Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live

WAKAZI ELFU 16 KONDOA VIJIJINI WAONDOKANA NA KERO YA MAJI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Kondoa

ZAIDI ya wakazi elfu 16 wa vijiji vitatu vya Mauno, Makiranya na Kinyasi-Majengo, katika Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma wameondokana na adha ya kukosa maji baada ya kuzinduliwa kwa visima viatu vya maji vilivyojengwa kwa msaada wa wahisani kutoka nchini Uturuki kupitia ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa visima hivyo katika Kijiji cha Mauno, Kata ya Bumbuta, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini Dokta Ashatu Kijaji, amesema kuwa kuzinduliwa kwa visima hivyo kunalifanya jimbo lake lifikishe visima 41 hatua ambayo amesema itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika jimbo lake.

Dkt. Kijaji ameushukuru Ubalozi wa Uturuki kwa kuratibu msaada huo wa zaidi ya Dola za Kimarekani elfu 36, sawa na shilingi milioni 81, zilizotumika kuchimba visima hivyo pamoja na kuweka miundombinu mingine zikiwemo jenereta zinazotumika kusukuma maji hayo na kuwezesha upatikanaji wa maji hayo.

“Hivi sasa ujenzi wa visima 15 kati ya 25 vinavyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji unaendelea huku wahisani wakiwa wametujengea visima 36 hivyo kufikisha idadi ya visima 61 katika kipindi cha miaka miwili tu tangu Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aingie madarakani hali ambayo haijawahi kutokea na lengo letu ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote 84 vinapatiwa huduma ya maji ifikapo mwaka 2020” Alisisitiza Dkt. Kijaji
Mmoja wa akina mama wa kijiji cha Mauno, Kata ya Bumbuta, Jimbo la Kondoa Vijijini akiongea na vyombo vya habari kuhusu furaha yao baada ya kisima cha maji kuzinduliwa hatua iliyowaondolea kero ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, na Mbunge wa Jimbo la KOndoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa mradi wa kisima cha maji pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na viongozi wa dini katika kijiji cha Mauno, wilayani Kondoa.
Wanakijiji wa Kijiji cha Mauno Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakichota maji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
Wanakijiji wa Kijiji cha Mauno Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakichota maji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
Wakazi wa kijiji cha Mauno wakiwa wamemwangusha ng’ombe kwa ajili ya kupata kitoweo ikiwa ni namna ya kujipongeza na kusherehekea baada ya kuzinduliwa kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango.



KLABU YA SINGIDA UNITED YAMSIMAMISHA MSHAMBULIAJI WAKE MUDA USIOJULIKANA

$
0
0
Na Zaynab Nyamka 

KLABU ya Singida United imemsimamisha kwa muda usiojulikana mshambuliaji wake raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kambale Salita Gentil kwa utovu wa nidhamu.

Taarifa ya Singida United iliyotolewa leo, kwa vyombo vya habari imesema kwa utovu nidhamu alioufanya Kambale jana kwenye mchezo wa hatua ya 32 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) anasimamishwa mara moja.

Kambale alimpiga ngumi mchezaji wa Green Warriors kipindi cha kwanza na kutolewa kwa kadi  nyekundu, hivyo kuiachia mzigo timu wa kucheza pungufu katika sehemu kubwa ya mchezo.Hata hivyo, Singida United ilishinda kwa penalti 4-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 na kusonga mbele hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

UONGOZI WA CCM MKOA WA PWANI WALAANI VIKALI VITENDO VYA WATU WANAOHUJUMU ZAO LA KOROSHO

$
0
0
VICTOR MASANGU-PWANI

SAKATA la kuhujumu zao la korosho linalofanywa na baadhi ya wanunuzi,wakulima,pamoja na viongozi wa vyama vya ushirika hatimaye limechukua sura mpya baada ya uongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kuamua kuliingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwabaini wale wote ambao wanahusika kwa namna moja au nyingine ili waweze kuchukulia hatua kali za kisheria.

Uamuzi huo wa CCM mkoa wa Pwani umekuja kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kuibuka vikundi vya watu wachache ambao wana lengo la kukwamisha juhudi za serikali ya awamu ya tano kutokana na kuamua kufanya vitendo vya kuhujumu zao hilo kwa kuweka mawe,michanga, na takataka katika magunia ya korosho kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

Akizungumza katika ziara ya kushitukiza katika ofisi za Chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya jambo hilo Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa Ramadhani Maneno alisema kuwa suala hilo limemchukiza sana hivyo hawezi kulifumbia macho na atalivalia njuga kwa lengo la kuweza kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kupambana na watu ambao ni wezi na mafisadi.

“Sisi kama chama cha CCM mkoa wa Pwani tumeamua kuja hapa kwa ajili ya kupata maelekezo juu ya suala hili la baadhi ya watu ambao wanahujumu zao la korosho kwa kweli na kwa kuwa tunatelekeza ilani ya chama kwa kweli hatuwezi kulivumilia tutahakikisha tunashirikiana na vyombo vya dola katika kulifanyia kazi suala hili la kuwapata wale ambao wanajihusisha,”alisema Maneno.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa chama kikuu cha ushirika (CORECU) hawapo pichani baada ya kufanya ziara katika ofisi zao kupata taarifa ya baadhi ya watu wanaohujumu zao la korosho.
Mwenyekiti wa chama kikuu vha ushirikika Mkoa wa Pwani (COORECU) Rajab Ng’onoma akitoa ufafanuzi kwa viongozi wa CCM Mkoa wa Pwani kuhusiana na mwenendo mzima wa zao la korosho pamoja na changamoto amabzo zinawakabili katika utendaji wao wa kazi.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya CORECU wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani mara baada ya kumalizika kwa kutano wa kujadili masuala mbali mbali ya zoa la korosho.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU.


KAMISHNA MKUU KICHERE AWATAKA WAFANYAKAZI SIRARI KUENDELEA NA UTOZAJI WA KODI STAHIKI

$
0
0
Na: Veronica Kazimoto-Sirari

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere amewataka Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali wakiwemo wa mamlaka hiyo wanaofanya kazi katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja cha Sirari kilichopo wilaya ya Tarime mkoani Mara kufanya kazi kwa ushirikiano na kuhakikisha wanaendelea kutoza kodi stahiki.

Akizungumza wakati wa ziara yake kituoni hapo, Kamishna Mkuu Kichere alisema nchi inaendeshwa kwa kodi za ndani hivyo ni muhimu kila taasisi iliyopo eneo hilo kutimiza wajibu wake katika suala zima la ukusanyaji wa kodi.

“Wote mnajua umuhimu wa kodi na pia mnafahamu kuwa, kwa kupitia kodi hizi, Serikali inajenga miundombinu ya barabara, umeme, inasomesha wanafunzi, inajenga shule, inalipa mishahara ya wafanyakazi wake na mambo megine mengi. Hivyo, mfanye kazi kwa bidii na kwa weledi ili mkusanye kodi inayotakiwa kukusanywa kwa mujibu wa sheria bila kumuonea mtu yeyote.” alisema Kichere.

Kichere aliongeza kuwa, wafanyakazi wote kituoni hapo wana wajibu wa kukusanya kodi ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo kwa kutumia mapato yanayokusanywa nchini kupitia kodi mbalimbali.Aidha, Kamishna Mkuu huyo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tarime kwa ushirikiano wanaoutoa kwa TRA.

Klabu za Fema Hip zasema "Ukatili wa kijinsia sasa Basi"B

$
0
0

Kongamano la kumi la Fema Clubs kutoka kote nchini limemalizika leo jijini Dar es Salaam likiwa limekutanisha wanafunzi zaidi ya mia moja pamoja na walimu wao. Hawa ni wawakilishi kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Hili ni tukio ambalo shirika la Femina Hip hulifanya kila mwaka kama sehemu ya kuwaongezea uwezo vijana wanachama wa Clubs za Fema na pia walimu wao walezi, katika kutekeleza azma ya kuleta mabadiliko ya tabia na kujenga kizazi kinachozingatia mitindo bora ya maisha.

Kila mwaka kongamano huongozwa na mada maalum, na kwa mwaka huu kauli mbiu ni Ukatili wa Kijinsia Sasa Basi. Kauli mbiu hii inaakisi mkazo unaowekwa na shirika pamoja na wadau wake kupambana na matukio na tabia ambazo huwaumiza watu kwa sababu ya jinsi zao. 

Toleo jipya la jarida la Fema limesheheni simulizi za kweli na uzoefu wa watu ambao ama walifanya ukatili au walifanyiwa, lakini sasa wanasimama na kutuhimiza sote kuukataa ukatili wa kijinsia. Toleo hili lilizalishwa pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo UNICEF, CDF na Plan International, na kama anavyosema Mkurugenzi Mkuu wa Femina Hip, Dr Minou Fuglesang, “Juhudi zetu hizi ni sambamba na juhudi za serikali kutokomeza ukatili dhidi ya wananawake na watoto kama zilivyoainishwa katika mpango wa kitaifa uliozinduliwa mwaka jana.”

Mafunzo na mijadala ambayo ilifanyika wakati wa kongamano hili ililenga kuwaandaa wana Fema Club kuwa vinara wa mabadiliko, kuongoza mchakato muhimu wa kuelimisha jamii zao na kuhamasisha tabia zinazopingana na ukatili huu.

Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa mwalimu Kahwa Mpunami wa Misungwi High ambao wameshinda (BEST FEMA CLUB OF THE YEAR 2017) Klabu Bora ya mwaka 2017 kutoka shule ya sekondari ya Myunzi Korogwe Tanga baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika kongamano la kujadili namna ya kupunguza ukatili wa Kijinsia kwa watoto wa kike likiwa na kauli mbiu ya "Ukatili wa Kijinsia sasa BASI" na kushirikisha Klabu mbalimbali za FEMA kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania , Kongamano limemalizika leo na lilikuwa likifanyika kwenye hoteli ya Seascape Mbezi Beach jijini Dar es salaam kwa siku nne mfurulizo, Kongamano hilo limehusisha pia mafunzo ya mambo mbalimbali. , Katika picha anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa Mayombo Lutego ambaye ameshinda (BEST FEMA CLUB MENTOR OF THE YEAR 2017) .kutoka shule ya Sekondari ya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Upendo Abisai kutokamwanachama wa Youth For Change Project uliopo chini ya Plan International Tanzania akitoa mada katika kongamano hilo kutoka kushoto ni watoa mada wengine Lydia Charles Mtangazaji wa Kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show, Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig, Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip na Koshuma Mtengeti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childrens Dignity Forum (CDF)

Baadhi ya wanafunzi shule mbalimbali za sekondari nchini kutoka klabu za Fema Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.

MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI

$
0
0
Na Stella Kalinga-Simiyu

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeshauriwa kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo viatu, mikoba na mikanda kinachomilikiwa na kikundi cha Usindikaji Ngozi Senani kilicho kata ya Senani wilayani Maswa, ili kuongeza thamani ya ngozi zitokanazo na mifugo.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo katika wilaya MASWA.

Mtaka amesema katika kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda , Halmashauri ya Maswa inapaswa kuwekeza katika viwanda vinavyoanzishwa na vikundi ili kuviwezesha katika upatikanaji wa malighafi ya kutosha, kuongeza thamani ya mazao ya mifugo pamoja na kilimo ili viwanda hivyo viweze kuzalisha kwa tija.

“Tungehitaji kuwa mkoa ambao utawekeza sana katika viwanda vidogo na ndiyo maana tulianza dhana ya Wilaya moja bidhaa moja kiwanda kimoja na sasa tunakwenda kwenye Kijiji Kimoja Bidhaa Moja Kiwanda kimoja; tunataka kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya Mkoa” alisema Mtaka.Aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wanakikundi kuweka mifumo mizuri ya kutengeneza soko la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kuuza katika minada yote ya wilaya hiyo na kuimarisha soko la nje.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko amesema Halmashauri itahakikisha kiwanda hicho kinapata malighafi ya kutosha ambapo amebainisha kuwa Halmashauri imeingia mkataba na Chuo cha DIT Mwanza kuhakikisha kuwa inazalisha malighafi(ngozi) kwa wakati kwa ajili ya kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akivaa viatu vilivyotengenezwa katika Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za Ngozi kilichopo Senani Wilayani Maswa wakati wa Ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa pamoja na viongozi wakuu wa Wilaya ya Maswa wakielekea katika Kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa Ngozi katika Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akifuatilia hatua mbalimbali za utengenzaji wa viatu vya ngozi kwenye kiwanda cha kutengeneza bidhaa ngozi kilichopo Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Njiapanda wilayani Maswa, wakati alipotembelea eneo ambalo kitajengwa kiwanda kidogo cha kutengeneza ungalishe kitakachomikiwa na shule za Msingi 30 za Maswa,wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo wilayani humo.


KUMBILAMOTO AKABIDHI KIFAA CHA KUPIMIA PUMU ZAHANATI YA VINGUNGUTI

$
0
0
  Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akikabidhi kifaa cha kupimia Pumu kwa  Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti.
 Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akikabidhi Vifaa vya Kujifungulia wajawazito  kwa  Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti.
 Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akizungumza kabla ya kukabidhi kifaa cha kupimia pumu kwa watoto na watu wazima na Vifaa vya Kujifungulia katika Zahanati ya Vingunguti , ambayo Wanawake hufika hapo bila ya kuwa na Vifaa vya kujifungilia, hivyo vitaweza kuwasaidia wale ambao hawatakuwa na uwezo.
Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto na  Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, wakikabidhi Mbuzi  kwa ajili ya  Madkatari na wauguzi wa Zahanati ya Vingunguti.

RC RUVUMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA VYEMA MAADILI YA WAUMINI WAO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA BI CHRISTINA MNDEME amewataka viongozi wa dini mkoa humo kusimamia vyema maadili ,unywaji pombe uliokithiri pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini katika ikulu ndogo mjini songea habari kamili hii hapa video yake

KIKOSI CHA YANGA KAMILI KUIVAA LIPULI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo jijini Mbeya kuelekea Iringa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Lipuli siku ya Jumamosi.

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Uwanja Samora utakuwa wa ushindani mkubwa kwa timu zote huku Yanga wakitaka kulipa kisasi kwa Lipuli.

Yanga ilikuwa mkoani Mbeya kwa ajili ya mechi dhidi ya timu ya Ihefu FC ikiwa ni hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya juzi.

Akizungumza na Michuzi Blog, Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kikosi chote kilichosafiri na timu kimeelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Lipuli utakaofanyika Jumamosi.

"Kikosi cha Yanga kimeondoka kuelekea Iringa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Lipuli ikiwa ni mchezo wa marudiano wa raundi ya pili na wachezaji wote waliosafiri na timu kutoka Dar es salaam wameondoka,"amesema.

Katika mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Uhuru ulimalizika kwa sare ya 1-1 ambapo Donald Ngoma aliwasiwazisha goli hilo huku Seif Karihe akifunga kwa upande wa Lipuli.

HALMASHAURI YA MJI WA MBULU WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 16

$
0
0
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara, limepitisha bajeti ya shilingi 16, 225,661,581 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019. 

Mkurugenzi wa Mji wa Mbulu, Anna Mbogo akizungumza wakati wa kupitishwa kwa bajeti hiyo amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Halmashauri hiyo na miradi ya maendeleo.

Mbogo amesema bajeti hiyo imelenga kuwezesha miradi ya elimu, afya na maji kwenye baadhi ya kata za Halmashauri ya Mji huo. Alisema bajeti hiyo haijahusisha fedha za ujenzi wa barabara kwani zimehamishiwa serikali kuu kupitia wakala wa barabara wa mjini na vijijini (Tarura). 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Valerian Gidshanga alisema kupitishwa kwa bajeti hiyo ni jambo moja na utekelezaji wake ni mwingine hivyo kila mmoja atimize wajibu wake. "Sisi madiwani kwa pande wetu tutekeleze wajibu wetu, watumishi wa halmashauri nao wafanye kazi kwa nafasi yao na wananchi kwa ujumla watuunge mkono katika kufanikisha bajeti yetu," alisema Gidshanga. 

Diwani wa Kata ya Tsawi, Anthony Genda amesema bajeti hiyo imejikita kwenye sekta tofauti za miradi ya maendeleo. Genda amesema kwa upande wa kata yake bajeti hiyo imezingatia suala la ujenzi wa kituo cha afya hivyo kuwa na manufaa kwa jamii. 
  Mkurugenzi wa Mji wa Mbulu Anna Mbogo, akizungumza baada ya Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji huo kupitisha bajeti yao. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara, Valerian Gidshanga akifungua kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo. 
 Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara, wakiendelea na kikao cha Baraza la madiwani kilichopitisha mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu. 

TAARIFA YA UPIMAJI KANSA KWA WENYE UALBINO

$
0
0

Kaka na dada wetu,

@imetoshafoundation wa kushirikiana na Umoja wa watu wenye ualbino Tanzania, na Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, tumeandaa upimaji wa Kansa kwa watu wenye ualbino waishio jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada zetu katika kujaribu kupunguza vifo vya watu wenye ualbino vinavyosababishwa na saratani ya ngozi. 

Watu wengi hufariki baada ya kugundua ugonjwa ukiwa umwshaenea mwilini, na inawezekana kuutibu ukiwa bado haujafikia hatua mbaya.
Hivyo basi kama unamjua mtu mwenye ualbino umpe taarifa kwamba kuna upimaji wa BURE Ocean Road kwa siku mbili, ili kutambua afya yake na kuanza kupata tiba kabla ugonjwa haujamuathiri.
Sambaza ujumbe, tuokoe maisha

maadhimisho siku ya maahakama yafana Njombe

$
0
0
Mawakili wa Kujitegemea Mkoani Njombe Wamewatupia Lawama Watoa Maamuzi Katika Muhimili wa Mahakama Kwakuwa na Visingizio Mbalimbali Vinavyosababisha Mashauri ya Watuhumiwa Kuahirishwa Mara Kwa Mara na  Kusababisha Kuongeza Gharama Katika Uendeshaji  Kesi.

Akitoa taarifa katika Maazimisho ya  Kilele Cha Wiki ya Sheria Ambayo Kimkoa Imefanyika Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe Wakili wa Kujitegemea Bwana Barnaba Mwangi Kupitia Taarifa ya Chama Cha Wanasheria Afrika Mashariki Anasema Miongoni Mwa Changamoto Kubwa Inayowakwamisha ni Visingizio Vinavyofanywa na Baadhi ya Mahakimu Kwa Kuahirisha Kesi Mara Kwa Mara Bila Sababu za Msingi Jambo Linalo Minya Upatikanaji wa Haki Kwa Wakati.

John Kapokolo ni Hakimu Mfawidhi  wa Makahama ya Hakimu Mkazi Njombe Ambaye Anasema Kuwa Mfumo Mpya wa TEHEMA Utakapoanza Kufanya Kazi Katika Muhimili wa Mahakama Kama Ambavyo Kauli Mbiu ya Wiki Sheria Inasema Basi Huenda Ikawa Muarobaini wa Kupatikana Kwa Haki Kwa Wakati na Kwa Weledi Mkubwa.

Miongoni Mwa Changamoto Zilizotajwa na Hakimu Kapokolo Katika Taarifa Yake ni Pamoja na Gharama Kubwa ya Upimaji wa Maeneo ya Mahakama za Mwanzo Hoja Inayotolewa Majibu na Mgeni Rasmi Katika Maazimisho Hayo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka.

Baadhi ya Wadau Mkoani Njombe Akiwemo Mexon Sanga Hapa Anasema Anaamini Mfumo wa TEHEMAUtakwenda Kusaidia Sana Katika Upatikanaji wa Haki Kwani Hata Yeye Amekuwa Muhanga wa Namna Vyombo Vya Dola Vinavyo Shindwa Kuheshimu Muhimili wa Mahakama na Kuwakandamizi Wananchi.
Kaulimbiu ya Wiki ya Sheria Kwa Mwaka Huu Inasema ''Matumizi ya TEHEMA Katika Utoaji Haki Kwa Wakati na Kuzingatia Maadili"Kaulimbiu Inayokwenda Kuweka Bayana Kila Ushahidi Unaotolewa Mahakamani Kwa Njia ya Kunakiliwa Kwa Sauti na Video Bila Ubabaishaji Kama Inavyofanyika Katika Vikao Vya Bunge.

IGP SIRRO KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA

$
0
0


Na Nyakongo Manyama-MAELEZO
DAR ES SALAAM

MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Kutetea Maslahi ya Wafugaji Mbwa unaotarajia kufanyika tarehe 3 Februari mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam  Mkurugenzi wa  taasisi hiyo, Dkt Sinare  Sinare (pichani kushoto)  amesema kuwa  uzinduzi una lengo la kuwakutanisha wadau na wamiliki wa mbwa , kuhamasisha ufugaji na umiliki bora wa mbwa unaojali maslahi ya mbwa kwa wamiliki.
“Uzinduzi wa Chama chetu una lengo la kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa ufugaji mbwa kwa usalama wao pamoja na kusimamia na kushauri kuhusu uzalishaji bora wa mbwa kwa wanachama, wadau na serikali”.
Dr. Sinare ameeleza kuwa katika uzinduzi huo, Jeshi la Polisi kikosi cha mbwa  wanatarajia kufanya maonesho ya kuonesha weledi wa mbwa wao katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Dr. Sinare amefafanua aina tano za uanachama ambazo ni Mwanachama wa kawaida ambao ni kwa ajili ya wamiliki wa mbwa, Mwanachama mshiriki ambae ni mtu au kampuni ambayo shughuli zinahusiana na ustawi wa mbwa, Mwanachama kampuni ambao ni kwa kampuni ambayo shughuli zake zinahusiana na matumizi au uzalishaji wa mbwa.
Nyingine ni uanachama utakaopewa mtu yeyote ambae kwa mawazo ya wanachama atasaidia kuendeleza na kutekeleza madhumuni ya TCAL na Mwanachama mgeni kwa ajili ya wageni ikiwemo watu wa kampuni ambazo sio wenyeji wa Tanzania. 
Dr. Sinare ameeleza kuwa ili kuwa mwanachama wa kundi lolote la uanachama utajaza fomu maalumu kwq ajili ya kujiandikisha kisha umtu atalipia shilingi laki moja  kama kiingilio na kupewa kitambulisho.

TASWIRA MBALIMBALI ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mbeba mizigo katika soko la Buguruni akiwa amebeba matenga ya kubebea nyanya leo jijini Dar es Salaam.
 Mwananchi akifanya usafi wa mazingira nje ya soko la Buguruni bila ya kuwa na vifaa vya usafi leo jijini Dar es Salaam,hali ambayo anaweza kupatwa na magonjwa ya kuambiza ikiwemo ya ngozi.
Kazi ikiendelea Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Tatu Mzuka yazindua kampeni ya Valentine, ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’

$
0
0

• Zaidi ya milioni 300 kutolewa katika msimu huu wa Valentine

 Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka, leo wamezindua kampeni mpya ya Valentine, ambayo inaanza rasmi leo hadi tarehe 18 ya mwezi wa pili.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao pia kupata fursa ya kushinda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, bwana Sebastian Maganga, alisema Tatu Mzuka imekuwa na utaratibu wa kuwa na kampeni zinazoendana na misimu ya sherehe za kitanzania.‘Kwa msimu huu wa Valentine peke yake, zaidi ya shilingi MILIONI 300 zitatolewa kwa washindi wetu watakaocheza kuanzia tarehe 1 hadi 18 ya mwezi huu’ alisema Maganga.

Kama sehemu ya kampeni hiyo pia, Maganga alisema pia KILA SIKU kwa siku 18 kiasi cha MILIONI 10 zitakuwa zinatolewa, ambapo MILIONI 5 itakuwa ya mshindi na MILIONI 5 itakuwa ya mtu ambaye mshindi atamchagua.‘Lakini pia kubwa kuliko, ukicheza kuanzia leo hadi tarehe 18 utapata pia fursa ya bure kuingia kwenye Valentine SUPA MZUKA Jackpot, ambapo mamilioni yatatolewa kwa washindi, ambapo pia mamilioni ya ziada yatakwenda kwa wanaowapenda’ alisema Maganga. 
 Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga,akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kampuni hiyo kuzindua kampeni mpya ya Valentine  ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’  , ambayo inaanza rasmi leo hadi februari 18,2018.Pichani kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwae Nandy pamoja na Aslay (kushoto) ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kampeni hiyo
 Msanii mahiri wa Muziki wa Kizazi kipya Aslay akighani moja ya wimbo walioimba pamoja na msanii mwenzake aitwaye Nandy 'subah lakheri' kama sehemu ya kionjo kwa wanahabari walioshiriki mkutano huo mapema leo jijini Dar.
 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo.


TBL YASEMA MFUMO WAKE WA TAARIFA UKO SALAMA

$
0
0
*Yapunguza bei ya bia ya Castle Lite Premium Lager

Na ripota Wetu,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizozagaa mitandaoni za kudukuliwa kwa mfumo wake wa kuhifadhi taarifa zake na kusisitiza mfumo huo uko salama baada ya kujiridhisha. 

Mapema jana asubuhi kulionekana taarifa ya video kwenye mtandao wa YouTube ikioesha kuna mtu aliyekuwa amevalia kofia iliyofunika uso (Mask) ikieleza kuwa, mfumo wa kuhifadhi taarifa wa TBL umedukuliwa na hivyo kuhatarisha kuvuja kwa taarifa zake muhimu. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL - Afrika Mashariki, Thomas Kemphuis amesema baada ya uchunguzi wa kina kampuni hiyo imejiridhisha pasipo na shaka kuwa hakuna tukio la aina hiyo lililotokea.

"Mfumo wetu wa taarifa uko salama , nitumie nafasi hii kuwahakikishia wanahisa wetu,wadau pamoja na umma kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi,"amefafanua.

Imeelezwa nia ya TBL kuendelea kutoa huduma bora huku Kemphuis akifafanua kampuni hiyo inachukulia kwa uzito mkubwa suala la usalama wa mifumo yake na ndiyo sababu ya kufanya uchunguzi wa haraka na wakina mara baada ya kupata taarifa za uvumi kuhusu  udukuzi. 

Mkurugenzi huyo amesema kuwa TBL itaendelea kutengeneza mifumo imara ya ulinzi wa taarifa zake ili kuepuka matukio yasiyotarajiwa kama udukuzi. 

Wakati huo huo, TBL imetangaza habari njema kwa wateja wake baada ya kutoa punguzo la bei kwa bia yake pendwa ya Castle Lite Premium Lager kutoka bei ya sasa ya shilingi elfu 2,500 hadi shilingi 2,000.

Kwa mujibu wa Kemphuis, punguzo hilo la bei ni zawadi kwa wateja wa bia hiyo kwa kuwa wateja waaminifu na zaidi kwa kuiunga mkono kampuni ya TBL kupitia bidhaa zake. 

“Kupunguza bei ya bia ya Castle Lite Premium Lager kunadhihirisha shukrani zetu kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono kwa kipindi kirefu. TBL siku zote ipo tayari kuwasikiliza wateja wake na kuwapa kile wanachokitaka,"amebainisha. #CastleLiteHacked

TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI JUU YA “UVUMI” UNAOENEA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU IDARA YA UHAMIAJI KUTANGAZA NAFASI ZA KAZI ZA MKAGUZI MSAIDIZI, KOPLO NA KONSTEBO

$
0
0
Kumekuwepo na uvumi unaoenezwa kupitia baadhi ya Mitandao ya Kijamii kuwa Idara ya Uhamiaji imetangaza nafasi za ajira kwa nafasi za Mkaguzi Msaidizi, Koplo na Konstebo. Kufuatia kuwepo kwa uvumi huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi kuwa:

1.   Idara haijatangaza nafasi zozote za ajira katika kipindi cha hivi karibuni, hivyo tunawaomba wananchi wasirubuniwe au kushawishiwa na mtu yeyote kutoa kitu chochote ili waweze kusaidiwa kupata kazi Idara ya Uhamiaji kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na pia hakuna mtu anayeruhusiwa kulipa fedha ili apate ajira katika Idara ya Uhamiaji.


2.   Taarifa za kutangazwa nafasi za kazi zilizotolewa kupitia Mitandao hiyo ya kijamii hazina ukweli wowote, bali ni uzushi uliofanywa na watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayoyajua wao.
3.   Idara ya Uhamiaji, kama Taasisi ya Serikali inao utaratibu maalum wa kutangaza nafasi za ajira kwa uwazi kupitia Magazeti, Televisheni na Tovuti yake ambayo niwww.immigration.go.tz
4.   Idara inatoa onyo kwa mtu au watu wanaojihusisha na utoaji wa taarifa za upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii, kuhusu huduma za uhamiaji ikiwa ni pamoja na suala la nafasi za ajira. Aidha, Idara haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakao bainika kujihusisha na vitendo hivyo.

  
Imetolewa na;


KITENGO CHA UHUSIANO,


IDARA YA UHAMIAJI

MAKAO MAKUU, DAR ES SALAAM.

01 FEBRUARI, 2018

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 01.02.2018

UNNewsKiswahili: Kijana wa kitanzania angara katika jukwaa la Umoja wa Mataifa New-York

VOA Swahili: Duniani Leo 1st February 2018

Viewing all 109936 articles
Browse latest View live




Latest Images