Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

DKT. MOLLEL ASHINDA UBUNGE SIHA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia mgombea wake Dkt Godwin Mollel kimeshinda kiti cha ubunge katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 sawa na asilimia 80 akimshinda mpinzani wake Elvis Mosi (Chadema) aliyepata kura 5,905 sawa na asilimia 18.5.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Cheti cha uthibitisho kwa kuchaguliwa kwake,Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Valerian Juwal amesema mgombea Tumsifueli Mwanry (CUF)  amepata kura 274 sawa na asilimia 0.9 huku mgombea wake chama cha Sauti ya Umma (SAU) akipata kura 170 sawa na asilimia 0.6.  
 Dkt Godwin Mollel  akikabidhiwa cheti cha uthibitisho kwa kuchaguliwa kwake na Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Valerian Juwal 

  Dkt Godwin Mollel akifurahia pamoja na watu aliombatana kushuhutia tukio hilo

WAZIRI JAFO ABAINI KUWEPO WANAFUNZI 472,WALIMU SHULE SEKONDARI MAKULUNGE WILAYANI KISARAWE KUKABILIWA NA TATIZO LA VYOO

$
0
0

VICTOR MASANGU, KISARAWE 

WANAFUNZI wapatao 472 na walimu zaidi ya 25 katika shule ya sekondari Makulunge iliyopo katika kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa sasa wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo UTI,na kipindu pindu kutokana na vyoo ambavyo wanavitumia kwa sasa vipo katika mazingira hatarishi na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo wakati mwingine inawalazimu kwenda kujisaidia katika maeneo mengine.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ambayo imefanyika katika kata ya Kiluvya na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambapo baada ya kutembelea shule hiyo ya sekondari ameweza kubaini kuwepo kwa mapungufu makubwa ya walimu wa shule hiyo kutokuwa na choo chao hivyo kuchangia na wanafunzi wao.

Wakizungumza kwa masikitiko wanafunzi hao akiwemo Waziri Mwinjuma na Zuwena Mohamed wamebainisha kwamba kwa sasa wanapata shida kubwa sana kutokana na kuwepo kwa mazingira magumu ya miundombinu ya vyoo na kwamba kunahatarisha usalama wa afya zao kutoka na kukithiri kwa uchafu pamoja na miundimbinu kuwa mibovu na baadhi ya vyoo hazina milango na sehemu za ukuta zimeanza kubomoka.

Walisema kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya wanafunzi wengine hususan wa kike wanapata ugonjwa wa UTI kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na matundu ya vyoo yaliyopo hivyo wakati mwingine wanafunzi kujisaidia sehemu ambayo sio salama kabisa.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Makulunge iliyopo kata ya kiluvuya katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea shule na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziaara yake ya kikazi aliyoifanya katika kaata ya Kiluvya kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Mmoja wa walimu wa shule ya sekondari Makuunge Ester Matemu akizungumza kuhusiana na changamoto ambayo ianwakabili ya ukosefu wa vyoo,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

TOHARA MBADALA SULUHISHO LA UKEKETAJI HAPA NCHINI - Dkt. Faustine Ndugulile

$
0
0
Ngariba wa Jamii ya Wamasai wameteketeza vifaa vyote vyote vya kufanyia tohara baada ya Shirika la Kimataifa la AMREF kutoa elimu ya tohara mbadala inayowawezesha Wamasai kuendelea na mira zao bila kufanya tohara kama ilivyokuwa desturi yao.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  amewataka wadau wote wa Maendeleo wanaojihusisha na masuala ya kupambana na ukeketaji kuendelea na juhudi hizo kwa maslahi mapana ya Afya ya mama na mtoto.
 Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku moja ya kupinga ukeketaji yaliyofanyika Wilayani Kilindi  katika kijiji cha Elerai kata ya kiberashi kijiji ambacho asimilimia kubwa ya wakazi wake ni Jamii ya Wamasai.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Tanzania Dkt. Frolence Temu akitoa hotuba yake kwa Naibu Waziri wa Afya amesema  Maadhimisho ya Siku moja kuhusu Siku ya Kimataifa ya Ukeketeji Duniani yamefanyika kijini hapo kwa kuwa shirika lake limechagua kufanya maadhimisho kwa Jamii ya mahitaji tofauti na maadhimisho yafanyikayo maeneo ya mijini. 
Maadhimisho haya ufanyika kila tarehe 6 Mwezi wa pili lakini imeadhimishwa leo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na AMREF Tanzania. 
Naibu Waziri wa Afya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustini Ndugulile amesema kuwa Kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya Tanzania ya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa mwanamke 1 kati ya 10 nchini amekeketwa. 
Ametaja mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukeketejji kuwa ni  mikoa inayoongoza kwa ukeketaji ni Manyara (58%), Dodoma (47%),Arusha (41% ), Mara ( 32%) na Singida (31%).
Waziri amesema lengo la maadhimisho haya ni kulindawanawake na watoto wa kike dhidi ya mila na desturi zenye madhara na kuzorotesha maendeleo yao  wakati huohuo akiwataka AMREF na mashirika mengine yenye mtazamo sawa wa  kupinga ukeketaji Tanzania kwa kutetea haki na maslahi bora ya watoto hapa nchini. 
Aidha kupitia maadhimisho haya tutaweza kujipima ni kwa namna gani tumeweza kukabiliana na ukeketaji na changamoto zilizojitokeza katika mapambano haya ili kubuni mikakati mipya ya kutokomeza ukeketaji nchini.

Waziri Ndugulile ameyataja madhara yatokanayo na ukeketeji kuwa ni pamoja na kupoteza damu nyingi na kusababisha vifo, maambukizi ya VVU/UKIMWI na kusababisha matatizo wakati wa kujifungua. 
Ameongeza kuwa Watoto wakati wa kukeketwa hawawezi kuhudhuria vipindi mashuleni kwa muda mrefu na hivyo kuzorotesha maendeleo yao kielimu na kuongeza kuwa Serikali inapinga, inalaani na kukemea tabia ya kuendelezwa kwa vitendo hivi vya ukatili unaomdhalilisha mtoto wa kike na mwanamke kwani unamsababishia madhara makubwa kiafya, kielimu, kisaikolojia na kimaendeleo.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akivishwa vazi la kimila la Kimasai tayari kwa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika  Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga.
 Laigwenani Mkuu wa Kabila la Kimasai Mzee Simon Mchamya akitoa maoni yake kwa Mgeni rasmi hayuko pichani kuhusu masuala ya ukeketeji katika jamii ya Wamasai wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika  Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akipewa ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na shirika la kimataifa la AMREF na Meneja wa shirika hilo Wilayani Kilindi Dkt. Jane Sempaluo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika  Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga.
 Wanawake wa Jamii ya Kimasai wakiigiza namna binti wa Jamii ya Kimasai anavyopelekwa ndani kwa ngariba kwa ajili ya kufanya tohara Jamii hiyo kwasasa inaachana na mira hiyo potofu na kuendelea na tohara mbadala baada ya kupatiwa elimu kuhusu madhara ya tohara na shirika AMREF.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wamasai waliopatiwa vyeti baada ya kushiriki na kukubali kuachana na mira ya tohara swakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika  Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga.

HABARI-PICHA TOKA WILAYANI TUNDURU MKOA WA RUVUMA

$
0
0
 Wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho Africa Ltd. kilichopo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa kazini. Wakazi zaidi  750 kutoka katika wilaya hiyo wamepata ajira katika kiwanda hicho kinachotajwa kama mkombozi mkubwa wa umaskini kwa wilaya ya Tunduru.
 Wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho Africa Ltd. kilichopo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakiendelea na kazi.
 Daraja  linalojengwa na serikali chini ya wakala wa ujenzi mjini na vijijini Tarura wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kwa gharama ya shilingi bilioni 115.804 lenye urefu wa mita 45 katika mto  Nanyungu lililopo  kijiji cha Fundimbanga kama linavyoonekana ambapo  litakapokamilika litasaidia kurudisha mawasiano ya uhakika kati ya wakazi wa kijiji hicho na maeneo mengine ya  wilaya ya Tunduru. Picha na Muhidin Amri.

HOJA YA HAJA: "WAPINZANI BADILISHENI NAMNA YAKUENDESHA SIASA ZENU NCHINI"

$
0
0


Na Moses Machali.
Wapinzani  na hasa CDM  na Kwa mbali  Kiongozi  wa  ACT mmefikia mahala mnajiona mna akili Sana na kwamba mnaweza kuwafanya watu wote kuwa wapumbavu wasioweza kuchanganua pumba na mchele ktk Ulimwengu wa siasa.
Kosa moja mmelofanya na mnaloendelea kulifanya hadi sasa ni kufanya siasa za chuki na ulaghai dhidi ya Uongozi wa serikali na mamlaka za nchi; Siasa za chuki na ulaghai dhidi ya chama kilichoko madarakani Kwa kukifitinisha na wananchi. Nawaelezeni tena maneno haya ambayo nimewahi kuwaelezeni tukiwa pamoja huko nyuma kwamba Kamwe siasa za chuki na ulaghai dhidi ya mamlaka za nchi na kufitinisha Mamlaka za nchi na watu wake haziwezi kuwafanya mpate ukubalifu  wa KISIASA KWA PANDE ZOTE yaani upande wa mamlaka za nchi na upande wa Raia wa kawaida. Upinzani jisahihisheni Kwa kuacha tabia hiyo mjenge utamaduni wa kuwaunganisha Watanzania bila ya vitisho dhidi ya mamlaka za nchi na chama tawala.
Siasa zenu za kutishia mamlaka za nchi; chama tawala na Raia wa kawaida wanaounga mkono serikali na chama tawala haziwezi kuwafikisha mbali Kwa sababu Kwanza hamna ubavu wa kupambana na mamlaka au vyombo hivyo. tumieni busara na taaluma muanze kukua kama alivyowahi kuwaambia Edward Lowasa kwamba Mfike mahali mtoke kwenye siasa za harakati na Mu-graduate sasa Kwa kuanza kufanya siasa Kwa sababu Miaka ya tangu mfumo urejee toka 1992 ni umri mkubwa na kwamba hampaswi kufanya siasa namna hiyo. Yalikuwa maneno ya hekima Sana na mlipaswa myatafakari na kuyafanyia kazi. Hivi unamtisha mwenye mamlaka kwamba utamshughurikia; unategemea akupishe utawale? Tumieni akili.
Akili nayotaka muitumie ni ninyi wapinzani mnaotishia dola muache kufanya siasa za vitisho na badala yake mfanye siasa za kidugu na muishawishi mamlaka ya nchi na chama tawala viwaone kuwa kweli nanyi ni Watanzania wenye nia njema na watu wanaoweza kukabidhiwa dola na kuiimarisha na kuistawisha nchi yetu ktk Nyanja ya UMOJA MIONGONI MWA WATANZANIA na hatimaye taifa liweze kuendelea KIUCHUMI; KIJAMII NA KISIASA.
Kama CDM na Kiongozi wa ACT hamna tamaa ya kutawala nchi Kwa maslahi Binafsi ya viongozi wa vyama hivyo; mnao wajibu wa kubadili namna ya kufanya Siasa zenu Kwa kuacha vitisho dhidi ya mamlaka za nchi na chama tawala na Raia wote ili muaminiwe na kila mtu. Siasa zenu za kuwagawa watu hazina tija hata kidogo. Na kamwe hamtaweza kuchukua dola Kwa njia hiyo. Uzoefu ni mwalimu mzuri: Angalieni Maalum Seif kaishia wapi? Angalieni Raila Odinga kaishia wapi? Angalieni Kiza Besigye kaishia wapi? NK, uzoefu wa hao iwe ni fundisho kwenu. James Mbatia amewahi kuwa muumini wa hili ninalolizungumza kwenu leo lakini sijui msimamo wake hivi sasa. Badilikeni Kwa kuonesha kwamba lengo lenu siyo uchu wa madaraka unaoligawa taifa hili Kwa kufanya siasa zisizo na vitisho dhidi ya mamlaka za nchi Raia WA kawaida. Kama taifa tunao wajibu wa kujenga nchi ya udugu na siyo taifa la kugawanywa na siasa uchwara.
Wapinzani mnaweza mkajitetea kwamba Mko hivyo mlivyo leo hii eti Kwa sababu chama tawala na serikali wameafanyia hivi na vile. Hakika nawaelezeni ya kwamba hampaswi ku-have namna hiyo Kwa sababu mnapofanya mambo mqbaya dhidi ya serikali na chama tawala mjue nao watawajibu kama mnavyostahili. He, mnajenga au mnabomoa. Kumbukeni kwamba Mtoto hakui Kwa Mzazi wake hata kama hampendi. Serikali na CCM wanewatangulieni kufanya siasa na kukua kiasiasa na hivyo mkiwatendea isivyo stahili au namna isiyo na heshima msitegemee wao wakutendeeni matendo yanayokupa heshima lazima watajibu mapigo na Wana ubavu mkubwa Tu dhidi yenu. Acheni mara moja na mjirudi Kwa kuanza kufanya siasa zenye staha la sivyo msilalamike. Mnafanya siasa za fitna halafu mnataka wenzenu wawalipeni Kwa siasa Safi. Inawezekana kweli? haiwezekani.
Mnapokuwa mnapika majungu na fitna dhidi ya CCM na serikali huku mkifikiri CCM na mamlaka za nchi hawana akili na macho ya kujua lengo lenu; mnajidanganya Sana. Serikali na CCM Wana macho yanayowawezesha kuona na kufika mbali kabla na baada ya ninyi kutekelezea mipango yenu. Kwa hiyo Siasa za kitoto hazina nafasi ktk ujenzi wa jamii mpya. Acheni Kuwatisha watu kwa maneno ya akina Martin Luther ya kwamba ipo siku itakuwa kama Marekani sijui Zimbabwe, sijui Ethiopia. Kumbukeni Watanzania siyo waethiopia wala wakenya, wala wazimbabwe. Sisi ni Watanzania tu na tutabakia kuwa Watanzania Kwa Mila na desturi zetu. Hatupendi fujo wala vita kama mnavyotamani siku moja ije kutokea.

Nawatakia mabdadiliko mema Kwa kuacha kufanya siasa ambazo kamwe haziwezi kumtisha CCM na mamlaka za nchi.
18/02/2018

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WATEMBELEA MICHUZI MEDIA GROUP

CCM YAIBUKA KIDEDEA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

$
0
0
 Bw. Maulid Mtulia wa Chama cha Mapinduzi(CCM)  akionesha hati yake ya ushindi baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Ubunge, Jimbo la Kinondoni, mkoani Dar es salaam  baada ya kupata kura 30,313 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salum Mwalim (CHADEMA) aliyepata kura 12,353...Chini ni fomu rasmi ya matokeo hayo.

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI

$
0
0
*Waziri Ndalichako asema Taifa limepata pigo kubwa, aomba utulivu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI kupitiza Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema itagharamia mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) Aqwilina Akwiline ambaye amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam

Imesema kifo cha mwanafunzi huyo ni pigo kubwa kwa familia, Serikali,Wizara ya Elimu,wanafunzi, ndugu, jamaa na marafiki huku ikiomba Watanzania wote kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati uchunguzi wa kifo hicho ukiendelea kufanywa na vyombo vya dola.

NI PIGO KWA TAIFA

Akizungumza Dar es Salaam leo kuhusu kifo cha Aqwilina aliyepigwa risasi akiwa kwenye daladala, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema Taifa limepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mwanafunzi huyo ambaye hakuwa na hatia ya aina yoyote.

Amesema kabla ya tukio la kupigwa risasi mwanafunzi huyo alikuwa amebeba barua kwenda kuomba kufanya mafunzo kwa vitendo lakini kifo kimekatisha ndoto zake na harakati za kuisaka elimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Prof.Ndalichako amesema tukio la kifo hicho kimegusa hisia za watanzania wengi na Rais ,Dk.John Magufuli mbali ya kutoa pole kwa familia na wananchi wote ameonesha kuguswa na tukio hilo.

"Ni msiba mkubwa ambao umelipata Taifa letu kwa kifo cha mwanafunzi wetu mpendwa.Kifo kimetokea wakati wa kudhibiti maandamano yaliyofanyika Februari 16 mwaka huu huko Kinondoni.Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji.

"Serikali imepata pigo kubwa kwani inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuosmesha wanafunzi wa kitanzania na mwanafunzi aliyefariki ni miongoni mwa wanafunzi aliyekuwa anasoma kwa mkopo wa Serikali.Mwanafunzi huyu alikuwa mtiifu na amefariki .Ni msiba ambao hakika umetugusa sisi wote,"amesema.

SERIKALI KUGHARAMIA MSIBA 

Wakati huo huo, Profesa Ndalichako amesema imeamua kuchukua jukumu la kugharamia msiba huo hadi pale mwanafunzi huyo atakapopumzishwa kwenye nyumba yake ya milele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

"Kama ambavyo nimetangulia kueleza hapo awali namna ambavyo kila mmoja wetu ameguswa na kifo cha mpendwa wetu lakini Serikali kwa niaba ya Wizara ya Elimu tumechukua jukumu la kugharamia msiba huu.

"Tunaomba katika kipindi hiki Watanzania wote tuungane katika kushiriki kwenye msiba wa mpendwa wetu na nitoe rai kwa wanafunzi wote wakiwamo wa elimu ya juu kuwa watulivu wakati hatua mbalimbali zikiendelea kufanyika.Waliohusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria,"amesema Prof. Ndalichako.

Ameomba wananchi wote kuwa kwa sasa si vema kuanza kulaumiana na badala yake ni kuwa wamoja na wenye utulivu wa kati mwili wa mwanafunzi huyo ukisubiriwa kupumzishwa na wakati hatua nyingine za vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi wake.
Pichani kati ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana jijini Dar,kuhusu kifo cha Mwanafunzi  wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) Aqwilina Akwiline ambaye amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni -Kinondoni jijini Dar es Salaam,kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni pamoja na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Dkt.Akwilapo
Baadhi ya Waandishi wa vyombo vya habari wakiendelea kurekodi na kusikiliza yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi waandamizi wa Serikali kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo,kilichotokea kwa kupiga risasi hivi karibuni Kinondoni,jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.

Ndalichako,Masauni watoa mkono wa pole kwa wafiwa kifo cha Mwanafunzi aliyepigwa risasi

$
0
0
  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni  wakimfariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar,Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuiya maandamano ya chama cha CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema itabeba jukumu la Mazishi yake.

Aidha Rais Dkt John Pombe Magufuli  amesema amesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi huyo,Aqwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT)."Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili",Ilisema sehemu ya taarifa yake iliyotolewa mapema leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako (tatu kulia) akiwafariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina pamoja na ndugu jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar,Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuiya maandamano ya chama cha CHADEMA.
 Mama wa Marehemu Akwiline akilia kwa uchungu mara baada ya kuona viongozi wa Waandamizi wa serikali walipofika nyumbani kwake,Mbezi Kimara jioni ya leo kwa lengo la kutoa pole na kufahamu taratibu mbalimbali za msiba huo.

UCHUNGUZI WAANZA KUBAINI WALIOMUUA KWA RISASI MWANAFUNZI CHUO CHA USAFIRISHAJI

$
0
0
*Wizara ya Mambo ya Ndani yaelezea kinachoendelea
*Rais Magufuli aagiza waliohusika wachukuliwe hatua 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imewahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Aqwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi utafanyika kwa haraka na weledi mkubwa na kufafanua waliohusika na kifo hicho kwa namna yoyote ile hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Imesema tukio la mwanafunzi huyo limewasikitisha Watanzania wote na Wizara hiyo imeanza kufanya uchunguzi ili kupata taarifa sahihi za tukio la kupigwa risasi mwanafunzi huyo na kwamba iwe kwa ofisa wa polisi au viongozi wa kisiasa wakithibitika kuhusika watachukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine kwani Serikali haipo tayari kuona raia hata mmona anapoteza maisha.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusufu Masaun wakati anaelezea tukio la kifo  cha mwanafunzi Aqwilina aliyekuwa anasoma mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

UCHUNGUZI WAANZA 

Akizungumzia hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa kutokana na mauaji ya mwanafunzio huo, Masaun amesema tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimenza kuchunguza tukio hilo ili kubaini waliohusika na kwa sasa ni mapema kusema fulani ndio amehusika moja kwa moja.

Amesema Serikali imesikitishwa na kifo hicho lakini uchunguzi unaendelea na atakayebainika kuhusika kwa namna yoyote hatua za kisheria zitachukuliwa.

"Tutahakikisha hatua zinachukuliwa haraka kwa waliohusika na hakuna ambaye ataachwa iwe ofisa wa polisi au viongozi wa vyama vya siasa.Kiujumla matatizo ya uvunjifu wa amani lazima yachukuliwe hatua na waliohusika kwenye hilo nalo lazima wachukuliwe hatua kali,"amesema Masaun.

Amefafanua wapo viongozi wa kisiasa ambao walikuwa wanatoa kauli za kuashiria uvunjifu wa amani ambao nao lazima wachunguzwe.

Amesema lengo la uchunguzi huo ni kupata taarifa sahihi ili asije kuoonekana hatua zimechukuliwa bila kufanyika uchunguzi, hivyo wameanza na uchunguzi ambao anaamini utakamilika kwa haraka.

Ameongeza uchunguzi huo utafanyika kwa weledi na umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha haki inatendeka huku akieleza kwa sasa hawawezi kusema wamekamatwa watu wangapi kutokana na tukio hilo  ila uchunguzi ukikamilika watatoa taarifa kwa umma hatua zinazofuata.
Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa abari mapema leo mchana jijin Dar,kuhusu kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Aqwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi Mkwajuni,Kinondoni jijini Dar.Masauni amewahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi wa kifo utafanyika kwa haraka na weledi mkubwa na kufafanua waliohusika na kifo hicho kwa namna yoyote ile hatua kali za kisheria zitachukuliwa.Picha Michuzi Jr.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wadhamini Kili Marathon wafanya amsha amsha

$
0
0
Wadhamini wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametoa wito kwa watanzania na washiriki wengine kuhakikisha wanajiandikisha mapema ili kushiriki katika mbio za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi na kuwavutia watu wengi zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.

Rai hii inakuja takriban wiki mbili kabla kufanyikakwa mbio hizo maarufu ndani na nje ya nchi ambazo huwaleta pamoja zaidi ya washiriki 10,000 kutoka nchi zaidi ya 45 mjini Moshi ambapo mbhio hizi hufanyika.

Akizungumza jinini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu, alisema tayari usajili umeshafunguliwa na kuwataka washiriki hususan wale wa mbio za kilometa 42 zinazodhaminiwa na bia hiyo, kujisajili kwa wingi ili Milioni 20 walizotenga za zawadi zibaki Tanzania.

“Bila shaka tunatarajia kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi ndio maana tunasisitiza kuhusu usajili mapema ili kuepuka usumbufu dakika za mwisho,” alisema huku akiwapongeza waandaaji kwa maandalizi mazuri huku wakazi wa Dar es Salaam wakipewa nafasi ya kujisajilipia Februari 24 na 25 katika viwanja vya Mlimani City.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo inadhamini Kilimanjaro Marathon, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon Moshi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AKUTANA NA MUANZILISHI WA TAASISI YA DORIS MOLLEL

$
0
0
 Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimsikiliza Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel aliyemtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuona namna ya kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), ambao huitaji uangalizi wa hali ya juu baada ya kuzaliwa kwao. 
Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo azungumza jambo na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel aliyemtembelea ofisini kwake leo.

TRA KUENDELEA KUWACHUKULIA HATUA KALI WAFABIASHARA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MAGENDO

$
0
0


Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inatoa onyo kali kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na Biashara za Magendo na aina mbalimbali za ukwepaji kodi kupitia Viwanja vya Ndege, Vituo vya Forodha Mipakani, Njia za panya pamoja na Bandari bubu kuacha mara moja vitendo hivyo. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo
Bw. Charles Kichere, hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayebainika kusafirisha bidhaa kwa kutumia njia za magendo na kukwepa kodi ikiwa ni pamoja na kutaifishwa mali zote zitakazokamatwa pamoja na chombo kilichotumika kusafirisha au nyumba iliyohifadhi bidhaa hizo. 
 Taarifa hiyo imesema kwamba, kukwepa kodi ni Kosa la Jinai kwa mujibu wa Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2005 na Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015. Aidha, taarifa hiyo imesisitiza kuwa, ukwepaji kodi husababisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuikosesha Serikali mapato yake halali ya kuimarisha uchumi ambayo yangeiwezesha Serikali kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake na kuwepo kwa ushindani usio kuwa wa haki na usawa kati ya bidhaa zinazoingizwa nchini zikiwa zimelipiwa kodi na zile zinazouzwa bila kulipiwa kodi stahiki kutoka nje ya nchi. 
 Vilevile, ukwepaji kodi huhatarisha maisha ya walaji kwa kuingiza bidhaa ambazo hazijathibitishwa viwango vya ubora na usalama wake kupitia mamlaka husika ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). 
Pia, huhatarisha uchumi na usalama wa nchi kwa sababu ya uwezekano wa kuingiza vitu vya hatari kama vile silaha. 
 Taarifa hiyo ya Kamishna Mkuu wa TRA imewaomba wananchi kutoa taarifa ya mfanyabiashara au kampuni yoyote inayojihusisha na vitendo vya Biashara ya Magendo na ukwepaji kodi kwa kupiga simu namba +255 22 2137638 au +255 784 210209.

SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kufanya mapitio na ukaguzi wa zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma katika Halmashauri zao.
Lengo la maelekezo hayo ni kujiridhisha na sifa za watumishi waliojiriwa kwa cheti cha darasa la saba na walioajiriwa kwa sifa ya cheti cha ufaulu wa Kidato cha Nne kama wamewasilisha vyeti vyao na kuhakikiwa.Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo katika kikao kazi na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe.
Dkt. Ndumbaro ametoa angalizo kwa  Makatibu Tawala wa Mikoa  nchini kuhakikisha wanawaondoa katika Utumishi wa Umma watumishi ambao hawajawasilisha vyeti vya Kidato cha Nne kwa ajili ya uhakiki na wale waliodanganya kuwa ni darasa la saba ili kukwepa zoezi la uhakiki wa vyeti vya kidato cha Nne,Sita na Ualimu.
Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, ofisi yake itatoa Waraka wa kuzitaka Mamlaka za Sekretarieti za Mikoa kwenda kufanya ukaguzi katika Halmashauri zao ili kujiridhisha na namna zoezi la uhakiki liliyofanyika.
Katibu Mkuu Dkt. Ndumbaro katika kikao kazi hicho amepokea changamoto mbalimbali na kuzitolea ufafanuzi ili kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma nchini.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaroakizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya  Mkoa wa Njombe katika kikao kazi na waumishi hao chenye lengo la  kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
 Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
Mmoja wa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe akiwasilisha hoja yake kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa  kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi. 
 
Imetolewa na James Katubuka Mwanamyoto
Afisa Habari
Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora

WAZIRI LUKUVI ATEMBELEA NA KUSULUHISHA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA MBONDOLE KATA YA MSONGOLA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Mbondole kata ya Msongola Dar es Salaam wakati apokwenda kusuluhisha mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.
 Wakazi wa Mbondole kata ya Msongola wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi mhe. William Lukuvi. 
 Wakazi wa Mbondole wakimpokea Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi wakiwa na mabango

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi mhe. William Lukuvi akikagua maeneo yaliyovamiwa katika eneo la Mbondole kata ya Msongola Dar es Salaam. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi mhe. William Lukuvi akikagua maeneo yaliyovamiwa katika eneo la Mbondole kata ya Msongola Dar es Salaam.

Jeshi la polisi na benki ya CRDB waendelea kutoa elimu kwa umma juu Matumizi salama ya huduma za kibenk mkoani lindi

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango  akiwa katika Picha ya Pamoja  Ofisini kwake baada ya kutembelewa na Naibu Kamishina wa Polisi DCP Ahmada.A. Khamis Mkuu wa Kitengo  cha Polisi Jamii, Mkuu wa Kituo cha Polisi Nachingwea, SP Kasigwa, na Meneja Mwandamizi wa huduma za Uwakala Benki ya CRDB  Bwa.Donath Mushi, Wengine ni Abel Laswai  meneja mauzo wa wateja wadogo (wa kwanza kushoto) na Inspekta Issa Asali kutoka kitengo cha Polisi Jamii (wa mwisho kulia). Jeshi la Polisi pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB  kutoka Makao Makuu Dar es salaam wapo Mkoani Lindi kwa ajili  kutoa elimu kwa umma juu Matumizi salama ya huduma za ki benk pamoja na elimu juu ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao.
 Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango akimkabidhi zawadi ya Korosho  kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo Naibu Kamishina wa  Polisi DCP Ahmada.A.Khamis. Zawadi hiyo ilitolewa kama shukrani na wananchi  wa wilaya hiyo kutokana na elimu waliyopewa.
Meneja Mwandamizi wa huduma za uwakala kwa Benki ya CRDB Donath Mushi akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Naipingu iliyopo wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, Jana juu ya matumizi salama ya Huduma za bank ma uhifadhi salama wa fedha katika benki hiyo.

MABENKI 29 YAFANIKIWA KUJIUNGA ASILIMIA 100 NA MFUMO WA KULIPA KODI KIELEKTRONIKI (e-RCS)

PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wakazi wa wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, kuilinda miundombinu ya barabara iliyokamilika kujengwa ili kupunguza gharama za matengenezo ambayo yanaepukika.
Ametoa rai hiyo Wilayani humo, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusema kuwa barabara hiyo itawaunganisha wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kukuza uchumi kupitia mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye mikoa hiyo.
"Barabara hii sasa imekamilika ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie kuilinda na kuhakikisha inadumu kwa kipindi kilichokadiriwa", amesema Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa barabara hiyo itakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi watakaotumia usafiri wa reli ya kisasa pindi utakapokamilika kwani watatoka kwenye mikoa ya jirani kupandia kwenye stesheni ya Malyampaka ambayo iko kwenye barabara hiyo.

Aidha, amewapongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe, ameishukuru Serikali kwa kukamilisha sehemu ya barabara hiyo na kumuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa miundombinu hiyo italindwa ili idumu muda mrefu.

"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuikamilisha barabara hii kwa kiwango cha lami kwani kwa sasa muda na gharama za usafirishaji wa mazao zitapungua", amesema Dkt. Shekalaghe.

Naye Meneja wa TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema mradi mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 98 na kazi zilizobaki ni kuweka alama za barabarani na ujenzi umezingatia viwango vinavyohitajika.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 imejengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 61.46 na zote zikiwa zimefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na  uongozi wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu, wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya miundombinu ya barabara mkoani humo. Wa Kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe.
 Gari maalum likimwaga lami ya mwisho katika barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3, wilayani Maswa, Mkoani Simiyu. Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 61.46.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe kuhusu umuhimu wa kutunza barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Simiyu,
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3, wilayani humo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Kushoto ni Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 kutoka kwa Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent (wa pili kulia), mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo, wilayani Maswa, mkoani Simiyu.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

UKAGUZI WA TFDA WAKUTANA NA DAWA ZA SERIKALI KATIKA MADUKA BINAFSI , DAWA BANDIA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
 MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) iliendesha ukaguzi maalum wa dawa , vifaa tiba na vitendanishi katika Halmashauri na Manispa zilizo Kanda ya Kati na kubaini kuwepo kwa vifaa tiba na vitendanishi bandia duni ambavyo hajasajiliwa pamoja na dawa za serikali katika maduka ya dawa binafsi. 
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Agnes Kijo amesema kuwa mamlaka haitawaacha watu wafanye vitu kiholela pamoja na kuwafikisha watuo ho mahakamani. 
 Amesema ukaguzi huo umefanyika kati ta Februari 5 hadi 7 mwaka huu katika Manispaa ya Dodoma , Morogoro na Mkoa wa Singida umefanyika katika wilaya ya Manyoni , ,iramba , Wilaya ya Gairo ,Mvomero , Kongwa na Chamwino. 
 Kijo amesema jumla ya maeneo yaliyofanyiwa ukaguzi 172ambapo 48 ni Famasi za dawa za binadamu , tano ni Famasi za dawa za mifugo ,tatu ni Hospitali na tatu zingine vituo vya afya , 76 ni maduka ya dawa muhimu za binadamu , 30 ni maduka ya dawa muhimu za mifugo, 1 ni zahanati pamoja na sita vituo vya huduma za tiba za mifugo . 
 Amesema kuwa katika ukaguzi wamepata makopo 12 ya dawa bandia aina ya Ampicillin 250mg ambapo ni tofauti na dawa halisi ya Ampicillin iliyosajiliwa na TFDA.  Amewataka ambao wenye bidhaa ambazo wanaziuza na kuweka katika mitandao wajisalimishe bila kufanya hivyo hatua kali za zitachukuliwa.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akionyesha kopo lenye dawa aina ya Ampicilin isiyosajiliwa na mamlaka hayo  jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi , Mkuu  Msaidizizi wa Makosa ya  Kihalifu ya Mitandao , Joshua Mwangasa akizungumza kuhusiana na makosa ya kimtandao kwa wanaotangaza dawa  katika mitandao ya kijamii leo jijini Dar es Salaam.

Introducing "Beautiful" Official Audio by Sam Money

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images