Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

KIJANA ATIWA MBARONI KWA UTAPELI NA UBAKAJI JIJINI DAR ES SALAAM


ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam imesema imetumia zaidi ya Sh.bilioni 5.5 kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo  kwa bajeti ya kuanzia Julai mwaka 2017 hadi Desemba mwaka huo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu amesema fedha hizo zimetumika katika utekelezaji wa miradi inayohusisha  ujenzi wa vyumba  vya madarasa ,vyoo na hosteli.

"Kwa upande ya elimu ya msingi  shule mpya  nne zimejengwa kutokana na ongezeko la wanafunzi na ongezeko la wanafunzi ambalo limetokana na mpango wa Serikali wa elimu bila malipo,"amesema.

Pia  ametaja kuwa katia mpango huo madarasa 28 yamejengwa katika shule za msingi Bonyokwa, Mongo la ndege, Mbondole, Mji Mpya, Kibaga, Bangulo na Misitu. "Madarasa sita yamefanyiwa ukarabati darasa moja Kinyerezi na Mchikichini vyumba vitano" amesema Tabu.

Amesema katika fedha hizo jumla ya matundu ya vyoo 96 yamejengwa katika shule hizo huku matundu 40 yakiwa katika shule za zamani na yaliyobakia katika shule mpya.

Shaibu ameongeza pia fedha hizo zimetumika kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali ili kukabiliana na changamoto ya usafiri wa wanafunzi wanaokaa maeneo ya mbali na shule.

Aamesema halmashauri imefanya ukarabati wa huduma za mama na mtoto katika zahanati ya Msongola na Mvuti kwa kutumia mapato ya ndani ikiwa pamoja na ukamilishaji na ukarabati wa miradi ya maji katika kata ya Minazi, Tabata, Majohe, Vingunguti, sekondari Pugu, Mkera na Pugu stesheni.

Amesema katika kipindi hicho halmashauri imepeleka kiasi cha Sh. 543,400,000 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu na kukarabati miundombinu ya jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa DMDP.
 Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza juu ya taarifa ya utekelezwaji wa bajeti ya Halmashauri hiyo katika kipindi cha julai hadi Desemba 2017.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini Taarifa hiyo ambayo inatolewa na Tabu Shaibu.

MECHI YA LIPULI, NDANDA YASOGEZWA MBELE

0
0
Na Agness Francis Globu Ya jamii

MCHEZO uliokuwa uchezwe na timu Lipuli dhidi ya Ndanda katika dimba la Samora mkoani Iringa Wasogezwa mbele kwa maandalizi zaidi. 

Bodi ya Ligi (TPLB), imefanya mabadiliko ya mchezo huo namba 153 kati ya timu hizo mbili uliokuwa uchezwe Ijumaa ya Machi 2 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa leo, imeeleza kuwa sababu za kusogezwa mbele mchezo huo ni kutaka kuipa nafasi na muda zaidi Ndanda FC kusafiri kutoka Mtwara baada ya kumaliza mchezo wao wakiwa wenyeji dhidi ya Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga.

Ambapo sasa umepangwa kuchezwa Jumatano ya Februari 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona. Bodi ya Ligi (TPLB) imeamua mchezo huo wa Lipuli na Ndanda sasa umesogezwa mpaka siku ya Jumapili.Mchezo utachezwa kwenye Uwanja ule ule wa Samora mkoani Iringa. 

Ambapo mzunguko uliopita Lipuli alilazwa chali kwa bao 2-1 na Ndanda wakiwa ugenini katika Dimba la Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara. "Kupelekea mbele kwa mchezo huu sisi wachezaji umetupa muda zaidi wa kuendelea kufanya mazoezi,"amesema Beki namba 4 wa kikosi cha Lipuli, Martin Kazira.

MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifukuzia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk.William Morris raia wa Marekani dhidi ya mke wake Dk.Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira kwa garama.

Dk.William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo, akiomba, mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha DNA.Katika Maombi hayo Dk. Morris ambae ni mume wa (mdaiwa wa Pili, Philis Nyimbi) anaiomba Mahakama itoe amri ya mkewe Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA.

Lengo ni kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.Katika madai yake, Dkt. Morris anadai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume( 9).

Mapema mahakamani hapo,akisoma hukumu hiyo leo February 26 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dk.Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonesha mahusiano ya kimapenzi kati ya Dk.Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa Dk. Morris ni matokeo ya mahusiano ya kimapenzi kati ya Dk.Phills na Mchungaji Mwingira.Hivyo mahakama imeifukuzia mbali kesi hiyo ya madai na kueleza mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.

"Si tu ameshindwa moja kwa moja lakini ameshindwa kiasi ambacho Mahakama hii inalazimika kutoa amri kuwa alipe garama walizotumia wadaiwa kwenye shauri hili" amesoma Hakimu Simba.Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo Wakili wa mdai, Respicius Ishengoma amesema hawajaridhika na uamuzi huo na watakata rufaa.

Hukumu hiyo iliyoandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini imesomwa leo nyakati za saa 8 mchana.Awali kwenye utetezi wa Dk.Phills Nyimbi aliieleza Mahakama hiyo hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MTWARA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa jengo la wazazi katika kituo cha afya Chiwale, Wilayani Masasi, akiwa ameanza ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua wodi ya wazazi katika kituo cha afya Chiwale, mara baada ya kuweka jiwe la msingi kituoni hapo, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa Chiwale, Wilayani Masasi, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wazazi katika kituo cha afya Chiwale. Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kulipa ushirikiano wa kina Jeshi la Polisi Nchini katika kuona Amani ya Taifa pamona na Raia wake inaendelea kudumu muda wote. 

Alisema Zanzibar ina changamoto nyingi zikiwemo za Kisiasa, Dawa za Kulevya na ukosefu wa Maadili unaopelekea kuibuka kwa kasi zaidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia ambazo zinahitaji kushughulikiwa ipasavyo ili kuleta ustawi na Utulivu. 

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan aliyefika kujitambulisha Rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli hivi karibuni. 

Balozi Seif alisema masuala ya udhalilishaji pamoja na Dawa za kulevya hivi sasa yamekithiri na kuleta sura mbaya ndani ya Jamii kiasi cha kulazimika kutungwa sheria ili kujaribu kupambana na kadhia hiyo inayotoa picha mbaya katika uso wa Dunia. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliviagiza vyombo vya Dola kuwasaka na baadae kuwashughulikia ipasavyo wale wote wanaohusika na uingizaji wa Dawa za Kulevya Nchini kwa vile wao ndio chanzo cha balaa zote zinazotokea katika Mitaa mbali mbali Nchini. 

Hata hivyo Balozi Seif alikemea tabia ya baadhi ya Maofisa wa Vyombo vya Dola kujaribu kufifilisha kesi za Dawa za kulevya kwa kuwapa afuweni Watuhumiwa huku wakizingatia zaidi kupokea Rushwa badala ya kuwaonea huruma wale wanaoathirika kutokana na wimbi la Dawa hizo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akizungumza na Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan alipofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika yeye na Mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria walipofika kuaga rasmi. Kati kati yao ni Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria Muhidin Ali Mboweto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Muhidin Ali Mboweto Kushoto na Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Dr. Slaa Kulia na Balozi Seif Kulia wakifanyiana mzaha walipokuwa wakikumbushana utumishi wao wakati walipokuwa Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya M,uungano wa Tanzania mara baada ya mazungumzo yao.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

ALIYEKUWA MGOMBEA UDIWANI KATA YA MPINGA AHAMIA CCM

0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno akizungumza alipotembelea kata ya Mapinga ,wilaya ya Bagamoyo wakati wa muendelezo wa ziara yake anayoendelea nayo mkoani hapo kushukuru kuchaguliwa nafasi hiyo.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani ,(hayupo pichani) wakati alipokuwa amefanya ziara yake ya kushukuru wilayani humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Mapinga kupitia ACT Wazalendo uchaguzi mkuu uliopita ,Tabia Juma akiongea baada ya kuhamia CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno aliyoifanya wilayani Bagamoyo,pamoja na hilo uongozi mzima wa ACT kwenye kata hiyo ulihamia CCM.

IGP SIRRO AWATAKA ASKARI KUTENDA HAKI KWA WANANCHI WANAOWAHUDUMIA BARIADI, SIMIYU

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (wapili kushoto), akikagua baadhi ya vielelezo katika kituo Kikuu cha Polisi wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari mkoani humo, IGP Sirro amewataka askari kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima kutoka kwa askari wa kikosi maalum cha Jeshi hilo wakati alipowasili Bariadi mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi IGP Sirro pia aliwataka askari kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni wakati alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuzungumza na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo (hawapo pichani), kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mhe. Antony Mtaka. Picha na Jeshi la Polisi.

MAVUNDE AAGIZA WAAJIRI MWANZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF)

0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ameagiza Wakurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya JASCO LTD,AIRCO na JB BELLMONT HOTEL kufikishwa Mahakamani kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF).

Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jennister Mhagama ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo 30.09.2017.

Katika Mkoa wa Mwanza, Mavunde amesema jumla ya waajiri takribani 700 hawajajisajili katika mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi ambapo zoezi la msako wa waajiri hao litaendelea kwa wiki nzima na kuwachukulia hatua stahiki wale waajiri wote wataokuwa hawatii matakwa ya sheria ya Fidia ya Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 71(4) Mwajiri yoyote atakayeshindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh.50,000,000 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Pamoja na hayo, Mavunde amemuagiza Afisa Kazi Mfawidhi wa Mwanza kuwapa waajiri hao Amri tekelezi ya siku 30 kutekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004 kwa kuwapa Wafanyakazi wao mikataba,malipo ya mshahara kwa kima cha chini cha sekta husika na kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye ziara yake mkoani Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jenister Mhagama.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika ukaguzi wa viwango vya kazi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika ukaguzi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye ziara yake mkoani Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jenister Mhagama.
 

KUTOKA JESHI LA POLISI DAR: MWANAUME NA MWANAMKE WASHIKILIWA TUHUMA YA MAUAJI KADA WA CHADEMA DAR

0
0

*Polisi yaendelea kuchunguza kifo cha Akwilina,waua majambazi  Dar

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema linamshikilia mwanamke mmoja na mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusishwa na mauaji ya kada wa Chadema  Daniel John  aliyekutwa amekufa maeneo ya Coco Beach jijini.

Akizungumza leo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kutokana na uchunguzi unaendelea kuhusu mauaji hayo huko maeneo ya Hananasifu Kinondoni wamefanikiwa kuwakamata  watu wawili.

Amesema majina ya watu hao yamehifadhiwa kwa lengo la kutoharibu uchunguzi unaoendelea kuhusu tukio hilo la mauaji ya kada huyo wa Chadema.

UCHUNGUZI KIFO CHA AKWILINA WAENDELEA

Wakati huohuo, Kamanda Mambosasa amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usafirishaji Akwilina Akwiline aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi.

Mambosasa amesema bado wanaendelea kuchunguza tukio hilo ambalo limegusa hisia za watu wengi na baada ya kukamilisha uchunguzi wao watatoa taarifa kwa umma ili ujue.

WAKAMATA SILAHA TANO, RISASI 35

Pia Mambosasa amesema Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa takriban wiki mbili sasa wamekuwa wakifanya operesheni ya kukamata wahalifu wanaojihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jijini.

Amesema maeneo ya Pugu  alikamatwa mtu mmoja aitwaye Peter Kwema a.k.a Babu na alipohojiwa alikiri kujihusisha na matukio ya ujambazi katika mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Arusha,Tanga na Kilimanjaro.Pia ametaja baadhi ya wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao.

"Baada ya kumhoji alikubali kwenda kutuonesha ambako wenzake wapo lakini baadae aliamua kupiga kelele kuwashutua kwa lengo la polisi washambuliwe ili yeye atoroke.

KIGWANGALLA ATOA MIEZI TISA WANANCHI KULIPWA FIDIA WAPISHE HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE,PORI LA AKIBA MKUNGUNERO

0
0

Na Hamza Temba-WMU-Manyara

........................................................................

Serikali italipa fidia na vifuta jasho kwa vitongoji ambavyo vipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero ili viweze kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.


Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Kimotorok katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambao ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya za Simanjiro, Kiteto na Kondoa.


Alisema fidia hiyo italipwa kwa vitongoji viwili vya kijiji cha Irkishbo vya Maasasi na Lumbenek  vilivyopo katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ambavyo vilikutwa ndani ya Pori la Akiba Mkungunero wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 1996 kwa Tangazo la Serikali Na. 307.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho kukakua maeneo hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara. 

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na viongozi wa hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho kukakua maeneo ya mapito ya wanayamapori na mipaka ya hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara jana. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATANZANIA KUPENYA SOKO LA KENYA

0
0
Jonas Kamaleki- MAELEZO.

Serikali imetoa wito kwa  wafanyabiashara wa Tanzania kupeleka bidhaa zao katika soko la Kenya ili kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda wakati wa kikao cha Maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya.

Prof. Mkenda alisema kuwa ni nia ya Serikali kuhakikisha watanzania wanapenya katika masoko ya kimataifa ili kuongeza pato la mtu binafsi na la Taifa kwa ujumla.“Hali ya biashara kwa sasa ni nzuri sana, hivyo vikwazo visiwepo kabisa kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki”, alsiema Prof. Mwaikenda.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kuwa watanzania inabidi wathubutu na kuingia katika soko la Afrika Mashariki hususan soko la Kenya.Amesema kuwa wafanyabiashara wa Kitanzania wasiogope kuingia katika masoko ya nje ya nchi, wajitahidi ili waweze kuongeza vipato kutokana na ukubwa wa soko lililopo nchini na Kenya kwa ujumla.

“Mkifanya biashara Kenya mtaongeza mitaji, ajira na kipato kwa ujumla kwani nchi hizi mbili zina zaidi ya watu milioni 90”, na hii inaendana na falsafa ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya Uchumi wa Viwanda, hivyo hatuna budi kufuata maono ya Kiongozi wetu na kutengeneza na kuuza bidhaa za viwandani nje ya nchi”, alisema Balozi Pindi Chana.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akifafanua jambo kwa washiriki wa kikao cha kujadili maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kuia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dk. Pindi Chana na katikati ni Mtendaji Mkuu wa TANTRADE Edwin Rutageruka.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha kujadili maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Eliphace Marwa - MAELEZO.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO

0
0
Na Ripota Wetu, Arusha

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amepata ajali ya gari katika eneo la Mdori mkoani Manyara.

Taarifa kuhusu tukio hilo zinadai kuwa Kamanda Mkumbo amepata ajali leo, baada ya gari aliyokuwa akiitumia kupasuka gurudumu la nyuma.

Baada ya kupasuka kwa gurudumu hilo, gari ilipoteza muelekeo na kisha kupinduka.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Ambapo amesema ndani ya gari hiyo kulikuwa na watu watatu akiwamo Msaidizi wa Kamanda Mkumbo pamoja na dereva wake na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.

Ilembo amesema ajali hiyo imetokea leo saa nane mchana wakati Kamanda Mkumbuko akiwa njiani kutokea mkoani Singida kwenda Arusha na alipofika eneo la katikati ya Mdori na Minjingu ndipo guruduma la nyuma upande wa kushoto la gari hiyo lilipasuka na kusababisha ajali hiyo.

Amesema Kamanda Mkumbo ameumia kidole chake cha shahada na baada ya ajali hiyo amepelekwa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Arusha ambako anaendelea na matibabu wakati dereva wake naye analalamika maumivu kwenye paja la upande wa kushoto na msaidizi wake anasema hajaumia kwani hasikii maumivu mahali popote.

Amewataka wananchi wa Arusha kutokuwa na hofu kwani Kamanda Mkumbo hali yake inaendelea vema na kubwa ni kumuombea ili arudi kwenye hali yake ya kawaida na kuendelea na majukumu mengine ya kulitumikia Taifa.
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio a ajali hiyo.

SIMBA YAIBUGIZA MBAO FC BAO 5 - 0

0
0
 Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi akishangilia moja ya bao alilofunga katika mchezo dhidi ya Mbao FC mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo. Simba iliibugiza Mbao FC bao 5 - 0.
 Beki kisiki wa Simba SC, Erasto Nyoni akiwa katika furaha na Kiungo Mkabaji wa Kikosi hicho, James Kotei.
Emmanuel Okwi akiwa chini baadayakuchezewa ndivyo sivyo na Beki wa Mbao FC.
 Mashabiki wa Klabu ya Simba akifutilia mtanange huo, ambapo timu yao iliibuka na ushindi wa bao 5 - 0 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC.

VOA Swahili: Duniani Leo 26th February 2018


BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 26.02.2018

INTRODUCING "SO HIGH" BY JANB

Habari za UN: Bila hatua za haraka njaa Sudan kusini ni janga lisilo kwepeka - FAO

Introducing "Fire Fire" by Sultan King ft Msafiri Dioff

MNEC SALIM ASAS ATOA MSAADA WA MILIONI TANO KWA JUMUIYA YA WAZAZI KILOLO

0
0
MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Iringa Salim Asas ameichangia jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi ( UWT) wilaya ya Kilolo shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano.
Akifungua kikao cha baraza kuu la UWT Wilaya ya kilolo, Asas alisema kuwa lengo la kusaidia jumuiya hiyo ni kuitaka ijitegemee pia kuwa na miradi yake kwani ameona ni vema kuiwezesha jumuiya hiyo kupata ndoano kuliko kuipa samaki na kuwa kwa kipindi chake chote cha miaka mitano atakayokuwepo madarakani ataichangia jumuiya hiyo kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi huo "Ahadi yangu nitapaswa kuiweka katika maandishi ili familia yangu ijue pale nitakapo tangulia mbele za Haki ahadi hii iweze kutekelezwa na familia maana hatujui la kesho"
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images