Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MALIASILI, ARDHI,TAMISEMI KUAMUA HATMA MGOGORO PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA

0
0


Na Hamza Temba - Kondoa, Dodoma
.....................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7 februari, 2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo kusubiri uamuzi wa Serikali  utakaoshirikisha Wizara yake,  Wizara ya Ardhi na Tamisemi katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya ardhi katika pori hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu.

Dk. Kigwangalla ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alitembelea vijiji vinne vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujiridhisha na  kujifunza juu ya mgogoro uliopo baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero.

"Nimefika hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi lakini pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba niende nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na mwisho wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na changamoto ambazo zimekuwepo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuwa akimunesha mpaka wa kijiji hicho na Pori la Akiba Mkungunero wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteja jambo na Meneja wa Pori la Akiba Mkungunero, Emannuel Bilaso wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea mabango ya malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisondoko kuhusu Pori la Akiba Mkungunero na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MBARAWA AMKABIDHI NAIBU SPIKA MWONGOZO WA WATUMIAJI HUDUMA NA BIDHAA ZA MAWASILIANO

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia) Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa niaba ya Wabunge. Wakishuhudia watatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akionesha Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Wabunge. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akimweleza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia) umuhimu wa Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa Wabunge mara baada ya kumkabidhi Mwongozo huo kwa niaba ya Wabunge ili waweze kusoma, kuelewa na kuelimisha wananchi namna ya kutumia vema huduma na bidhaa za mawasiliano nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia) kuhusu Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Wabunge. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma

WAZIRI MHAGAMA AKITETA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Bungeni mjini Dodoma Februari 8, 2018.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MSTAHIKI MEYA SELEBOSI AONGOZA KIKAO BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA

0
0

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga(CCM) Alhaji Mustapha Mhina Selebosi akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani leo kwenye ukumbi wa Halmashauri kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Naibu Meya wa Jiji hilo,Mohamed Haniu
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudio Mayeji akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo,Alhaji Mustapa Mhina Selebosi anayefuata ni Naibu Meya Mohamed Haniu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja
Naibu Meya Mohamed Haniu akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi
Waheshimiwa madiwani wa Jiji la Tanga wakifanya dua kabla ya kuanza kikao hicho
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi katika akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia na Naibu Mstahiki Meya Mohamed Haniu wakipitia taarifa mbalimbali wakati wa kikao hicho leo 

JAFO ASHUSHA NEEMA YA LAMI CHANG’OMBE, AMFAGILIA MAVUNDE KWA UCHAPAKAZI WAKE

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo, amemfagilia Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo kwa wananchi wake, huku akiuagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha katika bajeti yao ya mwaka 2018/19 wanaingiza kwenye mpango ujenzi wa barabara ya lami Chang’ombe hadi Chuo cha Mipango.

Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa anazindua soko jipya la kisasa kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo kata Chang’ombe lililojengwa na Serikali kwa kusaidiana na wafanyabiashara na Mbunge Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana.

Ujenzi wa soko hilo ulianza mwaka 2017 na kukamilika mapema mwaka huu na litakuwa na wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali takribani 342 na limegharimu kiasi cha Sh.Milioni 70.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Jafo amesema katika ziara zake za miradi ya maendeleo alizotembelea katika Manispaa ya Dodoma, Mbunge Mavunde ameonekana kushiriki katika kila sekta kwa kusaidiana na wananchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge akizungumza katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.

DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE

0
0
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI

SERIKALI wilayani Kibaha,Mkoa wa Pwani imemtaka mwekezaji ambaye alichukua eneo lenye ukubwa wa hekari zipatazo 5000 za ardhi bila ya kuzingatia sheria na taratibu kuzirudisha kwa kipindi cha siku tisini kutokana na kushindwa kuliendeleza kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane kama walivyokubaliana katiba mkataba na wananchi wa kijiji cha lukenge kata ya Magindu.

Sakata la mgogoro wa ardhi baina ya wananchi hao na mwekeaji limechukua sura mpya kufuatai Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hivyo kumtaka mwekezaji huyo kuzirudisha hekari hizo 5000 kwa wananchi ambazo alikuwa amepewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya uwekezaji wa ufugaji wa kisasa wa ng’ombe pamoja na samaki lakini ameshindwa kutekeleza makubaliano aliyopatiwa hapo awali.

Akizungumza katika mkutano maalumu wa adhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kujadili sakata hilo Mkuu huyo wa Wilaya amesema eneo hilo mwekezaji huyo alipewa kwa ajili ya kuliendeleza lakini amekuwa akijinufaisha mwenywe na kuwanyonya wakazi wa eneo hilo bila ya kuwaletea maendeleo ya aina yoyote tofauti na makubaliano yao.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na umati wa wananchi wa kijiji cha Lukenge kata Magindu hawapo pichani katika mkutano wa adhara ambao aliuandaa kwa ajili ya kuweza kutatua mgogoro wa aradhi kati ya wananachi hao na mwekezaji ambao umedumu kwa kipindi kirefu
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akiwa anatoka kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha lukenge alipokwenda kwa ajili ya kumaliza sakata la mgogoro baina ya wananachi hao pamoja na mwekezaji.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha lukenge wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wakati wa mkutano wa adhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kusikiliza mgogoro uliopo katia ya wananchi na mwekezaji.
Wananchi wa kijiji cha lukenge wakiwa wameshika mabango yaliyokuwa yameandikwa ujumbe wa kumkataa mwekezaji huyo, ambapo walipita mbele kwa ajili ya kuweza kumuonyesha Mkuu wa Wilaaya ya Kibaha.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU


RC MNYETI AENDESHA HARAMBEE NA KUPATIKANA SHILINGI MILIONI 17 UJENZI WA MAABARA

0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti ameendesha harambee iliyopatikana sh17. 5 milioni ya umaliziaji wa jengo la maabara ya shule ya sekondari Bishop Hando ya Wilayani Mbulu.

Pia, Mnyeti amewapa zawadi ya sh1 milioni walimu wa shule hiyo na wanafunzi wakapewa magunia 100 ya mahindi ya chakula kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017.Aliendesha zoezi hilo kwenye ziara yake ya siku saba ya kutembelea halmashauri ya wilaya ya Mbulu ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero na kuzungumza na wananchi.

Mnyeti akizungumza kwenye shule hiyo amemuagiza mkuu wa wilaya hiyo Chelestino Mofuga kuhakikisha maabara hiyo inakamilika ndani ya muda wa miezi mitatu.“Hata mimi niliwahi kuwa mkuu wa shule ya sekondari, natambua gharama za ujenzi zilivyo, hapa panahitajika sh40 milioni, sisi tumechangia sh17. 5 milioni sasa pambaneni mlimalize jengo hili,” alisema Mnyeti.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Bishop Hando iliyoshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana Wilayani Mbulu, ambapo aliwapa zawadi ya shilingi milioni moja walimu wa shule hiyo na wanafunzi aliwapa chakula, magunia 100 ya mahindi baada ya kushika nafasi hiyo.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bishop Hando ya Kata ya Masqaroda Wilayani Mbulu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alipotembelea shule hiyo ambapo aliendesha harambee ya umaliziaji wa ujenzi wa jengo maabara na kupatikana shilingi milioni 17.5.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akimsikiliza mwalimu wa shule ya sekondari Bishop Hando, ya Wilayani Mbulu Samuel Surumbu alipotembelea shule hiyo na kufanya harambee ya umaliziaji wa ujenzi wa jengo la maabara na kupatikana shilingi milioni 17.5 Wanafunzi wa shule ya sekondari
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bishop Hando na wananchi wa Kata ya Masqaroda Wilayani Mbulu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alipotembelea shule hiyo kwenye ziara yake ya siku saba ya kutembelea wilaya ya Mbulu, ambapo anakagua miradi ya maendeleo, kuwasikiliza wananchi na kuzungumza nao.

SERA ZA MAGUFULI ZITAIBADILISHA KINONDON-MTULIA

0
0
--
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi Maulidi Mtulia akizungumza kuomba kura katika Mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera Livingstone  Lusinde akizungumza kumnadi mgombea mara baada ya kupokea wafuasi wawili kutoka CHADEMA ambao kwa hiari yao wenyewe wameamua kujiunga na CCM.
 Kampeni Meneja wa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi katika Kinyang'anyiro cha Ubunge Kinondoni, Iddi Azzan akizungumza wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa Chama chake Maulid Mtulia.
 Wabunge wa Chama Cha Mapindzui wa Mkoa wa Dar es Salaam  wakifatilia mkutano wa Kampeni
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi Maulidi Mtulia akizungumza kuomba kura katika Mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wananchi wakifatilia mkutanowa Chama Cha Mapinduzi katika kata ya Makumbusho 

MATUKIO KATIKA PICHA WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIZUNGUMZA NA WABUNGE MJINI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 8, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 8, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Februari 8, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 8, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Murad Sadiq wa Mvomero (kulia), Suleiman Nchambi wa Kishapu (katikati) na Richard Ndassa wa Sumve kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 8, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuulia panya wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya.

Amesema kuwa ameisikia changamoto hiyo ya uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya kutoka kwa vijana mbalimbali wanaojishughulisha na mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya changamoto za kuendeleza misitu.

“DC tafuta dawa ya panya, wauliwe huko mashambani, ili panya wasiwepo na miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa panya tutawaua kwa sumu huko mashambani wasiwe chanzo cha mioto ambayo mnachoma huko kuwatafuta hawa panya ili wafie huko huko mashimoni msiwapate,” Alisisitiza.

Agizo hilo amelitoa katika muendelezo wa kampeni ya upandaji miti mijini na vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, kata ya Mpwapwa, Wilayani Sumbwanga baada ya kuwauliza wananchi wa Kijiji hicho juu ya changamoto aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya, japo wananchi walikataa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipanda mti katika shule ya msingi Mpwapwa, kata ya Mpwapwa Wilayani Sumbawanga ikiwa ni kampeni ya kufikisha miti Milioni 6 kwa Mkoa kwa mwaka 2017/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule akisaidiana na mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Mpwapwa Joanita Mwanandenje kupanda mti ili kuwahamasisha wanafunzi kuwa na utamaduni wa kupanda miti na kufikisha miti milioni 3 kwa Wilaya ya Sumbawanga.
Mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP George Kyando akijiandaa kuapanda mti katika Shule ya Msingi Mpwapwa ikiwa ni kampeni ya Mkoa kufikisha miti milioni 6 na kuhifadhi mazingira ya Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi miche kwa Didas Kosam M/kiti wa kitongoji cha Katupa, Kijiji cha Mpwapwa chenye vitongoji vinne. Ambapo kila kitongoji kilipewa miche 200.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

ACACIA YAKABIDHI HUNDI BILIONI 1.1 ZA USHURU WA HUDUMA KAHAMA MJI NA MSALALA

0
0
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu Acacia kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imekabidhi hundi za shilingi bilioni 1.1 kwa halmashauri ya wilaya ya Mji wa Kahama na Msalala mkoani Shinyanga kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2017. 

Acacia imekabidhi hundi ya shilingi milioni 924,881,819.78 kwa halmashauri ya wilaya ya Mji wa Kahama zilizotolewa na mgodi wa Buzwagi na hundi ya shilingi milioni 153,591,456 kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu na kufanya jumla kuwa shilingi bilioni 1.1. 

Meneja Mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Benedict Busunzu amekabidhi hundi hizo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurulu leo Alhamis Februari 8,2018 mjini Kahama. 
Katikati ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akikabidhi hundi ya shilingi153,591,456 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2017. Kulia ni Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akikabidhi hundi hiyo ya shilingi milioni 153 kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Simon Berege 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkuru,Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu,Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Simon Berege wakiwa wameshikilia hundi ya shilingi milioni 153. 

Dkt MWINUKA atembelea Kituo cha Kupoza,Kusambaza Umeme, Shinyanga

0
0
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, ametembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli, kilichopo Mkoani Shinyanga.
Katika ziara hiyo, Dkt. Mwinuka amejionea shughuli mbalimbali zinazofanyika kituoni hapo. 

Kituo hicho ni mojawapo ya vituo vilivyofanyiwa upanuzi wakati wa utekelezaji wa Mradi wa njia ya Kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 (Backbone) kutoka Mkoani Iringa hadi Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, akisaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Wageni Wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli, kilichopo Mkoani Shinyanga.
Muonekano wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli, kilichopo Mkoani Shinyanga.

WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii irudi kwenye maeneo yote yenye migogoro ya mipaka na iungane na Halmashauri za wilaya ili waweze kutoa majibu kwa wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 8, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Urambo, Bibi Margaret Sitta wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.

Bibi Sitta alitaka kujua Serikali imeweka taratibu na mikakati gani ya kumaliza migogoro ya mipaka inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya hifadhi za misitu nchini kwa kuwa wananchi wanahitaji maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo.

Waziri Mkuu amesema Serikali iliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iweke vigingi kwenye maeneo yote yanayozunguka hifadhi za misitu ili kuweka alama zitakazopunguza migogoro ya kuingiliana kati ya wananchi walioko kwenye vijiji na wahifadhi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu hiyo.

Amesema maagizo hayo yalitolewa baada ya kugundua kuwa kuna migogoro mingi kati ya wananchi walioko katika vijiji vya jirani na misitu iliyohifadhiwa kisheria ambayo ina ramani.

“Lakini tunatambua kwamba wanapoendelea na zoezi hilo la uwekaji alama, inaweza kutokea kijiji kikajikuta kipo ndani ya mipaka ya hifadhi na inaweza kusababisha kutoelewana kati ya wanakijiji na wenye mamlaka ya hifadhi.”

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DYNIA

UNICEF YATOA MSAADA WA LAPTOP 200 KWA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR

0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa msaada wa Komputa aina ya Laptop 200 kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo.

Laptop hizo zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 400 zimetolewa ikiwa ni mwendelezo wa UNICEF kuiunga mkono Serikali katika kuimarisha huduma za matibabu hasa ya akinamama na watoto.Akikabidhi Msaada huo katika Ukumbi wa Wizara hiyo Mnazi mmoja Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin amesema upatikanaji wa taarifa sahihi ni jambo muhimu linalofaa kupewa kipaumbele.

Amesema uwepo wa taarifa sahihi za Wajawazito na watoto huisaidia Serikali kujua idadi ya ongezeko la watu wake hali inayopelekea kupanga mipango vyema ya matibabu kulingana na idadi ya watu husika.Amewataka Watendaji kwa ujumla kuunga mkono juhudi zinazotolewa na UNECO ili kuhakikisha afya za Watoto na Wajawazito zinaimarika.

Francesca ameongeza kuwa Shirika hilo la UNICEF litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za kimatibu na kuipongeza Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kutoa matibabu bure kwa wananchi wake.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo kushoto na akikabidhiwa Msaada wa Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kwa Wizara ya Afya Zanzibar ili zisaidie kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.

KANGI LUGOLA ASIKITISHWA NA UTENDAJI WA DUWASA

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola hii leo amefanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) ikiwa ni pamoja na kutembelea miundombinu ya Mamlamka hiyo.

Waziri Lugola amesikitishwa na namna Mamlaka hiyo ilivyoshindwa kuhimili kiasi cha maji taka yanayozalishwa katika Mji huo wa Dodoma na kutitiririka katika makazi ya watu bila kutibiwa (Treated).

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Kangi Lugola ameitaka Mamlaka hiyo kuja na mpango wa haraka wa kudhibiti maji hayo kwa lengo la kudhibiti usafi wa Mazingira na Ustawi wa Wananchi. “DUWASA mmekuwa mkitiririsha maji taka bila kuyatibu kwenye makazi ya watu, na kwenye kilimo cha mpunga, na mmepelekea baadhi ya watu kuyahama makazi yao.” Lugola alisisitiza.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akielekeza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) David Palangyo wakati wa ziara ya kutembelea mabwawa ya kuhifadhi maji taka yanayotumiwa na DUWASA katika eneo la Swaswa mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akiwa pamoja na Ujumbe toka DUWASA akikagua mabwawa ya kuhifadhi maji taka katika eneo la Swaswa na Ilazo mjini Dodoma ambapo alifanya ziara.
Sehemu ya mabwawa ya kuhifadhia maji taka inayotumiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) katika eneno la Swaswa.

KISHAPU KUWAHAMISHIA WALIMU WA SEKONDARI KUFUNDISHA SHULE ZA MSINGI KUONGEZA UFANISI

0
0

Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ipo katika mchakato wa kuwahamishia walimu wa ziada wa masomo ya sanaa wa shule za sekondari kwenda kufundisha shule za msingi zenye upungufu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Stephen Magoiga wakati akizungumza katika kikao kikao kilichowakutanisha wadau wa elimu wilayani Kishapu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya elimu ya msingi na sekondari ili kuboresha viwango vya ufaulu.

Alisema mchakato huo unafanyika kutokana na maelekezo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuboresha ikama ya walimu baada ya kubaini upungufu au ziada kwa kila shule.Kwa mujibu wa takwimu kutokana na uhakiki kuna ziada ya walimu wa masomo ya sanaa kwenye shule za sekondari na upungufu wa walimu wa sayansi na hisabati katika shule za msingi.

Kutokana na changamoto hiyo kwa kuanzia Kishapu itaanza kuwahamisha walimu wa ziada sekondari na kwenda kufundisha shule za msingi zilizo karibu na kuwa uhamisho huo hautaathiri mishahara na stahiki nyingine za walimu.Akifafanua zaidi Magoiga alisema kuwa hilo ni zoezi la kawaida na kuwa walimu wengi katika shule za sekondari wana vipindi vichache kulinganisha na wale wa msingi na hivyo litasaidia kuleta ufanisi bila kuathiri utendaji.

“Mwalimu wa sekondari nikikuhamishia shule ya msingi kufundisha usijisikie vibaya na kujiona kama nimekushusha bali nimekuongezea majukumu mengine kwa mamlaka niliyo nayo, na ntapita nihakikishe unakuwepo kituo nilichokupangia kufundisha,” alisisitiza.Aidha alihimiza ushirikiano baina ya wadau wote wa elimu ili kuwepo na maandalizi mazuri kwa wanafunzi wafanye vizuri katika masomo yao huku akisema wazazi wanapaswa kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao.

Wakichangia kwa nyakati tofauti baadhi ya madiwani akiwemo Mh. Lucas Nkende wa kata ya Mwamashele alisema mahudhurio hafifu ya wanafunzi ndi changamoto zinazoporomosha kiwango cha ufaulu.Alishauri pawepo na mfumo mzuri wa kusimamia wanafunzi huku akisisitiza mamlaka iangalie walimu wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi wa madarasa ya chini ambapo ndio msingi wa elimu.

Kikao hicho kimehusisha waheshimiwa madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, maofisa elimu msingi na sekondari kutoka makao makuu na kata, wakuu wa shule za msingi na sekondari, wanafunzi na wadau kutoka Programu ya Kuinua Ubora wa Elimu (Equip).

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza katika kikao cha kijadili namna ya kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla. Wengine pichani kushoto ni Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Paul Kasanda na mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mwaweja, Makanasa Kishiwa.
Washiriki mbalimbali wakiwemo maafisa elimu kata, walimu wakuu shule za msingi na sekondari na baadhi ya wanafunzi wakiendelea kufuatilia kikao hicho.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mwaweja, Makanasa Kishiwa akizungumza. Kushoto ni Afisa Elimu Sekondari, Paul Kasanda
Afisa Elimu Msingi, Sostenes Mbwilo akisisitiza jambo kwa washiriki wa kikao hicho (hawapo pichani).

Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paul Sheka akichangia katika kikao cha wadau wa elimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha sekta ya elimu wilayani humo.
Washiriki wakiendelea kufuatilia kikao hicho.

WANANCHI KONDOA WAIOMBA SERIKALI IWAREJESHEE SEHEMU YA ARDHI YAO PORI LA AKIBA MKUNGUNERO

0
0
Wakazi waishio jirani na Pori la Akiba la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, wameiomba Serikali iwarejeshee eneo la kilometa 12 kuanzia kwenye vijiji vyao kwenda ndani ya Pori hilo ambalo wanadai limechukuliwa kinyemela na Wizara ya Maliasili na Utalii na kuathiri maisha yao yanayotegemea kwa kiasi kikubwa kilimo na ufugaji.

Wakazi wa vijiji vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko, wametoa maombi hayo mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipofanyaziara katika vijiji hivyo vinavyozunguka Pori hilo la Akiba ili kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya Pori hilo na wananchi wanaolizunguka.

Wananchi na viongozi wa vijiji hivyo wameeleza kuwa uwekaji wa mipaka ya Pori hilo haukuwa shirikishi na kwamba maeneo makubwa ya vijiji yaliyokuwa yakitumiwa na wananchi kwa shughuli zao za kilimo, ufugaji na makazi yametwaliwa na kusababisha mgogoro huo.

Malalamiko mengine ya wananchi hao ni kunyanyaswa na watumishi wa Pori la Akiba Mkungunero kwa kupigwa, kunyang'anywa mifugo yao, na baadhi yao kudai kuumizwa na baadhi ya wenzao kuuawa kwa risasi na askari wanaolinda Pori hilo.

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji, ameiomba Serikali kutumia busara na kurejesha eneo lililochukuliwa kimakosa kutoka kwa wananchi ili waweze kujiendeleza kiuchumi na kuishi kwa amani na utulivu.

"Najua wewe ni mwadilifu ndio maana umeaminiwa na Mhe. Rais, najua utawatendea haki wananchi wa vijiji hivi ili nao wajione ni wananchi halali katika Taifa lao huru la Tanzania tukienda hatua kwa hatua bila kuvunja sheria za nchi" alisisitiza Dkt. Kijaji

Amefafanua kuwa maeneo yaliyochukuliwa na Pori hilo yalikuwa yakitumiwa na wananchi kwa muda mrefu na kwamba mchakato wa kupandisha hadhi eneo hilo kutoka Pori Tengefu hadi kuwa Pori la Akiba la Mkungunero haukuwashirikisha wananchi.
 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikengwa, Nade Laida, akibubujikwa machozi wakati wa mkutano kati ya wanakijiji na msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mwanamke huyo ni mmoja wa waathirika wa mgogoro baina ya Pori la Akiba Mkungunero na wananchi wa vijiji vinavyozunguka pori hilo.
 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Keikei Tangini ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiwa ameshikilia bango linaloeleza kuwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero imesogezwa kwenye kijiji chao.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati)  akizungunza wakati wa mkutano ulioitishwa na Waziri wa Maliaasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala katika kijiji cha Keikei Tangini ili kusikiliza malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Pori la akiba Mkungunero kuhusu kumegwa kwa maeneno yao na Pori hilo, wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali Haitaivunja Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Kwa Kuwa Bado Inahitajika

0
0
Serikali imesema iko tayari kupokea ushauri wa namna bora ya kuimarisha utendaji wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza Taasisi hiyo kwani bado inahitajika na madhumuni ya kuanzishwa kwake yana tija kwa Taifa.

Akizungumza wakati akijibu Hoja za Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Waziri wa Elimu Sayansi na Teknplojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika hivyo Serikali inaangalia namna ya kuiboresha na si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

“ Taasisi ya Elimu ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wale waliokosa katika mfumo rasmi na pia kutoa mafunzo endelevu hivyo bado kuna umuhimu wa kuendeleza Taasisi hii” Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Akifafanua Prof. Ndalichako amesema kuwa Taasisi hiyo inaweza kuimarishwa zaidi ili kuendana na mahitaji ya sasa ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha na kukuza kiwango cha elimu nchini.

Akizungumzia mikakati yakuimarisha elimu nchini Profesa Ndalichako amesema kuwa kwa sasa Serikali inafanya ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini, vyuo vya Ualimu, na Ujenzi wa maktaba yakisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja hiyo ikiwa ni sehemu ya miradi yakuboresha elimu inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yalipendekeza kuwa TEWW ivunjwe ambapo Serikali imesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika na ina tija hivyo kitakachofanyika ni kuiboresha zaidi ili kukuza elimu hapa nchini na Si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

Taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 139 ya mwaka 1989 na iko chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknoloji.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akionesha kwa wabunge baadhi ya Vitabu vyenye ubora unaotakiwa kwa matumizi ya wanafunzi ikiwa ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha elimu nchini ambapo pia alibainisha kuwa Serikali haitaivunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima badala yake inaangalia namna bora yakuimarisha Taasisi hiyo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa wabunge wakati akijibu hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni Mjini Dodoma.

SERIKALI YA UINGEREZA : MSHIRIKA KATIKA PROGRAMU ZA MABADILIKO KATIKA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao ofisini kwake Dodoma na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.


Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke (kulia), pamoja na ujumbe wake, wakiwa katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) haonekani pichani, mjini Dodoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akijadli masuala ya utumishi na utawala bora pamoja Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, Dodoma.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live


Latest Images