Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110118 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: TTCL sasa kuwa Shirika la Mawasiliano


MAHAKAMA KUTOA UAMUZI ONYO LA POLISI,MDEE KESI YA LUGHA CHAFU KWA RAIS

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu  imesema Machi 1 mwaka huu, itatoa uamuzi dhidi ya maelezo ya onyo yaliyotolewa Polisi na Mbunge wa Kawe Halima Mdee, (Chadema), katika kesi ya kutumia lugha ya matusi (chafu),dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Magufuli yapokelewe kama kielelezo au la.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya shahidi wa upande wa mashtaka D/SSGT Albogast  kuomba kuyatoa maelezo hayo ya onyo mahakamani hapo kama kielelezo na Wakili wa Utetezi Peter Kibatala kupinga kwa madai yalichukuliwa nje ya muda.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama hiyo kusikiliza pande zote mbili ule wa utetezi na mashtaka na kueleza Machi Mosi, mwaka 2018 atatoa uamuzi kama maelezo hayo ya onyo yapokelewe ama yasipokelewe kama kielelezo.

Katika kesi hiyo, Mdee anadaiwa kuwa, Julai 3, mwaka 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.

VETA YAWASILISHA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KWA KWA WADAU

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Blogu ya jamii

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeandaa mkutano wa wadau kwa lengo la kuwasilisha mpango mkakati wake wa miaka mitano na kupokea maoni yao.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Bodi ya VETA, Suleiman Lolila amesema mpango mkakati huo utatoa picha halisi ya mamlaka inachotarajia kufanya ndani ya miaka mitano.Lolila ametaja baadhi ya malengo hayo ni kuboresha utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi , kupanua wigo wa utoaji mafunzo ya elimu na ufundi stadi ili kufikia makundi mengi zaidi na kuimarisha menejimenti ya VETA .

Amesema malengo mengine ni kupunguza maambukizi wa virusi vya Ukimwi na kuboresha huduma saidizi na kutekeleza mpango wa taifa dhidi ya rushwa.Pia amewaomba wadau kutoa mawazo yao ili kuboresha mpango mkakati huo na Bodi hiyo itapokea mawazo hayo na kuyajumuisha katika mpango mkakati na kusimamia utekelezaji wake kwa kuweka mazingira rafiki na kutoa usimamizi wa karibu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk. Bwire Ndazi amesema mpango mkakakati huo umeandaliwa kwa kuzingatia hali halisi ya kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha ajenda ya Serikali ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.“Katika miaka mitano ijayo (2018/2019 hadi 2022/2023) mamlaka hiyo imejikita katika uboreshaji wa utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili kuwa na mafundi stadi mahiri na wa kutosha nchini,”amesema.

Dk.Ndazi amesema baadhi ya malengo waliojiwekea ni kuongeza udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ufundi stadi kutoka 200,000 hadi 700,000, udahili wa watu 400 wenye mahitaji maalum kila mwaka, udahili wa vijana 2400 wanaotoka katika mazingira magumu kila mwaka.

Amesema wataongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa kike kutoka asilimia 35 hadi 45,utambuzi na Urasimishaji wa vijana 200,000 waliopata mafunzo kupitia mfumo usio rasmi,Ujenzi wa vyuo vipya vya VETA visivyopungua 13 nchini.

Mkutano huo umehusisha wadau mbalimbali wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo maofisa wa Serikali, wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa likiwamo Shirika la Kazi Duniani(ILO), ISTEP, IYF na VSO, wawakilishi kutoka katika viwanda, watoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na wazazi.
 Mjumbe wa Bodi ya VETA, Suleiman Lolila akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa wadau wa VETA wa  kutengeneza mpango wa miaka mitano leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mikakati ya miaka mitano iliyopita na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ajira , Hildegardis Bitegera akizungumza kuhusu maendeleo ya VETA  katika suala la ajira leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau wa katika mkutano wa kutengeneza mkakati wa miaka mitano 

PWANI YAWATAKA WAFANYABIASHARA , KUSAJILI TIN NUMBER KWA TRA PWANI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

SERIKALI mkoani Pwani,imewaasa wafanyabiashara, wawekezaji na wenye viwanda ,kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoani humo, ifikapo machi 30 mwaka huu.

Hatua hiyo itasaidia mkoa huo kunufaika na wafanyabiashara hao ambao wengi wao kwasasa wanalipa kodi katika maeneo ya mikoa waliojisajili .Mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alitoa agizo hilo ,mjini Kibaha wakati wa mkutano wa baraza la biashara la mkoa .

Alisema kutokana na wafanyabiashara wengi mkoani hapo kulipia kodi nje ya Mkoa kunasababisha kudidimiza uchumi wa mkoa."Kila mmoja abebe mzigo wake,mchango wetu kama mkoa hauonekani,na hatunufaiki ,unakuta tuna miviwanda mingi lakini wamekata TIN no.Kinondoni, Ilala ,jijini Dar es salaam ,mapato yake yote yanahesabika huko"

"Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa mkoa wa Pwani unachangia asilimia 1.6 ya pato la taifa ambalo liko chini, kumbe wafanyabiashara na makampuni hawatulipi kodi kwenye mkoa jambo ambalo sio sawa," alisema Ndikilo.
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mkutano wa baraza la biashara la Mkoa  wa Pwani
 Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amekizungumza wakati wa mkutano wa baraza la biashara la mkoa ,mjini Kibaha. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoani Pwani, Abdallah Ndauka ,akionekana pichani akizungumzia masuala mbalimbali ya kibiashara katika mkutano wa baraza la biashara la Mkoa huo.(picha na Mwamvua Mwinyi)

NDEGE MPYA ZA ATCL KUWASILI MWEZI JULAI MWAKA HUU

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA NA JOC

$
0
0
MKUUWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba ambao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.

Viongozi hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei ambao kwa pamoja wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.

Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo (Jumatatu, Februari 12, 2018) jijini Dar es Salaam na amesema kwamba wakulima waliitikia wito wa Serikali wa kufufua zao hilo, hivyo mwaka huu wanatarajia kupata mavuno mengi.

Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiandae kununua pamba nyingi kwa sababau mwaka huu wakulima wamelima pamba ya kutosha baada ya Serikali kuwahamasiha waongeze uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of Industries,na JOC. Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi (kushoto mwenye miwani nyeusi) . Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini Tanzania. Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. PICHA NA OFISI YA WAZIRI 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO

$
0
0
Mtanganzaji mkongwe nchini Emmanuel Likuda,leo amejiunga rasmi na A.FM RADIO kama mtanganzaji akijikita zaidi katika kipindi cha Amka tofauti. 

Akiongea wakati wakumtambulisha Likuda kwa wasikilizaji,Meneja mkuu wa A.FM Bw. Tatenda Nyawo amesema,hiyo ni zawadi maalum na upendo kwa wasikilizaji wa a.fm 92.9 Dodoma,hasa katika msimu huu wa siku kuu ya Wapendanao (VALENTINES).

Bw.Tatenda ameongeza kuwa Likuda ni mtangaji mwenye uzoefu wa kutosha katika masuala ya utangazaji,hivyo kujiunga kwake na Af.m ni njia moja wapo ya kukipeleka kitu hicho katika hatua nyingine,kama ilivyo kauli mbiu ya A.fm kwa mwaka huu ‘’2018 level Nyingine”.

Kwa upande wake Likuda amesema ni furaha sana kujiunga na A.fm na kutokana na uwezo na uzoefu alionao,ana Imani kuwa A.fm itasonga mbele Zaidi katika kutimiza dhima yake kwa jamii hasa wakazi wa Dodoma na kwamba vipo vitu vingi ambavyo amejipanga kuvitoa kama zawadi kwa wasikilizaji wa A.FM kupitia kipindi cha AMKA TOFAUTI ambacho hurushwa kila siku kuanzia JUMATATU- IJUMAA saa 11:00 Mpaka saa 03:00 Asubuhi.
 Meneja mkuu wa A.fm Radio Tatenda Nyawo (kushoto)akiwa kwenye picha ya pamoja na mtangazaji  Emmanuel Likuda mapema leo,baada ya mtangazaji huyo kutambulishwa rasmi kwa wasikilizaji kama mtangazaji wa kipindi cha Amka Tofauti kinachorushwa na A.FM
  Likuda kwenye picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha  Amka Tofauti  Victor Simon na Elizabeth Kachenje.
 Mtangazaji Likuda akiwa na watangazaji wa kipindi cha  Amka Tofauti,kushoto ni  Victor Simon,Elizabeth Kachenje na msimamizi wa Vipindi Ally Mohamed (Kulia).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Naibu Waziri Kakunda Amsimamisha Mhandisi wa Maji Chemba

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah,Chemba.

Naibu Waziri Ofisi yaRais- TAMISEMI Mhe. Joseph George Kakunda ameiagiz ahalmashauri ya Wilaya ya Chemba kumsimamisha Mhandisi wa Maji wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kusimamia miradi ya maji.

Mhe.Kakunda alitoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani humo aliyoifanya ambapo alikagua miradi ya maji na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Lahoda,Kisande na Honta.

Baada ya kufanya ukaguzi huo na kubaini mapungufu yaliyopo kwenye miradi ya maji sambamba na kumsimamisha Mhandisi wa Maji pia aliagiza OR-TAMISEMI kufanya Ukaguzi wa Kitaalamu (Technical Audit) ya miradi yote ya maji ambayo imeonekana kwa macho kutotekelezwa kwa kiwango na bado haijaanza kufanya kazi katika Halmashauri ya Chemba.

“Serikali imetoa Fedha nyingi sana kwa ajili ya miradi hii ili kupunguza kero kwa wananchi wetu lakini wasimamizi wa Miradi hawatekelezi wajibu wao ipasavyo katika kusimamia miradi hiyo na wananchi wetu bado wananednelea kuteseka kwa sababu ya Uzembe wa watu wacheche hii haitakubalika lazima wachukuliwe hatua” Alisema Kakunda.

Naibu Waziri Kakunda wakati wa ziara hiyo pia alitembelea Shule ya Msingi Lahoda na alikutana na mwananfunzi mwenye ulemavu wa ngozi na kuelekeza Halmashauri ya Chemba iwei na mpatia mahitaji muhimu mwanafunzi huyo.
Naib wa Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akikagua mradi wa maji Lahoda-Kisanda wakati wa ziara yake Wilayani Chemba.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe.Joseph kakunda (kulia) akizungumza na mwanafunzi Fatuma Ramadhani wakati alipotembelea shule ya Msingi Lahoda.
NaibU Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akikagua mradi wa maji Lahoda-Kisand
NaibU Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lahoda,Kisanda na Honta wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya mazungumzo.
PICHA NA IKULU 

TRL YAPATA HASARA BILIONI TANO

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania (TRL) limepata hasara ya takribani shilingi bilioni tano katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya njia ya reli ya kati kusombwa na mafuriko katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu ya reli hiyo na kusema kuwa Serikali imejipanga kupata suluhisho la kudumu la uharibifu katika maeneo hayo ambapo mara kadhaa yamekuwa yakiathiriwa na mvua kutokana na mabwawa yaliyopo kujaa mchanga na hivyo kusababisha uharibifu huo.

“Serikali kwa sasa inayafanyia kazi mapendekezo matatu yaliyowasilishwa na RAHCO ikiwemo kuihamisha reli kwenye milima jirani, kuihamishia eneo ambapo inajengwa reli ya kisasa ya SGR ama kujenga tuta kubwa, huku tukizingatia gharama halisi za kazi hiyo kabla ya kufanya maamuzi”, amesema Prof. Mbarawa.
Mhandisi Mkuu kutoka Shirika la Reli (TRL), Mhandisi Nelson Ntejo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) kuhusu maendeleo ya kazi ya ukarabati wa eneo lililoathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka, katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro, wakati Waziri huyo alipokagua reli hiyo Mkoani humo, hivi karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkuu kutoka Shirika la Reli (TRL), Mhandisi Nelson Ntejo, alipokagua ukarabati wa njia ya reli ya kati ya eneo la Kilosa mkoani Morogoro iliyoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kazi zinazoendelea katika eneo la Kilosa, ambapo ukarabati umekamilika na treni za mizigo zimeanza kupita.
Muonekano wa sehemu ya njia ya reli ya kati eneo la Kilosa iliyokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha, mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwaka huu.
Muonekano wa treni ya mizigo ikianza safari zake katika stesheni ya Kilosa, mkoani Morogoro kuelekea mkoani Mwanza mara baada ya njia hiyo kukarabatiwa.

TANZANIA INATUMIA DAWA ZILIZO SALAMA KWA UHAKIKA MKUBWA

$
0
0

Na.WAMJW-DAR ES SALAAM

TANZANIA ni miongoni mwa nchi inayotumia dawa zilizo salama na ubora wa hali ya juu barani Afrika kutokana na udhibiti na umakini unaofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mamlaka wa Udhibiti na ubora wa dawa barani afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam.

”Sisi kama Tanzania tunafanya vizuri sana katika udhibiti wa madawa yanayoingia,nataka niwathibitishie kwamba Tanzania dawa zetu tunazozitumia ni salama na zipo salama kwa uhakika mkubwa” alisema Dkt. Ndugulile .Aidha ,Dkt. Ndugulile alisema kuwa ongezeko la matumizi ya dawa ambayo hayana kiwango na kutumika katika mfumo wa tiba umeleta changamoto katika kuongeza gharama za matibabu nchini na barani Afrika

Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema changamoto hizo zinasababisha wagonjwa wengi kukaa hospitalini,kuongeza gharama, kuathiri matokeo ya mgonjwa na hatimaye vifo pamoja na kuleta usugu wa dawa kwa kutumia dawa zisizo na kiwango .
WaziriAfya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika unaofanyika Jijini DaeEs Salaam na kuhudhuliwa na n chi zipatazo 17 za Afrika.
Dkt.Ndugulile akifuatilia mada (mwasilishaji hayupo pichani) katika mkutano huo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi.Agnes Kijo akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika
Msimamizi wa kitengo cha Afya katika Shirika la Maendeleo ya Afrika (NEPAD) yenye makao makuu yake nchini Afrika ya Kusini Bi.Margareth Ndomondo akiongea wakati wa uzinduzi huo.Shirika hilo katika afya linasaidia kupunguza magonjwa yanayoikabili nchiza Afrika.

 
 

Mwakyembe akutana na Waziri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujadili mapokezi ya viongozi wa FIFA na CAF nchini

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe ameitaka Tanzania kuitendea haki heshima ya kupewa nafasi ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa FIFA na CAF hapa nchini unaotarajiwa kufanyiaka kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi Februari. 


Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia ujio wa viongozi wa FIFA na CAF nchini kwa ajili ya kufanya mkutano hapa nchini ambao wanatarajia kuwasili nchini na kufanya mkutana wao tarehe 21 hadi tarehe 22 Februari mwaka huu. 

Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Seriakali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameona ni vyema kukutana kujadili namna ya kupokea ugeni huo mkubwa kwani Tanzania ina sifa ya kupokea wageni kwa ukarimu wa hali ya juu hivyo kuhakikisha kuwa watakachokifanya wakifanye kwa hadhi na hali ya juu ya taifa letu bila ya migogoro ya aina yoyote. 

“Ugeni unaokuja kwa kweli ni mkubwa hivyo fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili ugeni huo uamue tena kwa mara nyingine kuja hapa nchini kufanya vikao vyake na kuitangaza Tanzania duniani kote” amesema Mhe. Mwakyembe 

 Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (wapili kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Willium (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam

Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM


WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA NA JOC

$
0
0
WAZIRI MKUU  Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of Industries,na JOC. Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba ambao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Viongozi hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei ambao kwa pamoja wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.

Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo (Jumatatu, Februari 12, 2018) jijini Dar es Salaam na amesema kwamba wakulima waliitikia wito wa Serikali wa kufufua zao hilo, hivyo mwaka huu wanatarajia kupata mavuno mengi.Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiandae kununua pamba nyingi kwa sababau mwaka huu wakulima wamelima pamba ya kutosha baada ya Serikali kuwahamasiha waongeze uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa maelekezo ya uhamasishaji wa kilimo hasa mazao makuu ya biashara, tayari tija imeanza kuonekana ambapo zao la korosho limepata mafanikio makubwa na sasa linafuatia zao la pamba.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei (Kulia). na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi (kushoto mwenye miwani nyeusi) . Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.Nchini Tanzania.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation

IGP SIRRO AMUAPISHA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimuapisha kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, leo Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, akiweka saini hati ya kiapo baada ya kuapishwa na Mkuu wa Jeshi hilo IGP Simon Sirro, Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, Kamishna Haji aliteuliwa na Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, akitoa neno mbele ya Maofisa Wakuu Waandamizi na askari wa vyeo mbalimbali (hawapo pichani) baada ya kuapishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, kuwa kamishna wa Polisi Zanzibar huku akiahidi kufanyakazi kwa uzalendo na kumsaidia IGP Sirro katika majukumu ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, na Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, wakiwa katika picha na Maofisa wa Jeshi hilo baada ya hafla ya kumuapisha kamishna wa Polisi Zanzibar kukamilika leo Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

MICHUZI TV LIVE: MKUTANO WA KAMPENI ZA UBUNGE CCM JIMBO LA KINONDONI ENEO LA KIGOGO LEO

Droo ya tatu ya SHINDA NA SMATIKA INTANETI: Airtel yagawa Simu za Smatiphone kwa washindi

$
0
0

  • Washindi wengine 3,000 wajishindia kifurushi cha intaneti 1GB kila mmoja
Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za smartphone Airtel Tanzania imewazadia washindi wa droo ya tatu ya promosheni yaSHINDA NA SMATIKA Intaneti katika droo iliyochezwa leo jijini Dar es Salaam.
Katika droo hiyo ya leo, washindi 10 wameweza kujishindia simu za kisasa  za smartphone pamoja na modem huku wengine 3,000 wakijishindia kifurushi cha intaneti cha 1GB BURE. Hii ni droo ya tatu tangu kuzinduliwa kwa promosheni hiyo ambapo mpaka leo jumla ya washindi 8,000 tayari wamezawasiwa  zawadi ya kifurushi cha intaneti cha 1GB BURE.
Akizungumza baada ya droo ya leo, Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa promosheni ya SHINDA NA SMATIKAIntaneti ni maalum kwa  wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Yatosha Intaneti nchi nzima.
‘Promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti bado inaendelea, ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kambambe’, alisema Mmbando.
 Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akionyesha baadhi ya simu za smartphone ambazo ni zawadi kwa washindi wa SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Jumla ya wateja 3000 walijishindia 1GB ya intaneti bure, watano simu tano za smartphone na tano modem.


 Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na washindi wa SHINDA NA SMATIKA Intaneti wakati wakuchezesha droo leo jijini Dar es Salaam ambapo washindi 3000 walijishindia 1GB bure, watano simu tano za smartphone na tano modem.

Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na washindi wa SHINDA NA SMATIKA Intaneti wakati wakuchezesha droo leo jijini Dar es Salaam ambapo washindi 3000 walijishindia 1GB bure, watano simu tano za smartphone na tano modem.

VPL: KAGERA SUGAR YATOSHANA NGUVU NA AZAM FC KWENYE UWANJA WA KAIATABA LEO

$
0
0

Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 34 sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.
Kagera Sugar yenyewe inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 18 na sasa inajinasua mkiani ikirudi nafasi ya 15 kwa wastani wa mabao tu baada ya kulingana kwa pointi na Njombe Mji FC. 
Katika mchezo wa leo, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la beki Eladslaus Mfulebe dakika ya 50, kabla ya Iddi Kipagwile kuisawazishia Azam FC dakika ya 53.


Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa: Ramadhani Mohammed, Mwaita Gereza, Eladslaus Mfulebe, Juma Shemvuni, Mohammed Faki, George Kavila/Peter Mwalyanzi dk57, Suleiman Mangoma, Ally Nasoro ‘Ufudu’, Japhary Kibaya/Edward Christopher dk79, Ally Ramadhani na Venance Ludovic/Atupele Green dk69.
Kikosi cha Azam FC: Kipa Razack Abalora, Saleh Abdallah/Iddi Kipagwile dk46, Bruce Kangwa, David Mwantika, Yakub Mohammed, Abdallah Kheri, Stephan Kingue/Paul Peter dk74, Frank Domayo, Salmin Hoza, Mbaraka Yussuph/Ennok Atta Agyei dk46 na Shaaban Idd.

Shangwe kwa Kagera Sugar, wameumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Timu ya jijini Dar es salaam Azam Fc.
Kikosi cha Timu ya Azam Fc kilichoanza leo dhidi ya Kagera Sugar.


Mshambuliaji wa Azam Fc Mbaraka Yusuph akigombea mpira

Uwe Valentine Wangu - mkongwe John Kitime

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Ahutubia Siku ya Sheria Zanzibar

$
0
0

r
 RAIS wa Chama cha Mawakili Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Vitabu vya Sheria wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar yaliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Hafla ya Siku ya Sheria Zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Hafla ya Siku ya Sheria Zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,katika picha ya pampja baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar yaliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar. Picha na Ikulu.
Viewing all 110118 articles
Browse latest View live




Latest Images