Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

SIMIYU YAPATIWA CHUPA MIL 2 ZA VIUAWADUDU WA PAMBA

$
0
0
NA COSTANTINE MATHIAS, SIMIYU.

SERIKALI imewahakikishia wakulima wa Pamba Mkoani Simiyu kuwapatia pembejeo za kilimo ili kukabiliana na wadudu waharibifu ambao wameanza kushambulia zao hilo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe alipofanya ziara ya kukagua mashamba ya wakulima na kujionea changamoto zinazowakabili, ikiwemo mazao yao kushambuliwa na wadudu katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

‘’tumeanza kusambaza pembejeo kwa wakulima mkoani Simiyu baada ya kuona mahitaji ya dawa ni makubwa…awali tulipanga kusambaza chupa milioni 1.8, Lakini mahitaji yamekuwa ni makubwa tumeongeza na kufikia chupa milioni 2 ili kusuru zao hilo’’ alisisitiza Katibu Mkuu.

Aliongeza kuwa wizara ya kilimo imesambaza watalamu 30 nchini ili kusaidiana na wataalamu kilimo ngazi ya mkoa, wilaya na kata katika kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya dawa, pia namna ya kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao.

Mtigumwe aliwataka wataalamu wa kilimo kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ili kuhakikisha dawa zinazosambazwa zinatumika ipasavyo.Tindigwe Masuke mkulima wa Pamba kijiji cha Mbiti alisema kuwa dawa zinazosambazwa na serikali hazitoshelezi mahitaji ya wakulima ambao wahamasika kulima, wamekuwa wakipata kidogokidogo hali inayowafanya kushindwa kuwakabili wadudu wa pamba.

Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya Pamba kanda ya Ziwa, Jones Bwahama alisema kuwa serikali kwa kusirikiana na bodi ya Pamba imeleta timu ya wataalamu saba katika mkoa wa simiyu ili kusaidia na maafisa ugani kuelimisha wakulima jinsi ya matumizi sahihi ya pembejeo.

Mkoa wa Simiyu unahitaji chupa za dawa 1,810,839 huku kukiwa na jumla ya wakulima wa pamba 309,511 ambao wamelima ekari 602,409 likitarajiwa kuzalisha tani 421,686.3 za pamba kwa wastani wa kilo 700 kwa ekari moja.
Dawa za kuuwa wadudu wa Pamba.
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mathew Mtigumwe (mwenye miwani) akimsikiliza mkulima wa pamba Tindigwe Masuke wa kijiji cha Mbiti alipokuwa akiongelea juu ya uhaba wa dawa, unaowakabili wakulima hao.
Meneja wa Bodi ya Pamba kanda ya ziwa Jones Bwahama akitoa maelezo kwa katibu mkuu wizara ya kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe namna walivyojipanga kuhakikisha wanasambaza dawa zilizotolewa na selikali ili kukabiliana na wadudu wanaoshambulia zao hilo.
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akipata maelezo namna wadudu wanavyoshambulia zao la pamba toka kwa Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Bariadi Alfred Chagula, walipotembelea mashamba ya wakulima jana huko mbiti.PICHA NA COSTANTINE MATHIAS

SERIKALI YAWASIMAMISHA KAZI MAAFISA UTUMISHI HALMASHAURI WILAYA YA KWIMBA KWA KUTOWAJIBIKA

$
0
0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akikagua moja ya jalada la mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kujiridhisha juu ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akimhoji Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba sababu za kutomchukulia hatua mmoja wa watumishi mwenye tatizo la cheti licha ya kuwepo taarifa ambazo zinamuwezesha kuchukua hatua.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika kikao na Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kujiridhisha juu ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Zephania Mshanga (katikati) akipitia orodha ya watumishi waliohakikiwa vyeti vya ufaulu wa kidato cha nne na cha sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika mazungumzo ya kikazi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi, Bw. Clodwing Mtweve alipomtembelea Ofisini kwake Katibu Tawala huyo. Katikati ni Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Zephania Mshanga akifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.

JAFO AAGIZA TATHMINI YA KINA IFANYIKE KUKAMILISHA JENGO LA HALMASHAURI YA CHAMWINO.

$
0
0
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kuagiza Wakala wa Majengo(TBA)na Suma JKT kuangalia njia bora ya kulifanya jengo hilo liweze kukamilika kwenye ubora unaotakiwa ili watumishi wahamie.

Watumishi wa Halmashauri hiyo kwasasa wanatumia jengo la Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na jengo lao kutokamilika.Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari mosi mwaka huu.Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi huo, Jafo amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa zilizofanya kukwama kukamilishwa kwa jengo hilo.

“Jengo hili awali lilikuwa linajengwa na mkandarasi mwingine lakini kutokana na utendaji wake kutoridhisha tuliamua kumpatia Suma JKT na niliagiza jengo likamilike Januari mosi mwaka huu, lakini bado halijakamilika,”alisema


Amesema sababu zilizotolewa ambazo mkandarasi amekumbana nazo ameona ni vyema watumishi wakaendelea kuvumilia kutumia ofisi ya Mkuu wa wilaya hadi hapo itakapokamilika kwenye ubora unaotakiwa.Waziri Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na kwamba kwa kuwa wanaelekea katika mipango ya bajeti wataangalia namna ya kushirikiana na Halmashauri ili jengo liweze kukamilika.

  
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATENDAJI TIMIZENI WAJIBU WENU KUONDOA MIGOGORO – IYOMBE

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe amewaasa watendajii wa mkoa wa Manyara kuchukua hatua stahiki zinazohusu masuala ya watumishi ili kupunguza au kuondoa migogoro mkoani Manyara.

Katibu Mkuu Mhandisi Iyombe ameyasema hayo mjini Babati wakati akiongea na watendaji na watumishi wa Mkoa wa Manyara, Halmashauri ya Mji Babati na Halmashauri ya Wilaya Babati kwamba kiwango kikubwa cha migogoro hasa ya ardhi mkoani humo inatokana na baadhi ya watendaji kutotimiza wajibu wao ipasavyo hali wakizingatia sheria na taratibu za nchi.

“migogoro mingi inaanzia Sight (sehemu wanazotwaa ardhi ili kupima) kwa kuleta taarifa iliyo na mapungufu na pia zingatieni sheria za ardhi, migogoro ipungue kwa kwa kutenda”

Pia Mhandisi Iyombe amesema wapo Watendaji ambao wanashindwa kutumia Mamlaka waliyopewa na kuzuia migogoro ya ardhi ambayo inazuilika lakini pia amehoji mbona mipaka ya mikoa na wilaya ipo wazi na kwanini sehemu nyingine za kiutawala, “msilazimishe migogoro ya ardhi kwani tumewapa mamlaka kwa kufanya Ugatuaji wa madaraka (D by D) hivyo amueni”
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Babati wakati wa ziara yake leo
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Babati wakati wa ziara yake leo
Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) walioshiriki ziara ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI Mha. Mussa Iyombe wakiwa katika chumba cha mikutano Babati leo
Katika picha ya pamoja ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Misaile Mussa wakisikiliza taarifa ya Halmashauri ya Mji Babati
Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Mkoa wa Manyara, Babati Mji na Halmashauri ya Wilaya Babati wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe alipokuwa akiongea nao mjini Babati leo
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe alipowasili katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Babati kuongea na watumishi leo.

Tanzania Yaendelea KupunguzA Vikwazo Vya kibiashara Visivyo Vya kiushuru Na Tozo Mbalimbali

$
0
0
Tanzania yaridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani
40 kwa wasafirishaji wa mizigoTanzania imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 (USD40) inayotozwa kwa kila stika kwenye magari yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi. Hatua hii imefikiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla.

Tozo hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi. Baada ya tathimini Serikaliimebaini kuwa tozo hii inasababisha usumbufu na kuongeza gharama kwa wasafirishaji wa mizigo. Hata hivyo hatua hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa mtekelezaji mzuri wa makubaliano na itifaki mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huu uliofanyika kwa kipindi cha siku tatu tarehe 7 hadi 9 Februari 2018, pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru (NTBs) ambavyo vimekuwepo
kwa muda mrefu katika Jumuiya. Mkutano huu umefikia tamati leo katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.

Taratibu za kuanza kufuta
tozo hii zinaanza kutekelezwa mara moja.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
9 Februari 2018
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. CharleS Mwijage(Mb) akifuatilia Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. CharleS Mwijage(Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki 
Mkutano ukiwa unaendelea

MAKAMU WA RAIS KATIKA SIKU YA PILI WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akisoma taarifa ya wilaya yake mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati ziara ya Makamu wa Rais wilayani Kilolo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Wilaya ya Kilolo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (kulia) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
 Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA

$
0
0
Na: Sekela Mwasubila - Kondoa

Mamlaka ya Elimu Tanzania imekabidhi rasmi mradi wa ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa tukio lililofanyika katika ukumbi wa shule hiyo hivi karibuni.

Akikabidhi mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Elimu Tanzania Graceana Shirima alisema ni matumaini yao kuwa fedha hizo zitatumika kwa ufanisi mkubwa na makusudio waliyoyaweka na matokeo yake yaonekae kwani iliyotolewa ni nyingi.

Aidha aliongeza kuwa lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha kuwa shule inakuwa na mazingira mazuri kwa ajili ya kupata elimu iliyokusudiwa na kuongeza ufaulu kwani miundombinu ya maabara, maktaba na madarasa vyote vitakarabatiwa na kuwa na mwonekano mzuri kwa mwanafunzi kusoma.

“Tuna imani uongozi wa Halmashauri ya Mji na Bodi ya Shule hawatatuangusha katika usimamizi na watatumia fedha hizi kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taratibu zote za manunuzi zinazingatiwa na hatutasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwenda kinyume na taratibu za manunuzi sababu mradi huu force akaunti ambayo inatumia jamii zaidi” Alisema Bi Graceana

Akiongea kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mh. Hamza Mafita alisema wanaishukuru serikali kwa kuwaletea fedha zote za mradi kwani fedha hizo zitabakia kwa wananchi wa Kondoa kwani mafundi watanunua vifaa vyote Kondoa na mafundi ni wenyeji wa Kondoa na kuwataka mafundi kumaliza mradi huo kwa wakati na haoni sababu ya kuchelewa ikiwa fedha zote zipo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Khalifa Kondo akipokea mradi huo alisema kuwa anashukuru kupata mradi huo sababu ingekuwa ni jukumu la Halmashauri kukarabati kwa kutumia mapato ya ndani na kuahidi kuzisimamia fedha hizo kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri na Bodi ya shule ili kuhakikisha lengo la mradi linakamilika.

Mamlaka ya Elimu Tanzania imetoa kiasi zaidi ya bilioni kumi kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe Tanzania ikiwemo Shule ya Wasichana Kondoa ambapo imepewa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo.
Sehemu ya Mabweni yanayoendelea na ukarabati katika shule ya Wasichana Kondoa
Kaimu Mkurugenzi wa Malmaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo orodha ya vifaa kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa. 
Mafundi wakiendelea na uchimbaji wa shimo la maji machafu ikiwa ni sehemu ya ukarabati wa mfumo wa miundombinu ya maji machafu katika shule ya wasichana Kondoa
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Wasichana Kondoa.
Picha ya Uongozi wa Mamlaka ya Elimu na Halmashauri ya Mji katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Wasichana Kondoa.

yanga yaiduwaza st.louis,yaikuna bao 1-0

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Yang wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya st Louis ya Visiwa vya Shelisheli katika mchezo uliochezwa leo Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kwanza katika hatua ya mtoano uliopigwa leo, ilichukua takribani dakika 67 kwa Yanga kuandika goli la kwanza na la ushindi kupitia kwa mchezaji wake Juma Mahadhi aliyeingia kuchukua nafasi ya ibrahim Ajib.

Yanga ilishindwa kutumia nafasi walizozipata katika kipindi cha kwanza ikiwemo penati aliyoipiga Obrey Chirwa na kuitoa nje.St Louis imepoteza mchezo wao wa kwanza lakini walionekana wakijilinda kwa mda wote.

Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema kuwa wameona wapi walipokosea ila katika mchezo wa marudiano  utakaofanyika wiki mbili zijazo.

Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu hatua inayofuata ya Klabu Bingwa Afrika mechi itakayochezwa Februari 19 mwaka huu.

WILAYA YA TUNDURU YAPIGWA JEKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAKAYAYA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera kulia, akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 25 kutoka kwa  meneja mawasiliano wa Shirika la maendeleo la Petroli Nchini(TPDC) Marie Msellemu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya wilayani humo.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera katikati na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya  hiyo Chiza Malando kulia,wakifurahia mfano wa Hundi ya shilingi milioni 25  iliyotolewa na Shirikala maendeleo ya Petroli Nchini(TPDC) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya ambacho kinatajwa mara kitakapokamilika kitasaidia kusogeza huduma za matibabu kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka  kituo hicho kushoto ni meneja mawasiliano wa TPDC Marie Msellemu.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera,akimtembeza meneja mawasiliano wa Shirika la Petroli Nchini Marie Msellemu maeneo mbalimbali ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Nakayaya ambacho ujenzi wake umeibuliwa na kuanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kwa kutumia wafadhili mbalimbali.Picha na Muhidin Amri
 Sehemu ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya Nakayaya kiendelea kengwa,kikiwa chini ya simamizi mkbwa wa DC Homera,kituo hicho kinataraiwa kukamilika Septemba mwaka huu 2018. 
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera kushoo akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Vinesh Mathew wa korosho Africa  Ltd kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya wilayani humo.


Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma amepokea hundi ya fedha kutoka shirika la maendeleo ya petrol Tanzania TPDC ambayo ilikabidhiwa na Bi Marie Mselemu Mkurugenzi wa Mawasiliano TPDC .

Bi Marie Mselemu aliongozana na wasaidizi wake akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya petroli Eng Musomba, hata hivyo Bi Marie Mselemu alisema walifikia maamuzi ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Nakayaya ili kuunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya ndg Juma Zuberi Homera na pia waliandikiwa barua na  DC Homera ambaye aliibua wazo hili kwa lengo la kukabiliana na msongamano mkubwa wa wagonjwa ulioko hospital ya wilaya Tunduru.

Kwa upande wake DC Homera alilishukuru shirika hilo na kaimu Mkurugenzi huyo kwa moyo wa kizalendo walioonesha kwa wananchi wa Tunduru na pia Homera alisema shirika limeunga mkono jitihada za Mhe Rais Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo .

Aidha kwa upande wao kiwanda cha korosho cha Tunduru, Korosho Africa wamechangia fedha za kitanzania million 5 Kati ya million 10 walizoahidi kwa ajili ya kutengeneza madirisha ya chuma ya kituo hicho yani (gril) .kituo hicho mpaka sasa kinaendelea kusimamiwa na Mhe Homera na kinatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka huu 2018.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO FEBRUARY 11,2018

UJENZI WA BARABARA YA KIDATU-IFAKARA KUKUZA UCHUMI WA MOROGORO

$
0
0
Serikali imesema imeanza ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 kwa kiwango cha lami ambapo kukamilika kwake kutachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya za mkoa wa Morogoro.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Reynolds Construction kutoka Nigeria anayejenga barabara hiyo kujenga kwa viwango na kukamilisha kwa wakati.

“Mradi huu umesuburiwa kwa siku nyingi na wananchi wa wilaya hii na mkoa kiujumla, mategemeo ya Serikali ni kuwa mradi huu utaukamilisha mapema mwezi Aprili, 2020 kwa kuzingatia vipengele vya mkataba na kwa viwango stahiki”, amesema Prof. Mbarawa.

Amesema kuwa ujenzi katika barabara hiyo unatarajiwa kuhusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili, madaraja madogo manne, makalvati makubwa na madogo 271 na unatarajiwa kudumu kwa miaka 20.

Aidha, Prof Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itahakikisha wananchi wa mkoa huo wanapewa kipaumbele kwenye ajira mara tu kazi itakapoanza ili kuongeza kipato chao.“Mradi umeanza na nimemuelekeza mkandarasi kuajiri afisa mwajiri ili kuhakikisha nafasi nyingi za ajira zinapatikana kwa wazawa kwani nafasi 70 walizoajiri mpaka sasa ni za mwanzo tu, ila nafasi nyingine zitaongezwa”, amefafanua Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo, ameipongeza Serikali kwa jitihada inazozifanya kuboresha miundombinu ya barabara hapa nchini na amemuahidi Waziri Prof. Mbarawa kuwa wananchi na uongozi wa usalama wa Wilaya yake watatoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo ili waweze kunufaika na mradi huo mapema.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, amesema kuwa kazi halisi itaanza mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu na watahakikisha wanamsimamia mkandarasi kwa karibu ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na viwango.

Ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara KM 66.9 kwa kiwango cha lami unatarajiwa kujengwa kwa miezi 30 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 111.4 na unafadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (European Union), Shirika la Misaada la Uingereza (UK aid) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Nicholas O’Dwyer, Frank Lynham, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu hatua ya maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 inayojengwa kwa kiwango cha kisasa cha lami, wakati alipotembelea kambi ya mkandarasi, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akikagua eneo la Ruaha lililopo katika Wilaya ya Kilombero ambapo ujenzi wa daraja kubwa lenye urefu wa mita 130 linatarajiwa kujengwa katika barabara ya Kidatu-Ifakara KM 66.9, mkoani Morogoro. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga.
Muonekano wa daraja la zamani katika eneo la Ruaha ambapo litajengwa daraja kubwa la Great Ruaha lenye urefu wa mita 130 katika barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa KM 66.9, mkoani Morogoro.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo, wakisalimia wananchi wa kijiji cha Sululu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kukagua kambi ya Mkandarasi anayejenga barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa KM 66.9, kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo (kulia), katika ziara yake ya kikazi wilayani humo, mkoani Morogoro.

ASYA IDAROUS KHAMSIN AACHIA JUKWAA KWA MOYO MMOJA

$
0
0
 Kila jambo hakika huwa halikosi mwisho msemo huu huwa na ukweli ndani yake ilikuwa kama ndoto kwa Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin kutangaza kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red, lakini ndoto hiyo imetimia kabisa bila kipingamizi mbele ya hadhara kubwa ya watu usiku wa 9 Feb 2018 ndani ya King Solomon Hall.

Lad in Red 2018 limekuwa ni Onyesho la Mwisho kwa  Designer mkongwe ambaye ndiye mwanzilishi wa Onyesho hilo Asya Idarous Khamsin. Kiukweli Jukwaa la mwisho la Lady in Red lilikuwa na mvuto, kwa taswira ya mbali inaonyesha kabisha ni jukwaa mabalo lilikuwa na ushirikiano mkubwa sana wa wadau na wanamitindo wengine toauti ilivyo zoeleka.

Mwisho ni pongenzi kwa Asya kwa kuamua kuwaachia jukwaa wanae yaani Designers walio lelewa na Lady in Red, maana angekuwa na roho  mbaya pengine Onyesho lingeishia mitini Hongera sana Asya.








Introducing "Nimekubali" (Official music video) by Davista

UNESCO CONDUCTS 7 DAY TRAINING WORKSHOP FOR MEDIA PERSONNEL

$
0
0
The UNESCO Dar es Salaam Office is conducting a 7-day training workshop for community radio practitioners on Editorial, Programming and Monitoring on Issues of Local Concern. The training which started on Tuesday February 06 has brought together 49 community media practitioners from 24 UNESCO supported community radios.The main objective of the training is to build capacity of community radio journalists and reporters on news formats. The move is meant to enable them report on issues of local concern through investigative journalism, sports news reporting and monitoring the quantity and quality of news bulletins.Participant contributing her points.[/caption] Participants to the training comprise of journalists and reporters as well as monitoring focal points previously trained on M&E by UNESCO.UNESCO has localized Gender Sensitive Indicators for Community Radios to emphasize on “sex disaggregated participation list for workshops”. To put this into practice, selection of participants from community radios will adhere to gender balance aspects.Mentorship in journalism for local public interest, in particular investigative journalism will come after the training where 72 journalists are expected to gain knowledge through peer learning.Feedback session.[/caption] UNESCO with the financial assistance from the Swiss Development Corporation (SDC) supports community radios and the Community Media Network (Tanzania Development Information Organization- TADIO).The support is meant to ensure that people in Tanzania, especially the poor, women and girls, have the capacity to make informed decision on issues that affect their daily lives.Above and below discussion groups of participants on news editing session.[/caption] Community radios in attendance under the SDC support with their regions in brackets are Nuru FM (Iringa), Pambazuko FM (Morogoro), Fadhila FM (Mtwara) Jamii Mtukwao FM (Mtwara), Loliondo FM (Arusha), Baloha FM (Shinyanga), Kahama FM (Shinyanga) Ileje FM (Songwe) and Tripple A FM (Arusha). In the list are Storm FM (Geita) and Sengerema FM (Mwanza), Kwizera FM (Kagera), Dodoma FM (Dodoma) and Kitulo FM (Njombe). Others are Uvinza (Kigoma), Mpanda (Katavi), Pangani (Tanga), Boma (Kilimanjaro), Mazingira (Mara), Mtegani FM (Unguja South,) Mkoani FM (Pemba South), Micheweni FM (Pemba North) Tumbatu FM (Unguja North), Ruangwa FM (Lindi) respectively.The training covers 77.4% of all regions in the United Republic of Tanzania.

MSHAMBULIAJI wa Simba John Bocco ndiye mchezaji bora wa LIGI KUU mwezi Januari

$
0
0
MSHAMBULIAJI wa Simba ya Dar es Salaam John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.
Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na Awesu Awesu wa Mwadui kutokana na uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana wiki hii kupitia ripoti za makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.
Alitoa mchango mkubwa kwa Simba mwezi huo ikipata pointi tisa katika michezo mitatu iliyocheza na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za usaidizi wa bao.

Pia kiwango cha mshambuliaji huyo aliyecheza dakika zote 270 za michezo mitatu ya Simba mwezi huo kilikuwa juu karibu kila mchezo.
Kwa upande wa Okwi aliyecheza dakika 206 kati ya 270 ilizocheza timu yake, alitoa mchango mkubwa kwa Simba kupata idadi hiyo ya pointi na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku akifunga mabao manne. Simba iliifunga Singida United mabao 4-0,ikaifunga Kagera Sugar mabao 2-0 na kisha ikailaza Majimaji mabao 4-0.
Awesu aliingia katika hatua hiyo kutokana na kung’ara katika michezo ambayo Mwadui ilicheza mwezi huo, akiibuka Mchezaji Bora katika mchezo wao dhidi ya Yanga, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam uliomalizika kwa timu hizo kutofungana, pia aliibuka mchezaji bora wa mchezo wo dhidi ya Njombe uliofanyika Uwanja wa Mwadui, Shinyanga na timu hizo kufungana mabao 2-2.
Mshambuliaji huyo aliyecheza kwa dakika 322 kati ya 360 ilizocheza Mwadui alifunga bao moja na kuisaidia timu yake kupata pointi sita katika mechi nne ilizocheza mwezi huo, ikitoka sare tatu na kushinda moja, ikiendelea kubaki nafasi ya kumi.
Kutokana na ushindi huo, Bocco atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Ligi, Kampuni ya Vodacom Tanzania.
Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba) na mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba).

Bamiza Music Chart 10th February 2018

Introducing "Mamalao" by ChindoMan Ft Rayvanny

RC MNYETI AWAFAGILIA MOFUGA NA KAMOGA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Hudson Kamoga kwa kutimiza wajibu wao ipasavyo wakati wanapowatumikia wananchi wa eneo hilo. 
RC Mnyeti akizungumza kwenye majumuisho ya ziara yake ya siku tano ya kutembelea halmashauri ya wilaya hiyo, alisema viongozi hao wanastahili pongezi kutokana na utendaji kazi bora wao kwa jamii. 
Alisema tangu akiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kabla ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa Mkoa wa Manyara, alikuwa anawasiliana na DC Mofuga kutokana na utendaji kazi bora anaoufanya. 
"Mheshimiwa mkuu wa wilaya kupitia nafasi hii nakupongeza kwa dhati kutokana na utendaji kazi wako, na nakutakia kila la heri ili siku moja upande cheo uwe mkuu wa mkoa," alisema Mnyeti. 
Alisema DC Mofuga ni kiongozi mwadilifu mwenye kuwatumikia wananchi wa Mbulu hivyo viongozi na wananchi wa wilaya hiyo wanapaswa kumpa ushirikiano wa kutosha.
“Ukiona kiongozi anabishana na mkuu wa wilaya basi huyo atakuwa na matatizo, wewe mkuu wa wilaya chapa kazi kwani hakuna mtu mwenye mapembe au sharubu kwenye wilaya hii ya Mbulu zaidi yako wewe Mofuga,” alisema Mnyeti.
Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga ni kiongozi mchapakazi anayetekeleza wajibu wake ipasavyo na miaka ijayo atapandishwa cheo na Rais John Magufuli.
“Mkurugenzi wewe chapa kazi, Rais ana vyombo vyake vingi vya uchunguzi atakuona tuu hata kama hayupo hapa kuna watu wake wanaandika andika na kufikisha taarifa ipo siku atakuona zaidi na kukupandisha cheo,” alisema Mnyeti.
Alisema Kamoga japokuwa ana muda mchache tangu ateuliwe na Rais Magufuli kushikilia nafasi hiyo ametimiza wajibu wake ipasavyo kwa kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao huku akisimamia vyema miradi ya maendeleo.
“Sina shaka na uadilifu wako kwani unafanya kazi kwa uadilifu umeanza vizuri wewe chapa kazi, mimi nilikuwa mkuu wa wilaya na leo ni mkuu wa mkoa kutokana na kufanya kazi hivyo fanya kazi utapanda cheo tuu,” alisema Mnyeti.
Alisema Kamoga ameanza kazi yake ya ukurugenzi wa halmashauri vizuri hivyo aendelee hivyo hivyo kwa kuwasimamia vyema wakuu wa idara ili kuhakikisha wananchi wananufaika kwa kuwatumikia.
Hata hivyo, aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza maelekezo na maagizo yote alioyatoa kwenye ziara hiyo kwa kadiri muda alioupanga ili kuhakikisha wananchi wanapata majawabu ya changamoto na matatizo waliotoa kwa kutimiziwa kwa wakati muafaka.
 Wakazi wa Kata ya Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wakiwa wamepanda juu ya mti wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti akizungumza nao.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akiwa amembeba mtoto wa jamii ya Hadzabe wa bonde la Yaeda Chini, alipotembelea eneo hilo kwenye ziara yake ya siku tano, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Celestino Mofuga.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexanda Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa bonde la Yaeda Chini kwenye ziara yake ya siku tano Wilayani Mbulu ya kuzungumza na wananchi, kukagua miradi na kuwasilikiza wananchi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akizungumza kwenye bonde la Yaeda Chini. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na msafara wake, wakikagua ujenzi wa kituo cha polisi Bonde la Yaeda Chini Wilayani Mbulu.

AZAM FC WATUA BUKOBA, TAYARI KWA MCHEZO WAO NA KAGERA SUGAR KESHO JUMATATU

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetua Mjini Bukoba asubuhi hii ikitokea Jijini Dar es salaam. Tayari kwa mchezo wao na Wenyeji wao Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba kesho jumatatu. Azam FC katika mchezo uliopita ilifungwa na Simba bao 1-0. Msimu uliopita Kagera Sugar ilifungwa na Azam Fc bao 3-2 kwenye Uwanja wa Kaitaba na msimu huo huo Kagera Sugar waliwafunga bao 1-0 Azam Fc na kuumaliza msimu huo wakiwa nafasi ya tatu. 
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2013/2014, wataendelea kuikosa huduma ya Nahodha Himid Mao ‘Ninja, aliyepewa mapumziko maalum kufuatia majeraha ya goti la mguu wa kulia yanayomsumbua, pamoja na mshambuliaji Wazir Junior na beki Daniel Amoah, ambao nao ni majeruhi. Aidha itamkosa nahodha wake msaidizi, Agrey Moris, aliyekusanya kadi tatu za njano, zinazomfanya kukosa mechi moja ijayo, lakini wachezaji wengine wote waliobakia wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo, ukiondoa majeruhi wa muda mrefu Joseph Kimwaga, ambaye anaendelea na programu ya mwisho (recovery) ya kurejea dimbani kwenye ushindani.
Mpaka sasa Azam FC imejikusanyia jumla ya pointi 33 kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa sawa na Singida United iliyonafasi ya nne, ikizidiwa pointi nane na Simba iliyojikusanyia pointi 41 kileleni huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointi zake 34.

Kocha wa Azam Fc Idd Nassor Cheche akiteta jambo na mwandishi wa habari(hayupo pichani) mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Kaitaba. Kocha huyo  amesema kilichowaleta ni pointi tatu hakuna kingine huku akiwamiminia sifa wenyeji wao kuwa ni timu nzuri na kwa sasa ipo kwenye sehemu mbaya hivyo mechi hiyo itakuwa  ngumu lakini watafanya jitihada na hatimae wazoe pointi zote tatu.

Mshambuliaji wa Timu ya Azam Fc Mbaraka Yusuph nae ameambatana na kikosi hicho. Mbaraka Yusuph alikuwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Kagera Sugar.
Wachezaji wa Azam Fc wakiteta Jambo na Kocha wao Idd Nassor Cheche mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba.


RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUA MKUTANO MKUU CHAMA CHA WALIMU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Walimu wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama cha Walimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar wakati wa ufunguzi huo
BAADHI ya Walimu wa Chama cha Walimu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano wa Sita uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa viongozi wa meza kuu wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa solidariti foreva wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama cha Walimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
KAIMU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pia ni Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kuufungua mkutano huo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha picha ya sura yake aliokabidhiwa zawadi na Chama cha Walimu Zanzibar wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Walimu Zanzibar baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni.
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live


Latest Images