Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI NACHINGWEA ASUBUHI HII

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea kuanza ziara ya kazi mkoani Mtwara Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MPINA ATOA MAAGIZO YANAYOTAKIWA KUTEKELEZWA NDANI YA WIKI MBILI

0
0
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepewa wiki mbili kufanya tathmini kuona kama kuna haja ya kuagiza maziwa na mazao yake kutoka nje ya nchi na kama waagizaji wanafuata taratibu na masharti ya kisheria yaliyowekwa na Serikali.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa katika ziara ya kutembelea kituo cha Taifa za uzalishaji wa mbegu Bora za Mifugo kwa njia ya chupa kilichopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Waziri Mpina pia aliitaka Wizara yake kuandaa mpango kazi utakao wezesha kuzalisha Ng’ombe milioni moja kwa mwaka kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 ili kuweza kusaidia kujenga viwanda vya maziwa na kuweza kumudu soko la ndani na hata kuhudumia bara zima la Afrika na kusaidia kuongeza pato la Taifa.

“Kuna makampuni 43 nchini yanayoingiza maziwa toka nje ya nchi,na makampuni 81 yanayojishughulisha na maziwa na mazao yake,Wizara ifanye tathmini kama kweli tunahitaji kuingiza maziwa hayo. Alisisitiza Mpina.” 

Aliongeza kuwa maziwa mengi yanaingia ndani ya nchi kwa kupitia njia za panya, na kusema kuwa wale wote wanaojishughulisha na biashara hizo wapo hatarini kukamatwa na sheria itachukua mkondo wake. “Mimi na Wizara na yangu tumejipanga kimwili kiroho na kiakili tutawashughulikia wote wanaofanya biashara hizi kimagendo hakuna suluhu kwa yeyote atakaye kamwatwa. Alisisitiza.” 

Sambamba na hilo, Waziri Mpina pia alimpongeza katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo kwa kazi kubwa ya kuhakikisha kuna kuwepo na mbegu za kutosha kwa kuwepo kwa madume bora 26 hadi sasa yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya dozi 3,120,000 kwa mwaka.

Kwa upande wake, Dkt. Mashingo alimshukuru Waziri kwa kutoa maelekezo ambayo yanalenga kuleta mapinduzi ya mifugo na kwamba ameyapokea na yatatekelezwa mara moja kama alivyoagiza.
Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake akiwa akiwa katika ziara katika kituo cha Taifa cha uzalishaji Mbegu bora za Mifugo kwa njia ya chupa, (NAIC) kilichopo Mjini Arusha.
Katikati Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo akisoma Hotuba katika zoezi la uzinduzi wa madume ya kisasa ya mbegu bora za Ng’ombe katika kituo cha taifa cha uzalishaji mbegu bora kilichopo mjini Arusha, Kushoto ni waziri wa Mfugo na Uvuvu Mhe. Luhaga Mpina, na kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara hiyo, Dkt.Lowlence Asiimwe.
Katikati Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia dume bora la kisasa kutoka nchi ya New Zealand katika kituo cha Taifa cha Uhimilishaji cha (NAIC) Arusha jana alipokuwa katika ziara maalum ya uzinduzi wa Madume hayo.kulia ni Dkt Paul Mollel, Mkurugenzi wa Kituo hicho.
Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madume bora ya kisasa kutoka nchi ya South Africa na New Zealand yaliyoletwa nchini kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu bora za mifugo. Pembeni yake ni katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo na ujumbe wake

TUNZENI MAJALADA YA HATI ZA ARDHI KWA KUFUATA TARATIBU- NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA

0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akieleza namna bora ya kuhifadhi majalada ya hati za ardhi katika halmashauri ya Tarime mkoa wa Mara wakati za ziara yake mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akizungumza na watumishi wa halmashauri za Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake mkoa wa Mara.
 Mkuu wa wilaya ya Tarime Grorious Luoga akizungumza wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na watumishi wa halmashauri ya Tarime.
 Baadhi ya watumishi wa halamashauri ya Tarime wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula. 
  Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoka Kanda ya Ziwa, Wizarani whauri ya Tarime na Naibu Waziri Angelina Mabula.
 Baadhi ya watumishi wa halmashauri wakiwa katika mkutano.
Baadhi ya watumishi wakiwa katika kikao.

DC SHINYANGA AFANYA OPARESHENI USAFI NA MAZINGIRA,AKAMATA NA KUTOZA FAINI WENYE MITI ILIYOKUFA

0
0

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendesha oparesheni ya usafi na Mazingira kukagua usafi na miti iliyotelekezwa na kuwawajibisha wananchi ambao miti yao imekufa kwa kulipa faini ya shilingi 50,000/= kwa kila mti na kuwataka wapande miti mingine. 

Mkuu huyo wa wilaya amefanya oparesheni hiyo Februari 24,2018 katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga ambapo kila mwananchi ambaye miti iliyopandwa kwenye eneo lake imekufa aliwajibishwa kwa kufanya uzembe na kusababisha miti ife. 

Katika opareshini hiyo kila mwananchi aliyepigwa faini alikuwa anapatiwa risiti ya malipo na aliyeshindwa kulipa alikuwa anapandishwa kwenye gari la polisi kwa hatua zaidi za kisheria. Akizungumza wakati wa oparesheni hiyo Matiro ambaye alikuwa ameambatana na maafisa mbalimbali na askari polisi alisema hataki kuona miti iliyopandwa kupitia kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa Septemba 23,2017 yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ inakufa kwa uzembe kwani walikubaliana kila mwananchi atunze miti hiyo. 

“Miezi mitano iliyopita tulianzisha kampeni ya upandaji miti wilayani hapa ili kuboresha mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa,tukapanda miti na kumtaka kila mwananchi atunze iliyopo kwenye eneo lake”,alieleza Matiro. “Nimeanza kukagua miti hii ili nione imefikia hatua gani,kama mti uliopo kwenye eneo lako lazima tukuwajibishe,wote tuliokuta miti imekauka tumewapiga faini ya shilingi 50,000/=”,aliongeza. 

Matiro alisema wilaya hiyo imepiga marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=. Afisa Misitu wa Manispaa ya Shinyanga,Emmanuel Nyamwihura alisema wanatoza faini hizo kwa mujibu wa sheria ya Usafi na Mazingira ya Mwaka 2014. 
Mmoja wa wananchi katika kata ya Ibinzamata akijitetea kwa kuonesha dumu la maji alilokuwa analitumia kumwagilia maji mti wake uliokufa.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. Kushoto ni Afisa Misitu wa Manispaa ya Shinyanga,Emmanuel Nyamwihura - Picha zote na Kadama Malunde1 blog 
Wananchi ambao miti iliyopandwa mbele ya makazi au biashara zao imekufa wakipanda kwenye gari la polisi. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza mwananchi ambaye miti yake imekua vizuri. 
Mwananchi akionesha mti wake uliokufa kabla ya kulipa faini ya shilingi 50,000/=. 

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI,MASONGA WAHUKUMIWA MIEZI 5 JELA KWA KOSA LA UCHOCHEZI

0
0

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Hukumu hiyo imetolewa leo Feb. 26, 2018 na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite baada ya kuridhika ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Pia mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miezi sita katibu wa chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga kwa kosa hilo.

Washtakiwa hao wanatajwa kutenda kosa la kutoa maneno ya kumfedhehesha rais Disemba 31, 2017 katika viwanja vya Luanda Nzovwe wakati wakizungumza na wananchi.

TEKNOLOJIA YA KISASA KUTUMIKA KUKABILIANA NA UJANGALI HIFADHI ZA TAIFA,MAPORI YA AKIBA

0
0

Na Woinde Shizza,Kilimanjaro

IMEELEZWA kuwa teknolojia mpya itaanza kutumika kwenye hifadhi za Taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya Serikali kwa lengo la kupambana na ujangili hasa maeneo ambayo yameathirika zaidi.

Hivyo maofisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini watatumia teknolojia hiyo kukomesha jangili.

Hayo yamesemwa leo  na maofisa wa Wanyamapori,Maliasili,Ulinzi na Uhifadhi was mazingira katika hiadhi za Taiga na mapori ya akiba ya wanyama ya Serikali nchini.

Maofisa hao walisema matumizi ya simu na kompyuta zenye programu ya smart ambayo hutumiwa kuainisha maeneo hatarishi kwa ujangili na uvunaji holela wa miti yanaweza kuwekewa alama maalum za kitaalam na kuimarisha ulinzi zaidi.

Ofisa wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka, Rudolf Philemon amesema matumizi ya teknolojia hiyo yatasaidia kukabiliana na kupunguza vitendo vya kijangili.Pua uvunaji haramu wa misitu na kurahisisha mbinu za kuwakamata majangili.

Rudolf amesema kwa kutumia program hiyo ipasavyo inatarajia kupunguza vitendo vya ujangili katika Hifadhi za taifa na mapori ya akiba ili mali asili za Taifa ziwe salama kwa manufaa ya Watanzania wote.

Mhifadhi wa Pori la Akiba la Ugalla mkoani Tabora Braka Balagaye amesema programu hiyo pia itasaidia katika kukusanya ushahidi wa matukio mbali mbali ya majangili wanapokamatwa katika hifadhi za taifa, mapori ya akiba na misitu ya Serikali ambao unaweza kutumika mahakamani.

“Programu hii itawarahisishia kazi askari wanaofanya doria katika hifadhi kuweza kuifanya doria yao kimkakati na kuzaa matunda kwa kudhibiti ujangili ambao ni tatizo sugu barani Afrika katika hifadhi nyingi,"amesema Baraka.

Mkufunzi wa Programu hiyo kutoka shirika la uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori (WCS) kutoka nchini Thailand Antony Lyman amesema, programu hiyo ikitumika ipasavyo ina uwezo mkubwa wa kutokomeza kabisa matukio ya ujangili katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Maafisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za Taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini Wakifuatilia mafunzo ya naamna ya kutumia teknolojia ya Smart kwa njia ya simu na kompyuta kukabiliana na Ujangili na uharibifu wa misitu .Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka
Maafisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini Wakifuatilia mafunzo ya Namna ya kutumia teknolojia ya Smart kwa njia ya simu na kompyuta kukabiliana na Ujangili na uharibifu wa misitu. Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI MASASI

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, akiwa ameanza ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara  Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza nao
    

MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA

0
0
Miongoni mwa maeneo ya kitalii ambayo hayapewi kipaumbele au kutokuwa maarufu ni pamoja na Kusini mwa Tanzania. Tofauti na vivutio vya kitalii vya kanda ya Kaskazini kuwa maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro, kuna uwezekano mkubwa kwamba Kusini mwa Tanzania kuna hazina kubwa ya vivutio kwa watalii ambavyo havitangazwi au kuvumbuliwa na wengi.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikikwamisha shughuli za kitalii kwa ukanda wa Kusini ni pamoja na miundominu hafifu kama vile barabara, viwanja vya ndege ambavyo hupelekea maeneo hayo kufikika kwa ugumu pamoja na upungufu wa malazi kama vile hoteli za kisasa na zinazokidhi vigezo.

Kwa kutambua umuhimu wa ukanda huu, serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanya jitihada za makusudi ambazo zitakuwa ni chachu katika kukuza utalii. Jitihada hizo ni pamoja na kuzinduliwa kwa mpango wa uwekezaji katika miundombinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa Kusini mwa Tanzania (REGROW) eneo la Kihesa, Kilolo mkoani Iringa. Mradi huo ulizinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Bi. Samia Suluhu na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala. 
Pamoja na jitihada hizo watalii na watanzania kwa ujumla wanahitaji kujua vivutio vinavyopatikana katika eneo hilo. Kwa kutambua umuhimu wa kutoa elimu juu ya vivutio mbalimbali nchini Tanzania, Jumia Travel imekukusanyia vivutio na shughuli zifuatazo za kitalii pindi utembeleapo eneo la Kusini mwa Tanzania.
Iringa. Mkoa wa Iringa ni kivutio tosha kutokana na historia yake ndefu tangu enzi za utawala wa kikoloni wa Wajerumani. Ni eneo ambalo Wajerumani walijenga ngome yao kwa ajili ya kupambana na vuguvugu za harakati za kukataa kutawaliwa kutoka kwa kabila la Wahehe ambazo ziliongozwa na Chifu Mkwawa. Mji huu ambao ulijengwa tangu karne ya 19 una mambo mengi ya kujifunza na kujionea pindi utembeleapo ambayo hayapatikani sehemu yoyote nchini. 
Isimila. Mbali na harakati za wazi za kupinga ukoloni wa Wajerumani, eneo la Kusini linasifika kwa kupatikana kwa mabaki ya historia za kale. Eneo hili limegundulika kuwa na masalia ya kutosha ya zana za kale za Zama za Chuma kuliko eneo lolote duniani, ambapo inasemekana ni maeneo ya mwanzo kabisa kuzalisha zana za viwandani na vichwa vya mishale.
Bonde la Kilombero. Ukubwa wa bonde hili ambalo hujaa maji kwa msimu umelifanya kuwa ndilo kubwa katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kuna shughuli nyingi za kufanya kama mtalii na mambo kadhaa ya kujifunza pindi utembeleapo eneo hili linalopatikana mkoani Morogoro. Miongoni mwa shughuli za kufurahia ni pamoja na kujionea ndege wa aina mbalimbali wa kuvutia pamoja na shughuli za kijadi za wakazi wa eneo hilo kama vile uvuvi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATUMISHI WA UMMA MSINYANYASE WACHIMBAJI WADOGO – BITEKO

0
0
Serikali imesema itawachukulia hatua za kinidhamu watendaji wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa wachimbaji wadogo wa madini nchini ili kujipatia kipato kinyume na taratibu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Dhahabu ya Kitunda yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora.

Wakielezea changamoto zinazowakabili, wachimbaji wa machimbo hayo kwa nyakati tofauti walimueleza Biteko masikitiko yao juu ya unanyasaji wanayofanyiwa na baadhi ya Maafisa wa Serikali wasiowaaminifu wakiwemo Askari Polisi na Maafisa Madini.

Wachimbaji hao walisema kumekuwepo na tabia ya kushinikizwa kutoa rushwa ama kugawana faida kwa vitisho kuwa watazuiwa kuendelea kufanya shughuli zao kwenye maeneo husika.

“Kuna baadhi ya Maafisa Madini na Askari Polisi wamekuwa wakitulazimisha nao tuwape mgawo wa mawe tunayochimba vinginevyo watafukia maduara yetu,” alisema Alfred Kulwa mmoja wa wachimbaji kwenye machimbo hayo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mwenye kipaza sauti) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda ya Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora. Biteko alifanya ziara kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli zinazoendelea sambamba na kuzungumza na wachimbaji.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri wakiwa kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa machimbo ya dhahabu ya Kitunda yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Katavi.
Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) alipofika kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli wanazofanya pamona na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) alipofika kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli wanazofanya pamona na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akiwasilikiza baadhi ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge wakiuliza maswali na kuelezea changamoto mbalimbali ziazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mwenye kipaza sauti) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda ya Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora. Biteko alifanya ziara kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli zinazoendelea sambamba na kuzungumza na wachimbaji.

TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME

0
0
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kupitia kikosi kazi maalum limeendesha kampeni kabambe ya kubaini na kutokomeza matukio ya wizi wa umeme pamoja na uhujumu miundombinu ya Shirika Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa jitihada endelevu za TANESCO katika kudhibiti upotevu wa mapato ya Shirika. 
Akiongea katika kampeni hiyo, Kaimu Meneja wa TANESCO Makao Makuu anayesimamia Wateja Wakubwa Mhandisi Fredrick Njavike ambaye pia ameongoza Zoezi hilo alisema kuwa, ndani ya siku tano kupitia kampeni hiyo tayari wamekagua takribani wateja 2000 katika Wilaya ya makambako pekee huku Njombe Mjini wakitarajia kukagua wateja 1000. 

Njavike ameongeza kuwa katika idadi ya wateja waliokaguliwa, wateja kadhaa walibainika kujihusisha na vitendo vya wizi wa Umeme. Kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe wahalifu hao walichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa gharama za kiasi chote cha umeme walichokuwa wakiliibia Shirika baada ya kupigiwa mahesabu.

"Zoezi hili la ukaguzi na msako wa wezi wa umeme ni zoezi endelevu linalofanyika Nchi nzima na niwatahadharishe wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kwani ni lazma watagundulika na hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia ya kiasi cha umeme walicholiibia Shirika. 

Hivyo niwaombe Wananchi kuendelea kutupa ushirikiano kwa kufichua watu wenye viashiria vya Wizi wa Umeme. Lakini pia niwaombe wateja wetu kutoa taarifa TANESCO pale wanapona hitilafu zozote katika mita zao pamoja na kuepukana na vishoka wanaowashawishi waibe umeme kwani kupitia msako huu hakuna atakayeiba Umeme na akasalimika bila kukuamatwa na kuchukuliwa hatua" Alisema Mhandisi Njavike
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wezi wa Umeme popote walipo ili waweze kuchukuliwa hatua na kuokoa upotevu wa mapato ya Shirika kwa ujumla.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi walioshuhudia msako huu ukifanyika mitaani waliipongeza TANESCO kwa kuanza kutambua thamani ya mali zao na kulinda umeme wao ambapo mwanchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mponzi alisema kuwa Matukio ya wizi wa umeme yapo mtaani na wakati mwingine yamekuwa yakisababisha hata vifo kwa wahusika kunaswa na umeme wakati wakijaribu kuiba umeme hivyo ni vyema TANESCO pia Wakatoa na Elimu juu ya madhara ya Wizi wa umeme kwa wananchi wote wafahamu.

Aidha TANESCO imekuwa ikiingia hasara kutokana na vitendo vya wateja wachache ambao kwa makusudi kabisa wamekuwa wakiliibia Shirika umeme kwa katika maeneo mbalimbali na hivyo kulikosesha Shirika mapato stahiki na kurudisha nyuma jitihada za TANESCO na Serikali Katika kusambaza Umeme Nchi nzima na hivyo kufifisha kasi ya Uimarishaji wa Miundombinu ya Uzalishaji, Ufuaji na Usambazaji umeme Nchini.

MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA MBALI MBALI VYA WALEMAVU KUTOKA SERIKALI YA KUWAIT

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Vifaa vya Walemavu vilivyotolewa na Serikali ya Kuwait ,pichani ni Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al Najem (katikati) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vifaa vya walemavu vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem, wengine pichani ni Msaidizi wa Balozi wa Kuwait Bi. Zainab Ally (kushoto) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijaribu kusukuma kiti maalum cha magurudumu kwa ajili ya walemavu mara baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem (kulia), wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa na Msaidizi wa Balozi wa Kuwait nchini Bi. Zainab Ally.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

WATAALAM WA AFYA MOJA WAJIPANGA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI NCHINI

0
0
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wamejipanga kudhibiti vimelea hatarishi kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo .

Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu alibainisha kuwa serikali kupitia Dawati la uraribu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuandaa mpango wa kudhibiti vimelea hivyo ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii na pia kamati maalum ya wataalam hao imeundwa iili kuufatilia na kusimamia mpango huo.

“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Maafa ndiyo yenye dhamana ya kuratibu maafa kama ya magonjwa ya mlipuko kama kimeta, Hivyo jitihada za serikali za kuwakutanisha wataalam hawa ili ni kuweza kuijenga jamii salama ambayo haiathiriki na magonjwa yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia mpango huu.” Alisema Taratibu.

Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa kuandaliwa kwa mpango wa kuzishirikisha sekta zote za afya kutaimarisha afya za binadamu kwakuzingatia kuwa upo mwingiliano mkubwa kati ya binadam na. wanyama.

Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika DTRA wameandaa mkutano wawadau hao.
Mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Jacob Lusekelo akiwasilisha mada juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi , wakati wa mkutano wa wataalam wa afya moja mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi mjini Morogoro, tarehe 2 Februari, 2018.
Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi.

DK.SHEIN AZUNGUNGUMZA NA MABALOZI WAPYA (WILBROAD SLAA NA ALLY MBOWETO) LEO

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe.Wilbroad Peter Slaa alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha pia na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe.Muhidin Ally Mboweto alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe.Wilbroad Peter Slaa (katikati) na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe.Muhidin Ally Mboweto walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe.Wilbroad Peter Slaa (katikati) wakati wa mazungumzo yao na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe.Muhidin Ally Mboweto (kushoto) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Picha na Ikulu

PLAN INTERNATIONAL,UMOJA WA ULAYA YAWAWEZESHA KIUCHUMI VIJANA 592 WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU KIBAHA

0
0

VICTOR MASANGU, KISARAWE

JUMLA ya vijana wapatao 592 wanaoishi katika mazingira magumu,yatima,na wasichana waliopata mimba katika umri mdogo kutoka katika Wilaya ya Kisarawe Kibaha Mkoani Pwani wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ya ufundi stadi wa aina mbali mbali pamoja na kukabidhiwa vifaa vya kazi kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini ambalo limekuwa likiwakabili.

Vijana hao wamepatiwa msaada wa vifaa mbali mbali vya kuendeshea shughuli za ujarisiamali kupitia mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi ujulikanao kwa jina (YEE) ambao unasimamiwa na Shilika lisilokuwa la kiserikali la Plan Internationala kwa ufadhili wa jumuiya ya umoja wa Ulaya.

Wakizungumza katika halfa fupi ya makabidhiano hayo baadhi ya vijana hao walionufaika na mradi huo akiwemo Magnalena Mwendo na Piusi Charles walisema kwamba msaada huo na mafunzo na vifaa walivyopatiwa vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini ambapo pia wameiomba serikali kuwasaidia kupata mikopo ya fedha mfumo wa maendeleo ya vijana.

“Sisi vijana tumefarijika sana kwa kupata vifaa hivi ambavyo kwa kweli vitaweza kutusaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondoka na janga la umasikini kwani hapa awali tulikuwa tunaishi katika mazingira magumu hivyo kwa upande wetu tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa shirika la Plan international pamoja na Umoja wa ulaya amnbao ndio wamefadhuli mradi huu wa kuwawezesha vijana kiuchumi hasa sisi tuliokuwa katika hali dumu,”walisema.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tamisemi Sememani Jafo Kulia wa Meneja wa mradi wa Yee kutoka Shirika lisolokuwa la kiserikali la Plan international Simon Ndembeche wa kushoto wakikagua vifaa mbavyo vimetolewa kwa vijana wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kiluvya Wilayani Kisrawe katika halfa fupi ya kukabishi vitendea kazi
Diwani wa kata ya Kiluvya Aidan Kitare akizungumza jambo wakati wa sherehe ya kukabiddhi vifaa kwa vijana wa kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu, ambapo wamesomeshwa na kupatiwa vitendea kazi na shirika la Plan International kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na janga la umasikini.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza katika halfa ya kukabidhi vifaa kwa vijana wa kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu, na wengine yatima.
Baadhi ya vijana wanaoishi katika mazingiza magumu katika kata ya Kiluvya Wilayani Kibaha ambao wamewezeshwa kiuchumi na shirika la Plan Innternationala ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasisiki.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU.

Tigo Yamwaga Smatifoni Kwa Washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

0
0
‘Kwa sasa mama yangu anatumia simu ya kawaida ambayo haituwezeshi kuwasiliana kikamilifu kwa njia ya mtandao. Kwa mfano siwezi kumtumia picha za wajukuu wake. Ndio maana nitampa zawadi ya simu hii mpya niliyoshinda kutoka Tigo leo ili iturahisishie mawasiliano yetu na kumfanya awe sehemu ya ulimwengu wa kisasa wa mawasiliano.’ Haya ni maneno ya Margareth Martin Hiza, mfanyabiashara na mkaazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka moja wa washindi wa simu mpya za kisasa senye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 4G katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na Tigo Tanzania. 

Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu janja 900 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka Nyaka Bonus, promosheni murwa inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwaya *147*00#.
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Rajabu Saidi Yote (kulia), ambaye ni mkaazi wa Tandika Dar es Salaam, akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo. 
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Tinna Sharon Masatu (kulia), ambaye ni mkaazi wa Mbezi Beach akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa katika promosheni hiyo. 
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Margareth Martin Hiza (kulia), ambaye ni mkaazi wa Ubungo, Dar es Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWS ALERT: UTEUZI WA DIWANI WA VITI MAALUM - CHADEMA

0
0
  Kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Kikao chake cha tarehe 23 Februari, 2018, imemteua Ndugu JANE JAPHALY JOJO kuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
            Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ndugu Ester L. Mpwiza.
Tume baada ya kupokea Taarifa hiyo, ilikifahamisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kiliwasilisha jina la anayependekezwa kuteuliwa kuwa Diwani wa Viti Maalum kutoka katika orodha ya majina yaliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015.
Imetolewa leo Jumatatu, tarehe 26 Februari, 2018 na: 
Kailima, R. K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

VIONGOZI TOWNSHIP ROLLERS YA BOTSWANA WATUA DAR

0
0

Na Agness Francis Globu ya jamii 

VIONGOZI wa Timu ya Township Rollers inayotarajia kumenyana na mabingwa wa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC  katika dimba la Uwanja wa Taifa  wameamua kufanya ziara jijini Dar es salaam. 

Wakizungumza leo, viongozi hao ambao ni Motshegetsi Mafa na Sydney Magagane wamesema lengo la kufanya ziara hiyo ni kuandaa mazingira mazuri ya timu yao sehemu itakapofikia kwa ajili ya mchezo huo na mipango mingine.

Kwa siku ya jana walifika hadi maeneo yaliyopo Makao Makuu ya  timu ya Yanga SC eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam na kuonana na wenyeji wao ambao ni uongozi wa klabu hiyo na kufanya mazungumzo.

Pia wametembelea Uwanja wa Taifa jijini ambao ndio  utakaotumika kwa mtanange huo unaotarajia kupigwa Machi 6 mwaka huu. Timu zote mbili zinashauku ya kusonga mbele kuendelea na michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika.

KIJANA ATIWA MBARONI KWA UTAPELI NA UBAKAJI JIJINI DAR ES SALAAM

POLISI KANDA MAALUM WAMSHIKILIA 'MTU HATARI', ANAYEJIFANYA FREEMASON NA KUFANYA UKATILI KWA WANAWAKE

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia, Rajabu Mohamed(25) anayejifanya ni Freemason na amekuwa akifanya ukatili,unyanyasaji wa kijinsia na kupora mali hasa kwa wanawake.

Pia amekuwa akiwatishia wanawake anaowafanyia ukatili kuwa wakitoa taarifa zake atawaua kwa kuwanyonya damu na kuwakata sehemu zao za siri.

 Akizungumza leokukamatwa kwa mtu huyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Februari 25 mwaka huu Polisi walimkata akiwa maeneo ya Mwenge  ambako ndiko anakoishi.

Amesema mtu huyo amekuwa akitumia gari naomba T 172 BLH aina ya Fun Cargo rangi ya Silva ambapo amekuwa akikamata wanawake kwa kuwalaghai kuwa ni mfanyabiashara na wakishaingia kwenye gari lake hutumia nguvu na kuwanyang'anya vitu vilivyomo kwenye mabegi.

Amesema baada ya kunyang'anya mabegi hayo huanza kuwazungusha barabarani huku akiwatisha kuwa yeye ni  Freenason na kuwa atawaua kwa kuwanyonya damu au kukata sehemu zao za siri.

"Kupitia vitisho hivyo huwalazimu wotoe namba za siri za simu zao na kuchukua kadi zao za benki na kuwaibia fedha zao kwenye ATM na baada ya hapo kuwashusha na kuwatelekeza kwenye vichochoro.

"Huyu mtu tumemuhoji anasema kwa sasa ameacha,ukimuangalia sura yake ni ya binadamu lakini ni mnyama wa hali ya juu kabisa.Amefanya mambo mengi ya kishenzi.

" Tunaendelea na taratibu nyingine na baada ya hapo atapelekwa mahakamani ili ajibu tuhuma za makosa ambayo yanamkabili ,Sheria tunataka ichukue mkondo wake,"amesema Kamanda Mambosasa.

Ameongeza kuwa matukio ambayo anatuhumiwa kufanya mtu huyo kwa baadhi yawanawake ambao wametoa taarifa zake hata mnyama ambaye yupo mbugni na  wanyama wezake  hawezi kufanya.

Amesema kuwa iwapo atakuwa na Ukwimwi maana yake atakuwa ameambukiza wanawake wengi na hafai kabisa kwenye jamii.

Mambosasa ametoa rai kwa watu ambao wamefanyiwa ukatili na mtuhumiwa huyo kufika polisi kutoa taarifa."Si mtu mwema hata kidogo ingawa sura yake ni ya kibinadamu,"

SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, msanii wa Filamu na Miss Tanzania mwaka 2006  Wema Sepetu  alimueleza askari polisi kuwa anatumia bangi kama starehe.

Shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, WP 6441 DC Mary (35) ameyaeleza hayo leo Februari 26 mwaka huu alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wafanyakazi wake wawili.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, WP Mary amedai, Februari 4, 2017 alipewa maelekezo na mkuu wake wa kazi OC CID Denis Mujumba kumtoa Wema mahabusu na kwenda nyumbani kwake kufanya upekezi.

Amedai waliondoka  yeye, OC CID Mujumba, Inspekta Wille, Koplo Robert na DC Hassan na kuwa wkiwaa njiani alimuuliza Wema kuhusu tuhuma zinazo mkabili kama anahusika na uuzaji wa dawa za kulevya ama kutumia.

Shahidi huyo alieleza,  Wema alimjibu kuwa yeye hajishughulishi na uuzaji wa dawa za kulevya ila anatumia bangi kama starehe.Alidai kuwa alimuuliza Wema kuwa ni lini ilikuwa mara mwisho kutumia bangi  nakwamba siku hiyo ilikuwa Jumamosi ya Februari 4,mwaka 2017 na Wema alimwambia kuwa  Mara ya mwisho kutumia bangi ilikuwa siku ya Jumatatu.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images