Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAIPONGEZA HOSPITALI HUBERT KAIRUKI KWA UJENZI JENGO LA KISASA KUSAIDIA WAJAWAZITO

$
0
0
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na  Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki (wa pili)  wakiangalia ramani ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kinachotarajiwa kujengwa na Hospitali ya Hubert Kairuki hivi karibuni Bunju jijini Dar es Salaam. 
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG

Serikali imetoa pongeza kwa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki kupitia Hospitali ya Hubert Kairuki kwa kujipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida. Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ali Hapi kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. 

Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. "Hatua Moja nzuri sana kwa manispaa yetu, maana huduma hii itapatikana hapa nchini jambo ambalo linaleta faraja sana kwa kuboresha huduma za afya kwa vile awali huduma kama hizo zilikuwa zikipatikana nje ya bara la Afrika... Mungu ni mwema itapatikana Tanzania," alisema Dkt. Dugange. Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki alisema kuwa tatizo hilo lipo dunia nzima, na shirika la afya duniani lilitoa takwimu milioni 48 wanachangamoto ya kupata watoto. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki akielezea juu ya ujenzi wa kituo hicho cha kisasa.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kujionea shughuli mbali mbali zilizokuwa zikiendeshwa na Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) kwa kipindi chote tokea Febriari 1-6, 2018 katika kuadhimisha Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone, Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki pamoja na mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SHEHENA YA MAGOGO 297 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MIL.26.3 YATAIFISHWA MANYONI

$
0
0
Na Jumbe Ismailly-ITIGI 

SHEHENA nyingine ya magogo 297 yenye thamani ya shilingi milioni 26,370,000/= yaliyokuwa yakimilikiwa na Kampuni ya ARIZONA ENTERPRISES iliyopo katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida yametaifishwa na serikali wilayani Manyoni na hivyo kufanya jumla ya magogo 720 yaliyotaifishwa na serikali baada ya kubainika kwamba mmiliki wa kampuni hiyo alikiuka taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu.

Mapema mwezi Oktoba,2017 serikali wilayani Manyoni ilitaifisha shehena ya magogo 423 yenye thamani ya shilingi milioni 283,022,000/= yaliyokuwa yamefichwa kwenye mashamba ya Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi,Yahaya Masare katika Kijiji cha Damwelu,kata ya Ipande,wilayani Manyoni,baada ya mmiliki wa mashamba hayo kuyakana kuwa siyo mali yake,licha ya kwamba mmoja wa watu waliokuwa wakishikiliwa na polisi wilayani Manyoni,Hassani Masare ni ndugu yake.

Akithibitisha shehena hiyo ya mazao ya misitu kutaifishwa,Afisa Ardhi na Maliasili Halmashauri ya Itigi,Rodney Ngalamba alisema baada ya kukamilisha taratibu za kisheria,mtuhumiwa au mshukiwa wa magogo hayo aliweza kulipa serikalini faini ya shilingi milioni 46.

Kwa mujibu wa afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya ardhi na Maliasili aliweka bayana pia kwamba katika upekuzi iligundulika kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria kwa maana baadhi ya shehena katika kiwanda ARIZONA ENTERPRISES kilichopo mjini Itigi kulikuwa na mzigo zidifu wa magogo 297.

“Kwa hiyo baada ya hapo mzigo huu wa magogo 297 pamoja na mzigo ule uliokamatwa awali shambani vimewekwa chini ya uangalizi wa serikali kwa ajili ya kupigwa mnada hapo baadaye kama taratibu za sheria za misitu namba 14 ya mwaka 2002 inavyoeleza.”alisisitiza Ngalamba.
Hata hivyo Ngalamba alithibitisha pia kwamba kimsingi magogo hayo yanaonekana ni ya HARIMU ENTERPRISES ambaye ni mshirika mkubwa wa kiwanda cha ARIZONA ENTERPRISES kinachomilikiwa na Yahaya Omari Masare kilichopo Itigi mjini.

Akizungumzia kuhusu hatua itakayofuata baada ya mtuhumiwa kutozwa adhabau ya faini,Ngalamba aliweka bayana kuwa shehena hiyo ambayo imetaifishwa na serikali itauzwa kwa njia ya mnada na baada ya kupatikana kwa nyaraka zinazohalalisha mzigo uliopo kiwandani,mmiliki wa Arzona Enterprises ataweza kurudishiwa ili aweze kuendelea na shughui zake za uchakataji wa magogo hayo.

Kuhusu shehena nyingine ya magogo iliyogundulika kwenye kituo cha reli Itigi,afisa huyo alibainisha kuwa magogo hayo bado yapo kituoni hapo na kwamba baada ya kupatiwa nyaraka halali ikiwemo TP,ndipo ataendelea na utaratibu wake ikiwepo kupeleka kwenye soko la kuuzia mazao hayo.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Halmashauri hiyo,Gilbert Modesti Kalanda aliyekuwa mmoja wa wajumbe sita wa tume iliyokwenda Kaliua,alisema akiwa mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo walikwenda Mkoani Tabora,na wilayani Kaliua kwenye eneo ulikotoka mzigo huo la Mpandaline mpakani mwa Kaliua na Katavi.

Kwa mujibu wa Kalanda baadhi ya mapendekezo ya tume hiyo yalikuwa ni pamoja na kuainisha makosa ya kukutwa na mazao ya misitu bila kufuata sheria na walimtaka mtuhumiwa kulipa shilingi milioni 26,370,000/= ambazo ni gharama za mzigo wote

“Lakini sheria inaenda mbali zaidi kwamba baada ya kulipa hizo gharama tajwa faini tajwa nini kinatakiwa kifanyike kwenye mzigo ambao unahusika kwenye ufanyikaji wa makosa hayo ya kisheria,tunaelekezwa pia na kifungu namba 95 kinachohusiana na masuala ya Compound tunatakiwa kutaifisha mzigo husika wa mazao ya misitu na kuwa mali ya serikali ambao utauzwa kwa taratibu za kimnada”alisisitiza.
 Mwanasheria wa Halmashauri ya Itigi,Gilbert Modesti Kalanda akitoa maelezo ya sababu zilizofanya magogo 297 kutaifishwa na kusubiri kuuzwa kwa njia ya mnada na serikali ya wilaya ya Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly) 
baadhi ya magogo yaliyotaifishwa na serikali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 26.3 kutokana na kukiuka taratibu za kisheria zinazosimamia misitu.

wawili wapendanao wajishindia milioni 10 za tatu mzuka

$
0
0
Mwakilishi wa kampuni ya TatuMzuka,Milard Ayo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,alipokuwa akiwatambulisha washindi wa TatuMzuka Daily,waliojinyakulia Milioni 10 wakiwemo wapenzi walioingia kwenye kampeni ya Valentine iliobeba kauli mbiu ya ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’.Pichani kulia ni washindi wa kampeni ya Valentine Jumanne Kabwe na Mariam Omary ambao wote kwa pamoja walijishindia milioni 10 na kushoto ni Nicolaus Chilipweli aliyejishindia milioni 10.
Pichani kushoto ni Mshindi wa TatuMzuka Daily,Nicolaus Chilipweli mkazi wa Bagamoyo akielezea namna alivyojishindia Kitita cha Milioni 10 kupitia mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka na namna atakavyozitumia fedha hizo.
Pichani ni washindi wa kampeni ya Valentine waliotimiza kauli mbiu ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’  Jumanne Kabwe na Mariam Omary ambao wote kwa pamoja walijishindia milioni 10

Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka ilizindua kampeni mpya ya Valentine, ambayo ilianza rasmi hivi karibuni mpaka Februari 18,2018.Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao pia kupata fursa ya kushinda.

UCHUMI CUP YAFUNGULIWA HANDENI KUHAMASISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA VIJANA

$
0
0
Katika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za maendeleo hususani kilimo mashindano ya mpira wa mguu na mpira wa pete UCHUMI CUP yamefunguliwa rasmi kwa ngazi ya robo fainali na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mapema mwishoni mwa wiki.

Akifungua mashindano hayo kwenye viwanja vya Kigoda Stadium Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi.Upendo Magashi alisema kuwa michezo ni furaha na amani hivyo fursa hiyo itumike kukuza vipaji lakini pia kujiunga katika vikundi vya uzalishaji hususani kilimo ukizingatia Handeni shughuli kuu ni kilimo.

Aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhakikisha vijana wanatumia vipaji walivyonavyo katika kuhakikisha wanainua uchumi wao na kuendana na falsafa ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU!.

Kwa upande wake mratibu wa mashindano Bw. Baraka Nkatura alisema kuwa Mashindano yalianzishwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe na kuamua kuyatumia kwenye msimu huu wa kilimo ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiinua kiuchumi.

“Tunaamini mbali ya kukuza mahusiano baina yetu, tutaweza kubadilishana uzoefu utakaotusaidia kukuza vipaji vyetu na kujiinua kiuchumi” alisema Mratibu.
 Wachezaji wa Kurugenzi FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mashindano dhidi ya Nyika FC
 Timu ya mpira ya Nyika FC wakiwa tayari kuikabili timu ya Kurugenzi FC
 Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi wa kwanza kushoto, waratibu wa michezo wawili upande wa kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na wachezeshaji wa mpira kabla ya mechi kuanza
 Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi akifuatiwa na waratibu WA michezo wakisalimiana  na Timu na uongozi wao kabla ya mechi kuanza
 Mechi Kati ya Kwamkono United na Vibaoni united ikiendelea

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Karani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA ahukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu imemuhukumu Karani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, Winfred  Businge (33) kulipa faini ya Sh milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Baada ya kupatikana na hatia ya tuhuma za kushindwa kutolea maelzo USD  milioni moja kwa afisa forodha.

Businge ambaye ni raia wa Uganda alifanikiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha cha Sh milioni 100 na kukwepa adhabu hiyo ya kifungo.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa, kukubali kosa.

Katika hati ya mashtaka,  ilidaiwa Desemba 11, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ndani ya jiji la Dar es Salaam Businhe alikutwa ameingia nchini na USD milioni 100 ambazo ni sawa na sh. Bilioni 2  fedha ambazo alishindwa kuzitolea  maelezo kwa wakala wa forodha.

Kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Wakili wa serikali mwandamizi, Awamu Mbagwa, kwa upande wa utetezi alikuwa akiwakilishwa na Wakili Hudson Ndusyepo.

TICTS WASHEHEREKEA REKODI YA ONGEZEKO SHUGHULI 2017-

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya TICTS, Jared.H. Zerbe akiongea kwenye hafla ilioyandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mwishoni mwa wiki iliyopita kusheherekea rekodi ya ongezeko la shughuli kwa mwaka 2017 ambapo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 300 ikilinganishwa na kiasi walichoshughulikia mwaka 2000.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya TICTS, Jared.H. Zerbe akiongea na wageni pamoja na wadau kwenye hafla ilioyandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mwishoni mwa wiki iliyopita kusheherekea rekodi ya ongezeko la shughuli kwa mwaka 2017 ambapo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 300 ikilinganishwa na kiasi walichoshughulikia mwaka 2000.
Wageni na wadau mbali mbali wakiwa kwenye hafla iliyoandaliwa na kampuni ya TICTS mwisho wa wiki iliyopita katika hotel ya Hyatt Regency ambapo TICTS walisheherekea rekodi ya ongezeko la shughuli kwa mwaka 2017 ambapo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 300 ikilinganishwa na kiasi walichoshughulikia mwaka 2000.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchini, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Viana, Akira na Wende Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto)  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba (katikati), Bungeni mjini Dodoma Februari 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Capt. George Mkuchika,  Bungeni mjini Dodoma, Februari 6, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Agness Marwa, Bungeni mjini Dodoma , Februari 6, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 6, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 6, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 6, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma Februari 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Na Agness Francis,  Globu ya jamii 
MABINGWA Afrika Mashariki na kati Azam FC watakuwa wageni dhidi ya vinara aa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc katika mchezo wao wa 2 mzunguko wa 2.

Mchezo huo  utakaorindima kesho  katika  dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Mzizima jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema wapo vizuri katika kumkabili mnyama Simba na kuhakikisha wanaondoka  na ushindi wa maboa ili kuweza  kuwasogelea  vinara hao wenye pointi 38.

Wakati  Azam FC wakiwa nyuma kwa pointi 33 wakiwazidi Yanga SC  wenye alama 31.

"Tunajua ni mchezo  utakaokuwa mgumu dhidi ya Simba SC kwa kuwa wana kikosi kipana na kizuri ila sisi tumejipanga kuhakikisha tunarudi na  ushindi nyumbani na vijana wapo vizuri wote wana morari ya  kufanya vizuri  katika mchezo huo "amesema Jaffary Maganga. 

Aidha amesema katika mchezo huo wa vuta ni kuvute dhidi ya wekundu hao  wa Msimbazi wataendelea kuwakosa wachezaji wao ambao wapo majerui, Waziri Junior na Joseph Kimwaga  ambaye bado hayupo vizuri mpaka sasa kwa kuwa  alifanyiwa upasuwaji wa goti hapo siku za nyuma.. 

"Mchezaji wetu Aboubakar Salum  maarufu kama (Sure boy) atarejea mchezoni Kesho akiwa amemalizia kutumikia adhabu yake ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa 16 wa kukamilisha mzunguko wa 1 uliochezwa pale Chamazi na Mabingwa watetezi YangaSC na kusababisha  kukosa mechi iliyopita dhidi ya NdandaFC," amesema Maganga.
Msemaji Mkuu AzamFc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi zao Mzizima Jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi yanayoendelea katika kikosi chake ambapo kesho watavaana  na mnyama simba katika Dimba la Uwanja wa Taifa majira ya saa 10 jioni.

JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
MKUU  wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa Gofu wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya jeshi kwa kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora wanaowakilisha nchi kimataifa.

Aliyasema hayo Makao Makuu ya Jeshi Upanga  jijini Dar es Salaam  wakati akiagana na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano ya wazi ya wanawake nchini  Nigeria IBB Ladies Open Championship  2018 yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Jenerali Mabeyo amesema kama ilivyokuwa katika michezo ya iiadha na ngumi sasa tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.

“ Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji  wa Gofu na hata Michezo mingine kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa chachu kwa wengine,” alisema  Jenerali Mabeyo.
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akimkabidhi Bendera  ya taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la  Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini Nigeria Hivi karibuni ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la  Wananchi wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini Nigeria Hivi karibuni.
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa  Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la  Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini Nigeria hivi karibuni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UTARATIBU WA SHERIA UNAPOHAMISHA OFISI ZA KAMPUNI.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Vijana  wengi  wamefungua  makampuni. Mengine  tayari  yanafanya  kazi  na  mengine  hayafanyi  kazi. Kutokana  na  sababu  mbalimbali  vijana  wamekuwa  wakihamisha  ofisi  za kampuni  zao. Wengine  sababu  za  kodi  ya  pango, wengine  kutafuta  maeneo  mazuri  zaidi  ya  biashara, na  sababu  nyingine  nyingi.Natumia neno vijana kwakuwa ndio wengi japo hili ni kwa kila mwenye kampuni.


Hata  hivyo  wengi  wao  wamekuwa  wakihamisha  ofisi  zao  kiholela. Kwa  maana  wanahamisha  kwa  utashi  wao  bila kuzingatia  kuwa  kuna  utaratibu  wa kisheria  unaotakiwa kufuatwa.  Niseme  tu  kuwa  unapokuwa  umefungua  kampuni  tayari  tafsiri  yake  ni  kuwa  upo  katika  mfumo  rasmi.  Mfumo  rasmi  maana  yake  biashara  zako zinalindwa  na  sheria  halikadhaliki biashara  hizohizo  zinawajibika  chini ya  sheria.


Lolote  utakalofanya  yafaa  ujue  sheria  inasemaje  kuhusu  hilo  ili usije  kuingia  katika  makosa au usije  ukajikosesha haki  zako. Niseme tu  kuwa  Sheria  Namba 12 , Sheria ya Makampuni imelifanya  kosa  tendo  la  kuhamisha  ofisi  bila kufuata  utaratibu  wa  kisheria  kama  tutakavyoona  hapa.

1.      OFISI  ZA  KAMPUNI  NI  ZIPI ?.


Mtakumbkua  kuwa  unapokuwa  unasajili  kampuni kuna  pahala huwa  unatakiwa  kujaza/kueleza  ni  wapi itakuwa  ofisi  za  kampuni  yako. Kipo  kifungu  cha  pili  katika  kila  katiba  ya  kampuni  ambacho  huwa  kinahitaji  kueleza  makao  makuu  ya  ofisi  za  kampuni (head office).Lakini  pia  ipo  sehemu  unapokuwa  unajaza  fomu  namba 14(a)  huwa  inakutaka  kueleza  wapi  zitakuwa  ofisi  za  kampuni yako. 

Hapa  huwa  unatakiwa  kueleza  kinagaubaga. Hapa maelezo  ya  wapi  zitakuwa  ofisi  za kampuni huwa yanatakiwa yajitosheleze  kiasi  kwamba  mtu  akisoma  aweze  kufika  ofisi  ilipo  bila  hata  kuuliza.


Isiwe  tu ,P.O.BOX 200 DAR ES  SALAAM  bali  mtaa, kitongoji, kata, hata  nyumba  namba kama  ipo au  namba  ya  mlango na ghorofa  nk nk.  Hii  ndio huitwa  anuani  kamili  ya  ofisi  za  kampuni na  hizo  ndizo  ofisi  za  kampuni. Ni  kosa  kukutwa  umeweka  ofisi eneo  tofauti na  lile  lilioandikwa  kwenye  nyaraka. Vinginevyo  ofisi  ziwe  zimebadilishwa  tena kwa  utaratibu  huu  hapa  chini.



                    KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

TANZIA

RAIS WA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA BALOZI WA INDONESIA NCHINI TANZANIA IKULU LEO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Ratlan Pardede, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Balozi Ratlan Pardede, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Balozi Ratlan Pardede na Viongozi wa Serikali baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

STARTIMES YAMKUTANISHA STAA MAU DOU DOU NA WASANII WA FILAMU NCHINI

$
0
0
Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imefanya hafla fupi ya kumkutanisha muigizaji maarufu wa China Hai Qing maarufu kama Mau Dou Dou na wasanii wa Kitanzania pamoja na mashabiki wake.

Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (NICC) na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali maarufu akiwemo Natasha, Yvone na Davina. 

Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing maarufu kama Mau Dou Dou amekuja nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili ambapo moja ni kutangaza kampuni ya Startimes.Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif amesema kuwa msanii huyo sehemu kubwa anatangaza Kiswahili katika king’amuzi cha Startimes.Amesema kuwa msanii huyo amekuwa na kazi nyingi kwa Ubalozi wa nchini China pamoja na Startimes ikiwa ni kukuza Kiswahili.
Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou" (kushoto) akizungumza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari, wasanii wa filamu nchini pamoja na mashabiki wake leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro(kulia) akifanya mahojiano na Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou"  alipokutana na wasanii wa filamu pamoja na mashabiki wake leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi tuzo Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou" (kushoto)  kwa niaba ya watanzania ambao ni mashabiki wake.
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Suzan Lewis "Natasha "(kulia) akitoa shukrani kwa niaba ya wasanii wa filamu nchini wakati wa ziara ya  Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou Dou"  alipofika na kufanya mazungumzo nao leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO

$
0
0
*Maduka yamepungua,baadhi ya wamiliki waingia mitini
*Kati ya maduka 297 ya awali sasa yamebaki 70,matawi 40
*BoT yaendelea kuchambua leseni za maduka 65, 

Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT)imesema wakati mchakato wa kutoa upya wa leseni kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ukiendelea, maduka yaliyokidhi vigezo hadi sasa ni 71 na matawi 40 kati ya maduka 297 yaliyokuwepo awali.

Juni mwaka jana, wamiliki was maduka hayo walitangaziwa kuwa wanatakiwa kuomba upya leseni za maduka ya kubadilisha fedha na hatua ilitokana na tuhuma mbalimbali za maduka hayo ikiwamo ya kwamba kuna baadhi ya maduka yanatumika katika utakashiji fedha.

Akizungumza mchakato kuhusu utoaji upya wa leseni kwa maduka hayo , Meneja wa Huduma za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha chini ya Usimamizi wa Idara ya Mabenki, Eliamringi Mandari amefafanua watatoa taarifa rasmi kuhusu mchakato huo.

Mandari wakati anatoa mada inayohusu kanuni mpya za usimamizi wa maduka ya fedha kwa waandishi wa habari waliopo kwenye semina iliyoandaliwa na BoT.Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa taarifa sahihi zinazohusu uchumi,biashara na fedha,ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kati ya maduka hayo 297ni maduka 71 tu ndio yamekidhi vigezo.

"Naomba hapa tuelewane kwanza,mchakato wa kutoa leseni kwa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni bado unaendelea na utakamilika siku za karibuni na baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi."Hii ambayo tunaeleza si kwamba ndio taarifa ya mwisho ila naelezea hatua ambayo tumefikia hadi sasa.Mchakato huo ulianza Juni mwaka jana na ulitakiwa kukamilika Desemba mwaka jana.

DC HANANG AFUNGA MAFUNZO YA MGAMBO

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Hanang, Sarah Msafiri  akikagua gwaride wakati  alipofunga Mafunzo ya Mgambo katika tarafa ya Bassotu wilayani humo mwishoni mwa wiki. (Picha kwa Hisan ya New Hanang Photo Studio)


RC NDIKILO AIAGIZA CBT KUMLIPA MALIPO MKANDARASI GHALA LA KUHIFADHIA KOROSHO MKURANGA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha inamlipa ,malipo ya awali kiasi cha sh.bilioni 1.6, mkandarasi wa ghala la kuhifadhia korosho wilayani Mkuranga.

Alitoa agizo hilo ,wilayani Mkuranga alipotembelea ujenzi wa ghala hilo linalojengwa na kampuni ya BQ Contractors Ltd .Alieleza kabla ya ujenzi waliingia mkataba wa kulipa asilimia 30 ya malipo ya awali ya ujenzi wa ghala hilo la kisasa ambalo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.5 hadi kukamilika kwake.

Aidha Ndikilo alisema, kampuni hiyo ilitoa malalamiko kuwa zimepita siku 52 wakiwa hawajapewa hata shilingi moja kwa ajili ya ujenzi huo hali ambayo inasababisha ujenzi huo kuwa mashakani kukamilika kwa wakati.

“CBT ihakikishe inatoa fedha hizo ndani ya wiki hii, bodi ya korosho ambao ndiyo wamiliki wa ghala hilo na endapo watashindwa kufanya hivyo atawapeleka kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya hatua zaidi";
MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,(kulia)akielekeza jambo baada ya kuonyeshwa ramani ya ghala la korosho ambapo linatarajia kujengwa huko Mkuranga, wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa ghala hilo .(Picha na Mwamvua Mwinyi) .


TANZANIA,CHINA KUSHIRIKIANA KUONGEZA WATALII.

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

TANZANIA na China zimeamua kushirikiana kwa lengo la kukuza soko la utalii nchini.

Hivyo imeelezwa watu maarufu na mashuhuri wa nchi ya China akiwamo mwigizaji maarufu wa nchi hiyo Maododo atakuwa miongoni mwa watakaokuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.Hatua inakuja kipindi ambacho kumekuwa na uchache wa watalii wa kutoka China kuja Tanzania,hivyo moja ya mkakati wa kuongeza watalii hao ni kuweka ushirikiano kwenye eneo la utalii.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) uliofanyika leo Dar es salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema uhusiano wa China na Tanzania ni wa muhimu sana.

Amefafanua kuwa wana wanampango wa kubadilisha mfumo ili Wachina waingie kwa wingi nchini na kuboresha soko la utalii nchini China.Amesema fursa ya Wachina kushirikiana katika utalii i ni nzuri hasa  ikitumika ipasavyo.

"Kwani wamepata nafasi ya kuwatumia watu maarufu kutoka nchini China ili kusaidia kutangaza utalii wa Tanzania na moja ya watu maarufu watakaotumika kama mabalozi wa kutangaza Utalii ni muigizaji maarufu kutoka China.
 Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua  mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya Utalii jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Miyayo akizungumza kuhusiana na utalii nchini wakati wa mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya Utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori  na Mtafiti wa Sokwe Mtu  Sokwe wa Mkoa wa Kigoma ,Dk. Jane Goodal akizungumza kuhusiana na Utalii nchini leo jijini Dar es Salaam.
 Msanii Maarufu nchini China, Nanping Liu akikabidhi zawadi Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori  na Mtafiti wa Sokwe Mtu  Sokwe wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Jane Goodal katika Mkutano wa Utalii jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa wadau utalii kati ya Tanzania na China leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. 

Miongoni mwa mambo waliyojadili ni kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha maeneo ya vivutio na miji ya ukanda huo pamoja na viwanja vya ndege ndani ya hifadhi viwe na hadhi na ubora wa kutua ndege kubwa ikiwemo za Air Tanzania. 

"Nawapongeza kwa mradi huu ambao ni mzuri sana kwenye uhifadhi lakini una mapungufu kidogo kwenye biashara ya utalii jambo ambalo ni muhimu kuangaliwa ili uwe na tija zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla" alisema Dk. Kigwangalla.

Alimuomba mratibu huyo kuona namna ya kubadilisha vipengele vya utekelezaji wa mradi huo ili uweze kuwa na tija zaidi hususan suala la miundombinu ya kuunganisha hifadhi mbalimbali za ukanda huo na miji ili kurahisisha usafiri wa kufikia vivutio hivyo kwa muda mfupi na kwa wakati.

Kwa upande wake mratibu huyo alisema jambo hilo linajadilika na kwamba uendelezaji wa maeneo hayo ni mtambuka ukihusisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambazo nazo zimeahidi kuboresha miundombinu ya maeneo hayo.

Mradi wa REGROW unatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 Februari mwaka huu Mjini Iringa na Mhe. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Mwezi Agosti mwaka jana Serikali ya Tanzania ilisaini mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani Milioni 150 sawa na takriban bilioni 340 za Tanzania kwa ajili ya kuendeleza mradi huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 baada ya kujadili mambo kadhaa ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Katikati ni Mratibu wa mradi huo kutoka Tanzania, Someni Mteleka. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WMU)

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI AITAKA GOLF LUGALO KUREJESHA HESHMA YA JESHI MICHEZONI

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Gofu ya Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya jeshi kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora wanaowakilisha nchi kwa mafaniko.

Aliyasema hayo Makao Makuu ya jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano ya wazi ya wanawake nchini Nigeria IBB Ladies Open Championship 2018 yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Jenerali Mabeyo alisema kama ilivyokuwa katika Michezo ya Riadha na Ngumi sasa tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.

“ Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji wa Gofu na hata Michezo mingine kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa chachu kwa wengine” Alisema Jenerali Mabeyo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Bendera ya taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni
Mwenyekiti wa wa Chama cha Gofu nchini Joseph tango (Aliyesimama) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya jeshi Upanga ambapo Timu ya Wanawake ya Klabu ya jeshi ya Lugalo walikabidhidhwa bendera kwa Ajili ya kushiriki Michuano ya Wazi nchini Nigeria aliyeka Kushoto ni Mwenyekii wa Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni (Picha na Luteni Selemani Semunyu


MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA

$
0
0
Mtoto mwenye umri wa miaka Mitano Jazaka Mussa, ameuwawa kikatili kwa kukatwa na Panga kichwani na mtu asiyefahamika katika kijiji cha Lipwidi, halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Akithibitisha taarifa za tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema muuwaji alimvamia mama wa mtoto huyo, Amina Saidi ambae alimbeba mwanae mgongoni na kumkaba huku akimlazimisha awe mke wake, kabla ya mama huyo kumdondosha mtoto na kukimbia.

Aidha, kamanda huyo wa Polisi ameongeza kuwa, baada ya tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walifika eneo la tukio na kisha kumshambulia mpaka kufa muuwaji huyo na kisha kumchoma moto.

Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kujua undani wake, ambapo bado muuwaji hajafahamika kwa majina na makazi yake.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images