Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUBORESHA MAFUNZO KWA WATU WENYE ULEMAVU

0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi vya Watu wenye Ulemavu ili kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri na kupata ujuzi mbadala wa kumudu maisha yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Stella Ikupa leo Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Mukasa lililohusu umuhimu wa kuwatazama vijana wenye ulemavu mbalimbali kwa namna ya kipekee.

Mhe. Ikupa amesema kuwa Serikali inatambua Vijana wenye ulemavu kuwa ni kundi mojawapo miongoni mwa watanzania wenye ulemavu ambalo linakabiliwa na changamoto mbalimbali.

“Kwa kutambua umuhimu wa kundi hili la watu wenye ulemavu wakiwemo vijana, Serikali iliunda Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu ambalo kazi yake kubwa ni kutoa ushauri kwa Serikali na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya watu wenye ulemavu juu ya namna bora ya kushughulika na changamoto zao zikihusisha zile za kundi la vijana wenye ulemavu,” amefafanua Naibu Waziri Ikupa.

Aidha, Mhe. ikupa amesema kuwa Serikali imeendelea kuunda kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri ya Wilaya, Kata na Mtaa kwa lengo la kuhakikisha masuala ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa ili kuondokana na kero mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu Elimu, Afya, Ajira na Mikopo ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Hata hivyo, Naibu Waziri Stella Ikupa amewahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia ipasavyo utekelezaji wa suala hilo ambalo liko kisheria na pia ametoa wito kwa Wakurugenzi hao kuhamasisha walemavu kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ikiwemo vikundi vya vijana.

WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA

0
0

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa, ameitisha kikao cha wadau wa pamba nchini, ili kujadili namna bora ya kuongeza tija ya zao hilo.

Kikao hicho kitakachofanyika jijini Mwanza Februari 15 hadi 16, 2018, kinatarajiwa kuondoa sintofahamu iliyogubika sekta ya pamba, kuhusu mustakabari wa kilimo cha mkataba kutokana na kusudio la Serikali kuanzisha ununuzi wa pamba kwa njia ya mnada kupitia vyama vya ushirika.  

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuonesha kusudio la kusitisha kilimo cha mkataba, na uwezekano wa pamba kuuzwa kwa njia ya mnada.Kulingana na taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, kikao hicho muhimu kimelenga kuondoa hali ya sintofahamu, juu ya kilimo cha mkataba na uuzwaji wa zao hilo kwa njia ya mnada.



Kusudio hilo la Serikali la kuuzwa pamba kwa njia yamnada, limeonekana kuleta wasiwasi kwa makampuni yaliyowekeza kwenye sekta hiyo muhimu katika uchumi wa nchi. 
Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo Charles Tizeba kabla ya kuanza ziara ya kuona utekelezaji wa kilimo cha Pamba na uzalishaji wa mbegu bora za pamba za UKM08 Msimu 2017/2018 uliofanyika jana tarehe 04 feb 2018.
Akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa mkoa huo Agrey Mwanri, Waziri Tizeba pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wakulima na kugundua kuwa bado elimu ya unyunyiziaji dawa haijakaa sawa.
"Tunakwenda kujadiliana nao wanunuzi hawa wa pamba, hususani walioingia kilimo cha mkataba. Asilimia 40 ya Watanzania wote wanategemea uchumi wao kupitia pamba," alisema Waziri Tizeba.Alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwa ziara ya kukagua mafanikio ya zao la pamba, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment inayojihusisha na ununuzi wa pamba, Gasper Gaki, alisema: “Tunakingoja kwa hamu sana kikao hiki na Waziri Mkuu, naamini kitakuwa na mafanikio.”Katika hatua nyingine, Waziri huyo mwenye dhamana ya Kilimo alisifu juhudi za kilimo cha pamba, ambapo Mkoa wa Tabora umevuka lengo lake la uzalishaji zao hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

ZIMAMOTO YAJIWEKA TAYARI KWA MAOKOZI MAJINI

0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye katika picha ya pamoja na Kikosi cha Maokozi cha Jeshi hilo, wakati alipotembelea Kikosi hicho kilipokuwa kikionesha zoezi la maokozi, kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Bashiri Madhehebi ambaye ni Mkuu wa kikosi hicho.
Wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo pichani), jinsi wanavyoweza kufanya maokozi katika maji alipotembelea eneo la daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni walipokuwa wakifanya zoezi hilo, mapema leo asubuhi (kushoto) ni Sajini wa Zimamoto Salehe Salla na aliyevaa boya maalum kwa ajili ya maokozi ni Koplo wa Zimamoto Omary Katonga.
Mzamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini wa Zimamoto Saidi Sekibojo akiwa katika mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea.
Sehemu ya Askari wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Koplo Omary Katonga (kulia) wakionesha utimamu mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo picha) mara baada ya kufanikiwa kumuokoa mhanga aliyekuwa kazama katika kina kirefu cha maji, wakati wa mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea.
Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

0
0
Serikali imejipanga kutumia tiba mtandao kuboresha huduma za afya nchini kwenye hospitali zote za ngazi ya taifa, rufaa na wilaya ili kuwawezesha wagonjwa waishio sehemu mbali mbali nchini kupata huduma za afya kwa wakati na kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la LAPF, Dodoma.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha watendaji wakuu wa hospitali za taifa nchini, madaktari bingwa wa sekta ya Afya, wakuu wa taasisi zinazoshughulika na sekta ya Afya, Wizara ya TAMISEMI, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; taasisi nyingine za Serikali; sekta binafsi na wabia wa maendeleo ili kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja wa kufanikisha utekelezaji wa huduma za tiba mtandao ili kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na madawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na yanayotokana na ajali za barabarani. “Hadi hivi sasa ni asilimia 37 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ndio wanaotambulika na kupatiwa huduma na Wizara ya Afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo, tiba mtandao itawezesha upatikanaji wa wagonjwa na ufikishaji wa huduma kwao kwa wagonjwa wengine asilimia 63”, amefafanua Dkt. Ulisubisya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza jambo kwa wataalamu wa sekta ya afya wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa tiba mtandao nchini kwa wataalamu wa sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Peter Phillip Mwasalyanda (aliyeketi katikati), akisikiliza kwa makini kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma
Wataalamu wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (hayupo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma


RAIS MAGUFULI AONGOZA MAZIKO YA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi  la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

 Wajukuu wa marehemu pamoja na wafiwa wengine wakiwa katika hali ya majonzi makaburini hapo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji mara baada ya maziko ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe

0
0
Na Robert Hokororo- Ofisi ya Mkurugenzi 

Halmashauri ya wilaya ya Kishapu imeweza kupiga chapa jumla ya ng’ombe 225,131 katika zoezi la utambuzi na usajili wa mifugo linalofanyika katika kata zote zenye wafugaji wilayani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Stephen Magoiga amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na limeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa.Alisema zoezi hilo ni agizo kutoka serikalini na kinachofanyika ni kulitekeleza kwa kiwango kinachotakiwa na kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo mbalimbali katika kata za wilaya hiyo.

“Zoezi la upigaji chapa ng’ombe tulilipokea na tumeweza kulitekeleza ingawa zipo changamoto mbalimbali zikiwemo baadhi ya maeneo kutokuwepo kwa wafugaji tumefanikiwa kuifikia mifugo hiyo,” alisema.Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri hiyo, Dk. Alphonce Bagambabyaki alisema Wilaya imeweza kufikia lengo hilo kwa zaidi ya asilimia 75 ya lengo ambalo ni ng’ombe laki tatu.
Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki akishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe.
Wananchi wakishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katiia kijiji cha Wishiteleja kata ya Mondo.
Moja wa ng’ombe akiwa tayari amepigwa chapa katika sehemu ya mguu.



VOA SWAHILI: Duniani Leo 5th February 2018

UNNewsKiswahili leo Februari 5, 2018


Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari

0
0
Na Ali Issa - MAELEZO 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu  amesema uwendeshaji wa kesi kwa mwaka uliomaliza haukuwa mbaya na kwamba  kiasi Idara ya Mahakama imefanikiwa katika utekeleza wa majukumu yake.
Hayo ameyasema leo huko Afisini kwake Vuga  mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea maazimisho ya wa wiki ya sheria duniani ambayo kilele chake hufanyika February 12 ya kila mwaka. Amesema pamoja na changa moto zinazoikabili Idara ya Mahakama lakini wamefanikiwa kuzitolea hukumu kesi mbalimbali ikiwemo za udhalilishaji na Madawa ya kulevya nchini
Amesema licha ya Wananchi wengi kulalamikia Idara hiyo kwa kushindwa kutoa hukumu kama wanavyodai lakini changamoto kubwa inayojitokeza ni kushindwa kutoa mashirikiano ipasavyo hasa katika kutoa ushahidi. Jaji Makungu amesema ni vyema Wananchi kutoa mashirikiano ipasavyo ikiwemo kutoa ushahidi kila inavyohitajika ili kuwatia hatiani wale wanaofanya makosa na jinai mbalimbali nchini.
“Huwezi kumtia mtu hatiani bila kutolewa ushahidi wa kutosha..Wananchi wengi wanashindwa kutoa ushahidi” Alisema Jaji Mkuu Makungu. Akielezea mafanikio amesema Mahakama imefanikiwa kuyakarabati Majengo yao na kuwa katika hali bora na hivyo kuwarahisishia Watendaji wa mahakama kuwajibika vizuri.
Aidha alisema wameweza  kuweka vizuri Maktaba yao hali ambayo inawejengea uwezo Wanasheria kwa kupata taluma na miongozo ya kazi kupitia Maktaba hiyo.
Akizungumzaia kuhusu shamra shamra za maadhimisho hayo Jaji Makungu amesema wanatarajia kufanya maonesho ya siku tatu kuazia February 9 hadi 11 katika viwanja vya maisara. Jaji Makungu alisema  kilele cha sherehe hizo zitafanyika baraza la wakilishi la zamani na mgeni rasmi wanatarajia atakuwa DKT. Ali muhamed shein na Ujumbe wa mwaka huu ni kuimarisha utwala wa sheria na uchumi .
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu katikati akizungumza na Waandishi wa Habari   kuhusiana na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja. Ujumbe wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.kulia yake ni Kaimu mrajisi wa Mahkama Yessaya Kayange na kushoto ni Hakimu wa Mahkama ya Watoto Sabra Ali Mohammed.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria  Mkutano wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.

Kaimu Mrajisi wa Mahkama  Yessaya Kayange akitolea ufafanuzi wa baadhi ya maswali yalioulizwa katika  Mkutano wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.kushoto ni Hakimu wa Mahkama ya Ardhi Said Hemed.

KENYA – A Country At Economic and Political Crossroads by ZURIEL ODUWOLE: The Next Chapter(s)

0
0
Believing that the best way to change the negative perception on Africa is to show investors potential partners on the continent, Film Maker Zuriel Oduwole has continued her series, focusing on the East African economic powerhouse; Kenya

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA UTAFITI WA MAPATO,MATUMIZI KWA KILA KAYA GEITA

0
0
Na,Consolata Evarist,Geita

Wananchi Mkoa wa Geita wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye zoezi la utafiti wa mapato na matumizi kwenye Kaya binafsi ili kutoa takwimu za hali ya umasikini zitakazosaidia serikali na wadau wengine kutathimini hatua zilizofikiwa katika kutimiza malengo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. 

Miongoni mwa Malengo hayo ni pamoja na yale yaliyoainishwa katika mpango wa pili wa maendeleo ya miaka mitano pamoja na maendeleo endelevu.Kata, Vijiji, Mitaa na vitongoji 34 mkoani humo vinatarajia kufanyiwa utafiti huo ili kupata taarifa zinazohusu Kaya na wanakaya, Uzazi na unyonyeshaji, elimu, afya, uraia, uhamiaji, ulemavu, bima, hali ya ajira, biashara na mapato ya kaya na makazi ya kaya.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alisema utafiti huo utasaidia kuweka misingi katika kutambua viashiria vya kiuchumi, ajira na ustawi wa jamii vitakavyofuatiliwa kwa kipindi husika na kupata makadirio ya jumla ya mwenendo wa matumzi ya kaya ili kuandaa fahirisi za bei.

“Napende kuwahakkisa wananchi wa mkoa wetu kuwa katika kutekeleza maagizo ya serikali ,uongozi wa mkoa umeendelea kuhimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”Alisema Luhumbi.
Mkuu wa mkoa Geita ,mhandisi Robert Luhumbi kushoto akiwa na Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafisi Tanzania Bara wa mwaka 2017/18. 
Katibu tawala wa Mkoa wa Geita,Celestine Gesimba akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi. 
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja  akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Mkoani humo. 

MAGAZETI YA JUMANNE LEO FEBRUARY 6,2018

Ujumbe Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Lesotho Wakutana na Naibu Waziri Kwandikwa

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kushoto) akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) ameongoza ujumbe huo uliokuja kwa ziara ya mafunzo nchini Tanzania. 
Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini wakiwa kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale akielezea namna TANROADS inavyotekeleza kazi zake kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu na wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa nchi ya Lesotho, Mathabathe Hlalele (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania. 

KUMBUKUMBU YA MAMA OMWANA THERESIA NYAMICHWO RUTAGERUKA

0
0

TAREHE 6 – FEBRUARI 2018, UMETIMIZA MIAKA 24 TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.
TUNAADHIMISHA KUMBUKUMBU HII TUKIOMBA MWENYEZI MUNGU AWAKUTANISHE KWENYE RAHA YA MILELE NA MUME WAKO MPENDWA MWALIMU NOVATI RUTAGERUKA AMBAYE SIKU ZOTE ALIKUKUMBUKA KATIKA SALA ZAKE KABLA YA KUTWALIWA NA BWANA TAREHE 5 MEI 2010.
MNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WENU FROLIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU ITAADHIMISHWA JUMANNE TAREHE 6 - FEBRUARI - 2018 KATIKA KANISA LA MTAKATIFU MAURUS, KURASINI, DAR-ES-SALAAM SAA 12.30 ASUBUHI.
BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA


MICHUZI TV: MWANAMITINDO ASIA IDAROUS ATANGAZA KULIACHIA TAMASHA LA LADY IN RED

wanahabari wapewa somo USIMAMIZI WA MABENKI NA TAASISI ZA FEDHA mkoani Mtwara

0
0
1
 Meneja Usimamizi wa Mabenki (BOT), Eliamringi Mandari akiwasilisha mada ya Usimamizi wa shughuli za Mabenki na Taasisi za Fedha katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali inayofanyika kwenye ukumbi wa (BoT) mkoani Mtwara, ambapo wanahabari wamepata ufafanuzi mbalimbali katika masuala ya ya shughuli zinazofanywa na mabenki katika biashara ya kifedha nchini Tanzania kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
4
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo inayoendelea kwa siku ya pili leo mjini Mtwara.
7
 Mkurugenzi Tafiti za Uchumi (BoT),Jonson Myella akichangia mada kuhusu Mabadiliko ya Mfumo mpya wa Kuandaa sera ya Fedha, Mapitio ya Maendeleo ya Uchumi nchini, Kikanda na Kimataifa Duniani iliyotolewa katika semina hiyo.
9
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa.
11
Jonson Myella Mkurugenzi Tafiti za Uchumi (BOT), Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BoT) na Eliamringi Mandari Meneja Usimamizi wa Mabenki (BoT) wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa semina hiyo. 

SERIKALI YATOA SIKU SABA WANANCHI WALIOVAMIA JUMUIYA HIFADHI WANYAMAPORI YA JUKUMU KUONDOKA

0
0
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na wa TAMISEMI imetoa siku saba kwa wananchi waliovamia kwa kuendesha maisha yao na kufanya shughuli za kilimo pamoja na kulisha mifugo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo katika Halmashuri ya Morogoro vijijini kuondoka katika hifadhi hiyo.

Hali hiyo inafuatia baada ya wananchi hao kwenda mjini Dodoma kuonana na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na kumuelezea malalamiko yao kuwa wao ni wakazi halali katika eneo hilo lakini hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Regina Chonjo amekuwa akiwalazimisha kuondoka.

Kufuatia hali hiyo , Waziri Mkuu K Majaliwa alimuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa TAMISEMI kwenda huko kwa ajili ya kushughulikia tatizo hilo ambapo Mawaziri hao kutokana na kubwana na majukumu mengine waliwaagiza Manaibu Waziri wao kutembelea eneo. .

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda jana walitembelea eneo hilo na kujionea uharibifu unaoendelea.Katika ziarz hiyo Manaibu Waziri hao walizungumza na wananchi hao kwa kumtaka mwananchi yeyote mwenye nyaraka halali za kuishi katika eneo hilo aziwasilishe katika mkutano huo lakini hata hivyo hakuna mwananchi yeyote aliyeziwasilisha

Kutokana na wananchi hao kukiri kuishi kinyume na sheria katika eneo hilo la Hifadhi, Wananchi hao waliowaomba viongozi hao wapewe muda ili waweze kutafuta sehemu ya kuhamia kwa vile hawana sehemu ya kwenda,Kulingana uharibifu mkubwa waliojionea katika eneo hilo hali ya mazingira, Mnaaibu Waziri hao waliweza kuagiza mambo yafuatayo huyo. Kama.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza waliovamia eneo la Mkesa ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph kakunda kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikati
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa ndani ya Jumiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikatiMkuu wa wilaya ya Morogoro akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara akiwa ameongozana na Manaibu wawili wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda wakati walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto) wakimsikiliza miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa yeye ni mkazi halali katika eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU wakati wa ziara iliyofanyika jana kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .Baadhi wananchi wakiwasilikiliza Manaibu Waziri katika mkutano uliofanyiak jana katika eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati wakati wa ziara kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .

VILABU VITATU VYA MICHEZO VYAPONGEZWA KWA KUPANDA DARAJA

0
0
Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kinazipongeza timu za JKT Tanzania, KMC na African Lyon  kwa kufanikiwa kuwa miongoni mwa timu sita zilizopanda ligi kuu daraja (VODACOM Premier League) kwa msimu wa 2018/19.
 
DRFA inaamini mafanikio waliyopata timu za JKT, KMC na African Lyon yametokana na uongozi bora pamoja na mipango mizuri waliyojiwekea katika vilabu vyao. Kwahakika wameutendea HAKI Mkoa wa Dar es Salaam.
  
Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kinawahakikishia vilabu hivyo vilivyopanda na vilabu vingine vilivyopo katika ligi kuu (VODACOM Premier League) kuwa DRFA itaendeleza ushirikiano uliopo na uongozi wake pamoja na kamati nzima ya utendaji ya vilabu hivyo katika masuala mbalimbali ya kuendeleza soka la Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla.
 
Kwa niaba ya kamati ya utendaji ya DRFA na familia ya mpira wa Miguu katika mkoa wa Dar es Salaam tunawapa pongezi za dhati kwa mafanikio hayo mliyoyapata na kuomba kuitumia nafasi hiyo kuweza kujipanga na kuwa na maandalizi mazuri kwa ajili ya kufanya vizuri zaidi katika ligi kuu (VODACOM Premier League) msimu wa 2018/19 na inayofuata.
 
Mbali na pongezi hizo kwa vilabu vya Dar es Salaam vilivyopanda ligi kuu (VODACOM Premier League), DRFA pia imeipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Rais Walace Karia pamoja na Bodi ya Ligi (TPLB) kwa usimamizi mzuri wa Ligi ya daraja la kwanza (FDL) msimu wa 2017/18 iliyomalizika jana bila ya viashiria vyovyote vya upangaji wa matokeo.

Almasi J. Kasongo,
Mwenyekiti
Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa Wa Dar es Salaam (DRFA)

CCM LUSHOTO YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU CHA IRENTE

0
0
 Katika kusherehekea miaka 41 ya CCM , Katibu wa CCM  wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu ameongozana na wanachama wa CCM wengine kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Irente na kuwakabidhi misaada  ya vitu mbalimbali.
 Katibu wa CCM  wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu akiwa ameongozana na baadhi ya wanachama wakikabidhi sehemu ya msaada huo kwa mmoja wa wawakilishi wa kituo hicho kulelea watoto yatima cha Irente ,wilayani Lushoto.
Baadhi ya Wanachama wa CCM wakiwa sambamba na  Katibu wa CCM  wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu wakiwafariji baadhi ya watoto waliopo kituoni hapo,aidha Muwakilishi wa kituo hicho cha Irente alieleza moja ya changamoto inayokikabili kituo hicho ni chakula,hivyo amewaomba Watanzania kusaidia chochote kile walichonacho kuhakikisha kituo hicho kinaendelea na kutoa huduma ya kuwatunza watoto hao walipo kituoni hapo. 
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images