Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

WANANCHI RUHURU WAJICHANGISHA FEDHA KUJENGA ZAHANATI

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WANANCHI wa Kijiji cha Ruhuru wilayani Kakonko mkoani Kigoma wamejitolea kuanza ujenzi wa Zahanati itakayogharimu zaidi ya Sh.milioni 50 kwa lengo la kutatua changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hali inayosababisha wengi wao kupoteza maisha maisha wakiwa njiani.

Wakizungumza jana wananchi hao wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Hosea Ndagala aliyefika kukagua ujenzi wa Zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za wananchi, wameiomba Serikali kuchangia jitihada hizo walizoanzisha za kujenga msingi na kuinua ukuta ili kumaliza tatizo la ukosefu wa kituo cha afya na Zahanati.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ruhuru Bahati Kimpaye amesema kijiji hicho kina wakazi 2016 ambao wameanzisha ujenzi wa Zahanati hiyo baada ya kuona wanapata shida ya huduma ya afya hasa wajawazito.
Amesema usafiri mkubwa unaotumiwa na wananchi ni pikipiki ambapo kwa mama mjazito inakuwa ni changamoto huku akieleza wengine wanalazimika kutembea kwa miguu umbali wa saa tatu kufuata huduma katika vijiji vya Gwarama, Nyakayenzi na Nyanzige.

Amesema wapo baadhi ya wananchi ambao wamepoteza maisha wakiwa njiani wakifuata huduma za afya hali iliyokuwa ikiwaumiza wananchi na kuamua kuchangishana fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

Kwa upande wake Mkazi wa kijiji hicho Nesia Semagogwa amesema siku za nyuma kulikuwa na gari inafika kijiji hapo lakini sasa haipo na matokeo yake wananchi kuwa na wakati mgumu katika kupata huduma za afya.

Akizungumzia uamuzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewapongeza wananchi hao kwa kujitoa katika ujenzi huo na kuahidi yeye binafsi atatoa mifuko 20 ya saruji yeye binafsi na kuna fedha Sh.milioni 100 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya ambazo zitatolewa kwa ajili ya kijiji hicho ili wamaliziea zahanati yao kwa kununua vifaa mbalimbali.
Pia Kanali Ndagala amewaagiza wananchi na viongozi wa vijiji vingine kuiga juhudi hizo na Serikali inahitaji wananchi kuwa na umiliki wa miradi kwa kuonesha juhudi zao kwenye masuala ya maendeleo

SERIKALI YATOA BILIONI 1.92 KUBORESHA AFYA NANYAMBA

$
0
0

SERIKALI imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.

Hayo yalibainika jana (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza na wakazi wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara yake.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi alisema fedha hizo zilitolewa na Serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.Alisema jumla ya sh. bilioni 1.2 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kwenye Kata ya Njengwa, ambapo aliwasisitiza watendaji kutobadilisha matumizi.

Waziri Mkuu alisema ujenzi huo utahusisha chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha kuhifhadhia maiti.“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”

Aidha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka masharti ya kumlinda mtoto wa kike hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa alisema Serikali itawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuwapa watoto wa kike dawa za uzazi wa mpango ili kuwazuia wasipate mimba.Bw. Byakanwa alisema wanafunzi wa kike katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wamebainika kuwa wanatumia dawa za kuzuia mimba wakiwa shuleni, hivyo kuwaruhusu kushiriki katika matendo yasiyokuwa ya kimasomo.

Alisema Serikali itafanya msako wa kuwatafuta wote wanaotumia dawa hizo pamoja na wanaowapa na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa sababu jambo ni hatari kwa maendeleo ya wanafunzi hao.Naye, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Josephat Kakunda alisema alisema Serikali imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ili kuboresha huduma za afya.

Asema kati yake sh. milioni 700 zilipelekwa katika kituo cha afya cha Nanyamba ambapo sh. milioni 300 zilitumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa na sh milioni 400 ukarabati wa kituo, huku sh. bilioni 1.2 ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Njengwa.Haya hivyo, Waziri huyo alisema kuwa Serikali inampango wa kuifanyia marekebisho sheria ya mtoto kwa kuondoa kipengele cha dhamana kwa watu watakaotuhumiwa kuwapa mimba watoto wa shule.

Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya watuhumiwa hao wanapopewa dhamana kwenda kuzungumza na wazazi au walezi wa binti jambo linalochangia katika kuharibu ushahidi.” Ni bora wakakaa rumande hadi hukumu itakapotolewa na kama hawatokutwa na hatia watarudi uraiani”.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 01, 2018.

MEYA JIJI LA DAR AMJULIA HALI MWANASIASA MKONGWE CHADEMA,AMPELEKA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA MATIBABU

$
0
0

Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii

MEYA  wa Jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita ametemtembelea nyumbani kwakwe na kisha kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwasisi na mkongwe wa Chadema Victa Kimesela ambaye anaumwa kwa muda mrefu sasa.

Kimesela ni miongoni mwa waasisi walioshiriki kuandaa Katiba ya chama hicho mwaka 1992, anaugua kwa muda ambapo familia yake ilimueleza Meya Mwita kuwa alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hivyo kuruhusiwa Jumatano iliyopita.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Ofisi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam Christina Mwagala amesema muda fupi baada ya  Meya Mwita kufika nyumbani  kwa mwasisi huyo, afya yake ilibadilika.

Hivyo kwa kushirikiana na familia hiyo  walitoa taarifa Muhimbili ili kupatiwa gari ya kubebea wa gonjwa.Aidha  gari hiyo ilifika na kisha Mwita na familia hiyo waliambatana pamoja kumuwahisha kwa mara nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu awali.

 Mwagala amesema kuwa Kimesela amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chadema, ikiwepo kuwa Katibu mtendaji wa chama hicho wakati wa utawala wa mzee Edwin Mtei.

Pia amewahi kuwa Katibu mkuu wa muda wakati wa utawala wa Bob Makani(marehemu)na hivyo kumuachia nafasi hiyo Dk.Wilblod Slaa ambaye kwa sasa amestaafu siasa tangu  mwaka 2015.
 
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita akiwa pamoja na familia ya Kimesela ,wakitoa msaada wa kumpakiza kwenye gari ya kubebea wagonjwa ya hospital ya Taifa Muhimbili jana alipomtembelea nyumbani kwakwe.Kimesela anaumwa na kwa sasa amelazwa katika hospital ya Taifa Muhimbili.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na mke wa Kimesela , Suzani Kimesela alipomtembekea nyumbani kwake jana .

DK MWAJELWA AWAPONGEZA WAKULIMA WA CHAI NA PARACHICHI MKOA WA NJOMBE

$
0
0
 




NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na sehemu ya wakulima wa chai alipowasili kwenye kijiji cha Lwangu Wilaya ya njombe mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
Sehemu ya wakulima wa chai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipozungumza nao. 
Sehemu ya wakulima wa chai wakikusanya zao hilo baada ya kutoka kuvuna wakati Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara na kuzungumza nao. 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea na wakulima wa chai alipotembelea kijiji cha Lwangu Mkoa wa Njombe hivi karibuni. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MZEE JORAM MOLLEL MAARUFU KAMA "BABU" APATA NAMBA YAKE YA KUSHIRIKI TIGO KILI HALF MARATHON 2018

$
0
0
Mzee Joram Mollel maarufu BABU mwenye umri zaidi ya miaka 90 akijisajili kushiriki mbio za kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya Jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akimkabidhi Babu Molell  NAMBA ya ushiriki wa mbio za  kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Mtoa huduma wa Tigo, Mohammed Ally akiwasajili Aghata Philii na Poling Nikesa raia wa Zambia kushiriki mbio za Tigo Kili Half Marathon kwenye viwanja vya Kibo Palace Arusha juzi. Mbio zinatarajiwa kutimua vumbi jumapili ya wiki hii Moshi, Mkoani Kilimanjaro

SERIKALI YATOA BILIONI 1.92 KUBORESHA AFYA NANYAMBA

$
0
0
SERIKALI imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.

Hayo yalibainika jana (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza na wakazi wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara yake.Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi alisema fedha hizo zilitolewa na Serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Alisema jumla ya sh. bilioni 1.2 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kwenye Kata ya Njengwa, ambapo aliwasisitiza watendaji kutobadilisha matumizi.Waziri Mkuu alisema ujenzi huo utahusisha chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha kuhifhadhia maiti.

“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”Aidha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka masharti ya kumlinda mtoto wa kike hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa alisema Serikali itawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuwapa watoto wa kike dawa za uzazi wa mpango ili kuwazuia wasipate mimba.

WIZARA YA ARDHI YAWATULIZA WANANCHI ARUMERU ,YAWAAMBIA MGOGORO WAO UNASHUGHULIKIWA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akizungumza na wakazi wa kata ya Sing’isi alipokuenda kuwasikiliza kuhusu mgogoro wa ardhi dhidi ya muwekezaji
 Sehemu ya wananchi wa kata ya Sing’isi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Angelina Mabula.
 Diwani wa Seela-Sing’isi Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha Penzila Pallangyo akimueleza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula kuhusu mgogoro wa ardhi wa eneo la kata ya Sang’isi.
Maofisa kutoka Wizara ya Ardhi na Kanda ya Kaskazini wakifuatilia mkutano baina ya wananchi wa kata ya Sang’isi wilaya ya Arumeru na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.

KASI UHARIBIFU WA MISITU HANANG YAONGEZEKA

$
0
0

Na. Jumbe Ismailly
KUTOKANA na hali ya uharibifu wa misitu katika wilaya ya Hanang kuwa kubwa sana,Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara, Sara Msafiri ameziagiza kamati za maendeleo za kata kujenga utamaduni wa kujadili katika vikao vyao juu ya hali ya uhifadhi wa misitu katika maeneo yao.
Akitoa agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa wilaya huyo aliyataja baadhi ya maeneo ya vijiji vya Lalaji. Balangida na maeneo mengine hali ya mazingira ni mbaya sana.
“Kwa hiyo niwaombe kwamba kamati za maendeleo za kata mjadili na hali ya hifadhi ya misitu na ninazo taarifa za kutosha na nimejirisha wapo viongozi wengine  ni wa kisiasa wanashiriki katika biashara ya kukata miti, kuchoma na kuuza mkaa.”alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya kupitia serikali kuu wameshatoa maagizo kwa watendaji kwamba mtu yeyote tule atakayetaka kukata miti hata kama aliupanda mwenyewe ni lazima apate kibali kutoka kwa Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo Sara alisisitiza kwamba ni ukweli usiopingika na alioufanyia uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa,wakiwemo madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji wanajihusisha na biashara ya kukata micti kuchoma mkaa na kuuza mazao hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Hanang,Sara Msafiri akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
 Mbunge wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Dk.Mary Nagu (katikati) akipitia taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na kisha kutaka kufahami shilingi milioni 300 zilizoagizwa kwenye mkutano wa LAC Dodoma zitalipwa lini ili vikundi vya wanawake,vijana na walemavu viweze kunufaika na kujiongezea mitaji yao.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara, Teddy Athumani (wa kwanza kushoto) akipitia makabrasha ya mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang kujiridhisha namna watendaji wa Halmashauri wanavyotekeleza ilani ya chama tawala.
Katibu wa vikao vya Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Stevine Yonah(kushoto) akinukuu maazimio yote ya mkutano wa Baraza hilo ili watendaji waweze kutekeleza kikamilifu maazimio hayo. (Picha zote Na Jumbe Ismailly)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Na Zainabu Nyamka, Globu ya Jamii

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Simba, Arthur Mambeta amefariki dunia  jana Alhamisi  baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.

Mambeta aliyeanza kukipiga katika kikosi cha wanamsimbazi Simba SC mwaka 1960 ikiwa inaitwa   Sunderland akicheza nafasi kiungo mshambuliaji hodari kuanzia katika klabu yake hadi timu ya Taifa. 

Katika historia ya Arthur, aliyewahi kocha wa Tanzania miaka hiyo, Milan Celebic raia wa Yugoslavia alikaririwa akisema kuunda timu ya taifa bila ya Arthur Mambeta ni sawa na kula chakula bila ya chumvi au chai iliyokosa sukari.

 Arthur Mambeta ndiye mchezaji pekee wa Tanzania aliyekuwemo Katika kiķosi cha kwanza cha kombaini ya Afrika Mashariki iliyocheza na West Bromwich Albion ya England mwaka 1974 Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, Uganda.

Katika mechi hiyo ilijumuisha wachezaji wa timu ya mbalimbali kutoka  Afrika Mashariki akiwamo na mchezaji mwingine wa Tanzania aliyeteuliwa, Kitwana Manara alikuwa bechi kama kipa wa akiba kabla ya kuhamia kwenye ushambuliaji ambako pia alikuwa tishio hadi anastaafu soka.

Baada ya kustaafu soka, Mambeta alindelea kujihusisha na mchezo katika utawala na amewahi kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi Simba SC.

Hata hivyo, Mambeta alianza kujitoa taratibu kwenye soka baada ya kuanza kusumbuliwa na maradhi ya saratani yaliyosababisha akatwe miguu yake yote miwili. 

Taarifa zaidi kuhusu msiba huo na taratibu zake zinataolewa kutolewa na familia ya marehemu Alhamisi.

 Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Arthur Mambeta. Amin.

JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI

$
0
0
KAMPUNI  ya Jumia Tanzania  inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo.

Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.

“Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’  "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania.

" Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema.

Ameongeza ni  mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott.
 Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI  ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo ambayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess
Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.


KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE

$
0
0
SERIKALI ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro..

Mheshimiwa Mavunde ameyasema hayo jana (Machi 1, 2018), wakati akiendelea na ziara yake ya kushtukiza ili kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.

Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hatajisajili kwenye Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,000 (Milioni Hamsini) au kifungo kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.

Mheshimiwa Mavunde ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.
Naibu Waziri ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, (kulia) na Mhasibu wa Shule ya Scolastica, Bw.Moshi W.Moshi, wakati wa ziara yake ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi, (WCF) ambapo ilibainika shule hiyo kubwa mjini Moshi haijatekeleza takwa hilo la kisheria 
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika na Afsia Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bw. Sebere Fulgance.
Mhe. Mavunde akizungumza na Mkurugenzi wa Machare Investments, (kulia).

MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii

MSEMAJI wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema hivi karibuni wamezindua jezi zake za mashabiki.

Amesema uzinduzi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happyness Seneda.

"Baada ya uzinduzi huo, jezi za mashabiki wa Ruvu Shooting za nyumbani (Bluu) na za ugenini (Orange), kwa idadi jumla ya jezi 1,000 ziliingizwa sokoni, tayari kwa mauzo, kila jezi moja (ya juu) ikiuzwa kwa Sh.20,000.

"Mheshimiwa Seneda baada ya kuzindua jezi hizo, aliipiga mnada jezi moja iliyonunuliwa kwa fedha taslimu za Kitanzania Sh.100,000," amesema.
Masau amesema jezi zote 1,000 zilizokuwepo kwa ajili ya kuuzwa kwa mashabiki, siku iliyofuata baada ya uzinduzi zilinunuliwa zote kwa kugombaniwa.

Amesema idadi kubwa ya mashabiki waliohitaji kununua jezi hizo walikosa baada ya kununuliwa zote,hivyo ikalazimu uongozi kufanya mazungumzo na mdhamini, Kampuni ya HAWAII PRODUCTS SUPPLIES LTD kupitia maziwa ya Cowbell, moja ya bidhaa wanazozisambaza ili kuagiza jezi nyingine.

"Wadhamini walikubali, tayari wameanza mchakato wa kuagiza jezi 4,000 ulaya kwa ajili ya mashabiki wa Ruvu Shooting," amesema.Amefafanua hitaji la jezi hizo limekuwa kubwa kwani watu mbalimbali, vyama na baadhi ya timu za soka, rafiki wa Ruvu Shooting wamekuwa wakipiga simu kuomba kununua jezi hizo, mfano, chama cha soka Rufiji walitaka jezi 50 ambazo fedha za malipo yake zipo tayari.

"Niwaombe radhi mashabiki wetu kwa kukosa jezi, lakini niwatie moyo kwamba, Mei mwaka huu zitakuwa zimefika, zenye ubora wa hali ya juu sana," amesema.Ameongeza "Katika hali na mazingira hayo, kwa nini TUSIWAPAPASE? Mtapapaswa sana, tumejipanga, tuko vizuri, kwa zamu, kila mmoja ATAPAPASWA," amesema Masau.

WIZARA ZA UJENZI ZANZIBAR, TANZANIA BARA ZAFANYA MAZUNGUMZO ZANZIBAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe akisisitiza jambo katika Mkutano wa mashirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji(SMZ) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi (SMT) uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Zanzibar. Kushoto ni  Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(SMT), Dkt. Leornard Chamuriho.
 Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa mashirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji(SMZ) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi (SMT)uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Zanzibar.
 Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(SMT), Dkt, Leornard Chamuriho, akifafanua baadhi ya hoja zilizotolewa  katika Mkutano wa mashirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji(SMZ) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi (SMT)uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Zanzibar.
Katibu Mkuu Wzara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe na  Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(SMT), Dkt. Leornard Chamuriho wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa  Mkutano wa mashirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji(SMZ) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi(SMT) uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashanti Kijaji amesema kuwa mamlaka ya Masoko na Mitaji ni injini katika maendeleo ya uchumi hivyo ni lazima mamlaka hiyo iwafikie wateja.

Kijaji aliyasema hayo wakati akitunuku vyeti kwa wahitimu wa mamlaka hiyo waliopata kwa kushirikiana na chuo cha Uingereza CISI katika fani ya masoko na mitaji, amesema kuwa watu hawana uelewa juu ya masoko na mitaji hivyo wanatakiwa kufikia wateja katika kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano yenye Kauli mbiu ya nchi ya viwanda.

Amesema Mamlaka kwa kutumia watalaam hao lazima wafanye kazi katika kujenga nchi  na kutoa elimu  kuhusiana na masoko na mitaji.Amesema kuwa kampuni zipo nyingi lakini hazijaweza kuingia katika soko la hisa ni kutokana na kampuni hizo kushindwa kufikiwa ikiwa ni pamoja na kupata elimu.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika kufanya kazi mamlaka hiyo lazima iweke mpango mkakati katika kuhamasisha kampuni ziingie katika soko la hisa.Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Dk.John Mduma amesema kuwa wanaendelea katika kutoa huduma ikiwa ni pamoja kufanyia kazi maagizo ya Naibu Waziri katika kuwafikia wateja na kuleta matokeo chaya ya maendeleo ya uchumi.

Dk. Mduma amesema kuwa katika kuwa sasa watafungua dirisha la  uhamasishaji katika  kufikia kampuni ziweze kuingia katika soko la hisa.
Afisa Mtendaji Mkuu , Nicodemus Mkama amesema mkataba wa huduma kwa wateja waliouzindua watawafikia wateja wote kuingia dhamana ya masoko na mitaji katika kuendrleza miradi mbalimbali nchini.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizungumza mara baada ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko ya mitaji na uzinduzi wa Mkataba wa huduma kwa Wateja.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi w akitabu cha huduma kwa wateja.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizindua kitabu cha Msaada wa huduma kwa wateja
 Mwenyekiti wa TSEBA,George Fumbuka akitoa neno la Shukrani kwa waziri mara baada ya kumaliza kuzinduliwa kwa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa wateja.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko
 Baadhi ya Wadau walioshiriki katika uzinduzi wa kitabu cha huduma kwa wateja

KIPINDI MAALUM KUAMSHA ARI YA WANANCHI KUSHIRIKI SUGHULI ZA MAENDELEO WILAYA YA KISARAWE PWANI.


Vanessa Mdee aungana na mastaa maarufu duniani wanaomiliki majukwaa ya mtandaoni

$
0
0
Vee Money App katika kilele cha maendeleo ya mziki Afrika na dunia nzima
Vanessa Mdee anaungana na mastaa maarufu duniani ambao wanamiliki ‘majukwaa ya mtandaoni’ ya kuwasiliana na mashabiki wao

Je unafahamu kitu gani kinachowafananisha Taylor Swift, Ciara, na Vanessa Mdee? Naam, pamoja na kwamba wote ni wasanii wenye sauti nzuri na vipaji vikubwa, wote watatu wanamiliki majukwaa ‘app’ za kuwasiliana na mashabiki wao mtandaoni.

Hii ni njia mpya inayotumiwa na wasanii wakubwa ambao wana mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, ukweli ni kwamba pamoja na mitandao hiyo mikubwa ya kijamii kutengeneza mabilioni ya dola kila mwaka wasanii hawapati mapato ya moja kwa moja kutokana na biashara hiyo.

Sababu nyingine kubwa ambayo inawafanya wasanii kama Kim Kardashian kuwa na majukwaa yao mtandaoni ‘app’ ni kwa sababu hawamiliki mashabiki wao wa mtandaoni ila mitandao ya kijamii ndiyo ina haki juu ya watu wanaoitumia, hii inamaanisha msanii mkubwa akifungiwa akaunti yake ya Facebook au Instagram anaweza kukosa njia ya kuwasiliana na mashabiki wake (Rob Kardashian ni mfano halisi).

Pamoja na ukweli kwamba majukwaa‘app’ pia zinaruhusu wasanii maarufu kuuza bidhaa mbalimbali na tiketi kwenye simu za mkononi lakini cha muhimu zaidi, inasaidia wasanii kufaidika kutokana na makampuni makubwa kutangaza kupitia majukwaa yao.

WANNE WANASWA KWA TUHUMA MTANDAO WA UJANGILI NA MAUAJI YA FARU

RAIS SHEIN AWAAPISHA MAWAZIRI NA WAKUU WA WILAYA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe.Salama Aboud Twalib kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Waziri wa  Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya kale  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Waziri wa Afya.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.,Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe.Maudline Cyrus Castico kuwa Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe. Juma Makungu Juma kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, na Nishati  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Naibu Waziri wa  Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe. Choum Kombo Khamis kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Naibu Waziri wa   Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo.(Picha na Ikulu) 

Mkazi wa Lindi akabidhiwa Kirikuu yake aliyojishindia katika kampeni ya Malengo ya Benki ya NBC mjini Tanga leo

$
0
0
 Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi funguo ya gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa.
 Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi kadi ya gari ya gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa.
 Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi kibao cha namba za gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa.

REUBEN BULUGU NDIYE MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 10 KTK DROO YA “DAKA MKWANJA”

$
0
0


Bw. Muganyizi Bisheko Meneja wa Masoko Utafiti na Maendeleo Benki ya BOA akikabidhi zawadi ya shilingi milioni 10 kwa Bw. Reuben Bulugu Kinamhala mshindi wa Bahati nasibu ya “Daka Mkwanja” iliyoendeshwa na Benki hiyo kwa muda wa miezi minne kwa wateja wake kuweka fedha kwenye akaunti zao na kutunza kiwango kisichopungua shilingi milioni moja , Bw. Reuben Bulugu ambaye ni mtumishi katika kanisa ni mteja wa benki hiyo katika tawi la Mtoni Temeke jijini Dar es salaam.

Katika picha kulia ni Mke wake Jane Bulugu akishiriki kupokea kiasi hicho cha fedha na kutoka kulia wanaoshiriki kukabidhi fedha hizo kwa mshindi ni Linda Mario Mkuu wa uratibu wa Mauzo na Nimael Mdeme Meneja wa Matawi ya Benki ya Boa Kanda ya Dar es salaam na Zanzibar.
Bw. Muganyizi Bisheko Meneja wa Masoko Utafiti na Maendeleo Benki ya BOA akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake pamoja na washindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo.
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images