Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2018 amezindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Kabla ya kuzindua mfumo wa uhamiaji mtandao Mhe. Rais Magufuli amekagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielektronikia (e-Passport) ambayo pia imeanza kutolewa leo.
Pasipoti mpya za kielektronikia pia zimetolewa kwa viongozi wengine wakuu wa Serikali, Bunge na Mahakama wa Tanzania Bara na Zanzibar, waliohudhuria uzinduzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Dkt. Peter Makakala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiiangalia kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea passipoti yake mpya ya kielektronikia kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea pasipoti yake mpya ya kielektronikia kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akisubiri hatua inayofuata baada ya kuweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya ya kielektronikia makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018. PICHA NA IKULU