Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SPIKA MAKINDA AFUNGUA BARAZA LA KATIBA LA CHAMA CHA WABUNGE WANAWAKE TANZANIA (TWPG) BAGAMOYO LEO

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika meza kuu na viongozi wa TWPG pamoja na mtoa mada katika kikao cha Baraza hilo Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa
 Naibu Katibu Mkuu wa TWPG Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akiwakaribisha wajumbe
 Katibu Mkuu wa TWPG ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (MB) akielezea Muhtasari wa Baraza hilo, Malengo na Matokeo yanayotarajiwa kwa mgeni rasmi.

Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini azungumza na wana Diaspora wa Zanzibar leo

$
0
0
 Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,akizungumza na Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) ,walipokutana  leo katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mnazi Mmoja  Mjini Zanzibar

SIYO KILA MABADILIKO YANA FAIDA - NAPE NNAUYE

$
0
0
NAPE NNAUYE
MWANZA, Tanzania 

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye amesema japokuwa mabadiliko ni muhimu kwa maisha ya binadamu lakini lazima kila yanapohitajika yafanywe kwa umakini mkubwa ili yasiwe na madhara.

Amesema ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana CCM imekuwa ikisisitiza umakini na busara kubwa vitumike wakati huu ambao Tanzania ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya.

Nape amesema miongoni mwa mambo ambayo CCM inaona kwamba lazima yatazamwe kwa umakini na busara kubwa kabla ya hatua ya mwisho, ni kuhusu Tanzania kuwa na serikali ngapi, ambapo rasimu ya kwanza ya Katiba inapendekeza serikali tatu.

Nape ambaye alikuwa akizungumza wakati akifungua Kongamano la Vijana mkoani Mwanza lililofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu (BOT) Kapripoint jijini Mwanza, juzi, alisema, kwa upande wake CCM kuhusu kipengele hicho cha Tanzania kuwa na serikali ngapi, msimamo wake ni serikali mbili.

"Sisi CCM tunapotangaza msimamo wetu kwamba nchi hii inastahili kuwa ya serikali mbili, haina maana kwamba tunadharau au kuwaona wapuuzi  wanaopendekeza ziwe tatu, la, msimamo wetu huu tunaueleza kwa hoja ili hatimaye jamii ya Watanzania ikiziona zina mantiki watuunge mkono", alisema Nape.

Aidha Nape alisema, umuhimu wa kuwa makini na kutumia busara katika jamii kuhitaji mabadiliko unatokana na kwamba jamii ikiyapokea kwa pupa huambulia yasichotarajia, ikiwemo machafuko au uongozi wasiohitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yao ya maendeleo.

Nape alisema  katika pupa ya kutafuta mabadiliko, zipo baadhi ya nchi kama Misri ambazo hadi sasa zimekosa utulivu kutokana na kupokea vibaya dhana ya mabadiliko, wakaingia mitaani lakini bila kuchukua tahadhari, hatimaye wamejikuta mabadiliko waliyopata nayo hawayataki tena, wanataka mengine.

Akifafanua alisema, CCM inatambua kwamba, muundo wa serikali mbili ndio utafaa katika kudumisha Muungano, kuliko serikali tatu ambazo CCM inaona kwamba mbali ya kuwa mzigo zaidi kwa wananchi, pia ni kuongeza changamoto juu za zile zilizopo sasa kwenye muungano.

THE TANZANIA CONVENTION-TRADE AND INVESTMENT FORUM UK 2013

$
0
0
Tickets are selling fast for our annual conference -. THE TANZANIA CONVENTION-TRADE AND INVESTMENT FORUM UK 2013.This two-day conference, held on the 6th &7th December 2013, will bring together professionals from a variety of different disciplines to explore topics, share experiences and debate the issues at the heart of the Diaspora Concerns ,socially, politically, economically and culturally.

We also invite you to support our community Leaders Gala Awards Dinner that will be held on the same evening of the 7th December 2013. The evening provides an opportunity for you to join us in celebrating the vital work of Tanzanians in the Diaspora and friends of Tanzania as well as helping to deliver our mission to bring the UK and Tanzania closer together through our pioneering activities in business, policy and culture.

Funds raised from the dinner contribute directly towards the success of our programmes; highlights of which include our conferences (Tanzania Convention-Trade and investment Forum), policy briefings , and our film, culture and literature festivals.

We present these annual awards to those individuals who exemplify the concept of the ‘Servant Leader’. These awards highlight the links between economic success, professional excellence accompanied by moral leadership, and service to society. By recognising individuals who embody the ‘Servant Leader’ ideal, we seek to encourage widespread recognition and adoption of these values among the global Tanzania community.

Based on feedback from previous conferences, this two day event is designed to be informative, practical and, most of all, interactive.

Book your tickets now ,register or nominate someone by sending your email to newdealafarica@yahoo.co.uk TEL +447960811614

Thanks

The Tanzania Convention team

Newdeal Africa

NEWS ALERT: Jaji Francis S.K.Mutungi ateuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuchukua nafasi ya Mhe. John Tendwa aliyestaafu

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi (pichani) kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Article 14

RAIS UHURU KENYA AANDAA FUTARI KWA WAISLAMU IKULU YA NAIROBI

magereza yatia fora katika maonesho ya mifugo dodoma

$
0
0
Maafisa Mifugo wa Jeshi la Magereza wakiwapitisha Mbuzi wa Maziwa mbele ya Jopo la Majaji na Watazamaji wakati wa Mashindano Maalum ya Mifugo Kitaifa kwenye Arena iliyopo katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane, Nzuguni Dodoma leo
Maafisa Mifugo wa Jeshi la Magereza wakiwaswaga Ng'ombe wa Nyama wakati wa Mashindano Maalum ya Mifugo Kitaifa ambayo yamefanyika leo Agosti 05, 2013 katika Arena ya Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane iliyopo Nzuguni, Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Benedict Ole Nangoro. Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

KONGAMANO LA VIJANA NA RASILIMALI ZA TAIFA LAFANYIKA DAR

$
0
0

 Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana na Rasilimali, lililofanyika leo RiverSide, Ubungo jijini Dar es Salaam, Christopher Ngubiagai, akifungua mjadala kuhusu mada mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo na watatu ni mtoa mada, Wakili Evod Mmanda ambaye pia ni Mjumbe wa NEC wa CCM. Ngubiagai pia ni Katibu wa CCM mkoa wa vyuo vya elimu ya Juu.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhomgo akitoa mada kuhusu rasilimali ya madini, wakati kwenye kongamano la vijana na rasilimali za taifa, leo Ubungo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu wa CCM, Vyuo vya elimu ya Juu, Christopher Ngubiagai ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa kongamano hilo na watatu ni mwanasheria Evod  Mmanda aliyetoa mada kuhusu rasimu ya Katiba.
Wakili Mmanda akitoa mada kwenye kongamano hilo
 Ngubiagai akizungumza kwenye kongamano hilo
 Baadhi ya viongozi wa Vijana wa CCM  kutoka mkoa wa vyuo vya elimu ya juu wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Baadhi ya wadau wakiwa kwenye kongamano hilo
 Baadhi ya wadau wakifuatilia mada kwenye kongamano hilo
 Wadau wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kongamano hilo
 Baadhi ya wawakilishi kitoka vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio kwenye kongamano hilo
 Meza ya usajili wa waalilkwa waliofika kwenye kongamano hilo. 
Picha na Bashir Nkoromo

NSSF YAZIDI KUWAELIMISHA WANACHAMA WAKE FAIDA YA MFUKO HUO MAOENESHO YA NANE MJINI MOROGORO.

$
0
0
 
 MKUU wa idara ya Uhusiano NSSF Taifa Eunice Chiume (mwenye t-shirt ya kijani) akisikiliza malezo yanayotolewa kwa mmoja wa wanachama wa mfuko huo na Afisa mfawidhi Matekelezo NSSF Mkoa wa Morogoro Christopher Msagati  Katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu Nanenane nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
Afisa mwandamizi wa mafao katika mfuko wa NSSF Mkoa wa Morogoro Adolfrida Mulokozi akitoa elimu ya faida ya mfuko huo kwa wanachama wapya ndani ya viwanja vya  Mwalimu Julius Nyerere maarufu Nanenane nje kidogo ya Mji wa Morogoro pembeni ni mwenye T-shirt ya kijani ni mkuu wa idara ya uhusiano NSSF Taifa Eunice Chiume.

Congrats mdau SHAUKU KIHOMBO

$
0
0

Its a honour to the family of Mr. & Mrs Starford Kihombo that their son SHAUKU KIHOMBO has been enrolled to continue with Master's Degree at BEIJING INSTITUTE OF TECHOLOGYon 10th september 2013.Shauku is going to major on Masters of Business Administration specifically on Technological Business and Innovation.
The efforts that he has made during his undergraduate programmes has resulted to this important post.

MR AND MRS STANFORD KIHOMBO 
Shauku Sharing crucial Ideas with Vice President of Beijing institute of Technology,China University.Prof. Zhao Shanglu

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya The Whispers ya 'Rock Steady' iliturusha sana!

KUMBUKUMBU

$
0
0
EDDA JOSEPH PANJA (MRS PETER MALEKELA) 
 28/10/1960 – 06/08/2012


TUMEHESABU SIKU, WIKI, MIEZI, HADI SASA NI MWAKA MMOJA TANGU ULIPOTUTOKA TAREHE 06/08/2012 KATIKA HOSPITALI YA MKOA MOROGORO. TUNAKUKUMBUKA KWA WEMA WAKO, USHAURI NA MCHANGO WAKO KWA FAMILIA YETU. MIMI MUMEO PETER MALEKELA WATOTO BARAKA, MARIA, BEATRICE, BABA YAKO MZAZI JOSEPH PANJA, DADA YAKO SOPHIA NA SHEMEJI YAKO MTOI. WOTE WANAKUKUMBUKA AIDHA SHUKRANI ZIWAENDEE MADAKTARI WA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO NA SHUKRANI ZA PEKEE ZIMFIKIE DR. MWAIPAJA WA SHIRIKA LA MZINGA MOROGORO WALIOJARIBU KUOKOA MAISHA YAKO BILA YA MAFANIKIO.


BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA


JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. 

grandmalt yapata iftar ya pamoja na wadau wake.

$
0
0
Meneja masoko wa Tbl Fimbo Mohamed Buttala akizungumza na waandishi wa habari kwenye futari maalum iliyoandaliwa na kinywaji cxha GrandMalt ikiwa ni sehemu ya kutambua Mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo futari hiyo iliandaliwa na kinywaji kisicho na kilevi cha GrandMalt.
 Mkurugenzi wa masoko wa TBL Kushilla Thomas mwenye shati jeupe akishirikiana na wadau mbalimbali katika futari maalum iliyoandaliwa kwaajili kufuturu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo futari hiyo iliandaliwa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt.
 Wadau mbalimbali wakiongozwa na Kabula Nshimbo (hayupo pichani) wakishirikiana na wadau mbalimbali katika futari maalum iliyoandaliwa kwaajili kufuturu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo futari hiyo iliandaliwa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt. 

MKUU WA MKOA WA RUKWA ATEMBELEA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (katikati) akikagua mfumo wa umwagiliaji bustani za mbogamboga katika maonesho yanayoendelea ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) juu ya gari iliyotengenezewa mfumo wa nishati ya gesi katika maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua bidhaa mbalimbali kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya. Mkuu huyo wa Mkoa ameridhishwa na vifungashio vingi vilivyotumika katika maonesho hayo mwaka huu na wajasiriamali wa Mkoa wa Rukwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiangalia "shamba jiko" ambalo staili yake ni ya kupanda mbogamboga nyumbani katika eneo dogo kwenye maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua maji aina ya Dew Drop, maji pekee yanayotengenezwa Mkoani Rukwa Mjini Sumbawanga na Mjasiriamali wa ndani, maji ambayo wananchi na wadau wengi wanasifia ubora wake kuwa ni ya kiwango cha juu. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima wakikagua banda la Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga ambalo limesifika kwa umaridadi wake.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article4376-live.html

PAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA MUHEZA TANGA SIKU YA IDI PILI

$
0
0
MPAMBANO  mwingine wa masumbwi unatarajia kufanyika Muheza mkoa wa Tanga wakati wa siku kuu ya idi pili kwa ajili  ya kutoa burudani kwa wakazi wa Muheza akizungumza kuhusu mpambano huo mratibu wake ambaye ndiye mwandaaji wa mpambano huo Hatibu Mwijuma amesema mpambano huo umeandaliwa maalumu kwa ajili ya kutoa burudani wakati wa sikukuu ya Idi na mpambano utafanyika katika viwanja vya jitegemee

Mpambano huo utakaowausisha mabondia kutoka Dar es salaam na wa Muheza, Mbena Rajabu wa Dar atakaeoneshana kazi na Jumanne Mohamedi mpambano wa raundi sita huku George Allan wa Muheza ataoneshana ubabe na  Muhamed Meme wa Tanga

na mapambano mengine mengi ya kukata na shoka uku kukiwa na burudani ya muziki alitaja kiingilio kwa siku hiyo kwa kuwa tunaitaji kila mtu aje kushudia mchezo wa ngumi kwani  ni nafasi ya pekee tuliyoipata kingilio kitakuwa ni 2000,kwa 1000,

ili watu waweze kuangalia ulinzi ni wa uwakika mchezo uho utakaosimamiwa na Oganaizeshani ya ngumi za Kulipwa nchini TPBO umereta faraja kwa wakazi wa muheza kwani wana kiu kubwa ya kuangalia mchezo huo wa masumbwi unaopenda na watu wengi

WAKAZI WA KIJIJI CHA KIWERE NA KIPERA MKOANI IRINGA WALAZIMIKA KUTEMBEA UMBALI WA KM 50 KUFUATIA KIVUKO CHAO KUZOLEWA NA MAJI

$
0
0
 Wakazi wa kijiji cha kiwere na Kipera vilivyopo kata ya Karenga wilaya ya Iringa wakitembea juu ya kivuko chao cha miti cha muda baada ya kivuko chao kuondolewa na maji,aidha Wakazi hao wanalazimika kutembea umbali wa km 50 baada ya daraja la mti kuzolewa na maji.

WAKAZI wa kijiji cha kiwere na Kipera vilivyopo kata ya karenga wilaya ya Iringa wanalazimika kutembea umbali wa km 50 baada ya daraja la mti kuzolewa na maji.
 
 Akizungumza mwenyekiti wa kijiji cha kiwere,Yustin  Lipita alisema kuwa kutokana na ubovu wa daraja ambalo linaunganisha vijiji hivyo viwili wanakijiji hao wanalazimika kutembea umbali mrefu ili kufuata zahanati ya serikali ambayo ipo katika kijiji cha kipera .
  
“tunaiomba serikali kutujengea daraja ili wakazi wa kiwere na kipera waondokane na adha ya kutembea umbali mrefu kupitia Mlambalasi mpakani mwa Tarafa ya Pawaga na Kalenga palipo na umbali wa klm.46 kufuata shughuli zao za kilimo pamoja na huduma muhimu za kijamii”alisema Lipita.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha kipera Bonifasi Mgomati alisema kuwa Changamoto nyingi zimejitokeza kutokana na ubovu wa kivuko hicho ni vifo vya wakazi wa vijiji hivyo pamoja na kupoteza vitu vingi kama mizigo na Baiskeli kuendana  maji.
    
“Ni kivuko cha mudamrefu katika eneo hili toka mwaka 1975 Ingawa kabla ya hapo ilitumika kamba ya katani iliofungwa Ng’ambo na Ng’ambo na mvukaji kuitegemea anapovuka “alisema mgomati.
 
Sambamba na hayo mkazi mmoja wa kijiji cha kipera Antoni Kigehe alisema wanalazimika kutumia kivukohicho wanapokwenda katika Mashamba yao yaumwagiliaji  yaliopo kijiji cha Kiwere jambo ambalo ni hatari kutokana na  mazingira ya Daraja hilo la Miti pia ni vigumu watoto wadogo kuvuka pekeyao kwakuhofia usalama.

Mhasibu Aibuka mshindi wa Nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando  akiongea wakati wa  kuchezesha droo ya kwanza ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza  kupitia promosheni ya Airtel yatosha , kushoto Msimamzi wa  bodi ya  michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao kulia Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel yatosha ilimpata mshindi wa nyumba bwana Silvanus Juma kutoka mkoa wa iringa.

 Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando , Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao kulia Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakisubiri draw ya kutafuta mshindi itafutenamba ya mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza kupitia promosheni ya Airtel yatosha. 
Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia akiongea na mshindi wa nyumba mara baada  ya kupatikana katika draw ya mwenzi iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel morocco ambapo bwana
Silvanus Juma kutoka mkoa wa iringa aliibuka mshindi wa nyumba hiyo wakishuhudia Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao katikati akifatiwa na Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw,
Jackson Mmbando

=========   ========   =======
Airtel Tanzania imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba  kupitia
promosheni ya Airtel yatosha Shinda nyumba inayoendelea  na
kuwazawadia wateja wake kila siku.

Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni
mhasibu katika shirila la Tanzania Rural women and children
development foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa  nyumba kisasa iliyojengwa na shirika na nyumba la taifa NHC iliyopo kigamboni jijini Dar es saalam.

Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel
bwana Jackson Mmbando alisema" kama tulivyowangazia awali leo ndio ile
siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba  na tumeshuhudia bwana Silvanus Juma  akiibuka mshindi kupitia droo ya kwanza tuliyoichezesha hapa.

Sambaba na hilo leo tunao washindi 7 wa wiki  kutoka katika mikoa
mbalimbali ambao hawa wataondoka na pesa taslimu shilingi  milioni
moja kila moja, washindi hawa ni pamoja na  Peter Ignasho kutoka
Muheza Tanga, Edita Rweyabura  kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh
Ali Mauji, Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo
kutoka Manyoni Singida and Vero Mispela Kiwango kutoka Bihalamulo.

Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kuendelea kutumia huduma ya
Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi mbalimbali na kupata nafasi ya
kujishindia zawadi mbalimbali , kujiunga nirahisi piga  *149*99#
kisha nunua kifurushi chacko cha  siku, wiki au mwezi  na kisha
kuingizwa moja kwamoja kweny droo ya kuweza kushinda milioni moja kila
siku au zawadi kubwa ya Nyumba.

Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi Bwan Silvanus Juma
alisema"Ninayofuraha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel
napenda kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel waendelee
kutumia huduma ya Airtel yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo.
Binafsi sijawahi kushinda Bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini
kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba
ushindi ni wa uhakika usio na upendeleo wala ubaguzi hivyo wajaribu
nao wanaweza kuwa washindi.

Kwa upande wake moja ya wafanyakazi wenzake Bwana Beatus Magoti ambaye ni Mshauri wa fedha na utawala TARWOC alisema"  tumefurahi sana kuona kijana mgodo mwenzetu ambaye ni mchapa kazi ameweza kushinda nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha.  Hii imetupa hamasa na sisi
kushiriki na kueneza habari kwa wengine kushiriki na kushinda kama
laivyoshinda Silvano.

Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu
ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye
gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel yatosha.  Sambamba na hilo
Airtel pia imewawezesha wateja wake nchi nzima  kutuma na kutoa pesa
bure bila makato yoyote

Vodacom Foundation yakabidhi sadaka ya vyakula na vifaa vya shule gombani-pemba

$
0
0
 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom na baadhi ya wanafunzi wa Madrasa za Kisiwani Pemba mara baada ya zoezi la kukabidhi sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi hao muda mfupi kabla ya wote kushiriki futrari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwenye uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwishoni mwa wiki.
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Jaffary Juma akikabidhi vyakula vilivyotolewa na Vodacom Foundation kwa wanafunzi wa madrasa mbalimbali za Kisiwani Pemba tukio lililohusisha pia futari kwa ajili ya wanafunzi hao na wadau wa Vodacom Kisiwani humo iliyofanyika uwanja wa Gombani mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) na wafanyakazi wa Vodacom.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akizungumzia kampeni ya Pamoja na Vodacom namna inavyotekelezwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuandaa futari na kutoa sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi wa madrasa sehemu mbalimbali nchini. Mwaka huu Vodacom Foundation ilitenga Sh. 50 Milioni kwa ajili ya kampeni hiyo na kuwafikia wanafunzi zaidi ya 2500.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Uwanja wa Gombani Pemba tayari kuongoza hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wanafunzi wa Madrasa na wadau wa kampuni hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images