Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109992 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA ATEMBELEA ENEO LINALOTARAJIWA KUEKEZWA NDANI YA MKOA WAKE

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Omar Khamis Othman (kati) akimsikiliza afisa kutoka Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) zone ya Pemba, Nd. Ali Shaaban Suleiman akitoa ufafanuzi wa maeneo yanayotegemewa kuwekezwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi. Salama Mbarouk Khatib akimkaguza   Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Omar Khamis Othman katika eneo linalotarajiwa kuwekezwa Hoteli kubwa ya kitalii eneo la Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Eneo la fukwe Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba linalotarajiwa kuekezwa.
Picha na Mwamize Muhammed Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pemba.

BREAKING: WAZIRI MPINA AKAMATA MELI YA MALAYSIA IKIFANYA UVUVI HARAMU, AWAPA WAMILIKI SIKU SABA KULIPA FAINI MILIONI 770/-

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekamata meli ya uvuvi mali ya Kampuni ya Buah Naga 1 ya nchini Malaysia na kuitoza faini ya Dola za kimarekani 350,000 sawa na Sh.milioni 770 kwa kosa la kukutwa na mapezi ya samaki aina ya papa yenye uzito wa kilo 90 bila miili yake.

Ambapo hiyo ni kinyume cha Kanuni ya 66 ya kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.

Meli hiyo ilikamatwa Januari 26 mwaka huu baada ya kufanyika ukaguzi uliosimamiwa na kikosi maalum cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao yake wakati ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara.Pamoja na kukutwa na mapezi hayo ya papa, meli hiyo ilikutwa pia na bastola aina ya Bereta ikiwa na risasi 10 bila ya kuwa na nyaraka za umiliki wake.

Akizungumza mjini Mtwara ambako meli hiyo ndiko inakoshikiliwa na Serikali Waziri Mpina ameagiza fedha hizo zilipwe ndani ya siku saba huku akitoa onyo kali kwa wamiliki wa meli waliopewa leseni za uvuvi wa Bahari kuu kufuata masharti ya vibali vyao na katika zama hizi za utawala wa Rais, Dk.John Magufuli watachukuliwa hatua kali zaidi.

"Enzi za Serikali ya Awamu Tano ya Rais Magufuli mtakaguliwa na kupekuliwa kuliko wakati wowote, hivyo ni vizuri mkatii sheria za nchi kwa mujibu wa leseni zenu,"amesema Mpina huku akisilizwa na Kapteni wa meli hiyo Han Ming Chuan  raia wa Taiwan.

Mpina amesema meli hizo zimekuwa zikitumika pia kufadhili biashara nyingine haramu ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya ,usafirishaji haramu wa  binadamu na biashara ya silaha.Pia zinatumika kutorosha nyara za Serikali ikiwemo meno ya tembo, samaki na madini.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Francis Mkuti wakionesha baadhi ya Samaki waliovuliwa na Meli hiyo.
 Hosea Mbilonyi Kaim Mkurugenz mamlaka ya Usimamiz wa Bahari Kuu  DFSA akimuonesha waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina shehena ya Samaki  tani 4.5 wasiotakiwa kuvuliwa ambao wanatakiwa Kupigwa Mnada Siku Yoyote.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akilekea katika Meli Buah Naga one kukagua Samaki walivuliwa kinyume na Taratibu

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWS ALERT: RAIS DKT MAGUFULI ATEUA MWANASHERIA MKUU NA NAIBU WAKE WAPYA

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi

MAGAZETI YA IJUMAA LEO FEBRUARY 2,2018

BREAKING: MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU HATUNAYE TENA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
 MWANASIASA mkongwe na maarufu nchini Tanzania mzee Kingunge Ngombale-Mwiru(87), amefariki dunia,akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu. 

Akizungumza na Michuzi Blog asubuhi hii kuhusu taarifa za kifo cha mzee Kingunge ,rafiki wa mkubwa na wakaribu wa mtoto wa Kinje, Abdull Msembo amesema ni kweli amefariki saa 9:30 ya alfajiri ya leo akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. 


"Ni kweli mzee wetu amefariki saa 9:30 alfajiri ya kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu.Taarifa rasmi itatolewa kuhusu taratibu nyingine lakini kwa sasa tunaendelea na kikao na kisha tutaufahamisha umma. 

 "Msiba uko nyumbani kwake kwa Kingunge Victoria jijini Dar es Salaam.Kadri muda utakavyokuwa unakwenda tutaendelea kufahamisha.Mzee wetu hatunaye tena,"amesema Msembo wakati anaelezea taarifa za kifo cha Mzee Kingunge ambazo zilianza kusambaa tangu mapema ya leo kwenye mitandao ya kijamii. 

 Kabla ya kukutwa na umauti Januari mwanzoni Mzee Kingunge alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa majeraha yaliyotokana na kuumwa na mbwa nyumbani kwake na akafanyiwa upasuaji. Na wakati anaendelea kupatiwa matibabu, mke wake Peras alifariki dunia mwezi uliopita. 

KINGUNGE MWANASIASA MWENYE HISTORIA Mzee Kingunge enzi za uhai wake katika harakati zake za kisiasa alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Ameitumikia CCM na Serikali kwa kipindi kirefu na miongoni mwa wanasiasa wenye historia ndefu nchini. Pamoja na kuwa CCM kwa muda mrefu, wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Kingunge aliamua kuondoka CCM na kisha akatangaza kumuunga mkono Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye naye aliondoka CCM na kujiunga Chadema na kisha kupata fursa ya kuogombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa). 
 Wakati anaondoka CCM alitoa sababu nyingi lakini kubwa alidai kuwa kinachomuondoa aliona kuna ukiukwaji wa Katiba ya chama hicho. 

 ALIAHIDI KUTOHAMA CCM 
 Hata hivyo mzee Kingunge baada ya kujiweka kando na masuala ya kiasisa tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, alikuwa kimya na historia inaonesha kuwa amekuwa CCM tangu ilipoanzishwa mwaka 1977. Kutokana na historia yake na CCM, siku za karibuni Rais ,Dk.John Magufuli alikwenda kumjulia hali mzee Kingunge alipokuwa amelazwa Muhimbili akiwa Wodi ya Mwaisela ambapo alitumia nafasi hiyo kumueleza Rais kuwa bado anaipenda sana CCM.

SPIKA NDUGAI AMLILIA MAREHEMU MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru kufuatia kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 2 Februari 2018, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.


“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, natoa pole kwa familia ya  marehemu na Watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza mwanasiasa Mkongwe katika nchi hii ambaye licha ya kuwahi kuwa Mbunge lakini pia ameitumikia Serikali katika nyadhifa mbalimbali,” alisema.


“Binafsi nilifanya kazi kwa karibu na Mzee Kingunge wakati wa Bunge letu na pia kwenye Bunge la Katiba ambapo tulikuwa wote kamati namba nane nikiwa Mwenyekiti wake, mchango wake ulitusaidia sana”aliongeza Mheshimiwa  Spika.


Mheshimiwa Spika amemuomba Mwenyezi Mungu awape subira, nguvu na faraja familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mpendwa wao.


 Imetolewa na:     Ofisi ya Spika

S.L.P. 941


DODOMA

Dr. Jane Goodall t hold live video screening in Dar es salaam on Monday

SOGA ZA DIASPORA | S01E04 - Mahojiano na Ben Pol na Swebbe Santana


TANZIA: MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU AFARIKI DUNIA, RAIS DKT MAGUFULI AOMBOLEZA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWANASIASA mkongwe na maarufu nchini Tanzania mzee Kingunge Ngombale-Mwiru(87), amefariki dunia,akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Michuzi Blog asubuhi hii kuhusu taarifa za kifo cha mzee Kingunge ,rafiki wa mkubwa na wakaribu wa mtoto wa Kinje, Abdull Nsembo amesema ni kweli amefariki saa 9:30 ya alfajiri ya leo akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

"Ni kweli mzee wetu amefariki saa 9:30 alfajiri ya kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu.Taarifa rasmi itatolea kuhusu taratibu nyingine lakini kwa sasa tunaendelea na kikao na kisha tutaufahamisha umma.

"Msiba uko nyumbani kwake mtaa wa Kingunge Victoria jijini Dar es Salaam. Kadri muda utakavyokuwa unakwenda tutaendelea kufahamisha. Mzee wetu hatunaye tena,"amesema Msembo wakati anaelezea taarifa za kifo cha Mzee Kingunge ambazo zilianza kusambaa tangu mapema ya leo kwenye mitandao ya kijamii.

Kabla ya kukutwa na umauti Januari mwanzoni Mzee Kingunge alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa majeraha yaliyotokana na kuumbwa na mbwa nyumbani kwake na akafanyiwa upasuaji.

Hata hivyo wakati anaendelea kupatiwa matibabu,mke wake Peras  alifariki dunia mwezi uliopita.

KINGUNGE MWANASIASA MWENYE HISTORIA

Mzee Kingunge enzi za uhai wake katika harakati zake za kisiasa alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM).Ameitumikia CCM na Serikali kwa kipindi kirefu na miongoni mwa wanasiasa wenye historia ndefu nchini.

Pamoja na kuwa CCM kwa muda mrefu, wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Kingunge aliamua kuondoka CCM na kisha akatangaza kumuunga mkono Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye naye aliondoka CCM na kujiunga Chadema na kisha kupata fursa ya kuogombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa).

Wakati anaondoka CCM alitoa sababu nyingi lakini kubwa alidai kuwa kinachomuondoa aliona kuna ukiukwaji wa Katiba ya chama hicho.

ALIAHIDI KUTOHAMA CCM

Hata hivyo mzee Kingunge baada ya kujiweka kando na masuala ya kiasisa tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, alikuwa kimya na historia inaonesha kuwa amekuwa CCM tangu ilipoanzishwa mwaka 1977.

Kutokana na historia yake na CCM, siku za karibuni Rais ,Dk.John Magufuli alikwenda kumjulia hali mzee Kingunge alipokuwa amelazwa Muhimbili akiwa Wodi ya Mwaisela ambapo alitumia nafasi hiyo kumueleza Rais kuwa bado anaipenda sana CCM.

MAHAKAMA YAAMBIWA AFYA MMILIKI IPTL, RUGEMARILA ZINA MASHAKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa afya ya mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila zinaendelea kuwa za mashaka.

Hayo yameelezwa leo mapema na Wakili wa utetezi, Respicius Didas baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya kizuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Leornad Swai kudai kuwa upelelezi katika  kesi hiyo bado haujakamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi Wakili Swai ameomba kesi hiyo iahirishwe na kwamba walienda Magereza kuchukua maelezo ya Seth lakini ilishindika kwa sababu afya yake haikuwa nzuri.

Kutokana na taarifa hiyo, Wakili Didas alidai kuwa wakati afya za washtakiwa zikiendelea kuwa za mashaka wanauomba upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi.

Amesema ni vema kila kesi hii inapoahirishwa baada ya siku 14 kuwe na kitu kipya kuhusu hatua zilizochukuliwa, lakini inavyoonekana upande wa mashtaka unachukulia kawaida kuahirishwa kwa kesi hiyo.

"Upande wa mashtaka unacheza na mamlaka, utambue hali za washtakiwa ni mbaya, hivyo ukamilishe upelelezi" amesema Wakili Didas.

Swai alidai, Serikali inajitahidi kuangalia afya za washtakiwa kwani hata mara ya mwisho Serikali ilizungumzia afya ya Seth ambaye alidai anataka madaktari wake wawepo wakati akifanyiwa upasuaji.

Kuhusu upelelezi, Swai amedai ni kweli unachukua muda mrefu ila upo katika hatua za mwisho na kitu kinachochelewesha ni upelelezi mwingine kuwa nje ya nchi (Malysia)

Mshtakiwa Rugemarila aliieleza Mahakama kuwa hajawahi kupelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, pia anahisi ana Cancer kwa sababu ya uvimbe alionao, pia Swai amesema daktari wake alisema hana cancer, "anabahati amefiwa angekuja Mahakamani kusema kwamba nina cancer,"

Hakimu Shaidi amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri wakatibiwe nje ya nchi na alishatoa amri kwamba watibiwe Muhimbili na kama inahitajika wakatibiwe nje ya nchi serikali ndio itasimamia. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 16, mwaka huu

Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.

NYUMBA INAUZWA IPO CHAMAZI SAKU DAR ES SALAAM, TANZANIA

$
0
0
Nyumba inauzwa mil.30 Eneo la Chamazi Saku, Wilaya ya Temeke,Dar es Salaam Ina Vyumba 3 ,Jiko na stoo yake (Food pantry), sitting room, Dinning, vyumba viwili ni master bedroom pia Kuna common bath na toilet na eneo dogo lina baki kwa ajili ya ku park gari kwa anayehitaji kupaona awasiliane na Ndugu Duke Gervalius Tel +255 767 111 020 na kama upo USA piga simu 210 784 9204
Kiwanja kina ukubwa wa Square Fit 70 urefu na Square Fit 60 upana

Kina Hati ya Mauziano ya serikali ya kijiji/mtaa pia Risiti za TRA zipo kinalipiwa kila mwaka Leseni ya makazi.Hivyo mnunuzi atanzia hapo kufatilia kupima kiwanja ofisi za Ardhi.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge  akiongoza kikao cha nne cha mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Nyongo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa kikao cha nne cha cha mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha nne cha cha mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Iringa Mhe.Rose Tweve akiuliza swali wakati wa kikao cha nne cha cha mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Stella Manyanya akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha nne cha cha mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Ester Bulaya wakati wa kikao cha nne cha cha mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Mjini Dodoma.


Picha zote na Daudi Manongi, MAELEZO,DODOMA.

Kumbukumbu ya Kifo cha marehemu mama yetu mpendwa Joyce Bartlett Kallaghe

$
0
0
Ni mwaka moja umepita tokea ulipotuacha. Tokea ulipotoweka hakuna siku inayopita ambapo haupo katika mioyo na akili zetu. Enzi za uzima wako matendo yako yaligusa mioyo mingi kwa namna ya kipekee ambayo Wewe tu uliweza. 

Roho yako ya huruma bado ipo pamoja nasi na mara kwa mara hugusa mioyo na akili zetu na kutupa sababu ya kutabasamu. Umejitwalia nafasi yako miongoni mwa nyota za mbinguni na shime ung’ae milele. Unakumbukwa sana na kila mtu hapa duniani. Ulitoweka kwa uchungu sana bila  hata ya kutuaga. 

Tunakufikiria sana kimyakimya. Hakuna jicho linaloweza kutushuhudia tukiomboleza, ila machozi mengi yanatiririka ndani kwa ndani. Tunafarijika kwa kutambua kuwa ipo siku tutakutana na Wewe tena. Unakumbukwa sana na watoto, wakwe na wajukuu wako.

Familia ya Marehemu Balozi Cecil A Kallaghe inawaalika ndugu na marafiki wote katika Misa ya Kumbukumbu tarehe 3 Februari 2018 itakayofanyika katika kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano Dar es Salaam saa 2 asubuhi. Mkesha utafanyika nyumbani Mbezi Temboni tarehe 2 Februari 2018. 

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema maboresho ya TEHAMA yanayofanywa na mhimili wa mahakama nchini utasaidia kupunguza foleni za wananchi wanaofika ofisi za Wakuu wa Wilaya na kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta haki zao.

Amesema kuwa kitendo cha mwaanchi kuweza kujua mwenendo wa kesi bila ya kufika mahakamani ni maendeleo makubwa yanayofikiwa na mhimili huo na kuwaasa kuanza kufanya kazi baada ya kuwa likizo ya mwisho wa mwaka.

Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo hufanyika tarehe 1, Februari ya kila mwaka katika Viwanja wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi.

“Mwaka 2018 na jitihada zilizofanyika na mahakama umekuwa mwanzo mzuri, wananchi watajitokeza kutafuta elimu hii ya sheria na wanapoipata itatupunguzia msongamano kwenye ofisi zetu za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ili tufanye kazi za maendeleo sio kusuluhisha migogo ya ndoa, mirathi na ardhi ambayo yote imekaa katika misingi ya kisheria,” Alieleza.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria  yaliyofanyika katika Viwanja wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo  (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga John Mgeta (wa kwanza kushoto) na Jaji Mkuu  wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga  Dk. Adam Mambi  (wa pili kutoka kulia) na Mwanasheria wa Serikali mkoa wa Rukwa Prosper Regerera. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo  akisalimiana na  Jaji Mkuu   wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga  Dk. Adam Mambi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Kampuni ya Total wamekubaliana kuharakisha hatua zote za awali katika Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima Tanga ili shughuli za ujenzi rasmi zianze mwezi Mei mwaka huu.
Makubaliano hayo yalifikiwa Alhamisi, Februari 1, wakati Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alipokutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo wizarani Dodoma.
Aidha, makubaliano mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwa kazi za awali za maandalizi ya ujenzi ziwe zimekamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
“Ni lazima tuharakishe mchakato huu kama Mheshimiwa Rais Magufuli alivyoagiza. Hivyo, tumekubaliana kwamba shughuli zote za maandalizi ziwe zimekamilika ifikapo Machi mwaka huu ili kuwezesha shughuli rasmi za ujenzi wa Bomba kuanza mwezi Mei,” alifafanua Waziri Kalemani.
Vilevile, katika kikao hicho, Rais wa Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy Maurice ambaye alikuwa kiongozi wa Ujumbe huo, alibainisha nia ya kampuni yake kuwekeza katika shughuli nyingine mbalimbali zinazohusiana na Mradi wa Bomba jambo ambalo alisema litainufaisha zaidi Tanzania.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akiongoza kikao baina ya viongozi na wataalam wa Wizara (kulia) na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total (kushoto). Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy Maurice (kulia) wakati wa kikao baina yao kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.
 Viongozi na wataalam wa Wizara ya Nishati, wakiwa katika kikao baina ya Wizara na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Ujumbe kutoka Kampuni ya Total wakiwa katika kikao baina yao na Viongozi na wataalam wa Wizara ya Nishati kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).

MAKALA MAALUM YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

RC MAKONDA AKOSHWA KASI YA UJENZI OFISI ZA MAKAO MAKUU BAKWATA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ambapo amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo.

Ujenzi wa jengo hilo la kisasa ni jitiada za RC Makonda kuthamini na !kuwapa heshima Viongozi wa Dini kwa kuhakikisha wanafanyakazi katika mazingira mazuri na yenye hadhi kutokana na thamani na mchango wao mkubwa katika jamii. 

Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Nne pamoja na Ground floor lina Ofisi ya Mufti wa Tanzania, Ofisi ya katibu, VIP room, kumbi za mikutano, Ofisi za wafanyakazi, ofisi za mshauri,Jiko,Vyoo, sehemu ya Kufanya Dua pamoja sehemu ya Mapokezi. 

RC Makonda amesema kazi wanayofanya Viongozi wa Dini ni kubwa hivyo tunapaswa kuthamini kwa kuwaweka mazingira mazuri ya kufanya kazi. Aidha RC Makonda amesema shauku yake ni kuona hadi mwezi wa Ramadhani jengo linakuwa limekamilika na kuanza kutumika. Aidha RC Makonda amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Amani Taifa na viongozi wake.
Kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber amemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea jengo hilo na kusema katika Miaka 50 BAKWATA haijawahi kuwa na jengo zuri na lakisasa Kama hilo hivyo RC Makonda anaweka historia ya kwanza.

Mufti amesema jengo lililokuwepo lilikuwa likiwafanya kuona hata haibu hata kupokea ugeni wa viongozi wa kislamu ulimwenguni.Katika ziara hiyo Viongizi wa Dini kwa pamoja wamemuombea Dua RC Makonda pamoja na Rais Dr. John Magufuli kwa kuwezesha kujengwa kwa msikiti wa Mfalme wa Morocco wenye uwezo wa kuchukuwa watu 8,000 ampapo ujenzi unaendelea. 

UJENZI STENDI KUBWA YA KISASA DODOMA KUANZA MACHI, NI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi

UJENZI wa stendi ya mabasi kubwa na ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma unatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi mwaka huu katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

Jumla ekari 50 zimetengwa katika eneo hilo lililopo mashariki mwa Mji barabra ya Dodoma-Dar es Salaam, ambapo ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kukamilika baada ya kipindi cha miei 24.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika Mjini hapa kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali za kimaendeleo zilizotekelezwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 kinachoanzia Mwezi Septemba hadi Desemba 2018.

Kunambi aliwaambia wajumbe wa Mkutano huo kuwa, stendi hiyo ni kubwa na ya kisasa yenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi, na kwamba itakuwa ya mfano kwa Nchi zote za ukanda wa afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana. Wa pili kushoto ni Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe akiteta jambo na Naibu Meya Jumanne Ngede. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Wageni waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana.

DC SHINYANGA AKABIDHI HUNDI ZA MIKOPO MIL 25 VIKUNDI VYA VIJANA,WANAWAKE

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Fedha hizo zinatokana na asilimia 10 ya makusanyo kutoka katika vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai 2o17 hadi Disemba 2017.

Vikundi vilivyokabidhiwa hundi ni kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule na vikundi vya vijana vya Umoja wa bodaboda, Jikwamue, Shukrani Group vilivyopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akikabidhi hundi hizo kwa wawakilishi wa vikundi hivyo leo Ijumaa Februari katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo,Matiro aliwataka walionufaika na mikopo hiyo watumie pesa walizopata kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Kila mtu aliyepata pesa akafanye kile alichokusudia kufanya, serikali inajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo ili mjikwamue kiuchumi,naomba mfanye kazi kwa bidii ili kubadilisha maisha yenu”,alieleza Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza vijana na wanawake waliopata mikopo kutumia fedha walizopata kwa malengo waliyokusudia. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Bakari Kasinyo Mohammed. Kulia ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira.

Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 5,000,000/= kwa Joyce Charles aliyewakilisha Kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kata Didia chenye wanufaika watano kinachojihusisha na utengenezaji wa sabuni.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 6,800,000/= kwa Majaliwa Kihangaji aliyewakilisha kikundi cha Umoja wa Bodaboda kinachojihusisha na ubebaji wa abiria kwa pikipiki kilichopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia chenye wanufaika 60.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 10,250,000/= kwa Methusela Jackson kutoka kikundi cha Jikwamue kilichopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia chenye wanufaika 20 kinachojihusha na ufyatuaji wa matofali ya saruji.

Viewing all 109992 articles
Browse latest View live


Latest Images