Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

News alert: Wakongwe watao wa Goju Ryu Karate-do Kupewaa Hadhi ya "Sensei" Jundokan Tanzania

$
0
0
Mwakilishi wa chama cha Karate Jundokan Tanzania, Sensei Rumadha Fundi amewapa hadi ya ualimu wa sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu mtindo wa Goju Ryu Karate-Do  cheo cha "Sensei" kwa wanafunzi wakongwe 5 wa mtindo wa "Okinawa Goju Ryu Karate-Do". 
Masensei hao ni: 
Sensei  Yusuf Kimvuli
Sensei Abdul  Waheed
Sensei Bilal Mlenga
Sensei Seif Sood 
Sensei Omary Gregory. 
Sensei Rumadha ametoa pongezi kwa moyo na kujitolea kwao katika kuiendeleza sanaa ya Karate, na kusema kwamba hapo wote ni walimu wa ngazi ya pili au "Nidan", na dhamana hii ya sensei itaendelea kuzingatiwa chini ya kanuni na misingi ya chama cha Jundokan Tanzania na ulimwenguni kote.
 Maandalizi ya mwisho ya "Kata "kabla ya mitihani ya mikanda mieusi Zanaki dojo na Kaizen dojo la  Jamhuri jijini Dar es salaam hivi karibuni.
 Sensei Rumadha Fundi (Black Belt 4th Dan), "Shibu-cho" mkuu wa tawi  la Jundokan Tanzania akiwa na Sensei Daudi Magoma na wanafunzi wakongwe wa Hekalu la Kujilinda jijini Dar es salaam baada ya kuwapandisha cheo  
Sensei Rumadha Fundi (Black Belt 4th Dan), "Shibu-cho" au mkuu wa tawi  la Jundokan Tanzania.

Orodha Ya Majina Ya Watumishi Wa Umma Wanaostahili Kulipwa Madai Ya Malimbikizo Ya Mishahara

KTV-TZ: WATANZANIA WANUNUA KANISA UINGEREZA NA KULIGEUZA MSIKITI

WAZIRI MKUCHIKA AMPONGEZA TENGA KWA KUTEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BAMITA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala BoravMhe. George H. Mkuchika akimpongeza Sir Leodegar Chilla Tenga kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BAMITA), akichukua nafasi ya Dionis Malinzi aliyemaliza muda wake. Hapo walikuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi kushuhudia pambano la soka la Ubingwa wa Afrika baina ya Yanga na Sr. Louis ya Ushelisheli. Yanga walishinda kwa bao 1-0

RC Paul Makonda akipambana na migogoro ya ardhi mkoa wa Dar es salaam

NAIBU SPIKA TULIA NA LUSINDE WAONGOZA WABUNGE KUMNADI MTULIA TANDALE

$
0
0
Mbunge wa Mtela ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde ‘Kibajaj’ akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)
Mbunge wa Mtela ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde akihutubia wananchi wakati akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Akson akimuombea kura Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Kinondoni Said Mtulia katika Mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akimuombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Kinondoni Saidi Maulidi Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya shule ye msingi Tandale jijini Dar es Salaam

Mbunge wa Mtela ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde ‘Kibajaj’ akipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa CCM Said Mauli Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam
Wananchi wakishangilia kwa hamasa wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam

AZAM FC WATUA BUKOBA, TAYARI KWA MCHEZO WAO NA KAGERA SUGAR KESHO JUMATATU.

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba.


KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetua Mjini Bukoba asubuhi hii ikitokea Jijini Dar es salaam. Tayari kwa mchezo wao na Wenyeji wao Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba kesho jumatatu. Azam FC katika mchezo uliopita ilifungwa na Simba bao 1-0. Msimu uliopita Kagera Sugar ilifungwa na Azam Fc bao 3-2 kwenye Uwanja wa Kaitaba na msimu huo huo Kagera Sugar waliwafunga bao 1-0 Azam Fc na kuumaliza msimu huo wakiwa nafasi ya tatu.  

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2013/2014, wataendelea kuikosa huduma ya Nahodha Himid Mao ‘Ninja, aliyepewa mapumziko maalum kufuatia majeraha ya goti la mguu wa kulia yanayomsumbua, pamoja na mshambuliaji Wazir Junior na beki Daniel Amoah, ambao nao ni majeruhi.

 Aidha itamkosa nahodha wake msaidizi, Agrey Moris, aliyekusanya kadi tatu za njano, zinazomfanya kukosa mechi moja ijayo, lakini wachezaji wengine wote waliobakia wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo, ukiondoa majeruhi wa muda mrefu Joseph Kimwaga, ambaye anaendelea na programu ya mwisho (recovery) ya kurejea dimbani kwenye ushindani. 

Mpaka sasa Azam FC imejikusanyia jumla ya pointi 33 kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa sawa na Singida United iliyonafasi ya nne, ikizidiwa pointi nane na Simba iliyojikusanyia pointi 41 kileleni huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointi zake 34.

Walipowasili asubuhi hii kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba, Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Kocha wa Azam Fc Idd Nassor Cheche akiteta jambo na mwandishi wa habari(hayupo pichani) mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Kaitaba. Kocha huyo  amesema kilichowaleta ni pointi tatu hakuna kingine huku akiwamiminia sifa wenyeji wao kuwa ni timu nzuri na kwa sasa ipo kwenye sehemu mbaya hivyo mechi hiyo itakuwa  ngumu lakini watafanya jitihada na hatimae wazoe pointi zote tatu.

TRA YAKAMATA BIDHAA MBALIMBALI MPAKANI NAMANGA ZIKITOKEA NCHINI KENYA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata na kutaifisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na tani moja ya sukari na chumvi, majani ya chai mifuko 18, mirungi kilogramu 16, vifaranga vya kuku 5000 na mayai kasha 416 katika mpaka wa Namanga mkoani Arusha zikitokea nchini Kenya kupitia njia zisizo rasmi.
Akizungumza mara baada ya kukamata bidhaa hizo, Meneja Msaidizi wa Forodha mkoani hapo Edwin Iwato alisema bidhaa hizo ni mali ya Joseph Sekino, Innocent Minja na Andrew Lyimo wote wakiwa ni wafanyabiashara kutokea Tanzania na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
"Tumewakamata wafanyabiashara watatu ambao ni Joseph Sekino akiwa amepakia tani moja ya sukari na chumvi na majani ya chai mifuko 18 kwenye gari Na. T 785 AWV, Innocent  Minja akiwa na mayai kasha 416 na mirungi kilo 16 kwenye gari Na. T 443 CQU na Andrew Lymo akiwa na vifaranga vya kuku 5000 kwenye gari Na. T 441 DHW wote wakitokea nchini Kenya kuja mkoani Arusha," alisema Iwato.
Iwato alieleza  kwamba, wafanyabiashara hao waliingiza baadhi ya bidhaa hizo kwa kutumia vifungashio vya bidhaa nyingine za nchini Tanzania ili kuficha uhalisia wake huku wakiwa hawana vibali wala kulipa ushuru wa Serikali kama inavyotakiwa.

Alifafanua kuwa, mirungi ilikamatwa ndani ya mifuko ya plastiki maarufu kama Rambo ikiwa imefichwa kwenye boneti ya mbele ya gari aina Noah Na. T 443 CQU sehemu ya injini.
Naye, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Richard Kayombo alisema, tabia ya wafanyabiashara hao siyo tu inawahujumu wafanyabiashara wenzao bali inakwamisha azma ya Serikali ya kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya kila mwananchi.
"Tabia ya wafanyabiashara hawa siyo nzuri kwa kuwa inakwamisha ukusanyaji mapato ya Serikali na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine wanaofikiria kufanya biashara pasipo kutumia njia rasmi na kulipa ushuru ipasavyo", alisema Kayombo.
Aidha, Kayombo aliongeza kuwa, bidhaa zote haramu zilizokamatwa zitateketezwa kwa mujibu wa Sheria, zile zinazofaa kwa matumizi ya binadamu zitagawiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zenye uhitaji kwa mujibu na taratibu zilizowekwa na TRA na magari yote yaliyotumika kusafirisha bidhaa hizo yametaifishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Utaifishaji wa magari na bidhaa ambao usafirishaji wake haufuati sheria na taratibu, unalenga kukomesha shughuli za magendo nchini ambazo kwa kiasi kikubwa zinakwamisha juhudi za Serikali katika ukusanyaji wa mapato.


Meya Mwita aungana na wananchi jiji la Dar es Salaam kupima magonjwa ya Kisukari,Presha.

$
0
0
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameungana na wakazi wa jijini hapa katika kongamano la  kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha lililoandaliwa na Lions Clubs International kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Irania  kilichopo jijini hapa.

Katika kongamano hilo Meya Mwita amewapongeza waandaaji  na kuwaeleza kuwa wasiishie hapo hivyo wafikishe huduma hiyo kwenye halmashauri nyingine za jiji la Dar es Salaam ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo.

Meya Mwita amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kucheki afya zao hususani inapojitokeza fursa hizo kwa kuwa baada ya kupata majibu ya vipimo hivyo inawapa urahisi katika kupata matibabu.Amesema Taasisi hizo zimekuwa na mchango mathubuti  kwa wananchi kutokana na uzalendo mkubwa waliokuwa nao na hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

"Jambo hili ni muhimu sana, ninawapongeza, ombilangu kwenu, angalieni namna ya kuendelea kuwasaidia wananchi wengine katika jiji letu la Dar es Salaam, huduma hii ni ya muhimu sana na kila  mwananchi anahitaji kuipata" amesema Meya Mwita.

Awali akimkaribisha Meya Mwita, Rais wa Lions Clubs Shaheen Alam amempongeza na kumueleza kuwa  wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha  Iranian kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao.

Imetolewa leo Februali 11 na  Christina Mwagala Afisa Habari Ofisi ya Meya wa Jiji. 
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akijiandaa  kupima Kisukari leo aliposhiriki kongamano la kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha .
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata kipimo cha Presha kutoka kwa Dokta Mahmod Shahamati ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Iranian kilichopo jijini hapa.

Chama cha AFP chafanya uchaguzi mkuu, chajipanga kushika dola 2020

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) ,Said Sudi Said amesema chama kimejipanga kushika dola katika uchaguzi  mkuu utakaofanyika mwaka 2020 kutokana na mikakati walioiweka ya kushika dola hiyo.
Said  ambaye ni Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyasema hayo katika Uchaguzi Mkuu chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Executive  jijini Dar es Salaam, amesema kuwa AFP ni chama chenye mtazamo chanya katika masuala ya uongozi ya kuwatumikia wananchi.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweza kuleta amani kwa wananchi lakini wenyewe wakishika dola watafanya zaidi kudumisha amani.
Nae Katibu Mkuu wa Chama hicho, Rashidi  Rai amesema kuwa wabunge waangalie sheria ya uchaguzi mdogo kuwa imebadilishwe kwa mtu atakayejiuzulu uchaguzi usifanyike badala yake Mbunge wa jimbo lilokaribu ataweza kutumikia.
Amesema kuwa ni gharama kubwa ya uchaguzi kwa fedha hizo zinaweza kutumika katika masuala mengine ya maendeleo ya wananchi kutokana na changamoto zilizopo za kukosekana kwa fedha.
Katika uchaguzi Mkuu Said Sudi Said alishinda nafasi hiyo kwa kura zote za wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na Katibu Mkuu huku na nafasi zingine za jumuiya zilishapata  viongozi
 Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) , Said Sudi Said akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho pamoja na uchaguzi mkuu uliofanyika katika katika ukumbi wa Executive jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Chama cha AFP, Rashidi Rai akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu kuhusiana na utaratibu wa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Executive jijini Dar es Salaam. 
 Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Chama cha AFP.
Sehemu ya Wasimamizi wa uchaguzi Mkuu wa Chama cha AFP.

Welcome to Uzi Crafts where we teach sewing to kids, teenagers and adults

$
0
0
Greetings,
I would like to invite you to our world of Sewing DIY (Do it Yourself) at UZI Crafts where we teach sewing to kids, teenagers and adults as a much needed life skill.
You will find more information on our website www.uzi.co.tz and you can follow our blog as we explore and expound on the beautiful neglected life skill craft of sewing.
The first blog post talks about how Uzi Crafts came to be, see if you can find yourself there.
Should you no longer wish to receive emails from us, just click on unsubscribe link below. Otherwise welcome aboard.
Super excited by the possibilities.
P.S. Do share with those you believe will benefit from this information.
Kind Regards
Mary MugurusiCEO and Founder
info@uzi.co.tz
+255 628 88 99 44

WANANCHI WASHUKURU SERIKALI UJENZI WA DARAJA LA MTO KILOMBERO

$
0
0
Wananchi wa wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza ahadi waliyoitoa kwa wananchi hao ya kuwajengea daraja la mto kilombero ambalo lilikuwa kilio chao cha muda mrefu.
Wakizungumza mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika kijiji cha Kivukoni, mkoani Morogoro, wakazi hao wamemueleza kuwa hivi sasa changamoto zao zimetatuliwa baada ya kukamilika kwa daraja hilo.
“Tunaishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja hili kwani limekuwa mkombozi kwetu wananchi wa wilaya za ulanga na kilombero kwani hapo nyuma vifo vingi vimetokea pasipo kutegemewa wakati tukitumia kivuko kufuata huduma za kijamii wilaya jirani ambapo ndio kuna huduma zote za muhimu”, amesema Bi. Zainabu Mtalanga
Aidha Waziri Prof. Mbarawa ametoa wito kwa wananchi hao kulilinda daraja hilo kwa kutojihusisha na vitendo vya kuchimba kokoto chini ya daraja, kuiba alama za barabarani na kuacha kupitisha mifugo juu ya daraja kwani Serikali imetumia gharama kubwa kujenga daraja hilo na barabara unganishi katika eneo hilo.
Ameongeza kwa sasa Serikali  ipo katika hatua za kujenga kituo cha polisi katika maeneo hayo ili kimarisha ulinzi na kuhakikisha usalama unakuwepo kwa saa 24 siku saba kwa wiki.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga amemueleza Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa daraja hilo umejengwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba na mkandarasi wa kampuni ya M/S China Railway 15 Group Corporation.
Kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 ambazo zimegharamiwa na Serikali na daraja hilo litarahisisha shughuli za usafirishaji wa mazao, ufugaji na madini katika wilaya hizo na wilaya jirani.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akikagua daraja la mto Kilombero lenye urefu wa mita 384 ambalo linaunganisha wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro ambapo mpaka sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100. Katikati ni ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Ulanga, alipokuwa akikagua Daraja la Kilombero mkoani Morogoro.
 Muonekano wa Daraja la Kilombero lenye urefu wa mita 384 ambapo ujenzi wake umegharimiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 50.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


ROTALY CLUB YATOA MICHE YA MITI 4000 KWA SHULE 6 MANISPAA YA SONGEA

$
0
0
 Viongozi wa Club ya Rotaly tawi la Songea moani Ruvuma wakiangalia kitalu kimojawapo cha miti kilichooteshwa na klub hiyo,ili miti iweze kusambazwa katika shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Songea.
Rais wa club ya Rotaly Tawi la Songea Albert Kessy wa pili kushoto pamoja na  baadhi ya viongozi wakikabidhi miche ya miti kwa mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali  ya Roots And Shoots inayofanya kazi ya uelimishaji kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari moani Ruvuma katika uhifadhi wa mazingira jamii na wanyama Oddo Ngatunga katikati.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI MUFINDI

$
0
0
 ​Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ikiwa na lengo la kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi  la upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo leo alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.

Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi  la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia  huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .

Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya Ihongole Mafinga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Mgololo, Mufindi mkoani Iringa mara baada ya kulifungua ,pembeni yake ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Rai wanaomiliki kiwanda cha Mufindi Paper Mills Bw. Jaswant S. Rai na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza. 


MICHUZI TV: MKUTANO WA KAMPENI ZA UBUNGE CCM JIMBO LA KINONDONI LEO


TANAPA YAKADIDHI MIRADI YENYE THAMANI YA SH,MILIONI 99 WILAYANI CHATO

$
0
0
Na,Joel Maduka,Geita

Shirika la hifadhi ya Taifa (TANAPA) limedhamini ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu wa shule mpya ya sekondari ya Kikumbaitale iliyopo kata ya Kigongo pamoja na Boti yenye injini kwa kijiji cha Mwekani vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 99.

Akikabidhi miradi hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita mwenyekiti ya Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi alisema mradi wa vyumba vya madarasa umetekelezwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe,kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimekadkugharimu juml a ya shilingi milioni 6.

"Madarasa haya yatapunguza tatizo la upungufu wa vyumba kusomea ambalo lipo katika shule za sekondari ya Kigongo .Kukamilika kwa madarasa haya kutasaidia kuanzishwa kwa shule ya sekondari ya Kikumbaitale ikiwa ni sehemu ya shule ya Kigongo mpaka itakapopata usajili wa kudumu",alisema Kijazi.

Aidha Dkt. Kijazi alisema TANAPA imeamua kufadhili boti ya kisasa yenye injini na maboya ikiwa na thamani ya shilingi milioni 47 kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutokana ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria “ ni kutokana na ushirikiano huo TANAPA kupitia hifadhi kisiwa cha Rubondo ilipokea na kupitisha maombi toka kwa wananchi wa kijiji cha Mwelanina kuwapatia mradi wa Boti, injini na maboya yake ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel ameishukuru TANAPA kwa ufadhili wa miradi hiyo na kuahidi kuwa mkoa itasimamia vyema miradi hiyo na pia amewataka wakazi wa Chato kuendelea kutoa taarifa za kuhusiana na uvuvi haramu na kwamba wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kubaini nyavu haramu ambazo bado hazijasalimishwa.
Boti ya kisasa yenye injini na maboya ikiwa na thamani ya shilingi milioni 47 imekabidhiwa kwa kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutokana ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria. 
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo wakiwa kwenye hafra fupi ya makabidhiano. 
Vyumba vya madarasa ambavyo vimejengwa na TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe,kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimekadkugharimu juml a ya shilingi milioni 6. 
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi akizungumza na wananchi namna ambavyo wameweza kutekeleza miradi yote miwili na kutoa kwa wananchi ambao wanazunguka kisiwa cha hifadhi ya Rubondo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara akizungumza na wananchi ambapo aliwasisitiza kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale. 

WANANCHI WASHUKURU SERIKALI UJENZI WA DARAJA LA MTO KILOMBERO

$
0
0
Wananchi wa wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza ahadi waliyoitoa kwa wananchi hao ya kuwajengea daraja la mto kilombero ambalo lilikuwa kilio chao cha muda mrefu.

Wakizungumza mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika kijiji cha Kivukoni, mkoani Morogoro, wakazi hao wamemueleza kuwa hivi sasa changamoto zao zimetatuliwa baada ya kukamilika kwa daraja hilo.
“Tunaishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja hili kwani limekuwa mkombozi kwetu wananchi wa wilaya za ulanga na kilombero kwani hapo nyuma vifo vingi vimetokea pasipo kutegemewa wakati tukitumia kivuko kufuata huduma za kijamii wilaya jirani ambapo ndio kuna huduma zote za muhimu”, amesema Bi. Zainabu Mtalanga
Aidha Waziri Prof. Mbarawa ametoa wito kwa wananchi hao kulilinda daraja hilo kwa kutojihusisha na vitendo vya kuchimba kokoto chini ya daraja, kuiba alama za barabarani na kuacha kupitisha mifugo juu ya daraja kwani Serikali imetumia gharama kubwa kujenga daraja hilo na barabara unganishi katika eneo hilo.
Ameongeza kwa sasa Serikali  ipo katika hatua za kujenga kituo cha polisi katika maeneo hayo ili kimarisha ulinzi na kuhakikisha usalama unakuwepo kwa saa 24 siku saba kwa wiki.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga amemueleza Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa daraja hilo umejengwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba na mkandarasi wa kampuni ya M/S China Railway 15 Group Corporation.
Kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 ambazo zimegharamiwa na Serikali na daraja hilo litarahisisha shughuli za usafirishaji wa mazao, ufugaji na madini katika wilaya hizo na wilaya jirani.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akikagua daraja la mto Kilombero lenye urefu wa mita 384 ambalo linaunganisha wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro ambapo mpaka sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100. Katikati ni ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Ulanga, alipokuwa akikagua Daraja la Kilombero mkoani Morogoro jana.
Muonekano wa Daraja la Kilombero lenye urefu wa mita 384 ambapo ujenzi wake umegharimiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 5
0.

WAKAZI WA KIPUNGUNI KUPISHA UPANUZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA JULIUS NYERERE (JNIA)

$
0
0

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kipunguni A na Mashariki, Dar es Salaam kuhusu ulipwaji wa fidia kwa wananchi hao, ili kupisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongele.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo, akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kipunguni A na Mashariki, Dar es Salaam kuhusu ulipwaji wa fidia kwa wananchi hao kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Mkazi wa Kipunguni Mashariki Dar es Salaam leo akichangia mada katika mkutano wa ulipwaji wa fidia kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


Mkazi wa Kipunguni Mashariki, Bw. Daudi Peter, akichangia hoja katika mkutano wa ulipwaji wa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayon gela, akizungumza na wanannchi Kipunguni A na Mashariki, kuhusu ulipwaji wa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege.

Introducing "Kibenten" by Beka Flavour

WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO WA KWENYE ZOEZI LA UANDIKISHAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA UNAOENDELEA NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dr. Mwiguli Lameck Nchemba awewataka watanzania kuwa wazalendo wa kweli kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye mikoa 19 ya Tanzania kwa kuwafichua wale wote wanaojipenyeza kutaka kusajiliwa kama Raia.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizindua shughuli za Usajili na Utambuzi wa Watu katika Mkoa wa Morogoro Jumamosi katika viwanja vya Shujaa mkoani humo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew Massawe akisoma taarifa ya zoezi la Usajili na Utambuzi  wa Watu kwa mikoa 19 inayoendelea na Usajili; amesema mkoa wa Morogoro unakusudiwa kusajiliwa zaidi ya wananchi 960,000 wenye umri wa miaka 18  na kuendelea. Zoezi ambalo limepangwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili,2018.
“ Mkoa wa Morogoro zoezi litahusisha Wilaya zote isipokuwa Kilombero ambayo ilikuwa Wilaya ya kwanza ya mfan kufanyiwa usajili mwaka 2012 na hivyo idadi kubwa ya wananchi wake tayari wana Vitambulisho vya Taifa na kwasasa wanaosajiliwa ni wale wanaotimiza umri wa miaka 18 na wanaohamia “ asisisitiza
Aidha ndugu Massawe amemweleza Mhe. Waziri mbali na Usajili Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wengine imeanza matumizi ya Vitambulisho vya Taifa ikiwemo Usajili wa Makampuni unaofanywa na Brella ambao kwa sasa unataka kila anayesajili Kampuni kuwa na Kitambulisho cha Taifa. Huduma nyingine ambazo kwa sasa huwezi kuzipata bila kuwa na Kitambulisho cha Taifa ni upatikanaji wa Hati za kusafiria(Passport), Usajili wa namba za simu na huduma nyingine za kifedha n.k
Katika hotuba yake Mhe. Waziri amekemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kudai posho au kuhusisha michango na tozo mbalimbali wakati wa kuwasajili wananchi wakati zoezi hilo ni bure. Amesisitiza Mamlaka  zote za Serikali kuhakikisha zinasisimia na kutoa ushirikiano kwa NIDA kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa kwa wakati wakiwemo Wageni na Wakimbizi kwani shughuli ya usajili kwa sasa inahusisha makundi yote.  Pindi wakati utakapofika kwa wale wote ambao watakuwa hawakusajiliwa watakuwa na cha kujieleza kwanini hawakusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakati Serikali imewekeza fedha nyingi kukamilisha zoezi hili.
Amesisitiza Usajili Vitambulisho vya Taifa si hiyari ni wajibu wa kila Raia, Mgeni na Mkumbizi kusajiliwa kwa kufuata taratibu, sharia na kanuni za Usajili zinazosimamiwa wakati wa utekelezaji wa Usajili.
“ Kama mnavyofahamu Serikali ya Awamu ya Tano chini Mhe. Dr. John Pombe Magufuli ina vipaumbele vingi na mahitaji kwa wananchi ni mengi. Sasa Rais ameacha mambo mengine akaamua kuwekeza kwenye Vitambulisho vya Taifa mradi unaoigharimu Serikali fedha nyingi sana; sasa ole wao ambao hawatasajiliwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe amewataka wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kusisitiza hatowafumbia macho wale wote watakao husisha zoezi hilo na itikadi za vyama au dini, au kudai rushwa kuwahudumia wananchi pindi wanapojitokeza kwenye vituo vya kusajiliwa.
Zoezi la Usajili wanachi Vitambulisho vya Taifa linakusudiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kuwa wamesajiliwa na kupata namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) wakati hatua za Uzalishaji zikiendelea sambamba na kuvigawa kwa wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe akisoma taarifa kuhusu mkakati wa mkoa kuwasajili wananchi zaidi ya 960,000 wakati wa sherehe za Uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
 Mbunge wa Morogoro Mjini  Mhe. Aziz Abood akitoa salamu kwa wananchi waliofurika kushuhudia sherehe za Uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa Morogoro.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Dr. Mwigulu Lameck Nchemba akihutubia wananchi wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu wenye lengo la Kutoa Vitambulisho vya Taifa Morogoro.

  Mhe. Waziri (Katikati)  akizindua rasmi kuanza kwa Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro. Wengine ni  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Steven Kebwe (Wa kwanza kulia), Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Aziz Abood (Wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndugu Andrew  Massawe (watatu kulia), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kiyanga ( wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo (wa kwanza kushoto).
 Mhe Waziri wa Mambo ya Nchi pamoja na viongozi wengine wakishuhudia mmoja wa wananchi Bi. Rehema Abdallah akisajiliwa kwa mara ya kwanza na taarifa zake kuingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa NIDA wakati wa sherehe za Uzinduzi Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro.
Pamoja na kuzindua kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho mkoani Morogoro Waziri Mwigulu pia alizindua kuanza kutolewa Vitambulisho kwa wananchi ambao wamekamilisha taratibu za Usajili.  Hapa anamkabidhi Bi. Jackline Kayombo kitambulisho chake.
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live


Latest Images