Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110152 articles
Browse latest View live

Article 4


KUMBU KUMBU YA BALOZI FULGENCE KAZAURA

DCC LUSHOTO YASITISHA MPANGO WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI

$
0
0
Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC) imeamua kusitisha mpango wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lilokuwa lijengwe kwenye eneo jipya la Kwehangala hadi hapo suluhu ya mgogoro baina ya viongozi wa halmashauri hiyo itakapopatikana. 

Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika (Pichani Juu) alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuwepo sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu ya suala hilo. .

Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao juu ya wapi pajengwe majango ya makao makuu ya Halmashauri hiyo. Baadhi ya viongozi wanadai utaratibu wa fedha za manunuzi haukufuatwa katika kufikia maamuzi ya kujenga jengo la Halmashauri katika eneo la Kwehangala na kuacha majengo yaliyokwisha jengwa Bumbuli kwa gharama ya Sh. milioni 700.

Kutokana na mvutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kikao kiliafiki kisitishe zoezi hilo mpaka maelewano yatakapopatikana." Wajumbe wameshauri suala la kuhamisha makao makuu lisitishwe hadi hapo utakapopatikana utangamano,kwani tayari imeonekana kuna mgogoro ambao umeleta utengano kwa viongozi" Alisema Lugangika .

DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BODI YA UTALII (TTB)

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utaliii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Februari 20, 2018, amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu zaidi.

Akizungumza na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha mbalimbali za Kimataifa.


Aidha,amewataka kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA).


Hata hivyo amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara.


Pamoja na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo.


Akiwa katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kupata maelezo machache kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

$
0
0
JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.

Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. 

Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.

MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO

$
0
0
NA  YEREMIAS  NGERANGERA
Upepo  mkali ulioambatana na mvua umeleta tafrani katika kijiji cha Njalamatata kata ya Mkongo Nakawale wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma .

Tafrani  hiyo ilitokea siku ya  jumatatu  wiki hii  baada ya nyumba tano kuezuliwa na upepo na wananchi waliokumbwa na dhahama hiyo kubaki wakitafuta makadhi  ya kujihifadhi kwa majirani.

Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana Adelin Nchimbi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama  walifika eneo la tukio na kuongea na  waathirika wa tukio la kuezuliwa nyumba katika  kijiji cha Njalamatata.

Aidha bwana Nchimbi alisema kuwa katika tukio hilo Nyumba tano ziliezuliwa na  upepo  lakini   hapakujitokeza  mwananchi yoyote kujeruhiwa au kuwepo kwa  maafa katika tukio hilo.

Alitaja majina ya wananchi walioathirika katika tukio hilo ni  Clavery Ponera ,Donatus Kapinga,James Mdagi ,Sadiki Kapinga ,Rusti  Kimbili na Lotary Hongo wote ni wakazi wa kijiji hicho cha Njalamatata wilayani humo.
 Kamati  ya ulinzi na usalama  ya wilaya ya Namtumbo pamoja  na kutoa pole kwa waathirika wa tukio hilo ilifanya mahojiano na waathirika kubaini hasara iliyopatikana  kutokana na tukio hilo.
Kamati ya ulinzi  na usalama ya wilaya ya Namtumbo pamoja na pole hizo iliwashauri wananchi wa kijiji hicho kujenga nyumba na kuziezeka kwa kuweka tengo za kushikizia kwenye ukuta baada ya kubaini baadhi ya nyumba hazikuwekwa tengo hizo.

WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.


Pia Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.

Alizindua kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

“Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na kuuza.”

Pia aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga aliishukuru Serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.

Bw. Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha, aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.


RAIS MAGUFULI AWASILI UGANDA, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVEN

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake katika Mazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI

$
0
0
Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya katavi na kigoma.

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati aliposimamishwa na wakazi wa kijiji cha Tura, wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, alipokuwa akikagua kambi ya mkandarasi na kuangalia hatua za awali za matayarisho ya ujenzi wa barabara hiyo.

Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 117.9 na utachukua miezi 24 mpaka kukamilika kwake."Serikali imeanza rasmi ujenzi wa barabara hii na sasa ni jukumu lenu kuhakikisha mnampa ushirikiano mkandarasi huyu ili mradi uwahi kukamilika mapema", amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani. Ameongeza kuwa sasa Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka daraja la Kikwete mpaka Uvinza, mkoani Kigoma na hivyo itasaidia wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi kutoka mkoa wa Dar es Salaam mpaka mikoa ya katavi na Kigoma kupita kwenye lami njia nzima.
Mkandarasi kutoka kampuni ya CHICO kutoka China, Bw. li, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiwaonesha Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi na Mbunge wa Jimbo la Igalula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami itajengwa, mkoani Tabora.
Tingatinga likikata miti kwa ajili ya kusafisha eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami utaanza, mkoani Tabora. 



WAZIRI MKUU AKUTANA NA WADAU WA PAMBA JIJINI MWANZA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara  Wenye Viwanda  (TCCIA) mkoa wa Mwanza, Christopher Mwita Gachuma wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza  kuongoza kikao cha wadau wa zao la pamba alichokiitisha, Februari 21, 2018.Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula na kushoto ni Mbinge wa Sumve, Richard Ndassa.
 Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la pamba ulioitishwa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Februari 21, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 21, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Februari 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


MKUTANO WA MAKAMU WA RAIS MWANDOYA JIMBO LA KISESA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mwandoya jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa amewataka Viongozi wa mkoa na wilaya mkoani Simiyu kusimamia sheria na kutowafumbia macho wanaowapa mimba wanafunzi.

Akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwandoya Kisesa, wilayani Meatu.

Makamu wa Rais alisema “Jamani mnadhulumu watoto wetu hapa kuna kina Samia wa baadae mnapokuja kuwapa ujauzito mapema mkawavunjia safari zao, mkawaoa mapema, wakina Samia hawataibuka Meatu, tutatoka huko nje tutaibuka hapa Meatu, tunataka Samia atoke hapa Meatu waachieni wasome, masuala ya mimba za utotoni wapunguzieni.”

Makamu wa Rais aliwahimiza wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye mifuko ya bima ya afya kwani inafaida kubwa sana.“Magonjwa yaweza kukufika wakati huna pesa na kitu pekee kitakachokusaidia ni bima yako ya afya hivyo wananchi hakikisheni mnapovuna na kuuza mazao yenu mnapata bima ya afya”

Makamu wa Rais aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Meatu kwa kulima pamba kwa wingi ambapo wilaya hiyo inategemea kilo 84 na kuwaahidi wananchi hao kuwa dawa za kuulia wadudu zitapatikana kwa wingi kuanzia mwisho wa mwezi huu kwani serikali imetoa fedha zaidi ya bilioni 9 .

Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa barabara zote ambazo ilani ya uchaguzi imeahidi kuzijenga zitajengwa na zile ambazo hazipo kwenye ilani ila zina umuhimu zitaingizwa kwenye bajeti ijayo.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luaga Mpina alisema kuwa kati ya kata 13 ni vijiji vine tu vina maji hivyo alimuomba Waziri wa Maji kusaidia zaidi upatikanaji wa maji.Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe aliahidi kusimamia kwa ukamilifu upatikanaji wa maji .

Benki ya CRDB yazindua TemboCard Credit cards

$
0
0
Benki ya CRDB kwa kushirikiana MasterCard International leo wamezindua rasmi kadi mbili zenye mfumo wa “Credit-Card” zijulikanazo kama “TemboCard World Rewards na TemboCard Gold Credit-Card, katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya Benki hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema kadi hizo zenye mfumo wa “Credit-Card” ni za kwanza kuingizwa sokoni na Benki ya CRDB. “Credit-Card ni mfumo maalum wa kadi za kibenki ambapo mteja anaweza kutumia kadi yake kufanya manunuzi au malipo kwa kiwango cha fedha zaidi ya zile alizonazo kwenye akaunti yake” alisema Dkt. Kimei.

Akizungumzia juu ya faida ya kadi hizo Dkt. Kimei alisema zinamuongezea mteja uwezo wa kufanya manunuzi pasipo kuwa na wasiwasi wakutokuwa na fedha za kutosha katika akaunti yake. “Kadi hizi zitamuwezesha mteja kupata mkopo wa muda mfupi na hivyo kumuwezesha kutimiza malengo yake” alisema Dkt. Kimei Dkt. Kimei alisema TemboCard World Rewards ni maalum kwa ajili ya wateja wakubwa, ambapo mteja atapata mkopo wa hadi shilingi milioni 50, huku muda wa kurudisha mkopo ukifika hadi siku 50. TemboCard Gold Credit Card yenyewe ni maalum kwa ajili ya wateja wa kati na wajasiriamali, ambapo mkopo wao unaenda hadi shilingi milioni 20, na muda wa kurudisha mkopo ukiwa ni siku 45.

“Mbali ya kuwa kadi hizi zinawapa wateja wigo mpana wakufanya manunuzi, wateja pia watakuwa wakinufaika na punguzo la bei katika maduka, hoteli, migahawa na sehemu mbalimbali duniani endapo watafanya malipo kupitia kadi zao, bima ya safari na bidhaa watakazonunua kupitia kadi zao pamoja na fursa ya kutumia zaidi ya kumbi za VIP katika viwanja mbalimbali vya ndege duniani kote” alisema Dkt. Kimei.

Akizungumzia namna ambavyo kadi hizo zitakwenda kusaidia kukuza uchumi wa nchi Dkt. Kimei alisema Credit card zinawezesha watu kufanya malipo ya manunuzi ambayo pengine wasingeweza kumudu kwa wakati huo hivyo kupelekea biashara kuzalisha mapato ambayo kiuhalisia wasingeweza kuyapata, jambo ambalo hupelekea kukua kwa mzunguuko wa fedha na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Dkt. Kimei alihitimisha hafla hiyo kwa kuwakaribisha wateja wa Benki ya CRDB na watanzania kwa ujumla kutembelea matawi yaliypo karibu yao ilikujaza fomu za maombi ya kupata kadi hizo za “TemboCard World Rewards na TemboCard Gold Credit-Card. “Fomu za maombi pia zinapatikana kupitia website ya Benki, tunawakaribisha hata wale ambao sio wateja bado, tutawafungulia akaunti na kuwapa kadi hizi”, alisema Dkt. Kimei.

Benki ya CRDB ndio Benki ya kwanza kuingiza sokoni kadi yake ya malipo iliyopewa jina la “TemboCard” ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuwapa wateja wa Benki hiyo uhuru wa kupata huduma kwa muda na mahali wanapotaka. Tokea ilipoingia sokoni TemboCard imepata umaarufu mkubwa hasa baada ya kuungana na makampuni makubwa yanayotoa huduma za kadi ya Visa, MasterCard na China Union na hivyo kuunda TemboCardVisa, TemboCard MasterCard na hivi karibuni TemboCard China Union Pay.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi mpya (TemboCard Word Rewards na TemboCard Gold Credit) uliofanyika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam, Februari 21, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB Tully Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akionyesha kadi mpya za TemboCard World Reward na Tcembocard Gold Credit zilizozinduliwa leo hii (February 21, 2018) makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA

$
0
0
*Baadhi ya matumizi hayatawezekana kwasababu za kisheria

Na Said Mwishehe,Globu wa Jamii

SERIKALI imesema imepokea bajeti ya gharama ya mazishi ya aliyekuwa Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Usafirishaji (NIT) Aqwilina Akwiline(pichani enzi za uhai wake) ya Sh 80,150,000 kutoka kwa familia huku ikieleza baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwani kisheria hayagharamiwi na Serikali.

Pia imesema kwenye makisio hayo kuna gharama zilizokuwa zimepewa makadirio ya juu.Hivyo Serikali kupitia Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia jana jioni imekaa na familia ili kuondoa changamoto hiyo na hatimaye kupata bajeti ya pamoja.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mwasu Sware imesema Wizara hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu wake  Dk.Leonard Akwilapo ilipokea makisio ya gharama za mazishi kiasi hayo kutoka kwa Msemaji wa familia hiyo Festo Kavishe. 

"Kumekuwepo na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha makisio ya gharama za mazishi ya Aqwilina Akwiline. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaufahamisha umma kuwa bajeti hiyo inayosambaa kwenye mitandao ni makadirio yaliyoandaliwa na familia ya marehemu.

"Baada ya kupokea makisio hayo Katibu Mkuu Dk.Akwilapo alitahadharidha kuna baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwa kuwa kisheria hayagharamiwi na Serikali .Pia katika makisio hayo kuna gharama ambazo zilikuwa na makadirio ya juu,"amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo Dk.Akwilapo aliagiza kuwe na kikao kati ya Wizara na ndugu wa marehemu ili kuweka sawa changamoto hizo ili kuwa na bajeti ya pamoja.Hivyo kikao kilifanyika jana jioni na kufikia muafaka."Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa taratibu nyingine za 
mazishi zinaendelea vizuri,"amesema Sware.

JALADA KESI YA MHASIBU TAKUKURU ANAYEDAIWA KUMILIKI MALI ZA BILIONI 3/-BADO LIPO KWA DPP

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

JALADA la kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh.bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake, bado lipo mikononi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi.

Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Thomas Simba wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Awali, jalada hilo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kulirejesha TAKUKURU na kuelekeza baadhi ya maeneo yafanyiwe uchunguzi zaidi na kisha kurudishwa kwa DPP.

Alidai maeneo hayo yamekwishafanyiwa kazi na jalada limerejeshwa tena kwa DPP kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi.Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Alex Mgongolwa alidai kesi hiyo imekuwa ya muda mrefu na kila siku wanaambiwa upelelezi haujakamilika na jalada lipo kwa DPP.

" Tunaomba tarehe ijayo upande wa mashtaka watueleze wamefikia wapi upelelezi, ili kesi hii iweze kuendelea na hatua nyingine, kwa sababu wateja wangu gerezani.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili kesi hiyo iendelee na hatua nyingine.

Hakimu Simba alisema " Katika kesi hii sitakuwa na utani , nataka kesi hii itakaporudi, upande wa mashtaka mje na maelezo ya kujitosheleza" alisema na kuongeza kuwa " Sitaki kesi hii ichukue muda mrefu, nataka upande wa mashtaka mhakikishe upelelezi unakamilika kwa haraka, maana upelelezi usipokamilika haraka, jamii inachukulia kuwa mahakama ndio inachelewesha kesi," amesema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 6, mwaka 2018, Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera. Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

MASAUNI AONGOZA KIKAO BARAZA LA TAIFA USALAMA BARABARANI KUJADILI UPUNGUZAJI WA AJALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu (kulia meza kuu), akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mjumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Geoffrey Silanda, akichangia hoja wakati wa wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Wengine ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Hidaya Mohamed na Mwakilishi kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Elimboto Mtatulu (kushoto).
Wajumbe wa kikao kinachojadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakishiriki kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

UHAMIAJI YAWASHIKILIA WATANZANIA TISA KWA KUKWAMISHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIU

$
0
0
Na Leandra Gabriel,Globu ya Jamii

IDARA ya Uhamiaji nchini inawashikilia watanzania 9, ambao ni  wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) jijini Dar  es Saalam kwa madai ya kuzuia maofisa wa idara yao kutofanya kazi yao walipofika chuoni hapo.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa  Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda amesema watu hao tisa wamekamatwa  jana kwa tuhuma za kuzuia maofisa wa idara hiyo wasitimize  majukumu yao na kwa sasa wanawahoji. 

"Watu hao baada ya maofisa wetu jana kufika pale KIU waliamua kuwazuia kwa kufunga milango ili tusipate nafasi ya kufanya kile ambacho kimetupeleka,"amesema.

Hivyo kukamatwa kwa watu hao kunafanya idadi ya wanaowashikiliwa na Idara ya Uhamiaji kufikia 48."Idara ya Uhamiaji inaendelea kuwahoji na kati ya hao wanaoshikiliwa wapo raia wa Nigeria watano, raia wa Congo mmoja, raia wa Uganda 30, raia wa Kenya 3 pamoja na hao raia wa Tanzania 9,"amesema.

Amefafanua Idara ya Uhamiaji itaendelea kukagua vyuo mbalimbali  nchini kwani ni agizo la Wizara ya Elimu, Sayansi na  Teknolojia. Alipoulizwa kwanini wameanza na KIU amejibu huo ni  mwanzo tu kwani watapita kwenye maeneo mbalimbali.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

$
0
0
JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.
Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. 

Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.

Alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. 

Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo.

Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na juhudi za Serikali katika mapambado dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na fedha za umma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Anthony Bahebe akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kuapamba na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) jijini Mwanza Februari 21, 2018 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA ELIMU YA JUU NA UCHUMI WA VIWANDA SIMIYU

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kushirikiana na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Alliance, Bariadi mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,  Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi na Viwanda lililofanyika Bariadi mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO akutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo

$
0
0
Na Koleta Njelekela, STAMICO
Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Mhandisi John Nayopa amekutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambaye alifika katika Ofisi za Makao Makuu ya STAMICO jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana naye na kuzungumzia namna ya kuimarisha ushirikianao katika upashanaji habari za STAMICO kwa Watanzania.
Viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika suala zima la kuelimisha Watanzania kuhusu shughuli za STAMICO kwa kutumia mitandao ya kijaamii (Social Media) ya Idara ya Habari Maelezo,  Jarida la Nchi yetu linaloratibiwa na Idara hiyo na Vyombo vya Habari kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dakta Abbasi amesema Idara yake iko tayari kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa STAMICO katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji yao, ili kuwajengea uwezo zaidi katika taaluma zao.

“ Kulingana na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Idara yangu inaweza kutoa mafunzo ya kuanzia kwa wataalamu wako kuhusu Sayansi ya Mitandao ya Kijamii na uendeshaji wake; Mawasiliano kwa Umma wakati wa Majanga (Crisis Communication); pamoja na Sera na Miongozo ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii” Alifafanua Dk. Abbasi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Nayopa amemshukuru Dakta. Abbasi kwa kumtembelea ofisini kwake na ameahidi kuimarisha ushirikiano na Idara ya Habari Maelezo katika kuelimisha Watanzania kuhusu mchango wa STAMICO katika kuleta matokeo chanya kwenye Serikali ya awamu ya tano.
 Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Mhandisi John Nayopa akipata maelezo  kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, kuhusu majukumu ya  Idara ya Habari Maelezo na Mfumo wa Upashanaji Habari na Mawasiliano Serikalini ofisini kwake jijini Dar es Salaam .
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi (kushoto) akikabidhi Jarida la Nchi Yetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisni kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Jarida hilo linaratibiwa na Idara ya Habari Maelezo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dakta Hassan Abbasi (kushoto) akitoa maelezo kwa ufupi kuhusu Jarida la Nchi Yetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisni kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. 

Yanga, StLous nani kuibuka mbabe leo?

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii 

MABINGWA watetezi Tanzania Bara  Yanga SC wanashuka dimbani Stade Linite kufuana na mabingwa wa  Shelisheli St Lous kwenye Michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika. 

Mtanange huo utakaopigwa  saa za Afrika Mashariki 10  jioni ambapo ni mchezo  wa marudiao baada ya kushinda bado 1-0  wiki iliyopita katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. 

"Tumejipanga vema kushinda mchezo wa leo nimewapanga vijana kuwa makini dakika zote 90,lakini nimewaambia kuwa makini na dakika 20 za mwanzo tutajitahidi kushinda na kumiliki mpira",amesema Lwandamina. 

Aidha wachezaji watakaoukosa mchezo huo wachezaji wake mahiri Obrey Chirwa ambaye aliumia goti katika mchezo wao uliopita dhidi ya MajimajiFc, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Yohana  Nkomola pamoja na Hamisi Tabwe ambao wanaendelea na mazoezi binafsi baada ya kupona majeraha.
Viewing all 110152 articles
Browse latest View live




Latest Images