa kila kukicha.
Wakizungumza jana katika kikao cha baraza hilo, madiwani hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipewa majibu ambayo hayaeleweki huku wakiahidiwa miradi hiyo itakamilika ndani ya mwezi mmoja baada ya kikao cha baraza la madiwani na mpaka sasa kimekuwa kitendawili kisicho na majibu.

Diwani wa Kata ya Gwarama Elia Kanjero amesema imekuwa kama desturi kupewa majibu mepesi katika suala hilo na hawataendelea kuona miradi hiyo ikionekana kuwepo katika maeneo yao bila faida yoyote kwa wananchi.

Alisema ni aibu miradi hiyo hata wafadhili wakija kuiangalia wanaweza kuacha kutoa fedha zao katika miradi mingine."Miradi hii inaonesha kutokuwa na tija kwa wananchi na haifai kabisa kutokana na fedha zilizotumika na ukizingatia fedha zote zimekwishalipwa lakini miradi ni mibovu," amesema.
Aidha Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ambaye kwenye baraza hilo alikaimu nafasi Mwenyekiti, Toy Butono amesema baraza linapendekeza Mhandisi wa Maji wilaya hiyo avuliwe madaraka yake.Pia achunguzwe kutokana na kushindwa kufuatilia miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa adhabu nyingine ili kukomesha uzembe kwa watumishi unaoweza kuigharimu halmashauri.

"Baraza tunaikataa miradi hii na tunaomba Mhandisi wa Maji anyang'anywe madaraka kwa kipindi hiki apewe mtu mwingine, yeye kazi hii imemshinda kila siku tunapokea malalamiko kutoka kwa wananchi." Kuhusu miradi hiyo kwa sasa hatuihitaji hadi itakapo kamilika na Mhandisi atuambie labda alishiriki kufanya miradi hiyo isikamilike kwanini ashindwe kufuatilia", amesema Butono.

Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago amesema suala hilo atalifikisha Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) ili hatua zichukuliwe kwa wanaokwamisha miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa wananchi.

"Wapo baadhi ya wananchi waliochangia nguvu zao bila kupewa haki zao mpaka sasa na kuwapongeza madiwani kwa uamuzi mgumu waliouchukua," amesema.Kwa upande wake Ofisa Utumishi wa halmashauri hiyo , Lusajo Ngabo ametoa ushauri kuhusu uamuzi uliochukuliwa na kuomba nhusika apewe siku 18 ili ajitetee kuhusu tuhuma zinazomkabili na baada ya hapo sasa ndio hatua nyingine zifuatwe.

MLIPUKO WA TRANSFOMA WASIMAMISHA KWA MUDA SHUGHULI ZA MAHAKAMA KISUTU

0
0

Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii
HALI ya taharuki imeibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutokea kwa mlipuko wa moto uliosababishwa na Transfoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa Mahakama hiyo, Gasto Kanyairita amesema moto huo umetokea saa nne asubuhi.
Amesema wakati mlipuko huo unatokea kulikuwa na kesi nyingi zikiendelea mahakamani.

"Baada ya kufuatilia tulibaini kuwa ni transformer ambapo ilisababisha kuungua kwa waya wa TTCL, simu na Internet ambapo shughuli za Mahakama zilisitishwa kwa muda," amesema.

Pia amesema shughuli za Mahakama zinaendelea ambapo data za kesi zipo salama.
"Niwatoe hofu Watanzania mlipuko uliotokea ni wa shoti ya umeme na ni kawaida kutokea, hivyo waepukane na taarifa za uongo,"amesema.


Mmoja wa mashuhuda tukio hilo, amebainisha kuwa walisikia kishindo kikubwa cha mlipuko ambapo iliwabidi wakimbizane kutoka nje ya Mahakama.

"Ilitubidi tutoke nje kutokana na hofu tuliyokuwa nayo, lakini tunashukuru hakuna madhara yoyote ya kibinadamu,".
 Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Gasto Kanyairita, akifafanua juu ya mlipuko uliotokea leo asubuhi na kusababisha taharuki kwa wananchi waliokuwepo mahakamani hapo.
Wananchi mbali mbali wakitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusikia mlipuko wa moto ndani ya mahakama uliosababishwa na Transformer.

 Gari la zimamoto likiwa limefika eneo la tukio

KAMATI YA BUNGE MASUALA YA UKIMWI,DAWA ZAKULEVYA YATEMBELEA WATU WANAOISHI NA VVU MBOZI

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Capt. Chiku Galawa (kulia) akizungumza na Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Mhe. Venance Mwamoto (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dkt. Jasmine Tisekwa Bunga (katikati) pale kamati hiyo ilipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya kutembelea konga ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Capt. Chiku Galawa (kulia) akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU (NACOPHA) pamoja na JSI, iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga (wa pili kushoto) kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya kutembelea konga ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.
 Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Mhe. Zaynab Vulu (kulia) akisalimiana na wana konga ya watu wanaoishi na VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe pale kamati hiyo ilipowatembelea katika ziara yake ya kikazi.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga (aliesimama)akizungumza na wana konga wanaoishi na VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe pale kamati hiyo ilipotembelea konga hiyo kwa ajili ya kuamasisha utumiaji wa dawa na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU). (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

ULEGA AWEKA JIWE LA MSINGI ZAHANATI KIJIJI CHA KIBAMBA JIMBONI MKURANGA

0
0
Na Emmanuel Masaka ,Globu ya Jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega ameweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kibamba iliyopo Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za wanachi kwa kushirikiana na Mbunge huyo itagharimu zaidi ya Sh. million 98,ambapo mpaka sasa zaidi ya Sh. million 43 zimeshatumika katika ujenzi huo.

Huku zaidi ya Sh.million 50 zikihitahika kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.Aidha katika kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika kwa wakati Ulega aliendesha harambee kijiji hapo ambapo zilipatikana Sh. 430800,mifuko ya saruji 35, mabati 19 na ahadi 150000.

Hata hivyo, Ulega alimpongeza Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Kibamba kwa kusimamia fedha za ujenzi wa jengo hilo kwa uaminifu."Huyu bwana ni muadilifu na mwaminifu wake ndio umefanikisha ujenzi wa jengo hili,hivyo natoa mwito kwa wanachi kuwa waaminifu pindi mnaposimamia miradi msitumie fedha kwa matumizi yenu," amesema.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega kwa kushirikiana na watendaji mbalimbali akiweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kibamba iliyopo Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga ,Abdalah Ulega aliendesha harambee kijiji hapo ambapo zilipatikana Sh. 430800,mifuko ya saruji 35, mabati 19 na ahadi 150000
Muonekano wa jego la Zahanati ya Kibamba iliyopo Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga ,Abdalah Ulega akikagua ujenzi wa shule ya msingi Chatembo iliyopo kata ya Mwandege.

Msanii Roma Mkatoliki afungiwa miezi sita kutofanya kazi za sanaa

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ibrahim Mussa a.k.a Roma Mkatoliki amefungiwa kwa kipindi cha miezi 6 baada ya kukaidi agizo la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) la kurekebisha wimbo wake wa Kibamia.

Roma aliitwa na BASATA baada ya agizo la Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  Juliana Shonza la kumuita na kumtaka abadilishe maudhui ya wimbo wake unaojulikana kwa jina la Kibamia aliomshirikisha msanii mwingine Stamina na Maua Sama.

Agizo la kufungiwa kwa msanii Roma Mkatoliki limetoka leo kutoka BASATA linalosema kumfungia kwa kipindi cha miezi 6 kutokujihusisha na masuala ya muziki.

Wimbo wa Roma ulitoka takribani miezi mitatu iliyopita na alipoitwa BASATA alikiri wimbo kuwa na lugha isiyo nzuri na akaahidi kubadilisha maudhui ya  wimbo huo ila muda umezidi kwenda bila kuufanyia marekebisho.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuufungia wimbo huo kutokupigwa katika vyombo vyote vya habari.

MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa mbunge wa Kawe jijini Dar as Salaam, Halima Mdee aliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo. 

Ofisa wa Polisi, D/SSGT Arbogast ameyaeleza hayo leo,wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya kutupilia mbali kielelezo cha maelezo ya onyo kilichotolewa na upande wa mashtaka.

Akisoma uamuzi uliotupilia mbali kielelezo, Hakimu Nongwa amesema ametupilia mbali kielelezo cha upande wa mashtaka kwa sababu maelezo ya onyo ya mshtakiwa yalichukuliwa nje ya muda.

Akitoa ushahidi wake Arbogast amedai yenye ndiye aliyemfanyia mahojiano Mdee ambaye alikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari,  July 3,mwaka  2017.Amedai mshtakiwa alimwambia ni kweli aliitisha mkutano na waandishi wa habari na lengo lake lilikuwa ni kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo. 

Shahidi huyo amedai Mdee katika kituoni  Oysterbay,  July 8, mwaka jana na wakati akimhoji alimsikilizisha CD iliyokuwa na matamshi ya lugha ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Machi 29,  ambapo upande wa mashtaka utaendelea kuleta mashahidi.

Mdee anakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli, ambapo alitenda kosa hilo Julai 3,mwaka 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema imtaa wa Ufipa Kinondoni.

WAZIRI UMMY AKUTANA NA UGENI KUTOKA UTURUKI

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amekutana na ugeni kutoka nchini Uturuki ukiongozwa na Balozi wao Dkt. Ali Daoutoglu mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.

Ugeni huo umejadili namna ya kuboresha Sekta ya Afya nchini hususani katika kuboresha huduma za dharura, uzalishaji wa dawa na ubadilishanaji uzoefu wa Wataalamu wa Afya kati ya nchi hizo mbili.

Balozi Ali Daoutoglu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tazania na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuimarisha Sekta ya Afya nchini.
 

MA-DED WATAKIWA KUSIMAMIA WATOTO YATIMA WAPATE ELIMU.

0
0
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakurugenzi Watendaji wote kuhakikisha watoto yatima ambao hawana ndugu maeneo wanawasidia kupata fursa  ya elimu na huduma nyingine zitakawasaidia kujiendeleza.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati wa mkutano wa wadau wa elimu uliokuwa ukijadiliana juu ya kuboresha elimu mkoani humo.

Alisema Wakurugenzi Watendaji wanapaswa kusimamia kama wazazi wa watoto yatima ili wawezeshe kupata elimu kama walivyo watoto wengine ili hatimaye waweze kushiriki katika ujenzi wa Taifa katika nafasi mbalimbali.

Mwanri alisema kuwa pamoja na majukumu mengine waliyonayo Wakurugenzi Watendaji wanapaswa kushirikiana na jamii katika kuhakikisha wanawasaidia watoto kufikia malengo yao ya kupata elimu kama njia ya kwanza ya kumsaidia.

“Wakurugenzi Watendaji ndio baba na mama wa watoto yatima ni lazima muwasimamie na kuwaendeleza  na njia pekee ya kuwasomesha watoto hao …miongoni mwao tutapata Madakitari , Wakuu Mikoa na viongozi mbalimbali” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Aliongeza kutowasaidia watoto hao unaweza kukuta unaacha kundi muhimu katika ujenzi wa Taifa.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema Tabora inatakiwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika elimu ili iweze kupata maendeleo ya kasi na kubadilisha maisha ya wananchi wake.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaomba viongozi mbalimbali wa dini na Wakuu wa Wilaya kusaidia kupambana na mimba za utotoni na zile zinazokatisha ndoto za baadhi ya wasichana kufikia malengo yao.Alisema ni vema viongozi hao wa kiroho wakatumia nafasi waliyonayo katika jamii kuelimisha jamii ili waachie watoto wa kike wasome.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua  jana mjini hapa kongamano la wadau wa maendeleo ya elimu mkoani humo. Lengo la kongamano hilo ilikuwa ni kujadiliano juu ya vikwazo vinakwamisha sekta hiyo kwa ajili ya kuvitafutia ufumbuzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi akitoa maoni yake jana kwenye kongamano la wadau wa maendeleo ya elimu mkoani humo. Lengo la kongamano hilo ilikuwa ni kujadiliano juu ya vikwazo vinakwamisha sekta hiyo kwa ajili ya kuvitafutia ufumbuzi. Picha na Tiganya Vincent

SERIKALI YAMUONYA NAY WA MITEGO

0
0
Na Zainabu Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza amemtaka Msanii Emmanueli Elibariki maarufu Ney Wamitego kuacha kutumia maneno yenye utata yanayolenga kuleta mmomonyoko wa maadili ya mtanzania anapoandaa nyimbo zake.

Shonza ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam ambapo japo Serikali inafahamu sanaa ni ajira, lakini ajira hii imekua ikitumika vibaya kwa kuharibu maadili ya mtanzania kulingana na maneno yanayotumika sambamba na kuwa na mavazi ya uchi katika picha jongevu hivyo kudhalilisha utu hasa kwa mwanawake.

Amesema Ney wa Mitego wamemuonya kutokana na nyimbo anazozitoa kutumia maneno yenye utata.

Pia wakati mwingine kuwa na picha jongevu zinazodhalilisha utu wa mtu na kwam a walikubaliana naye  atabadilika na kuzingatia maadili ya mtanzania kwa kazi zake za mbeleni.

Wakati huohuo Shonza ameigiza BASATA kuanzia sasa inapotokea kuwa wimbo unatolewa na msanii yeyote na unakiua maadili ya mtanzania wimbo huo uchukuliwe hatua kwa haraka.

 Wakati huohuo Ofisa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) Rolf Kibaja amesema rai kwa vituo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia kanuni za utangazaji.

Amefafanu vituo hivyo vinapopewa leseni hupewa na sheria na kanuni za uendeshaji wa vituo hivyo.

"Hivo tunawataka waandaaji na wasimamizi wa vipindi kuzingatia kanuni hizo kwani Mamlaka ya mawasiliano imejipanga kuhakikisha kuwa nyimbo zote zitakazokua zinaenda kinyume na maadili zitachukulia hatua kwa mujibu wa sheria kanunu na taratibu zilizopo," amesema Shonza.

Akizungumza baada ya kauli ya Shonza Ney Wamitego ameishukuru wizara hiyo kumweka sawa na kumpa nafasi nyingine ya kujirekebisha katika kazi zake za sanaa.

Ney wa Mitego ameahidi kufanya mambo mazuri yatakayokuwa tofauti na aliyowahi kufanya awali.

Amesema lengo la wizara ni kuona anafanya kazi ambazo zipo kwenye ubora unaokubalika na kwamba atatumia kipaji chake kwenye muziki huo kuwa na kazi ambazo zitazingatia sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa.
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na msanii  wa muziki Ney Wamitengo kuhusu namna ya kuboresha na kufuata maadili ya mtanzania katika kazi ya sanaa anayoifanya leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza
 Msanii wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki (Ney Wamitego) (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo naye kuhusu namna ya kuboresha na kufuata maadili ya mtanzania katika kazi ya sanaa anayoifanya leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu -WHUSM

JWTZ KUWAAGA MAJENERALI WASTAAFU KESHO

Waliomaliza Shule ya Msingi Bunge 1997 watoa msaada wa viti 20 kwa shule hiyo

0
0
Umoja wa Wanafunzi waliomaliza Shule ya Msingi Bunge mwaka 1997 iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam wametoa msaada wa viti 20 kwa shule hivyo ambayo vitatumiwa na walimu ambao wanafundisha katika shule hiyo. Akizungumza kuhusu msaada huo, Mwenyekiti wa umoja huo, Bernard Chezue alisema msaada huo ni sehemu ya shukani yao kwa shule hiyo kwa kuwapatia eleimu ambayo imewasaidia kimaisha mpaka sasa wakiwa na mafanikio. Alisema wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuisaidia shule hiyo ili iwe na mwonekano mzuri jambo ambalo litachochea wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997, Bernard Chezue akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi viti 20 kwa uongozi wa shule ya Bunge.
"Tumekabidhi vitu hivi sabau tunaona tuna umuhimu wa kusaidia kwa sababu tumsoma hapa na sisi tumekuwa na mafanikio kwa kupitia shule hii, tumekuja kutoa shukrani kwa waliu wetu na shule kw ujumla, "Huu ni mwanzo tu tutaumika nafasi yetu kutoa misaada zaidi na zaidi kwa namna Mungu anavyotujalia maana kuja kupata rangi, kubadilisha madarasa na hata baadae kuja kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri," alisema Chezue. Pia Chezue aliwataka watu wengine ambao walisoma katika shule hiyo kuungana kwa pamoja na kusaidia mahitaji mbalimbali ambayo yanahitajika shuleni hapo. 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997 kwa kutoa msaada wa viti 20 kwa shule hiyo.

RC MTAKA AWATAKA WANANCHI, VIONGOZI SIMIYU KUTOA USHIRIKIANO UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi na Viongozi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wataalam wa Takwimu katika utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi unaoendelea hapa nchini ili kuwezesha upatikanaji wa  takwimu halisi na sahihi Mkoani humo.

Mtaka ameyasema hayo katika Mkutano wake na   waandishi wa habari, wataalam wa Takwimu na Viongozi wa madhehebu ya dini uliofanyika Februari 28 Mjini Bariadi.

Amesema Utafiti huo utatoa makadirio ya uchumi jumla(macroeconomic), hususani matumizi ya kaya kwa ajili ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product-GDP), kupata mwenendo wa matumizi ya moja kwa moja ya kaya  ili kuwezesha uchambuzi wa hali ya soko na kupata taarifa za umilikaji wa vifaa vya kudumu pamoja na nyenzo za uzalishaji wa kipato.

Amesema kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2015 kila mwananchi anawajibika kushiriki katika utafiti kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu rasmi ambazo zitatumika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Bariadi.
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donatus Weginah akifafanua jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
 Meneja wa Takwimu, Mkoa wa Simiyu, Ndg.Nestory Mazinza akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUANZA KWA MVUA LEO

0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
KWA mara ya kwanza wamepatia!Ndivyo ambavyo kwa siku ya leo
baadhi ya wananchi hasa wa Jiji la Dar es Salaam wanavyodai baada
ya mvua kunyesha kama ambavyo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA )ilivyotabiri.
Kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakidhani TMA wamekuwa wakibahatisha kwenye tabiri zao hasa pale inapotokea walitabiri mvua kunyesha katika eneo fulani halafu mvua hainyeshi na kusababisha maswali.

Siku za hivi karibuni, TMA ilitoa taarifa kwa umma kuwa mwanzo mwa Machi mwaka huu mvua zitaanza kunyesha na kuomba wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka athari za mvua.
Hivyo kitendo cha mvua kunyesha leo jijini Dar es Salaam ambayo ni mwanzoni mwa Machi , wananchi ambao wamezungumza na Michuzi Blog wamedai ni kwa mara ya kwanza Mamalaka ya Hali Tanzania imetabiri kwa usahihi na kuwataka kuendelea kutoa tabiri ambazo zinaendena na ukweli ili kuendelea kuaminika.

Mshana John ambaye ni mkazi wa Kigamboni ametoa pongezi kwa TMA huku akidai alikuwa anasubiri ka hamu Machi ifike ili aone kama utabiri kuhusu mvua ulikuwa wenye ukweli lakini sasa ameamini na kusisitiza kwake ni mara ya kwanza kuona kilichotabiriwa kinakwenda na wakati.

"Niwe kweli nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa taarifa kuhusu hali ya hewa, ila kuna wakati wanatabiri kuwa mvua itanyesha lakini matokeo yake hakuna mvua na jua linabaki kuwa kali.Ila kwa mara ya kwanza wamepatia lazima tuwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanya.

"Huenda sasa watakuwa wamejiimarisha kwa kuwa na vifaa ambavyo vinakwenda na taarifa sahihi na ndio maana wametabiri uhalisia .Walisema mvua itanyesha mwanzoni mwa Machi na leo ndio mwanzo wenyewe na kweli imenyesha,"amesema John.

MAKONDA: WALIOZILALAMIKIA TAASISI ZA KIFEDHA WAJE OFISINI KWANGU KESHO

0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatangazia wananchi wote ambao wamewasilisha malalamiko kwenye ofisi yake dhidi ya taasisi za fedha na benki kufika ofisini kwake kesho kuanzia saa mbili asubuhi.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari ambayo ameitoa leo, Makonda amesema wananchi hao wafike kwa ajili ya kupatiwa majibu yao na kufafanua walengwa ni wale waliosikilizwa na jopo la wataalamu na wanasheria wakati wa wiki ya RC Makonda kutoa msaada wa kisheria kwa wanyonge iliyofanyika January 29 hadi February 03 mwaka huu.

.Mchakato wa kutoa majibu unaendelea ambapo leo ilikuwa ni zamu ya wananchi wenye malalamiko dhidi ya kazi na ajira pamoja na mirathi.

"Kilichofanyika leo na kitakachofanyika kesho ni mwendelezo wa kutoa majibu kwa wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekimbilia kwa Mkuu wa Mkoa ili kupata msaada wa kisheria,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.
RC Paul Makonda.

AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED

0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii

TIMU ya Azam FC imeendelea kujifua kikamilifu kwa lengo la kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Singida United, utakachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki hii.

Mchezo huo utachezwa saa moja usiku na utakuwa na msisimko wa aina yake hasa kwa kuzingatia timu zote mbili zinakaribiana kwa ponti kwenye msimamo wa ligi.Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 35 wakati Singida United ipo nafasi ya nne ikiwa na alama 34.

Wakati timu hizo zikiwa kwenye nafasi hizo, Simba ndio ipo kileleni kwa kuwa na pointi 45 wakati Yanga inashika nafasi ya pili.Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche na kiungo Frank Domayo wamesema kuwa wanauhakika wa ushindi kwenye mchezo huo.

Cheche amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wachezaji wote wako vizuri na wana morali ya mchezo."Tuko vizuri tunaangalia michezo iliyopita, matatizo tuliyokuwa nayo kwenye michezo iliyopita tunajaribu kuyasawazisha yasijirudie katika mchezo ujao."Halafu tunaiangalia Singida jinsi gani ilivyo ina uzuri gani ina udhaifu gani ili tutumie madhaifu yao na mazuri yao tuweze kuyadhibiti,"amesema Cheche na kuongeza 

"Tahadhari lazima tuingie nayo kwani hatutaki kufungwa .Tunataka kushinda."Kiungo Frank Domayo amesema watapambana na kufuata maelekezo ya mwalimu ili kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Singida United.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, bao la Azam FC ilikifungwa na Paul Peter huku Singida wakitangulia kutupia mchezaji wake Danny Sengimana.

TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Warace Karia amesema atasimamia suala la bima kwa wachezaji wanaoshhiriki katika Ligi Kuu pamoja na ligi mbalimbali zinazosimamiwa na shiriki hilo ili wachezaji wapate haki zao kwa haraka pindi wanapopata matatizo wakiwa michezoni kwenye maisha yao ya soka.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,wakati anafungua mafunzo kwa viongozi wa vilabu mbalimbali nchini kuhusu umuhimu wa bima yaliyoratibiwa na Taasisi ya ISDL kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Aliance life Insurance, Karia amesema atahakikisha anasimamia suala hilo ili litekelezeke.

"Lazima niwaambie ukweli kuhusu hili suala la bima, kwa sasa nafuatilia kwa ukaribu sana kwa kuhakikisha kila mchezaji aliyesajiliwa katika klabu ya Ligi Kuu na Shirikisho anapatiwa bima ya maisha ili kumsaidia kupunguza pindi yatakapojitokeza wakiwa uwanjani au baada kumaliza mpira wake,"amesema Karia.

Ameongeza kwa sasa lawama nyingi zinatumwa kwa TFF kuwa wameshindwa kuhudmia wachezaji wa zamani lakini kimsingi wa jambo lenyewe kuondokana na lawama hizo ni kuhakikisha wachezaji kila mmoja anapata bima ya maisha yake."Lengo ni kumsaida katika kujikwamua pindi anapopatwa na matatizo na hasa yanayohus maradhi,"amesisitiza.

Ametumia nafasi hiyo kutoa salamu za rambirambi kwa msiba wa mwanamichezo mkongwe aliyewahi kuichezea Klabu ya Simba Arthur Mambeta ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu..
 Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Semina kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Michuano ya Shirikisho nchini.
 Mwenyekiti wa ISDL , Dkt Katunzi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia  kuzindua Semina kwa ajili ya Vilabu mbalimbali hapa nchini.
Viongozi wa klabu mbalimbali nchini wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa TFF katika Semina Maalum iliyoandaliwa na ISDL kwa kushirikiana na Aliance Life Insuarance.

TCRA NA MAKAMPUNI YA SIMU WAZINDUA MFUMO MPYA WA USAJILI WA LAINI ZA SIMU UNAOTUMIA ALAMA ZA VIDOLE

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za mkononi  Tigo, Sylvia Balwire akisaini ubao wa uzinduzi wa mfumo usajili wa laini za simu unaotumia alama za vidole kuhakiki taarifa za wateja wa makampuni ya simu Tanzania(BIOMETRIC), anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Mawasiliano ,Dkt. Maria Sasabo leo kwenye viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa wizara ya Mawasiliano ,Dkt. Maria Sasabo (mwenye kilemba) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano TCRA, Mhandisi. James Kilaba na Wakuu mbalimbali wa makampuni ya simu Tanzania leo.


Mtaalam wa Kitengo cha Upatikanaji wa Wateja Wapya Tigo, Keneth Ndulute akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa mfumo usajili wa laini za simu unaotumia alama za vidole kuhakiki taarifa za wateja wa makampuni ya simu Tanzania(BIOMETRIC).

Mtaalam wa Kitengo cha Upatikanaji wa Wateja Wapya Tigo, Keneth Ndulute akielezea jambo kwa Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi. James Kilaba.



Meneja Mradi wa Biometric wa Tigo, Mohamed Sufian akiwa kwenye banda la Tigo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa laini za simu.


MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE ASHIRIKI UFUNGUZI WA OFISI YA KATA KIMANGE

0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ashiriki katika Ufunguzi wa Ofisi ya Kata ya Kimange na kuzungumza na Wananchi mafinikio yaliyofikiwa ktk kutatua migogoro ya Wakulima na Wafugaji, Elimu, Afya, Mazingira, Miundombinu ya Barabara, Changamoto ya Maji.

JAJI MKUU WA GAMBIA AMTEMBELEA MWANASHERIA MKUU WA TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, leo (Alhamisi) amekutana na kuwa na mazungumzo na  Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Gambia Mhe.   Hassan Bubacar Jallow.
Jaji Mkuu wa Gambia, yupo hapa  nchini kwa  ziara ya kikazi    ya kujifunza na kujipatia uzoefu kuhusu mfumo wa utoaji haki  hapa nchini pamoja na maboresho mbalimbali  yakiwamo ya maslahi ya  watumishi yanayoendelea katika   Mahakama ya Tanzania na Taasisi  nyingine za  Sheria na  utoaji  haki.
Jaji Mkuu  Jallow amemueleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dk. Adelardus Kilangi kwamba, Gambia, baada ya mabadiliko ya Serikali yaliyofanyika mwaka jana nchini humo, ipo katika mchakato wa kuifanyia  mabadiliko na maboresho   sekta ya sheria nchini humo.
"Nimekuja kwa ziara ya kikazi kwa madhumuni ya  kujifunza  kutoka Tanzania namna gani na sisi (Gambia) tutakavyoweza kuboresha na kuifanyia mageuzi makubwa  sekta  yetu ya Sheria na mfumo mzima wa  utoaji wa haki".
Akabainisha kwamba, anafahamu, namna gani  Mahakama ya Tanzania imeweza,  kwa kushirikiana na   Serikali na  Wadau wa  Maendeleleo  hususani Benki ya Dunia  kufanya  mageuzi  na maboresha makubwa  katika mfumo wa utoaji haki.
 Mwanasheria Mkuu  Dk. Adelardus Kilangi akisalimiana na  Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe  Wilbroad Slaa walipokutana nje ya Jengo   ambalo lina Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki . Mwanasheria Mkuu alikuwa akimsubiri kumpokea mgeni wake Jaji Mkuu wa Gambia Mhe.  Hassan Jallow ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimlaki Mgeni wake Jaji Mkuu wa Gambia  Mhe. Hassan Bubacar Jallow mara alipowasili kwa mazungumzo. Jaji Mkuu Jallow alisoma  sheria Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (1970-1973) na pia amewahi kuwa Mwendesha Mashtaka wa iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
( ICTR) (2003-2015).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dk. Adelardus Kilangi akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Gambia Mhe. Hassan Bubacar Jallow, leo Ofisi kwa Mwanasheria Mkuu. Jaji Mkuu yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi yenye madhumuni ya kujifunza uboreshaji wa sekta ya  sheria na utoaji haki hapa nchini. Baadhi ya mambo waliyobadilishana mawazo ni pamoja  na uwezeshwaji kwa wanasheria  wa Serikali na watumishi wengine katika  sekta ya  sheria  kimaslahi na kimafunzo.
Habari kamili BOFYA HAPA

KARIA ASEMA SUALA LA BIMA ALIKWEPEKI KWA WACHEZA SOKA WA TANZANIA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya jamii
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Warace Karia amesema atasimamia suala la bima kwa wachezaji wanaoshhiriki katika ligi mbalimbali zinazo simamiwa na shiriki hilo hili kuweza kuwawezesha wachezaji kupata haki zao kwa haraka pindi wanapopata matatizo wakiwa michezo katika maisha yao ya Soka.
Karia amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mafunzo kwa viongozi wa vilabu mbalimbali nchini juu ya umuhimu wa bima yaliyoratibiwa na Tasisi ya ISDL kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Aliance life Insurance ya hapa nchini Tanzania.
"lazima niwaambie ukweli hili suala la Bima mimi kwa sasa nitalifatilia kw aukaribu sana kwa kuhakikisha kuwa kila mchezaji aliyesajiliwa katika kalbu ya ligi kuu na shirikisho anapatiwa Bima ya maisha hili kuweza kupunguza matatizo yanayoweza kujitokeza pindi mchezaji wanapopata matatizo wakiwa uwanjani aua mara baada ya kumaliza mpira wake"amesema Karia.
amesema kuwa kwa sasa lawama nyingi zinatumwa kwa shirikisho la sokoa kuwa aliwahudumii wachezaji wa zamani lakini msingi wa jambo lenyewe kuondokana na lawama hizo ni kuhakikisha kuwa wachezaji hawa kila mmoja anapata Bima ya Maisha yake hili aweze kijikwamua pindi anapopata matatizo.
Karia pia alitumia fursa hiyo kutoa Salamu za rambirambi kwa msiba wa mwanamichezo mkongwe aliyekuwa anakipiga na klabu ya Simba Arthur Mambeta amefariki dunia siku ya jana Jumatano baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.
 Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Semina kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Michuano ya Shirikisho nchini.
 Mwenyekiti wa ISDL , Dr T.M Katunzi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia  kuzindua Semina kwa ajili ya Vilabu mbalimbali hapa nchini.

Viongozi wa klabu mbalimbali nchini wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa TFF katika Semina Maalum iliyoandaliwa na ISDL kwa kushirikiana na Aliance Life Insuarance.
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images