Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

DK. KIGWANGALLA AMALIZA MGOGORO WA HIFADHI NA WANANCHI WILAYANI RUFIJI

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Utete katika wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa ili kumaliza mgogoro huo.

Na Hamza Temba (WMU) -  Rufiji, Pwani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka minne baina ya Hifadhi ya Msitu wa Utete maarufu kama Msitu wa Kale na vitongoji vinavyopakana na hifadhi hiyo vya Siasa, Nyawanje, Kindwitwi na Utunge katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Dk. Kigwangalla amemaliza mgogoro huo kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuunda timu ya wataalamu watakaoshirikiana na wataalamu wa mkoa wa Pwani na wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kufanya tathmini ya eneo lenye mgogoro na kuanzisha mchakato wa kisheria wa kurekebisha mipaka ya eneo hilo na hatimaye kuligawa kwa wananchi.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Utete, wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi mkoani humo.
“Nimejiridhisha kwamba hakutokuwa na madhara yeyote yale, kama tutamega eneo la msitu wa Hifadhi kidogo ambalo wananchi wamekuwa wakilima miaka yote hii na kulirusha kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo kuliko kuendelea kulihifadhi wakati wananchi wanakosa mahala pa kupata riziki yao.
“Naagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, uunde timu ya wataalam waje washirikiane na wataalam wa mkoa na wilaya, wafanye tathmini kwenye lile eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilima kabla hata msitu haujawa ‘gazerted’ (haujatagazwa) kuwa hifadhi ili muone ni kwa kiasi gani mnaweza mkamega eneo na kulirudisha kwa wananchi ili waweze kuendelea na kilimo,” aliagiza Dk. Kigwangalla.


Ameagiza pia kamati hiyo ifanye tathmini ya eneo la chemchem ambalo ni sehemu ya hifadhi hiyo ambalo limevamiwa kwa kiasi kikubwa na makazi ya wananchi ili waweze kurekebisha mipaka yake na hatimaye wananchi wabaki na eneo lao la makazi na eneo litakalobakia liendelee kuhifadhiwa.


“Kamati hiyo pia ije ifanye tahtmini inawezaje kuhamisha mipaka ya hifadhi ili kupisha zile nyumba ambazo zimeshajengwa pale kwa sasa na hapo sasa wananchi wawe hawana mgogoro na hifadhi, waishi kwenye eneo lao na waiache hifadhi upande wa pili, lakini sasa waishi kwa mujibu wa sheria kuliko ilivyo hivi sasa tunavyowachukulia kama wavamizi;” alisema Dk. Kigwangalla.
Aidha Dk. Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kutafuta eneo mbadala la msitu ambalo ni mali ya vijiji likabidhiwe kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ili liweze kuhifadhiwa ikiwa ni fidia ya eneo hilo la Hifadhi ya Msitu wa Utete litakalokabidhiwa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo na makazi.
Mbali na maagizo hayo Dk. Kigwangalla ameagiza pia wananchi waliolima kwenye bonde katika Hifadhi hiyo wasiondolewe katika msimu huu wa kilimo wakati zoezi la uwekaji wa mipaka likiwa linaendelea.


Hifadhi ya Msitu wa Utete ilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 1cap 132p 1351 la tarehe 1 Oktoba, 1957 ikiwa na jumla ya ekari 2,346. Desemba 2015 msitu huo ulipimwa tena na kuchorewa ramani.
Wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo wamedai kuwepo katika baadhi ya maeneo hayo ya hifadhi hata kabla ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo, hivyo wameiomba Serikali iwamegee maeneo katika hifadhi hiyo ili waweze kuendeleza shughuli zao za kilimo na makazi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuhusu kivutio cha utalii cha Chemchem ya Maji ya Moto yanayofikia nyuzi joto 75 katika Msitu wa Hifadhi wa Chemchem wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijadili jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rufiji, Rajab Mbonde na Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa ili kumaliza mgogoro huo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rufiji, Rajab Mbonde kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa ili kumaliza mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa. 

Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan  Kushoto akisalimiana na Kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es salaam.
Mh. Samia Suluhu Hassan Kulia akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Mikutano na Vikao vya kawaida vya kubadilishana mawazo ya kiutendaji  Serikalini kati ya Viongozi wa ngazi ya Juu ya Serikali za SMT na SMZ. Picha na – OMPR – ZNZ.

Tutafanya Kazi kwa Maslahi ya Taifa - Balozi Dkt. Slaa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Kilangi atembelea Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu

$
0
0
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dk. Adelardus Kilangi akijadiliana jambo na  Majaji wa Mahakama ya  Haki  ya  Afrika ya   Mashariki  (EACJ) wakati alipoitembelea mahakama jijini Arusha Ijumaa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dk, Adelardus Kilangi akiwa katika mazungumzo na  Rais wa Mahakama   ya Haki ya Afrika Mashariki ( EACJ), Mhe Jaji Dk. Emmanuel Ugirashebuja na katika mazungumzo yao Rais wa  EACJ alimweleza Mwanasheria Mkuu kwamba mahakama hiyo imekuwa ikizitegemea  Ofisi za Wanasheria Wakuu ikiwamo  ya Tanzania katika utekelezaji wa Majukumu yake.

 Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Mhe. Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazungumzo na Rais wa  Mahakama   ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu  (AfCHPR) Jaji  Sylvain Ore walipokuta  Jijini  Arusha. Katika mazungumzo yao, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliahidi kushirikiana wa Mahakama hiyo ambapo kwa upande wake Rais wa  AfCHPR alisema mahakama hiyo imekuwa ikipata ushirikiano mzuri kutoka kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa Mawakili wa Serikali ambao wamekuwa wakiiwakilisha serikali katika mashauri mbalimbali.. Mwingine katika picha ni Katibu wa Mwanasheria Mkuu, Wakili wa Serikalil Mkuu  Ephery Sedekea.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiangalia namna mfumo wa   habari  na mawasiliano wa mahakama hiyo unavyofanya kazi wakati alipoitembelea  Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki  leo Arusha


UNNewsKiswahili: Sikukuu ya wapendanao yaleta nuru kwa Dominica

DKT. MWIGULU AMUAGIZA IGP KUFANYA UCHUNGUZI MAUAJI YA DANIEL JOHN

RC MAKONDA APOKEA SHEHENA YA MAKONTENA YENYE SAMANI ZA OFISI ZA WALIMU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea shehena ya Makontena 20 Kati ya 36 yenye samani (furniture) zenye thamani ya Shillingi Billion 2 zilizotolewa na Diaspora waishio Nchini Marekani waliounga mkono kampeni ya RC Makonda ya ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar es salaam.

Ndani ya Kontena hizo zipo Meza za umeme zenye hadhi ya kimataifa 2500, Meza za kawaida 2500,Viti zaidi ya 5,000,Makabati makubwa ya vitabu 1300, Ubao za kisasa (writing board) zisizotumia chaki 700 ambazo kwa kiasi kikubwa utaenda kupunguza mateso ya walimu kuumwa vifua kutokana na vumbi la chaki.
IMG-20180216-WA0072
Vifaa hivyo vya kisasa vimetolewa na Jumuiya ya watanzania waishio Marekani ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington iliyomuunga mkono RC Makonda kutokana na kuguswa na kazi kubwa anayoifanya kwenye kuboresha mazingira ya walimu.
IMG-20180216-WA0073
Akizungumza wakati wa kupokea makontena hayo RC Makonda amesema jumla ya kontena zilizotolewa na jumuiya hiyo ni 36 na Kati ya hiyo 20 yamefika na mengine 16 yapo njiani ambapo ameshukuru jumuiya kwa kutambua thamani ya mwalimu.

RC Makonda amesema lengo lake ni kuboresha mazingira ya walimu na kurejesha heshima yao ili  wapate morali ya kufundisha wanafunzi na mwisho wa siku kusaidia taifa kuwa na wataalamu wa kutosha. 
IMG-20180216-WA0071
Aidha ameshukuru Bank ya Walimu kwa kusaidia kulipia usafirishaji wa makontena matatu na kuwaomba wadau kusaidia kulipia gharama za usafiri wa makontena mengine Kama mchango wa kutambua thamani ya mwalimu.
Walimu walioshuhudia makontena hayo wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyoboresha mazingira yao ya kufanya kazi na kueleza kuwa vifaa walivyovishuhudia leo wanaamini sasa watafanya kazi kwa bidii zaidi na kuongeza ufaulu kwa walimu.

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO FEBRUARY 17,2018


POLISI NA CRDB WATOA ELIMU KWA WANANCHI MKOANI LINDI JUU YA WIZI KATIKA MITANDAO

$
0
0
 Jeshi la Polisi kitengo cha Polisi Jamii kutoka Polisi Makao Makuu Dar es salaam likiongozwa na Naibu Kamishina wa Polisi  DCP Ahmada Khamis, pamoja na Maafisa kutoka Bank ya CRDB wametoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank.
 Naibu Kamishina wa Polisi  DCP Ahmada Khamis akitoa  elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank.
Afisa kutoka Bank ya CRDB akitoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 16.02.2018

MHE MUDHIHIR M MUDHIHIR NDANI YA KIPINDI CHA DANGA CHEE

MAFUNZO YA MSAADA HUDUMA ZA KISAIKOLOJIA KWA WAHUDUMU VITUO VYA HUDUMA,TIBA MWANZA YAFUNGWA

$
0
0
Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele amefunga mafunzo ya siku tano kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya huduma na tiba kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vilivyopo katika halmashauri 7 za wilaya mkoa wa Mwanza. 

Mafunzo hayo yalikuwa yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Midland Hotel jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Februari 12,2018 hadi Ijumaa 16 Februari ,2018 yakiendeshwa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC). 

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Dk. Masele aliwataka wahudumu hao wa jamii kutumia vyema ujuzi na elimu waliyopewa ili wakaboreshe huduma za afya kwenye vituo vyao. "Nawashukuru AGPAHI kwa kutoa mafunzo haya,naamini mafunzo mliyopata yawatasaidia pia katika kuwaelimisha na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma",aliongeza Dk. Masele. 

Nao washiriki wa mafunzo hayo, Hawa Radhamani kutoka hospitali ya wilaya ya Misungwi Kija Robert kutoka kituo cha afya Nyamilama halmashauri ya wilaya ya Kwimba walisema wamepata uelewa mkubwa kuhusu masuala ya VVU na Ukimwi yatawasaidia kuboresha zaidi huduma za afya kwenye vituo vyao na jamii kwa ujumla. 
Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele akifunga mafunzo ya siku tano kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii kutoka halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza.
Dk. Masele akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Sospeter Lameck kutoka halmashauri ya wilaya ya Buchosa.Wa kwanza kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona. Wengine wawezeshaji wakati wa mafunzo hayo Dk. Joseph Musagasa (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Gaston Kakungu ambaye ni Afisa Muuguzi Mstaafu.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akifundisha namna ya kujaza taarifa katika daftari la mtoa huduma za VVU na Ukimwi katika jamii. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakijaza fomu ya namna ya kufuatilia wateja waliopotea katika huduma. 

RC MTAKA ASITISHA MALIPO YA SHILINGI BILIONI 1.9 KWA WAKANDARASI WALIOSHINDWA KUKAMILISHA MIRADI

$
0
0
Na Stella Kalinga

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesitisha malipo ya shilingi bilioni 1.9 kwa wakandarasi watatu, ambao ni Simiyu Investiment Co. Ltd, Nselema Associtates Co. Ltd na Great Lakes Construction Co.LTD, wanaotekeleza miradi saba ya maji wilayani MEATU ambayo imeshindwa kukamilika tangu mwaka 2014.

Agizo hilo amelitoa wilayani Meatu, mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Lubiga, Itinje na Bukundi na kutoridhishwa na kazi iliyofanyika.

“Tunasitisha malipo yote ya wakandarasi watatu wanatekeleza miradi saba ya maji ndani ya Wilaya ya Meatu, malipo yafanyike baada ya Wataalam wetu wanasheria, wahandisi wa maji wa Halmashauri ya Meatu, Mhandisi wa Maji Mkoa, Mwanasheria ya Mkoa na timu ya Mkoa kujiridhisha; ikiwa wanastahili kulipwa watalipwa ikibainika hawana sifa tunavunja mkataba” alisisitiza Mtaka.

Pamoja na kusitisha malipo hayo Mtaka amesema makampuni hayo hayataruhusiwa kufanya kazi za ukandarasi katika miradi yoyote wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthoy Mtaka(kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na Wilaya ya Meatu wakiondoka eneo la mradi wa maji wa Itinje mara baada ya kukagua mradi huo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akitoa maelezo juu ya mradi wa Lubiga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akihoji jambo juu ya ujenzi wa tanki katika mradi wa Maji wa Itinje wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akifafanua jambo wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani humo.

Introducing HAPPY (Official Music Audio) by Juma Kakere

AHUKUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA WIZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA MANYONI-ITIGI CHAYA

$
0
0
Na-Jumbe Ismailly MANYONI  

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida imemuhukumu Musa Haruna (47) mkazi wa Kijiji cha Mtimkavu,kata ya Itigi,wilayani Manyoni kutumikia adhabu ya mwaka mmoja jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la wizi wa bomba tatu za chuma zenye thamani ya shilingi milioni mbili laki mbili elfu na themanini mali ya Wakala wa barabara Tanzania(TANROADS).
Mahakama hiyo ilimtia hatiani mshitakiwa baada ya kukiri na kukubaliana na hoja zote za mashtaka,ikiewemo kukamatwa na bomba tatu za chuma zilizopatikana kwa njia isiyo halali,kufikishwa polisi na kufikishwa Mahakamani.
Awali Mwendesha Mashtaka wa serikali,Geofrey Luhanga alidai kwamba sept,23,mwaka jana saa 1;30 usiku katika eneo la mtaa wa Majengo,mjini Itigi,Musa Haruna alikutwa na bomba za chuma tatu zenye thamani ya shilingi milioni 2 na laki mbili elfu na themanini zilizopatikana kwa njia isiyo halali mali ya Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS).
Aidha Luhanga alidai pia kwamba hakuna kumbukumbu za makosa ya nyuma hivyo aliiomba Mahakama hiyo kwamba adhabu zinazotolewa na Mahakama kwa makosa ya aina hiyo ziwe kali ili ziwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka huyo wa serikali mabomba hayo yalikuwa yakitumika kwa alama mbali mbali za barabarani na makosa hayo yamefanywa kwa makusudi na mshitakiwa huyo na kutokana na kukosekana kwa alama hizo imekuwa vigumu kwa watumiaji barabara kujua maeneo hatarishi kwa kuwa hakuna alama zinazoonyesha tahadhari hizo.

Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere atembelea mpaka kati ya Tanzania na Zambia

$
0
0
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwa ameshikilia jiwe la mpaka kati ya Tanzania na Zambia katika Kituo cha Forodha cha Mosi kilichopo Mkoani Rukwa, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za utendaji wa Mamlaka hiyo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye tai nyekundu) akiwa akiangalia jiwe la mpaka kati ya Tanzania na Zambia katika Kituo cha Forodha cha Mosi kilichopo Mkoani Rukwa, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za utendaji wa Mamlaka hiyo.

wananchi wa kawe jijini Dar es salaam waomba serikali kuingilia kati mgogoro wa kiwanja chenye msikiti

$
0
0
 Mwanaharakati na Mzawa Kawe James Mwakibinga akizungumza na wakazi wa Kawe wakati walipokuwa wakitoa ombi lao kwa Rais Magufuli kupitia Waziri Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuingilia kati mgogoro wa kiwanja namba 196 kilichojengwa Msikiti ambapo mmoja ya mfanyabiashara mmoja  anataka kuubomoa Msikiti huo
 Katibu wa Msikiti huo akitoa tamko la Msikiti kutangaza kuwa hawakubaliani kamwe na maamuzi ya Mahakama kwa madai kuwa  haki aikutendeka katika utekelezwaji wa hukumu yao ya kutaka msikiti huo uvunjwe
Sehemu ya Waandishi wa Habari na Wakazi wa Kawe wakifatilia kwa Makini Mkutano wa Msikiti wa Kawe ukwamani kupinga kubomolewa Msikiti wao na Wafanyabiashara.

PROF. MBARAWA AAHIDI KUKAMILIKA KWA UJENZI WA DARAJA LA MTO MARA

$
0
0
Serikali imesema ujenzi wa daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 lililopo katika barabara ya Tarime-Mugumu-Nata litakamilika mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka huu.

Amezungumza hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua ujenzi wa daraja hilo ambalo linaunganisha wilaya ya Tarime na Serengeti na kuwatoa hofu wananchi wa wilaya hizo kuwa endapo daraja hilo likikamilika litaondosha adha waliyokuwa wanaipata ya kuvuka hasa vipindi vya masika.

“Niwahakikishieni daraja hili litamalizika mapema mwezi wa nne pia nimemuagiza mkandarasi huyu ambaye ni mzawa kuhakikisha anazingatia viwango na wakati” amesema Prof. Mbarawa.Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo itakuwa dira kwa wakandarasi wazawa kupewa miradi mikubwa kwani pamekuwa na changamoto kwenye utekelezaji wa miradi hususani kwa wakandarasi wazawa.

Kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya M/S Gemen Engineering & Mayanga, Mhandisi Andrew Nyamtori, amesema kuwa mradi umekamilika kwa sehemu kubwa hivyo kazi zilizobakia ni kutandika vyuma juu ya daraja ili likamilike na kuanza kutumika na hivyo kuiomba Serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wazawa kwa kuwapa miradi mingine mikubwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Gemen Engineering & Mayanga, Mhandisi Andrew Nyamtori (kulia), alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Mara, linalounganisha Wilaya ya Tarime na Serengeti, Mkoani Mara.
Muonekano wa Daraja la Mto Mara lenye urefu wa Mita 94 na kuunganisha Wilaya za Tarime na Serengeti likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Bertha Bankwa, wakati akikagua kiwanja hicho. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (wa pili kulia) mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Mara, linalounganisha Wilaya ya Tarime na Serengeti, Mkoani Mara.

Tuna kila sababu ya kumuita Mother Fii

$
0
0

Tarehe 13 Februari 2018, mwanzilishi wa Sekondari ya Kifungilo Sr. Mary Fidesta Rimisho C.P.S., alitangulia mbele ya haki. Kikawaida kila mtu ana wazazi wa kumzaa, wa kumlea au wakujitolea ambao huwa wanampatia mwongozo. Sr. Fidesta, akiwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kifungilo amesimamia watoto wengi wa kike kwa kuwapatia elimu na mafunzo mengine ya Maisha.

Unapotokea msiba watu wa karibu wanaumia sana, na msiba huu wa Sr. Fidesta hauna tofauti. Wote tulimuita Mother Fii, kwani alikuwa Mama yetu. Wengi wetu tulikutana naye awali tukiwa na umri mdogo (miaka 7 hadi 18). Mother Fii alitujengea msingi imara katika kusali, kujali wengine, kujiamini, kuongoza, kuelimika na uwajibikaji. Vile vile misingi katika kupongeza na kushukuru. 
Mother Fii ni mama wa ukweli, alikuwa mwepesi kupongeza na kukemea kila wakati bila upendeleo, kiukweli usawa kwake ulikuwa muhimu. Kwa Mother Fii nidhamu ya muda ndio msingi wa kuishi kwa amani na kutimiza ahadi zote za msingi. Alitupa Kanuni ya Dhahabu, "Usimtendee mwenzako usichopenda kutendewa wewe."
Mother Fii pia alitupa fursa ya kuendeleza vipaji mbalimbali. Tuliweza kumudu elimu, kazi za nyumbani na sasa hata  tunaendeleza msingi huu tulioupata kitambo. Wote tuliosoma Kifungilo tuna fahari kuwa familia kubwa inayojali utu wa kila mtu kutokana na uwezo na kipaji chake tu, sio fedha, mali au cheo. 
Kweli Mother Fii alikuwa zaidi ya Mwalimu kwani kama wanawake alitupatia ufunguo mkubwa katika maisha yetu.
Kweli Mother Fii mwendo umeumaliza, nasi umetuachia jukumu la kuwafundisha watoto, hasa watoto wa kike, umuhimu wa kufanya kila jambo kwa umakini. Tumekuwa viongozi, waalimu, madaktari, wanasheria, wajasiriamali na chochote tunachotaka kupitia misingi uliyotulea.


Asante sana kwa mambo yote mema 
Sr.   Fidesta (Mother Fii). 


Tutakuenzi Daima.

Pumzika kwa Amani Mama
Wanakifungilo

Dkt. Makame ashiriki katika uzinduzi wa Kiti cha AXA cha Uchumi na Fedha katika Chuo Kikuu Cha London

$
0
0
Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mheshimiwa Dkt Abdullah Hasnuu Makame (PhD) ameshiriki kama Mgeni Mashuhuri wa uzinduzi wa Kiti cha AXA cha Uchumi na Fedha katika Chuo Kikuu Cha London {School of Oriental and African Studies). AXA ni taasisi ya kifedha ya kimataifa yenye makao makuu yake nchini Uingereza; ambayo hivi Karibuni imebuni Kiti hicho kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha London kwa lengo la kufanya utafiti utakaowezesha miradi ya kupambana na umasikini katika Bara la Afrika. Kiti hicho kwa sasa kinakaliwa na Profesa Victor Murinde ambaye kabla ya hapo alikuwa Chuo Kikuu Cha Birmingham. Dkt Makame na Profesa Murinde Washachapisha makala mbalimbali za kitaaluma ya maeneo ya Uchumi na fedha katika majarida na makongamano mbalimbali.
 Kutoka kushoto ni Bi. Annabel Bligh Mhariri wa Biashara na Uchumi katika shirika la The Conversation UK, Hassan El-Shabrawishi Afisa Maendeleo wa Mikakati wa Afrika wa AXA, Bi Christine Oughton Profesa wa Utawala wa Uchumi  - SOAS - Chuo Kikuu Cha London, Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mheshimiwa Dkt Abdullah Hasnuu Makame. Bw Laurent Clavel Mkuu wa Divisheni ya Utafiti wa Uchumi  AXA, Profesa Victor Murinde, Mwenyekiti  wa AXA Uchumi na Fedha na Dkt George Kararach Mtafiti Mwandamizi wa Kamisheni ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA
 Mheshimiwa Dkt Abdullah Makame akiwasilisha neno la uzinduzi wa Kiti akisikilizwa na Profesa Christine Oughton
 Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mheshimiwa Dkt Abdullah Hasnuu Makame akichangia mada. Pembeni yake ni  Dkt. Hassan El-Shabrawishi Afisa Maendeleo wa Mikakati wa Afrika wa AXA
 Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mheshimiwa Dkt Abdullah Hasnuu Makame akibadilishana mawazo na mmoja wa washiriki katika uzinduzi wa Kiti cha AXA cha Uchumi na Fedha katika Chuo Kikuu Cha London {School of Oriental and African Studies).

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images