Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

NGOWI TV: BREAKFAST DEBATE DISCUSSING THE BOOK "LIFTING THE VAIL OF SECRECY"


MFANYABIASHARA WA NGUAO KARIAKOO AJISHINDIA MILIONI 60 ZA TATUMZUKA

$
0
0

Mwakilishi wa TatuMzuka,Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi Neema  Mtewele (38),ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za akina mama Kariakoo jijini Dar Es Salaam,aliyeibuka na kitita cha shilingi milioni 60 za TatuMzuka mwishoni mwa wiki.
Neema  Mtewele (38),ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za akina mama Kariakoo jijini Dar Es Salaam,akifafanua mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda mamilioni hayo ya Mchezo wa kubahatisha wa Tatumzuka.Neema alisema kuwa amekuwa akiucheza muda mrefu mchezo huo bila mafanikio,lakini hakukata tamaa,alindelea kucheza na hatimae akabahatika kuibuka mshindi wa milioni 60.

"Hizi fedha kwakweli matumizi yake makubwa yatakuwa ni kuendeleza na kuunyanyua zaidi mtaji wangu niliokuwa nao kwenye biashara yangu,bado nahitaji kuikuza zaidi biashara yangu",alisema Neema huku akionesha furaha ya wazi kwa kushinda kitita hicho cha milioni 60.

LYATONGA MREMA KUUNGURUMA LEO STENDI YA MABASI MWENGE JIJINI DAR

$
0
0
KATIBU MKUU WA TLP, Mhe Nancy Mrikaria,anapenda kuwataarifu  akina mama na akina baba  kuwa Mhe.Augustino Lyatonga Mrema Mwenyekiti Wa Taifa wa bodi ya Parole na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa TLP atafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika leo tarehe 01/02/2018  muda saa nane kamili mchana (8:00) katika viwanja vya stendi ya zamani ya mwenge.

Mhe Mrema,atamwaga sera na kumnadi mgombea Ubunge wa chama cha Tanzania Labour paty(TLP) Dr. Godfrey Malisa, watasikiliza shida ,KERO na changamoto za wananchi na kutoa suluhisho la matatizo ya wananchi wa jimbo la kinondoni,anawaomba wanakinondoni bila kujali chama kufika kwa wingi tusikilize sera za mgombea wao ,amekumbusha kuwa hii ni fursa ya wanakinondoni kusikiliza na kupima uwezo na sera bora ili kupata muelekeo wa kujua nani anastahili kuchaguliwa na nani anaweza kuwa mwakilishi wao makini na anayeweza kumaliza shida ZAO.

ikumbukwe kuwa UCHAGUZI NI tendo na utashi na itakuwa makosa IKIWA mwananchi atabaki nyumbani akiamini ATAKAYECHUGULIWA NI CHAGUO LA WOTE BILA YEYE BINAFSI KUPIMA NA KUJIRIDHISHA ATAKUWA ANAJINYIMA HAKI YAKE YA MSINGI.
KARIBUNI.
Imetolewa na ofisi ya Katibu MKUU,
chama cha TLP
MAKAO MAKUU - MAGOMENI 
DAR ES SALAAM

WITO WATOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA KUTII SHERIA WAKATI WA UCHAGUZI.

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amevikumbusha vyama vya siasa kutii Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za uchaguzi na kanuni zake wakati wa uchaguzi.

Wito huo umetolewa kupitia barua aliyoviandikia vyama vya siasa yenye kumbukumbu HA.322/362/01/165 ya tarehe 30 Januari, 2018.

“…natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi ndogo za Ubunge na Udiwani zinazoendelea katika majimbo na kata. Hivyo, natumia fursa hii pia kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika chaguzi hizo, kwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kidemokrasia. 
 
Aidha, naviasa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kuheshimu na kufuata sheria za nchi, hasa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kanuni zake, kwa kuepuka vitendo vya fujo na lugha za matusi na uchochezi” imenukuliwa barua hiyo. 

Jaji Mutungi pia ametoa wito kwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au chama kinachoshiriki uchaguzi kutoa taarifa katika mamlaka husika kuliko kujichukulia sheria mkononi, endapo kitashuhudia kwa kuona ama kusikia uvunjifu wa Sheria unaohusu chaguzi zinazofanyika.

Msanii Wastara awashukuru watanzania kwa kuchangia matibabu yake

$
0
0
Na Genofeva Matemu – WHUSM

Msanii wa filamu nchini Bibi. Wastara Issa ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha moyo wa kuguswa na tatizo linalomsumbua na kuweza kumpatia kiwango cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya mguu pamoja na mgongo.
Bibi. Wastara ametoa shukrani hizo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa awali ilikua aondoke nchini tarehe 28 mwezi januari mwaka huu kwenda mjini Mumbai kwa ajili ya matibabu lakini kutokana na baadhi ya mipango kutokaa vizuri safari hiyo ilisogezwa hadi jumapili tarehe 4 Februari 2018 ambapo anatarajia kuondoka mida ya jioni na kufika Mumbai mapema alfajiri siku ya jumatatu ambapo ataanza matibabu siku hiyo hiyo.

Bibi. Wastara amesema kuwa katika safari hiyo ataongozana na nesi mmoja kutoka hospitali ya TMJ pamoja na mtu mmoja kutoka katika familia yake ambapo matibabu yake yatafanyika katika hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai na kutarajia matibabu hayo kuchukua takribani wiki tatu na zaidi.

Aidha msanii Wastara Issa ameishukuru wizara inayosimamia tansia ya filamu kwa kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia huku akimshukuru Waziri mwenye dhamana na tasnia ya filamu nchini, Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa pamoja na watanzania wote kwa kuonyesha upendo wa dhati kwake.

“Asanteni sana watanzania mmeonyesha moyo wa dhati kwangu kwa muda mrefu sasa, mmekua pamoja nami tangu kipindi cha matibabu ya Saduki hadi sasa, uzito wa neno asante kutoka kwangu leo hauwezi kulipa fadhila kwa dua na michango yenu kwangu, mwenyezi mungu aendelee kuifanya nchi yetu kuwa na amani na upendo” amesema msanii Wastara Issa

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa serikali kupitia bodi ya filamu inashukuru kwa kupata taarifa kamili ya safari ya msanii Wastara Issa ilipofikia kwani bodi ya filamu inapenda kumuona Wastara akiwa katika afya nzuri na kurudi katika hali yake ili aweze kuungana na wanatasnia wenzake kuendeleza tasnia ya filamu nchini.

Bibi. Fissoo amesema kuwa Watanzania wengi wamekua wakiwasiliana na Wastara kwa njia mbalimbali, kumchangia na hata kufika kumuona, hivyo serikali inatambua kuwa msanii Wastara Issa yupo katika maandalizi ya safari ambapo awali alikua asafiri  tarehe 28 mwezi januari mwaka 2018 lakini kutokana na taratibu za safari kutokukamili kumepelekea safari hiyo kusogezwa hadi tarehe 4 februari mwaka huu. 
Msanii wa Filamu nchini Bibi. Wastara Issa (wapili kulia waliokaa chini) akizungumza na waandishi wa  habari  nyumbani kwake kuhusu maandalizi ya safari yake ya matibabu kuelekea Mjini Mumbai walipofanya naye mazungumza leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo

"101 Letters from a Vocal Coach" Goes to Amazon, Barnes & Noble

$
0
0

At last, my new book, available in paperback, is now in globalREACH retail distribution via the world’s top online bookstores Amazon and Barnes & Noble. Which means, anyone on the planet who is accustomed to buying books from these two bookstore platforms will now be able to purchase 101 Letters from a Vocal Coach from a familiar bookstore.



I know some of us feel safe to shop online only in familiar territory. If you've hesitated to make that purchase when my book first surfaced on Lulu, well now you can go right ahead and buy my paperback online from Amazon and Barnes & Noble with ease. 

If you like my article, do me a HUGE favor and Share this blog post with others by clicking the Social Links below. And if you want to consider private lessons via Skype, you'll find more information here!

You Are the Instrument, Learn to Sing Like a Pro!


JOETT- Vocal Coach & Author:


  

Msanii Wastara awatoa hofu watanzania kuhusu matibabu yake

$
0
0

Na: Genofeva Matemu – WHUSM 

Msanii wa filamu nchini Bibi. Wastara Issa ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha moyo wa kuguswa na tatizo linalomsumbua na kuweza kumpatia kiwango cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya mguu pamoja na mgongo. 

Bibi. Wastara ametoa shukrani hizo jana  Jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa awali ilikua aondoke nchini tarehe 28 mwezi januari mwaka huu kwenda mjini Mumbai kwa ajili ya matibabu lakini kutokana na baadhi ya mipango kutokaa vizuri safari hiyo ilisogezwa hadi jumapili tarehe 4 Februari 2018 ambapo anatarajia kuondoka mida ya jioni na kufika Mumbai mapema alfajiri siku ya jumatatu ambapo ataanza matibabu siku hiyo hiyo. 

Bibi. Wastara amesema kuwa katika safari hiyo ataongozana na nesi mmoja kutoka hospitali ya TMJ pamoja na mtu mmoja kutoka katika familia yake ambapo matibabu yake yatafanyika katika hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai na kutarajia matibabu hayo kuchukua takribani wiki tatu na zaidi. 

Aidha msanii Wastara Issa ameishukuru wizara inayosimamia tansia ya filamu kwa kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia huku akimshukuru Waziri mwenye dhamana na tasnia ya filamu nchini, Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa pamoja na watanzania wote kwa kuonyesha upendo wa dhati kwake. 

“Asanteni sana watanzania mmeonyesha moyo wa dhati kwangu kwa muda mrefu sasa, mmekua pamoja nami tangu kipindi cha matibabu ya Saduki hadi sasa, uzito wa neno asante kutoka kwangu leo hauwezi kulipa fadhila kwa dua na michango yenu kwangu, mwenyezi mungu aendelee kuifanya nchi yetu kuwa na amani na upendo” amesema msanii Wastara Issa.


Msanii wa Filamu nchini Bibi. Wastara Issa (wapili kulia waliokaa chini) akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu maandalizi ya safari yake ya matibabu kuelekea Mjini Mumbai walipofanya naye mazungumza jana Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS FEBRUARY MOSI,2018


EXIM IMEKABIDHI VITANDA NA MAGODORO 40 KWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MBEYA, WODI YA WAZAZI META.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji was hospital ya rufaa ya Mbeya Dr Godlove Mbwanji akitoa shurkani kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (kushoto) baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda na magodoro 40 kutoka benki hiyo jana asubuhi kwa ajili ya wagonjwa katika hospitali hiyo kitengo cha wazazi-Mbeya jijini Mbeya.  Wa pili kulia ni Mkuu wa idara ya wodi ya wazazi-Meta, katika hospitali hiyo Dr John France.

HOSPITALI na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa.  Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa , Exim Bank Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa  imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.

Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania. Kama benki ya kiTanzania iliyoanzishwa mwaka wa 1997, Benki ya Exim inafafanua mafanikio kwa jinsi inavyoleta mabadiliko kwa wateja na jamii kwa ujumla.

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya, ni hospitali ya sita kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, Arusha mwezi uliopita, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo wodi ya wazazi META na mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dr. Godlove Mbwanji.

Mohammed Enterprises yazindua shindano la Pindua Ushinde

$
0
0
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imezindua shindano la Zawadi ya Chini ya Kizibo (UTC) la “Pindua Ushinde” litakalofanyika kwa muda wa siku 45, linalotarajiwa kuisha Machi 10 mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Masoko MeTL, Fatema Dewji ameeleza namna ya kushiriki shidano hilo, kwamba ili ujishindie zawadi, inatakiwa kununua maji ya Mo Maisha na Masafi yenye ujazo kuanzia Mili lita 600 hadi lita 1.7.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tunawaletea shindano la zawadi ya chini ya kizibo kwa bidhaa za maji. Hii ni kwa maji ya Mo Maisha na Masafi yenye ujazo kuanzia Mili Lita 600, lita 1 na lita 1.7 ambazo huja kwako katika chupa za plastiki. hii haijawahi kutokea popote nchini Tanzania,” amesema.Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Dewji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shindano la Zawadi ya Chini ya Kizibo (UTC) la “Pindua Ushinde”

Amesema, Pindua Ushinde inakupa fursa ya kujishindia zawadi ya Maji ya bure au pesa taslimu kuanzia Sh. 1,000 hadi 100,000, ambapo ili kujionea ulichoshinda, unatakiwa kupindua kizibo cha chupa ya maji ya Mo Maisha au Masafi.

“Maji ya Mo Maisha na Masafi ni safi na salama kwa afya yako na hutayarishwa katika mazingira bora ya usafi wa hali ya juu. Pia,chupa zetu ni safi na salama zilizorafiki kwa matumizi yako zimetengenezwa ili kukidhi viwango vya kimataifa. Kumbuka unapokunywa maji yetu unajiepusha na magonjwa yanayoenezwa kwa maji yasiyo safi na salama,” amesema.


 
Vile vile, Fatema Dewji amezindua Kampeni ya kutunza mazingira inayofahamika kwa jina la “Tanzania Safi” iliyolenga kuhakikisha ardhi haiharibiwi kwa uchafu wa chupa za plastiki.

“Tutatoa ushirikiano kuondoa chupa za plastiki zitakazoonekana mitaani ili zitumike kama malighafi katika uzalishaji viwandani. Hii si mara ya kwanza kufanya kampeni za utunzaji mazingira, awali MeTL ilifanya kampeni ya utunzaji mazingira kwa kusafisha ufukwe wa Coco Beach," amesema na kuongeza.“Pia tuliendesha kampeni ya kuelimisha jamii namna ya kuepuka magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama ambapo wataalamu wa afya walielimisha jamii.”

Naye Meneja Mauzo wa Kiwanda cha A 1 kilicho chini ya MeTL kinachozalisha Maji ya Mo Maisha na Masafi, Godfrey Mangungulu amesema washindi wa maji bure na fedha kuanzia 1,000 hadi 50,000 watapewa zawadi zao waliponunua maji, na watakaoshinda zaidi ya fedha hizo watachukua bidhaa zao kwenye Kiwanda cha A1 kilichopo Kurasini.
“Tumeamua kurudisha fadhila kwa jamii, kwa zaidi ya miaka 20 tunauza bidhaa zetu , hivyo tumeamua kurudisha sehemu ya mauzo ya bidhaa zetu kwa jamii. MeTL tuajivunia bidhaa bora na usambazaji wetu unafika nchi nzima,” amesema.

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

DK.MPANGO ,MKURUGENZI BENK YA BARCLAYS WATETA UJENZI RELI YA KISASASA,MRADI UMEME WA STIGLER'S GORGE

$
0
0
Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Bw. Peter Matlare na kuiomba Benki hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR) mradi wa miundombinu ya umeme wa Stieglar's Gorge ili kurahakisha maendeleo ya kiuchumi kupitia viwanda.

Amemweleza kiongozi huyo kwamba Serikali imeimarisha uchumi Mkuu kwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao uko katika kiwango chatarakimu moja cha wastani wa asilimi 5.3 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.

"Tumewekeza kwenye miundombinu kama vile Elimu, maji, kilimo, afya, madini, na biashara na kwamba katika kipindi kifupi cha miaka 2 zaidi ya viwanda 80 vimejengwa katika eneo la Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo kuwa karibu na Bandari ya Dar es Salaam.

Dkt. Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) ambao amesema utarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza biashara kwa kiwango kikubwa.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare  akielezea umuhimu wa kushirikiana katika kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Benki yake wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
 Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakifuatilia mazungumzo kati yao na ugeni kutoka  Benki ya Barklays  nchini Afrika Kusini (hawako pichani), mkutano uliofanyika mjini Dodoma
 Ujumbe kutoka Benki ya Barclays uliongozwa na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (kulia), wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati yao na  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (hayupo pichani), kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano katika kukuza biashara kati ya Tanzania na benki yake, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
 Maafisa Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV LIVE: HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAHAKAMA

IGP SIRO MGENI RASMI UZINDUZI WA CHAMA CHA WAMILIKI WA MBWA

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Canine Association Ltd (TCAL) Sinare Sinare, akizungumz na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, leo wakati akitangaza uzinduzi rasmi wa Chama cha Wamiliki wa Mbwa utakaofanyika katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni siku ya jumamosi,Januri 3,2018. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Inspector General wa Polisi (IGP) Simon Siro. Kushoto kwake ni Wajumbe wa Kamati ya uzinduzi huo, Felicia Bulu na Deo Rweyunga. (kushoto) ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi, Dkt. Egyne Emmanuel. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Mkutano ukiendela.

WATANZANIA WATAKIWA KUACHA KUTUMIA VIPODOZI VISIVYOKUWA NA KIWANGO


RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na Majaji Wastaafu baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Godwin Ngwilimi baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.

Picha na IKULU

MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA ATEMBELEA ENEO LINALOTARAJIWA KUEKEZWA NDANI YA MKOA WAKE

$
0
0
 Afisa kutoka Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) zone ya Pemba, Nd. Ali Shaaban Suleiman akitoa ufafanuzi wa maeneo yanayotegemewa kuekezwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi. Salama Mbarouk Khatib akimkaguza   Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Omar Khamis Othman katika eneo linalotarajiwa kuwekezwa Hoteli kubwa ya kitalii eneo la Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Eneo la fukwe Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba linalotarajiwa kuekezwa.
Picha na Mwamize Muhammed Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pemba.

BALOZI WA CUBA NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akisalimiana na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa na changamoto zinazolikabili Jeshi hilo Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.

Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades akizungumza jambo wakati mazungumzo yao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto), Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo hawapo pichani na Katibu wa Balozi na Mkalima, Sultan Hamud Said (Kulia) Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa katika picha na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam wengine ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Michael Shija wanne kutoka (kulia), Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage wa kwanza (kulia) na Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko wa tano kutoka (kulia). Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiagana na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji).

KAIMU KATIBU IDARA YA VYUO,VYUO VIKUU AKABIDHI KADI 1500 KWA KATIBU HAMASA SENETI YA DAR

$
0
0
Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndugu Daniel Zenda akikabidhi  kadi 1500 za wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa Katibu wa Hamasa Seneti ya mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Juakali Kuwanya katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya UVCCM, Upanga  jijini Dar es Salaam.


Zenda amesema, kadi hizo amezikabidhi ili zigawiwe kwa wananchama wapya ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi katika Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake, kutokana na mwamko mkubwa wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuunga mkono CCM kutokana na kuvutiwa na Utendaji kazi  wa Rais John Magufuli na Serikali yake ya awamu ya tano



Imetolewa na 

Uvccm Seneti Mkoa Dsm.

TATIZO LA MAJI LINDI MJINI KUBAKI HISTORIA.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amefanya ziara kutembelea mradi wa maji wa Ng'apa  Mkoani  Lindi  wenye thamani ya  Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali. 

Profesa Mkumbo amesema  kuwa wananchi  wa Lindi wanaanza  kupata huduma ya maji   leo Februari mosi huku   kazi ndogondogo zilizobaki katika mradi huo zikiendelea kukamilishwa.

Akifafanua amesema kuwa mradi huu unatarajia kuzalisha kiasi cha lita milioni 7 za maji  kwa siku kiasi ambacho kitakidhi mahitaji ya maji   Lindi mjini kwa sasa na kuchochea ukuaji wa uchumi  na uzalishaji, Aidha mahitaji  ya maji ya mji huo ni kiasi cha lita milioni 5 kwa siku .

“ Mamlaka ya maji na usafi wa  mazingira Lindi (LUWASA) itafanya kazi ya ukarabati wa miundombinu iliyopo pamoja na kuongeza mtandao katika vitongoji ambavyo havina mtandao wa mabomba “ Alisisitiza Profesa  Mkumbo. 

Aidha,  Profesa Mkumbo ametoa wito kwa wananchi Mkoani Lindi kulinda miundombinu ya maji na  kulipa ankara za maji waliyotumia ili huduma hiyo iwe endelevu na ichangie katika kuleta maendeleo.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha huduma za jamii hasa zile zinazowagusa wananchi wanyonge ikiwemo upatikanaji wa maji safi na Salama  kwa wananchi wake kote nchini hali inayochochea kasi yautekelezaji wa miradi ya maji katika Mikoa na Wilaya mbalimbali hapa nchini.

Mradi huo umetekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji  ambapo mkandarasi ni Kampuni ya  OIA ya nchini india.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji  Profesa Kitila Mkumbo akisikiliza maelezo kutoka  kwa mshauri muelekezi  wa mradi  maji wa Ng'apa  Mkoani Lindi bw.Colman Ngainayo (wakwanza kulia), wakati  wa ziara  yake yakukagua mradi huo wenye thamani ya  Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali, mradi huo utawanufaisha wakazi wa Lindi mjini kuanzia leo Februari mosi, kushoto ni meneja wa mradi huo kutoka Kampuni ya OIA ya nchini india
 Bw. Rajeev Rai.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi  wa maji wa Ng'apa  Mkoani  Lindi  utakaowanufaisha wakazi wa Lindi mjini kuanzia leo Februari mosi.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images