Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

SERIKALI, MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WAJADILI MPANGO UTEKELEZAJI SERA IDARA MAENDELEO YA JAMII

0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba (wa tatu kulia)akifungua kikao baina ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs ) na Serikali kilicholenga kujadili mpango wa pamoja katika utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kilichofanyika Makao Makuu Dodoma tarehe 30.1.2018.
 Katibu wa kikao cha ushirikiano baina ya Serikali na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Bi. Tausi Mwilima (kulia)akisoma Muhtasari wa kikao kilichopita kwa wajumbe wakati wa kikao cha pamoja moja kilicholenga kujadili mpango shirikishi wa utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii ili kuharakisha Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike(kulia) akiwasilisha taarifa fupi juu ya Mpango wa Kuamsha Ari ya wananchi kujitolea katika kufanya shughuli za maendeleo wakati wa kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali(NGOs )na Serikali kilicholenga kujadili mpango shiriki na endelevu wa utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya  Maendeleo ya Jinsia Bi. Slyvia Siriwa(kulia) akiwasilisha mada kuhusu uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi na utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao kati Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Serikali kilicholenga kujadili mpango ushiriki wa utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KARUMA AKUMBUSHA SOKA LA WANAWAKE KUZINGATIA SHERIA 17 ZA MPIRA

0
0
Na Agness Francis,  Globu ya Jamii. 

MWENYEKITI wa Chama cha Soka  cha Wanawake Tanzania Amina Karuma amewakumbusha viongozi  wa timu mbali mbali za soka la  wanawake  zilizoingia 8 bora katika Ligi ya  Serengeti Primer Lite  kuzingatia sheria na kanuni 17  za Mpira wa Miguu. 

Karuma amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Chichi Kinondoni wakati wa Semina elekezi kwa viongozi hao  24  huku akiwataka watambue wajibu wao kulea wachezaji  wazuri ili kuisadia  kufikia malengo  ya kupata timu bora ya Taifa hapa nchini. 

Aidha Karuma amesema wapo karibuni kuingia kambini  na wanatarajia kucheza mechi ya kwanza na Zambia katika Kombe la Womes World ,
kabla ya kwenda kwenye challenge Cup nchini Rwanda kutetea ubingwa wao mara baada ya kuwasiliana  na Baraza la Soka la Afrika. Mashariki na Kati (CECAFA) 

Hata hivyo,  Karuma amesema licha ya wachezaji kujitahidi, ametoa mwito kwa wadhamini waendelee kujitokeza kufadhili timu hizo ili kusaidia kuleta maendeleo ya soka la wanawake  hapa nchini.Kwa upande wa Kocha Mkuu  Aliance Girls Ezekiel Chobaka amezungumzia utendaji mzuri wa timu yake tangu alipoanza rasmi kuifundisha Mei 5 mwaka jana.

"Maendeleo  ni mazuri  kwa timu yangu na ninamatumaini  kufanya vizuri  katika Ligi Kuu, vilevile tumeweza kuchukua ubingwa katika   Ligi kuu Mkoa  wa Mwanza,"  amesema Chabaka.
 Mwenyekiti wa Chama cha Soka  cha Wanawake Tanzania, Amina Karuma akizungumza na Viongozi wa Timu zilizoingia 8 bora ya Ligi ya Serengeti Primer Lite katika semina elekezi iliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika.
 Viongozi mbalimbali wa Timu hizo zilizoingia 8 Bora Ligi ya Wanawake Serengeti Premier Lite wakisikiliza mafunzo na maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka   cha Wanawake Tanzania, Amina Karuma leo Jijini Dar es Salaam.

AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA

0
0

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeendesha warsha kwa WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

WAVIU washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa,kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

Warsha hiyo ya siku tatu imeanza Jumatatu Januari 29,2018 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja WAVIU Washauri takribani 75 kutoka halmashauri za wilaya za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga, Kahama Mji, Ushetu na Msalala.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo WAVIU Washauri ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma.

“Kupitia warsha hii tutapeana mikakati mbalimbali jinsi ya kuwatafuta wateja waliopotea katika huduma na kujadili namna ya kuboresha zaidi huduma katika vituo vya tiba na matunzo lakini pia kutoa elimu kuhusu haki za WAVIU Washauri”,alieleza Tesha.
Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya WAVIU Washauri halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Aminael Tesha akielezea malengo ya warsha hiyo.
Mwezeshaji katika warsha hiyo,Vedastus Mutangira akitoa elimu kuhusu VVU na Ukimwi. Aliwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
MVIU Mshauri Neema Anthony kutoka kutoka CTC ya Segese katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA

0
0
Na,Jumbe Ismailly IRAMBA

KITUO cha Msaada wa sheria kwa Wanawake( WLAC) kimeanza kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili kwa kijinsia na ukeketaji pamoja na madhara yake kwa watoto wa shule za msingi za Nguvumali,Songambele na sekondari ya Ndago wilayani Iramba,Mkoani Singida ambapo katika kipindi cha wiki moja jumla ya wanafunzi 600 kutoka katika shule za msingi na sekondari walinufaika na mafunzo hayo.

Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa sheria na Wanawake (WLAC) Abia Richard aliyasema hayo kwenye mafunzo waliyotoa kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Tarafa ya Ndago,wilayani Iramba.

Aidha Mwanasheria huyo wa WLAC alifafanua kwamba katika kipindi hicho cha wiki moja zaidi ya watu 1000 wameshapatiwa mafunzo hayo ambayo kati ya hao wanafunzi wa darasa la tano mpaka la saba wa shule za msingi na kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ni 600 na watu wazima ni 500.

Akizungumzia sababu za kwenda kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi,Abia amezitaja kuwa  ni kizazi na taifa la kesho,jambo ambalo endapo wakifahamu madhara yake mapema watakapokuwa wakubwa itakuwa rahisi kuepukananavyo.Kwa mujibu wa Abia kituo cha msaada wa sheria na Wanawake na watoto kikifadhiliwa na The Foundation For Civil Society kimekuwa kikiendesha mradi wake wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake pamoja na kuzuia vitendo vya ukeketaji kwa wanawake.
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba wakiwa kwenye viwanja vya mikutano ya Kijiji hicho wakipatiwa mafunzo na Kituo cha Msaada wa sharia kwa wanawake (WLAC) juu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukeketaji pamoja na madhara yake.
Bi Esther Kileee (aliyemshikilia mkono ni Afisa mtendaji wa kata ya Ndago) kwanza    akitoa ushuhuda wa kuacha kujishughulisha na vitendo vya ukeketaji baada ya kuokoka na kwamba kabla ya kuokoka alikuwa akinufaika na shughuli hizo kwa kumpatia kipato chake na alaikuwa akiwakeketa wanawake wasiopungua 50 kwa mwezi.
  Mwanasheria wa WLAC,  Abia Richard akiwasilisha mada kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Kata ya Ndago,wilayani Iramba ambapo pamoja na mambo mengine alisema katika kipindi cha wiki moja zaidi ya watu 1000 walipatiwa mafunzo na kati yao,wanafunzi ni 600 na watu wazima ni 500.
 Mwanasheria wa WLAC, Abia Richard ajiteta jambo na afisa mtendaji wa kata ya Ndago, Abeli Philipo Shaluo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RC MNYETI AMTUMIA MBUNGE OLE MILLYA, SALAMU ZA KUACHA JIMBO LA SIMANJIRO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, amemtumia salamu mbunge wa Jimbo la Simanjiro James Ole Millya (Chadema) kutumia nafasi hii kuagana na wananchi wake kwani hawezi kushinda tena ubunge wake mwaka 2020.

Mnyeti aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya sekondari Emboreet kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation.Alisema Ole Millya anapaswa kuanza kupita kwenye vijiji vya jimbo hilo kwa ajili ya kuaga wananchi wake sababu hivi sasa wanataka kuongozwa na mbunge wa CCM.

"Mfikishieni salamu zangu rafiki yangu Ole Millya kwani tulikuwa naye CCM na namuhakikishia hawezi kuwa mbunge wa jimbo la Simanjiro mwaka 2020 kwa sababu CCM italirudisha hivyo aanze kuaga kabla hajaondoka," alisema Mnyeti.Hata hivyo, Ole Millya alisema Mnyeti ni kijana mwenzake wanayeheshimiana na waliyefahamiana kwa muda mrefu tangu wakiwa UVCCM, hivyo haamini kama maneno hayo yametoka kinywani mwake.

Alisema Simanjiro aliyoikuta wakati anachaguliwa mwaka 2015, ilikuwa imeharibiwa kwa siasa za maji taka, rushwa zinazodhalilisha utu wa watu na uuzaji wa ardhi uliokithiri."Kama nia yetu ni maendeleo kwa wananchi tunaowaongoza ni muhimu kushirikiana ili lengo litimie na Mungu akitufikisha mwaka 2020 wananchi waamue nani wa kumpa kura kwenye nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais," alisema Ole Millya.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro kwenye ziara yake ya siku saba ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kusikiliza kero zao na kuzungumza nao kwa kutoa maagizo na maelekezo mbalimbali kwa wananchi na viongozi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizindua ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya kidato cha sita ya sekondari Emboreet, Wilaya ya Simanjiro iliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation kwa kuchimba msingi kwa kutumia jembe.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (mwenye shati la maua) akimsikiliza Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, Peter Kiroiya Toima, juu ya ujenzi wa chuo cha ufundi cha Veta, ambacho kimejengwa na shirika hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme akutana na viongozi wa dini, waunda kamati ya amani ya mkoa

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini ambapo katika kikao hicho kamati ya Amani ya Mkoa imeundwa ikihusisha viongozi wa Dini zote. Katika  kikao hicho masuala mbalimbali ya maendeleo yamejadiliwa pia, na  amewashukuru viongozi hao kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuliombea Taifa na kukemea maovu. RC Mndeme  amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuliombea Taifa na pia ameahidi kuwapa ushirikaiano mkubwa kwa maendeleo ya Ruvuma na Taifa kwa ujumla pia kukemea maovu miongoni mwa jamii.
Kwa upande wao viongozi wa dini wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa hatua hiyo waliyoiita ya kihistoria, na wameahidi kushirikiana naye pamoja na serikali bega kwa bega ili kujenga jamii yenye kujali utu, maadili na inayochukia maovu.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  Mhe. leo katika picha ya pamoja na viongozi wa dini ambao wanaunda  kamati ya Amani ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kikao chao.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  Mhe. leo  akiwa na iongozi wa dini wanaounda  kamati ya Amani ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na wadau na maafisa kutoka katika ofisi yake.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 30.01.2018

WANAWAKE WANAOOMBWA RUSHWA YA NGONO WATOE TAARIFA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WANAWAKE wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono wametakiwa kuripoti katika vyombo vya sheria ili kupatiwa msaada.

Akizungumza na Michuzi blogu, Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Ofisa Mradi wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Asha Komba amesema rushwa ya ngono imekuwa jambo la kawaida katika jamii huku walengwa wanaofanyiwa vitendo hivyo wanashindwa  kutoa taarifa.

Komba amesema kitendo cha mwajiri au mwalimu kushawishi kufanya mapenzi kwa kuahidi kumpatia kazi au kufaulu masomo, inatambuliwa kama rushwa ya ngono.

Amesema, katika kukabiliana na hilo, wanatoa mafunzo kwa wanasheria, mahakimu, majaji na polisi kuhusu kumaliza unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono kwani hupunguza ufanisi wa kazi na kurudisha maendeleo,Ameongeza wamekuwa wakikusanya kesi za unyanyasaji na kuzichapisha ili Majaji na Mahakimu waweze kuzitumia wakati wa kutoa maamuzi yao.

Kwa upande wake, Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), Ruth Ndagu amesema adhabu ya mtu yoyote anayeomba rushwa ya ngono hufukuzwa kazi kwa matumizi mabaya ya madaraka au kifungo cha kuanzia miaka mitatu hadi mitano au kulipa faini ya kuanzia Sh.milioni moja hadi Sh.milioni tano.

Ndagu alisema rushwa ya ngono inafanyika kwa usiri na ni watu wachache wanaotoa taarifa kuhusu matendo hayo.

"Tunatumia sheria  ya kujamiiana ya mwaka 1999 katika kumshtaki anayetuhumiwa kwa rushwa ya ngono ambayo inakataza kuhusu kumdhalilisha mtu hata kwa kumshika maungo yake au kufanya mapenzi kinyume na maumbile, pia tunatumia sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11, kifungu namba 25 ya mwaka 2007," amesema Ndagu.

Amesisitiza kuwa wamekuwa wakipokea zaidi matukio ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto ambapo kwa mwaka wanaweza kupokea matukio 20 hadi 30 na kwamba watu wazima hawatoi taarifa.
 Ofisa mradi wa chama cha majaji wanawake Tanzania, TAWJA, Asha Komba akizungumza na mmoja wa mwananchi aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maonyesho ya wiki ya sheria, kupata ushauri juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono.

NAMNA MAHABUSU,WAFUNGWA WANAVYOTUMIA SEHEMU ZA SIRI KUINGIA NA SIMU, SIGARA GEREZANI

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

WAMETAFUTA mbinu mbadala! Ndivyo unavyoweza kuelezea kinachoendelea kwenye baadhi ya magereza yaliyopo nchini kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kwa ajili ya kuingia na simu za mkononi pamoja na sigara.

Sheria za magereza kuna baadhi ya vitu vimepigwa marufuku ikiwamo simu ya mkononi, dawa za kulevya, visu ,nondo na sigara lakini baadhi ya mahabusu na wafungwa wamekuwa wakiingia nazo kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mrakibu Msaidizi wa Magereza, makao makuu kitengo cha sheria Absalom Mokily ameiamba Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika leo alipokuwa kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria inayoendelea jijini Dar es Salaam kuwa kuna mbinu nyingi wanazozitumia mahabusu na wafungwa kuingia na vitu hivyo.

SEHEMU ZA SIRI ZINATUMIKAJE? IKO HIVI .

Akielezea zaidi kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kuingia na vitu ambavyo vimepigwa marufuku , Mokiry amesema wenye tabia hiyo wamekuwa wakijaza mizigo kupitia njia  za haja kubwa na njia ya mkojo.

Amesema kuwa wanaoingia na vitu hivyo hata askari Magereza wanashindwa kubaini kutokana na utaalamu wanautumia kificha vitu hivyo vilivyopigwa marufuku kuingizwa magerezani."Unaweza kuwapekua na usione chochote, hivyo unapomruhusu aondoke, anachokifanya anakwenda chooni na kisha kutoa vitu alivyoficha kwenye  sehemu zake za siri,"ameeleza.

Mokily amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Magereza namba 149 ya mwaka 2003 imezuia baadhi ya vitu kuingizwa magerezani.Ametaja baadhi ya vitu hivyo ni ni silaha, simu, visu, nondo, bangi, tumbaku na simu za mkononi."Ni marufuku kuingia na vitu,"amesema.

Amesema kuwa tabia hiyo si tu kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu wa kiume tu bali hata wanawake nao wanatabia hiyo kwa kuchukua vitu hivyo na kuficha sehemu zao za siri."Wanawake wenye tabia ya kuficha vitu wanachokifanya ni kukimbilia chooni na kisha huvitoa na baada ya hapo utashangaa kuona wanawasiliana na watu walioko nje kwa kutumia simu ambazo wameingia nazo kwa mtindo huo,"amesema.

Mrakibu wa Magereza Kitengo cha Sheria, Absalom Mokiry akifafanua mambo mbali mbali juu ya wafungwa na mahabusu waliopo mahakamani ikiwemo kuingiza simu na vitu vilivyokatazwa gerezani kwa kutumia njia zisizostahili.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI

0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania ( TWCC) jengo la maonyesho la IPP Ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali.

Jengo hilo pamoja na kuendeleza ujasiriamali litakuwa eneo la maonesho na kufunzia na Dk Mengi amesema amelitoa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Maamuzi ya kutoa jengo hilo yalifuatana na ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko aliyetaka jengo hilo kupewa wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi na kimafunzo.

 Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce-TWCC), Dk Mengi aliwataka wanawake kuwa macho na kutumia fursa zilizopo kujiwezesha kiuchumi. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mwakilishi wa TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen Mawalla (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC), Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC, Bi. Noreen Mawalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC Jacqueline Meney Maleko (hayupo pichani) kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wanachama wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TWCC uliofunguliwa jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dr. Reginald Mengi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO JANUARY 31,2018

KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA LAPEWA MIFUKO 25 YA SARUJI

0
0

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM)  Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi

0
0
Na Teresia Mhagama, Katavi

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefanya ziara mkoani Katavi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mwaka 2017 ya kukamilisha ufungaji wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme katika wilaya ya Mpanda  na Mlele mkoani humo.

Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo baada ya mitambo iliyokuwepo  katika kituo cha Mpanda kuharibika na hivyo kupelekea mkoa huo kuwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme huku baadhi ya maeneo katika wilaya ya Mlele yakipata umeme kutoka nchini Zambia.

  Meneja Miradi kutoka TANESCO, Stephen Manda alimweleza Dkt Kalemani kuwa,  ufungaji wa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda umekamilika na sasa kituo kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 huku matumizi ya wilaya ya Mpanda yakiwa ni megawati 2.3.

Manda alieleza kuwa, kukamilika kwa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda  kumewezesha vijiji 14 kusambaziwa umeme ikiwemo wilaya mpya ya Tanganyika ambayo imepata umeme kwa mara ya kwanza kutoka kuanzishwa kwake.

Akiwa katika wilaya ya Mlele, Dkt. Kalemani alielezwa kuwa, ufungaji wa mashine moja ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kilowati 476 umekamilika na kuwezesha baadhi ya wakazi wa Mlele hususan Makao Makuu ya wilaya hiyo (Inyonga) kupata umeme.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa nne kulia) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja  Jenerali (Mst), Raphael Muhuga  (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi kabla ya kuanza ziara ya kukagua  miradi ya kuzalisha umeme mkoani Katavi.
 Meneja  Miradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Makao Makuu, Stephen Manda (kulia), akitoa maelezo kuhusu mitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi. Anayesikiliza ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( katikati) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja  Jenerali (Mst), Raphael Muhuga  (wa kwanza kushoto).
 Mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi inayozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 kwa kutumia mafuta.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi wa Inyonge wilayani Mlele wakati alipofika wilayani humo kukagua mradi  wa uzalishaji umeme.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

VYAMA VYA SIASA VYAKUMBUSHWA KUTII SHERIA

0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amevikumbusha vyama vya siasa kutii Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za uchaguzi na kanuni zake wakati wa uchaguzi.

Wito huo umetolewa kupitia barua aliyoviandikia vyama vya siasa yenye kumbukumbu HA.322/362/01/165 ya tarehe 30 Januari, 2018.

“ Natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi ndogo za Ubunge na Udiwani zinazoendelea katika majimbo na kata.  Hivyo, natumia fursa hii pia kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika chaguzi hizo, kwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kidemokrasia. Aidha, naviasa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kuheshimu na kufuata sheria za nchi, hasa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kanuni zake, kwa kuepuka vitendo vya fujo na lugha za matusi na uchochezi” imenukuliwa barua hiyo.

Jaji Mutungi pia ametoa wito kwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au chama kinachoshiriki uchaguzi kutoa taarifa katika mamlaka husika kuliko kujichukulia sheria mkononi, endapo kitashuhudia kwa kuona ama kusikia uvunjifu wa Sheria unaohusu chaguzi zinazofanyika.

Mahojiano na mwanaDiaspora Dr Frank Minja kutoka Marekani

0
0
Karibu katika mahojiano na Dr Frank Minja. Mmoja wa wanaDIASPORA waishio Marekani ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia kuboresha huduma za X-Ray nchini Tanzania.
Dr Minja Mkurugenzi wa Neurology katika Hospitali ya Yale huko Connecticut nchini Marekani na Mwalimu katika Chuo Kikuu cha Yale.
Katika mahojiano haya, Dr Minja ameeleza mengi kuhusu historia yake na juhudi ambazo amekuwa akifanya kuboresha ELIMU na HUDUMA ya Afya Tanzania.Kati ya mambo aliyofanya kabla ya mahojiano haya ni pamoja na
MAKALA HII ya namna alivyoshiriki kuboresha huduma za Afya Tanzania
pamoja na Barua hii kwa wanafunzi wanaotafuta Scholarship.

JUKWAA LANGU ni kipindi kutoka Vijimambo Radio na Kwanza Production kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*

Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe na waalikwa wengine studioni kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 1
2 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)

Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570

PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe + special guests

PRODUCER: Mubelwa Bandio

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO LEO KWA WAZIRI MPINA

0
0
Na John Mapepele-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.

“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.

Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.

Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga chapa mifugo ambayo inatoka nje ya nchi ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na wafugaji kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo(mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. 
Dereva wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.


YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza  kikao cha pili cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akisoma muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma wa Mwaka 2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe.Kpt.George Mkuchika akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MSANII MKONGE KING MAJUTO HOSPITALINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali msanii mkongwe King  Amri Athumani maarufu kama Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimjulia hali na kumtakia apone haraka msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama  King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akimuaga baada ya kumjulia hali msanii mkongwe King  Amri Athumani maarufu kama Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018. 

BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA

0
0
Na Nyakongo Manyama
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na wabunifu wa Tanzania wamezindua Chama cha Mitindo Tanzania (FAT) kitakachowaunganisha wabunifu wote hatua inayolenga kuinua na kuiongezea hadhi sekta ya mitindo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu  Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa  (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza  amesema sekta ya mitindo nchini ikiimarishwa itaweza kuleta mapinduzi makubwa kwa kuzalisha ajira kwa vijana.

“Katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kujenga Tanzania ya viwanda, tasnia ya ubunifu wa mavazi, tumeamua kulima pamba ambayo ndiyo itakayozalisha mavazi, hivyo kusingekuwa na wabunifu hatungekuwa na mavazi yenye utamaduni wa Tanzania”

Aidha Mngereza aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa ngozi duniani, ambapo katika kutumia fursa hiyo, Chama cha wabunifu Tanzania kimepanga raslimali hiyo kwa kuzalisha  bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu, mikanda na mabegi .

Naye mwanzilishi wa chama hicho Bw. Mustafa Hassanali amesema kuwa  lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni katika kukuza, kuimarisha na  kuendeleza sekta ya mitindo Tanzania pamoja na kuwapatia ujuzi, uzoefu wadau wote wa   sekta ya mitindo Tanzania.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania, Adrian Nyangamalle amekipongeza chama hicho na kusema kuwa tasnia ya mitindo imetoa ajira kubwa kwa vijana na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano na jumuiya hiyo ili kutimiza malengo yake kwa haraka. 

Aidha Nyangamalle ameongeza kuwa Shirirkisho la Chama cha Ufundi kwa kushirikiana na BASATA wameanzisha mchakato wa kuwatambua wasanii wote nchini kwa kuandaa kanzi data itakayosaidia kufahamu wasanii waliopo nchini ili kuweza kutambulisha mchango wao katika kuinua uchumi.
  Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Chama  cha Wanamitindo Tanzania (FAT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Adrian Nyangamalle na kushoto ni Mwanamitindo mkongwe nchini Bi. Asia Idarous

Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (wa pili kulia) akizindua Chama  cha Wanamitindo Tanzania (FAT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam

MICHUZI TV: ALICHOKISEMA MZEE MAJUTO BAADA YA KUTEMBELEWA NA RAIS MAGUFULI HOSPITALINI

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images