Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUANZA KWA USAJILI WA LAINI ZA SIMU WA KIBAIOMETRIKI


WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

WAFUASI watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
leo, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa
tuhuma za kufanya mkusanyiko isivyo halali.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amewataja washtakiwa hao watatu
kuwa ni, Isack Ng'aga, Erick John na Aida Olomi ambao wanadaiwa
kupigwa risasi na jeshi la polisi waliofikishwa kizimbani kwa Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wakiwa na majeraha katika sehemu za miguu na mapaja yakiwa yamefungwa bandeji.

Washitakiwa hao Machi 8, mwaka huu wataunganishwa na wenzao
28, wanaodaiwa kutenda kosa pamoja.Kwa pamoja wanadaiwa,
Februari 16, mwaka huu, huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni
lililopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko
usio wa halali kinyume cha sheria kwa nia ya kufanya uvunjifu wa
amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Wametajwa baadhi ya washitakiwa hao 28 ni Thabita Mkude, Haji
Lukwambe, Emmanuel Kimoi,Mohammed Juma, Hussein Mrombo,
Abdallah Hamis, Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein
Nguli na Edna Kimoro.

Wengine ni Jonathan Lema,Salha Ngondo, Ramadhan Mombo,
Godwin Mwakasungura, Hassan Kibweda,Omary Hamad, Fatima
Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa,Dickson Kerefu,
Raphael Mwaipopo, At human Mkawa, Mussa Kusigila, OMARY Danga,
Jackson Masilingi,Asha Kileta na Ally Rajabu.

Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana.
Baada ya kuachiwa kwa washtakiwa hao watatu ndugu zao waliwakumbatia na kuangua vilio mahakamani hapo.Kwa upande wake Wakili wa washtakiwa Alex Masaba alisema wamemaliza suala la msingi la wafuasi hao waliokamatwa Mkwajuni,ambao mwanzo hawakuletwa mahakamani lakini wenzao 28 waliletwa mahakamani na walipata dhamana

Alisema walifuatilia katika vituo vya polisi kwa siku 12 ambapo
walishindwana na polisi ambapo Februari, 26,mwaka 2018
walipeleka maombi Mahakama Kuu na juzi walipangiwa tarehe ya
kusikilizwa maombi yao ambayo ni jana.

TADB, NDC SIGN MoU FOR AGRI-INDUSTRIAL RESOURCE MOBILIZATION

$
0
0
Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) and National Development Corporation (NDC) signed a Memorandum of Understanding of cooperation in resource mobilization, lending, distribution, and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania.

Speaking on the objective of cooperation, the acting managing director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha said that the signed MOU will facilitate establishment of country-wide demand for tractors and farm implements as well as to facilitate mobilization of sustainable financial resources for provision of loans, procurement, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania and to facilitate the application of sound lending principles in the provision of loans for purchase of tractors and farm implements, including loan monitoring and evaluation.

Other benefits will include facilitating establishment of more efficient means of procurement, distribution, and delivery of tractors and farm implements; and providing a framework for establishing effective and continuing collaboration between the Bank and the Corporation.

“This MoU between the Bank and the Corporation will draw mutual benefits from cooperation between the two organizations in resource mobilization, lending, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania,” he said.
 Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) together with NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali (right) sign MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania. The signing in ceremony held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam.
 Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) and his NDC’s counterpart, Eng. Ramson Mwilangali (right) display signed MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania.
TADB’s management together with NDC’s counterpart in the Memoir Group Photo after signing the MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE

$
0
0

Na Agness Francis, Globu ya jamii

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania, imeendelea kutoa zawadi kwa wateja wake kupitia promosheni ya SMATIKA yatosha na Intanenti Bando inayoendelea kufanyika nchini.

Ambapo wateja wa Airtel hujishindia GB na zawadi zingine ikiwa ni simu za mkononi aina ya Smartphone na Modern ya Maajabu. Pia leo kampuni hiyo imemkabidhi mshindi wa simu aina ya Smartphone Mussa Ngai ambaye ni mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza leo jijini, Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando baada ya makabidhiano hayo akiwa kwenye duka la Airtel money Ukonga Mzambarauni Dar es salaam kuwa sasa wamefikia droo ya 10 kufanyika katika promosheni hiyo ambayo bado inaendelea kwa siku 30 zaidi. 

"Tumetimiza wateja 21,000 waliojishindia GB za bure na 30 waliojishindia simu na Modern ya maajabu kwa wateja wetu endeleeni kununua bando ili muweze kujishindia zawadi mbalimbali kutoka kwetu,"amesema Mmbando. 

Aidha Msimamizi wa duka la Airtel money Ukonga Mzambarauni Dorice Opiyo amewakaribisha wateja ambao ni wakazi wa maeneo hayo kupata huduma za kurejesha laini na kujipatia salio kwa wale wanatoa huduma za mawaka

Mshindi wa simu aina ya Smartphone, Mussa Ngai mkazi ambaye ni mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, akizungumzia kushinda promosheni hiyo amesema amefurahi kushinda kwani hakutegemea na alikuwa akinunua bando na kujiunga mpaka siku alipopigiwa simu kutoka Airtel ya kuambiwa ameshinda simu aina ya Smartphone.
 Mshindi wa Smartphone Mussa Ngai akikabidhiwa zawadi leo na  Dorice Opiyo Msimamizi wa Brunch ya Airtel Money Ya Ukonga Mzambarauni Jijini  Dar es salaam.
Mshindi wa simu ya Smartphone   Mussa Ngai  akikagua simu yake mara baada ya zoezi la makabidhiano kumalizika leo katika  tawi la Airtel Money Ukonga Mzambarauni Jijini  Dar es Salaam.
 Mshindi wa simu ya Smartphone  Mussa Ngai akipiga picha na wasimamizi wa Brunch ya Airtel money Ukonga Mzambarauni Jijini Dar es Salaam mara baada ga kukagua zawadi yake aliyoshinda kupitia promosheni ya SMATIKA na yatosha Intanenti bando.

TANDAHIMBA DHIBITINI MIMBA KWA WATOTO WA SHULE-MAJALIWA

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kuhakikisha inadhibiti ongezeko la mimba kwa watoto wa shule.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba. Waziri Mkuu amesema ni lazima viongozi hao wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike katika wilaya hiyo wasipate mimba ili waendelee na masomo. 

“Kwa nini kila mwaka mimba Tandahimba zinaongezeka, viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukua hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.” Amesema lazima wahusika wote wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwa sababu wanaharibu elimu ya motto wa kike jambo ambalo si zuri. 

Waziri Mkuu ametolea mfano mwaka 2015 wafunzi 10 walipata mimba, mwaka 2016 waliopata mimba walikuwa 20, mwaka 2018 waliongeza na kufikia 57.Amesema takwimu hizo haziridhishi, hatua kali zichukuliwe kudhibiti vitendo hivyo na Serikali haitaki kusikia mwanafunzi ameacha shule kwa sababu ya kupata mimba.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu na wafuate sheria. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi amewasisitiza watumishi wa umma wawafuate wananchi vijijini na wawahudumie ipasavyo.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.“Serikali inataka kila mtumishi atimize wajibu wake na haina muda wa kuwalea watumishi wazembe, wala rushwa na wasiowajibika, hivyo watambue wajibu wao.” 

Pia amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo wahakikishe wanakwenda kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao. 

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATANO, FEBRUARI 28, 2018.

CCM IRINGA MJINI YATEKELEZA AHADI YA SOKO KUU

$
0
0
Na MatukiodaimaBlog 

CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimetekeleza ahadi ya TV iliyoahidiwa wakati wa kampeni za ubunge mwaka 2015 na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) katika soko kuu la Manispaa ya Iringa .

Akizungumza leo mara baada ya kukabidhi TV hiyo na king'amuzi chake kwa uongozi wa soko kuu mjini Iringa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya alisema kuwa CCM imelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya TV nchi 58 baada ya wafanyabiashara wa soko hilo kuomba kusaidiwa TV hiyo kwa ajili ya kufuatilia habari mbali mbali zinazojiri nchini wakiwa katika sokoni hapo .

Alisema pamoja na kuwanunulia TV hiyo aina ya Sumsung wamepata kuwanunulia king'amuzi pamoja na kuwalipia malipo ya mwezi mmoja kuwa lengo la CCM kufanya hivyo ni kuendelea kuwahudumia wananchi na kutatua kero mbali mbali za wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao .

" CCM tumeendelea kutekeleza ahadi mbali mbali ila kama mtakumbuka kata ya Kihesa kulikuwa na jengo ambalo lilikwama kwa zaidi ya miaka 10 ila baada ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kihesa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri aliahidi na tayari ametekeleza hivyo CCM tukiahidi tunatekeleza wenzetu wakiahidi wanatelekeza ahadi zao "
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya kushoto akiwakabidhi wafanyabiashara soko kuu TV na king'amuzi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyomshinda mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) miaka 10 toka ahahidi 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ,katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya wakiwa na wafanyabiashara baada ya kutekeleza ahadi iliyomshinda mbunge Msigwa

WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri. 

BALOZI SEIF AHAIRISHA MKUTANO WA TISA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano yake dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia vilivyokithiri katika maeneo mbali mbali Nchini, kamwe haitamvumilia, kumuonea aibu, wala muhali Mtu yeyote wa cheo chochote na ngazi yeyote pindi atakapobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukifanyika katika Majengo ya Baraza hilo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya na kutahadharisha wazi kwamba Viongozi na Wananchi wanapaswa kutambua kuwa Sheria ni Msumeno.

Balozi Seif alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua kali za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kushiriki katika kadhia hiyo ikiwemo wafanyaji na wale wote wanaoshiriki katika kuwalinda na kuwakingia kifua wahalifu wote wa masuala ya udhalilishaji wa kijinsia.

Alivinasihi vyombo vya ulinzi na usalama kupambana zaidi dhidi ya vitendo hivyo vinavyolitia aibu Taifa sambamba na kuharibu maisha ya Wananchi, huku Jamii ikipaswa kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo hivyo katika Mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo baya Kijamii na hata Kidini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar katika Majengo ya Baraza hilo yaliopo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipotoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar .
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Balozi Seif alipokuwa akisoma Hotuba ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar M,h. Zubeir Ali Maulid akiongozwa na Askari wa Baraza hilo wakitoa nje ya Ukumbi baada kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi huko Chukwani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.Picha na – OMPR – ZNZ.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Arusha

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo (pichani) ambaye amepata ajali ya gari juzi mkoani Manyara bado amelezwa Hospitali ya Mount Meru akiendelea kupatiwa matibabu.

Akizungumza leo kwa njia ya simu na Michuzi Blogu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Yusuf Ilembo amesema licha ya kuwa bado Kamanda Mkumbo amelezwa hospitalini hapo  hali yake inaendelea vizuri.

"Bado amelezwa Hospitali ya Mount Meru akiendelea na matibabu lakini hali yake inaendelea vizuri tu,"amesema Ilembo na kuongeza msaidizi wa Kamanda Mkumbo na dereva wake ambao nao walipata ajali hiyo walisharuhusiwa na sasa wapo nyumbani.

Juzi Ilembo alipokuwa anazungumzia ajali hiyo, alisema ilitokana na kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kushoto na kusababisha gari kupinduka.

Baada ya gari kupinduka Kamanda Mkumbo aliumia kidole cha shahada na hivyo kupelekwa hospitalini kwa matibabu.Ndani ya gari hiyo pia alikuwa na msaidizi wake na dereva.

RAIS DKT SHEIN AFANYA MABADILIKO MADOGO BARAZA LA MAPINDUZI

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri.

Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;na shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1.    OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

i.    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu

2.    OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA

i.    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman

ii.    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma Mwalim

3.    OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

i.    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar Kheri

ii.    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 77.3 KUJENGA NEW BAGAMOYO ROAD DAR ES SALAAM

$
0
0
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Februari 28, 2018, Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na kushuhudiwa na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Barabara nchini-Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale.

Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya ujenzi wa barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Bw. Doto James amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia  kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayotoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

"Upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo si tu kwamba utaondoa msongamano wa magari, bali pia ni kiungo muhimu cha Bandari ya Bagamoyo ambayo itarahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma kutoka Jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na mikoa mingine nchini" Alisema Bw. Doto James.

Ameishukuru Japan kwa msaada mwingine uliotolewa mwezi Septemba, 2017 wa kiasi cha fedha za Japan (Yen) milioni 69 sawa na shilingi bilioni 1.4 ambazo zimetumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hiyo itakayoanza kujengwa

Bw. James ameeleza kuwa  awamu ya kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge pamoja na kukamilisha ujenzi wa madaraja ya Mlalakuwa, Lugalo na Tegeta.

“Si mara ya kwanza kwa Japan kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza Bw. Doto James.

Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida ameeleza kuwa kutolewa kwa msada huo ili kuwezesha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara kuanza kutayafanya matokeo ya kujenga barabara hiyo kuanza kuonekana dhahiri ikiwemo kupunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa ili kuokoa fedha nyingi zinazotokana na changamoto za msongamano huo.

"Ili kukamilisha usanifu wa kina wa mradi huu, nilisaini mkataba wa usanifu wa kina wa mradi wa upanuzi wa barabara ya new Bagamoyo  (Awamu ya Pili) miezi mitano iliyopita, hatimaye sasa ninasaini mkataba wa sehemu kuu ambayo ni ujenzi wenyewe" Alisema Balozi Yoshida.

Balozi huyo wa Japan hapa nchini, amesema mradi huo utasaidia kuboresha ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini nchini na kwamba msaada huo ni mwendelezo wa kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Japan na Tanzania.

Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari  yanayokadiriwa 52,000 yanayopita kila siku katika barabara hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale. baada ya tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya njia ya nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida, baada ya tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya Mradi wa upanuzi wa  Barabara ya njia ya nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili yaMradi wa upanuzi wa Barabara ya njia nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam. Anayeangalia makaratasi nyuma ni Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Prof. Elisante Ahudhuria Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara EAC

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria kwenye Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. 
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, (kulia) akiagana na Makamu wa Rais wa Uganda, Mhe. Edward Sekandi (kushoto) kwenye Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mhe. Sekandi ndiye alikuwa Mgeni Rasmi na ndiye aliyefungua Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo, Nchini Uganda kuanzia tarehe 28 Februari hadi 01 Machi, 2018.

WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI

$
0
0
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza  magonjwa  kwa binadamu.

Mpango huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika kuvichukua  vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kuvisafirisha na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo tarehe 28 Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu  alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko  hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.  
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akieleza  jambo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Mtaalamu Masuala ya Mpango Mkakati  wa Maabara  kutoka Shirika la Maabara –SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Baadhi ya Wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,  wakijadiliana namna ya kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi  na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Wataalamu wa Afya moja wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya   mkutano wa kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AZINDUA WA BARABARA TANDAHIMBA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu iliyojengwa kwa fedha za halmashauri leo Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara yenye urefu wa kilomita tatu iliyojengwa kwa fedha za halmashauri leo Februari 28, 2018.

Wananchi wa Wilaya ya Tandahimba wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza nao mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara yenye urefu wa kilomita tatu iliyojengwa kwa fedha za halmashauri leo Februari 28, 2018. 

VIONGOZI MTWARA FUATILIENI WATU WANAOTAKA KUHARIBU MASOKO YA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Mtwara kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnunuzi aliyekataa kununua korosho kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa korosho alichokikuta ghalani.Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

“Tandahimba korosho zote ni daraja la kwanza sasa korosho chafu zinatoka wapi? Kuna kundi linataka kuharibu soko lazima tupambane nalo.”Waziri Mkuu ameongeza kuwa “lazima mshirikiane kuwabaini walioleta korosho chafu Tandahimba na wakipatikana wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Amesema haiwezekani mnunuzi amenunua korosho daraja la kwanza alafu anakuja anakuta korosho nyingine tena chafu, lazima waliozibadilisha wasakwe. Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms, ambapo ametoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho wafunge mashine mpya na kuanza uzalishaji.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, Abdulrahman Sinani, wakati alipotembelea kiwanda hicho, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbanguaji korosho Zuhura Abdallah, katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kuchambua korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ubora wa korosho, iliyo teyari kuliwa, wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



CASTLE LAGER KUWAPELEKA WATANZANIA ‘WORLD CUP’

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, akionyesha moja ya kipeperushi kinachoelezea mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside) yaliyozinduliwa leo katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Masoko, Udhamini na Promosheni za Wateja George Kavishe na kushoto ni Mkufunzi wa Timu ya Castle Lager Tanzania, Ivo Mapunda.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Bia ya Castle Lager, imezindua rasmi mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside). Mashindano haya yenye hadhi ya kimataifa yanashirikisha timu za wachezaji watano (5) kila upande, na kocha mmoja. Mechi zake zitakuwa zikichezwa kwa dakika saba (7) ili kata mshindi. Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania huko Zambia katika michuano ya kimataifa dhidi ya nchi nyingine 5 kutoka Afrika ambazo ni: Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Lesotho.

Baada ya hapo mshindi atapata fursa ya kwenda Urusi kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia baadaye mwaka huu, akiambatana na mashabiki wawili ambao watapatikana katika mchakato malumu pamoja na mchezaji mmoja mkongwe kutoka nchi ambayo ni bingwa. Kama Tanzania itafanikiwa kushinda, timu pamoja na mashabiki hao wawili wataongozana na mkongwe katika soka Ivo Mapunda aliyekua kipa wa Taifa Stars na Simba Sports Club.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, alisema kuwa, kuna michakato maalumu ya kupata timu shiriki kupitia katika baa mbalimbali jijini Dar es Salaam.

“Utaratibu wa kupata timu utawahusisha moja kwa moja mashabiki wa baa husika kupendekeza timu zao, kabla ya hatua nyingine za kuzipigia kura timu zinazotakiwa kushiriki. Mteja wetu atapata maelekezo maalumu kutoka kwa watu wetu ambao watakuwa wakipita katika baa hizo kwa nyakati tofauti. Sifa kubwa ya mteja wetu kushiriki katika mchakato huo ni pamoja na kununua bia ya Castle Lager,” alisema Kikuli.
Akitolea maelezo za ziada jinsi mchakato huo wa Castle Lager Africa 5s utakavyokua, Meneja Masoko, Udhamini na Promosheni za Wateja George Kavishe amesema kua, michuano hiyo inashirikisha baa 160, zitakazogawanywa katika makundi 10, huku kila kundi likiwa na baa 16. Kila kundi litatakiwa kuwa na kiwanja chake katika michuano ya awali ya timu 16 na kupata timu 8.

Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitashiriki katika michuano hii. Hapa tukimaanisha Kinondoni, Ilala, Temeke, Ubungo na Kigamboni. Bonanza za kuanza kuchagua timu wakilishi za wilaya zitaanza tarehe 17 Machi hadi 21 Aprili kisha Bonanza kuu itakayoleta timu 10 za fainali itakua tarehe 28 Aprili 2018.
“Katika hatua ya pili ya bonanza tutapata timu moja kutoka katika yale makundi 10 ya awali na kufikisha idadi ya timu 10 zitakazocheza katika bonanza kubwa pale Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, kupata timu tano (5) zitakazocheza kwa mtindo wa ligi na hatimaye kupata bingwa.” Alisema Meneja Kavishe.

Michuano hii inafanyika kwa miezi miwili, ambapo washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa miaka kati ya 24 na 34. Lengo la mashindano haya ni kuwaleta pamoja marafiki na mashabiki wa soka. Wachezaji walioko katika ligi mbalimbali nchini hawatoruhusiwa kushiriki katika michuano hii, hata kama wana kigezo cha umri uliotajwa hapo juu.

Article 7

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 28.02.2018

Habari za UN: Chuo kikuu cha wakimbizi kufunguliwa Kenya - UNHCR

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 1, 2018

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images