Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

AHADI YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI, ELIAS KWANDIKWA KWA MKUU WA WILAYA PANGANI KUHUSU UJENZI WA BARABARA YA TANGA-PANGANI-BAGAMOYO


Mwananchi wa Mbulu afurahia Alexander Mnyeti kuwa mkuu wa Mkoa wa Manyara

$
0
0
Mkaazi wa kata ya Daudi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Aloyce Bura amesema alifurahi na kuchinja nguruwe mara baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa Rais John Magufuli amemteua Alexander Mnyeti kuwa mkuu wa Mkoa huo, kwani wananchi wanyonge hivi sasa watakuwa wamepata mtetezi wao. 
 Bura aliyasema hayo mbele ya Mnyeti, wakati akizungumzia kero yake ya kunyang'anywa ardhi yenye makaburi ya familia yake na kigogo wa eneo hilo kwa ushirikiano na ofisa ardhi. Alisema miezi mitatu iliyopita aliposikia kwenye vyombo vya habari kuwa Mnyeti ameteuliwa na Rais Magufuli kuwa mkuu wa mkoa huo, alichinja nguruwe na kusherehekea na ndugu zake. Alisema alichinja nguruwe huyo na kusherehekea na familia yake kwani aliamini wanyonge watapata msaada kama alivyowasaidia wananchi wa Arumeru, wakati akiwa mkuu wa wilaya hiyo. 
 "Mimi nimekaa Arumeru kwa muda mfupi nimesikia sifa za Mnyeti kutetea wanyonge akiwemo kijana aitwaye Nyangusi wa Ngaramtoni alidhulumiwa ardhi lakini alisaidiwa na Mnyeti na kurudishiwa eneo lake," alisema Bura. 
 Alimuomba Mnyeti amsaidie arudishwe eneo lake ambalo lina makaburi ya babu na bibi yake lakini likaporwa na mtu mwenye fedha ambaye alisaidiwa na mmoja kati ya maofisa ardhi wa wilaya hiyo. "Nimefuatilia suala hili kwa muda mrefu hadi ofisi ya ardhi ngazi ya kanda kule Moshi lakini sijapata msaada, tunaomba mheshimiwa mkuu wa mkoa tusaidie kama ulivyowasaidia watu wa Arumeru," alisema Bura. 
 Alisema rushwa imetumika kumuondoa kwenye eneo hilo na yeye kunyimwa haki yake ila kutokana na utendaji kazi mzuri wa Mnyeti, ana matarajio makubwa ya kupatiwa ardhi yake na kuendelea kuimiliki upya. 
 “Haihitaji hata elimu ya shahada kujua kuwa sisi ndiyo tunamiliki eneo hilo kwani hata mtu wa darasa la saba atatambua hilo kwani kuna makaburi ya babu na bibi yetu, tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie hilo sisi wanyonge,” alisema Bura. 
 Hata hivyo, Mnyeti alimuagiza mkuu wa kitengo cha sheria wa ofisi yake Peter Mangala kupitia nyaraka za Bura ili kama zinaonyesha ndiye mmiliki halali wa eneo hilo apatiwe haki yake. 
 "Mpe mwanasheria wangu nakala ya hizo nyaraka zako ili azipitie na kuzifanyia kazi na ninakuhakikishia kama haki ni yako utarudishiwa eneo lako bila mashaka wala wasiwasi wowote," alisema Mnyeti.
Aliwataka watumishi wa idara ya ardhi kwenye halmashauri za mkoa huo kufanya kazi zao kwa haki, weledi na hofu ya Mungu kwani kwenye maeneo mengi wananchi wanawalalamikia kuwa wenyewe ndiyo wanaosababaisha migogoro ya ardhi. 
 "Ninyi maofisa ardhi ndiyo mnasababisha wananchi waichukie serikali yao kwani mnachukua virushwa na kupindisha haki sasa mimi nitapambana nanyi nione mwisho wenu kwani mnasemwa sana," alisema Mnyeti.

 Wanawake vikongwe wajasiriamali wa Kata ya Uhuru Mjini Mbulu, wakiwa wamepiga magoti mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, wakimuomba awasaidie wapate ardhi yao walioporwa na mfanyabiashara wa mjini hapo.
 Mkazi wa Kata ya Daudi Wilayani Mbulu, Aloyce Bura akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, juu ya ardhi yake yenye makaburi iliyoporwa na mfanyabiashara wa eneo hilo ambapo miezi mitatu iliyopita aliamua kuchinja nguruwe akifurahia uteuzi wa Rais John Magufuli alioufanya kwa Mnyeti ili awatetee wananchi wa mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa kata ya Nambris Halmashauri ya mji wa Mbulu, kwenye ziara yake ya siku saba ya kujitambulisha, kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi na watumishi wa eneo hilo na kusikiliza kero, changamoto na maoni yao.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akikagua msingi wa ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya sekondari Daudi Wilayani Mbulu.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa mji wa Mbulu kwenye ziara yake ya siku saba ya kujitambulisha, kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi na watumishi wa eneo hilo na kusikiliza kero, changamoto na maoni yao.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na viongozi na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwenye eneo la Isale linalotaka kununuliwa na Halmashauri hiyo.

MADIWANI KITETO WATAKIWA KUJIUNGA NA HUDUMA YA AKAUNTI YA AKIBA YA FAHARI BENKI YA CRDB

$
0
0
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, wametakiwa kujiunga na huduma ya akaunti ya akiba ya fahari ambayo ni jibu kwa kila mtanzania kuweka akiba na kufikia uhuru wa kibenki. 
Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Kiteto, Lucy John akizungumzia huduma ya akaunti ya akiba ya fahari kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto alisema huduma hiyo ni muhimu kwa jamii. 
Lucy alisema pia huduma ya SIMAccount ambayo ni rafiki na nafuu kwa kila mwananchi unaweza kujiunga kwa kubonyeza *150*62#Ok! 
Alisema pia huduma za insurance zinapatikana kwenye Tawi la CRDB, bima za magari, pikipiki, nyumba za makazi, hoteli na mazao ambayo yapo kwenye maghala. 
Meneja wa Benki ya CRDB wa Mkoa wa Manyara, Ronald Paul aliwaeleza madiwani hao juu ya ukarabati wa hospitali ya wilaya ya Kiteto.
Paul alisema anatambua fika kuwa madiwani wa halmashauri hiyo ya Kiteto na watumishi wao ni wateja wazuri wa benki hiyo hivyo wataendelea kushirikiana kwa  mbalimbali katika ujenzi wa Taifa.
 Meneja wa Benki ya CRDB Mkoa wa Manyara Bw.Ronald Paul akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
 Meneja wa Benki ya CRBD Tawi la Kiteto Mkoani Manyara Bi. Lucy John akizungumza juu ya huduma ya akaunti ya akiba ya fahari kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. 

Meneja wa Benki ya CRDB Mkoa wa Manyara Bw. Ronald Paul akiendelea kueleza juu ya ukarabati wa hospitali ya wilaya ya Kiteto kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

MKIKITA WATEMBELEA CHUO CHA KILIMO CANRE NA KUTOA MAFUNZO YA KILIMO BIASHARA

$
0
0
 Uongozi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania ukitembelea bwawa linatumiwa kufundishia wanafunzi ufugaji wa samaki katika Chuo cha Kilimo, Mifugo na Maliasili (Canre), kilichopo Bonyokwa nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Anaye waongoza ni Mkuu wa Chuo hicho, Sylvester Nakara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Myandao wa Kijani Kibichi Tanzania, Adam Nagamange akionesha kitabu alichotunga cha Wewe ni Bilionea wa Mtaji Sifuri, ambapo aliwaeleza wanafunzi na walimu wa Chuo cha Canre kuwa ili uondokane na umasikini jitahidi kukisoma kitabu hicho chenye mambo mengi muhimu ya kuyafuta hakika muda i mrefu utakuwa tajiri. Kwanza anza na Wazo, Uhusiano na Mawsiliano katika jamii ni muhimu, kusoma vitabu na kuhudhuria mafunzo mbalimbali, usisahau kuwa karibu na vyombo vya habari  pamoja na kufanya utafiti kwa yale yote unayotaka kuyafnya ili uwe na uhakika zaidi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Canre, Dk. Aloyce Masanja akizungumza na uongozi wa Mkikita uliomtembelea na kutoa mafunzo kwa wanafunzi na walimu wa chuo hicho kuhusu faida za uwekezaji katika kilimo biashara. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui  Steven Kissui, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange na Mdau wa Mkikita, Richard
Uongozi wa Mkikita ukiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Canre
Uongozi wa Mkikita ukitembelea maeneo ya Chuo hicho.

MICHUZI TV: NDOTO NA FAIZA ALLY

UBALOZI WA KUWAIT, TAASISI YA DORIS MOLLEL WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA VYA KUSAIDIA WATOTO NJITI KWA HOSPITALI ZA MAFIA NA WETE

$
0
0
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (kulia) akikabidhi Mashine maalum ya kumpa joto Mtoto anayezaliwa kabla ya wakati (Njiti) kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma wa Wizara ya Afya Zanzibar (Pemba), Dkt. Yussuf Hamad Iddi (kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba mbalimbali vilivyotolewa kwa msaada wa Ubalozi wa Kuwait nchini, iliyofanyika kwenye Hospitali ya Wete, Kisiwani Pemba, Zanzibar Februari 16, 2018. wengine pichani ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Wete, Sabra Salim Suleiman (wa pili kushoto) pamoja na Muwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel kwa upande wa Zanzibar, Warda Walid (wa pili kulia). 
Uongozi wa Taasisi ya Doris Mollel ulioongozwa na Muanzilishi wa Taasisi hiyo na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (wa pili kulia walioketi) na Muwakilishi wa Taasisi hiyo kwa upande wa Zanzibar, Warda Walid (kulia walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Wete, Kisiwani Pemba, Zanzibar Februari 16, 2018, baada ya kukabidhi vifaa tiba mbalimbali vilivyotolewa kwa msaada wa Ubalozi wa Kuwait nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma wa Wizara ya Afya Zanzibar (Pemba), Dkt. Yussuf Hamad Iddi (kushoto) akizungumza jambo na uongozi wa Taasisi ya Doris Mollel ulioongozwa na Muanzilishi wa Taasisi hiyo na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel(kulia) aliyeambayana na Muwakilishi wa Taasisi hiyo kwa upande wa Zanzibar, Warda Walid (wa pili kulia) wakati walipotembelea Hospitali ya Wete, Kisiwani Pemba, Zanzibar Februari 16, 2018. Katikati ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Wete, Sabra Salim Suleiman.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (kushoto) akipokea taarifa fupi ya Hospitali hiyo, kutoka kwa Mkuu wa Wadi ya Wazazi Hospitali ya Wete, Bikombo Abdalla Mastur. Katikati ni Muwakilishi wa Taasisi hiyo kwa upande wa Zanzibar, Warda Walid.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Zubeir Mzige (wa tatu kulia) akipokea kutoka kwa Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (kushoto) sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, vilivyotolewa kwa msaada wa Ubalozi wa Kuwait nchini, kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mafia, mwanzoni mwa wiki. makabidhiani hayo yalikuwa ni ya awali kabla ya kuelekea Hospitali ya Wete, Pemba.

Article 3

WASHINDI SHINDANO LA WATOTO VIBES WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO JIJINI DAR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHINDANO la kusaka vipaji wa watoto lililoandaliwa na asasi ya kiraia Voice of Change Tanzania lililoratibiwa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana limehitimishwa leo kwa washindi kupatiwa zawadi zao ikiwemo kuwaendeleza kimuziki.

Hitimisho hilo liliofanyika mbele ya waandishi wa habari washindi hao waliweza kukabidhiwa fedha taslimu mbele ya wazazi wao na waratibu wa shindano hilo kuwaahid kuwaendeleza kimuziki pamoja na shindano hilo likiwa ni ebdelevu kwa mwaka huu kwenda katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mbeya.

Akizungumza kabla ya kuwakabidhi zawadi zao, Mratibu wa mradi wa watoto Vibes Malega Wiliiams amesema kuwa mradi huu umelenga zaidi katika kuibua buna kukuza vipaji vya watoto wenye tija ya kutaka kuleta mabadiliko chanya katika jamii, kuongeza fursa za ajira na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika taifa la Tanzania.

Williams amesema kuwa, walengwa wakuu ni watoto wasiozidi miaka 15 kwani watoto wa rika hilo wana hazina, neema na uwezo wa kugusa na kubadilisha maisha ya watu kwa kutumia vipaji vyao ila mara nyingi huwa wanakosa mazingira rafiki, malezi na nafasi ya kufanya kazi zao hivyo huishia kudidimia na kushindwa kutimiza kusudi lao.
Mratibu wa mradi wa Watoto Vibes Malega Wiliiams akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza wa shindano la Watoto Vibes Ibrahim Heri wakati wa utoaji wa zawadi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


"Mashindano haya yanaendeshwa kwa mfumo wa mashindano ya kusaka vipaji ambapo washindi hujipatia zawadi ikiwa ni pamoja na mafunzo katika nyanja ya vipaji vyao, malezi na kurekodi na kutafutiwa fursa za kutumia vipaji vyao.


Jaji Mkuu wa Shinano hilo Bella Kombo ameeleza  kuwa watoto hao walionesha uwezo wa hali ya juu, ushindani mkubwa kiasi kwamba  walikuwa na wakati mgumu wa kuchagua washindi kwani watoto walikuwa wamejiandaa vizuri.


Mshindi wa kwanza aliweza kujinyakulia kiasi cha shilingi laki tano (500,000) mshindi wa pili ni laki tatu (300,000) na wa tatu akipokea laki mbili (200,000).

Shindano la mwaka 2018 linatarajiwa kuanza mwezi wa saba na litakuwa katika mikoa ya Arusha na Mbeya na Wtoto Vibes wanejiandaa na semina kwa wazazi wa sasa na wazazi watarajiwa kuhusu malezi bora kwa mtoto ambapo inatarajiwa kufanyika Machi 26 mwaka huu.

 Mratibu wa mradi wa Watoto Vibes Malega Wiliiams akitoa zawadi kwa mshindi wa pili wa shindano la Watoto Vibes  Ibrahim Urassa wakati wa utoaji wa zawadi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi wa Watoto Vibes Malega Wiliiams akitoa zawadi kwa mshindi wa tatu wa shindano la Watoto Vibes Rebbeca Steven wakati wa utoaji wa zawadi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Zainab Nyamka

ULEGA AWATAKA WANANCHI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA VIONGOZI WAO

$
0
0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega  akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Maragoro wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi na kuwapongeza kwa ufaulu mzuri wakiongoza kwa kata kwenye matokeo ya darasa la nne na la saba.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.



Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amewataka wananchi wa Kata ya Vianzi kumuunga mkono diwani wa kata hiyo Nassoro Chuma katika kuendeleza miradi mbalimbali ya Kijiji.

Hayo aliyasema wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga kwa kutembeklea kaya ya Vianzi na kujionea maendeleo yaliyofanywa na mengine yakiwa katika hatua nzuri ambayo yanasimamiwa na diwani Chuma kwa ushirikiano na viongozi wa vijiji
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega sambamba na diwani wa kata ya Vianzi Nassoro Chuma , Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga Ally Msikamo na mganga mfawidhi wa Zahanati ya Marogoroni Zulfa Makubui wakizundua nyumba ya mganga wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.

Mbali na ujenzi wa barabara pia tayari wakala wa barabara za vujijini na mijini (TARURA) wameshaanza mradi wa ujenzi wa daraja la kijiji cha Sangatini utakaogharimu kiasi cha milioni 122. 


Wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri Ulenga aliweza kuzindua Zahanati ya Mfuru Mwambao iliyojngwa kwa msaada wa kanisa na kisha kukabidhiwa kwa wanakijiji ikiwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba ya mganga na upatikanaji wa dawa kutoka bohari ya dawa ya taifa (MSD).

Pia kweye kijiji cha Marogoro Ulega alizindua nyumba ya mganga na aliweza kwenda kuona ujenzi wa shule ya msingi Sangatini iliyojengwa kwa nguvu za wananchi ikigharimu milioni 13.5 kwa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja ya mwalimu, na katika shule ya msingi Marogoro aliweza kutoa kiasi cha shillingi laki tatu (300,000) na mifuko 30 ya saruji kwa ajili ukarabati wa madarasa.

Akizungumza na wananchi mbalimbali Ulega amewataka kulitumia eneo lililokuwa limehifadhiwa kwa muda mrefu na likiwa limetengwa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege kwa kuendelea kufanya shughuli zao kijmaii namaendeleo.

Ulega atakuwa na ziara ya siku tatu akitembelea kata mbalimali za jimbo la Mkuranga na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ambapo hilo linmekuwa ni kawaida yake mara kwa mara kukaa na wananchi wake na kuwasikiliza.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akizunumza na wanakijiji wa Mfuru Mwambao wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiweka tofali kwenye kuendeleza ujenzi wa shule ya msingi Msangatini wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiwa sambamba na diwani wa kata ya Vianzi Nassoro Chuma wakizuru katika shule ya msingi Marogoro wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.Picha na Emmanuel Massaka.

DK KISSUI WA MKIKITA AWATAKA WATANZANIA KUOTA NDOTO KUBWA ZA MAFANIKIO

$
0
0
Na Richard Mwaikenda- Canre, Bonyokwa.

WATANZANIA wametakiwa kuota ndoto kubwa badala ya ndogo ili kupata mafanikio makubwa katika maisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), wakati wa mafunzo ya Kilimo Biashara kwa walimu na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo, Mifugo na Maliasili (Canre), Dar es Salaam.

"Ukitaka kufanikiwa Ota ndoto kubwa "Bring Big Dream" , acha kuota ndoto ndogo za kitoto zitakazokuchelewesha kupiga hatua za kimaendeleo," alisema Dk. Kissui ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kiuchumi.
Alisema daima amini kwamba ndoto unayoota itakuletea mafanikio chanya na utakuwa nani mbele ya safari.Pia, Dk. Kissui, aliataka watanzania kuachana na tabia ya kutegemea chanzo kimoja cha mapato, bali wawe na ujuzi mwingi, na kubuni vyanzo vingi vya kuwawezesha kumudu maisha yao ya kila siku.

Alisema moja jambo litakalowatoa kwenye lindi la umasikini ni Kilimo Biashara chenye mtazamo wa kuanza kutafuta masoko ndipo ulime zao kwa kiwango na ubora unaotakiwa na mnunuzi.Dk. Kissui alisema kuwa Mkikita inaendesha kilimo kwa kufuata utaratibu huo wa kuanza na masoko halafu ndo kinafuata kilimo. Hivi sasa Mtandao huo unaendesha kilimo cha Papai Salama, Muhogo, Mchaichai na Pilipili kichaa mazao ambayo yote yamepata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkikita, Dk. Kissui S.Kissui (katikati), akizungumza katika semina ya mafunzo ya kilimo biashara katika Chuo cha Kilimo cha Canre, Dar es Salaam. 

MUWSA MABINGWA UTOAJI HUDUMA BORA ZA MAJI TANZANIA

$
0
0
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji,Aisack Kamwelwe ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuukagua mradi wa maji wa Buchosa uliopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kwani anazotaarifa kuna vifaa vimenunuliwa havina ubora kabisa.

Maagizo hayo aliyatoa jana Mjini hapa wakati akizindua ripoti na utendaji wa Mamlaka za Maji za Miji na Mikoa na miradi ya kitaifa.


Uzinduzi huo uliandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo Mamlaka ya Maji ya Moshi ilichaguliwa kuwa ya kwanza kwa utoaji bora wa huduma za maji. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe (kulia) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa Mamlaka inayotoa huduma bora za Maji Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) ,Prof. Faustine Bee. Kushoto ni Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa MUWSA, Joyce Msiru. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma juzi.

MABALOZI WALIOAPISHWA JANA WAMUAGA MAKAMU WA RAIS LEO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wakutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

Mabalozi hao ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam .Makamu wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais

“Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa, Balozi Slaa alifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga akiwa tayari kuelekea kwenye kituo chake kipya cha kazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto aliyefika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo kipya cha kazi, katikati ni Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Bondia Francis Cheka apewa Ubalozi-Mtwara.

$
0
0

Chama cha Urafiki wa Wananchi wa Nchi ya Tanzania Na Msumbiji TAMOFA Kimempa Ubalozi Bondia wa Kimataifa Francis Cheka Ili kuweza Kutangaza Chama Hicho kwa lengo la Kujipatia wafadhili ndani na nje ya nchi.

Akiongea mara baada ya makabidhiano ya kadi ya ubalozi Mkoani Mtwara Francis Cheka anasema Urafiki wa msumbiji na Tanzania Umekuwa wa Muda Mrefu na hivyo kuhamasisha wananchii kujiunga na chama hicho hasa wale wanaofanya safari katika nchi hizo mbili.

Hamza Lichete ni katibu mwenezi wa TAMOFA anasema kazi kubwa ya chama hicho ni kuimarisha Mahusiano pamoja na kulinda  Umoja  kati ya nchi hizi mbili kwa lengo la kuimarisha uchumi pamoja na amani.

Cheka ambaye kwa sasa anaishi Mkoani Mtwara amezaliwa Nchini Msumbiji lakini kwa kiasi kikubwa amekuwa akiitangaza Tanzania katika mapambano mbalimbali ya Kimataifa ambayo yamempatia umaarufu yeye pamoja  Na Nchi ya Tanzania

Chama cha TAMOFA kiliasisiwa na marasi Hayati Jullius Kambarage Nyerere pamoja na Samora Mashel mwaka 1987.
Bondia Francis Cheka akiwa amesimama Mbele ya Jengo la Ofisi ya TAMOFA maara baada ya Kupewa Ubalozi wa Chama Hicho Mkoani Mtwara.
 Bondia Francis Cheka akionesha Kadi ya Ubalozi wa TAMOFA kwa Waandishi wa Habari Mara Baada ya Kukabidhiwa Mkoani Mtwara.
Picha1.Mwenyekiti wa TAMOFA Kanda ya Kusini Seleman Mstapha Akimkabidhi Kadi ya Ubalozi wa TAMOFS bondia Francis Cheka Mkoani Mtwara.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO FEBRUARY 18,2018

INTRODUCING "BAKORA" (OFFICIAL MUSIC VIDEO) BY WAKAZI


furaha ya mrejesho wa kitabu cha africans and americans

$
0
0

Na Profesa Joseph Mbele
Ni furaha na faraja kwangu kama mwandishi kupata mrejesho kutoka kwa wasomaji. Leo asubuhi, nilipoamka, niliona ujumbe kutoka kwa mwalimu wa chuo cha St. Lawrence. Ameandika:

Mimi ni ndugu Kitito. Tulikuwa wageni wako katika kongamano la African network. Mimi na Robin tunashukuru mno kwa kitabu chako "Africans and Americans." Tunakitumia darasani mwetu. Wanafunzi wamefaidika mno...

Huyu mwalimu Robin anayetajwa nilishaandika habari zake katika blogu hii. Baada ya mimi kusoma ujumbe wake, mwalimu Kitito amenipigia simu, akanielezea zaidi kuhusu kitabu kinavyotumiwa. Nami nilimwelezea nilivyokiandika, baada ya miaka mingi ya kukabiliana na maisha ya Marekani. Nilimweleza kwa nini nilitumia mtindo ambao si kawaida kwa wanataaluma.

Nimefarijika kupata mrejesho kutoka kwa waalimu hao ambao wanatumia kitabu changu, nami nimeona niweke kumbukumbu hii hapa, kama ilivyo kawaida yangu. 

Bamiza Music Chart 17th February, 2018

WAZIRI MBARAWA AITAKA TBA KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI

$
0
0
 Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amemtaka Wakala wa Majengo  hapa nchini (TBA), kuhakikisha anakamilisha kwa wakati  ujenzi wa miradi mbalimbali anayotekeleza.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa Hospitali  ya Mkoa, Nyumba za Viongozi wa Mkoa zinazojengwa na Wakala huyo eneo la Nyaumata mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani  Simiyu. 
Amesema kuwa TBA ni Taasisi ya Serikali  ambayo imeaminiwa na Serikali kwa kuwa  inafanya kazi vizuri lakini imekuwa ikichelewa kukamilisha miradi inayopewa  tofauti na muda uliowekwa kulingana na mikataba. 
“TBA ni Taasisi ya Serikali na katika Serikali hii ya awamu ya tano tumeipa miradi mingi tukiamini kuwa watafanya kazi nzuri zenye ubora na kukamilika kwa wakati, ubora upo lakini tatizo kubwa ni kutomaliza kazi kwa wakati” alisema Waziri Mbarawa. 
“TBA mjipange mhakikishe mnamaliza miradi kwa wakati vinginevyo hatutawapa kazi kwa sababu hatuwezi kuwapa fedha za Serikali jengo la mwaka mmoja mnajenga miaka mitano, naamini mkijipanga vizuri uwezo mnao na Serikali inawaamini” alisema Mbarawa.
Naye  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pia ametoa wito kwa Wakala wa majengo TBA kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo ili viongozi waweze kupata makazi. 
Wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema kuwa ameshalipa fedha kwa TBA ili waweze kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa na wameahidi kukamilisha na kukabidhi nyumba hizo mwezi Mei mwaka huu.
Awali akitoa maelezo ya Miradi inayotekelezwa na TBA mkoani Simiyu, Meneja wa TBA mkoani humo Mhandisi.Likimaitare Naunga  amesema wanashindwa kukamilisha baadhi ya miradi kwa wakati kutokana na kucheleweshewa fedha.
 Meneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu.Mhandisi.Likimaitare Naunga(katikati) akitoa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alipotembelea mradi huo wakati wa ziara yake Mkoani humo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa TBA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Likimaitare Naunga(kulia) wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo unaotekelezwa na TBA wakati wa ziara yake Mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa(mwenye kofia) na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakielekea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Katibu Tawala Mkoa ili aweze kukagua mradi huo wakati wa ziara yake Mkoani humo.

KAIMU MKURUGENZI WA VIWANJA VYA NDEGE AIOMBA SERIKALI KUTOA KIPAUMBELE UJENZI WA UWANJA WA NDEGE SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA),  Richard Mayongela ameiomba serikali kutoa kiupaumbele cha ujenzi wa Viwanja vya Ndege kwa mikoa ya Simiyu na Lindi katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ili kuongeza fursa za uwekezaji na utalii. 
Mayongela ametoa ombi hilo katika kijiji cha IGEGU kata ya Sapiwi wilayani  BARIADI katika eneo linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Prof. Makame Mbarawa mkoani Simiyu. 
Amesema hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa Uwanja huo zimekamilika ambapo usanifu na upembuzi yakinifu vimeshafanyika na makadirio ya awali yanaonesha kuwa mradi huo utagharimu takribani shilingi bilioni 95.56 na utakapokamilika utawezesha ndege zenye uwezo wa kubeba  kuanzia watu 75 na kuendelea kutua.
Ameongeza kuwa Ujenzi wa Uwanja huo utakapokamilika utakuwa ni chachu ya maendeleo kwa Mkoa huo katika nyanja za uchumi na utalii  na utachangia kuufungua mkoa wa Simiyu kiuchumi pamoja na mikoa mingine ya kanda ya Ziwa. 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kukamilika kwa Uwanja huo itakuwa ni faida kubwa kwa kuwa utakuwa  Uwanja pekee wa Serikali hapa nchini ambao Watalii watautumia kuifikia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa urahisi kuliko viwanja vingine.  
“Tunajenga Uwanja ambao kimkakati unakaa mpakani mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, karibu na uwanja huu kuna hii barabara ya inayotunganisha na Mkoa wa Shinyanga kupitia Malampaka ambako kutajengwa Reli ya Kisasa, hapa jirani  tuna eneo ambalo tutajenga Kiwanda cha Vifaa tiba, mbele yeke tunaanzisha Kanda ya Nanenane ...tunaamini kukamilika kwa mradi huu kutakuwa na faida sana  kwa Serikali na wananchi”  alisema Mtaka.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini,  Richard Mayongele (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(mwenye kofia)  kuhusu Uwanja wa Ndege wa mkoa wa Simiyu unaotarajiwa kujengwa Kijiji cha Igegu wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Waziri huyo leo Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akieleza juu ya umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa mkoa unaotarajiwa kujengwa Kijiji cha Igegu wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa  akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu, unaotarajiwa kujengwa Kijiji cha Igegu wilayani Bariadi wakati wa ziara yake leo Mkoani humo.
 Mkuruugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela akiwasilisha taarifa ya eneo la Igegu wilayani Bariadi linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege Mkoani Simiyu  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa alipokuwa kwenye ziara mkoani humo leo.
Diwani wa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi akimweleza jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa(kushoto) alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege Mkoani Simiyu, wakati alipokuwa katika ziara Mkoani Simiyu leo .

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ziarani Mkoa wa Mara

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakizungumza na Noella Tekela, mwanafunzi wa darasa la sita katika  shule ya msingi ya Masaunga wilayani Bunda baada ya kuwahutubia wavuvi, wafanyabiashara wa samaki na wananchi  kwenye kijiji cha Kisorya  Februari 17, 2018. Mtoto huyo alionekana akiandika kwa usahihi katika daftari hotuba yote ya Waziri Mkuu katika mkutano huo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmiliki wa Pantoni ya MV Nyehunge, Said Mohammed  kwenye gati la Kirumba wakati aliposafiri  na chombo hicho kutoka jijini Mwanza kwenda Ukerewe leo Februari 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Pantoni ya MV Nyehunge  kwenye gati la Kirumba wakati aliposafiri na chombo hicho kutoka jijini Mwanza kwenda Ukerewe leo Februari 18, 2018.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images