Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI KIGWANGALLAH AWASHUKIA VIONGOZI WANAOTAKA KUFUTWA KWA MAENEO YA HIFADHI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza ) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa tatu ) wakiruka viunzi wakati walipotembelea jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (katikati) wakipatiwa maelezo na Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri ya Iringa, Wilberd Mtongani ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkoa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa tatu kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama (wa kwanza kushoto) wakipatiwa maelezo na Afisa mipango miji wa Halmashauri ya Iringa, Wicliph Benda ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Naibu Waziri wa Wizara Japhet Hasunga ( wa kwanza ) akiwa ameambtana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakiruka viunzi wakati alipotembelea jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.


NAIBU GAVANA BENKI KUU TANZANIA (BOT) AFUNGUA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UCHUMI NA FEDHA MKOANI MTWARA

$
0
0
ki01
Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) akifungua semina ya siku tano ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya Uchumi inayofanyika katika ukumbi wa BOT Mtwara., Waandishi wa habari watapata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu masuala ya uchumi, Kama vile Mabadiliko ya Mfumo mpya wa Kuandaa sera ya Fedha, Mapitio ya Maendeleo ya Uchumi nchini, Kikanda na Kimataifa BDuniani, Mifuko ya Dhamana kwa wajasiliamali na mengine mengi.

Akizungumza wakati akifungua semina hiy.Banzi  amewashukuru waandishi wa habari kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuandika habari za Benki Kuu kuhusu masuala ya uchumi, na pia akawaasa kuandika habari zinazohusu utekelezaji wa miradi mikubwa mbalimbali inayoendelea nchini ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), Miradi ya Umeme , Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda Mpaka Tanga nchini Tanzania na mingine mingi inayoendelea kutekelezwa.
ki5
Mkurugenzi wa BOT,Lucas Mwimo Tawi la Mtwara akimkaribisha  Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC),Julian Raphael Banzi ili kufungua semina hiyo.
7
Mwenyekiti wa Semina hiyo Bw. Ezekiel Kamwaga akitoa maelezo mafupi kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
12
Bw. Casmir Ndambalilo kutoka Idara ya Habari Maelezo akitaka ufafanuzi wa jambo katika semina hiyo kulia ni Goodluck Msola kutoka EFM.
ki2
Bw. Khalfan Said wa K-Vis Blog akifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya semina hiyo.

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Nchini Lesotho Yaja Kujifunza Tanzania

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akiwa katika picha na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kushoto) baada ya kumpokea katika uwanja wa ndege wa JNIA kwa ziara ya mafunzo hapa nchini. Katika ziara hiyo Mhe. Moramotse kaambatana na Katibu Mkuu wake, Mathabathe Hlalele.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akibadilishana kadi ya mawasiliano na baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Lesotho baada ya kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa JNIA kwa ziara ya mafunzo nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa JNIA mara baada ya kuwasili kwa ziara ya mafunzo hapa nchini

FUATILIA LIVE KUAGWA KWA MWILI WA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU VIWANJA VYA KAMRIJEE HIVI SASA

BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT), imesema vyombo vya habari nchini mchango wao ni muhimu zaidi ili kufikia azma ya uchumi wa viwanda huku ikisisitiza haja ya kuandikwa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya chumi, fedha na biashara.

Hayo yamesemwa leo mkoani Mtwara na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT),upande wa Utawala na Udhibiti wa Ndani, Julian Banzi wakati anafungua rasmi Semina kwa waandishi wa habari yenye lengo la kuwajengea uwezo katika kuandika na kuchambua masuala ya uchumi, biashara na fedha.

"Nafasi yenu ni muhimu, hivyo muitumie kwa ajili ya kusaidia nchi yetu.Ni vizuri badala ya kutumia muda mwingi kuandika mambo ambayo hayana uhusiano na uchumi, sasa mkajikita kutumia muda wenu mwingi kuandika mambo yanayohusu uchumi."Ujenzi wa reli unaendelea ni vema waandishi wakaandika,kuna mradi wa bomba la mafuta ni vema vyombo vya habari vikaandika.Kwa kupitia vyombo vya habari tunaamini wananchi watapata taarifa sahihi ya maendeleo yanayoendelea kufanyika nchini,"amesema Banzi.

Amefafanua BoT inafuatilia kwa karibu makala mbalimbali zinazohusu uchumi na hilo ni jambo jema kuendelea kufanywa na vyombo vya habari na ikiwezekana muda wa kuzungumzia masuala yanayohusu uchumi uongezeke zaidi.Banzi amesema wananchi wanahitaji kupata taarifa sahihi zinazohusu uchumi, hivyo ni jukumu la waandishi wa habari na vyombo vyao kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi ambazo hazitakuwa za upotoshaji.

"Mtakapoandika taarifa sahihi zinazohusu uchumi na majukumu ya BoT mtasaidia kupunguza maswali ambayo wakati mwingine wananchi wanajiuliza,"amesema Banzi.Ametoa mfano wapo watu ambao kazi yao nikukaa vijiweni na kujadili uchumi wakati wenyewe wanashindwa kuchangia kwenye huo uchumi.

"Wanakaa vijiweni na kisha wanauliza kama uchumi umepanda mbona mifukoni hakuna kitu.Ni jukumu la vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa zitakazohamasisha wananchi kushiriki kwenye maendeleo ya uchumi kwa kufanya kazi badala ya kukaa vijiweni wakilalamika,"amesema Banzi.

Amesisitiza ni vema vyombo vya habari vikaajenga matumaini kwa wananchi ili washiriki kwenye kuleta mandeleo nchini."Ombi letu ni kuona vyombo vya habari vinaandika makala nyingi kuhusu uchumi,biashara na fedha".Kuhusu semina hiyo,Banzi amesema BoT imedhamiria kuwajengea uwezo waandishi wa habari na sababu kubwa ni kuona taarifa ambazo zinaandikwa zinakuwa sahihi.

"Kupitia semina hii mtajifunza majukumu mbalimbali ya BoT.Najua mtajifunza mambo mengi na mbali ya mafunzo mtapata nafasi ya kufanya ziara kwenye maeneo ya kiuchumi mkoani Mtwara.Mtakwenda maeneo ya kuchaka gesi kwani hilo nalo ni eneo muhimu la kiuchumi,"amesema Banzi.Banzi ametoa angalizo kuwa pamoja na kuwepo kwa taarifa sahihi ambazo zinahusu uchumi bado kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa za kupotosha na matokeo yake BoT inalazimika kutumia nguvu nyingi kuzungumzia taarifa sahihi.

"Kuna wakati zinaandikwa habari ambazo zinakatisha tamaa kutokana na kuendelea kwa taarifa za uchokozi BoT tutaendelea kuwaelimisha waandishi wa habari,"amesema.

MWANAHABARI PATRICK MWILLONGO ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU

$
0
0
Ndugu wanahabari mwenzetu Patrick Mwillongo yupo hoi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambako amelazwa kwa matibabu.

Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha hashindwe kujimudu kufanya jambo lolote.

Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea
 na anafanya shughuli zake wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa na Kampuni ya New Habari.

Kwa atakayegusa kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba MPESA-0754362990, Tigo Pesa ni 0712727062.

Wanahabari Hellena Mwango, Careen , Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo wakiwa wamekaa nje ya jengo la Hospitali ya Mkoa Temeke wakitafakari namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika  kumjulia hali leo hii asubuhi.

MICHUZI TV: MZEE KINGUNGE AAGWA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR

MWANAHABARI PATRICK MWILLONGO ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU

$
0
0
Wanahabari Hellena Mwango, Careen , Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo wakiwa wamekaa nje ya jengo la Hospitali ya Mkoa Temeke wakitafakari namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika  kumjulia hali leo hii asubuhi.

Na Mwandishi Wetu

Ndugu wanahabari mwenzetu Patrick Mwillongo yupo hoi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambako amelazwa kwa matibabu.

Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha hashindwe kujimudu kufanya jambo lolote.

Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea
 na anafanya shughuli zake wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa na Kampuni ya New Habari.

Kwa atakayegusa kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba MPESA-0754362990, Tigo Pesa ni 0712727062.

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ALIYEPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA BILA KIBALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachiwa huru mfanyabiashara Abdullah Hauga (73) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Nolle Prosequi kuwasilisha chini ya kifungu cha sheria namba 91(1) cha mwenenendo wa makosa ya jinai kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Hauga.

Kabla ya kuachiwa, Mahakama ilitupilia mbali hati ya kuzuia ya dhamana ya DPP na  kisha kutoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa.Mbali ya Hauga mshtakiwa mwingine ni Mkurugenzi wa Meli ya Lucky Shipping, Issa Haji (39).

Mapema, Wakili wa Serikali, Salim Msemo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya uamuzi kuhusu DPP kuzuia dhamana kwa washtakiwa.Katika uamuzi wake, Hakimu Nongwa amesema alisikiliza hoja za pande zote mbili na pia amesoma uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ambayo imemuondolea DPP mamlaka ya kuzuia dhamana.

Hakimu Nongwa amesema Mahakama ya Rufaa ndio ya juu nchini, hivyo maamuzi yake lazima yaheshimiwe kwani kuzuia dhamana kwa washtakiwa ni kuwanyima haki.Amesema kibali cha DPP kimewasilishwa wakati Mahakama ya Rufaa nayo imetoa uamuzi kuhusu suala hilo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

LIVE: MAZISHI YA MZEE KINGUNGE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

WADAU HAKI JINAI WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUTOA HAKI KWA WAKATI

$
0
0

Na Mary Gwera, Mahakama

WADAU wa Haki Jinai nchini wameazimia kwa pamoja kukuza ushirikiano baina yao katika kushughulikia uhalifu wa makosa yanayovuka mipaka kuanzia eneo la Ukusanyaji wa taarifa, Upelelezi, Uendeshaji wa Mashtaka pamoja na Mashauri ya namna hiyo.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki iliyopita Februari 02, 2018 na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo katika mahojiano maalum mara baada ya kuhitimishwa kwa Kongamano la Wadau wa Haki Jinai lililofanyika katika Kituo kipya cha kisasa cha Mafunzo na Habari kilichopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

“Katika Kongamalo hilo ambalo lilihusisha Wadau mbalimbali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkemia Mkuu wa Serikali, Jeshi la Magereza, Wizara ya Katiba na Sheria na wengineo tumeazimia pia mamlaka zinazofanya upelelezi ziwe na Maabara za kufanyia Upelelezi wa Kisayansi ‘Forensic Science’ ili kuharakisha uendeshaji wa kesi na hatimaye haki iweze kupatikana kwa wakati,” alisema Mkuu wa Chuo huo ambaye pia alikuwa Mwezeshaji katika Mafunzo hayo.

Mhe. Kihwelo anasema kuwa kwa sasa wenye Maabara hizo ni Polisi pamoja na TAKUKURU, lakini wengine wote wanategemea Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, na kuongeza kuwa Tume ya Kupambana na Madawa ya Kulevya ipo kwenye mchakato wa kuanzisha Maabara yao ya uchunguzi.

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akifunga Kongamano la Wadau wa Haki Jinai lililofanyika katika Kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, katika maneno yake ya kufunga, Mhe. Jaji Wambali amewataka Wadau kuendeleza ushirikiano ili kuiwezesha Mahakama kutoa haki kwa wakati.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) (aliyesimama mwenye tai akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi juu ya Mafunzohayo kabla ya kufunga rasmi Kongamano hilo.
Mgeni rasmi, Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akikabidhi cheti cha Ushiriki kwa mmoja wa Washiriki wa Kongamano hilo, Mhe. Jaji Firmin Nyanda Matogolo.

RAIA WAWILI WA UINGEREZA KORTINI WAKITUHUMIWA KWA MASHTAKA TISA,YAMO YA KUISHI NCHINI BILA VIBALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

RAIA wawili wa Uingereza na Mkurugenzi Mkuu wa Afri Transport, wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka tisa yakiwamo ya kufanya Kazi, kuishi na kupata vibali mbali mbali kwa njia ya uongo.

Wamepandishwa kizimbani leo Mahakamani hapo ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa na majina ya washtakiwa hao ni Mohammed Mabeeenullah Kashmiri (72) na Saleem Kashmiri (50) ambao wanashtakiwa pamoja na Mtanzania Mohammed Ameenullah Kashmiri (82) .
Katika kesi hii Ammeenullah ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Afri Transport anashtakiwa kwa kosa la kuajiri raia hao wa Ungereza bila ya kibali na kuwasaidia kupata vibali baada ya kutoa vibali vya ufeki.

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka  Uhamiaji, Gerald Mardai amedai, Oktoba 25 mwaka jana, katika Makao Makuu ya ofisi za Uhamiaji Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam mshtakiwa Ameenullah, alikamatwa akitoa taarifa za uongo kwa ajili ya kuwapatia vibali raia hao wa Uingereza kufanya kazi nchini.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MATUKIO YA WAZIRI MKUU MAJALIWA BUNGENI LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mji Mkongwe, Ali Saleh kwenye viwanja via Bunge Mini Dodoma Februari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ileje, Janet Mbene kwenye viwanja vya Bunge Mini Dodoma Februari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Kiteto, Emmanuel Papian, Bungeni mjini Dodoma Februari 5, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, Bungeni mjini Dodoma Februari 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Ismani na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Bungeni mjini Dodoma Februari 5, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wawekezaji Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mkoani Manyara

$
0
0

Na: Frank Shija – MAELEZO, Babati,

Wawekezaji wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Mkoa wa Manyara badala ya kukimbilia katika maeneo ambayo yamezoeleka na wadau wengi wa maendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo Mjini Babati na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara alipokuta na ujumbe kutoka Bodi ya Filamu Tanzania ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bibi. Joyce Fissoo mape hii leo.

Kaimu Katibu Tawala huyo ameema kuwa Mkoa wa Manyara unazo fursa nyingi za uwekezaji hivyo ni vyema sasa wawekezaji wakatumia fursa hizo na kuja kuwekeza katika Nyanja tofautitofauti za uwekezaji ikiwemo kilimo, viwanda na ufugaji.

“ Mkoa wetu wa Manyara unazo fursa nyingi ambazo kama wawekezaji wakijitokeza watanufaika nazo, hivyo ni wito wangu kwao kuwa waje mkoani Manyara watumie fursa hizo, tunayo maeneo yakutosha kwa shughuli za uwekezaji”, alisema Kaimu Katibu Tawala huyo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo mbele ya mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Raymond Musa (katikati) mara baada ya kuwasilia katika Ofisi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Mama Fissoo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu. Kutoa kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage na Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa wa Mkoa Kennedy Kaganda.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akizungumza jambo alipokutana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) leo Ofisini kwake mjini Babati, Mkoani Manyara. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akisoma kwa makini nakala za Sheria ya Filamu na Kanuni zake mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) Ofisini kwake leo mjini Babati. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MZEE KINGUNGE

$
0
0
 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi akitoa heshima zake mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanasiasa mkongwe na kiongozi wa muda mrefu marehemu Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole mtoto wa kiume wa marehemu Kingunge anayefahamika kwa jina la Kinjekitile mara baada ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee.
 Baadhi ya viongozi wa kiserikali na chama wakiwa  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Kingunge Ngombale Mwiru
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati wa kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya viongozi wa kiserikali na chama wakiwa  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Kingunge Ngombale Mwiru
 Baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru wakiwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Kingunge Ngombale Mwiru


POLEPOLE AZINDUA MUONEKANO MPYA WA GAZETI LA UHURU LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uendezi Humphrey Polepole (wapili kushoto) akifurahia nakala ya gazeti la Uhuru baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Uhuru Publications Limited UPL), mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Said Nguba aliyewahi kuwa Mhariri Mtendaji wa UPL, na Wengine kutoka watatu kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero, Mhariri Mtendaji wa zamani wa UPL Jose[h Kulangwa na Kaim Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
MWANZO
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akifungua mfuko wenye gazerti la Uhuru, kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo leo. Kulia ni kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero na Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa zamani saidi Nguba
Polepole akionyesha furaha yake baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo la Uhuru
Mhariri Mtendaji wa zamani Joseph Kulangwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali wakifurahia nakala ya Uhuru lenye muonekano mpya baada ya kuzinduliwa muonekano huo
 Ndani ya chumba cha habari cha UPL wakati mjadala ukiendelea.

NI WAJIBU WA KILA MWANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA KAYA-GABRIEL

VIWANJA VYA NDEGE 11 NCHINI KUFANYIWA UPANUZI NA UKARABATI

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali imeanza majadiliano na Benki ya Dunia ili kupata mkopo wa kugharamia ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Ndege 11 kwa kuzingatia mapendekezo ya ripoti ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambao ulizingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukuaji wa shughuli za kiuchumi, utalii na mahitaji ya usafiri wa anga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Ndikiye leo Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tanga Mhe. Mussa Mbarouk lililohusu Ujenzi wa Uwanja wa Ndege mkubwa na wa kisasa katika jiji la Tanga.

Mhandisi Ndikiye amesema kuwa kiwanja cha ndege cha Tanga ni miongoni mwa viwanja hivyo 11 vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa kugharamiwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa Transport Sector Support Project (TSSP).

“Katika upembuzi huo kiwanja cha ndege cha Tanga ni miongoni mwa viwanja vilivyopewa kipaumbele kwa mahitaji ya ukaribu hivyo katika majadiliano ya awali Benki ya Dunia imeonesha nia ya kugharamia ukarabati wake.”

“Kwa sasa majadiliano kati ya Serikali na Benki ya Dunia yanaendelea yakiwemo mapitio ya awali ya ripoti za miradi iliyopendekezwa pamoja na maandalizi ya taarifa mbalimbali zinazohitajika kabla ya mkataba wa mkopo kusainiwa na baadaye kutangaza zabuni,” amefafanua Mhandisi Ndikiye.

Hata hivyo, Mhandisi Ndikiye alivitaja viwanja vingine vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu ikiwemo Lake Manyara, Musoma, Iringa, Songea, Kilwa Masoko, Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida ambapo usanifu huo ulimalizika mwezi June 2017 kwa kuhusisha usanifu wa miundombinu ya viwanja hivyo kwa ajili ya upanuzi na ukarabati ili kukidhi mahitaji ya sasa.

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI YA KUWAZAWADIA WATEJA WAO

$
0
0
Na Agness Francis -Globu ya jamii

KAMPUNI ya Simu za mkononi Airtel Tanzania imeamua kuzindua promosheni ya Yatosha Intanenti kwa wale wanaonunua vifurushi vya bando la Yatosha SMATIKA Intanenti.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo,leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoka Airtel Tanzania Isack Nchunda, amesema kampuni hiyo imeamua kutoa zawadi kwa wateja wake wanaotumia bando la SMATIKA Intanenti.

Kwani wamekuwa waaminifu kwao na wanaendelea kutoa hamasa ili kuendelea kumtumia huduma zao. Nchunda amesema promosheni hiyo ya Yatosha Intanenti itakuwa ni ya muda wa siku 30, ambapo kutakuwa na droo 3 za kila wiki kati ya siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa,

"Kwa ndroo ya kila siku wateja 1000 watajishindia bando ya Intanenti yenye 1 Gb kwa kila mmoja, wakati droo kubwa itakuwa na washindi 10,huku 5 wakijishindia simu za Smartphone na wengine 5 kujinyakulia modern,"amesema Nchunda.

Aidha Meneja Uhusiano Airtel Tanzania,Jackson Mmbando amewataka wateja wao kutokuwa na hofu katika mchakato mzima wa uwendeshaji wa promosheni hiyo. "Itakuwa ni promosheni ya wazi sana itasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha hapa nchini.Kila mteja atakaeshiriki moja kwa moja ataingia kwenye droo ya bahati na kuambiwa kuwa ameshinda au hajashinda"amesema Mmbando.
 Kushoto Meneja uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando na kulia ni Mkurugenzi Masoko Airtel Isack Nchunda  katika zoezi la uzinduzi Wa Promosheni ya SMATIKA Intanenti leo makao makuu ya Airtel Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Masoko Wa Airtel Tanzania Isack Nchunda  akizungumza na waandishi Wa Habari leo katika Makao makuu ya Airtel Jijini Dar es Salaam  kuhusu promosheni hiyo itakavyokuwa ikifanyika ili Kuibuka mshindi Katiba Bahati nasibu hiyo.
Meneja uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akizungumza na waandishi  Wa Habari  leo katika Makao makuu ya Airtel Jijini Dar es salaam kuhusu promosheni  hiyo iliyozinduliwa kama zawadi kwa wateja wake.
 

AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA

$
0
0
NAHODHA Msaidizi wa Azam FC,  Agrey Moris ameweka wazi kuwa hawatawaangusha mashabiki kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba.

Moris ametoa kauli hiyo ikiwa zimebaki  siku mbili kabla ya timu yao ua Azam FC kupambana na Simba.Mchezo huo utakafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ,keshokutwa saa 10 jioni.Ni mchezo unaotarajiwa kuwa mkali ya wa aina yake kutokana na Azam FC iliyojikusanyia pointi 33 kuwa kwenye vita kali ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo dhidi ya wekundu hao walio kileleni kwa pointi 38.

Akizungumzia kuelekea mchezo huo, Moris amewataka mashabiki kuondoa hofu na kuwaomba kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa sapoti.“Kwanza tunamshukuru Mungu wachezaji wako katika morali ya hali ya juu yaani inaonesha wachezaji kila mmoja anajiandaa kuhakikisha kutaka kushinda mchezo huu,” amesema.

Moris amekiri ushindani utakuwa mkubwa kutokana na Simba kuwa kileleni mwa ligi, na kudai kwa sasa timu yake imeongezewa morali kutokana na ushindi wa juzi walipoichapa Ndanda mabao 3-1.“Hiyo inatupa morali zaidi ya kwenda kupambana kwa sababu sisi lengo letu ni kushinda mchezo huu kujihakikishia tunaifukuzia Simba katika nafasi ya juu,” amesema.

Tayari kikosi cha Azam kimeshaanza maandalizi kuelekea mchezo huo na wachezaji wakiendelea kukaa kambini tokea ulipomalizika mtanange dhidi ya Ndanda, yote hiyo ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha inaibuka na pointi zote tatu.Aidha itakumbukwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex Septemba mwaka jana, timu hizo zilitoka suluhu.

Ushindi wowote wa Azam FC kwenye mchezo huo, utazidi kupunguza pengo la pointi baina yake na Simba na kufikia mbili na hivyo kuendeleza mapambano ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo, walioutwaa mara ya mwisho msimu wa 2013/2014.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>