Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUJADILI UPUNGUZAJI WA AJALI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani,  Mkuu  wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu (kulia meza kuu), akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. 
 Mjumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Geoffrey Silanda  akichangia hoja wakati wa wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Wengine ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Hidaya Mohamed(kulia) na Mwakilishi kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Elimboto Mtatulu (kushoto). 
Wajumbe wa kikao kinachojadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara  ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakishiriki  kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


MISS KK KUZINDUA VIDEO YA WANANUNA JUMAMOSI

$
0
0
Na Karama ,Kenyunko,Globu ya jamii

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Latifa Mussa a.k.a Miss KK Jumamosi ya Februari 25, mwaka huu anatarajia kuzindua video yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Wananuna.

Uzinduzi wa video hiyo yenye Mandhari ya tofauti tofauti utafanyika katika kiota cha Pallet Mbezi Beach na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo wa kutoka Wanene entertainment ambao ni moja kati ya wafadhili wa msanii KK.

Katika Video ya Wananuna ambayo inamandhali ya kuvutia hasa ikiwa imeshutiwa jijini Arusha na Dar es Salaam na kufanyiwa editing nchini Afrika Kusini, wananchi watapa fursa ya kuona hata utalii wa ndani.

Msanii KK  aliyekuwa akifanya shughuli zake za mziki nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu amesema, lengo lake kubwa na kufanya muziki nchini ni kuwafanya wanamuziki kutoka Tanzania wana perfoam Afrika Kusini na vilevile kwa Afrika Kusini.

Aidha katika usiku huo kutakuwa na usiku wa black Carpet. " Napenda kuwaambia wasanii wapya wanaochipukia kwenye muziki, watuliee, waache papara kuwa na malengo na wasikubali kuyumbishwa."

 Sherehe za uzinduzi huo zinatatajiwa kuanza SAA Moja usiku na watu wakwanza kufika kuanzia muda huo mpaka saa tatu watapata kuponi za vinywaji za bure na kati yao watapata vocha kutoka kwa mdhamini wake Coast airline kwenda mbuga za wanyama za Ruaha kwa Siku  mbili.
Msanii wa Muziki, Latifa Mussa, mwenye shati nyekundu, akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uzindizi wa video yake inayokwenda kwa jina la wanune inayotarajiwa kuzinduliwa February 24, katika kiota cha Pallet Mbezi beach, pembeni ni Meneja wake, Erikson Kinywele aka DJ Kinywele

Article 3

USAJILI WA TIGO KILI HALF MARATHON 2018 WAANZA

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania leo imetangaza kuanza kwa usajili wa mbio ndefu za Tigo Tigo Kili Half Marathon kupitia namba *149*20#.

Kwa mwaka wa nne mfululizo, Tigo ndio mdhamini mkuu wa mbio za KM 21 za Tigo Kili Half Marathon ambazo zitafanyika tarehe 4 Machi mwaka huu, katika viwanja vya Ushirika,  mjini Moshi. Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa shindano la Tigo Kili Half Marathon 2018  linaunga mkono juhudi za serikali za kuinua viwango vya michezo na kujenga afya bora za Watanzania kupitia ushiriki wao katika michezo.

 “Usajili wa mbio za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Kujisajili, piga simu namba *149*20#, kisha fuata maelekezo rahisi ya kuchagua mbio unazotaka kukimbia na kulipia ada ya usajili kwa mbio husika. Baada ya kutuma ada ya ushiriki, utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utakaokujulisha kuhusu kukamilika kwa muamala wako.  Utunze ujumbe huu mfupi wa maneno na kisha nenda nao pamoja na kitambulisho chako halisi katika kituo utakachojulishwa katika miji ya Dar es Salaam, Arusha na Moshi ili kuchukua namba yako  ya ushiriki,’ Woinde alieleza.

Tigo inatoa jumla ya TZS 11m kama zawadi kwa washindi kumi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanaume na wanawake. Pia kuna medali  na vyeti vya ushiriki kwa watu 4,500 wa kwanza watakaomaliza mbio hizo.

‘Tunachukua fursa hii kuwakaribisha washiriki wote, ikiwemo wanariadha wa kimataifa, wa kitaifa, wapenda michezo na wanafamilia wote kuja kushiriki katika mbio hizi za Tigo Kili Half Marathon, ili waweze kutunza afya zao pamoja na  kufurahia kumbukumbu za matukio yanayoendana na shamrashamra za mashindano,’ Woinde alisema.

Naye Afisa wa Lipa Kwa Tigo Pesa, David Chinguile alisema kuwa Tigo imepanua huduma ya Tigo 4G kufikia miji 22 nchini Tanzania, ikiwemo katika mji wa Moshi na kanda yote ya Kaskazini.  Uwekezaji huu mkubwa utahakikisha kuwa watakaohudhuria Tigo Kili Half Marathon 2018 watapata huduma bora na za uhakika za mtandao wa simu utakaowawezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa, na marafiki pamoja na kutuma picha na video za matukio na kumbukumbu nyingine muhimu kwa kasi ya juu kupitia mtandao wa Tigo 4G.
     
Tigo inajivunia kuwa sehemu ya mbio za Tigo Kili Half Marathon 2018 ambazo zinazidi kujizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni mwaka hadi mwaka.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanza kwa usajili wa mbio za km 21 za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi tarehe 4 Machi ya mwaka huu. Kulia ni Afisa wa Lipa kwa Tigo Pesa, David Chinguile.

WASHIRIKI MAFUNZO YA ULINZI CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI WAFANYA ZIARA MAKAO MAKUU JESHI LA POLISI

$
0
0
 Mkurugenzi mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College –NDC) Tanzania Balozi, Peter Kallaghe akimkabithi zawadi Kamishna wa Utawala, Fedha na Lojistiki, Albart Nyamhanga, leo walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
 Kamishna wa Utawala, Fedha na Lojistiki, Albart Nyamhanga, akimkabithi zawadi Mkurugenzi mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College –NDC) Tanzania, Balozi, Peter Kallaghe leo walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. 
Kamishna wa Jeshi la Polisi wa Utawala, Fedha na Lojistiki Albert Nyamhanga wanne kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya Ulinzi wa Taifa kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College –NDC) Tanzania, walipokuja kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo wakiongozwa na Mkurugenzi mwandamizi wa Chuo hicho  Balozi, Peter Kallaghe wa pili kutoka kushoto. Picha na Jeshi la Polisi.

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA ASKARI WA MKOA WA TANGA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro (kulia) akizungumza na kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana walipokutana katika eneo la Msata Bagamoyo wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro akipokea salamu ya Kijeshi kutoka kwa Mkaguzi wa Polisi, Ali Masumbuko wakati alipowasili katika Kituo cha Polisi wilaya ya Handeni mkoani Tanga leo, akiwa safarini kuelekea mkoa wa Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro (wapili kulia) akizungumza na askari wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati alipowasili katika mkoa huo leo akiwa safarini kuelekea mkoa wa Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, IGP Sirro aliwataka askari hao kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),  Simon Sirro akiweka saini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika kituo cha Polisi wilaya ya Handeni mkoani Tanga leo, akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha. Picha na Jeshi la Polisi.

MICHUZI TV: "NDOTO" NA MCHEKESHAJI MAARUFU WAKUVANGA

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO FEBRUARY 22,2018


NAIBU WAZIRI MADINI AKERWA USIRI WA MAPATO YA MUWEKEZAJI MGODI WA SUNSHINE

$
0
0

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amekerwa na usiri wa mapato na matumizi ya muwekezaji wa mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Mhe Biteko ameonyesha masikitiko makubwa wakati akizungumza na uongozi wa mgodi huo mara baada ya uongozi wa mgodi huo kushindwa kumpatia taarifa ya mapato na matumizi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo kukagua shughuli za uchimbaji Madini.

Kumbukumbu hizo zimekosekana kufuatia viongozi wa ngazi ya juu ya mgodi kutokuwepo kwenye kikao hicho pamoja na kukiri kupokea taarifa ya ujio wake kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.Alisema kuwa viongozi hao kukosekana pamoja na kuwa na taarifa ya muda mrefu juu ya ziara hiyo ni utovu mkubwa na nidhamu kwa serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema kuwa pamoja na kutokuwepo kwao lakini taarifa zilitakiwa kuwepo ofisini kwani ni kosa kisheria kukosekana kwa taarifa za mgodi ilihali sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaeleza vyema kuwa mmiliki wa leseni ya Madini anatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi kwa miaka mitano.

"Endapo atashindwa kufanya hivyo serikali itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo cha mwaka mmoja jela ama faini ya shilingi Milioni 50 mpaka milioni 150" Alisema Naibu Waziri huyo.Mhe Biteko akizungumza huku akionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika eneo la ofisi ya mgodi huo huku wakishindwa kuhudhuria katika kikao hicho cha kazi alisisitiza kuwa muwekezaji wa mgodi huo anapaswa kuzingatia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi.

Sambamba na hayo pia Mhe Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kutoa taarifa sahihi za uwepo wa mashapu katika mgodi waliyokuwa wakichimba au kama mashapu katika mgodi huo yameisha wafuate taratibu za kisheria za ufungaji wa mgodi ikiwemo kuyarudisha mazingira katika halo take ya kawaida.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na mmoja wa kiongozi wa Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.

RC KILIMANJARO AKAGUA UTENDAJI KAZI WA TANESCO MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka, pembeni ni Mhandisi mkuu wa mkoa Bagabuje Joseph, Mkuu wa wilaya ya Moshi Mh. Kippi Warioba na Meneja wa Tanesco Himo, Bw, Mohamed Kayanda.
Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yared Ngalaba akifafanua kwa Mkuu wa mkoa Mh Anna Mghwira mifumo ya usafirishaji umeme mkoani Kilimanjaro.
Kutoka kushoto Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yaredi Ngalaba, Mhandisi mkuu Bagabuje Joseph, Afisa uhusiano Tanesco Kilimanjaro Bw. Samuel Mandari na Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira.
Msimamizi wa kituo cha kupoza umeme cha Kiyungi Joseph Mwisongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa Mh Anna Mghwira.


- KATIKA ZIARA HIYO AMETEMBELEA VITUO VYA KUPOOZA UMEME (SUBSTATIONS) ZA KIYUNGI, TRADE SCHOOL, BOMA MBUZI NA KIA.

Mkuu wa Mkoa Amewataka watumishi wa TANESCO kuendelea Kutekeleza majukumu yao  kwa bidii ili kuhakikisha huduma ya umeme inakuwepo muda wote na ameahidi kuwaunga mkono katika ulinzi wa miundombinu ya umeme mkoani hapa.

Nae meneja wa TANESCO Kilimanjaro mhandisi MAHAWA MKAKA amemuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwepo kwa umeme wa kutosha kwa wawekezaji wa viwanda Mkoani Kilimanjaro.

Katika Ziara hiyo Mkuu wa mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na wakuu wa wilaya za Moshi na Hai pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoa na Wilaya.

RC MAKONDA ATEMBELEA SHULE ZILIZOONGOZA KWA UANDIKISHAJI MKUBWA WA WANAFUNZI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amefanya Ziara kwenye Shule ya Msingi Mbande na Maji Matitu zilizopo Manispaa ya Temeke ambazo zimeongoza kwa kuandikisha idadi kubwa ya Wanafunzi wa Darasa la Kwanza kuliko shule yoyote Tanzania na kusababisha mlundikano mkubwa wa Wanafunzi Darasani.

Kwa Shule ya Msingi Mbande imeandikisha zaidi ya Wanafunzi 1,130 na kusababisha upungufu wa Vyumba vya Madarasa 115 na Matundu ya Vyoo 270 na Madawati 308 huku shule ya Msingi Maji Matitu nayo ikiandikisha zaidi ya Wanafunzi 976 hali iliyosababisha baadhi ya Wanafunzi kukaa kwenye Sakafu, Chini ya miti na Msongamano mkubwa Madarasani.

Hali hiyo imemfanya RC Makonda kufika kwenye shule hizo ili kujua mpango wa Manispaa katika kutatua changamoto hiyo iliyosababishwa na nia njema ya wazazi kuitikia wito wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ya kutoa elimu Bure.

Kama ilivyo kawaida ya RC Makonda kutafuta majibu kwenye Changamoto, amesema serikali inaanza Mara moja ujenzi wa shule tatu Mpya ambapo Shule mbili zitajengwa Maji Matitu na Moja Mbande.

Aidha RC Makonda amesema makadirio ya uandikishwaji wa wanafunzi wapya darasa la kwanza kwa Wilaya ya Temeke ilikuwa wanafunzi 7,800 lakini idadi imepanda hadi kufikia Wanafunzi 28,824 na idadi inazidi kuongezeka kila kukicha huku Mkoa ukiwa na malengo ya kuandikisha wanafunzi 78,000 lakini hadi sasa wamefanikiwa kuandikisha Wanafunzi 86,000.

RC Makonda amesema mwitikio huo wa wananchi kwenye elimu ni faida kubwa kwakuwa ndio ukombozi wa familia maskini hivyo amewasihi wananchi kuchangamkia fursa ya iliyotolewa na Rais Magufuli ya Elimu Bure.

Hata hivyo RC Makonda amewahimiza Wananchi kuunga mkono ujenzi wa shule hizo tatu mpya kwa kujitolea vifaa mbalimbali kama Saruji, Mchanga, Nondo, Kokoto, Mabati, Rangi, Mbao na nguvu kazi ya Watu ili wanafunzi wasome katika mazingira bora. 

Kwa upande wake kaimu afisa elimu ya msingi manispaa ya Temeke Bi. Sylvia Mtasingwa amesema licha ya shule ya Mbande kuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi imeendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani.

UKITAKA KUMKOMBOA MTOTO WA FAMILIA MASKINI MPATIE ELIMU, KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU DAR ES SALAAM.

JAJI MKUU AWATAKA MAHAKIMU KUSIMAMIA MABARAZA YA KATA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nzega alipowasili kukagua shughuli za Mahakama. Jaji Mkuu ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora na Kigoma ambayo ni Kanda ya Tabora.
Na Lydia Churi-Tabora

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo nchini kusimamia mabaraza ya kata yaliyoanzishwa kwa Shjeria yam waka 1985 kwa kuwa mabaraza hayo ni sehemu muhimu katika mfumo wa utoaji haki kutokana na kazi yake ya kusuluhisha na kupatanisha mashauri madogo madogo ya jinai na madai.

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga na Nzega pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Ziba na Nyasa mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata unawaunganisha wananchi tofauti na pale kesi inaposikilizwa Mahakamani ambapo mar azote aliyeshindwa hujenga uadui na aliyeshinda.

Jaji Mkuu amesema endapo mabaraza ya Kata yatasimamiwa ipasavyo ni wazi kuwa idadi ya kesi zinazofunguliwa kwenye Mahakama za Mwanzo nchini itapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa kesi nyingi zitaamuliwa kwenye mabaraza hayo kwa njia ya usuluhishi na upatanishi. Aliongeza kuwa kesi zote zinazosajiliwa nchini asilimia 74 ni za Mahakama za Mwanzo.

Amesema ili kuimarisha mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata, Mahakama ya Tanzania imeandaa mpango wa mafunzo utakaowakutanisha Mahakimu pamoja na wajumbe wa mabaraza ya kata.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngulupa akimpokea Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma alipowasili ofisini kwake Nzega.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Mkuu wa wilaya kitabu kinachoelezea Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Jarida la Mahakama alipofika ofisini kwake kumtembelea .

MAKAMU WA RAIS APOKEA MISAADA KUTOKA UBALOZI WA CHINA KWA AJILI YA MAENDELEO MKOANI SIMIYU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 178,488,00/- kutoka kwa Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Nkoma iliyopo Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Vyerehani 50 kwa ajili halmashauri ya mji wa Bariadi ili kuanzisha Kiwanda cha Ushonaji.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA JUMUIYA YA HIFADHI WANYAMAPORI WAMIMBIKI IPANDISHWE HADHI KUWA PORI LA AKIBA

$
0
0


Na Hamza Temba - WMU-Bagamoyo, Pwani
....................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.


Ametoa agizo hilo leo mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani yake pia kuna mapito ya wanyamapori.


Dk. Kigwangalla amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa jumuiya hiyo ikiwemo tuhuma walinzi wake kutoka katika vijiji vinavyounda jumuiya kujihusisha na vitendo vya ujangili. Hata hivyo alipokea ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Omari Tofiki ambaye aliiomba Serikali ichukue jukumu la kulinda hifadhi hiyo kwa asilimia 100.


"Sisi kama jamii tumeshindwa, tunaomba msaada wa Serikali, itusaidie kuondoa hawa wavamizi na ikiwezekana ichukue jukumu la kulinda hifadhi hii kwa asilimia 100," alisema Tofiki.


Alisema jumuiya hiyo ambayo ni muunganiko wa vijiji 24 inakabiliwa na changomoto kubwa ya ujangili uliokithiri ambao umepelekea kuuwawa kwa wanyamapori zaidi ya asilimia 90 ya waliokuwepo tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 1997.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Dunia inawaangusha watoto wachanga - UNICEF

$
0
0
Duniani kote, vifo vya watoto wachanga bado viko juu sana kiasi cha kuwa tishio, hasa miongoni mwa nchi maskini zaidi ulimwenguni, UNICEF imesema katika ripoti yake mpya kuhusu vifo vya watoto iliyozinduliwa leo mjini New York. Ripoti hiyo imebainisha kuwa watoto wanaozaliwa katika nchi za Japani, Iceland na Singapore wana nafasi kubwa zaidi ya kuishi, wakati wale wanaozaliwa katika nchi za Pakistani, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Afghanistani wanakabiliana na hatma mbaya kabisa ya maisha yao.

 “Wakati ambapo tumepunguza kwa zaidi ya nusu idadi ya vifo miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano katika robo karne iliyopita, bado hatujafaulu kwa kiwango kama hicho katika kukomesha vifo miongoni mwa watoto walio na umri wa chini ya mwezi mmoja,” alisema Henrietta H. Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF. 

“Kwa kuwa vifo hivi vingi vinazuilika, ni wazi kwamba, tumewaangusha watoto walio maskini zaidi duniani,” alisisitiza mkurugenzi huyo wa UNICEF. Ulimwenguni, katika nchi za kipato cha chini, wastani wa vifo vya watoto wachanga ni vifo 27 katika kila vizazi hai 1,000, ripoti inasema. Katika nchi za kipato cha juu, kiwango ni vifo 3 kwa kila vizazi hai 1,000. Nchini Tanzania, viwango vya vifo vya watoto wachanga ni 25 katika kila vizazi hai 1,000, kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya wa Tanzania (TDHS 2015-16). 

Ikiwa kila nchi itapunguza viwango vya vifo vya watoto wake wachanga hadi katika viwango vya nchi za kipato cha juu ifikapo mwaka 2030, maisha ya watoto milioni 16 yataokolewa, ripoti hiyo imebainisha. Ripoti hiyo inaeleza pia kwamba miongoni mwa maeneo 8 kati ya 10 yaliyo hatari zaidi kwa mtu kuzaliwa, basi Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, ni mojawapo, ambapo wanawake wajawazito wana uwezekano mdogo wa kupata msaada wakati wa kujifungua kwa sababu ya umaskini, migogoro na taasisi zisizo na ufanisi. Watoto wanaozaliwa katika nchi zenye hatari zaidi wana uwezekano wa hadi mara 50 wa kufa kulinganisha na wale wanaozaliwa katika nchi zilizo salama. 


DED MNASI AKAGUA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA ILEJE

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Ileje 

HALMASHAURI ya wilaya ya Ileje mkoani songwe imetumia zaidi ya shilingi milioni mia moja themanini katika ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za EPFR ambazo hutolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukagua miradi hiyo,mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi alisema kuwa jukumu la uongozi ni kuhakikisha kuwa pesa inayotolewa na serikali inatumika kama ilivyokusudiwa na serikali kuu kwa faida ya sekta ya elimu.

“Serikali inatoa pesa nyingi sana hivyo tusipo simamia vizuri pesa hizi zitapotea kitu ambacho Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli hataki kabisa kusikia kuna pesa ambayo haitumiki kama ilivyokusudiwa ndio maana nimeamua kuanza kukagua miradi yote ambayo inatekelezwa katika halmashauri yetu” alisema Mnasi 

Mnasi aliwaomba wananchi kuchangia nguvu zao kuhakikisha shughuli za ujenzi wa madarasa na vituo vya afya wanajitolea vilivyo ili kuendelea kufanya kazi sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano.“Mimi binafsi nawaomba wananchi wajitolee kufyatua tofali ,kuchota maji,kubeba mchanga na kusomba tofali ambazo zinakuwa zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya ujenzi ambao utakuwa na faida kwao na vizazi vijavyo” alisema Mnasi
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu na kuhakikisha wananchi wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu 
 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akibadilisha mawazo na baadhi ya viongozi walikuwa kwenye eneo la ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu.

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI(NDC) WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe(kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt Juma Malewa walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Februari 21, 2018(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt Juma Malewa akifanya mazungumzo mafupi na Maafisa Wakufunzi(hawapo pichani)kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Magereza leo Februari 21, 2018.
Maafisa Wakufunzi toka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza kabla ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kushoto) ni Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakiangalia meza iliyotengenezwa katika Kiwanda cha Uselemala cha Gereza Kuu Ukonga katika ziara yao ya mafunzo katika Jeshi la Magereza.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(kulia) akipokea zawadi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza kutoka kwa Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe(kushoto).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

INTRODUCING DASHIE - TULIA OFFICIAL AUDIO

MICHUZI TV: WAFANYABIASHARA WA PAMBA KUNUFAIKA NA MIKOPO YA BENKI

YANGA FC, TOWNSHIP ROLLERS YA BOTSWANA KUKUTANA

$
0
0
Na Agnes Francis, Blogu ya Jamii. 

MABINGWA watetezi  Tanzania Bara Yanga SC wamefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika ambapo watakutana na  Township Rollers kutoka nchini Botswana.

Ambapo mchezo huo utapigwa  katika Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam  kabla ya marudiano huko kwao. 

Hatua hiyo ni baada ya kulazimisha sare  ya bao 1-1 dhiidi ya St Louis  ya  Shelisheli Katika mchezo  wa marudiano uliopigwa katika  dimba la Stade Linite  kisiwani hapo. 

Ibrahimu Ajibu ndiye aliyeipatia timu ya Yanga SC  bao la kuongoza dakika ya 45+ baada ya kupokea pasi mujarabu kutoka kwa Hassan Kessy upande wa kulia na kuwainua kwa shangwe mashabiki na wapenzi wa timu hiyo, hata hivyo Bernard Esther  aliisawazishia timu yake dakika ya 93.

Mabingwa hao wa soka Tanzania Bara wamefuzu kwa ushindi wa  jumla ya mabao 2-1 ambapo walishinda bao 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliorindima Uwanja  wa Taifa Jijini Dar es salaam. 

Endapo Yanga SC itafanikiwa kumtoa mpinzani wake Township Rollers ya kutoka huko Nchini Botwasana itainga hatua ya makundi, lakini kama itashindwa basi itacheza raundi ya pili michuano ya shirikisho inayoshiriki klabu  ya wekundu wa Msimbazi SimbaSc.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images