Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

DMF, MAKJUICE WAWAPA FARAJA WAZAZI WA WATOTO NJITI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR KATIKA SIKU YA WAPENDANAO

$
0
0
 Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa wauguzi wa zamu wa Wadi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala, sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali hiyo ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya kuonyeshana upendo (Valentine's Day) ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Februari 14. Taasisi ya Doris Mollel walishirikiana na Kampuni ya MakJuice na baadhi ya wapigapicha, wanahabari pomoja na wadau wengine waliojitoa kufanikisha zoezi hilo, lililofanyika jana jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Warda Walid (Muwakilishi wa Taasisi ya DMF Zanzibar), Mariam Gerion (DMF Dar es salaam), Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee pamoja na baadhi ya wauguzi wa Hospitali hiyo.
 Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo pamoja na vitu vingine mbalimbali.
 Muwakiliwa wa Kampuni ya MakJuice, Zahir akimkabidhi zawadi ya khanga mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo na mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
 Wakinamama waliojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), wakipoza koo zao na Juice za Mak walipotembelea Hospitalini hapo.

WABUNGE CCM WAMIMINIKA KUMUOMBEA KURA MTULIA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali wameendelea kunadi sera za maendeleo na kumuombea kura mgombea wao wa ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam huku baadhi yao wakisema uchaguzi huo ni sawa na usajili wa dirisha dogo.

Hivyo wanatumia usajili huo kwa ajili ya kumpata Mtulia ambaye wanaamini ni mtu sahihi kwa maendeleo ya wananchi wa Kinondoni kwani alikokuwa awali hakuwa nafasi ya kushirikiana na Serikali ya Rais ,Dk.John Magufuli kufanya maendeleo.

Wakizungumza kwenye kampeni za uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Februari 17(Jumamosi ya wiki hii), viongozi wa CCM wakiwamo baadhi ya mawaziri ambao wamefika kwenye kampeni hizo kwa nafasi zao za ubunge,wamewaambia wananchi hao Mtulia ndio mtu sahihi kwao.

Mgeni rasmi kwenye kampeni zilizofanyika leo Kata ya Ndugumbi ambaye pia ni mbunge wa Mbinga Sixtus Mapunda amesema anatambua uwezo wa Mtulia na hivyo ni vema wananchi wakamchagua ili awatumikie kikamilifu.

Amewaeleza wananchi kuwa uchaguzi mkuu ulishafanyika mwaka 2015 na sasa ni uchaguzi mdogo ,hivyo Chama ambacho kimepewa dhamana ya kuongoza ni CCM na kwa maana hiyo Mtulia akiwa mbunge atashirikiana na viongozi wengine kuleta maendeleo ya wananchi.

Amefafanua anaufananisha uchaguzi huo na usajili wa dirisha dogo ambapo tayari CCM wanayo timu nzuri yenye ushindani wa hali ya juu na iliyokuwa na ari ya kuwatumikia wananchi,hivyo kwenye usajili huo wanamtaka Mtulia kuboresha timu yao.

 "CCM ni timu ambayo inawachezaji wazuri na waliotumia kwenye kila idara na kama mnavyojua kwenye usajili mdogo lazima msajili mchezaji ambaye atakuwa na uwezo na anaendana na kasi na timu ambayo tunayo.Hivyo Mtulia ni mtu sahihi kwetu.

"Kule alikokuwa mwanzoni hakuwa na uwezo wa kufanya maendeleo kwani kila akitaka kufanya wenzake wanamzuia kwa kigezo kuwa yakipatikana maendeleo ya Kinondoni upinzani hautakuwa na nafasi mwaka 2020.Hivyi akiwa CCM atafanya maendeleo kwa kasi kubwa na tutampa ushirikiano kadri ya uwezo wetu,"amesema Mapunda.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mipango ya Serikali ya kuendeleza kiwanja cha Ndege Mwanza kwa kuiboresha miundombinu ili kiwanja hicho kiwe cha Kimataifa, wakati alipokagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho. 
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa Mamlaka ya Viwanja Ndege Nchini (TAA), kukusanya fedha za madeni ambayo inadai kutoka kwa watoa huduma mbalimbali katika viwanja vyote vya ndege ili ziweze kutumika kuendeleza miundombinu.

Kauli hiyo ametoa jijini Mwanza, baada kukagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha ndege na hali ya uendeshaji katika kiwanja hicho ambapo amebaini kuwa kuna madeni ambayo yanaweza kulipika na kuweza kurahisisha shughuli za kiuendeshaji ikiwemo kujenga uzio ili kuongeza usalama kiwanjani hapo.

"Nataka TAA mkusanye madeni yote mnayodai, fedha hizi zikipatikana zinaweza kutumika kujenga uzio kwa ajili ya kulinda usalama wa uwanja ili wananchi wasiweze kuvamia na pia usalama wa ndege zinazoruka na kutua", amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi barabara ya Pasiansi hadi Airport KM 4.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza. 


Amefafanua kuwa kama Taasisi hizi zikikusanya madeni na watoa huduma wakalipa kodi kwa wakati kutasaida Serikali kuboresha maendeleo ya miundombinu.

Kuhusu maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho. Prof. Mbarawa amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi ambapo kwa sasa umefikia asilimia 60.

Ameongeza kuwa ujenzi huo unategemewa kumalizika mwezi Julai mwaka huu na utagharimu kiasi cha shilingi takribani bilioni 94.

Aidha amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria mara miradi inayoendelea kukamilika.
Muonekano wa eneo la kuegesha ndege ambalo ni moja ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi na uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza. 


Naye Msimamizi wa Kiwanja hicho ambaye ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mwanza, Mhandisi Joseph Mwami,  amesema kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kuongoza ndege, eneo la maegesho na njia za kuruka na kutua ndege

Mhandisi Mwami, amefafanua kuwa njia ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja hicho imeongezwa urefu wa mita 500 ili kuifanya kufikia urefu wa KM 3.5 ili kuwezesha ndege kubwa za kimataifa kuweza kutua na kuruka katika kiwanja hicho.

WAKAZI WA CHALINZE WATAABIKA NA UKOSEFU WA MAJI SALAMA

$
0
0
Madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo Mkoani Pwani ,wakifuatilia kikao cha bajeti cha baraza la madiwani huko Lugoba.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo Mkoani Pwani ,ambae pia ni diwani wa kata ya Talawanda Saidi Zikatimu akizungumza katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani huko Lugoba .(picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze

WAKAZI wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani, wataabika na kero ya ukosefu wa maji safi na salama takriban miezi mitatu sasa. Kufuatia kero hiyo baraza la madiwani la halmashauri ya Chalinze, limemuangukia rais Dk. John Magufuli kwa kumuomba aende kujionea mradi wa maji awamu ya tatu WAMI-CHALINZE ambao umekwama na kusababisha wananchi kukosa neema hiyo ya maji.

Madiwani hao wamesema Rais, ndiye mwenye mamlaka za mwisho kwani Waziri Mkuu alishafika kujionea mradi huo ambapo mkandarasi aliongezewa muda lakini mkataba umekwisha na hakuna kilichofanyika.

Wakitoa kilio hicho, wakati wa kikao cha kupitisha bajeti, baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa Talawanda ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Saidi Zikatimu alisema kuna kila sababu serikali ikaingilia kati na kutoa tamko ili kurejesha imani kwa wananchi. Alieleza tatizo hilo ni kubwa kwani zipo baadhi ya shule hazina maji safi na salama na wanahofiwa wanafunzi kupata magonjwa ya mlipuko.

"Maji ni tatizo mradi wa WAMI -CHALINZE, kamati ya fedha tulishaenda lakini majibu ya meneja wa CHALIWASA Christer Mchomba  hayakuturodhisha "

"Baraza hili linaimani na Mh.Rais jambo hilo lichukuliwe ufumbuzi wa haraka zaidi ya miezi miwili ama mitatu hakuna maji, serikali itoe tamko kuhusiana na mradi huo "; alisema Zikatimu .

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Maisha Magic Bongo kufadhili Harusi ya aina yake, Ni ya washindi wa shindano la ‘Harusi ya Ndoto Yako'

$
0
0
Wakazi wawili wa jiji la Dar es Salaam ambao ni wachumba Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard wameibuka washindi wa shindano la Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa likiendeshwa na chaneli ya Maisha Magic Bongo Dstv chaneli 160.

Wapenzi hao wameshinda zawadi ya ufadhili wa harusi yao ya kifahari itakayofanyika jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.  Pamoja na kushinda Harusi ya Ndoto Yao, wawili hawa pia watapewa zawadi ya fungate kwa hisani ya hoteli ya kitalii ya Voyager Beach iliyopo jijini Mombasa nchini Kenya.

Washindi hao walitangazwa jana katika kilele cha siku ya wapendanao katika hafla iliyofanyika makao makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washindi hao.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema channel ya Maisha Magic Bongo imeamua kuwatunuku watazamaji wake zawadi hiyo kupitia kipindi chake maarufu cha Harusi Yetu kinachorushwa na channel hiyo ambacho huonyesha harusi mbalimbali


Kipindi cha Harusi Yetu kilianza kuruka mnamo Novemba 2016 ambapo msimu wa pili wa kipindi hicho ulianza mwezi Julai mwaka 2017. Kipindi hicho hurusha harusi mbamlimbali huku kikiangazia walikotoka wanandoa, hatua wanazopitia katika mahusiano yao na hatimaye tukio la kufunga ndoa.

Kuanzia ilipoanza awamu ya pili Maisha Magic Bongo ilianzisha shindano maalum lililojulikana kama Harusi ya Ndoto Yako ambapo washiriki walikuwa wakijibu kuhusiana na kipindi cha harusi yetu ambapo kila wiki kulikuwa na swali moja. Hadi kufikia mwisho wa shindano mnamo mwezi Desemba mwaka jana jumla ya washiriki 1,112 walishiriki ambapo 448 waliingia kwenye mchujo wa wawali na hatimaye kubakia wanne ambao waliitwa kwenye usaili maalum uliokuwa na jopo la watahini saba.

Baada ya usaili huu, Solomon mkazi wa Dar es Salaam pamoja na mchumba wake Magreth waliibuka washindi na hivyo kupata zawadi ya kugharimiwa harusi yao itakayofanyika jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 28 mwezi April mwaka huu.

Akifafanua kuhusu zawadi hiyo, Maharage alisema zawadi hiyo inamaanisha maharusi hao watarajiwa watagharimiwa kila kitu kuanzia ukumbi, mavazi, chakula, vinywaji, burudani, pamoja na fungate la kukata na shoka katika moja ya hoteli za kitalii Voyager Beach Hotel katika ufukwe wa Mombasa nchini Kenya.
Wakizungumza katika hafla hiyo, Solomon pamoja na mchumba wake Magreth wamesema wamefurahi sana kushinda na kutuzwa ufadhili wa harusi yao. “Sote tunafahamu ni jinsi gani zoezi la harusi linavyokuwa na patashika hususan kwenye suala la gharama. 
Hivyo nafurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kushinda katika shindano la Harusi ya Ndoto Yangu kwani sasa sisi kazi yetu ni kufikiria tu jinsi tutakavyoendesha maisha yetu kwani suala la harusi limekamilika” alisema Solomon, Bwana Harusi mtarajiwa.

Ameipongeza Chaneli ya Maisha Magic Bongo kwa kubuni shindano hilo ambalo lilileta msisimko mkubwa na kwamba anaamini kuwa channel hiyo itaendelea kuimarika kwani kwa sasa imekuwa maarufu sana kwa kuwa ni chaneli inayowafanya watanzania wajivunie vipaji vyao.

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.

Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65 ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.

Taarifa ya kifo chame imethibitishwa na Makamu Rais wa chama chama cha MDC, Elias Mudzuri kupitia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jana jioni ya Februar 14.

Morgan Tsvangirai aliyekuwa ni mpinzani mkubwa wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe,  alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000, na kuanza kutoa changamoto kwa Rais Mugabe aliyekaa madarakani muda mrefu.

Kufuatia kifo hicho cha Tsvangirai, chama cha MDC kinaweza kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.

WAPIGA DILI,WALA RUSHWA HAWATAKIWI CCM

$
0
0
MWENYENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya kiwalani Mathias Kahinga Amesema katika kipindicho chote cha uongozi wake wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake nakudai mbeleko za kuwabebea zimechanika.

Amesema kwake ni kuchapa kazi aliyotumwa na wanachama wa Chama chake kwa lengo kuu la kutatua na kuisimamia Serikali huku akitoa rai kwa viongozi wezake ndani ya chama hicho kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wenye unyenyekevu kwa wananchi na kutatua kero zao.

Mwenyekiti na kada huyo wa Chama ameyasema haya jijini Dar es salaam katika ofisi za Chama hicho Kata zilizopo Kata hiyo ya kiwalani ndani ya manispaa ya Ilalat. Ambapo amesema kwake wapiga dili na wezi hawana nafasi kabisa.

"Nilikuwa na mambo kadhaa ambayo nilihaidi kwa wanaccm wakati nautaka uwenyekiti na moja ya kazi yangu kubwa ni kurejesha mtaa mmoja wa serikali ya mtaa ambao unatawaliwa na CUF kwa miaka 15 sasa na hakuna maendeleo yeyote ndani ya mtaa huo wa kigilagila. "amesema Kahinga
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kiwalani,Mathias Kahinga kulia)akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake,leo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Chama hicho Kata kiwalani,Eva Malenga (kushoto) akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI

$
0
0

Na Joel Maduka ,Chato

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea awamu ya tatu kwenye Vijiji na kata za Iparamasa na Kalembela, kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato.Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.

Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara zao.

Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.


Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.
Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. 
 

Hatimaye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aachia ngazi

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake. Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtakja ampe nafasi mamamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye sasa kiongozi mpya wa chama.
Bw Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi.Mapema Jumatano, polisi walivamia nyumba ya familia tajiri ya Gupta ambayo Zuma ana uhusiano wa karibu nayo.
Zuma alijiuzulu kwa njia gani?Alianza hotuba kwa kucheka na kufanya mzaha na waandishi wa hahari. Baada ya kuwashukuru wale ambao amefanya kazi nao kwa miaka kadhaa, Bw Zuma alisena kuwa ghasia na migawanyiko ndani ya ANC imesababisha ajiuzulu.
"Hakuna maisha yatapotea kwa sababu yangu wala ANC haiwezi kugawanyika kwa sababu yangu. Kwa hivyo nimefikia uamuzi wa kujiuzulu kama rais wa nchi mara moja. "Licha ya kutokubaliana na uamuzi wa chama changu, siku zote nimekuwa mwanachama mwenye nidhamu wa ANC."Ninapoondoka, niataendelea kuwatumikia watu wa Afrika Kusini sawa na ANC, chama ambacho nimekitumikia maisha yangu yote," alisema
Chanzo: BBC

tangazaji michezo redioni umeniimarisha- Jane John

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO FEBRUARY 14, 2018

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 15, 2018

INTRODUCING "AWAMU YA TANO UWANJANI" BY NGOMA AFRICA BAND

SHOW YA MIC TATA KURINDIMA DAR LIVE FEBRUARI 24,2018.

$
0
0

Uhuru FM kwa kushirikiana na ukumbi wa Dar Live inakuletea show ya Muziki  ijulilikanayo kwa jina la MIC TATA litakalokutanisha miamba wa Muziki hapa  nchini litakalofanyika katika ukumbi wa Darlive-Mbagala Zakem Februari 24 Mwaka huu.

SIMIYU YAJIPANGA KIMKAKATI KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU KWENYE ELIMU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Mkoa wa Simiyu umejipanga kimkakati katika  kuhakikisha unaongeza ufaulu kwenye Elimu na kuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri Kitaifa kutoka mahali ulipo sasa,  kwenda kwenye nafasi ya tarakimu moja(single digit) yaani nafasi ya kwanza hadi ya tisa.

Hayo yalibainishwa katika kikao maalum kilichofanyika jana Mjini Bariadi kati ya Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewataka walimu pamoja na watendaji wengine wa idara ya Elimu kuongeza bidii katika maeneo yao ili waweze kuufikisha mkoa katika nafasi ya tarakimu moja (single digit) kwa kuwa sababu, uwezo na nia ya kufika hapo ipo.

“Watu wa Sekta ya elimu Ombi langu kwenu wakati tukiwa tunajipongeza kuwa wa 14 katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017 tudhamirie kuongeza bidii ili tuingia kwenye ‘single digit’, sababu za kuingia kwenye ‘single digit’ zipo, uwezo upo kwa kuwa ninyi mpo na nia ya Simiyu kuonekana juu tunayo” alisema Sagini.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
 Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi..
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na walimu mahiri kwenye masomo mbalimbali katika Mitihani ya Kitaifa mwaka 2017 mara baada ya kikao cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na walimu hao, kumalizika jana mjini Bariadi.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

StarTimes yanogesha Siku ya Wapendanao

$
0
0
 Kampuni ya Star Media (T) Ltd inayomiliki chapa ya StarTimes, jana katika Siku ya wapendanao iliwapatia fursa wateja wao kupata chakula cha jioni na wapenzi wao katika mgahawa wa kifahari wa Akemi, Posta jijini Dar es Salaam.
 StarTimes ambayo kwa wiki kadhaa iliwapatia nafasi wateja wake kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii kutuma picha wakiwa na wapenzi wao ili kujipatia nafasi hiyo adhimu ya kupata chakula cha jioni pamoja. Katika picha zote zilizotumwa na wateja wa StarTimes katika kurasa zao za mitandao ya kijamii, watano walibahatika kuchaguliwa na baadaye walipatiwa taarifa jinsi ya kufika kwenye mgahawa kwa ajili ya zawadi maalum.
Kabla ya kupelekwa mgahawani wapenzi hao walipata nafasi ya kutembelea ofisi za makao makuu ya Star Media (T) Ltd zilizopo Bamaga, Barabara ya Bagamoyo, Dar es Salaam, na kujionea jinsi ambavyo StarTimes hufanya kazi kila siku, miongoni mwa ofisi walizotembelea ni kituo cha Simu (Call Centre), Chumba cha Kurushia matangazo na Duka la vifaa mbalimbali vya StarTimes.
Wapendanao hao baadaye walipelekwa mgahawani kwa ajili ya Chakula cha jioni. Yote ikigharimiwa na kampuni ya StarTimes katika kuonyesha upendo kwa wateja wake katika Siku ya Wapendanao.

JAPAN YAKABIDHI MRADI WA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA KASENDA WILAYANI CHATO

$
0
0
Serikali ya watu wa Japan imekabidhi mradi wa Soko la Samaki la kimataifa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wenye thamani ya shilingi milioni 320 na kusaini makubaliano ya ukarabati wa barabara ya Mganza - Kasenda ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya ziwani.

Akizungumza baada ya kukabidhi mradi huo kwa Serikali Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu amesema mradi huo umetolewa na Serikali ya Japan kwa watu wa Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa urafiki wa siku nyingi katika utekelezaji wa miradi ya kilimo na uvuvi. ''Mradi wa huu ulitolewa baada ya kuona soko la Kasenda liko katika hali mbaya na samaki kuharibika kwa kukosa miundombinu ya kuhifadhi ndipo Japan ikachukua hatua za haraka kwa kutoa fedha dola za kimarekani 148,146 kwa ajili ya kujenga soko na kukarabati soko la zamani''. Utekelezaji wa mradi ulianza mwaka 2017 na sasa wananchi wanaendelea kunufaika.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo kabla ya makabidhiano mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Joel Hari amesema mradi unahusisha ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia samaki na ukarabati wa sokola zamani.Ameeleza kuwa soko lipo chini ya Halmashauri ya Chato likiwa na wanachama 241 huku likikasimiwa kukusanya shilingi milioni 140 kwa mwaka huku likitoa huduma kwa nchi za Rwanda,Burundi, Uganda na Congo DRC.haa za kutoka ziwani.

 Balozi wa Japan Nchini Tanzania. Yoshida Masaharu pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, bw Joel Hari wakiweka jiwe la makabidhiano ya mradi wa Soko la Kimataifa la Samaki ambalo limefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa Gharama ya Shilingi milioni 320 kijiji cha Kasenda Chato.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Mhandisi Robert Gabriel(kushoto) na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Yoshida Masaharu  wakisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kijiji cha Kasenda kwa ajili ya Makabidhiano ya Mradi wa Soko la Samaki la Kimataifa na kusaini mkataba wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa Kilometa 1 ya kutoka Mganza kwenda Kasenda.
 Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu na Viongozi wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato baada ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Soko la Samaki la Kimataifa la Kasenda Wilayani Chato.Watatu kutoka kushoto kwa balozi ni Waziri wa Nishati (Mb) Mheshimiwa Medard Kalemani na Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya ya Chato na Kulia kwa balozi aliyevaa miwani na suti ya kijivu ni Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel pamoja na Bw; Joel Hari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato.
 Mradi wa ujenzi wa Soko la kimataifa la Samaki la Kijiji cha Kasenda Wilayani Chato uliojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege  wa Mwanza kuanza ziara ya kikazi mkoani humo Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabulla wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kuanza ziara ya mkoa huo, Februari 15, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na viongozi wa serikali, Vyama vya Siasa na viongozi wa dini kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kuwasili  na kuanza ziara ya kikazi mkoani humo Februari 15, 2018.  Watano kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

TANZANIA YASHINDA TUZO YA TEKNOLOJIA KATIKA MKUTANO WA DUNIA WA SERIKALI (WORLD GOVERNMENT SUMMIT 2018)

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshinda Tuzo za Kilele cha Serikali duniani (World Government Summit Awards) katika kundi la Tuzo ya Teknolojia bora inayoibuka Serikalini (Winner of the Best Government Emerging Technologies Award).

Tuzo hiyo ilitolewa na Mtukufu Shaikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nchi, Ofisi ya Rais ya Umoja wa Falme za Kiarabu) (UAE) na kupokelewa na Balozi wa Tanzania, UAE, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk kwa niaba ya Serikali, wakati wa kilele cha Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Government Summit) uliohitimishwa jijini Dubai tarehe 13 Februari 2018.

Tuzo hiyo ilitokana na juhudi za Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Kilimo ya Mikocheni (Mikocheni Agricultural Research Institute kufanikiwa kulipatia ufumbuzi tatizo la maradhi ya zao la muhogo “Cassava Brown Creek Disease,” na “Cassava Mosaic Disease,” kwa kutumia chombo cha kisasa kinachoitwa “Portable DNA Sequencer”.  Maradhi hayo yanasumbua sana zao la muhogo ambalo ni zao muhimu kwa Tanzania na nchi mbalimbali Afrika na duniani kwa ujumla.

Kwa kutumia teknolojia hii mpya wataalamu wanaweza kugundua magonjwa mbalimbali ya zao la muhogo yanayosababishwa na wadudu, virusi, bacteria na fangasi (pathogens) kwa muda wa siku 2 tu kulinganisha na teknolojia ya zamani ambayo huchukua miezi kadhaa na ina gharama kubwa.

Zao la muhogo ni zao muhimu la chakula na biashara linalotegemewa sio tu na  Tanzania bali na nchi nyingine nyingi duniani.  Inakadiriwa kuwa watu wapatao millioni 800 duniani wanategemea zao la muhogo kwa chakula na biashara. Hivyo, teknolojia hii mpya itanufaisha nchi mbalimbali duniani katika kusaidia na kuendeleza zao hilo.

Nchi nyingine zilizopata Tuzo hiyo ni India na Australia.

Wakati huo huo, Watanzania wenye sifa wanahimizwa kuomba nafasi ya kazi iliyotangzwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya mazingira (UNEP). Nafasi inayotakiwa kujazwa ni ya Chief Biodiversity Unit. Maelezo kuhusu nafasi hiyo yanapatikana katika mawasiliano http://careers.un/bw/jobdetail.aspx?id=88749 na siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni tarehe 25 Februari 2018.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 15 Februari 2018.

BALOZI WA JAPAN AKABIDHI SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI KASENDA

$
0
0
Na,Joel Maduka,Chato.

Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaharu Yoshida kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Geita amezindua rasmi soko la kimataifa la uuzaji samaki la kasenda lililojengwa kata ya mganza wilayani chato mkoani hapa kwa hisani ya watu wa Japani.

Soko hilo lililopo kata ya Muganza lina jumla ya wafanyabiashara wa samaki zaidi ya 240 limegharimu jumla cha Shilingi milioni 320 za kitanzania hadi kukamilika kwake ukarabati uliohusisha pia ukarabati wa soko la zamani.

Akikabidhi soko hilo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Balozi wa Japan nchini Tanzania mhe. Masaharu Yoshida amesema kukamilika kwa ujenzi wa ghala la kuhifadhia samaki na dagaa kutasaidia kuokoa mazao mengi kutoka ziwani hususan samaki na dagaa.

“Soko la samaki la Kasenda halikuwa na miundombinu ya kuhifadhia samaki ambapo zaidi ya tani 200 za samaki zilitupwa kila mwaka kutokana na kuharibika ambapo serikali” alisema Mhe Masaharu.

Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa na mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi baada ya kukabidhi soko la samaki la kimataifa la Kasenda lililopo kata ya Mganza Wilayani Chato lililojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akizindua kwa kuweka jiwa la msingi kwenye mradi wa soko la samaki la kimataifa la kasenda pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato ,Mhandisi Joel Hari.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida wakiweka saini kwenye vitabu vya wageni. 

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images