Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

HOJA YA HAJA: ATHARI YA UTANDAWAZI NA SIASA YA TANZANIA NA MAENDELEO YAKE

$
0
0
Na Saleh Jabir, UK

Nikiwa mwanafunzi ninayesomea sayansi ya kijamii, naandika makala hii kwa msukumo wa hisia ya uzalendo kwa nchi yangu na kwa kutumia maono yangu na akademia ya kisayansi kuhusu mambo ya kijamii yanayohusu jamii yetu kwa faida ya Watanzania wote. 

Uchambuzi wa moja kwa moja unaohusu jamii katika dunia hii ya leo ya utandawazi, utakuwa ni wa makosa iwapo hatujachambua siasa na uchumi kwa ujumla wake. Na uchambuzi wa moja kwa moja unaohusu siasa katika dunia hii ya leo ya utandawazi, utakuwa ni wa makossa iwapo hatujachambua uchumi na jamii kwa ujumla wake, na hali kadhalika. 
Kisayansi, utafiti na uchambuzi wa pamoja wa mambo yanayohusu jamii, siasa na uchumi ndiyo suluhisho la manufaa ya jamii ya karne ya 21 (21st century) na si vinginevyo.

Malengo ya makala hii ni kuangaza nchini kwetu Tanzania na kutolea mifano baadhi ya mataifa mengine ya jirani na ya mbali ambayo ni rafiki na Tanzania. Siyo kwasababu nyingine yoyote, ila ni kwasababu ya kuimarisha urafiki wa kweli na iwe ndiyo chachu ya maendeleo kwetu sisi kama Watanzania, kwa Afrika, na hata dunia nzima.
Tupo karne ya 21, na miaka 56 tangu tupate uhuru kutoka kwa mkoloni. Nchi yetu Tanzania inaelekea kubugikwa na utandawazi. Kipato cha mtu wa hali ya chini kimezidi kudidimia na kipato cha mtu wa hali ya juu kimezidi kuongezeka. Maadili kwa ujumla wake katika jamii yamezidi kuporomoka, na maadili katika utumishi wa umma kiasi fulani yameshuka. Tumeona baadhi ya wanasiasa, wanaharakati, na baadhi ya taasisi za kijamii zinatetea uovu na zinakemea yanayoonekana ni mema kwa faida ya jamii. Migongano ya kijamii yanayohusu ndoa za utotoni, ukeketaji na jinsia. Pia nitaelezea tofauti kati ya siasa na dini kisayansi. Yote haya ni changamoto za karne ya 21.
Makala hii ni yenye kuangalia athari ya utandawazi na siasa ya nchini kwetu Tanzania ili iwe ni kioo cha kuangalia wapi tunatoka, na iwe ni mizani ya kuangalia wapi tulipo, ili kwa umoja wetu, makala hii iwe ni moja ya mishale ya mwanga itakayoangaza mustakbali wa taifa letu na tunapoelekea. Ushauri wangu, mbali na kuisoma makala hii mpaka mwisho wake, makala hii iwe ni makala yenye kutusaidia kufikiri na kuzingatia yaliyomo ndani yake, kwasababu bila ya kujua wapi tunatoka, tutakuwa hatujui wapi tunaenda. 

MAELEZO TV: MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI MHE KANGI LUGOLA KWA DUWASA

MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO MAJIMBO YA SIHA, KINONDONI NA KATA NANE YANAKWENDA VIZURI

$
0
0
Na Margareth Chambiri
Zikiwa zimebaki siku 6 kabla ya Uchaguzi Mdogo wa Majimbo ya Siha, Kinondoni na Kata 8 kufanyika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi huo yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na ufumbuzi wa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi RAMADHANI KAILIMA amesema mara baada ya mkutano wa Watendaji wa Tuma na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni Bwana Aron Kagurumujuri.

Bwana Kailima amesema Tume inafuatilia kwa karibu maandalizi ya Uchaguzi Mdogo yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwa ni wajibu wake na kwamba Maafisa wa Tume wako maeneo mbalimbali yanayojiandaa kwa Uchaguzi huo Mdogo utakaofanyika jumamosi Februari 17, Mwaka huu.

‘Tumekuja kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ili kupata taarifa juu ya maendeleo ya Maandalizi. Tumekuja hapa kwa sababu hapa ni rahisi kufika’ amesema Bwana Kailima na kuongeza kuwa maafisa wa Tume wapo katika maeneo mbalimbali yanayofanya Uchaguzi kwa kuwa Tume ina wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Uchaguzi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi Tume imejiridhisha kuwa maandalizi yanayoendelea  vizuri na amepongeza jitihada zinazofanywa na Msimamizi wa Uchaguzi pamoja na Wasaidizi wake katika kuhakikisha kuwa changamoto zozote zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Aidha amewashauri Wasimamizi wa Uchaguzi kuendelea kukutana na Wawakilishi wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kutoa taarifa katika kila hatua ya kuelekea Uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Vyama vinapata taarifa ya kila hatua ya maandalizi ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya mchakato mzima wa Uchaguzi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amesema Tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya Elimu ya Mpiga Kura mfululizo hadi siku ya Uchaguzi, Elimu itakayohusu mada mbalimbali za Uchaguzi zikiwemo Haki na Wajibu wa Mpiga Kura, Wakala wa Vyama vya Siasa na Msimamizi wa Uchaguzi pamoja na taratibu zote za Upigaji Kura.

‘Nawasihi sana watu watembelee Online ya Tume Tv, website ya Tume, kwa jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, facebook na instagram lakini pia App ya Tume, kwa hiyo tumeanza Elimu ya namna hiyo kama eneo la kuelimisha Umma kuelekea tarehe 17 siku ya Kupiga Kura’ amesema Bwana Kailima.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na Udiwani katika Kata 8 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi Februari 17, Mwaka 2018.
 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Emmanuel Kawishe (wa pili kulia) akieleza jambo wakati Tume ilipomtembelea Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni kujua maandalizi ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi Irene Kadushi akieleza jambo wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kushoto) akiongoza kikao.

Mbunge mstaafu wa Kilombero Mhe. Abdul Rajabu Mteketa apelekwa Muhimbili kutibiwa

$
0
0
Mbunge mstaafu wa Kilombero Mhe. Abdul Rajabu Mteketa amepelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaa kwa matibabu, baada ya Jumamosi Februari 11, 2018 kuomba msaada wa kupatiwa matibabu ya upasuaji wa magoti yake. 
Mbunge huyo aliyetumikia jimbo la Kilombero baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka 2010, alitumia njia ya video mtandaoni kupeleka ujumbe kwa Rais na jana Jumapili gari la wagonjwa lilifika na kumchukua kumpeleka Muhimbili. Video ya kwanza inamuonesha Mhe. Mteketa akiomba msaada, unafuatia ukurasa wa Facebook wa mkewe unaomshukuru Rais kwa msaada huku ukisisitiza kuwa wao wasingeweza. Video ya pili inamuonesha mhusika akishukuru akiwa ndani ya gari la wagonjwa.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO FEBRUARY 12,2018

UNESCO KUADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI DODOMA

$
0
0
Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani. Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari. 

  Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo, usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo.Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni, Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo. 

  Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe.Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani.Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio. 

  Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki.Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi. 

  Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika. Si tu redio inatumika kubadilishana Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika.Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii. 

Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO. 

  Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo.Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii, kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na kuboresha uwezo wao katika kazi.

CCM YATOA SEMINA KWA VIONGOZI NA WANACHAMA KATA YA BONYOKWA

$
0
0

Katibu wa CCM Kata ya Bonyokwa, Mohamed Chende, akitoa hotuba yake wakati wa semina elekezi kwa viongozi wa CCM Kata ya Bonyokwa.
Washiriki wa semina hiyo.

Kada wa CCM, Ebeneza Emmanuel akitoa mada katika semina hiyo.

Meza Kuu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

LIVE: Makamu wa Rais Samia Suluhu kwenye uzinduzi mradi wa kuimarisha usimamizi wa Maliasili


UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipulizia dawa shamba la pamba wilayani Kwimba. Uzalishaji wa pamba nchini unatarajiwa kuongezeka mara tano msimu huu wa kilimo 2017/2018 kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Bodi ya Pamba kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha mazoea na kuanza kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba, kuimarika kwa mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo, ubora wa mbegu za kupanda zilizosambazwa kwa wakulima na kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba. 

Akiongea katika ziara ya kukagua maendeleo ya uzalishaji wa mbegu bora wilayani Igunga, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Bwana Marco Mtunga amesema, uzalishaji unatarajiwa kuongezeka kwa takriban asilimia 400 kutoka tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa 2016/17 hadi kufikia zaidi ya tani 600,000 msimu huu wa 2017/18.

 Aliendelea kueleza kwamba, eneo la uzalishaji wa pamba limeongezeka kutoka ekari 659,000 hadi ekari 3,000,000 ambapo jumla ya tani 26,500 za mbegu zimepandwa zikiwemo tani 8,000 za mbegu za msimu uliopita zilizokuwa kwa wakulima. Kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba kumetokana na uhamasishaji uliofanywa katika maeneo inakolimwa pamba, kuongezeka kwa mikoa mipya ya Dodoma na Katavi katika uzalishaji wa pamba na bei nzuri ya pamba waliyolipwa wakulima msimu uliopita.
Waziri wa Kilimo, Eng. Charles Tizeba, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakiongea na mkulima wa pamba wilayani Igunga. 
Waziri wa Kilimo, Eng. Charles Tizeba na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga wakikagua zao la pamba wilayani Igunga. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mtemi Msafiri wakikagua shamba la pamba wilayani Kwimba 


MICHUZI TV ITAKUWA LIVE KUANZIA SAA KUMI

MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

$
0
0
 NA SAMIA CHANDE, KATAVI.

Mradi wa Orio uliotekelezwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Uholanzi na Tanzania  kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesaidia kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 2.5 ambazo zimesaidia  kumaliza tatizo la umeme Wilaya ya  Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.


Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani  Katavi, Mhandisi Julius Sabu, kituo hicho kimesaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo, na kutoa umeme wa uhakika na wenye ubora.“Kituo hicho kinahudumia Wilaya za Tanganyika, Mpanda mjini, maeneo ya Starlike na Kakese”. Aliainisha Mhandisi Sabu.

Lakini pia Kituo kimepunguza gharama za uzalishaji umeme ukilinganisha na Kituo cha zamani.Wakaazi wa Wilaya ya Tanganyika wameishukuru Serikali na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa kuwaletea umeme kwani umekuwa mkombozi katika shughuli zao za kiuchumi, kama vile kuchomelea, "saloon",  na biashara ya maduka.

“Nawashauri Wananchi wenzangu, sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa hii inayotokana na kupata umeme wa uhakika katika kukuza shughuli zetu za kiuchumi.” Alisema Mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maneno Mtogwa mkazi wa Wilaya ya Tanganyika.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi ametoa rai kwa Wananchi wa Wilaya za Tanganyika, Mpanda Mjini, maeneo ya Kakese na Starlike kujitokeza kwa wingi kwenye madawati ya huduma kwa Wateja na Ofisi za TANESCO ili kupatiwa huduma kwani TANESCO imejipanga kuwahudumia Wananchi popote walipo na kwa viwango vya hali ya juu.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu kiwa anakagua mashine kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda mkoani Katavi.

 Kituo cha kufua umeme cha Mpanda Mkoani Katavi

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KAMPUNI TOOKU GARMENT YATOA MSAADA VIFAA VYA TEHEMA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (ACF) Maria Kullaya amepokea msaada wa Kompyuta mpakato moja na Printa moja kutoka katika Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd, kwa ajili ya kuboresha kitengo cha Takwimu cha Jeshi hilo.


Msaada huo wenye thamani ya sh.1.5 million ambao umetolewa na Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd umepokelewa mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliopo barabara ya Ohio Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati akipokea msaada huo Kamishna Msaidizi Maria alisema, msaada huu umetolewa wakati muafaka kwani utasaidia kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi katika ukusanyaji wa taarifa na utunzaji wa kumbukumbu tofauti na hapo awali.Tunatarajia kuvitumia vifaa hivi kwa lengo mahususi pamoja na kuvitunza vizuri “Vifaa hivi vitakuwa chachu kwa kitengo cha takwimu kwani tulikuwa na uhaba wa vitendea kazi” alisema Kamishna Msaidizi Maria.

Naye Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Rigobert Massawe, akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, alisema “lengo ni kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutimiza majukumu yake kwa ufanisi kwani kwa kufanya hivyo tunatimiza wajibu wetu wa kurudisha huduma kwa jamii”.


Kamishna Msaidizi Maria anaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapa msaada wa vitendea kazi hivyo, pia kupitia nafasi hii naomba wadau wengine waige mfano huu kwa kulisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Nyanja mbalimbali ili liweze kutimiza majukumu yake ya kuokoa Maisha na Mali za Watanzania.


 Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) akipokea msaada wa Kompyuta mpakato na Printa kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto). Vifaa vitakavyosaidia kutunza kumbukumbu za takwimu za majanga mbalimbali yanayotokea nchini, msaada huo umepokelewa Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo.

 Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto) akimkabidhi Kompyuta mpakato (Laptop) Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji). 
Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya wa nne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe wa tano kutoka (kulia), Meneja rasilimali watu wa Kampuni hiyo Bw. Danial Mbonea wa tatu kutoka (kulia) na Maafisa wa Jeshi hilo wakati wa makabidhiano ya msaada wa Komputa mpakato na Printa, mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo.

TIGO YAWALETEA WATEJA WAKE 'NYAKA NYAKA'

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza promosheni mpya inayokwenda kwa jina la Nyaka Nyaka ambayo itawawezesha wateja wa Tigo watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Wengine pichani ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza promosheni mpya inayokwenda kwa jina la Nyaka Nyaka ambayo itawawezesha wateja wa Tigo watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wake wote watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter.

Pamoja na haya, wateja hao pia watapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zaidi ya elfu moja ambazo zinatolewa na Tigo katika promosheni hiyo kabambe ya ‘Nyaka Nyaka Bonus’. Akitangaza ofa hizo jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema kuwa ofa hizo murwa ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaolenga kukutana na mahitaji ya wateja na kuwezesha kila mtu afurahie huduma za kidigitali katika mtandao ulioboreshwa wa Tigo.

“Kupitia mtandao wetu mathubuti wa 4G wateja wetu tayari wanafurahia huduma bora zaidi za intaneti. Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inatoa fursa kubwa kwa wateja wengi zaidi kumiliki simu janja zenye uwezo wa 4G na kupokea bonasi kubwa za data zitakazowawezesha kuwa sehemu ya mageuzi makubwa ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ alisema.

Tigo ndio mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake ambapo katika soko la simu za mkononi nchini, ni wateja wa Tigo pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila kifurushi wanachonunua. Tigo pia imejizolea umaarufu mkubwa kwa promosheni zake bunifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kupitia promosheni mpya ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inalenga kuongeza matumizi ya data pamoja na kuongeza matumizi ya simu janja za kisasa (Smartphone) nchini, hivyo kuisogeza Tanzania hatua moja mbele zaidi katika ulimwengu wa kidigitali. ‘Tunafahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado hawajafikiwa na huduma za mtandao na ndio maana Tigo inazidi kuwekeza katika kupanua na kuboresha huduma zake za mtandao.

Kupitia promosheni hii tunalenga kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini,’ alisema. “Tunawakaribisha wateja wetu wote kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00# ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter.

Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Tarik alisisitiza.

KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala  amewataka wamiliki wa shule binafsi zinazoanzishwa wilayani humo kuhakikisha wanatoa elimu iliyo bora na kujikita katika masomo ya sayansi.

Amefafanua kwa sasa nchi ya Tanzania inaingia katika ychumi wa Vlviwanda na kuwasaidia vijana hao wapate ajira kwa urahisi.

Kanali Ndagala aliyasema jana(juzi) wilayani Kakonko wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Berea iliyoko wilayani humo ambapo aliwataka wamiliki kutafuta walimu wenye uwezo wa kufundisha masomo ya sanyansi.

"Lengo la kujikita kwenye masomo ya sayansi ni kupata wataalamu wa viwanda vitakavyo anzishwa kwakua mpango wa Serikali ni kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda na nilazima wazingatie utoaji wa elimu iliyo bora," amesema.Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwa wasilizike na kumaliza elimu ya kidato cha nne, kwani huo ni msingi tu unao fungua maisha yao.

Pia kuhakikisha wanatumia fursa hiyo ya kuwekewa shule karibu kusoma kwa bidii na kuweza kufika mbali ilikuweza kuinua Wilaya ya Kakonko nayo kuwa na viwanda na wataalamu walio elimika.

Hata hivyo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kuwa wazalendo kwa kuwaunga mkono wale wote wanaoanzisha shule kwa kuwapeleka watoto waweze kupata elimu, na kuacha kuwakatisha tamaa wale wato wanaotaka kuwekeza, kwa maneno ya kejeri hali hiyo inapelekea Wilaya hiyo kushindwa kuinuka kiuchumi kwani wawekezaji ndio chachu ya maendeleo katika Wilaya.

"Niwatie moyo wote mnaotaka kuwekeza katika Wilaya hii, Serikali ipo kwa ajili ya kuwatia moyo, na Serikali inahitaji wawekezaji."Nikupongeze mmiliki wa shule hii kwani najua umepitia changamoto nyingi umepitia lakini hukukata tamaa umekuwa mzalendo kuja kuwekeza nyumbani.

"Changamoto zilizopo zifanye kuwa fursa ili tuweze kuhakikisha wilaya yetu inainuka katika elimu na uchumi kwa ujumla", alisema Kanal Ndagala.Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule ya Berea Baraka Mathias alisema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano aliopata ikiwa ni pamoja na  kupatiwa usajili wa shule hiyo.

Ameomba wananchi kuacha tabia ya kuwavunja moyo wale wote wenye nia ya kuinua Wilaya ya Kakonko kwa kuleta maendeleo.Pia amewataka vijana kusimamia malengo yao na ndoto walizonazo kuziishi ili kufanikisha mipango yao na kuwaomba wawekezaji wengine kuja kuwekeza Katika wilaya hiyo ambayo imesahaulika ilikuweza kufungua fursa na kusaidia kuinua uchumi wa Wanakakonko.

Amesema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 103 na ni moja kati ya shule zilizo fanya vizuri wilayani humo, pamoja na changamoto zote hakukata tamaa .Amefafanua amehakikisha anasimamia wazo lake la kuanzisha shula katika  wilaya hiyo na wanafunzi wapate elimu kwa ukaribu zaidi. 
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikata utepe kufungua shule ya Sekondari Berea
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza wakati wa kufungua shule ya Sekondari Berea -

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AKUTANA NA BALOZI WA KOREA KASKAZINI KIM YONG SU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya watu wa Korea Kaskazini Kim Yong Su alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Februari 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama akimueleza Balozi wa Jamhuri ya watu wa Korea Kaskazini Kim Yong Su jinsi ofisi yake inavyoratibu masuala ya kazi na ajira. Katikati ni katibu wa Balozi Jang Myong Su.
Balozi wa Jamhuri ya watu wa Korea Kaskazini Kim Yong Su akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama baada ya mazungumzo yaliyofanyika tarehe 12 Februari 2018, jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA KUENDELEZA UTALII UKANDA WA KUSINI (REGROW)

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi. 

Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima .

Makamu wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.

Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

MICHUZI TV: BILIONI 560/- KUKAMILISHA JENGO LA KIWANJA CHA NDEGE JNIA 'TERMINAL 3'

WAKURUGENZI, WAKURUGENZI WASAIDIZI NA BAADHI YA WATUMISHI OFISI YA BUNGE WAPATIWA SEMINA JINSI YA KUKABILIANA NA VIHASHIRIA HATARISHI NDANI YA OFISI YA BUNGE

$
0
0
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa Wankanga akifungua semina ya Jinsi ya kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya Bunge kwa Wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi, Wakuu wa Vitengo na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Bunge iliyoanza leo katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakifuatilia semina iliyotolewa na Wahadhiri waandimizi kutoka Chuo kikuu cha Mzumbe Jinsi ya kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya Bunge, iliyofanyika leo katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo kikuu Mzumbe, Ndg. Alloyce Maziku akizungumza na Wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi, Wakuu wa Vitengo na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakati akitoa maada katika semina ya Jinsi gani ya kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya Bunge iliyofanyika leo katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Bunge wakifuatilia semina iliyotolewa na Wahadhiri waandimizi kutoka Chuo kikuu cha Mzumbe Jinsi ya kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya Bunge, iliyofanyika leo katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.PICHA NA OFISI YA BUNGE.

NEWS ALERT: SHIRIKA LA MAWASILIANO TANZANIA LAZALIWA, LABATIZWA JINA LA TTCL CORPORATION

HALMASHAURI HANANG YASHAURIWA KUANZISHA CHANZO KIPYA CHA UTALII WA MLIMA HANANG

$
0
0
Na Jumbe Ismailly -HANANG        
PAMOJA na serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini wazazi na walezi wa wanafunzi katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang bado wamekuwa kikwazo cha watoto wao kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Brycosen Kibassa aliyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na kituo hiki alipokuwa akizungumzia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya hiyo kutokana na wazazi au walezi kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani yao ya kumaliza masomo yao.
Aidha Mkurugenzi huyo aliweka bayana kwamba mwaka 2017 Halmashauri hiyo iliweka mpango na wakakubaliana kwamba kiwango cha ufaulu kwa wastani uwe asilimia 80 kwa wilaya na licha ya kufanya majaribio mengi kabla ya kufikia mtihani wa taifa,ambapo katika mtihani wa majaribio walipata wastani wa asilimia 75.
Kwa mujibu wa Kibassa baada ya kufanya mtihani huo wa kitaifa wamepata asilimia sita hali ambayo ni dhahiri kwamba iliwashitua sana na kuanza kuangalia kilichosababisha hali hiyo na katika taarifa za awali walizonano inaonekana wazazi wenye mwamko mdogo wa elimu katika eneo hilo waliwatuma kwa makusudi kabisa watoto wao kwamba wahakikishe hawafanyi vizuri katika mitihani yao.
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,CharlES Yona akisisitiza juu ya umuhimu wa kudumisha ushirikiano katika utendaji wa shughuli zote za Halmashauri ya Hanang,lengo likiwa ni kuisogeza mbele kimaendeleo Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Bryceson Kibassa (wa kwanza kulia) akimpongeza diwani wa kata ya Nangwa,Portagia Baynet muda mfupi baada ya kuapisha na kula kiapo cha uadilifu.


 Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara wakiwa wamesimama kwa muda wa takribani dakika tano kuashiria kumkumbuka mmoja wa madiwani hao aliyepoteza maisha katika siku za hivi karibuni.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nangwa waliohudhuria mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo wasikiliza kinachojadiliwa na wawakilishi wao waliowachagua.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images