Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

RAIS MTEULE WA ROTARY INTERNATIONAL AWASILI NCHINI TANZANIA

0
0

RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin amewasili nchini Tanzania jana na kulakiwa na wenyeji wake District Governor, Bwana Kenneth Mugisha, District Governor Mteule, Sharmila Bhatt pamoja na viongozi mbalimbali wa baada ya kuwasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. 

Rais huyo aliyetumikia Rotary Club kwa Takribani Miaka 37 amewasili na kujionea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na Taasisi hiyo hapa nchini hususani kwa jiji la Dar es Salaam, ambapo atakutana na vijana wadogo wa Club hiyo' Rotaractors' na kubadilishana nao mawazo kuwahamasisha kujitolea na kufanya shuguli mbalimbali za kijamii ili kuleta maendeleo chanya kwa umma.

Rotary Club ina takribani matawi 38 ambapo nane kati ya hayo yapo Dar es Salaam. Rais Rassin anatokea Rotary Club ya Mashariki Nassau, Jimbo jipya la Nchini Bahamasi ambapo ni msomi wa taalum ya maswala ya afya na Utawala wa Tiba kutoka Chuo kikuu cha Florida Nchini Marekani. 
RAIS Mtarajiwa wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) na mkewe Esther (kulia) wakilakiwa na District Governor aliyemaliza muda wake, Bwana Kenneth Mugisha, District Governor Mtarajiwa, Sharmila Bhatt pamoja na viongozi mbalimbali wa baada ya kuwasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211. (Picha na Robert Okanda Blogs)
District Governor Mteule, Sharmila Bhatt akimpa muhtasari Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kulia) alipowasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Pamoja nao ni District Governor, Bwana Kenneth Mugisha. 
Baadhi ya viongozi wa Rotary Club wakiwa Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, wakati wa kumpokea Rais Mteule wa Rotary International Bary Rassin kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. 
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kulia) akikaribishwa Past District Governor Jayesh Asher alipowasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. 
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa sita kulia) na mkewe Esther (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na District Governor aliyemaliza muda wake, Bwana Kenneth Mugisha (wa nne kushoto), District Governor Mtarajiwa, Sharmila Bhatt (wa tano kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wa baada ya kuwasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. 

EKARI 130,000 ZA MITI KUTUNZA NA KUPANDWA NA WAKAZI WA UYUI

0
0

NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tabora imeagiza kila kaya katika eneo hilo kuhakikisha inapanda miti ekari moja na kutunza miti asili ekari moja ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha zoezi la uhifadhi wa mazingira na upandaji wa miti linakuwa endelevu.

Kauli hiyo ilitolewa jana katika Kijiji cha Mbuyuni Kata na Kigwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahoondi wakati aliposhiriki zoezi la wiki ya upandaji miti kwa upande wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali(NGO,s) mkoani Tabora.

Alisema kuwa kwa kutumia idadi ya kaya 65,000 zilizopo katika Halmashauri hiyo watapanda jumla ya ekari 130,000 za miti asili na ile ya kupanda.Ntahondi alisema lengo ni kuzifanya kila kaya kuwa kuwa na mistu yao kwa ajili ya kuwajengea utamaduni wa uhifadhi wa mazingira na upandaji wa miti endelevu kwa ajili yao na nchi kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora aliongeza kuwa mpango mwingine wanaoendelea nao ni pamoja na kuhakikisha kuwa kila kaya inapanda miti mitano ya matunda tofauti katika eneo la nyumba yao.

Alisema kuwa hatua itawawezesha kupanda miti ya matunda 325,000 katika kaya zote 65,000 zilizopo katika Halmashauri hiyo.Ntahondi alisema kuwa miche hiyo ya matunda ni nje ya ile iliyopandwa kwa mujibu wa makubaliano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuwa wanapanda matunda mahuleni, hospitalini, Maofisini na barabarani.

Alisema lengo ni kutaka kuwa na matunda mengi kwa ajili ya matumizi ya familia na ya ziada kwa ajili ya uuzaji.

Dkt. Shein Afungua Jengo Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja,kushoto Waziri Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Makungu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

BAADHI ya Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja wakati wa uzinduzi wake
BAADHI ya Majaji na Mahakimu wa Mahakama za Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa jengo hilo

Dkt. Marry Nagu: ununuzi wa mbolea kwa pamoja mkombozi kwa mkulima

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja(Fertilizer Bulk Procurement) umesaidia kuwawezesha wakulima wadogo kupata mbolea yenye ubora na kwa bei nafuu kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dkt. Mary Nagu wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Kamati hiyo kwa kipindi cha Januari, 2017 hadi Januari, 2018.

Dkt. Nagu amesema kuwa Sera ya Kilimo ya mwaka 2013 inaeleza umuhimu wa kuongeza matumizi ya pembejeo za kisasa kama mbolea, madawa ya kilimo, mbegu bora na zana za kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji mazao, kupunguza umaskini na kuwa na usalama wa chakula na lishe.

“Aidha, Kamati ilieleza kuridhika na faida zinazotarajiwa kupatikana kutokana na mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja ikiwamo udhibiti wa bei ya mbolea kwenye soko holela” amefafanua Dkt. Nagu.

Aidha, Dkt. Nagu ametaja faida nyingine ya mfumo huo ikiwemo nchi kunufaika kwa ununuzi wa pamoja kwa lengo la kupata punguzo kutokana na kiasi kingi kinachonunuliwa na kupunguza gharama za uendeshaji.

“Pia mfumo utaongeza ufanisi kwa kudhibiti mbolea kutoka nje kwa kuagiza mara chache kwa kiwango kikubwa, tofauti na hali ilivyo sasa ambapo mbolea imekuwa ikiingizwa mara nyingi kwa kiwango kidogokidogo pamoja na kuongeza na kuhamasisha matumizi ya mbolea nchini”ameongeza Dkt. Nagu.

Mbali na hayo Dkt. Nagu amesema kuwa kamati imepokea taarifa ya Hali ya Chakula nchini ambapo kwa msimu wa mwaka 2016/2017 hali ya chakula imeendelea kuimarika kulingana na mavuno mazuri nay a ziada yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016.

TANZANIA:UNAWEZAJE KUPATA PASPOTI MPYA YA KUSAFIRIA YA KIELEKTRONIKI? FUATILIA VIDEO HII.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO MAALUM YA KIJESHI MAPINGA MKOANI PWANI

0
0
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa Pili kushoto anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na wa kwanza kushoto anayepiga makofi ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya ufunguzi wa kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.

HABARI ZAIDI BOFYA 

KUMBUKUMBU YA MAMA OMWANA THERESIA NYAMICHWO RUTAGERUKA

0
0

TAREHE 6 – FEBRUARI 2018, UMETIMIZA MIAKA 24 TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.
TUNAADHIMISHA KUMBUKUMBU HII TUKIOMBA MWENYEZI MUNGU AWAKUTANISHE KWENYE RAHA YA MILELE NA MUME WAKO MPENDWA MWALIMU NOVATI RUTAGERUKA AMBAYE SIKU ZOTE ALIKUKUMBUKA KATIKA SALA ZAKE KABLA YA KUTWALIWA NA BWANA TAREHE 5 MEI 2010.
MNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WENU FROLIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU ITAADHIMISHWA JUMANNE TAREHE 6 - FEBRUARI - 2018 KATIKA KANISA LA MTAKATIFU MAURUS, KURASINI, DAR-ES-SALAAM SAA 12.30 ASUBUHI.
BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali akutana na Katibu wa Bunge mjini Dodoma

0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.Adelardus Kilangi leo  Jumanne amemtembelea  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Stephen Kigaigai ofisini kwake mjini Dodoma kwa ajili ya  kujitambulisha.  Katika  mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamesisitiza haja na umuhimu wa   Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  na Bunge kuendelea  kushirikiana ipasavyo na kufanya  kazi kwa karibu. 
Picha kwa hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

KAULI YA YANGA KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA SC DHIDI YA AZAM FC

AZAM TV: YANGA 4-0 NJOMBE MJI (MAGOLI YOTE, CHIRWA AKIPIGA HAT-TRICK) - VPL 06/02/2018

VOA Swahili: Duniani Leo 6th February 2018

NI KWELI WA CHEZAJI WA MAJI MAJI WANAGOMBANIA CHAKULA ?

0
0
Fahamu mambo makuu matatu kuhusiana na Club ya Maji Maji inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara 2017-2018 katika mahojiano maalum yaliyofanywa na Ruvuma Tv on line na Msemaji wa club hiyo Onesimo Emeran .

Introducing Kingman 107 track

MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI

0
0
Na Wankyo Gati, Arusha
UHABA wa fedha na watumishi katika uendeshaji wa shughuli za Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ), unachangia kukwamisha baadhi ya mashauri mahakamani hapo.
Akielezea changamoto zinazoikabili mahakama hiyo jana mjini hapa ofisini kwake Rais wa EACJ Jaji Dk. Emmanuel Ugerashebuja alizitaja changamoto mbili kubwa kuwa ni fedha pamoja na watumishi.
“Mambo haya ni kizungumkuti kinachotukabili hapa, upatikanaji kwa wakati fedha za kutusaidia kuendesha shughuli za mahakama kwa wakati imekuwa changamoto,” alisema Dk. Ugerashebuja na kuongeza: 
“Jambo hili linatufanya kushindwa kufikia malengo kama EACJ tuliyopangiwa kwenye mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya yenyewe lakini pia Mahakama hii,” alisema
Dk. Ugerashebuja aliendelea kufafanua changamoto nyngine kuwa ni uhaba wa wafanyakazi wanaowasaidia Majaji mahakamani hapo kutekeleza shughuli za kila siku za Kimahakama.
“Kwa kweli tunaona jinsi ambavyo nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliosaida kuanzisha mahakama hii wanavyojaribu kutafuta dawa ya changamoto hizi zinazototkabili,” alisema Dk. Ugerashebuja.
Alisema uhitaji huo wa wafanyakazi kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na mahakama hiyo kuwa na kesi 282 ikilinganishwa na kesi moja iliyofunguliwa mwaka 2001 walipokuwa wakiapishwa majaji wa kwanza.
“Kwa sasa tuna kesi nyingi sana ukiangalia histroria yetu nyuma tuliwahi kuwa na kesi moja baada ya miaka minne tangu kuanzishwa,” alisema Dk. Ugerashebuja.
Aidha Rais huyo wa EACJ aliyataja mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo kuwa ni pamoja na kufunguliwa kwa ofisi za Msajili katika kila nchi mwanachama.
Kwa upande wake Msajili wa Mahakama Yufnalis Okubo alisema kwa sasa mahakama hiyo ina wafanyakazi 28 huku uhitaji ukiwa ni wafanyakazi 10 wenye taaluma mbalimbali.
“Kwa sasa mahakama hii imeendelea kupokea kesi nyingi tukifanikiwa kuongeza wafanyakazi 10 tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kutekeleza yale tuliyopangiwa.
“Hapa kuna kesi nyingine zimefunguliwa zihusisha Taasisi mbili za Serikali zilizoshitakiana na wamekuja kwenye mahakama hii,” alisema Msajili Okubo na kuongeza:
“Hawakuchangua kwenda kwenye mahakama zilizopo kwenye nchi zao wamekuja hapa, kwanini wanaamini watapata uamuzi sahihi kwenye mashauri waliyoshitakiana,” alisema.
Mwisho.
Kushoto ni Rais wa eacj jaji dr Emmanuel Ugerashebuja na kulia ni Msajili wa Mahakama hiyo Yufnalis Okubo

Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Sarah Msafiri afunga Mafunzo ya Mgambo katika tarafa ya Bassotu

0
0
 Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Sarah Msafiri  akikagua gwaride wakati alipofunga Mafunzo ya Mgambo katika tarafa ya Bassotu wilayani humo mwishoni mwa wiki. (Picha kwa Hisan ya New Hanang Photo Studio)


UNNewsKiswahili: Abdullah aibuka kinara dhidi ya FGM nchini Sudan na habari zingine kem kem

NEWS ALERT: LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO

0
0

*Maduka yamepungua,baadhi ya wamiliki waingia mitini

*Kati ya maduka 297 ya awali sasa yamebaki 70,matawi 40

*BoT yaendelea kuchambua leseni za maduka 65, 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
BENKI Kuu ya Tanzania(BoT)imesema wakati mchakato wa kutoa upya wa leseni kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ukiendelea, maduka yaliyokidhi  vigezo hadi sasa ni 71 na matawi 40 kati ya maduka 297 yaliyokuwepo awali.
Juni mwaka jana, wamiliki was maduka hayo walitangaziwa kuwa wanatakiwa kuomba upya leseni za maduka ya kubadilisha fedha na hatua ilitokana na tuhuma mbalimbali za maduka hayo ikiwamo ya kwamba kuna baadhi ya maduka yanatumika katika utakashiji fedha.
Akizungumza mchakato kuhusu utoaji upya wa leseni kwa maduka hayo , Meneja wa Huduma za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha chini ya Usimamizi wa Idara ya Mabenki, Eliamringi Mandari amefafanua watatoa taarifa rasmi kuhusu mchakato huo.
Mandari wakati anatoa mada inayohusu kanuni mpya za usimamizi wa maduka ya fedha kwa waandishi wa habari waliopo kwenye semina iliyoandaliwa na BoT.
Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa taarifa sahihi zinazohusu uchumi,biashara na fedha,ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kati ya maduka hayo 297ni maduka 71 tu ndio yamekidhi vigezo.
"Naomba hapa tuelewane kwanza,mchakato wa kutoa leseni kwa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni bado unaendelea na utakamilika siku za karibuni na baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi.
"Hii ambayo tunaeleza si kwamba ndio taarifa ya mwisho ila naelezea hatua ambayo tumefikia hadi sasa.Mchakato huo ulianza Juni mwaka jana na ulitakiwa kukamilika Desemba mwaka jana.
" Hats hivyo umechelewa kukamilika kwasababu wamiliki wa maduka wengi walileta maombi tarehe 29 ya Desemba mwaka jana.Hivyo tumefunga maombi ya leseni na kinachoendelea no kupitia maombi maduka 65 na tukimaliza ndio tutatoa taarifa rasmi,"amesema Mandari.
Akifafanua zaidi Mandari amesema hadi sasa maduka ambayo yamekidhi masharti na vigezo vilivyotolewa na BoT ni 71 pamoja na matawi 40.Wamiliki wengine wa maduka hayo wapatao 50 wameshindwa kuomba maana hawajasema chochote ila wameona wapo kimya.
"Maduka 297 ya kubadilisha fedha za kigeni ndio yalikuwepo lakini kutokana na mchakato unaoendelea wapo walioshindwa kutimiza vigezo vilovyowekwa.Matokeo yake maduka yaliyokidhi vigezo ni 71 na matawi 40,hivyo tunaweza kusema ni kama maduka 111," amesema Mandari.

Ameongeza kwa kuwa muda wa maombi ulishakwisha maana yake hata kama maduka 65 ambayo maombi yake ndio yanaendelea kupitiwa hata kama yote yatapita bado idadi ya maduka haitafikia ile ya mwanzo kwani yamepungua.
Alipoukizwa maduka ambayo yamefungwa wameshindwa katika vigezo gani,amejibu wapo walioshindwa kwasababu ya kushindwa kuelezea mtaji wa fedha zao ,kwani wapo ambayo wamesema wamesema mitaji yao ilitokana na kuuza mali zao.
Pia wamiliki wengine wa maduka hayo wameshindwa kuelezea pesa zao zimetokana na mini kwani hata unapowauliza wapo wanadai wametoa fedha kwenye daladala lakini wanapoombwa wapeleke vielelezo wanashindwa.

Alipoulizwa je wamebaini uwepo wa maduka hayo kujihusisha na utakatishaji fedha,amejibu kuwa hawezi kulitolea majibu maana wanaohusika na hilo utakatishaji fedha ni taasisi nyingine.
Kuhusu walioshindwa kuomba tena leseni ya maduka hayo wakati zamani walikuwa wanatoa huduma za kifedha amejibu ni ngumu kujua sababu kwani hajaomba tena ,ni kama vile wameingia mitini.

Hata hivyo ,Mandari amesema mchakato huo umesaidia Serikali kupata fedha maana wapo ambao waliianzisha maduka kwa kuuza mali lakini hawakuwa wamelipa fedha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Walipokuja kwetu tuliwaelekeza na hivyo wapo waliokwenda TRA kuchukua baadhi ya nyaraka na ili wazipate walitakiwa kulipa fedha ambazo mwanzoni hawakuwa wamelipa," amesema Mandari.

WAFANYABIASHARA WADANGANYIFU KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

0
0
NA DITHA NYONI RUVUMA 

Mkuu wa mkoa wa RUVUMA BI CHRISTINA MNDEME amewataka wafanyabiashara katika mkoa wa huo kuhakikisha wanatumia vyema mashine ya kutolea risiti EFD kwa ajili kuongeza mapatao na kuweza kuwa baini wafanyabiashara wanaoiibia serikali mapato hayo ameyasema wakati akizungumza na wafanya biashara wa manispaa ya songea .

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

UWT KILOLO KUTATUA TATIZO LA VYOO SHULE YAMSINGI ILULA,ISOLIWAYA MKOANI IRINGA

0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa. 

WALIMU wa shule ya msingi Ilula na Isoliwaya zilizoko katika kata ya Ilula Wilaya ya Kilolo wanakabiriwa na magonjwa ya Mlipuko kwa kukabiliwa na changomoto ya choo.

Shule hizo zilizotenganishwa baada idadi kubwa ya wanafunzi, walimu 49 wanalazimika kutumia choo Chenye matundu mawili hali inayohatarisha usalama wa afya zao.

Akizungumza mbele ya Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer, mwalimu Msaidizi wa shule ya Msingi Isoliwaya, Huruma Mbena alisema hali hiyo inahatarisha afya za walimu kutokana na changamoto hiyo.

Mbena alisema kuwa baada ya shule hizo kutenganishwa vyoo vya walimu vilibaki kwa shule ya Ilula hivyo kutokana na idadi kubwa ya walimu wanalazimika kutumia vyoo hivyo licha ya kutotosheleza kutokana na idadi kubwa ya walimu.
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiongea na baadhi ya viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Isoliwaya wakatika wa kukabidhi msaada huo kwa ajili ya kujengea vyoo ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho Leah Moto na Nancy Nyalusi walikuwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41 ya chama cha mapinduzi 
Hili ni moja ya jengo lashule ya msingi Ilula iliyopo katika tarafa ya mazombe wilayani kilolo mkoani Iringa 
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiwa katika kusherekea miaka 41 ya kuzaliwa chama chao kwa kufanya shughuli za kijamiii


Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images